Search

Mahubiri

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-1] Ukombozi Wa Milele (Yohana 8:1-12)

(Yohana 8:1-12)
“Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlimani wa Mizeituni. Hata asubuhi kulipokucha akaingia hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha, Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati wakamwambia Mwalimu mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga, kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaji? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu kumshitaki. Lakini Yesu akainama akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi kumhoji alijiinua akawaambia. Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamira zao; wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata mwisho wao; akabaki Yesu peke yake na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akijiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende tena. Basi Yesu akawaambia tena, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu yeye anifuataye hatakwenda gizani, kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
 
 
Ni dhambi ngapi 
Yesu alizifuta?
Dhambi zote za Ulimwengu.

Yesu ametupatia Ukombozi wa milele. Hakuna awae yote duniani hapa atakaye achwa kukombolewa ikiwa atamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi. Alitukomboa sisi sote. Ikiwa yupo mwenye kuteseka na dhambi leo hii, ni kwa kuwa tu mtu huyo hajaelewa kwamba Yesu alimkomboa kutoka dhambini kupitia ubatizo na kusulubiwa kwake.
Sote yatupasa kuelewa na kuamini juu ya siri ya wokovu. Yesu alizibeba dhambi zetu zote katika ule ubatizo wake na kubeba hukumu ya dhambi hizo kwa kufa msalabani.
Unapaswa kuamini wokovu utokanao na maji na kwa Roho; ukombozi wa milele kwa dhambi zote. Unapaswa kuamini upendo huu mkuu ulio kufanya kuwa mwenye haki. Amini Yesu alichokufanyia katika wokovu wako pale Mto Jordan na katika Msalaba.
Yesu alitambua juu ya dhambi zetu za sirini pia. Baadhi ya watu huelewa vibaya juu ya dhambi. Hufikiri kwamba baadhi ya dhambi wazitendazo hawatoweza kukombolewa nazo. Yesu alitukomboa na dhambi zote, kila moja ya dhambi.
Hakuna dhambi yeyote katika dunia hii aliyoiacha nyuma. Ikiwa basi alizifuta dhambi zote za dunia, ukweli ni huu kwamba hakuna wenye dhambi tena. Je, umegundua kuwa Injili imetukomboa kutoka dhambi zetu zote hata zile zijazo mbeleni? Amini juu ya hili na uokolewe na umpe Mungu utukufu wote.
 
 
Mwanamke aliyekamatwa katika tendo la uzinzi

Ni wangapi wenye kuzini
Duniani?
Ni watu wote.

Katika Yohana 8, ipo hadithi ya mwanamke aliyekamatwa akizini na tumeona vile Yesu alivyomwokoa. Tungependa kushiriki naye hii neema aliyoipokea. Siyo vibaya tukisema kwamba kila mtu hufanya zinaa kwa kiwango fulani katika maisha. Kila mmoja hufanya zinaa.
Ikiwa hufikiri hivyo, ni kwa sababu tendo hili hulifanya mara kwa mara hivyo kujiona kwamba hufanyi. Kwa nini? Tunaishi na zinaa katika maisha yetu.
Hebu tizama mwanamke huyu katika Yohana 8, naweza kufananisha ikiwa hakuna au yupo kati yetu ambaye hajawahi kufanya uzinzi. Wote tumekwisha kutenda na kusingizia hatujafanya;
Je, unafikiri nimekosea? La! Sidhani. Tazama kwa uangalifu ndani yake. Kila mtu juu ya uso wa dunia hii ametenda hili. Wametenda hata kwa kuangalia kwa tamaa wanapokuwa wakitembea mitaani, katika mawazo yao na matendo kila wakati na mahala pote.
Hawajielewi wanapotenda hili. Wapo wengi wasiotambua hili hadi siku ya kufa wanapogundua wana idadi kubwa ya dhambi ya zinaa walizotenda maishani mwao. Si wale tu waliokamatwa. Hata wale walionayo katika mawazo yao na matendo yao sirini. Je, hii si sehemu ya maisha yetu?
Je, umechukizwa nalo? Huu ni ukweli. Tunaficha juu ya hili kwa kuwa ni fedheha kubwa. Ukweli ni kwamba, watu siku hizi hufanya zinaa wakati wote bila kugundua walifanyalo.
Watu hufanya zinaa katika mawazo yao pia. Sisi sote tulioumbwa na Mungu, tuishio hapa duniani bila kujitambua huwa tunatenda uzinzi wa kiroho. Kuabudu miungu wengine ni sawa na uzinzi kiroho kwani Bwana ndiye Mume wa wanadamu wote.
Mwanamke aliyekamatwa katika tendo hili ni mwanadamu, kama sisi sote, na alipokea neema ya Mungu, kama vile sisi tulivyo ipata katika ukombozi wetu, lakini Mafarisayo walio wanafiki walimweka kati yao wakimzunguka kwa kumnyooshea vidole wakidhani ni wenye haki ya kuhukumu na hata kutaka kumpiga kwa mawe. Walitaka kumkemea na kumhukumu wakidhani wao walikuwa ni safi na hawakuwahi kuzini.
Wakristo walio washirika wenye kujitambua nafsi zao kuwa ni wenye wingi wa dhambi, mara zote hawawezi kuwahukumu wengine mbele za Mungu. Bali hutambua kwamba wao pia ni wenye kutenda uzinzi maishani mwao kote, na hupokea neema ya Mungu ambayo ilitukomboa sote. Ni kwa wale tu wenye kugundua hili ndiyo wenye haki ya kukombolewa mbele ya Mungu.
 
 
Ni yupi apokeaye Neema ya Mungu?

Ni yupi apokeaye
Neema ya Mungu?
Wasio na thamani.

Je, ni yupi kati ya hawa mwenye kupokea Neema, anayeishi bila ya kutenda uzinzi kabisa au yule asiye na thamani mwenye kukubali ya kwamba ni mwenye wingi wa dhambi katika uzinzi? Atakayepokea neema ni huyu aliyepokea wingi wa neema ya ukombozi. Ni wale wasioweza, wadhaifu na wasio na msaada hupokea ukombozi. Ndiyo walio juu ya neema yake Mungu.
Wale wenye kufikiri kuwa hawana dhambi itakuwa vigumu kwao kukombolewa wataipokeaje neema ya ukombozi wa Mungu ikiwa hawana cha kukombolewa ndani yao?
Waandishi na Mafarisayo walimburuta mwanamke aliyefumaniwa katika kitendo cha uzinzi kwa Yesu na kumweka kati wakimuuliza, “mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini, nawe wasemaje?” kwa nini walimleta mbele zake kwa kumjaribu yeye? (Yesu)
Wao pia walitenda uzinzi mara nyingi, lakini walijaribu kutaka kuhukumu na kuua kupitia Yesu wakitaka lawama hizi ziwe juu yake.
Yesu alikwishaelewa nini kilichopo akilini mwao na kujua juu ya mwanamke yule. Hivyo akasema “yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe kwanza wa kumtupia jiwe.” Ndipo waandishi na Mafarisayo kwa kuanzia wazee hadi vijana, walipotoka na kumwacha Yesu na yule mwanamke.
Waliondoka walikuwa waandishi na Mafarisayo, viongozi wa dini walikuwa wakitaka kumhukumu mwanamke aliyefumaniwa wakidhani wao siyo wenye dhambi.
Yesu aliutangaza upendo wake duniani. Alikuwa ni Bwana wa Upendo. Yesu aliwalisha watu chakula, alifufua wafu, alimpa uhai mtoto wa mjane, alimfufua Lazaro wa Bethani, aliponya viwete na kutenda miujiza kwa masikini. Alibeba uovu wa wenye dhambi wote na kuwarudishia wokovu.
Yesu anatupenda. Yeye ni mwenye enzi pekee awezaye yote, hali Mafarisayo na Wanasheria walidhani kwamba yeye ni adui kwao. Na ndiyo maana walimleta yule mwanamke mbele yake ili wamjaribu.
Walimuuliza “Mwalimu, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii, nawe wasemaji?” Walifikiri kwamba angewaambia wampige kwa mawe. Kwa nini? Ikiwa tungetoa hukumu kulingana na kile kilichoandikwa kwenye sheria ya Mungu, kila mmoja wetu aliyefanya uzinzi angelipondwa kwa mawe hadi kufa bila huruma.
Wote walipaswa kupigwa kwa mawe hadi kufa na wote wamehukumiwa kwenda jehanamu. Malipo ya dhambi ni mauti. Ingawa Yesu hakuwaambia wampige mawe. Badala yake alisema “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Kwa nini Mungu alitupa
Vipengele 613 vya Sheria?
Ili tuweze kujitambua kuwa 
ni wenye dhambi.

Sheria huleta hasira ya Mungu. Mungu ni Mtakatifu na yeye mwenyewe ni Sheria. Sheria hii Takatifu ilikuja kwetu katika vipengele 613 sababu Mungu kutupatia vipengele hivi 613 vya sheria yake ilikuwa ni kutufanya sisi wanadamu kwamba ni wenye wingi wa dhambi; si wakamilifu inatufundisha kwamba tunahitaji sana Neema ya Mungu kutukomboa. Kama tusinge jua hili na kufikiri tu juu ya sheria basi tungepaswa kupigwa kwa mawe hadi kufa kama ilivyo yule mwanamke aliye fumaniwa.
Waandishi na Mafarisayo ambao hawakujua ile kweli ya sheria ya Mungu wangefikiri ya kwamba wangeweza kumpiga kwa mawe mwanamke yule, labda hata sisi tungefanya hivyo. Lakini ni nani atathubutu kurusha jiwe kwa mwanamke huyu asiye na tumaini ikiwa sisi pia ni viumbe waovu mbele ya Mungu.
Ikiwa yule mwanamke na wengi wetu sisi tukihukumiwa kwa sheria tu, sisi na mwanamke huyu tungepokea adhabu ya kutisha na kali. Lakini Yesu alituokoa sisi sote wenye dhambi, kutoka kwenye dhambi zetu na kutoka katika ile hukumu ya haki. Sisi na dhambi zetu zote, ikiwa sheria ya Mungu itatumika kwa umakini kila neno ni nani angesimama hai? Kila mmoja wetu angekwenda motoni.
Lakini waandishi na Mafarisayo walijua sheria tu kama ilivyo andikwa. Ikiwa sheria hii ingetumika kwa haki na kweli kama hukumu ya kweli, hakika wangestahili kifo. Kwa kweli sheria ya Mungu ililetwa ili watu waweze kuelewa dhambi zao ni zipi mbele ya Mungu, ingawa wanateseka kwa kutoelewa ipasavyo na kuitumia visivyo.
Mafarisayo wa leo, kama walivyo wale wa kwenye Biblia wanaijua sheria kama ilivyo andikwa tu!. Wanapaswa kuelewa neema, hukumu na kweli ya Mungu, kwa kufundishwa juu ya ile Injili ya ukombozi ili waokolewe.
Mafarisoyo walisema, “sheria imetuamuru kuwapiga mawe wanawake namna hii, nawe wasemaje?” Walimuuliza kwa hakika huku wakibeba mawe mikononi mwao. Walifikiri hakika Yesu hangekuwa na lakusema juu yake. Walimsubiri yeye ili wachukue hatua zao.
Ikiwa angetoa hukumu kulingana na sheria, hata yeye wangempiga mawe. Nia yao ilikuwa kuwapiga wote wawili. Ikiwa angesema wasimpige, wangesema kwamba Yesu ameidharau sheria ya Mungu, na wagempiga kwa kosa la kuasi. Ilkuwa ni mpango mbaya.
Lakini Yesu aliinama chini na kuandika ardhini kwa vidole vyake, na wakaendelea kuhoji, “Wewe wasemaje?” Unaandika nini kwenye aridhi? Hebu tujibu swali letu. Unasamaje?” Walimsumbua kwa maswali.
Na ndipo Yesu aliposimama na kuwaambia kwamba yule asiye dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe. Waliposikia hili walijiona kuhukumiwa nafsi zao na kuondoka mmoja baada mwingine kwa kuanzia yule mkubwa hadi mdogo. Yesu akibaki peke yake na mwanamke akisimama mbele zake.
 
 
“Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Kumbukumbu ya dhambi
Zetu huwekwa wapi?
Katika vibao vya mioyo yetu
Na kwenye kitabu cha
Matendo.

Yesu aliwaambia “yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe,” na kuendelea kuinama akandika aridhini. Baadhi ya wakubwa walianza kuondoka. Mafarisayo walio wazee ambao ndiyo wenye dhambi zaidi na ndiyo wangekuwa wa kwanza. Wako wadogo nao walifuatwa. Na tuseme Yesu angekuwa amesimama kati yetu na sisi tuwe tumemzunguka huyu mwanamke. Ikiwa Yesu atasema kwetu, yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe kwanza kumtupia jiwe, je,wewe ungefanya nini?
Yesu alikuwa akiandika nini pale chini? Mungu aliyetuumba sisi huandika dhambi zetu katika sehemu mbili tofauti.
Kwanza huandika dhambi katika vibao vya mioyo yetu. “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao na katika pembe za madhabahu zenu” (Yeremia 17:1). 
Mungu amezungumza nasi kupitia Yuda, ambaye ni mwakilishi wetu. Dhambi za wanadamu zimechorwa kwa kalamu ya chuma, yenye ncha ya almasi. Zimewekwa kumbukumbu katika vibao vya mioyo yetu. Yesu aliinama na kuandika kwenye ardhi ya kwamba wanadamu wote ni wenye dhambi.
Mungu anajua ya kwamba tunatenda dhambi na ameziandika dhambi zetu katika vibao vya mioyo yetu. Kwanza kabisa, ameweka kumbukumbu za matendo yetu, dhambi tulizo tenda, kwa kuwa sisi tu wanyonge mbele ya sheria. Kwa jinsi dhambi zetu ziandikwavyo mioyoni mwetu, tunagundua kwamba tu wadhambi tunapolinganisha na sheria kwa kuwa zimehifadhiwa ndani ya mioyo yetu kwa hisia, basi tunaweza kuona kwamba tu wenye dhambi mbele ya Mungu.
Yesu aliinama kwa muda mara ya pili na kuendelea kuandika katika ardhi. Maandiko vile vile yanasema kwamba dhambi zetu zote zimewekwa kumbukumbu katika kitabu cha Matendo mbele ya Mungu (Ufunuo 20:12). Kila jina la mwenye dhambi limehifadhiwa kwa kumbukumbu ndani ya Kitabu hicho. Na pia imeandikwa katika vibao vya moyo wake. Dhambi zetu zimeandikwa katika kitabu cha Matendo na katika vibao vya mioyo yetu.
Dhambi zimewekwa kumbukumbu katika vibao vya mioyo ya vijana na wazee. Na hii ndiyo maana wale waliomshitaki yule mwanamke hawakuwa na la kusema mbele za Yesu. Wale waliotaka kumpiga yule mwanamke hawakujizuia mbele ya maneno ya Yesu.

Ni lini dhambi zetu zilizowekwa
kumbukumbu katika sehemu
hizo mbili hufutwa?
Tunapokubali ukombozi katika maji na katika
damu ya Yesu ndani ya mioyo yetu.

Hivyo unapopokea wokovu wa Yesu, dhambi zako zote katika kitabu cha Matendo zinafutwa na jina lako kuorodheshwa katika kitabu cha Uzima. Wale wote walio na majina katika kitabu cha Uzima watakwenda Mbinguni. Matendo mema, mambo waliyofanya katika ulimwengu huu kwa niaba ya Ufalme wa Mungu na haki zake vimeandikwa pia katika kitabu cha Uzima. Wamekubalika Mbinguni. Wale wote waliokombolewa kutoka dhambini wataingia katika uzima wa milele.
Ikumbukwe kwamba kila dhambi za mtu zimeandikwa katika sehemu kuu mbili, hivyo si rahisi kwa yeyote kumdanganya Mungu. Hakuna ambaye hajatenda dhambi au kuzini katika moyo wake. Watu wote ni wenye dhambi na wapungufu.
Wale wote ambao hawajaukubali ukombozi wa Yesu katika mioyo yao hawana namna zaidi ya kuteseka kwa dhambi zao. Hawana ushupavu ndani yao humwogopa Mungu na wanadamu wenzake kwa sababu ya dhambi zao. Lakini pindi wanapokubali Injili ya ukombozi katika maji na kwa Roho ndani ya mioyo yao, dhambi zote zilizo andikwa vibao vya mioyo yao na katika kile kitabu cha matendo hufutwa na kusafishwa. Hukombolewa kutoka katika dhambi zao zote.
Kipo kitabu cha Uzima kule Mbinguni. Majina ya wale walio amini ukombozi katika maji na kwa Roho yamehifadhiwa kwa kumbukumbu ndani yake, hivyo watakwenda Mbinguni. Wataingia Mbinguni si kwa sababu hawakutenda dhambi hapa duniani bali kwa kuwa walikombolewa kutoka katika dhambi zao zote kwa imani juu ya ukombozi kwa maji na kwa Roho. Hii ni “sheria ya imani” (Warumi 3:27).
Walio Wakristo, Waandishi na Mafarisayo walikuwa wenye dhambi kama alivyo mwanamke yule aliyefumaniwa.
Ukweli ni kwamba, yawezekana walikuwa wamewahi kutenda dhambi zaidi ya moja na kujiaminisha mbele za watu kwamba wao si wadhambi. Viongozi wa dini walikuwa wezi wenye vibali vya zamani wezi wa roho, au kwa maneno mengine wezi wa uzima. Walithubutu kufundisha wengine kwa mamlaka, ingawa wao wenyewe hawakuwa wamekombolewa.
Hakuna awaye yote asiye na dhambi kutokana na maandiko ya sheria. Lakini mtu aweza kuwa mwenye haki si kwa sababu hajatenda dhambi, bali ikiwa amekombolewa na dhambi zake zote. Mtu wa aina hii huwekwa kumbukumbu katika kile kitabu cha Uzima. Jambo muhimu hapa ni ikiwa jina lake limehifadhiwa katika kitabu cha Uzima au la! Ikiwa mtu hawezi kuishi bila kutenda dhambi katika maisha yake, basi yampasa kukombolewa ili jina lake liwekwe kumbukumbu katika kitabu hicho.
Ikiwa utakubalika kuingia Mbinguni itategemea kama utaamini Injili iliyo ya kweli au la! Kupokea au kutopokea neema ya Mungu hutegemea kukubali kwako wokovu wa Yesu. Nini kilimpata Mwanamke yule aliyefumaniwa? Angeliweza kuangukia magoti na kufunika macho yake kwa kuwa alijua angekufa kwa mawe tu! Labda alikuwa akilia kwa kuogopa na kujutia. Ukweli ni kwamba watu wanapokutana na mauti ndipo wanapo kuwa wenye uaminifu ndani ya nafsi zao.
“Ah, Mungu, ni sawa kwangu kufa! Nakusihi uipokee roho yangu mikononi mwako, na unionee huruma. Nakusihi unionee huruma, Yesu.” Mwanamke huyu alimsihi Yesu kwa upendo wa ukombozi. “Mungu ukinihukumu, nitahukumiwa, na ikiwa utasema sina dhambi tena basi dhambi zangu zitafutika. Ni hiyari yako.” Labda alinena haya yote. Alikiri kuwa yote aliyaweka mbele za Yesu.
Mwanamke huyu aliyeletwa mbele ya Yesu hakusema, “Nimetenda dhambi ya uzinzi, naomba unisamehe,” bali alisema “Nakusihi, uniokoe na dhambi zangu. Ikiwa utaniokoa, nitaokoka. Ikiwa sivyo nitakwenda motoni. Nahitaji ukombozi wako. Nahitaji upendo wa Mungu na nahitaji huruma yake,” alifunika macho yake na kutubu makosa yake.
Na yesu akumuuliza, “Wako wapi wale washitaki wako?” “Je, hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?” Akajibu “hakuna Bwana.” 
Naye Yesu akamwambia “wala mimi sikuhukumu.” Yesu hakumhukumu kwa sababu alikwisha zibeba dhambi zake zote kwa kupitia ubatizo wake katika ule mto Jordani na tayari alikwisha kombolewa. Hivyo sasa, ni Yesu na wala si yule mwanamke tena aliyepaswa kuhukumiwa kwa dhambi.
 
 
Akamwambia, “wala mimi sikuhukumu.”

Je, ali hukumiwa
Na Yesu?
Hapana.
 
Mwanamke huyu alibarikiwa na wokovu katika Yesu. Alikombolewa na dhambi zake zote maishani. Bwana wetu Yesu ametuambia kwamba amekwisha tukomboa na dhambi zetu zote na hivyo sote tu wenye haki.
Anatuambia hili katika Biblia. Alikufa msalabani ili kulipia madhambi yetu ambayo aliyabeba pale katika ubatizo wake mto Jordani. Kwa uwazi anatuambia kwamba ametukomboa sisi wale wenye kuamini ubatizo wake na hukumu ile ya msalaba. Sisi sote tunahitaji maandiko ya Neno la Yesu na kuyashikilia. Na ndipo tutakapo barikiwa na huu ukombozi.
“Mungu, sina urithi mbele zako, sina chochote kilicho chema ndani yangu. Sina la zaidi ya dhambi mbele yako. Lakini namwamini Yesu kuwa ni Bwana wa Ukombozi. Alizichukua dhambi zangu zote katika mto Yordani kwa upatanisho wake pale msalabani. Alizichukuwa dhambi zangu zote kwa ubatizo wa damu yake. Nakuamini wewe Bwana.”
Hivyo ndivyo unavyookoka. Yesu hatuhukumu. Anatupa haki ya kuwa watoto wa Mungu. Kwa wale tu watakao amini ukombozi katika maji na kwa Roho, amezichukua dhambi zetu zote na kutufanya wenye haki.
Rafiki zangu! Mwanamke yule alikombolewa. Mwanamke aliyefumaniwa alipata baraka ya ukombozi wa Bwana wetu Yesu. Hata sisi leo hii tunaweza kupata baraka ya aina hii. Kwa yeyote mwenye kuzikiri dhambi zake na kumwomba Mungu huruma yake, na kwa yeyote mwenye kuamini ukombozi wa maji na kwa Roho katika Yesu hupokea baraka ya ukombozi kwa Mungu. Wale wenye kukiri uovu wao mbele za Mungu watakombolewa lakini wasiotambua juu ya dhambi zao hawawezi kubarikiwa na ukombozi huu.
Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu (Yohana 1:29). Mwenye dhambi yeyote katika dunia hii aweza kukombolewa ikiwa atamwamini Yesu. Yesu alimwambia mwanamke “wala mimi sikuhukumu.” Alisema hivi kwa sababu, dhambi zake zote alikwisha zibeba katika ubatizo wake. Alichukua dhambi zote kwake, na alihukumiwa badala yetu.
 

Yatupasa tukombolewe mbele ya Yesu

Lipi ni kuu, Upendo wa Mungu
au hukumu ya Mungu?
Upendo wa Mungu.

Mafarisayo wakiwa na mawe mikononi mwao na wale viongozi wa kidini kwa nyakati hizi, hutafsiri sheria hizi kwa kila neno. Huamini kwamba, kwa kuwa sheria inasema usizini, na afanyaye hilo atapigwa kwa mawe hadi kufa. Hata wao walimkodolea macho kwa kumtamani huku wakiwa na unafiki wa nafsi zao kwamba hawatendi uzinzi kwa wakati huo. Hawawezi kukombolewa wala kuokolewa. Mafarisayo na Waandishi ni watu wa kimwili katika ulimwengu huu wa leo. Hawakuwa wameitwa na Yesu na wasingeweza kuelewa pale aliposema “wala mimi sikuhukumu.”
Ni yule mwanamke pekee aliye fumaniwa aliweza kusikia maneno haya ya kufurahisha na yenye matumaini kwake. Ikiwa nawe ni mkweli mbele zake, waweza pia kubarikiwa kama yeye “Mungu, nimeshindwa, maishani mwangu naendelea kufanya uzinzi. Nimekufa ganzi moyoni kwa kuwa nimekwisha zoea kufanya hili. Natenda kila siku.”
Tunapoikubali sheria na ukweli ya kuwa sisi tu wadhambi na lazima tufe kwa uaminifu tunapomwendea Mungu kwa kusema “Mungu hivi ndivyo nilivyo; Naomba uniokoe.” Hakika Mungu atakubariki na ukombozi wake.
Upendo wa Yesu, Injili ya maji na kwa Roho ilikwisha ishinda hukumu ya Mungu. “Wala mimi sikuhukumu” Hatuhukumu. Anasema “umekombolewa” Bwana wetu Yesu Kristo ni Mungu wa huruma. Alitukomboa kutoka katika dhambi zote za ulimwengu.
Mungu wetu ni Mungu wa Haki na Mungu wa Upendo! Upendo wa maji na kwa Roho ni mkuu zaidi ya Hukumu yake.
 
 
Upendo wake ni mkuu zaidi ya hukumu yake

Kwa nini alitukomboa 
sisi sote?
Kwa kuwa upendo wake ni Mkuu
zaidi ya Hukumu yake.

Ikiwa Mungu angeshurutisha hukumu yake ili kukamilisha haki yake, angelihukumu wale wote wenye dhambi na kuwatupa motoni wote. Lakini kwa kuwa upendo wa Yesu, ulituokoa kutoka hukumuni ni mkubwa mno! Mungu alimtuma kwetu mwanawe wa pekee, Yesu. Yesu alibeba dhambi zetu zote na kupokea hukumu ya dhambi hizo mwenyewe kwa niaba yetu. Hivyo, kila amwaminiye Yesu kama ni mwokozi hufanywa kuwa mwana wa Mungu mwenye haki. Kwa kuwa upendo wake ni mkuu kupita haki yake, ndiyo maana ametukomboa sisi sote.
Tumshukuru Mungu kwani yeye hatuhukumu kwa haki yake. Wakati Yesu alipowaambia Waandishi. Mafarisayo na wafuasi wao “Nenda na mjifunze hii maana yake nini: ‘Nataka rehema, wala si sadaka.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Mathayo 9:13). Wengine wanaweza kuendelea kutoa sadaka ya ng’ombe au mbuzi kwa kuchinja kila siku ili kumtolea Mungu na kuomba, “Mungu nisamehe dhambi zangu kila siku.” Mungu hazihitaji sadaka zetu, bali imani yetu katika ukombozi wa maji na kwa Roho. Anapenda tukombolewe na kuponywa. Anapenda kutupa upendo wake na kuikubali imani yetu. Je, wote mnaona hii? Yesu ametupatia wokovu ulio kamili.
Yesu huchukizwa na dhambi, lakini ana Upendo mkuu juu ya wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu, alikwisha amua hata kabla ya uumbaji kutufanya kuwa wana kwake, na kuzifuta dhambi zetu kwa ubatizo na kwa damu. Mungu alituumba kwa wakati huo na kutukomboa, kutuvika katika Yesu na kutufanya kuwa watoto wake. Huu ni upendo alio nao juu yetu sisi tulio viumbe wake.
Ikiwa Mungu hutuhukumu kwa sheria yake tu, sisi tulio na dhambi tulipaswa kufa. Lakini alitukomboa kupitia ubatizo na hukumu ile ya Mwana wake Yesu pale msalabani. Je, unaamini hili? Hebu, na tulithibitishe hili katika Agano la Kale.
 
 
Haruni aliweka mikono yake juu ya sadaka ya kuachiliwa (Azazeli)

Nani aliyeweka mikono juu ya 
kichwa cha Mbuzi ili kuwakilisha
dhambi Zote za wana wa Israel?
Kuhani Mkuu.

Dhambi zote za ulimwengu zililipwa kwa Imani kupitia Ibada ya Agano la Kale na kwa ubatizo wa Agano Jipya. Katika Agano la Kale dhambi zote za mwaka mzima za wana wa Israeli zililipiwa kuwa kupitia Kuhani Mkuu, ambapo aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Mbuzi aliye hai asiye na doa.
“Ni Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule Mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao, naam dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule Mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari” (Walawi 16:21). 
Hivi ndivyo walivyofanya upatanisho katika nyakati zile za Agano la Kale. Ili kukombolewa na dhambi za kila siku, ilipaswa kumleta kondoo au Mbuzi asiye na doa mbele ya madhabahu na kumchinja katika altare. Aliweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka hiyo na ndipo dhambi zake zote ziliwekewa juu ya toleo hilo la dhambi. Mnyama huyu wa kafara alichinjwa na kuhani aliweka damu yake kwenye pembe za altare.
Palikuwa na pembe katika kila kingo zikutanazo kuta za altare. Pembe hizi huwakilisha kitabu cha Matendo ilivyoandikwa katika ufunuo 20:12 Damu iliyobaki ya yule mnyama wa kafara ilinyunyizwa ardhini pia. Ardhi inawakilisha moyo wa mtu kwa kuwa aliumbwa kutokana na mavumbi. Hivi ndivyo watu walivyopatanishwa kwa dhambi za kila siku.
Ingawa haikuwa rahisi kwao kutoa sadaka hii ya dhambi kila siku, Mungu aliwaruhusu wapatanishwe mara moja kwa mwaka kwa dhambi zao zote za mwaka. Na hii ilifanyika katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, siku ya upatanisho katika siku hiyo, Kuhani Mkuu ambaye ndiye mwakilishi wa Waisraeli wote aliwaleta Mbuzi wawili na kuweka mikono yake juu ya vichwa vyao kuwekea dhambi zote za watu juu yake na kuwatolea kwa Mungu kwa upatanisho wa watu wote wa Israeli.
“Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule Mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao” (Walawi 16:21). 
Mungu alimteua Haruni, ali awe Kuhani Mkuu wa Israeli, mwakilishi. Badala ya kila mmoja kupaswa kuwekea mikono sadaka yake binafsi, kuhani mkuu akiwa mwakilishi wa wote, aliwekea mikono juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai kwa ondoleo la dhambi za watu wote kwa mwaka mzima.
Alizitaja dhambi zote moja hadi nyingine za wana wa Israeli mbele ya Mungu “Ee Mungu, watoto wako Israeli wamekutenda dhambi. Tumeabudu miungu wa sanamu tumevunja vipengele vyote vya sheria yako, tumetaja jina lako bure, tulijiundia sanamu na kuzipenda zaidi yako. Hatukuitukuza Sabato takatifu, hatukuwaheshimu wazazi wetu, tuliua, fanya uzinzi na kuiba… Tulijiingiza katika wivu na magombano.”
Alizitaja dhambi zote “Mungu si mimi wala si wana wa Israeli tulio zishika Amri zako. Ili tukombolewe kutoka dhambi hizi, naweka mikono yangu juu ya kichwa cha mbuzi huyu ili kuzitwika dhambi hizi zote. Hapo Kuhani Mkuu huweka mikono yake yote juu ya kichwa cha sadaka hiyo. Ibada hii au kuwekea mikono maana yake ni kubebesha, kuwekeza au kutwika” (Walawi 1:1-4, 16:20-21). 

Ni kwa namna gani upatanisho
ulifanywa wakati wa Agano
la Kale?
Kwa kuwekea mikono juu ya kichwa 
cha sadaka ya dhambi.

Mungu ametoa mpangilio wa kutoa kafara kwa watu wa Israeli ili dhambi hizo zibebeshwe na kuweza kukombolewa. Alitoa maelekezo ya kwamba sadaka hiyo ya upatanisho lazima iwe safi isiyo na dosari na ife kwa kuchinjwa kwa niaba ya mtoaji, Ukombozi wa kila mtu binafsi mwenye dhambi ulikuwa wa namna hii.
Kwa namna hii basi, katika ile siku ya upatanisho sadaka ya dhambi ilichinjwa na damu yake kuchukuliwa sehemu ya Patakatifu na kunyunyizwa kwenye kiti cha Rehema mara saba. Hivyo, watu wa Israeli walipatanishwa kwa dhambi zao za mwaka katika siku ya kumi ya mwezi wa saba.
Kuhani Mkuu aliingia Patakatifu peke yake kutoa sadaka, hali watu wengine waliobaki walikusanyika nje wakishikiliza sauti ya kengele za dhahabu katika mishipi izungukayo kifuko cha kifuani juu ya joho la Kuhani Mkuu. Kengele za dhahabu ziligonga mara saba damu iliponyunyizwa katika kiti cha rehema. Ndipo watu hufurahi kwa kuwa dhambi zao zimesamehewa. Sauti ya Kengele za dhahabu inafananishwa na suti ya Injili ya furaha.
Si kweli kwamba Yesu anaupendo na watu wa aina fulani na kuwakomboa wao pekee. Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu mara moja na kwa wakati wote. Dhambi zetu zisinge weza kombolewa kila siku, hivyo zilifutwa zote na kwa mara moja tu!
Katika Agano la kale, upatanisho ulitolewa kupitia Ibada na damu ya sadaka ya dhambi. Haruni aliweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi mbele ya watu wote na kuzitaja dhambi zote watu walizotenda kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Alizitwisha dhambi zote kwa yule mbuzi mbele ya watu wote wa Israeli. Je, ni wapi basi dhambi hizo zilikwenda baada ya Kuhani Mkuu kuwekea mikono sadaka ile ya mnyama? Alibeba yule mbuzi wa sadaka.
Ndipo mbuzi yule aliongozwa katika mikono ya “mtu aliye tayari.” Akiwa amezibeba dhambi zote za watu wa Israeli, alipelekwa jangwani ambako hakuna maji wala nyasi. Mbuzi huyo alitangatanga jangwani kwa jua kali na hatimaye kufa. Alikufa kwa dhambi za watu wa Israeli.
Huu ni upendo wa Mungu, upendo wa ukombozi.Hivi ndivyo ilivyokuwa namna ya upatanisho wenye thamani wa dhambi za siku zote. Lakini tunaishi katika nyakati za Agano Jipya Imekwisha kuwa karibu miaka 2000 tangu Yesu aje katika dunia yetu. Alikuja na kutimiza ile ahadi aliyowekwa katika Agano la Kale. Alikuja na kutukomboa kwa dhambi zote.
 

Kutukomboa sote

Nini maana ya YESU?
Mwokozi, yeye ndiye Atakaye waokoa 
watu Wake na dhambi zao.

Na tusome Mathayo 1:20-21 “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake YESU, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:20-21).
Baba yetu wa Mbinguni aliuazima mwili wa Bikira Mariamu kumtuma Mwana wake kuja duniani ili kusafisha dhambi za watu wa ulimwengu. Alituma malaika kwake Mariamu na kumueleza “Tazama, na utachukua mimba nawe utamzaa mwana nawe utamwita jina lake YESU.” Hii ina maana mtoto atakaye kuja kupitia Mariamu atakuwa Mwokozi. Yesu Kristo maana yake yeye atakaye wakomboa watu wake, kwa maneno mengine, Mwokozi.
Sasa ni kwa namna gani atatuokoa sisi sote na dhambi zetu? Namna Yesu alivyochukua dhambi zetu ni katika ule ubatizo wake pale mto Yordani. Wakati Yohana Mbatizaji alipombatiza, dhambi zote za dunia alizibeba kwake. Hebu na tusome Mathayo 3:13-17.
“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye.”
Yesu alikwenda kwa Yohana mbatizaji ili kutukomboa sisi sote kutoka dhambini. Alijitumbukiza kwenye maji na kuinamisha kichwa chake mbele ya Yohana “Yohana nibatize sasa. Ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Kama nilivyo ninataka kubeba dhambi zote za dunia kwa kuwakomboa wenye dhambi na hakika kuzichukua dhambi hizi kwa ubatizo huu. Nibatize sasa. Ruhusa iwe hivyo.”
Hivi ndivyo ilivyopaswa kutimiza haki zote. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto Jordan na katika wakati huo, haki zote za Mungu ziletazo ukombozi wetu zilitimizwa.
Na hivi ndivyo Mungu alivyozichukua dhambi zetu zote. Dhambi zote alitwikwa Yesu pia. Je unaelewa juu ya hilo?
Amini katika ukombozi wa ubatizo wa Yesu na kwa Roho na uokolewe.

Ni kwa namna gani
Haki zote zilihimizwa?
Kupitia ubatizo wa Yesu.

Mwanzo Mungu aliwaahidi wana wa Israeli kwamba dhambi zote za ulimwengu zitasafishwa kwa kuwekea mikono kafara ya sadaka ya dhambi. Hata hivyo kama isivyo rahisi kwa kila mmoja kuweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi kwa binafsi Mungu alimteua Haruni ili awe Kuhani Mkuu ili aweze kumtolea kafara kwa niaba ya watu wote. Na hii, aliweza kutwika juu ya kichwa dhambi zote za mwaka za watu wote kwa ile sadaka ya dhambi kwa mara moja. Hii ilikuwa ni Hekima ya Mungu na nguvu ya ukombozi. Mungu ni mwenye Hekima na wa ajabu.
Alimleta mwana wake Yesu kuukomboa ulimwengu wote. Hivyo sadaka ya dhambi ilikuwa tayari. Sasa, alihitajika mwakilishi wa wanadamu wote, yeye pekee atakayewekea mikono juu ya kichwa cha Yesu (sadaka ya upatanisho) na kutwika dhambi zote za ulimwengu kwake mwakilishi huyo alikuwa ni Yohana Mbatizaji Imeandikwa kwenye Biblia kwamba Mungu alimtuma mwakilishi wa wanadamu kabla ya Yesu.
Alikuwa Yohana Mbatizaji, kuhani wa mwisho wa mwanadamu. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo 11:11 “Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kulko yeye.” Ni mwakilishi pekee wa wanadamu. Alimtuma Yohana kama mwakilishi wa wanadamu wote ili aweze kumbatiza Yesu kwa kumtwika dhambi za dunia.
Ikiwa watu bilioni sita ulimwenguni watakwenda mbele za Yesu na kumwekea mikono ili kumtwika dhambi zao, nini kingetokea katika kichwa chake? Ikiwa zaidi ya watu bilioni sita ulimwenguni wakimwekea mikono Yesu, ingekuwa ni mahala pa ajabu. Wale walio wakereketwa wangeweza kumkandamiza kwa nguvu zaidi kiasi cha kumng’oa nywele! Hivyo basi katika hili kwa Hekima ya Mungu alimteua Yohana ili awe mwakilishi na kumtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu, mara moja na kwa nyakati zote.
Imeandikwa katika Mathayo 3:13. “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Jordan kwa Yohana ili abatizwe.” Na hii ilikuwa wakati Yesu ana umri wa miaka 30. Alitahiriwa akiwa na umri wa siku 8 baada ya kuzaliwa na kuanzia hapo hapakuwahi kuwa na kumbukumbu za habari zake hadi umri wa miaka 30. 
Sababu za Yesu kusubiri kuitimiza miaka hiyo 30 ilikuwa aweze kutimiza umri wa kisheria wa kuwa Kuhani mkuu Mbinguni kulingana na Agano la Kale. Katika Kumbukumbu la Torati, Mungu alimwambia Musa ya kwamba Kuhani Mkuu anapaswa awe kati ya miaka 30 kabla ya kupewa huduma ya Ukuhani. Yesu alikuwa kuhani wa Mbinguni aliye Mkuu. Je, waamini hili?
Katika Agano Jipya, Injili ya Mathayo 3:13-14 inasema, “Wakati huu Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordan kwa Yohana ili abatizwe lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” Ni nani mwakilishi wa wanadamu? Yohana Mbatizaji. Na ni yupi aliye mwakilishi wa Mbinguni? Yesu Kristo ndiye. Wawakilishi hawa walikutana. Sasa ni yupi aliye juu zaidi? Hakika ni yule wa Mbinguni ndiye aliye Mkuu zaidi.
Hivyo Yohana Mbatizaji, aliyekuwa jasiri kupaza sauti kwa viongozi wa dini kwa wakati huo, “Enyi wazao wa nyoka!” ghafla alinyenyekea mbele za Yesu, “mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”
Katika hatua hii, Yesu alisema “kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Yesu alikuja ulimwenguni kuitimiza haki ya Mungu na ilitimizwa pale Yohana Mbatizaji alipombatiza. 
“Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini, na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka Mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye.”
Hivyo ndivyo ilivyo tokea wakati Yesu alipobatizwa. Milango ya Mbinguni ilifunguka alipobatizwa na Yohana Mbatizaji na kubeba dhambi zote za ulimwengu.
“Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka” (Mathayo 11:12).
Manabii wote na Sheria ya Mungu ulitoa unabii juu ya Yohana Mbatizaji. “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu na wenye nguvu wauteka.” Kila mmoja anayeamini ubatizo wa Yesu huingia katika ufalme wa Mbinguni bila pingamizi.
 
 
“Wala mimi sikuhukumu”

Kwa nini Yesu
Alihukumiwa Msalabani?
Kwa sababu alibeba
dhambi zetu zote.

Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kubeba madhambi ya ulimwengu. Na baadaye aliweza kumwambia yule mwanamke aliye fumaniwa “wala mimi sikuhukumu.” Hakumhukumu yule mwanamke kwa sababu alikwisha zibeba dhambi zote za ulimwengu katika mto Yordani yeye binafsi na si yule mwanamke tena aliye paswa kuhukumiwa kwa dhambi hizo.
Yesu alizifuta dhambi za dunia. Tunaweza kuona ni kwa namna gani ilivyo mtia hofu juu ya maumivu aliyo paswa kuvumilia pale Msalabani, kwa kuwa “mshahara wa dhambi ni mauti.” (Warumi 6:23) Alimwomba Mungu mara tatu katika mlima wa mizeituni kuipishia hukumu hiyo mbali kwake. Yesu alikuwa mwenye mwili na damu kama ilivyo sisi sote,na hivyo inaeleweka kwamba alitishika na maumivu. Ilimpasa Yesu atoe damu ili kutimiza hukumu.
Kama ilivyo sadaka ya dhambi katika Agano la kale ilvyo paswa kutoka damu kulipia dhambi pia yeye ilimpasa atolewe sadaka pale Msalabani. Alikwisha zibeba dhambi za ulimwengu tayari na sasa ilimpasa kuyatoa maisha yake kwa ukombozi. Alifahamu hili kabla kwamba ilimpasa ahukumiwe na Mungu.
Yeye hakuwa na dhambi yoyote moyoni, lakini kama dhambi zote alizibeba katika ubatizo, basi ilimpasa Mungu kumhukumu kama Mwana wake. Hivyo mwanzoni katika hatua ya kwanza hukumu ya Mungu ilitimizwa, hatua ya pili alirejesha Upendo wake kwetu kwa wokovu wetu. Hivyo ilipasa Yesu ahukumiwe msalabani. 
“Wala mimi sikulaumu au kukuhukumu.” Dhambi zetu zote, za kudhamiria au kutodhamiria, za kujua au kutojua zilihukumiwa na Mungu.
Hata hivyo Mungu hakutuhukumu sisi, bali Yesu ndiye aliye hukumiwa kwa kubeba dhambi zetu mwenyewe kwa ubatizo wake. Mungu hakutaka kuwahukumu wadhambi kwa sababu ya Upendo wake na huruma. Ubatizo na damu ya Msalabani ulikuwa ndiyo ukombozi wa upendo kwetu, “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
Hivi ndivyo tunavyo uelewa Upendo wake. Yesu hakumhukumu yule mwanamke aliyefumaniwa. 
Alijua kuwa yeye ni mwenye dhambi kwa kuwa alifumaniwa. Hakuwa tu na dhambi moyoni, pia alizibeba mwilini. Hakuwa na jinsi ya kuzikana kwa kuwa aliamini kwamba Yesu alikwishabeba dhambi zake zote, aliweza kuokolewa. Nasi, ikiwa tutaamini ukombozi wa Yesu tutaokolewa. Amini hili! Ni kwa faida yetu.

Ni yupi mwenye Baraka zaidi?
Ni yule asiye na dhambi.

Watu wote hutenda dhambi. Wote huzini. Lakini hakuna anayehukumiwa kwa dhambi. Wote tumetenda dhambi, lakini wale wote wenye kuamini ukombozi wa Yesu Kristo hawana dhambi mioyoni mwao. Yule mwenye kuamini wokovu wa Yesu ni mwenye furaha zaidi. Wale waliokombolewa toka dhambi zao zote wamebarikiwa zaidi. Kwa maneno mengine, wamefanywa kuwa haki kupitia Yesu.
Mungu anatuambia kuhusu furaha katika Warumi 4:7 “Heri waliosamehewa makosa yao na waliositiriwa dhambi zao.” Wote tunatenda dhambi hadi kifo. Hatuna sheria na ukamilifu mbele za Mungu. Tunaendelea kutenda dhambi hata pale tunapofahamu sheria sisi ni wadhaifu.
Lakini Mungu anatukomboa kwa ubatizo na kwa damu ya Mwana wake wa pekee na kutuambia, mimi na wewe, kwamba si wadhambi tena na sasa ni wenye haki mbele zake. Anatuambia kwamba sisi ni watoto kwake.
Injili ya maji na kwa Roho ni Injili ya Ukombozi wa milele. Je, unaamini hivyo? Kwa wale wenye kuamini, Mungu huwaita kuwa wenye haki, waliokombolewa ni watoto wake. Ni yupi mwenye furaha duniani? Ni yule mwenye kuamini na amekwisha kukombolewa kwa kuamini Injili ya kweli. Je, umwekwisha kukombolewa?
Je, Yesu alisahau kuzichukua dhambi zako? La, alizichukua dhambi zote kwa ubatizo. Amini hili. Amini na uwe umekombolewa kwa dhambi zako zote. Na tusome Yohana 1:29.
 
 
Kama nisafishavyo na fagio

Ni dhambi kiasi gani
Yesu alizichukua?
Dhambi zote za
Ulmwengu.

“Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). 
“Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”
Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi za Ulimwengu kwa Yesu katika Yordani. Siku iliyofuata alishuhudia kwamba Yesu ni Mwana kondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu. Alizibeba kwenye mabega yake dhambi zote za ulimwengu.
Dhambi zote za ulimwengu, hii ina maana dhambi zote walizotenda wanadamu hapa ulimwenguni tokea kuumbwa hadi mwisho wake. Karibu miaka 2000 iliyopita, Yesu alizibeba dhambi za ulimwengu na kutukomboa. Akiwa Mwana kondoo wa Mungu, alizichukua dhambi zetu na kuhukumiwa kwa ajili yetu.
Kila dhambi ya mwanadamu anayotenda ilitwikwa kwake YESU. Alikuwa Mwana Kondoo wa Mungu achukuae dhambi zote za Ulimwengu.
Yesu alikuja ulimwenguni akiwa mtu mnyenyekevu, kama mmoja atakaye okoa wenye dhambi ulimwenguni. Tunatenda dhambi kwa kuwa sisi ni dhaifu, waovu wapumbavu, na kwa sababu tu wajinga na tusio wakamilifu. Kwa maneno mengine, tunatenda dhambi kwa sababu tumerithi dhambi toka kwa uzao wetu Adamu. Dhambi zote hizi zilisafishwa kwetu na kuwekwa juu ya kichwa cha Yesu kupitia ubatizo wake katika mto Yordani. Aliishia na yote haya katika kifo cha mwili wake Msalabani. Alizikwa lakini Mungu alimfufua toka kwa wafu katika siku ya tatu.
Alikuwa Mwokozi wa wenye dhambi kama mshindi, kama Hakimu ameketi mkono wa kuume kwa Mungu. Haitaji kutokomboa tena na tena. Yote yatupasa kumwamini yeye ili tuokolewe. Uzima wa milele unatusubiri sisi wote wenye kuamini, na uangamizi unawasubiri wale wasio amini. Hakuna chaguo lingine!
Yesu amewakomboa ninyi nyote. Nanyi ni wenye furaha zaidi ya wote ulimwenguni. Hakika yawezekana ukatenda dhambi baadaye kwa sababu ya udhaifu wako,lakini pia hizi nazo alizibeba.
Je, una dhambi iliyo baki moyoni? -Hapana.-
Je, Yesu ilzichukua zote? –Ndiyo- Alichukuwa.
Watu wote ni sawa. Hakuna aliye Mtakatifu zaidi ya jirani yake. Lakini wengi wenye unafiki, huamini kwamba wao hawana dhambi,hali ni wenye dhambi pia. Ulimwengu huu ni mahali penye rutuba ya dhambi, kijani kibichi.
Wakati wanawake wanapotaka kutoka matembezini, hujipaka rangi ya mdomo, poda, kutengeneza nywele zao, huvaa nguo maridadi na viatu virefu kisigino… Wanaume nao huenda kwa vinyozi kupunguza nywele zao, kujisafisha kuvaa shati safi na tai maridadi na kung’arisha viatu vyao.
Lakini wanapo onekana wana wa mfalme kwa nje, ndani yao ni wenye uchafu.
Je, fedha yaweza kumfanya mtu awe mwenye furaha? Afya yaweza kumfanya mwenye furaha? La, Ukombozi wa milele pekee, msamaha wa dhambi zote, ndiyo umfanyao mtu awe mwenye furaha ya kweli. Haijalishi ni kwa kiasi gani mtu anaweza kuonekana kwa nje, mtu huyo ni hovyo kabisa mwenye dhambi moyoni, na huishi maisha ya kuogopa hukumu.
Aliyekombolewa ni mwenye ujasiri kama simba, hata akiwa matambara. Hapana dhambi moyoni mwake. “Nakushukuru Bwana, ulimwokoa mwenye dhambi kama mimi. Ulizifuta dhambi zangu. Najua sikustahili kupokea upendo wako, lakini nakusifu kwa kuniokoa. Nimekombolewa milele dhambi zangu zote. Utukufu kwako Mungu.”
Mtu aliye kombolewa hakika ni mwenye furaha. Aliyebarikiwa kwa Neema ya Mungu ya ukombozi ni mwenye furaha sana.
Kwa kuwa Yesu “Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi ya Ulimwengu,” alikwisha chukua dhambi zetu zote, hatuna tena dhambi. “Amemaliza” wokovu wetu katika Msalaba. Dhambi zetu zote, zangu na zako zimejumuishwa kwenye dhambi za ulimwengu na hivyo wote tumeokolewa.
 
 
Kwa Mapenzi ya Mungu

Je, tuna dhambi moyoni
tunapokuwa ndani ya Yesu?
Hapana, hatuna.

Rafiki wapendwa, yule mwanamke aliyefumaniwa aliamini maneno ya Yesu na aliokolewa. Habari hii imeandikwa kama kumbukumbu katika Biblia kwa kuwa mwanamke huyu alibarikiwa kwa ukombozi ule wa milele. Hata hivyo wale wanafiki, Waandishi na Mafarisayo walitoweka mbele za Yesu.
Ikiwa utamwamini Yesu ni mbingu ikusubiriayo, lakini ukimkimbia utaishia motoni (jehanamu) Ukiamini matendo yake ya haki, ni sawa na mbingu na usipoamini kazi zake, hii ni jehanamu. Ukombozi si jitahada ya mtu binafsi awaye yote, bali ni kwa wokovu wa Yesu.
Na tusome Waebrania 10:1-10, “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi kwa wakati wote kuwakamilisha wakaribiao, kama ndivyo, Je, Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo lipo kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni asema, dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari. Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hakupendezwa nazo, Ndipo mliposema, Tazama nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi kuhuzitaka, wala hakupendezwa nazo, (zitolewazo kama ilivyoamuru torati) Ndipo aliposema, Tazama, mmekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu!” (Waebrania 10:1-10).
“Kwa mapenzi ya Mungu” Yesu aliyatoa maisha yake kubeba dhambi zetu zote kwa mara moja, na alihukumiwa kwa zote na kufufuka.
Hivyo tumetakaswa. “Mmepata utakaso” (Waebrania 10:10) imeandikwa kama tendo la nyakati iliyopita linaloendelea kwa nyakati iliyopo sasa. Ni kitendo kilichofanyika hapo zamani na ambacho kinaendelea hadi leo hii. Hii ina maana kwamba ukombozi wetu ulikamilika wote, na hauhitaji kufafutwa tena mmepata utakaso.
“Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya Ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu, tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa” (Waebrania 10:11-14). 
Nyinyi nyote mmetakaswa milele. Je, ukitenda dhambi kesho, utakuwa mwenye dhambi tena? Je, Yesu alizichukua dhambi hizo pia? Alizichukua. Alizichukua dhambi hata za nyakati zijazo pia.
“Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia kwa maana baada ya kusema, Hili ni agano nitakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao. Na katika nia zao, nitaziandika ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao, sitaukumbuka tena kabisa. Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya Dhambi” (Waebrania 10:15-18).
Yesu ni Mwokozi kwetu sisi sote, mimi na wewe. Mwamini Yesu alituokoa. Huu ni ukombozi katika Yesu na neema kuu na zawadi toka kwa Mungu mimi na wewe, tuliokombolewa na dhambi zetu zote ndiyo tuliobarikiwa zaidi.