Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-32. Ikiwa twasema kwamba Yesu alishaondoa dhambi zetu zote za zamani sasa, na zile zijazo mbeleni maishani mwetu, nikwa namna gani basi matarajio ya mtu mbeleni yatageuka ikiwa ataendelea kuwa na dhambi kwa kufikiri juu ya ukweli kwamba alikwisha samehewa dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake? Hata ikiwa ataua, yeye hutambua ya kwamba alikwisha patanishwa hata kwa kosa la aina hii kwa kupitia Yesu msalabani. Hivyo, ataendelea kutenda dhambi bila ya kusita kwa kuwa tunaamini Yesu alikwisha samehe hata dhambi zijazo maishani. Hebu tafadhali naombauelezee juu ya mambo haya.

Kwanza ya yote nakushukuru kwa kuleta maswali juu ya injili hii ya maji na kwa Roho. Swali uliloleta ndiyo moja ya maswali ambayo Wakristo waliyojiuliza hapo mwanzo kabla ya kuzaliwa upya. Najua kwamba una wasiwasi kwamba watu waliozaliwa upya wataendelea kutenda dhambi kwa kuwa wamefunuliwa juu ya injili iliyo sahihi ingawa napenda kukwambia kwamba watu hawawanaoamini injili ya maji na kwa Roho kamwe hawapo hatarini kuishi katika maisha ya aina hii unayotia wasiwasi juu yake, bali kwao wataishi maisha yale ya haki badala yake.
Yakupasa kwanza ufikiri juu ya hili. Ikiwa Roho Mtakatifu ni mkweli ndani yako,basi siku zote utazaa matunda matakatifu hata kama si kwa hiyari yako. Kwa upande mwingine, ikiwa Roho Mtakatifu hakai ndani yako, hatoweza kuzaa matunda ya aina yoyote ya Roho, haijalishi ni kwa namna gani utajaribu kwa bidii. Ni vipi mtu labda ataweza kuzaa matunda ya Roho ikiwa hana Roho Mtakatifu ndani yake hata kama anamwamini Yesu kwa namna gani? Hii haiwezekani !Bwana alisema kwamba mti mbaya hautoweza kuzaa matunda mema (Mathayo 7:17-18).
Napenda sasa nikuulize swali na unipe jibu lake Unaamini katika Yesu lakini je! kweli anaishi maisha yako huku ukishinda dhambi za ulimwengu? Je, unaishi maisha ya haki kama Mtumishi wa Mungu huku ukishinda dhambi za dunia,kumtumikia zaidi na kuwaongoza wengine kuokoka toka dhambini kwa kupeleka Injili ya maji na kwa Roho kwao? Je umekuwa kweli mwenye hak asiye na dhambi hata kidogo baada ya kuwa na imani juu ya Yesu? Imani pekee na Injili ambayo itaweza kukuruhusu kujibu ndiyo kwa maswali haya ni Injili ya maji na kwa Roho, ambayo Bwana iliyomshindia katika Agano la Kale na Jipya.
Tunaendelea kutenda dhambi hapa ulimwenguni hata baada kumwamini Yesu. Ijapokuwa Bwana wetu alibatizwa na Yohana na kumwaga damu yake msalabani kutuokoa na dhambi zetu zote ulimwenguni. Hivyo, Bwana ametenda jambo la haki kwetu na tumeokolewa toka dhambini kwa kupitia imani ya haki ya Mungu, ubatizo wa Bwana na damu ambayo iliondolea mbali dhambi zetu.
Napenda nikuulize maswali kadhaa tena. Je, upo huru kwa dhamira za dhambi? Je, wewe ni mwenye dhambi tena kama hapo awali hata baada ya kumwamini Yesu? Ikiwa hivi ndivyo kweli, bila shaka kwakuwa hukuifahamu injili ya maji na Roho. Hivyo basi umeangukia katika tatizo na uharibifu wa kurithiwa na mwili kwa sababu huna Roho moyoni mwako. Haijalishi ni kwanamna gani ulivyo muumini aliye mwaminifu, njia pekee ya kuepuka mawazo ya kimwili ni kuufungulia moyo wako kwa kuingiza injili ya maji na Roho. Yakupasa kuachana na mawazo yako ya kimwili na kurudia maandiko ya Neno la Mungu ili uelewe ukweli wa Injili ya maji na Roho iliyo ya kweli.
Wapo watu ulimwenguni humu wenye kubadili sheria ya wokovu ambao Bwana aliweka kwa namna wapendavyo ingawa humkiri Bwana kwa vinywa vyao. Ikiwa nawe mmoja wao kati ya watu wa aina hii, Bwana atakukana siku ile ya mwisho. Natumaini kwamba hili halitatokea kwa yoyote yule ulimwenguni. Nachukua nafasi hii kukuombea wewe mwenye kuamini juu ya damu ya Yesu msalabani ndiyo pekee iwezayo kuokoa, na hivyo uliuliza maswali kutokana na hamu ya kuishi maisha yaliyobaki katika muda wa uhai wako mbali ya dhambi.
Yamkini mawazo yako ni ya kimwili mbayo “hayatii sheria ya Mungu,wala hawezi kutii” (Warumi 8:7). Paulo husema “Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:8). Ikiwa kwa ukweli unatamani kuwa na imani yenye kumpendeza Mungu yakupasa uamini kazi ile njema ya Bwana ambayo iliyomfanya aje ulimwenguni kupitia Bikira Mariam, kuchukua dhambi za wanadamu kwa ubatizo alioupokea kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordan, na ndipo kuitiza haki ile ya Mungu.
Unafikiri ni nani awezaye kubeba kazi ile ya hali ya Mungu, aliye haki au mwenye dhambi? Mwenye dhambi yumo katikati ya dhambi kwa sababu hajapokea msamaha wa dhambi mbele za Mungu. Hivyo, jambo la pekee asubirilo ni hukumu ya Mungu kwa dhambi zake. Mungu hatoweza kamwe kumwacha mwenye dhambi aingie katika Ufalme wake kwa sababu “Maana hawi Mungu apendezwaye na ubaya, mtu mwovu hatakaa kwake” (Zaburi 5:4). Mungu alisema kwamba ikiwa mwenye dhambi angalikuja kwake na kumuomba kitu toka kwake, kamwe hatomsikiliza sala zake mwenye dhambi kwa kuwa “dhambi zake zimeuficha uso asiune” (Isaya 59:1-2). Mwenye dhambi bila shaka atakwenda motoni kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.
Wenye haki ndiyo pekee watakuwa Watakatifu na hivyo hawana dhambi mioyoni mwao kwa kutenda matendo ya haki. Kwa nyongeza. Roho Mtakatifu hukaa ndani ya wote wenye haki, wasio na dhambi baada ya kuamini ubatizo wa Yesu na msalaba wake. Mtume Petro alisema katika siku ile ya Pentekoste “tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38).
Kinachosemwa katika kifungu hiki ni kwamba, ikiwa unataka imani ya kweli na kupokea msamaha wa dhambi zako zote kwa imani, yakupasa basi kuamini yote mawili, Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Imani hii itaweza kukuruhusu “kupokea ubatizo katika Jina la Yesu” maana yake tunaweza kusema,utaweza kupokea msamaha wa dhambi zako kwa imani katika matendo ya haki ya Yesu. Bila shaka wafuasi wa Yesu walihudumia kwa ibada hii ya ubatizo kwa wale wenye kuzaliwa upya, wenye kuamini, walio na imani katika ubatizo wa Yesu na msalaba wake. Yesu aliamuru wafuasi kumbatiza yeyote katika Jina Baba na Mwana na Roho na Mtakatifu (Mathayo 28:19).
Zaidi pia Mtume Paulo alisema “lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyu si wake” (Warumi 8:9). Mungu kamtoa Roho Mtakatifu kwa wenye haki ili kuweka muhuri kuwa watoto wake. Roho Mtakatifu hattoweza kamwe kuwa ndani ya wenye dhambi, badala yake hupendelea Utakatifu(kwa kuwa mbali na dhambi). Roho pia huongoza wenye haki katika njia za haki kufuata mapenzi ya Baba. Sasa basi ni yapi mapenzi haya ya Baba? Ni kueneza Injili ya maji na Roho kwa watu wa mataifa yote na kuwabatiza kulingana na Amri Kuu.
Miili ya wenye dhambi haki na wenye dhambi hutenda dhambi hadi siku ya mwisho kifoni. Ijapokuwa Bwana amekwisha tenda tendo la haki la kufuta dhambi zote za watuwazitendazo katika mwili na mioyoni kwa ubatizo wake na damu yake. Hii ni haki ya Mungu ambayo Yesu aliitimiza. Hivyo imeandikwa katika Biblia “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani” (Warumi 1:17) Neno “ndani yake” ndiyo hii Injili iliyo ya kweli. Mtu aliyekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kuamini haki ya Mungu ataishinda ile “sheria ya kifo na dhambi” na badala yake kuifuata haki ya Kristo Yesu. Hii ndiyo pekee kwa kupitia Roho aliyekuja na kuishi ndani ya wale waaminio Injili ya maji na kwa Roho.
Dhambi zote za kale sasa na zijazo mbeleni za mwenye haki zilikwisha twikwa kwa Yesu siku ile alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Mwili wa mwenye haki pia na umekufa pamoja na Yesu. Mtu anapoamini, huungana na Yesu na kufanana pia na kifo chake. Hii huwa ni hukumu ya wote wenye dhambi (Warumi 6).
Hivyo basi, ingawa mwili wa mwenye haki unatenda dhambi mara kwa mara maishani mwake, Roho Mtakatifu akaaye ndani yake humwongoza katika kumfuata. Mwenye haki hunfuata Roho Mtakatifu na hufanya kazi ya Mungu kwakuwa Roho huyo Mtakatifu hukaa nadni yake siku zote.
Hata katika nyakati za Mitume, watu wengi walikuwa waki washutumu bila sababu wale waliozaliwa upya kwa sababu walikuwa na chuki ya kutoamini juu ya maisha ya watu wenye kuzaliwa upya ambao walikuwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Ijapokuwa watu wa aina hii walipotoka juu ya injili ya Kweli katika maji na kwa Roho ambayo Mitume walihubiri ikiwa walidhani ni mawazo ya kimwili. “Tuseme nini basi tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi 6:1-2) akaongeza. “Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, basi kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi” (Warumi 7:25).
Kwa hitimisho, mwili wa mwenye dhambi bado hajitoshelezi na hauna uchaguzi bali kuendelea kutenda dhambi isipokuwa utaendelea kumfuata Roho Mtakatifu, kwa kuhubiri Injili ulimwenguni pote. Mwenye haki hutembea katika Roho kwa kuwa moyo wake umetulia chini ya neema “Ni nini basi? tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! Hatujui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa Watumwa wake katika kumtii, mmekuwa Watumwa wake yeye mnayemtii kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki?” (Warumi 6:15-16).
Kama ilivyo maua bandi yalivyo tofauti na kweli yenye uhai, Bwana aliye ndani ya moyo wa mwenye haki na mwenye dhambi ni tofauti kwa kila mmoja. Ikiwa Bwana wa mwenye haki ni Roho Mtakatifu huyu ataenenda katika Roho na kufuata njia za kweli na za haki zizazompendeza Mungu. Kwa upande mwingine mwenye dhambi hana uchaguzi bali kufuata dhambi kwani bwana aliye ndani yake ndivyo alivyo. Mwenye dhambi kamwe kuishi maisha Matakatifu kwa sababu hana Roho wa Mungu, kwa kuwa ana uovu mwingi ndani yake.
Fikra za kwamba wenye kuamini Injili ya maji na kwa Roho hatoweza kwa kiasi fulani kuishi maisha Matakatifu ni aina za fikra na kanuni potofu zitokazo kwa kusema “Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyo yajua, na mambo wayatambuyo kwa asili wajiharibu kwa hayo kama wanyama wasio na akili” (Yuda 1:10). Walio wengi nyakati hizi hawaelewi ndani yao juu ya maisha ya haki hata ikiwa wanaikiri Injili ya maji na Roho kuwa ni Injili ya kweli kwa sababu hawaamini kikamilifu na hawajapokea hilo ndani ya mioyo yao.
Unafikiri nini juu matendo ya haki kwa aliyezaliwa upya? Wameachilia mambo yao yote yenye thamani hata nafsi zao kama sadaka iliyo hai, kwa mambo mema katika kueneza Injili ulimwenguni pote.kutokana na mawazo yako, kwa nini unafikiri kwamba wenye kuamini Injili ya maji na Roho wataweza kutenda dhambi kwa makusudi katika kificho cha sababu ya Injili waaminio?
Wenye haki hutenda mema kwa imani mbele ya uwazi wa kweli na haki ya Mungu. Wale wote watendao haki ya Mungu wamezaliwa upya. Tunatumaini wenye dhambi wote watarudia Injili ile ambyo Yesu aliyohuisha dhambi zao zote kwa ubatizo na damu yake.
Ndiyo hamu yetu ni kuona unapokea msamaha wa dhambi zako zote kwa kuamini Injili hii kwa moyo wako wote na kusubiri hadi Bwana atakapo kuja siku ile ya mwisho bila ya dhambi.