Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-25. Je unafikiri kwamba kuelewa juu ubatizo wa Yesu ndiyo lazima kwa wokovu ambao umeondoa sheria ya kifo cha msalaba katika Injili?

Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani ni mambo yaliyo na umuhimu sawa kwa wokovu wetu. Hatuwezi kamwe kusema kati ya moja ya haya ni muhimu zaidi ya jingine. Kwa njia hii, tabu ni hii kwamba Wakristo wa nyakati hizi hujua na kuitambua damu ya Yesu msalabani tu! Huamini walisamehewa kwa sababu Yesu aliwafia msalabani tu, lakini ukweli ni kwamba si kwa msalaba tu ambao Yesu alibeba dhambi za ulimwengu. Kwa kuwa alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kubeba dhambi za ulimwengu juu yake, kifo chake msalabani kingekuwa kwa kimatendo kuwa ni hukumu ya dhambi zetu zote.
Kuamini msalaba pekee bila kuamini au kuelewa juu ya ubatizo wa Yesu ni sawa na kutoa sadaka mnyama mbele ya Bwana bila kuwekea mikono juu yake. Wale watoa sadaka kwa namna hii hawatoweza kamwe kukombolewa kwa dhambi zao kwa sababu namna hii ya sadaka ilikuwa ni kinyume cha sheria ya sadaka, ambayo Bwana Mungu asingekubali. Bwana alimwita Musa na kunena naye mbele ya hema ya kukulania, akasema, “Matokeo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana. Kisha atawawekea mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa ajili yake” (Walawi 1:3-4).
Mungu ni mwenye haki na afuataye sheria kwa mpango wa matoleo ya sadaka ili kutakasa dhambi zetu. Tunapotoa sadaka ya haki, sadaka hiyo hukubaliwa na Bwana kwa upatanisho wetu. Pasipo kuwekea mikono, sadaka hiyo haitoweza kamwe kukubaliwa na Mungu. Kwa jinsi hiyo pia, ikiwa tutaondoa ubatizo wa Yesu katika Imani yetu kwake, hatutoweza kupata msamaha wa dhambi kwa imani ya sina hiyo.
Moja ya mafundisho potofu katika nyakati hizi za Imani ya Kikristo ni kwamba, utaweza kuokolewa unapo mkiri Yesu huwa Mwokozi kwa kuwa Bwana ni upendo. Biblia hata hivyo inasema “Yeyote aliitiaye jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21, Warumi 10:13) ambapo pia inasema “Si kila aniitaye ‘Bwana Bwana’ ataingia ufalme wa mbinguni, bali wale wote watendao mapenzi ya Baba yangu wa Mbinguni” (Mathayo 7:21).
Ili kumkiri Kristo Yesu kuwa ni Mwokozi, yatupasa kujua sheria ya wokovu wa Mungu aliouweka. Ikiwa tutaweza kuokolewa kwa kuamini kirahisi Jina la Yesu pasingekuwa na sababu basi kwa maandiko yeyote kuandikwa juu ya mpangilio wa utoaji wa sadaka katika Agano la Kale na kuhusiana na walo wote waendao kinyume na sheria katika Mathayo 7:21 kwa namna hii njia ya ajabu na sahihi ya wokovu wa Bwana ipo ndani ya biblia kwa wazi na kwa kueleweka. Hakika tutaweza kwa uwazi kuona katika kitabu cha walawi sura ya 3 na 4 kwamba wenye dhambi iliwapasa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka ili kumbebesha juu yake dhambi zao zote na kumchinja ndipo kunyunyizia damu anapotoa sadaka ya dhambi na ya amani. Kutoa sadaka bila kuwekea mikono au kutoa sadaka aliye na doa pia hii ilikuwa kinyume cha sheria ya upatanisho.
Yote haya, maneno ya Agano Jipya na lile la Kale yalikuwa na pande zifananazo kwa kila moja (Isaya 34:16) ubatizo wa Yesu Yordani ni sawa na mwenye dhambi kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka katika Agano la Kale. Yesu alipotaka kubatizwa katika Yordani na Yohana Mbatizaji, alisema “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15).
Hapa “haki yote” maana yake “sheria na usawa.” Hii maana yake ina mpasa Yesu kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu kwa kupitia njia hii. Ilimpasa pia yeye kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika namna ya kuwekewa mikono ili kubeba dhambi zote za ulimwenguni kwa njia ya usawa kulingana na mpango wa matoleo ya sadaka, uliojumuisha kuwekea mikono na damu ambao Mungu aliuweka katika Agano la Kale.
Kuamini msalaba pekee maana yake matokeo ya kifo cha Yesu hayana maana kwa dhambi zetu kwa sababu dhambi zetu zingeweza kuwekewa juu yake bila ya ubatizo wake. Hii huleta matokeo ya kuichukulia damu yake kuwa si takatifu na haina uwezo wa kutakasa dhambi (Waebrania 10:29).
Hivyo, damu ya Yesu itakuwa hakika yenye kuleta matokeo katika kutakasa dhambi mioyoni mwa wenye kuamini ikiwa tu wanaamini kwamba dhambi zao zote zilibebwa naye pale Yohana Mbatizaji alishuhudia kwamba kwa yeyote amwaminie Yesu kuwa ni mwana wa Mungu aliye kuja katika maji na damu, ataushinda ulimwengu. Yesu alikuja kwa maji na damu si kwa maji tu, au damu tu (1 Yohana 5:4-6).
Yesu Kristo alielezea kwa wafuasi wake juu ya mambo yamhusuyo yeye katika maandiko yote. Kuanzia Musa na manabii wote, aliwaonyesha kwamba sadaka ya dhambi katika Agano la Kale alikuwa ndiye mwenyewe. Daudi alisema katika Zaburi juu yake “Tazama nimekuja, (katika gombo la chuo nimeandikwa) – kuyafanya mapenzi yako Ee Mungu wangu” (Zaburi 40:7, Waebrania 10:7).
Na kwa matokeo haya, ubatizo wa Yesu hauondoi maana ya msalaba, bali kwa hakika ni sehemu ya Injili ya Bwana ambayo yenye kuhitimisha na kutimiliza maana ya msalaba. Pia hutufunza kwamba hatutoweza kuwa na ukombozi hadi pale patakapokuwepo na ubatizo na ile damu ya thamani ya Yesu Kristo. Kumaanisha kuokoka ni pale tu unapopata ondoleo la dhambi kwa kuamini juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu (1 Yohana 5:8, Matendo 2:38).