(Mathayo 3:13-17)
“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akamjibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi alikubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua. Akija juu yake, na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.”
Je, Kuna yeyote ambaye bado anasumbuka kwa dhambi?
Je, kifungo chetu
cha dhambi kilikwisha?
Ndiyo.
Bwana Mungu wetu alizikata pingu za dhambi kwa watu wote. Wale wote wenye wakati mgumu chini ya dhambi zao ni watumwa wa dhambi hizo; lakini kwa ukombozi wake, Bwana wetu alizikata hakika. Aliziondoa dhambi zetu zote Je, kuna yeyote ambaye bado anasumbuka kwa dhambi?
Tunapaswa kuelewa vita yetu dhidi ya dhambi ilikwisha hatutosumbuka kwa dhambi tena. Kifungo chetu cha dhambi kilikwisha pale Yesu alipotukomboa kwa ubatizo na damu yake. Dhambi zetu ndipo zilipoishia hapo. Mwana wa Mungu alijitoa kwa dhambi zetu. Mungu alizilipia zote kupitia Yesu aliyetuacha huru milele.
Je, unajua ni kwa kiasi gani watu huteseka kwa dhambi zao? Ilianzia kwa Adamu na Hawa Mwanadamu huteseka kwa dhambi ya urithi toka kwa Adamu.
Lakini Mungu wetu aliweka agano lililoandikwa katika kitabu cha Mwanzo 3:15, na agano hili lilikuwa kwamba Yeye atawakomboa wenye dhambi wote. Alisema kwamba watu watakombolewa na dhambi zao kupitia sadaka ya Yesu Kristo kwa maji na kwa Roho. Wakati ulipowadia, Mungu alimtuma Mkombozi, Yesu, ili aishi kati yetu.
Pia aliahidi kumtuma Yohana Mbatizaji kabla ya Yesu, hakika alitimiza ahadi hii.
Marko 1:1-8 Inasema “Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo’ Mwana wa Mungu kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako, atakaye itengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana yaonyesheni mapato yake. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, Nao wa Yerusalemu wote wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Na Yohana alikuwa amevaa singa na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Akahubiri akisema, yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kulikoni mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi nilibatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”
Yohana Mbatizaji kama Shahidi na Mhamasishaji wa Injili
John Mbatizaji ni nani?
Kuhani Mkuu wa mwisho na Mwakilishi
wa wanadamu wote.
Neno ubatizo kwa Kigiriki “baptizo” maana yake ni “zamisha”, lakini pia lina maana ya “kusafishwa. Wakati Yesu alipobatizwa, haki ya Mungu ilitimizwa “Haki” kwa Kigiriki ni “dikaiosune” na maana yake ni “kuwa mustahiki wa jambo” na pia “kuendesha jambo kwa kufuata inavyostahiki, uadilifu, uangalifu wa sawa, sahihi ndivyo, barabara sawasawa.”
Yesu alibatizwa ili aweze kuja kuwa Mwokozi katika hali iliyostahiki. Na hivyo, wale wote wenye kuamini ubatizo wake na msalaba kupokea zawadi ya ukombozi toka kwa Mungu.
Katika Agano Jipya, Yohana Mbatizaji ndiye Kuhani Mkuu wa mwisho wa Agano la Kale. Hebu na tuangalie Mathayo 11:10-11. Maandiko husema kwamba Yohana Mbatizaji ni mwakilishi wa wanadamu na kama Kuhani Mkuu katika kipindi cha Agano Jipya, alimwekea dhambi zote za ulimwengu Yesu. Hivyo kufanya huduma ya ukuhani mkuu kama ute wa kipindi cha Agano la Kale wa Haruni.
Binafsi Yesu alishuhudia juu ya Yohana mwenyewe. Alisema haya katika Mathayo 11:13-14 “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja,” kwa hiyo, Yohana Mbatizaji aliye mbatiza Yesu alikuwa ni wa uzao wa Kuhani Mkuu Haruni na ni kuhani Mkuu wa mwisho. Biblia pia inatushuhudia ya kuwa Yohana alikuwa ni wa uzao wa Haruni katika Agano la kale (Luka 1:5; Mambo ya Nyakati 24:10).
Sasa ni kwa sababu ipi Yohana aliishi nyikani akiwa peke yake, akivalia mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia? Ilikuwa ni kudhihirisha Ukuhani Mkuu. Akiwa mwakilishi wa wanadamu wote, Yohana Mbatizaji hakupaswa kuishi kati ya watu. Hivyo alipaza sauti kwa watu “Enye wazao wa nyoka, tubuni” na aliwabatiza kwa tunda la toba ili kuwarejesha kwa Yesu atakayeondoa dhambi zao zote. Juu ya yote, Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi za ulimwengu kwa Yesu kwa ajili ya wokovu alipomwekea mikono juu ya kichwa chake.
Aina mbili za Ubatizo
Kwa nini Yohana Mbatizaji
Aliwabatiza watu?
Kuongoza watu katika toba ya
Dhambi zao na kuamini ubatizo
wa Yesu kwa wokovu wao.
Yohana Mbatizaji aliwabatiza watu na baadaye Yesu. Huu wa kwanza ni “Ubatizo wa toba” unaowaita wenye dhambi kwa Mungu. Watu wengi waliosikia wito huu wa Mungu kupitia Yohana aliziacha sanamu zao na kumrudia.
Ubatizo wa pili ulikuwa ni wa Yesu, ubatizo ulio mbebesha dhambi za Ulimwengu zote. Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kuitimiza haki ya Mungu. Kwa maneno mengine, Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili kuwaokoa watu kwa dhambi zao zote (Mathayo 3:15).
Kwa nini Yohana ambatize Yesu? Ili kufuta dhambi za Ulimwengu, Mungu aliruhusu Yohana kumbebesha Yesu dhambi ili kwa kila mtu atakayemwamini Yesu aweze kuokolewa.
Yohana Mbatizaji alikuwa ni Mtumishi wa Mungu ambayye mpango wake uliwekwa ili kumtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo na kushuhudia juu ya Yesu ili wanadamu wote watubu na kutakaswa dhambi zao kwa kuamini Injili ya Ukombozi. Hivyo, Yohana alimpasa kuishi mwenyewe nyikani. Katika kipindi cha Yohana Mbatizaji, watu wa Israeli wote walikuwa waovu na waliooza kinani.
Hivyo Mungu akasema katika Agano la Kale, Malaki 4:5-6 “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya naye ataigeuza mioyo ya Baba iwalekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”
Mbele ya macho ya Mungu, watu wote wa Israeli waliomwabudu Yehova walikuwa waovu. Hakuna aliyekuwa mwenye haki mbele zake. Viongozi wa dini hekaluni, kwa mfano, Makuhani, wanasheria, waandishi wao hasa ndiyo walionza kwa kina zaidi Waisraeli pamoja na makuhani wao hawakuweza kumtolea Mungu dhabihu iliyo njema kulingana na sheria yake.
Makuhani waliacha kuwekea mikono na kafara za sadaka za damu ambazo Mungu aliamuru kwa upatanisho wa madhambi. Imeandikwa kwamba Makuhani katika kipindi cha Nabii Malaki waliacha mfumo wa sheria ya utoaji dhabihu, kuwekea mikono na kutoa sadaka ya damu ya mnyama wa kafara.
Kwa hivyo Yohana Mbatizaji hakuweza kukaa nao. Alikwenda nyikani na kupaza sauti huko. Alisema nini?
Imeandikwa katika Marko 1:2-3 ikinukuu maneno ya Nabii Isaya “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakayetengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani itengenezeni njia ya Bwana yanyosheni mapito yake.”
Sauti iliayo nyikani ikiwaambia watu juu ya ubatizo na toba. Nini maana ya “Ubatizo na toba” ambao Biblia inazungumzia? Ni ubatizo ambao Yohana Mbatizaji aliupigia kelele; ubatizo uliowaita watu kumrudia Yesu ili wakimwamini yeye azichukuaye dhambi zao wataweza kuokolewa. Ubatizo wa Toba uliwaongoza kwenye wokovu.
“Tubuni na kubatizwa. Mwokozi wetu Yesu atabatizwa kwa njia hiyo ili kuzichukua dhambi zetu zote.” Wito wa Yohana Mbatizaji ulikuwa kwamba Yesu atazichukua dhambi za ulimwengu na kuhukumiwa msalabani ili kuokoa watu wote ili waweze kurudishwa kwa upatanisho mbele za Mungu.
“Mimi niliwabatiza kwa maji, bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu” (Marko 1:8). Maana yake “kuosha.” Ubatizo wa Yesu katika mto Yordani unatuelezea juu ya Mwana wa Mungu alibatizwa na kubeba dhambi zetu zote ili kutuokoa.
Hivyo yatupasa kuyageuzia mgongo maisha yetu ya dhambi na kumwamini Yesu. Ni Mwana kondoo, azichukuaye dhambi za ulimwengu. Hii ni Injili ya ukombozi ambao Yohana Mbatizaji alishuhudia.
Jukumu la Kuhani Mkuu katika Upatanisho wa Madhambi
Nani aliyetayarisha
njia ya wokovu?
Yohana Mbatizaji.
Nabii Isaya alitoa unabii “Semeni na Moyo wa Yerusalemu, kuambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa umepokea kwa mkono wa Bwana adhabu mara dufu kwa dhambi zake zote” (Isaya 40:2).
Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zoto pasipo kuchagua dhambi za asili, dhambi za wakati huu na hata zile za wakati ujao zilisafishwa kupitia ubatizo wake. Alitukomboa sisi sote. Yatupasa kuelewa vyema juu ya ukombozi wa Mungu.
Ili kuokolewa na dhambi zetu, yatupaswa kuamini injili isemayo kwamba, Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote kwa kupitia njia ya ubatizo.
Hatupaswi kuelewa vibaya ya kwamba “ukiwa Mungu ni upendo, tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni kwa kumwamini Yesu tu hata kama tunazo dhambi mioyoni mwetu.”
Ili kukombolewa na dhambi zako zote, yakupasa kuamini ubatizo wake, ambao kupitia Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi za ulimwengu na pia kuamini Msalaba. Ni kwa njia ya “Maji” Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote za wanadamu.
Jambo la awali Mungu alilofanya katika kutuokoa lilikuwa ni kumtuma Yohana ulimwenguni. Akiwa mjumbe wa Mungu, Yohana Mbatizaji alitumwa kama balozi wa Mfalme, aliye mtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo. Alihudumu katika nafasi ya ukuhani mkuu zaidi ya wanadamu wote.
Mungu alisema yakwamba atamtuma mjumbe wake, Yohana Mbatizaji kwetu.
“Namtuma mjumbe mbele ya uso wako” Mbele ya uso maana yake ni kabla ya Yesu. Kwa nini Mungu alimtuma Yohana kabla ya Yesu? Ili kuzitwika dhambi zote za dunia juu ya Yesu mwana wa Mungu kwa ubatizo. “atakayeitengenezea njia yako” Na hii ndiyo maana halisi ya ujumbe huu.
Ni nani yule aliyetayarisha njia ili tukombolewe na kwenda Mbinguni? Yohana Mbatizaji. “Mbele ya” huyu ni Yesu, na “namtuma” huyu ni Mungu mwenyewe. Hivyo mwenyewe. Hivyo anaposema “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako,” maana yake nini?
Ni nani anayepaswa kutayarisha njia yetu ya kwenda Mbinguni? Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zetu zote kwa Yesu ili tuweze kuamini kwamba alizisafisha zote kwa kazi ile ya ubatizo wa Yesu Kristo. Ni Yesu na Yohana ndiyo waliofanikisha yote haya kwetu ili tuweze kuamini ile kweli na kukombolewa.
Wokovu wetu hutegemea nini? Hutegemea ikiwa kwamba tunaamini matendo haki ya Yesu, Mwana wa Mungu na ukweli kwamba mjumbe wa Mungu Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zote za ulimwengu juu ya Yesu. Wote yatupasa kuielewa Injili ya msamaha wa dhambi. Mungu Baba alimtuma mjumbe wake awali, ambaye yeye angembatiza Mwana wake, na kumfanya kuwa mwakilishi wa wanadamu. Kwa maana hii alikamilisha ile kazi ya ukombozi wetu.
Mungu alimtuma mtumishi wake Yohana Mbatizaji ili ambatize mwana wake ili atayarishe njia ya wokovu kwa wale watakao mwamini Yesu. Na hii ndiyo sababu Yohana kumbatiza Yesu. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji ulikuwa ni kuitimiza kazi ya ukombozi wa Mungu, ambapo dhambi zote za wanadamu alitwikwa Yesu ili wote wamwaminio waweze kuingia mbinguni.
Hata zile dhambi tutakazotenda mbeleni zilitwikwa kwa Yesu kupitia ubatizo huu. Yesu na Yohana Mbatizaji kwa pamoja walihusika kutayarisha njia ya kwenda Mbinguni kwetu. Kwa njia hii, Mungu alitufunulia siri ya ukombozi kupitia Yohana Mbatizaji.
Akiwa ni mwakilishi wa wanadamu, Yohana alimbatiza Yesu ili tuweze kuamini ukombozi wetu na kwenda Mbinguni. Alimtwika Yesu dhambi zote kupitia ubatizo. Hii ni habari njema ya kufurahisha juu ya ukombozi wetu.
Kwa nini Yohana Mbatizaji alizaliwa?
Kupitia nani tunaweza
Kumwamini Yesu?
Yohana Mbatizaji.
Katika Malaki 3:1 imeandikwa “Angalieni namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu” Yakupasa usome Biblia kwa makini. Kwa nini Mungu alimtuma mjumbe mbele ya Yesu? Kwa nini Yohana alizaliwa miezi 6 kabla ya Yesu?
Yatupasa kuielewa Biblia ina maana gani? Agano la Kale inaelezea jukumu la Kuhani Mkuu Haruni. Haruni alikuwa ni kaka mkuu kwa Musa Mungu alimpaka mafuta (alimsimika) yeye na watoto wake kuwa makuhani. Walawi wengine walifanya kazi chini yake, kumletea vyombo vilivyoteuliwa, kuchanganya siagi ya mkate na mengineyo, wakati watoto wa Haruni wakitoa dhabihu ndani ya hekalu takatifu.
Watoto wa Haruni walipakwa mafuta katika kufanya kazi kwa usawa kati yao, lakini katika siku ya Upatanisho, siku ya kumi ya mwezi wa saba; Kuhani Mkuu pekee ndiye aliyeruhusiwa kutoa dhabihu ya upatanisho wa dhambi za mwaka mzima kwa niaba ya watu wake.
Katika Luka 1:5 ipo habari ya uzao wa Yohana Mbatizaji. Yatupasa kwa makini kuelewa ujumbe wa Mungu ili tumwelewe Yesu, sawa sawa. Huwa tunajaribu kufikiri mengi sana juu ya Yesu lakini tunapuuzia zaidi juu ya Yohana Mbatizaji, ambaye alikuja kabla ya Yesu. Ningependa kwa hili nijaribu kukuelewesha.
“Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako atakayeitengeneza njia yako” (Marko 1:1-2). Injili ya Mbinguni nyakati zote huanza kwa Yohana Mbatizaji.
Tunapojifunza kwa ukamilifu juu ya Yohana Mbatizaji ndipo tunapoelewa kwa uwazi na kuamini Injili ya ukombozi wa Yesu. Ni sawa na kuwasikiliza mabalozi tuliowatuma duniani poti ili tuweze kuelewa juu ya hali ya mataifa yote. Tunapofahamu juu ya Yohana Mbatizaji, tunaweza kuelewa vizuri zaidi juu ya ukombozi wa Mungu.
Ni kwa namna gani ni masikitiko makubwa kwa wakristo walio wengi katika nyakati hizi hawajaona umuhimu wa Yohana. Mungu hakumtuma Yohana Mbatizaji kwa sababu alikuwa amechoka na hakua na la kufanya zaidi ya kumtuma. Injili zote katika Agano Jipya zimezungumzia juu ya Yohana Mbatizaji kabla ya kuzungumzia ukombozi wa Yesu.
Yakushangaza, wainjilisti wengi nyakati hizi humpuuza kabisa na kuwaambia watu wamwamini Yesu tu inatosha na wataokoka. Ukweli ni kwamba, huwaongoza watu kuendelea kuwa wenye dhambi maishani mwao pote na kuishia motoni. Ikiwa Wakristo wote watamwamini Yesu tu bila kuelewa jukumu la Yohana Mbatizaji, Ukristo utakuwa na kasoro na kuwa kama dini nyingine za duniani utakombolewa vipi kwa dhambi zako ikiwa hutaki kuelewa ukweli? Si rahisi!
Injili ya ukombozi sivyo ufikiriavyo wewe kwa wepesi na urahisi huo. Kwani watu wengi hudhani ukombozi huwa umewekwa kwa imani katika Msalaba kwa kuwa Yesu alikufa juu yake kwa ajili yetu. Ikiwa utaamini hilo tu katika kusulubiwa kwake bila ya kuelewa kweli yote juu ya kutwikwa kwa dhambi, hakika imani aina hii haitakupeleka katika ukombozi ulio kamili bila kujali imani yako ni imara vipi.
Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji ili kuufanya ulimwengu kutambua juu ya ukombozi utakaokwenda kubeba dhambi zote za dunia. Hii ni pale tu tutakapojua ukweli wote ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, aliyezichukua dhambi zetu zote.
Yohana Mbatizaji ndiye atuelezaye ukweli juu ya ukombozi. Anatuelezea ni kwa vipi alikuja kushuhudia juu ya Yesu kuwa ni Mungu na Nuru ya ukweli. Kwa uwazi yeye mwenyewe alikataa kuwa ndiye huo mwanga, bali ni mshuhudiaji wa mwanga. Alishuhudia katika Yohana 1 kuwa yeye amekuja kutayarisha Injili ya ukombozi kwa kumbatiza Yesu Kristo.
Kama tusingekuwa na ushuhuda juu ya ukombozi kupitia Yohana Mbatizaji tungeamini vipi juu ya Yesu? Hatukuwahi kumwona Yesu, na tumetoka katika tamaduni na dini mbalimbali, ingewezekanaje kuamini Yehova kuwa ndiye Mungu wetu.
Kuwa na dini mbalimbali duniani pote, ingewezekanaje kumjua Yesu Kristo? Tungefahamu vipi kuwa Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu, aliyetukomboa kwa kuchukua dhambi za ulimwengu juu yake?
Yatupasa kuangalia ndani ya Agano la Kale na kutafuta maandiko juu ukombozi tokea mwanzo kujua kwamba Yesu ni Mwokozi. Yatubidi kupata ufafahamu sahihi ili kuwa na imani iliyo ya kweli. Hakika hatoweza chochote bila kuwa na ufahamu wa kweli. Ili uweze kumwamini Yesu na uokolewe, itakubidi kujua Injili ya ukombozi ambayo Yohana Mbatizaji aliishuhudia na nafasi yake katika hilo. Ili kuweza kuwa na imani iliyokamilika katika Kristo yatupasa kufahamu ukweli juu ya ukombozi.
Hivyo, kama Yesu alivyo sema “na utajua ile kweli na itakuacha huru” (Yohana 8:32) yatupasa kuelewa kweli ya ukombozi wa Yesu.
Uthibitisho wa Biblia
Katika kipengele kipi
Injili imeanzia?
Katika ujio wa
Yohana Mbatizaji.
Hebu na tuendelee na ugunduzi wa ukweli wa ukombozi katika Biblia. Na tuweke wazi ni juu ya hizi Injili nne zinazungumzia juu ya Yohana Mbatizaji, alikuwa ni nani, na ni kwa nini aliitwa “mwakilishi wa wanadamu” au “kuhani mkuu wa mwisho” kwa namna gani dhambi za ulimwengu alitwikwa Yesu kupitia yeye, na endapo kama Yesu alizichukua dhambi zetu zote au la.
Yatupasa kuwa makini ili hakika Injili zote nne zianzie na Yohana Mbatizaji. Yohana 1:6 inaongelea juu ya moja ya ukweli ulio muhimu katika Injili. Inatuelezea juu ya nani aliyefanya kazi ya kutwikwa dhambi zote za ulimwengu kwa Yesu “Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Hivyo alikuja kushuhudia ile nuru wote wapate kuamini kuwa yeye” (Yohana 1:6-7).
Inasema “wote wapate kuamini kwa yeye” na ndiyo maana “alikuja kushuhudia ile nuru” Nuru ni Yesu Kristo. Ina maana kwamba Yohana alishuhudia juu ya Kristo ili wote waweze kumwamini kupitia yeye. Na hebu tuangalie kwa karibu katika Mathayo sura ya 3.
Katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe, lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwani ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote. Basi akamkubali Naye Yesu alipokwisha kubatizwa akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama ua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, ‘Huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naya’”
Kwa nini yatupasa kuelewa
juu ya uzao wa Yohana?
Kwa sababu Biblia inatueleza
juu ya Yohana kuwa ni Kuhani
Mkuu wa wanadamu.
Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kukamilisha msamaha wa dhambi zote za Ulimwengu. Ubatizo Yesu alioupata kutoka kwa Yohana ulikuwa na umuhimu mkubwa katika tukio la wokovu wetu. Na ili uweze kuelewa na kuamini ukweli wote kwa ujumla na kwa undani zaidi, yatupasa kwa karibu kujifunza juu ya Yohana Mbatizaji kwanza.
Katika Luka 1:1-14 “Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyohimizwa katikati yetu kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu upate kujua hakika ya mambo yale yaliyofundishwa. Zamani za Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na Kuhani mmoja jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya na mkewe alikuwa mmoja wapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Basi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia . Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule Malaika akamwambia, usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikia na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.”
Hapa, Luka mwanafunzi wa Yesu, anatueleza kwa undani juu ya uzao wa Yohana. Luka, mwanafunzi wa Yesu ameelezea uzao wa Yohana toka mwanzo Luka alimhubiria Injili mtu aitwaye Theofilo ambaye ni kutoka utamaduni tofauti naye na hakufahamu juu ya Bwana.
Na ili kumfundisha juu ya Yesu mwokozi wa wenye dhambi, Luka aliona umuhimu wa kuelezea kizazi cha Yohana Mbatizaji kwa undani. Nasi kama watu wa Mataifa toka jamii tofauti, hatuwezi kuelewa wokovu wa Yesu ikiwa hatutaelezewa kwa umuhimu hatua kwa hatua. Hebu tuangalie undani huu ni upi.
Katika Luka 1:5-9 inafafanua “zamani za Herode, mfalme wa Wayahudi palikuwa na Kuhani mmoja jina lake zakaria, wa zamu ya Abiya na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana la maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Basi ikawa walipokuwa wakifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, kama ilivyo desturi ya ukuhani, kura ikamwangukia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.”
Hapa jambo la ghafla lilimtokea Zakaria wakati akimtumikia Mungu kulingana na desturi ya ukuhani. Luka anashuhudia wazi kwamba Zakaria alikuwa wa uzao wa Haruni. Na ni katika kundi lipi akitokea? Hii ndiyo muhimu zaidi.
Alieleza “Basi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu.” Tunaweza kuona kwamba Luka alimfahamu Zakaria vizuri zaidi kwa kuelezea Injili ya ukombozi kwa kumtaja yeye na mke wake Eliabeti.
Yohana Mbatizaji alizaliwa kwa Zakaria na mkewe Elizabethi aliyekuwa bintiye Haruni sasa, na tuangalie uzao wa Zakaria, baba yake Yohana.
Ukoo wa Yohana Mbatizaji
Yohana Mbatizaji
alikuwa wa uzao wa nani?
Haruni, Kuhani Mkuu.
Ili kuelewa ukoo wa Yohana Mbatizaji yatupasa kusoma katika kitabu cha Agano la Kale 1 Nyakati 24:1-19.
“Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu na Abihu, na Eleazari na Ithamani. Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamani wakafanya Ukuhani. Akawagawanya Daudi na Sadoke wa wana wa Eleazari na Ahimeleki wa wana wa Ithamani katika utumishi wa kadiri ya usimamizi wao. Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Ithamani; wakagawanyika hivi, wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wana wa Ithamari sawasawa na mbari za baba zao, wane. Ndivyo walivyogawanyika kwa kura wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu wana wa Eleazari na wana wa Ithamani pia. Naye Shemaya, wana wa Nethaneli, mwandishi aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme na mbele ya wakuu na Sadiki kuhani, na Ahimeleki mwana wa Abiathari na wakuu wa mbari za baba za Makuhani, na za Walawi ikatwaliwa ya Ithamari kura ya kwanza, ikamtokea Yehoiaribu na ya pili Yedaya; ya tatu Harimu ya nne Seorimu ya tano Malkia ya sita Miyamini ya saba Hakosi ya nane Abia ya kenda Yeshua ya kumi Shekania ya kumi na moja Eliashibu ya kumi na mbili Yakimu ya kumi na tatu hapa, ya kumi na nne Yeshebeabu; ya kumi na tano Bilga ya kumi na sita Imari ya kumi na saba Hezuri, ya kumi na nane Hapisesi, ya kumi na kenda Pethahia ya Ishirini Ezekieli, ya ishirini na moja Yakini ya Ishirini na mbili Gamuli, ya ishirini na tatu Delaya ya Ishirini na nne Maazi. Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, kama Bwana Mungu wa Israeli alivyomwamuru.”
Na tusome mstari wa 10 tena “ya saba Hokoso ya nane Abia” Katika siku za Mfalme Daudi palikuwapo na idadi ya Makuhani, hivyo palikuwa na hitaji la kuweka taratibu ya mpango wa huduma. Hivyo Daudi alipiga kura kwa kila mtoto wa Haruni ili dhabihu zeweze kutolewa katika mpangilio (kama wote mjuavyo, Haruni alikuwa kaka yake mkubwa Musa. Mungu alimchagua Musa kama wakala, na Haruni kuwa Kuhani Mkuu wa Hema Takatifu mbele ya watu wa Israeli).
Walawi wote walikuwa chini ya Haruni na Makuhani, watoto wake wa kiume, ili kusimamia dhabihu zote mbele ya Mungu. Kabla Daudi hajapiga kura, Makuhani waliokuwa uzao wa Haruni, iliwapasa kupiga kura kila wakati na ilileta kutoelewana.
Hivyo, Daudi aliandaa mpangilio kwa kuweka kila kundi katika mpangilio. Palikuwa na makundi 24 kwa mpangilio kuanzia wajukuu wa Haruni na wanane alikuwa Abiya. Ilisemekana “palikuwa na Kuhani mmoja, jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.” Hivyo Zakaria alikuwa ni Kuhani wa kundi la Abiya na wote wawili walikuwa uzao wa Haruni Kuhani Mkuu.
Alikuwa ni Zakaria, Kuhani wa kundi la Abiya ambaye alikuwa Baba yake Yohana Mbatizaji. Kutokana na Biblia tunaelewa ya kwamba walikuwa wakioana kati ya familia za kikuhani.
Hivyo Yakobo chukua mke kwa mjomba wake kwa upande wa mama yake. Kwa ufafanuzi huu wa ukoo hii ndiyo misingi muhimu. Inasema “palikuwa na Kuhani mmoja, jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.”
Hivyo, alikuwa bila shaka uzao wa Haruni. Zakaria alikuwa ni nani? Baba yake Yohana Mbatizaji. Huu ni ukweli muhimu kuelezea ukombozi wa Yesu na huduma ya Yohana Mbatizaji na kumtwika Yesu dhambi za ulimwengu.
Ni watoto wa kiume wa Haruni pekee ndio Watahudumu kama Makuhani
Ni nani aliyeruhusiwa
kuhudumia kama kuhani katika
kipindi cha Agano la kale?
Haruni na katika aliowachagua
kizazi chake.
Hivyo, ni wapi katika Biblia inasisitiza kwamba watoto wa kiume wa Haruni walipaswa kuhudhuria wakiwa Makuhani? Hebu tupaangalie.
Katika Hesabu 20:22-29. “Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima wakafikilia mlima wa Hori. Bwana akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia Haruni alikusanywa awe pamoja na watu wake kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu niliasi kinyume cha neno la langu hapo penye maji ya Meriba. Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hari umvue Haruni mavazi yake ukamvike Eleazari mwanawe mavazi yako; kasha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. Musa akafanya kama Bwana alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote. Kisa Musa akamvua Haruni mavazi yake akamvika mwanawe Elezari mavazi yake, hayo. Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakatelemka mlimani. Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa wakamwombolea Haruni muda wa siku thelathini, maana nyumba yote ya Israeli ikamwombolea.”
Katika kitabu cha kutoka, sheria ya Mungu iliandikwa kwamba watoto wa kiume wa Haruni, Kuhani Mkuu ndio watakao shika wadhifa wa Ukuhani, na mmoja kati yao atakayechaguliwa ndiye atakaye chukua nafasi ya ukuhani mkuu kama ilivyokuwa kwa Baba yake kama wote wakifikia umri wa miaka 30.
Kutoka 28:1-5 “Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye miongoni mwa wana wa Israeli, ili amtumikie katika kazi ya ukuhani, Haruni na Nadabu, na Abihu na Eleazari na Ithamani, wana wa Haruni Nawe utamtamfanya Haruni ndugu yako mavazi matakatifu kwa utukufu na kwa uzuri. Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima niliowajaza na roho ya hekima waufanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani. Na mavazi watakayoyafanya ni haya; Kifuo cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urimbo; na kilemba na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo na wanawe mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau na ya rangi nyekundu na nguo ya kitani nzuri.”
Mungu alimwelekeza Haruni kaka yake Musa kwa uwazi wote juu ya ukuhani. Ukuhani haukuwa wazi kwa yeyote yule. Mungu alimwagiza Musa kumtakasa Haruni kama Kuhani Mkuu na kumtengenezea vazi rasmi kwa ajili yake kulingana na maagizo yake. Yatupasa kutosahau maagizo ya Mungu.
Pia katika kitabu cha Kutoka 29:1-9 “Nawe uwafanyie jambo hili ili kuwatakasa, wapate kunitumikia mimi katika kazi ya Ukuhani; twaa ng’ombe mmoja mume kijana na kondoo waume wawili walio wakamilifu na mkate usiotiwa chachu, yaliyokandwa kwa mafuta, na kaki zisizotiwa chachu zilizotiwa mafuta; utazifanya za unga mzuri mwembamba wa ngano. Nawe vitie vyote katika kikapu, na uvilete ndani ya kikapu, pamoja na hiyo ng’ombe na hao kondoo wa waume wawili. Kisha mlete Haruni na wanawe hata mlangoni pa hema ya kukutania ukawaoshe kwa maji. Kisha twaa hayo mavazi ya kumtwika Haruni ilie kanzu, na joho ya naivera, na kifuko cha kifuani na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba. Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kumiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.”
Nawe uwakaze mshipi, Haruni na wanawe na kuwavika kofia…. nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu…. Mungu alisisitiza kwamba Haruni na wanawe walipaswa kutakaswa kwa kuhudumia katika ukuhani milele. Aliposisitiza kuhusu “umilele” ina maana ukuhani uliendelea kufanya kazi hata kipindi cha kuja kwa Yesu duniani.
Luka anaelezea kwa undani kwamba Zakaria alikuwa wakutoka katika kizazi cha Haruni Kuhani Mkuu. Zakaria alipokuwa akihudumu kama Kuhani wa zamu mbele za Mungu katika Hekalu la Bwana, Malaika alimtokea na kumwambia sala zake zilifika mbele za Mungu na Elisabeti mkewe atapata mtoto wa kiume.
Zakaria hakuweza kuamini, na alisema “Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi?” Kwa sababu ya shaka lake, Mungu alimfanya kuwa bubu kwa muda ili kumwonyesha ya kwamba maneno yale yalikuwa ni kweli.
Kwa wakati muafaka, mkewe alipata mimba na baadaye Bikira Mariamu naye akapata mimba. Matukio yote mawili yalitayarishwa kwa kazi ya wokovu wa Mungu. Ili kuwaokoa wanadamu waliopotoka, ilimbidi amtume mtumishi wake Yohana Mbatizaji na Mwana wake wa pekee Yesu duniani.
Hivyo, Mungu aliruhusu Mwana wake abatizwe na Yohana ili kumtwika dhambi zote za ulimwengu ili wale wote watakaomwamini yeye wataokolewa.
Uweza Pekee wa Mungu
Mungu alimtayarisha nani
Kabla ya Yesu kwa ajili
ya kazi ya Ukombozi?
Yohana Mbatizaji.
Yesu Kristo alikuwa ni Mwokozi wa wanadamu aliyezaliwa katika mwili na mwanamwali Mariamu. Mariamu alichumbiwa na Yusufu mzao wa Yuda ilimbidi Yesu azaliwe kupitia uzao wa Yuda ili kutimiza Agano la Mungu, kama ilivyo Yohana Mbatizaji ilivyompasa kuzaliwa kutoka nyumba ya Haruni, Kuhani Mkuu.
Mungu aliwatayarisha wote wawili kuzaliwa katika ulimwengu katika mpangilio huo, Yohana kabla ya Yesu. Yohana alizaliwa ili aweze kuja kumbatiza Yesu na kumtwika dhambi zote za dunia kwake. Mzawa wa Kuhani Mkuu alitoa sadaka ya upatanisho ili kutimiza Agano la Mungu alilofanya katika Agano la Kale; hii ni Injili ya ukombozi wa Yesu ambayo ilipaswa kuchukuliwa kwa usahihi ili watu wote waweze kukombolewa.
Katika kitabu cha Kutoka, Mungu aliwapa Israeli sheria yake na Maagano; sheria ya Mungu na kanuni ya matoleo ya dhabihu katika madhabahu na pia kwa undani juu ya makuhani, maelezo juu ya dhabihu na jinsi ya kurithisha ukuhani kwa watoto wa kiume wa makuhani. Mungu alimweka Haruni pamoja na uzao wake kuwa makuhani wa kudumu milele.
Hivyo wale wote walio uzao wake waliweza, kutoa dhabihu na Makuhani wakuu walipatikana kutoka katika nyumba ya Haruni tu. Je, umeona kwa nini hii ilikuwa namna hii?
Kati ya walio wengi katika uzao wa Haruni, Mungu alimchagua kuhani fulani aitwaye Zakaria na mkewe Elisabeti. Alisema “Tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Wakati Mungu alipomwambia Zakaria kwamba atamwezesha Elisabeti kuwa na mtoto na angemwita jina lake Yohana, alipatwa na mshangao sana na kuwa bubu kwa amri ya Mungu hadi pale mtoto yule mume alipopewa jina.
Hii ndivyo ilivyo, mtoto mume alizaliwa katika nyumba yake. Na ilipowadia muda wa kumpa jina kulingana na desturi za Israeli, jina lake lilipaswa aitwe kama la baba yake au moja kati ya jamaa ya ukoo.
“Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotumia, alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu akasema la sivyo; bali ataitwa Yohana. Wakamwambia hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo. Wakamwashiria babaye wajue, akaandika ya kwamba jina lake ni Yohana wakstaajabu wote. Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia akaanza kunena akimsifu Mungu. Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima ya Uyahudi. Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye” (Luka 1:57-66).
Zakaria alikuwa bado ni bubu kabla ya mtoto wake kuzaliwa. Ilipofikia wakati wa kumpa jina mtoto wake, jamaa zake walipendekeza mtoto huyo aitwe Zakaria. Lakini mama yake alimwita Yohana. Katika hili, ndugu walisema ya kwamba hapakuwa na yeyote katika ukoo wao mwenye jina hilo na hivyo ingekuwa vyema angeitwa jina la baba yake.
Wakati Elisabeti akisisitiza kumpa jina hilo, ndugu walimwendea Zakaria na kumuuliza aitwe jina gani mtoto yule. Kwa kuwa hakuweza kuongea, walimwomba kuandika kwa mkono wake katika kibao, na aliandika jina “Yohana.” Ndugu wote walishangaa kwa namna hii ya upatikanaji wa jina.
Lakini baada ya kutoa jina hili, mdomo wa Zakaria ulifunguka mara. Alimsifu Mungu na alijazwa na Roho Mtakatifu kwa kutoa unabii.
Hivi ndivyo Luka anatueleza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji katika nyumba ya Zakaria “palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria wa zamu ya Abiya.” Kwa uweza pekee wa Mungu, Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu alizaliwa kutoka kwa Zakaria mzao wa Haruni.
Kupitia Yohana Mbatizaji na Yesu Kristo, ilimlazimu Mungu kukamilisha ukombozi wa wanadamu. Tumekombolewa dhambi zetu zote kwa kuamini kazi ya ukombozi, iliyofanywa kupitia Yohana na Yesu Kristo.
Ubatizo wa Yesu
Kwa nini Yesu
alibatizwa na Yohana?
Ili kuzichukua dhambi
zote za ulimwengu.
Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba, Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu na alichukua dhambi zetu zote Alikuwa ni Yohana Mbatizaji mtumishi wa Mungu aliyetumwa kubeba ushuhuda wa wokovu wa Mungu. Haina maana kuwa Mungu hatuelezi mwenyewe ya kuwa yeye ni Mwokozi. Mungu hufanya kazi kupitia Watumishi wake Makanisani na pia katika midomo ya watu wake walio okolewa.
Mungu husema “Semeni na moyo wa Yerusalemu kauambie kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote… Majani yakauka, au lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isaya 40:2, 8).
Mungu amekwisha toa ahadi zaidi ya miaka mia saba kabla ya kuzaliwa kwa Kristo “wewe si mwenye dhambi tena. Nimekwisha kupatanisha kwa dhambi zako zote na vita imekwisha.” Na hivyo, sauti ya Injili ya ukombozi inaendelea kutuita; Na hii ndiyo inayoitwa Injili iliyotayarishwa.
Tunapoelewa juu ya kazi za Yohana Mbatizaji na kuelewa kwa hakika ya kwamba dhambi zote za ulimwengu alitwikwa Yesu kupitia Yohana Mbatizaji; tunaweza wote kuwa huru kutoka dhambini.
Injili zote nne hutuelezea juu ya Yohana Mbatizaji na Malaki, nabii wa mwisho katika Agano la Kale pia alishuhudia ya kwamba Yohana Mbatizaji ni Mtumishi wa Mungu aliyetayarishwa. Agano Jipya limeanza na habari ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji na kutwika dhambi kupitia yeye.
Sasa ni kwa sababu gani anaitwa Yohana Mbatizaji? Ni kwa sababu alimbatiza Yesu. Nini maana ya Ubatizo? Una maana ya “kuwekea, kutwika, kuzika kusafisha” ni sawa na “kuwekea mikono” katika Agano la Kale.
Katika Agano la Kale mtu alipotenda dhambi, alimtwika dhambi zake zote mnyama wa kutolewa dhabihu, na alikufa kwa dhambi hizo. “Kuwekea mikono” maana yake ni “kubebesha.” Hivyo “kuwekea mikono” na “ubatizo” una maana sawa. Ingawa kuna onekana tofauti katika kitendo.
Hivyo, ubatizo wa Yesu ulikuwa una maana gani? Ubatizo wake ulikuwa ndiyo njia pekee kwetu kupokea ondoleo la dhambi. Mungu alianzisha sheria ili dhambi ziweze kuhamishiwa kwa dhabihu kupitia “kuwekewa mikono.” Hivyo katika nyakati za Agano la Kale, wenye dhambi iliwapasa kuwekea mikono juu ya kichwa cha yule mnyama wa kafara ili kutwika dhambi zao zote kwake. Na baada ya hapo, walimchinja kondoo na kuhani kuchukua damu yake ili kuweka katika pembe za altare ya sadaka za kuteketezwa Hii ilikuwa ndiyo njia pekee ya msamaha wa dhambi za kila siku.
Hivyo, ni kwa namna ipi walipata ondoleo la madhambi ya mwaka mzima?
Kwa jambo hili, Haruni, Kuhani Mkuu alitolea dhabihu kwa niaba ya Israeli yote. Kwa sababu Yohana Mbatizaji alizaliwa toka nyumba ya Haruni ilikuwa sawa kwake kuwa kuhani Mkuu na Mungu alimtambua kabla ya kuzaliwa kwake kwamba atakuwa Kuhani Mkuu kulingana na ahadi yake ya ukombozi.
Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu wa mwisho kwa sababu Agano la Kale limeishia wakati Yesu Kristo alipozaliwa. Ni nani zaidi ya Yohana Mbatizaji angeweza kutwika dhambi zote za Ulimwengu kwa Yesu katika Agano Jipya kama ilivyo Haruni alivyotolea dhambi za watu wake katika Agano la Kale? Kama alivyo Kuhani Mkuu katika Agano la Kale na mwakilishi wa wanadamu. Yohana Mbatizaji alizitwika dhambi zote za dunia kwa Yesu alipombatiza.
Kwa kuwa Yohana alimtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu, basi kuamini Injili ya maji na kwa Roho hakika itatukomboa. Yesu alikuwa mwanakondoo ili atuokoe wenye dhambi, hivyo alifanya kazi ya ukombozi ilivyopangwa na Mungu. Yesu alituambia ya kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ni Nabii wa mwisho, Kuhani mkuu wa mwisho aliyetwika dhambi zote ulimwengu kwake.
Kwa nini Yesu asingefanya mwenyewe? Kwa nini alimwitaji Yohana Mbatizaji? Palikuwa na sababu ya Yohana Mbatizaji kuzaliwa miezi sita kabla ya Yesu; Ilikuwa ni kuhimiza sheria ya Agano la Kale, kukamilisha ahadi.
Yesu alizaliwa toka kwa mwanamwali Mariamu na Yohana Mbatizaji alizaliwa toka kwa mwanamke mzee aliye tasa aitwae Elisabeti.
Hii ilikuwa kazi ya Mungu na aliipanga kwa hao ili, kuwaokoa wenye dhambi. Kutuokoa toka katika vita isiyokwisha dhidi ya dhambi pamoja na mateso yatokanayo na uovu uliopo kati yetu. Alimtuma Mtumishi wake Yohana, na baadae mwana wake Yesu. Yohana Mbatizaji alitumwa kama mwakilishi wa wanadamu, Kuhani mkuu wa mwisho.
Mtu katika uzao wa mwanamke aliye mkuu
Ni mwanadamu gani
aliyekuwa mkuu?
Yohana Mbatizaji
Na tuone Mathayo 11:7-14 “Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika jumba la Mfalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? naam nawaambia na aliye mkuu zaidi ya Nabii Tazama mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako,atakayeitengeneza njia yako,mbele yako. Amin nawaambieni hajaondokea mtu katika wazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu; nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.”
Watu walikwenda jangwani kumwangalia Yohana Mbatizaji aliyekuwa akipaza sauti. ‘Tubuni enyi uzao wa nyoka’ naye Yesu alisema “Lakini mlitoka kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.”
Yesu mwenyewe alitoa ushuhuda juu ya ukuu wa Yohana. “Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu wa msituni aliyevaa singa za ngamia apazae sauti yake kwa juu sana? Atakuwa amevalia singa za ngamia. Mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevalia mavazi mororo? Wale waliovalia mavazi mororo wamo katika nyumba za Wafalme.Lakini yeye ni mkuu zaidi ya wafalme” Lakini yeye ni mkuu zaidi ya Wafalme.” Yesu alishuhudia “Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme, lakini mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam nawaambia aliye mkuu zaidi ya Nabii.”
Katika nyakati za zamani Nabii alichukuliwa kuwa ni mkuu zaidi ya mfalme. Yohana Mbatizaji alikuwa ni zaidi ya mfalme, na zaidi ya Nabii. Alikuwa ni zaidi ya Manabii wote wa Agano la Kale. Hakika Yohana, Kuhani Mkuu wa mwisho na mwakilishi wa wanaadamu alikuwa ni muhimu zaidi ya Haruni Kuhani Mkuu. Yesu mwenyewe alimshuhudia Yohana kwa hilo.
Ni nani aliye mwakilishi wa wanaadamu? Zaidi ya Kristo mwenyewe, ni nani mwanadamu aliye mkuu ulimwenguni? Yohana Mbatizaji. “Naam nawaambia na aliye mkuu zaidi ya Nabii. Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, tengeneza njia yako mbele yako.”
Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba vita dhidi ya dhambi vilikwisha. “Tazama, mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Alikuwa ni Yohana Mbatizaji aliyemshuhudia Yesu ndiye azichukuaye dhambi za dunia.
Katika Mathayo 11:11 “Amin, nawaambia hajaondokea mtu katika wazao wa mwanamke aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji.” Je, hapakuwahi kuwa na mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji kati ya uzao wa mwanamke?
Ni nini maana ya “Kati ya uzao wa mwanamke?” Hii inawakilisha wanadamu wote, isipokuwa Adam na Hawa pekee. Wanadamu wote walizaliwa kupitia mwanamke. Ndio kati ya uzao wa mwanawake, hapakutokea mkuu kumshinda Yohana Mbatizaji. Hivyo alikuwa ni Kuhani Mkuu na mwakilishi wa wanadamu. Yohana Mbatizaji alikuwa mkuu, Nabii na mwakilishi wa wanadamu.
Katika Agano la Kale, Haruni na wanawe wa kiume walichaguliwa na Mungu kumtumikia milele. Dhambi zote zilisafishwa na Haruni na wanawe wa kiume. Ni Mungu aliyetoa agizo hilo.
Ikiwa Walawi wengine watajitokeza na hata kuthubutu kuacha Ukuhani, bila shaka wangekufa. Yote waliyoweza kufanya ni kukusanya kuni kwa ajili ya kuwasha moto katika altare, kuchuna ngozi wanyama, kutoa mafuta, kuosha utumbo na kutoa mabaki ya viungo vingine vya ndani nje ya makutano. Ikiwa wangedharau kwa kujaribu kwa kutumia nguvu zao kufanya kazi ya Ukuhani wangeweza kufa. Ni sheria ya Mungu wasingeweza kuvuka mstari.
Duniani hapajawahi kutokea Mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Alikuwa mkuu kati ya waliokuwa na mwili. “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”
Ukombozi wa mwanadamu ulikamilishwa pale Yohana Mbatizaji alipombatiza Yesu, na wale wote wamwaminio Yesu wataingia katika ufalme wa mbingu kwa kuwa wamefanywa haki kwa imani.
Sasa na tuangalie baba yake Yohana alivyoshuhudia juu ya mwanawe.
Ushuhuda wa Zakaria, baba yake Yohana
Zakaria alitoa unabii
gani juu ya mtoto wake?
Yohana angetayarisha njia ya Bwana kwa
kufundisha njia ya Wokovu kwa
watu wake.
Na tuangalie Luka 1:67-80. “Na Zakaria, baba yake akajazwa Roho Mtakatifu akatabiri akisema, Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa. Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi mtumishi wake. Kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; tuokolewe na adui zetu, na mikononi mwao wote wanaotuchukia, ili kuwatendea rehema baba zetu na kulikumbuka Agano lake takatifu, uapo aliomwapia Ibrahim, baba yetu ya kwamba atatujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu; na kumwabudu pasipo hofu, kwa utakatifu na kwa haki mbele zake siku zote. Nawe mtoto utaitwa Nabii wake aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za Uso wa Bwana umtengenezee njia zake, uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti na kuongoza miguu yetu kwenye njia ya amani. Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni, akakaa, majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.”
Zakaria alitoa unabii wa vitu viwili. Alitoa unabii wa Mfalme wa watu wote ajaye, toka msitari wa 68 hadi 73 altoa unabii kwa furaha. Mungu hakusahau ahadi yake na kwamba Yesu, kama Mungu alivyoahidi kwa Musa atazaliwa kwa mwanamwali Mariamu ili kuokoa uzao wake toka mikononi mwa adui azo.
Mwanzo wa mstari wa 74 “atatujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu na kumwabudu pasipo hofu”. Huu ni ukumbusho wa ahadi ya Mungu kwa Abrahamu na watu wa Israeli, na alitabiri “na kutujalia ili kumwabudu pasipo hofu.”
Mwanzo wa mstari wa 76 pia alitabiri juu ya mtoto wake “Nawe mtoto, utaitwa nabii wake aliye juu kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake. Uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti. Kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”
Alisema, “uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehe dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu.” Ni kwa nini aliyasema haya awajulishe kupatiwa wokovu? Yohana Mbatizaji je, nyote mnaweza kuona haya? Yohana Mbatizaji kupitia maneno ya Mungu, alipaswa kutujulisha ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu.
Sasa na tuangalie Marko 1 “Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, tazama namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayetengeneza njia yako. Sauti ya mtu aliaye nyikani, itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake. Yohana alitokea akibatiza nyikani na kuhubiri Ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakaziungama dhambi zao” (Marko 1:1-5).
Waisraeli walipomsikia Yohana Mbatizaji waliacha kuabudu sanamu zao za mataifa na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Lakini Yohana alishuhudia ya kwamba “Nawabatiza ninyi ili muweze kumrudia Mungu. lakini Mwana wa Mungu atakuja na kuwabatiza ninyi ili dhambi zenu zote ziweze kutwikwa kwake kwa namna hii. Na ikiwa mtamwamini yeye Ubatizo wake kama mlivyobatizwa nami, dhambi zenu zote atabebeshwa yeye kama vile dhambi zilivyoweza kuwekwa juu kwa kuwekewa mikono katika Agano la Kale.” Hii ndio maana ya ushuhuda alioutoa Yohana Mbatizaji.
Ukweli kwamba Yesu alibatizwa katika mto Yordani una maana ya kuwa alibatizwa katika mto wa mauti. Tunaimba “♪ katika misiba katika huzuni na uzuri, tutakutana Pwani njema, tutakutana Pwani hiyo njema.” Tutakapokufa tutavuka mto Yordan. Mto Yordani ni mto wa mauti. Yesu alibatizwa katika mto wa mauti kwa kuzibeba dhambi zetu za ulimwengu mahali hapo na “Mshahara wa mauti ni dhambi.”
Ubatizo ulichukuwa dhambi zetu.
Kuwekea mikono
ni badala ya nini katika
Agano Jipya?
Ubatizo wa Yesu
Katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akjibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. Naye yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake, na tazama, sauti kutoka mbinguni iksema Huyu ni Mwanangu, Mpendwa Wangu, Ninayependezwa naye.”
Yesu alikwenda Yordani na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Aliamuru “Nibatize.” Yohana akajibu “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu.” Kuhani Mkuu wa mbinguni alikutana na Kuhani Mkuu wa duniani.
Kama ilivyoandikwa katika Waebrania, Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu wa milele, kutokana na maelekezo ya Melkizedeki. Hii ina maana kwamba Yesu hakutoka katika ukoo wa mwanadamu. Yeye si uzao wa Haruni, au wa mtu yeyote duniani.yeye ni Mwana wa Mungu, Muumba wetu. Yeye ndiye aliye, hana ukoo. Yesu aliuacha Utukufu wake mbinguni na kuja duniani kuokoa watu wake.
Sababu ya kuja kwake ulimwenguni ilikuwa ni kuokoa watu wote wenye dhambi watesekao kwa ulaghai wa shetani. Kwa nyongeza alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji. “Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15).
“Kubali hivi sasa” Kubali hivi! Yesu aliamwamuru mwakilishi wa wanadamu kwa kuinamisha kichwa chake iliabatizwe. Katika Agano la Kale, wakati sadaka ya mnyama ilipokuwa ikitolewa kwa Mungu, kati ya mwenye dhambi au kuhani aliwekea mikono ili kuitwika dhambi. “Kuwekea mikono” maana yake ni “kutwika”.
Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu. Ilikuwa ni sawa na kuwekea mikono wakati wa Agano la Kale. “Kutwika” kuzikwa “Kusafishwa” na “kutolewa kwa kafara” vyote ni sawa. Agano Jipya ni ukweli hali kwa Agono la Kale ni kivuli.
Wakati wa Agano la Kale mwenye dhambi alipomwekea mikono mwanakondoo wa sadaka, dhambi zake zilitwikwa kwa mwanakondoo huyo na ilimpasa amchinje. Mwanakondoo huyo alipouwawa ndipo alipo futiwa dhambi. Dhambi za aliye wekea mikono juu ya mwanakondoo zilitwikwa kwa mwankondoo aliye sadaka, hivyo ilimpaswa auwawe kwa sababu ya dhambi alizo beba juu yake! Je, ikiwa dhambi zilitwikwa kwa mwanakondoo huyo, basi ina maana mwenye dhambi hakuwa tena na dhambi? Ndiyo.
Hebu na tuseme kwa mfano kitamba hiki cha mikono ni dhambi na kipaza sauti ni mwankondoo. Ninapo weka mikono yangu juu ya hiki kipaza sauti, hii ni kutwika dhambi juu yake, mwanakondoo. Mungu ndiye aliye amuru iwe hivyo. “Kuwekea mikoo”. Ili kuweza kukombolewa toka dhambini katika nyakati za Agano la Kale, ilimpasa mtu kuwekea mikono sadaka ya dhambi. Nabaada ya hapo hakuwa tena mwenye dhambi. Hali kadhalika, ubatizo wa Yesu ulikuwa ni kwaajili ya kusafisha, kuzika na kubebesha dhambi za ulimwengu juu yake. Na hii ndiyo maana halisi.
Nini maana ya kutimiza
Haki zote?
Ni kutakaswa dhambi zote
Kwa kumtwika Yesu.
Hivyo, Je, Yesu alipo batizwa, dhambi zote ulimwenguni hazikuwekewa juu yake? Dhambi zote za ulimwenguni zilitwikwa kwake Yesu na watu wote walikombolewa hakika. Ni sawa na kutwika dhambi kwa mnyama wa sadaka ya dhambi katika Agano la Kale. Yesu alitoka Galilaya kuja Yordani na kumwambia Yohana “Kubali hivi sasa: kwakuwa ndivyo itupasavyokuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15).
Ndipo Yohana akambatiza Yesu. Alimwambia Yohana ilifaa kwao kutimiza haki yote kwa ubatizo wake. “Haki zote” Maana yake “namna pekee ya kufaa.” “Kwa kuwa ndivyo” kwa maneno mengine, kwa njia ya ubatizo, haki zote zilitimizwa. Hii maana yake ilikuwa sawa kwa Yohana kumbatiza Yesu na Yesu kubatizwa na Yohana ili kumbebesha dhambi za ulimwengu.
Mungu alitupa ukombozi kupitia msingi wa Ubatizo wa Yesu, sadaka yake Msalabani, na imani zetu. “Watu wote huteseka kwa dhambi na kunyanyaswa na shetani kwa sababu ya dhambi zao. Hivyo ili waokolewe na kwenda mbinguni, wewe, kama mwakilishi wa wanadamu na uzao wa Haruni, yakupasa kunibatiza mimi kwa ajili ya watu wote. Nitabatizwa nawe, Yohana, ndipo kazi ya ukombozi itakapokamilika.”
“Nimeelewa” Yohana alijibu.
Hivyo Yohana alimbatiza Yesu. Alimwekea Yesu mikono yake kichwani na kumtwika dhambi zote za ulimwengu kwake. Hivyo Yesu alikuwa Mwokozi asafishaye dhambi zetu zote. Hivyo kuamini ukombozi wake kutatuokoa. Je, unaamini hivyo?
Baada ya Ubatizo wake katika Yordani, kupitia mikono ya mwakilishi wa wanadamu, Yesu alisafiri huku na kule na kuanza kuhubiri kwa miaka mitatu na nusu akiwa na dhambi zote za ulimwengu juu ya mwili wake akihudumia watu kwa mara ya kwanza.
Alimwambia yule mwanamke aliyefumaniwa “Nami pia sikuhukumu.” Asingeweza kumhukumu mwanamke huyu kwa kuwa tayari alikwisha zichukuwa dhambi zake na alikuwa mbioni kufa Msalabani kwa ajili yake. Alipokuwa akiomba katika sehemu iitwayo Gethesemani aliomba mara tatu akimsihi Baba akiepushe kikombe chake kimpishie mbali, lakini punde aliachia na kusema “Si kwa mapenzi yangu bali kwa mapenzi yako.”
“Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”
Ni dhambi kiasi gani
Yesu alizichukuwa?
Dhambi zote zaUlimwengu.
Yohana 1:29 Inasema “Siku ya pili ya amwona Yesu anakuja kwake, Tazama Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu na siku iliyofuata Yesu alikuja kwake, hivyo awaambia watu, “tazama, Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Ilikuwa ushuhuda wake.
Mwana wa Mungu alikuja duniani, na kuchukuwa dhambi zote. Yohana Mbatizaji alishuhudia tena katika Yohana 1:35-36, “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu akitembea akasema, tazama Mwanakondoo wa Mungu!”
Mwanakondoo wa Mungu inaonyesha ukweli kwamba Yesu ndiye Kweli na Halisi, sadaka iliyotajwa katika Agano la kale, ambayo ilikufa kwa ajili ya dhambi za Israeli. Kwako mimi na wewe, Mwana wa Mungu na Mwuumbaji wetu, alikuja ulimwenguni ili kuzichukuwa dhambi zetu zote; dhambi zote toka ulimwengu kuumbwa hadi siku yake ya mwisho, kuanzia dhambi ya asili hadi uovu wetu, toka mapungufu yetu, toka udhaifu wetu hadi makosa. Alitukomboa sisi sote kwa Ubatizo na Damu yake katika Msalaba.
Yesu alizichukua dhambi zetu zote na kutupa sisi wenye kuamini ukombozi kamili. Je, unaelewa hii? “Mwana kondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu.”
Miaka 2000 imekwisha pita tangu azaliwe hapa duniani na katika miaka 30 (BAADA YA KRISTO) Yesu alizichukua dhambi zote. Mwaka wa 1 (BAADA YA KRISTO) ndio ulikuwa mwaka uliozaliwa. BK. ni mwaka Baada ya Kristo na ni miaka 2000 imepita tangu Yesu aje duniani.
Katika mwaka 30 BK, Yohana alipaza sauti kwa watu akisema “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu.” “Tazama!” aliwaambia watu kumwamini Yesu, aliyezichukua dhambi zao zote. Alishuhudia kwamba Yesu alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu; yeye atuokoae sisi sote na dhambi zetu zote.
Yesu alizichukua dhambi zetu na kumaliza kabisa vita ile isiyokwisha ya dhambi. Sasa hakuna tena dhambi tangu Mwana wa Mungu alipozichukua. Yohana Mbatizaji alishuhudia ya kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote, zangu na zako “Huyu alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudiae ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye” (Yohana 1:7).
Pasipo ushuhuda wa Yohana, ni kwa namna gani tungefahamu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote? Biblia inatueleza mara kwa mara kwamba alikufa kwa ajili yetu, lakini ni Yohana Mbatizaji pekee ashuhudiae kwa uwazi zaidi kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote.
Ni dhambi ngapi
za dunia?
dhambi zote za watu toka
mwanzo hadi mwisho
wa dunia hii.
Wengi walishuhudia baada ya kifo cha Yesu, lakini ni Yohana pekee alishuhudia wakati yesu akiwa hai. Hata hivyo wanafunzi wa Yesu pia walishuhudia juu ya ukombozi wa Yesu. Walishuhudia kwamba Yesu alizichukuwa dhambi zetu zote, ni Mwokozi.
Yesu alizichukuwa dhambi zote za dunia, Sasa msomaji wangu wewe bado hujawa na umri wa miaka 100? Yesu alichukua dhambi zote za duniani akiwa na umri wa miaka 30. Tazama mchoro huu.

Kwa mfano ilikuwa miaka 4000 kabla ya Kristo kuja mwanadamu wa kwanza aliumbwa. Na imekuwa kidogo zaidi miaka 2000 tangu Yesu aje. Hatufahamu ni kwa miaka mingapi dunia itaendelea kuwepo, ingawa hakika upo mwisho utakuja. Yesu alisema “Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza” (Ufunuo 22:13).
Hivyo, hakika kutakuwa na mwisho. Kwa sasa tupo kipindi kioneshacho mwaka 2002. Yesu alizichukua dhambi zetu zote miaka 30 BK na ilikuwa miaka 3 kabla ya kifo chake msalabani.
“Tazama! Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu.” Alizichukua dhambi za dunia zangu na zako. Tupo miaka 2000 zaidi tangu kuzaliwa kwa Yesu na tunaishi miaka hii 2000 baada ya Yesu kuzichukua dhambi zetu zote. Tunaendelea kuishi kwa kuendelea kutenda dhambi siku hadi siku, ingawa Yesu ni mwana Kondoo wa Mungu aliyekwisha chukua tayari dhambi za ulimwengu huu.
Tunaanza na kuishi na kutenda dhambi tokea pale mwanzo tunapozaliwa. Je ni wote hutenda dhambi tangu tuzaliwapo au la? Ni wote! Hebu natuone mpango wote. Tangu siku tuliyozaliwa hadi kufikia umri miaka 10, je tunatenda dhambi au la? Tunatenda –Je dhambi hizo hakubebeshwa Yesu? Alizibeba.ikiwa basi alizibeba na Mwokozi wetu. Ikiwa sivyo, atakuwa vipi Mwokozi wetu? Dhambi zote ziliwekewa Yesu.
Toka mwaka 11 hadi 20 tunatenda dhambi au la? Tunatenda ndani ya mioyo yetu na kwa matendo… kwa ustadi mkuu. Tumefundishwa tusitende dhambi, lakini tumeumbwa kwa asili kutenda.
Mungu anatueleza ya kwamba, dhambi zote zilitwikwa kwake Yesu. Alifahamu jinsi ile tulivyo wenye dhambi na ndiyo maana aliziondoa kabla.
Na muda gani basi, tunaishi duniani? Hebu na tuseme miaka 70, ni kwa namna gani basi mzigo utakuwa mzito? Tukizipakiza katika lori la tani 8, hakika tutapakia zaidi ya malori 100.
Jaribu kufikiri ni dhambi kiasi gani tungetenda katika kipindi chetu chote cha maisha. Je, hisi sizo dhambi za ulimwengu ama sizo? Hizi ni sehemu za dhambi za ulimwengu. Tunatenda dhambi toka pale tunapozaliwa kufikia miaka 10, 10 hadi 20, 20 hadi 30 na kuendelea hadi siku tunapo kufa lakini yote haya yanajumuishwa katika dhambi za dunia ambazo tayari zilikwishabebwa na Yesu katika ubatizo wake.
Mwokozi wa watu, Yesu Kristo
Ni kiasi gani cha
dhambi Yesu alibeba?
dhambi zote za mababu zetu
na uzao wetu hadi mwisho
wa ulimwengu.
Yesu anatuambia ya kwamba, alikuja katika mwili kusafisha dhambi hizo. Lakini hakuweza kujibatiza mwenyewe, hivyo Mungu alimtuma mtumishi wake Yohana kabla yake, mteule mwakilishi wa wanadamu. Kama ilivyoandikwa “Na jina lake ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenyezi. Kwake mwenyewe, kwa Hekima yake na kwa shauri lake, alimtuma mwakilishi wa wanadamu mbele yake, na Yesu mwenyewe Mwana wa Mungu alikuja katika mwili kubeba dhambi zote za ulimwengu Je, jambo hili si wokovu wa ajabu wenye msingi ulioletwa na Mungu?
Ni wa ajabu, je si kweli? Hivyo, kwa ubatizo wa Yohana Mbatizaji, alisafisha dhambi za ulimwengu wote na kuwakomboa wanadamu wote kila mmoja toka dhambini kwa kusulubiwa kwake, mara moja na kwa wakati wote. Alitukumboa sisi sote. Hebu fikiri jambo hili. Hebu tuangalie dhambi zetu zote kuanzia miaka ya 20 hadi 30, 30 hadi 40, 40 hadi 60 hadi 70 na 100 na kuendelea na si hivyo tu hata za watoto wako. Je, alizifuta! Dhambi zote hizi au la? Ndiyo alizifuta. Ni Yesu Kristo, Mwokozi wa wanadamu.
Tangu Yohana Mbatizaji amtwikwe Yesu dhambi zetu, na kwa kuwa Mungu aliweka mpango huo hivyo, basi tutaweza kukombolewa na yeye tu ikiwa tutamwamini. Je, mimi na wewe si wenye dhambi? Je, dhambi zote alizichukua Yesu? Ndiyo, sisi si wadhambi tena, kwa kuwa dhambi zetu tayari zilikwisha bebwa na Yesu.
Ni nani athubutuye kusema kuna dhambi ulimwenguni? Yesu alikwisha zichukua zote. Alijua ya kwamba tutatenda dhambi tena na hivyo alizichukua hata zile zijazo. Wengi wetu hatujafikia umri wa miaka 50, na hata wengine hatujaishi hata nusu ya maisha yetu bado lakini wachache wetu tunazungumza juu ya kuishi tukidhani tutaishi milele.
Wapo wengi wenye kuishi maisha yenye kuelekea katika mitararuku ya aina mbalimbali. Hebu nifafanue namna hii. Yupo mdudu Fulani apendaye kutembea juu ya maji ya vijito, huishi katika umri wa saa 12.
“Lo! Yupo mtu Fulani alichota maji yenye wadudu hao katika mto na kunimwagia! Nilikimbia na kuanguka karibu kuzimia. Hakika hakuna mtu katili kama huyu katika maisha yangu.” Ajabu ni kwamba wadudu wale walikwisha karibia umri wao wa saa 12 lakini sikuacha kulalamika juu ya kitendo hiki. Nusu ya maisha yao ilikwisha isha.
Ikifikia saa 1 au 2 jioni, wanakumbana na kikomo cha maisha yao kwa muda huo mfupi, kifo. Wengine huishi saa 20 au 21, na wengine huvuna umri mzuri wa saa 24. Wanaweza kuzungumzia juu ya maisha yao marefu na waliyo pitia je hii ina maana gani kwetu? Tupo ishi miaka 70 au 80 kwa umri, tunaweza kusema “Usinichekeshe” umri wa wadudu hawa si kitu mbele yetu. Saa 24?
Hebu tufananishe mfano huu kati yetu na uhusiano tulio nao na Mungu. Mungu ni wa milele Anaishi milele. Anaamua mwanzo na mwisho wa dunia Aishivyo wakati wote, anaishi milele zaidi ya muda uliowekwa katika milele. Hutuangalia sisi maisha yetu na kuhusisha na umilele wake.
Hapo kale, Mungu alizichukua dhambi zetu zote za dunia, na kufa msalabani kwa kusema “IMEKWISHA.” Alifufuliwa baada ya siku 3 na kupaa mbinguni sasa amekaa mbinguni milele. Na hutuangalia sisi sote kila mmoja wetu.
Mtu mmoja aweza kusema “Oh, mpendwa mimi ni mwingi wa dhambi. Ingawa nimeishi umri wa miaka 20, nimetenda dhambi nyingi.” “Nimeishi miaka 30 na nimetenda dhambi nyingi. Ni nyingi sana Nitakuwa vipi bila dhambi?”
Lakini Bwana wetu wa milele atasema “Usinichekeshe. Sijakukomboa na dhambi zako tu sasa, bali hata zile za mababu zako kabla hujazaliwa na zile za kizazi chako ambacho kitakuja kuishi baada yako.” Huzungumzi hivi kutokana na mtazamo wa milele. Je, unaamini haya? Amini hili ili upokee wokovu wa bure wa milele. Ingia katika Ufalme wa Mbinguni.
Usifungwe na mawazo yako, bali amini neno la Mungu. “Hivi ndivyo itupasavyo kutimiza haki zote.” Mwana kondoo wa Mungu, azichukuae dhambi za ulimwengu alikwisha timiza haki zote. Yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu. Je ni kweli au si kweli? Ni kweli, alichukua!
Yesu alisema neno gani
mwisho alipokata roho?
“IMEKWISHA”
Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote ulimwenguni kupitia ubatizo wake, alihukumiwa kifo mbele ya Mahakama ya Pilata na kusulubiwa msalabani.
“Akatoka hali akijichukulia msalaba wake mpaka mahali paitwapo Fuvu la kichwa, au kwa kiebrania Golgotha. Wakamsulubisha huko, na wengine wawili pamoja naye mmoja huku na mmoja huku na Yesu katikati. Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa YESU MNAZARETI MFALME WA WAYAHUDI. Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi maana mahali pale aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania na Kirumi na Kiyunani” (Yohana 19:17-20).
Hebu na tuangalie nini kilitokea baada ya kusulubiwa msalabani “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe Alikwisha zibeba dhambi zote kulingana na maandiko akasema naona kiu, kulikuwa huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa kisopo wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” (Yohana 19:28-30).
Baada ya kuipokea sifongo iliyojaa siki, alipaza sauti na kusema “Imekwisha.” Aliinamisha kichwa na kufa. Hakika alikuwa amekufa. Yesu Kristo alifufuka baada ya siku 3 na kupaa mbinguni.
Hebu tuangalie Waebrania 10:1-9 “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayotawala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo ulimwenguni asema dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi kuhupendezwa nazo. Ndipo niliposema tazama nimekuja (katika gombo la chuo mmeandikwa) niyafanye mapenzi yako Mungu. Hapo juu asemapo, dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyo amuru torati) ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.”
Ukombozi wa Milele
Je, tunaweza vipi kutatua
tatizo la dhambi za kila siku tuzitendazo
baada ya kumwamini Yesu?
Kwa kuthibitisha ya kwamba Yesu alikwisha
zifuta dhambi zetu zote kwa
kupitia ubatizo wake.
Kwa maneno mengine, Sheria ya mpango wa sadaka ya upatanisho ilikuwa ni kivuli cha mambo mema yajayo. Sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale, ya Kondoo na mbuzi, imetuonyesha ya kwamba Yesu Kristo angekuja na kuchukua dhambi zetu katika ufunuo huo ili kuzufuta kabisa.
Watu wote katika Agano la Kale, Daudi, Abrahamu, na wengine wote, walijua na kuamini juu ya mfumo wa sadaka ya upatanisho ulivyo wa maana kwao. Ulifunuliwa juu ya Masiya Kristo (Kristo maana yake “mfalme mpakwa Mafuta”) angekuja siku moja kusafisha dhambi zao zote. Waliamini katika ukombozi waona waliokolewa kwa imani zao.
Sheria ilikuwa ni kivuli cha mambo mema yajayo. Sadaka ya ubatanisho wa dhambi zao za kila siku, mwaka hadi mwaka, isingeweza kuwakomboa kwa ukamilifu. Hivyo ukamilifu na kuwepo milele, yule asiye na doa, Mwana wa Mungu ilipasaje duniani kwa ajili hiyo.
Yesu alisema alikuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake kama ilivyo andikwa kitabuni juu yake. “Akasema Tazama, nimekuja ili niyatimize mapenzi yako.aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili.” Tumekombolewa kutoka dhambini kwa kuwa Yesu Kristo alichukua dhambi zetu zote kama ilivyoandikwa katika Agano la Kale, na kwa kuwa tunamwamini Yeye.
Hebu na tusome Waebrania 10:10 “Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” Kwa hivi tungeweza kutakaswa kupitia sadaka ya mwili wa Yesu Kristo mara moja. Je, hatujatakaswa? -Tumetakaswa.-
Hii ina maana gani? Mungu Baba alimtuma Mwana wake na kumtwika dhambi zetu zote kwake kupitia ubatizo wake. Alipokea hukumu kwa yote katika msalaba. Hivyo, alitukomboa sisi sote tulioteseka kwa dhambi. Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu.
Ili kutukomboa, Yesu alijitoa mwenyewe kama sadaka ya milele mara moja na kwa wakati wote katika msalaba ili tutakaswe. Tumetakaswa kwa sababu Yesu alijitoa sadaka mwenyewe kwa dhambi zetu zote na kufa kwa ajili yetu ili tusihukumiwe tena.
Sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale ilitolewa kila siku na kila mwaka kwa sababu dhambi zote za siku zilihitaji upatanisho mwingine ili kusafisha.
Maana halisi ya Yesu kusafisha miguu ya Petro kiroho
Je, zipo dhambi nyingine tena
tunazopaswa kuomba sala ya toba?
Hakuna.
Katika Injili ya Yohana 13 ipo habari ya Yesu kusafisha miguu ya Petro. Alisafisha miguu ya Petro ili kuonyesha ya kwamba, Petro angetenda dhambi katika kipindi kijacho na kumweleza ya kuwa alikwisha mkomboa kwa dhambi hizo pia, Yesu alikua Petro angetenda dhambi tena katika siku zijazo, hivyo alimimina maji katika karai na kuosha miguu yake.
Petro alijaribu kukataa, lakini Yesu alimwambia “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Kifungu hiki kina maana kwamba “utatenda dhambi tena baadaye. Utanikana na kutenda dhambi tena baada ya kuosha dhambi zako zote. Utatenda dhambi hata wakati nitakapo paa kwenda mbinguni. Hivyo, nasafisha miguu yako ili kumtaadharisha shetani asikutie majaribuni kwa kuwa nimekwisha zichukuwa dhambi zako hata zile zijazo za nyakati.
Je, unafikiri alisafisha miguu ya Petro ili kutueleza kwamba yatupasa kutubu kila siku? Hapana! Ikiwa tulipaswa kutubu kila siku ili tukombolewe basi ina maana kwamba Yesu isingempasa kuchukua dhambi hizo mara moja na kwa wakati wote wa maisha yetu.
Lakini Yesu alisema alitutakasa mara moja na kwa wakati wote Ikiwa tungehitajika kutubu kila siku, basi ingekuwa kama vile tumerudi katika kile kipindi cha Agano la Kale. Sasa, tungeweza kuwa wenye haki? Nani angeweza kukombolewa kwa ukamilifu? Hata kama tulimwamini Mungu, ni nani angeweza kuishi bila dhambi?
Nani atakayetakaswa kwa kutubu? Tunatenda dhambi pasipo kukoma kila siku hivyo ni vipi tunaweza kuomba msamaha kwa kila dhambi? Ni kwa namna gani tunaweza kuwa wavumilivu na kumuudhi Mungu kila siku kwa kuhitaji ukombozi? Tunajaribu kusahau dhambi zetu tulizotenda alfajiri hadi mwisho wa siku na zile za jioni hadi alfajiri nyingine. Ni vigumu kwetu kuomba toba kamili kwa dhambi zetu zote.
Hivyo, Yesu alibatizwa mara moja na kujitoa yeye mwenyewe msalabani mara moja ili tuweze kutakaswa mara moja na kwa wakati wote. Je, unaweza kuelewa hili? Tumekombolewa kwa dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote. Hatukombolewi kila pale tunapo ungama.
Tumeokolewa kutoka dhambini kwa kumwamini Yesu aliyezichukua dhambi zetu zote, zangu na zako.
“Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya Ibada na kutoka dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa Basi, ondoleo la haya likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:11-18).
Nini maana ya “basi ondoleo la hayo likiwapo” katika mstari wa 18 hapo juu? Hii ina maana ya kwamba, kila dhambi ilifutwa kabisa bila uchaguzi Mungu alizifuta dhambi zote na kutusamehe. Je, unaamini hili? “Hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”
Hebu na tufupishe kila kitu sasa. Ikiwa Yohana Mbatizaji ilimpasa kumwekea Yesu mikono, kwa maneno mengine, kama asingembatiza Yesu, Je, tungeweza kukombolewa? La! Bila shaka hapana! Tulifikiri nyuma tena. Ikiwa Yesu asingemteua Yohana Mbatizaji kuwa mwakilishi wa wanadamu na kuchukua dhambi za ulimwengu kupitia kwake, je, angewea kusafisha dhambi zetu? Asingeweza.
Sheria ya Mungu ni yenye haki. Ni ya usawa. Asingeweza kusema kwamba ni Mwokozi wetu na alichukua dhambi zetu. Alimpasa Yesu azichukue dhambi zetu kimatendo. Kwa nini Yesu aliye Mungu alikuja duniani akiwa katika mwili? Alikuja ili azichukue dhambi zetu zote sisi wanadamu kwa kupitia ubatizo wake. Yesu alizijua dhambi zetu zote za moyoni na mwilini ambazo zisingeweza kufutwa ikiwa asingekuja katika mwili ili kujitoa sadaka ya milele.
Ikiwa Yesu asingebatizwa dhambi zetu bado zingebaki pale pale, kama asingesulubiwa kabla kwanza ya kuchukua dhambi zetu, Kifo chake kisingekuwa na maana kwetu. Ingekuwa hina maana kabisa.
Hivyo alipoanza huduma, yake wazi katika umri wa miaka 30, alikwenda kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordani ili abatizwe. Huduma yake nje ilianza akiwa na umri wa miaka 30 na kuishi, akiwa na umri wa miaka 33. Alipokuwa na umri wa miaka 30 alikwenda kwa Yohana Mbatizaji ili abatizwe. “Kubali iwe hivyo, kutimiza haki zote ili watu wote waokolewe na kuwa wenye haki. Ni sahihi kwetu kutenda hili, sasa mbatizaji.” Ndiyo, Yesu Kristo alibatizwa ili aweze kuwakomboa watu wote.
Hivyo Yesu alibatizwa na kuchukua dhambi zetu zote, na kuwa dhambi zote alitwikwa yeye kupitia mikono ya Yohana Mbatizaji, Mungu mwenyewe aligeuza uso wake pembeni wakati Yesu alipokuwa akifa msalabani. Ingawa Yesu alikuwa ni mwana wake wa pekee, alimpasa amtoe sadaka.
Mungu ni upendo lakini ilimbidi amwachie mwana wake afe. Hivyo kwa masaa 3 palikuwa na giza juu ya nchi yote. Yesu alilia kabla ya kufa kwake “Eloi, Eloi, lama sabathani!” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Yesu alijitwika dhambi zetu zote na kupokea hukumu katika msalaba kwa niaba yetu. Hivyo, alituokoa sisi sote. Bila ubatizo wa Yesu, kifo chake kingekuwa hakina maana yoyote.
Je, wewe ni mwenye
dhambi au mwenye haki?
Mwenye haki asiye na dhambi
zozote ndani ya moyo.
Ikiwa Yesu angekufa malabani bila kuchukua dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake, kifo chake kingekuwa hakijakamilisha ukombozi. Ili kukamilisha ukombozi wetu, Yesu alibatizwa na Yohana, mwakilishi wa wanadamu, na kupokea hukumu katika msalaba ili wote wale wenye kumwamini waokolewe.
Hivyo, tangu kipindi cha Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu unachukuliwa kwa nguvu. Kwa sababu Yohana Mbatizaji alimtwika dhambi za ulimwengu Yesu, dhambi zetu zililipiwa Mimi na wewe leo tunaweza kumwita Mungu kwa Baba na kwa uhakika tutaingia ufalme wa mbinguni.
Katika Waebrania 10:18 “Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo kwa ajili ya dhambi.” Je, bado una dhambi? Sasa Yesu umekwisha lipia madeni yote, Je, unahitaji kulipia tena madeni hayo?
Palikuwa na mtu mlevi ambaye alikuwa anadaiwa na watu wengi. Basi, siku moja, mtoto wake wa kiume kwa bahati alimlipia madeni yote aliyodaiwa. Baba huyu hakuwa tena na madeni ingawa alikuwa ingawa alikuwa akidaiwa sana na kila mtu.
Hivyo ndivyo Yesu alivyo tutendea. Alilipa zaidi ya ziada ya dhambi zetu zote. Si dhambi zote maishani mwetu, bali zote za ulimwengu. Zote zilibebeshwa kwake Yesu alipobatizwa Je, wewe ni mwenye dhambi bado? Sasa wewe si mwenye dhambi tena.
Ikiwa tunataka kuelewa Injili ya Ukombozi toka mwanzo ni rahisi namna gani itakuwa rahisi ikiwa tutamwamini Yesu. Lakini kama ilivyo inaonekana ni mpya kwa watu na inashangaza.
Lakini hili si jambo jipya hata kidogo. Ilikuwepo tangu hapo awali tangu historia ya mwanadamu. Hatukutambua hili kabla. Injili ya kwa maji na kwa Roho imekuwa kwa wakati wote katika kumbukumbu ya maandiko na imekuwa ikitenda kazi. Imekuwepo hapo nyakati zote. Imekuwepo katika Biblia kabla yetu imekuwepo tangu uumbaji.
Injili ya Ukombozi wa Milele
Inatupasa tufanye nini
mbele ya Mungu?
yatupasa tuamini Injili
ya ukombozi wa milele.
Yesu Kristo, aliyechukua dhambi zetu zote, aliyafanya haya yote kabla ya kuzaliwa kwetu, mimi na wewe. Alizichukua zote. Je, bado una dhambi? –Hapana- Sasa vipi juu ya dhambi utakazotenda kesho? Nazo pia zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu, sivyo? Je, hakubebeshwa Yesu, au la? Ndiyo alibebeshwa.
Sasa, zile za kesho alibeba? Ndiyo alibeba, alichukua zote bila uchaguzi. Hakuacha hata moja nyuma Injili inatuambia kumwamini Yesu kwa moyo wetu wote, ambaye ndiye aliyezichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote na kuzilipia.
“Mwanza wa Injili ya Yesu Kristo, mwana wa Mungu” (Marko 1:1). Injili ya Mbinguni ni habari njema. Anatuambia “nimechukua dhambi zenu zote mimi ni Mwokozi wenu. Je, unaniamini?” Kati ya watu wengi ni wachache tu watajibu, “Ndiyo, naamini Naamini kama uniambiavyo. Imekuwa ni rahisi kuweza kuelewa mapema.” Wale wenye kukiri imani zao kama hivi hufanywa wenye haki kama Abrahamu.
Lakini wengine watasema “siwezi kuamini, Inaonekana kitu kigeni kwangu.”
Ndipo atasema “Hebu niambie, Je, si kuchukua dhambi zako zote au la?”
“Nilifundishwa kwamba alizichukua zile za asili tu na wala si zile za kila siku.”
“Naona wewe unaelewa zaidi kama ulivyo fundishwa sasa utakwenda kuzimu kwa kuwa sina cha kukueleza.”
Kuamini ukombozi ulio kamili umetuokoa wale wote wenyekutilia mkazo kwamba ni wenye dhambi watakwenda motoni wamejichagulia.
Injili ya ukombozi huanzia kutoka katika ushuhuda wa Yohana Mbatizaji. Tangu Yesu asafishe dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake kwa Yohana Mbatizaji, tumetakaswa tunapoamini.
Mtume Paulo alizungumzia juu ya Yesu katika nyaraka zake. Katika Wagalatia 3:2-7 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” “Kubatizwa katika Kristo” maana yake tumeungana na Kristo kwa kuamini ubatizo wake. Wakati Yesu alipobatizwa, dhambi zetu zote alizibeba kupitia Yohana Mbatizaji na zilisafishwa zote.
Katika 1 Petro 3:2, “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Ni wale tu wenye kuamini ushuhuda wa Yohana Mbatizaji, ubatizo wa Yesu na damu katika msalaba wanayo neema ya ukombozi toka juu.
Pokea ubatizo wa Yesu kama mfano wa wokovu ndani ya moyo wako na uokolewe.