(1 Yohana 5:1-12)
“Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Ni kila mtu ampendaye mwenye kuzaa ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huishinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo si katika maji na damu, Yesu Kristo, si katika maji tu, bali katika maji na katika damu Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiyo kweli kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni) BABA na NENO na ROHO MTAKATIFU, na watatu hawa ni wamoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaid.i Kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima, asiye na mwana wa Mungu hana huo uzima.”
Kwa namna gani
Yesu alikuja?
Maji, damu na kwa Roho.
Je, Yesu alikuja kwa maji? Ndiyo. Alikuja kwa ubatizo wake. Maji yanasimama badala ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordani. Ulikuwa ubatizo wa ukombozi ambao ulimbebesha dhambi zetu zote ulimwenguni.
Je, Yesu alikuja kwa damu? Ndiyo alikuja katika mwili wa mwanadamu na alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kuzilipia mshahara wa dhambi kwa kutoa damu yake pale msalabani Yesu alikuja kwa damu.
Je, Yesu alikuja kwa Roho? Ndiyo. Yesu alikuwa ni Mungu lakini alikuja akiwa Roho ndani ya mwili ili kuwa mwokozi wa wenye dhambi.
Watu wengi hawaamini ya kwamba Yesu alikuja kwa maji, damu na kwa Roho. Ni wachache wenye kuamini kwamba hakika Yesu ni Mfalme wa Wafalme na Mungu wa miungu. Wengi bado wanatangatanga “hivi kweli Yesu ni Mwana wa Mungu au mwana wa mtu?” Na wengi, pamoja na wana theologia na Watumishi, huamini Yesu kama mtu zaidi ya kuwa ni Mungu, mwokozi na Ndiye.
Lakini Mungu alisema kwa yeyote atakaye amini kwamba Yesu ni Mfalme wa wafalme, Mungu wa kweli na Mwokozi wa kweli atakuwa amezaliwa naye. Wale wampendaye Mungu humpenda Yesu na wale wenye kumwamini kweli Mungu humwamini Yesu kwa njia hiyo pia.
Watu hawawezi kuishinda dunia ikiwa hatazaliwa upya. N hivi, Mtume Yohana ametueleza kwamba ni wale Wakristo wa kweli tu ndiyo watakao ishinda dunia. Sababu kwa nini waaminifu wataweza kuishinda dunia, na kwamba wana imani katika maji, damu, na kwa Roho. Nguvu ya kuishinda dunia haiwezi kutoka kwa mapenzi ya mtu matamanio au hamu.
“Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliyo na upata uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu, kiasi cha kuweza kuhamisha milima kama sina upendo si kitu mimi; Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitioa mwili wangu niungue moto kama sina upendo hainifai kitu” (1 Wakorinto 13:1-3).
“Upendo” hapa una maana ya Yesu aliyekuja kwa maji, damu na kwa Roho. Katika Biblia neno “upendo” mara zote kumaanisha “ile kweli ya upendo” (2 Wathesolanike 2:10). Ukweli ni kwamba upendo wa Mungu ulidhihirika kupitia Mwana wake wa pekee (1 Yohana 4:9).
Ni Yule Tu Anayeamini Katika Maji Na Kwa Damu Ataweza Kuushinda Ulimwengu
Ni nani anayeweza kushinda
Ulimwengu?
Ni wale wenye kuamini katika ukombozi
wa Ubatizo wa Yesu na Damu
yake na kwa Roho.
1 Yohana 5:5-6 inasema “Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu , Yesu Kristo; si katika maji tu bali katika maji na katika damu. Yesu Kristo.”
Wapendwa Wakrito, Aliyeweza kumshinda Shetani na ulimwengu ni Yesu Kristo. Wale wenye kuamini neno la maji, damu na Roho la Yesu wanaweza pia kuushinda ulimwengu. Kwa namna gani Yesu aliushinda ulimwengu? Kupitia ukombozi wa maji, damu na kwa Roho.
Katika Biblia “maji” lina maana ya “Ubatizo wa Yesu” (1 Petro 3:21). Yesu alikuja duniani katika mwili. Alikuja kuokoa wadhambi wa dunia hii; alibatizwa ili kuzichukua dhambi hizo zote na kufa katika msalaba kulipia dhambi hizo.
Damu katika msalaba ina maana ya ukweli kwamba alikuja ulimwenguni katika mwili alikuja kama mwili ulio na dhambi kuokoa wenye dhambi na alibatizwa kwa maji. Hivyo, Yesu alikuja kwa yote mawili, kwa maji na damu kwa maneno mengine, alichukua dhambi zetu zote za ulimwengu kwa yote, maji ya ubatizo na damu ya kifo chake.
Ni kwa namna gani shetani anatawala ulimwengu? Shetani anasababisha wanadamu kutia shaka juu ya Neno la Mungu na kupanda mbegu ya uasi mioyoni mwao. Shetani hujaribu kubadilisha watu kuwa watumishi wake kwa kuwalaghai ili wasitii neo la Mungu.
Ingawa, Yesu alikuja duniani na kufuta kabisa dhambi zote kwa maji ya ubatizo wake na kwa Damu yake katika Msalaba; Alimshinda shetani na kufuta dhambi zote za ulimwengu.
Hii hutokea kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa Mwokozi wa wenye dhambi. Amekuwa Mwokozi wetu aliyekuja kwa maji na kwa damu.
Yesu Alizichukua Dhambi zote za Dunia kwa Ubatizo wake wa Ukombozi
Nini maana ya Yesu
Kuushinda Ulimwengu?
Aliushinda Ulimwengu kwa
Kuzichukua dhambi
zake zote.
Tangu abatizwe ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu na kufa ili kuzilipia, anaweza kutukomboa kwa dhambi zetu zote. Sababu Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu katika mto Yordan ilikuwa ni kuzifanya dhambi zetu zote ziwe juu yake badala yetu. Yesu alitoa maisha yake msalabani kwa mshahara wa dhambi. Alimshinda Shetani kwa kifo na ufufuo. Alilipa mshahara wa dhambi zote kwa kifo chake.
Yesu alikuja kwa wenye dhambi katika maji ya Ubatizo wake na Damu katika Msalaba
Kwa namna gani alishinda
Nguvu za shetani?
Kwa ubatizo, damu na Roho.
Mtume Yohana alisema, ukombozi si kwa maji tu bali kwa yote mawili, maji na damu. Hivyo, kama ilivyo Yesu kuchukua dhambi zetu zote na kuzifuta milele, wenye dhambi wote wataokolewa kwa kumwamini yeye, na kuwa waaminifu kwa maneno yake.
Yesu alipokuja ulimwenguni, hakizichukua dhambi zetu tu, bali pia alizilipia kwa damu yake katika kifo cha msalaba. Alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake pale Mto Yordan na kuzilipia katika msalaba kwa kifo chake. Sheria ya haki ya Mungu inasema “mshahara wa dhambi ni mauti” (Waruni 6:23) ilitimizwa.
Sasa, nini maana ya Yesu kuushinda ulimwengu? Imani inayoushinda ulimwengu ni ile imani juu ya Injili ya ukombozi ambao Yesu alituletea kwa maji na damu. Alikua akiwa na umbo la mwili na kushuhudia wokovu kwa ubatizo wa maji na kifo chake msalabani.
Yesu aliushinda ulimwengu, kwa jina shetani. Wafuasi wa Kanisa la kwanza walisimama kidete mbele ya kufia dini bila kujisalimisha kwa utawala wa Warumi au kwa aina zote za vishawishi vya ulimwengu.
Hii yote ni matokeo ya imani zao kwa Yesu aliyekuja kwa maji (alibatizwa kwa kuzichukua dhambi zote) na kwa damu yake Msalabani (alizilipia dhambi zote kwa kifo chake).
Yesu alikuja katika Roho (alikuja kwa mwili wa mwanadamu) na kuzichukua dhambi zote za wenye dhambi kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani ili sisi sote tuweze kukombolewa na tuweze kuushinda ulimwengu.
Upo mfano wa Mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoaa ninyi pia siku hizi; kwa kufufuka kwake Yesu Kristo (1 Petro 3:21)
Ni upi mfano wa wokovu?
Ni ubatizo wa Yesu.
1 Petro 3:21 inasema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.” Mtume Petro anadhihirisha kwamba Yesu alikuwa mwokozi na kwamba alikuja kwa maji ya ubatizo na damu.
Matokeo yake yatupasa kumwamini Yesu aliyekuja kwa maji na damu. Yatupasa pia kujua ya kwamba maji ya ubatizo wa Yesu ni mfano wa wokovu. Mtume Petro alitueleza kwamba “maji” ya ubatizo, damu na Roho “ni vyanzo hakika” vya ukombozi wetu.
Wanafunzi wa Yesu waliamini damu katika msalaba uliotokana na ubatizo wa Yesu. Kuamini damu pekee ni kushikilia nusu ya imani ya kweli. Imani iliyo upande mmoja au ukweli usio kamilika hufifia kwa muda. Kwa hakika wale wenye Imani katika Injili ya maji, damu na kwa Roho watakuwa, imara kwa muda wote.
Sauti ya Injili ya kwa damu tu, inaendelea kukua duniani nyakati hizi. Kwa nini hivi? Watu hawajui ukweli wa Neno la Mungu, ukombozi wa maji na kwa Roho, hivyo hawawezi kuzaliwa upya.
Wakati Fulani, Kanisa katika Mashariki ya mbali liliangukia katika imani za kichawi. Walionekana kustawi kwa muda, lakini watumishi wa shetani walisaidia kugeuza imani kuwa uchawi.
Uchawi ni kuamini kwamba shetani atakimbia ikiwa utachora msalaba katika kipande cha karatasi au kutengeneza msalaba wa mbao, na shetani atafukuzwa ikiwa mtu ataikiri imani yake juu ya damu ya Yesu. Shetani atadanganya kuwa ameogopa damu, kwa kusema Yesu alichoweza kukifanya kwa wenye dhambi ni kumwaga damu yake msalabani tu.
Ingawa Petro na wafuasi wengine walishuhudia Injili ya kweli ya Ubatizo wa Yesu na kwa damu katika msalaba. Lakini ni nini Wakristo wa nyakati hizi wanacho shuhudia? Hushuhudia damu ya Yesu tu.
Yatupasa kuamini maandiko katika Biblia na kuwa imani ya wokovu katika Roho, kwa ubatizo wa Yesu, na kwa Damu yake. Ikiwa tutapuuzia ubatizo wa Yesu na kushuhudia ukweli wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu msalabani pekee, wokovu wetu hautakamilika kamwe!
“Neno la ushuhuda” Wokovu wa Mungu katika Maji
Upo ushahidi gani kwamba
Mungu ametuokoa?
Maji, damu na kwa Roho.
Katika 1 Yohana 5:8, Bwana anasema “Kwa maana wako watatu washuhudiao duniani” Kwanza ni Roho, pili ni Maji ya ubatizo wa Yesu, na tatu ni damu yake msalabani. Vyote hivi vitu vitatu ni kimoja Yesu alikuja duniani kutuokoa sisi sote toka dhambini. Yeye akiwa mmoja alifanya yote haya matatu, ubatizo, damu na kwa Roho.
“Kwa maana wako watatu washuhudiao.” Yapo mambo matatu yatupayo uhakika kwamba Mungu ametuokoa nayo ni Maji ya ubatizo wa Yesu, damu yake na kwa Roho. Mambo haya matatu aliyatimiza Yesu kwa ajili yetu hapa duniani.
Ikiwa moja kati ya haya matatu itatolewa wokovu hautakamilika. Kwa maana wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na Damu.
Yesu Kristo aliyekuja kwetu katika mwili ni Mungu, Roho na Mwana wa Mungu. Alikuja duniani kama Roho ndani ya mwili wa mwanadamu na kubatizwa na maji ili kubeba dhambi zote za ulimwengu. Alichukua dhambi zote mwilini mwako na kutuokoa sisi wenye dhambi kwa damu yake msalabani. Alilipa madhambi yetu yote. Ni Injili ya ukombozi kamili katika maji, damu na kwa Roho.
Ikiwa moja kati ya haya itatolewa, itakuwa sawa na kuuukataa wokovu wa Mungu, aliotuokoa sisi sote toka dhambini. Kama tungekubaliana na wingi wa wanaoamini katika nyakati hizi, tungeweza kusema “Wapo wawili washuhudiao duniani damu na Roho.”
Lakini mtume Yohana alisema wapo watatu washuhudiao duniani; maji ya ubatizo wa Yesu, damu katika msalaba na Roho. Mtume Yohana ameweka wazi juu ya ushuhuda huu.
Imani inayo mkomboa mwenye dhambi ni imani katika Roho, maji na damu. Ni imani gani inayomwezesha mtu kuushinda ulimwengu? Na ni wapi yaweza kupatikana? Ni katika Biblia. Ni kuamini Yesu aliyekuja kwa maji, damu na kwa Roho. Uwe na imani nayo ili upokee Wokovu na Uzima wa milele.
Je, wokovu wa Mungu unaweza
Kukamilika bila ubatizo wa Yesu?
La! Hautoweza
Hapo mwanzo kabla sijaokoka, nami pia nilikuwa Mkristo aliyeamini kwamba ni damu tu katika msalaba na Roho, ndivyo viletavyo wokovu. Niliamini kuwa Yesu alikuja kama Roho na kufa kwa ajili yangu msalabani ili kuniokoa toka dhambi zangu. Niliamini hayo mambo mawili tu na nikawa mpotofu kwa kufikia hatua ya kuhubiri kwa watu.
Nikuwa na mpango wa kusomea Theologia na kuja kuwa Mmisionari ili nifanye kazi hadi mwisho wa maisha yangu kwa ajili ya roho zipoteazo kama Yesu. Niliweka malengo makubwa.
Lakini, kwa kuwa niliamini mambo hayo mawili tu, palikuwa na dhambi moyoni mwangu ikiendelea kuwepo. Matokeo yake, sikuweza kuushinda ulimwengu. Sikuweza kuwa huru toka dhambini. Nilipoamini mambo hayo mawil tu,damu na Roho, nilibaki na dhambi moyoni mwangu.
Sababu iliyonifanya kuwa na dhambi moyoni mwangu, ingawa nilimwamini Yesu, ilikuwa kwamba sifahamu juu ya maji, ubatizo wa Yesu. Uponyaji wangu haukukamilika hadi pale nilipokombolewa kwa imani iliyokamili katika maji ya ubatizo wa Yesu, damu na Roho.
Sikuweza kushinda dhambi za mwili kwa kuwa sikufahamu maana ya ubatizo wa Yesu. Hata wengi wenu mnamwamini Yesu, huku mkiendelea kutenda dhambi za mwilini. Watu bado wanaendelea na dhambi ndani ya miyoyoni mwao na kujaribu bila mafanikio kwa kuhuisha upendo wao wa kwanza waliokuwa nao kwa Yesu.
Hawawezi kuhuisha matamanio yao ya kwanza ya shauku kwa sababu hawajatakaswa kikamilifu na dhambi zao kwa maji. Hawajagundua kwamba dhambi zao zote zilibebwa na Yesu. Alpobatizwa, na hawatoweza kupata imani yao tena baada ya kuanguka.
Napenda kuweka bayana kwenu nyote juu ya hili. Tunaweza kuishi kwa imani na kuushinda ulimwengu ikiwa tu tutamwamini Yesu. Ijapokuwa hatujitoshelezi, haijalishi ni mara ngapi mara kwa mara tunaanguka dhambini tuwapo duniani, ikiwa tutamwamini Yesu kama Mwokozi wetu, aliyetufanya wakamilifu kwa kuwa huru na dhambi kwa ubatizo wake na kwa damu yake, hakika tutasimama kuwa washindi daima.
Kamwe haitojalisha ikiwa tutamwamini Yesu pasipo maji ya ubatizo wake, hatutoweza kukombolewa kabisa. Mtume Yohana ametueleza kwamba imani yenye kuushinda ulimwengu ni imani ile yenye kumwamini Yesu Kristo, aliye kuja kwa maji ya ubatizo, damu na kwa Roho.
Mungu alimtuma mwana wake wa pekee kuokoa wale wote wenye kuamini ubatizo na damu yake. Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Yesu, mwana wa pekee wa Mungu, alikuja kwetu kwa Roho (katika mwili wa mwandamu). Na baadaye kuitoa damu yake msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zetu. Hivi ndivyo alivyo wakomboa wandamu wote kwa dhambi.
Imani ituongozayo kuushinda ulimwengu huja kwa kuamini ukweli kwamba Yesu alikuja kwa maji, damu na kwa Roho, ambayo kwa hakika itatuweka huru na dhambi kikamilifu na daima.
Ikiwa hakuna maji kwa ubatizo na damu kwa msalaba, basi pasingekuwa na wokovu wa kweli. Ikikosekana moja kati ya hayo yaliyo matatu hakuna ukamilifu na wokovu wa kweli. Wokovu wa kweli ni kuamini maji, damu na kwa Roho. Ujue hili na utakuwa na imani ya kweli.
Nawaeleza ya kwamba hapatokuwa na wokovu wa kweli pasipo ushuhuda wa Maji, Damu na kwa Roho
Ni mambo gani matatu yaliyo
muhimu yabebayo ushuhuda
wa wokovu?
Maji, Damu na Roho.
Mtu anaweza kufikiri juu ya swali hilo hapo juu kwamba. “Yesu ni mwokozi wangu. Naamini damu yake msalabani na niko tayari kufa kama shahidi. Namwamini Yesu ingawa nina dhambi moyoni. Nimetubu kwa makini na kuwa mwangalifu kwa matendo mema haki na kujitoa kila siku. Nimetoa maisha yangu na tamaa zote za dunia hii kwako Yesu. Nimekuchagua wewe na kuacha ndoa. Itawezekana vipi Mungu kutonitambua? Yesu alikufa kwa ajili yangu msalabani. Mungu wetu Mtakatifu alikuja kama mwanadamu na kufa msalabani. Nakuamini, najitoa kwa ajili yako, natenda mema kwa uaminifu kwa ajili yako. Ingawa sina thamani na bado mwenye dhambi moyoni, Je, Yesu utanihukumu kwenda motoni? Hapana, sidhani.”
Wapo wengi wenye kufikiri namna hii. Hawaamini yakwamba Yesu alibatizwa ilikuzichukuwa dhambi zote za ulimwengu. Je, Wakristo hawa wa jina, wanaoamwamini Yesu hali mioyoni mwao ni wenye dhambi, wanapo kufa, watakwenda wapi? Watakwenda motoni. Niwenye dhambi tu!
Wapo wengi wenye kufikiri namna hii na kudhani Mungu anafikiri hivyo pia, wataishia motoni. Zaidi ya hayo wengine baadhi yao husema ya kwamba kwa kuwa Yesu alizichukuwa dhambi zote alipokufa pale msalabani, basi hakuna dhambi tena duniani. Ingawa hii ni kuzungumza juu ya damu na Roho pekee. Hii si imani kwa kweli itakayo waongoza watu katika ukombozi ulio kamili.
Yatupasa kuamini kwamba Yesu alichukuwa dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, alihukumiwa na kufa msalabani kwa ajili yetu, na akafufuka siku ya tatu, baada ya kifo chake.
Bila imani hii, ukombozi usingewezekana. Yesu Kristo alikuja kwetu kwa ubatizo, damu na Roho. Alichukuwa dhambi zote za ulimwengu.
Yapo mambo muhimu matatu yenye kushuhudia juu ya wokovu wake hapa duniani, Roho, maji na damu.
Kwanza; “Roho” Mtakatifu hushuhudia Yesu ni Mungu na alikuja katika mwili.
Pili; “Maji” hushuhudia ubatizo wa Yesu katika mto Yordani kwa Yohana Mbatizaji kupitia katika mto Yordani kwa Yohana Mbatizaji kupitia kwake dhambi zetu zote alimtwika Yesu. Dhambi zetu alizibeba Yesu alipobatizwa (Mathayo 3:15).
Tatu; “Damu” inasimama kama Yesu kukubali kujitoa kwa hukumu ya dhambi zetu. Alikufa ili afe kwa hukumu ya Mungu Baba na alifufuliwa siku ya tatu ili kutupa uhai mpya.
Mungu Baba alimtuma Roho ndani ya mioyo ya wale wote wenye kuamini ubatizo na damu ya mwana wake ili aweze kushuhudia ndani ya juu ya ukombozi.
Wale wote waliozaliwa upya wana neno ndani yao lenye kushinda ulimwengu. Waliokombolewa watamshinda Shetani, uongo wa manabii, walaghai, vikwazo au misukosuko ya ulimwengu ambayo haiachi kushambulia. Sababu ya kuwa na nguvu hii ni kwamba, tuna ushuhuda wa yale mambo matatu ndani ya mioyo yetu; Maji ya Yesu, Damu yake na Roho.
Tunaweza kumshinda
Vipi shetani?
Kwa kuamini ushuhuda
Wa mambo matatu.
Tunaweza kumshinda shetani na ulimwengu kwa kuwa tunaamini katika Roho, maji na Damu. Wale wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu wana uweza wote wa kuushinda ulimwengu na vishawishi vya manabii wa uongo kwa kungu hizi zitokanazo na maji, damu na Roho. Je, unaamini hili?
Haiwezekani kuzaliwa upya au kuushinda ulimwengu ikiwa huna imani katika ukombozi utakanao na ubatizo wa Yesu, Damu yake na kuamini Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi. Je, Imani hii imo ndani ya moyo wako?
Je, unayo Roho na maji ndani ya moyo wako? Unaamini kwamba dhambi zako zote alibeba Yesu? Je, unayo damu ya msalabani moyoni mwako?
Utaushinda ulimwengu ikiwa utakuwa na imani katika maji na katika damu ya Yesu ndani ya moyo wako. Ikiwa unaamini Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako na kubeba hukumu kwa ajili yako utaushinda ulimwengu.
Mtume Yohana aliushinda ulimwengu kwa sababu alikuwa na yote haya yaliyo muhimu ndani ya moyo wake. Pia alizungumzia juu ya ukombozi kwa ndugu zake kwa imani walistahimili vikwazo na vitisho katika huduma zao. Yesu alikuja kwa Roho, maji na damu. Kwa jinsi alivyoushinda ulimwengu hata sisi pia kwa wale walio waaminifu tutaushinda. Hii ndiyo njia pekee kwa waaminifu kuushinda ulimwengu.
Katika 1 Yohana 5:8 inasema “Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Wengi bado huzungumzia juu ya damu na Roho tu wakiacha maji ya ubatizo wa Yesu. Ikiwa wataacha habari ya maji, bado watandelea kudanganywa na shetani. Wanapaswa kuacha upotovu wao na kutubu na kuamini maji ya ubatizo wa Yesu katika kuzaliwa upya.
Hakuna yeyote mwenye kuushinda ulimwengu bila kuamini maji na damu ya Yesu. Nasema tena, hakuna! Yatupasa kupigana kwa kutumia maji na damu ya Yesu kama silaha nzito na kali za kiroho. Neno lake ni upanga wa Roho, Nuru.
Wapo wengi wasioamini ubatizo wa Yesu ulichukua dhambi zetu zote. Wapo wengi wenye kuamini mambo mawili tu. Hivyo, Yesu anapowaeleza “amka na uangaze”, hawawezi kuangaza kwa vyovyote vile. Bado wanazo dhambi mioyoni mwao. Ingawa wanamwamini Yesu, lakini bado watakwenda motoni.
Injili ya Ubatizo na Damu ya Yesu bila shaka ndiyo Inayoshuhudia ili watu wasikie, waamini na kuokolewa
Je, Imani katika ubatizo
wake ni aina ya mafundisho ya
kawaida katika kanuni?
Si mafundisho ya kanuni
Ni ukweli.
Tunaposhuhudia juu ya Injili, inapasa iwe hakika. Yesu alikuja kwa Roho, kwa ubatizo (uliozichukua dhambi zetu zote) na kwa damu (iliyolipia dhambi zetu zote) Yatupasa kuamini yote haya matatu.
Kinyume chake, basi hatujahubiri Injili bali ni dini ya kawaida tunahubiri. Wakristo wengi nyakati hizi huchukulia Ukristo ni aina ya dini kama dini nyingine, lakini Ukristo hauwezi kuwekwa katika hadhi ya dini. Ni imani ya ukombozi uliojengeka katika msingi wa ukweli wa kumtumaini Mungu. Hauwezi kuwa dini.
Dini ni kitu kilichoanzishwa na mwanadamu, hali imani ni kumtumaini Mungu atupaye wokovu. Hii ni tofauti yake halisi. Ikiwa utapuuzia ukweli huu, utauona Ukristo kama dini nyingine tu na kuhubiri kwa njia ya ustaarabu na kanuni za wanadamu zilizo njema kwa wanadamu.
Yesu Kristo hakuja kuanzisha dini ulimwenguni. Hakuwahi anzisha inayoitwa Ukristo. Kwa nini unaamini kuwa ni dini? Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa nini basi usiamini dini ya Budha badala yake? Unadhani nimekosea kusema hili?
Baadhi ya watu humwamini Yesu kama njia ya dini maishani mwao, na wakiishi wakisema tofauti iko wapi? Mbinguni Nirvana, Paradiso… Yote sawa tu, tofauti ni majina. Tutaishia sehemu moja kwa vyovyote.
Wapendwa Wakristo, yatupasa kusimama imara katika kweli, Yatupasa “kuamka na kuangaza” ndipo tutaweza kuhubiri kweli bila kusita.
Wakati wengine wanaposema “Hiyo haiwezi kuwa ndiyo njia pekee kwenda mbinguni” yakupasa ujibu kwa sauti ya uhakika “Ndiyo! Hakika ni njia pekee. Unaweza kwenda mbinguni ikiwa tu utamwamini Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji, damu na Roho.” Yakupasa uangaze kwa nuru ili roho nyingine ziweze kusikia Neno la ukombozi kwa kuzaliwa upya na kwenda mbinguni.
Uwe na imani sahihi: Wapendwa wasiomrudia Yesu ambao hawafahamu ukombozi katika ubatizo wa Yesu na Damu yake wataangamia
Ni nani wataangamia hata
Ikiwa wanamwamini Yesu?
Wale wote wasioamini
Ubatizo wa Yesu.
Kudai kwamba unamwamini Yesu pasipo kuwa na sababu ya msingi na ya kweli ni sawa kutorudia upendo wa Yesu na kuwa na njia fupi ya kuwa mkristo wa dini.
Meli ilipita katikati ya Bahari ya Pasifiki na kuzama, waliokoka watu wachache huku wakielea juu ya mabaki ya vipande vyake vilivyo vunjika. Wakatuma taarifa kwa alama ya kuomba msaada kwa meli nyingine zilizo mbali na pale, lakini kwakuwa bahari ilichafuka kwa mawimbi haikuweza kufikia meli nyingine zilizo mbali na pale. Hatima yake ndege ya ilifika na kuwashushia kamba ya kukwea. Ikiwa mmoja kati yao angeishika kama ile kwa mikono yake badala ya kuifunga kiunoni itakuwa ni sawa na kuanguka mbali na Upendo wa Yesu; kumwamini Mungu kwa namna yake. Hajawa salama bado, lakini atasema “Naamini Niokoe Naamini, hivyo nafikiri nitaokoka.”
Asiyefahamu kweli ya ubatizo wa Yesu na Damu yake hudhani ataokoka kwa kushikilia kamba.
Lakini atakapo vutwa juu, mikono yake italegea kushika kamba baada ya muda. Ni mbali kwake kufika ufukweni akiwa amening’inia kwa kushika kama hiyo kwa nguvu zake. Nguvu zitakapomwishia ataachia na kutumbukia baharini tena.
Kutokurudisha Upendo kwa Yesu ni sawa na hili la kurushiwa kamba, badala ya kuifunga kiunoni unashikilia kwa mikono kwa kutumia nguvu zako ambazo baada ya muda zitachoka. Wengi mnaweza kusema mnamwamini Mungu na Yesu; na kuamini Yesu aliyekuja katika Roho, lakini hii ni sehemu tu ya mlingano wa yale mambo matatu. Wanaweza wasiamini kweli na wasiwe ndani ya Injili, hivyo kujilazimisha kusema wanamwamini Yesu.
Kuamini na kujaribu kuamini ni mambo tofauti. Wanasema watamfuata Yesu hadi mwisho, lakini katika siku ya mwisho watatupwa kando kwa kuwa dhambi zilizobaki ndani ya mioyo yao. Wanapenda Yesu bila kuelewa kuwa alikuja ubatizo, damu na kwa Roho. Ikiwa watampenda Yesu kwa damu yake tu, watakwenda motoni.
Funga moyo wako kwa kamba ya Injili ya kweli, Injili ya maji na damu. Yesu anapokushushia kamba ya wokovu wale watakao jifunga viunoni kwa maji, damu na kwa Roho wataokoka.
Yule mwokoaji katika ile ndege alipaza sauti kwa kuwaambia “tafadhali sikilizeni kwa makini, nitakapotupa kamba kwenu chukueni na mzifunge kuzunguka kati ya makwapa katika sehemu ya kifua. Na msubiri hapo mlipo. Usining’inie kwa kamba kwa kutumia mikono yako kuishika bali mfunge kuzunguka vifua vyenu na mtulie. Na hapo mtachoka.”
Mtu wa kwanza akafuata maelekezo vyema na kujifunga kama ile na akaokolewa. Lakini yule mwingine akasema, “Usitie shaka. Mimi ni mwenye nguvu. Nafanya mara kwa mara mazoezi ya viungo. Hebu angalia misuli yangu! Unaona? Naweza kuning’inia maili nyingi tu.” Hivyo alishikilia ile kamba kwa mikono yake na kamba ilianza kuvutwa.
Wote wawili walivutwa. Lakini tofauti ilikuwa kwamba yule aliyefuata maelekezo alijifunga kuzunguka mwili wake kifuani bila ya kutumia nguvu zake katika kuning’inia. Ilifika wakati hata kujisahau ingawa aliendelea kuning’inizwa na kamba.
Yule mwenye majigambo ya nguvu zake baada ya muda alishindwa kung’ang’ania kamba kwa sababu kungu za mikono zilimwishia. Alikufa kwa sababu hakupenda kusikiliza na kufuata maelekezo.
Ili kupata ukombozi ulio kamili, yakupasa kuamini ukombozi wa maji ya ubatizo wa Yesu, na damu inayo okoa roho zote toka dhambini. Wokovu unapatikana kwa wale tu wenye kuamini kwa moyo wao wote neno; “nimekuokoa kikamilifu kwa ubatizo wangu kwa Yohana Mbatizaji na damu yangu katika kifo kile cha msalaba.”
Wale wenye kuamini damu tu, husema “usiwe na wasiwasi, ninaamini. Nitaishukuru damu ya Yesu tu hadi mwisho. Nitamfuata Yesu hadi mwisho wa maisha katika damu yenye kutosha kuushinda ulimwengu na dhambi zote maishani mwangu.”
Ingawa hii haitoshi. Wale Mungu anaowakubali kuwa watu wake ni wale wenye kuamini ushuhuda wa yale matatu: Yesu aliyekuja katika Roho, na alibatizwa (kwa kuzichukua dhambi zote katika mto Yordani kwa ubatizo wake) na alikufa katika msalaba kulipia gharama ya dhambi zote, na alifufuka siku ya tatu toka kifoni.
Roho huja kwa wale tu wenye kuamini mambo hayo matatu yanayoshuhudiwa. “Ndiyo, mimi ni mwokozi wako. Nimekuokoa kwa maji na damu. Mimi ni Mungu wako.”
Kwa watu wasioamini yote matatu, Mungu haweze kuwapa wokovu. Hata ikiwa ni moja, Mungu anasema “Hapana, bado hujaokoka.” Wale wafuasi wa Yesu waliamini yote matatu. Yesu anasema kwamba ubatizo wake ni mfano wa wokovu na damu yake ni hukumu.
Mtume Paulo na Petro nao pia walishuhudia vyote, ubatizo na Damu ya Yesu
Wanafunzi wa Yesu
walishuhudia nini?
Ubatizo wa Yesu na
Damu yake.
Je, Mtume Paulo aliongelea juu ya ubatizo wa Yesu? Hebu na tuone alizungumzia hili mara ngapi juu ya ubatizo wa Yesu. Amesema katika Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” Na katika 6:5 “Kwa maana kama mlivyo unganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake.”
Alisema pia katika Wagalatia 3:27 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” Mitume wa Yesu wote walishuhudia juu ya “maji” ubatizo wa Yesu. “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1 Petro 3:21).
Wokovu wa ukombozi wa Bwana ulikuja kwa Maji na kwa Damu ya Yesu
Ni nani anayeitwa
mwenye haki na Mungu?
Wale wote wasio na dhambi
mioyoni mwao.
Ukombozi ambao Yesu alimwekea mwanadamu ni wa maji ya ubatizo wake na damu yake katika msalaba. Kwa ukombozi huo twaweza kuamka na kuangaza. Kwa namna gani? Kwa kushuhudia haya matatu.
“Ondoka; uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa Bwana umekuzukia” (Isaya 60:1). Mungu ametuangazia na kutuambia tuangaze pia. Yatupasa kutii amri hii.
Tumekuwa tukihubiri Injili kwa nguvu zetu zote. Ijapokuwa watu wengi bado hawasikilizi. Amini Yesu na utakombolewa. Utakuwa mwenye haki. Ikiwa dhambi bado itaendelea kuwepo ndani ya moyo wako bado hujawa mwenye haki. Bado hujaishinda dhambi za Ulimwengu.
Huwezi kuachana na dhambi ndani ya moyo wako ikiwa huamini juu ya maji ya Yesu (ubatizo wake) Huwezi kamwe kuzuia hukumu ikiwa huamini juu ya damu ya Yesu. Huwezi kamwe kuzuia hukumu ikiwa huamini juu ya damu ya Yesu. Huwezi kuokolewa ikiwa huamini juu ya Yesu Kristo, aliyekuja kwa Roho. Huwezi kukamilika kuwa mwenye haki kama hutaamini mambo haya matatu yashuhudiayo.
Haki isingejitosheleza ina pelekea kupatikana kwa aina fulani nyingine ya haki. Ikiwa mtu yeyote atasema bado ana dhambi, lakini bado anajichukulia ni mwenye haki, basi mtu huyu bado hajawa ndani ya Yesu. Watu wengine siku hizi hujaribu kusimamia kwa muda katika ukombozi kwa kupitia aina fulani ya haki. Wameandika makala nyingi zisizo na maana juu ya somo la haki.
Je, Mungu humwita mtu kuwa asiye na dhambi ikiwa bado mtu huyo ana dhambi? Hakika hafanyi hivyo. Humwita mtu jinsi alivyo. Ni Mwenyezi hawezi kudanganya. Watu hawaelewi maana halisi ya haki. Tunaita kitu fulani “safi” ikiwa tu ni kisafi. Hatuwezi kusema “mwenye haki” ikiwa bado pana dhambi.
Unaweza kufikiri ya kwamba unaweza kuitwa mwenye haki na Yesu ingawa una dhambi moyoni, lakini bado si sahihi.
Yesu hutuita wenye haki ikiwa tu, tutamwamini yeye kama ndiye aliye kuja katika Roho, maji (kwa ubatizo wake alizibeba dhambi zetu zote) na kwa Damu (kwamba alikuja katika mwili na kufa kwa ajili yetu).
Wapendwa Wakristo, hizi aina fulani za haki hazina cha maana dhidi ya Injili ya maji na damu. Aina hizi za haki au kuitwa mwenye haki ikiwa bado unadhambi ndani ya moyo wako? Hakika hawezi na haijalishi ni kwa kiasi gani mtu huyu aweza kumwamini Yesu, Yesu hawezi kudanganya.
Je, bado unaweza kufikiri Mungu anaweza kumwita mtu fulani mwenye haki ikiwa ana dhambi moyoni? Hivyo ndivyo watu wadhaniavyo, si Mungu. Mungu hapendi uongo. Je anaweza kukuita mwenye haki ikiwa utaamini “maji” na “damu” tu? Kamwe!
Yupo mtu wa aina moja Mungu anaweza kumwita mwenye haki. Ni wale tu wasio na dhambi mioyoni mwao. Anawatambua wale wenye kuamini mambo matatu! Yesu aliye Mungu aliyekuja ulimwenguni katika mwili, akabatizwa mto Yordani na kutoa damu yake msalabani ili kufuta dhambi zetu zote.
Ni wale tu, wenye kuamini habari njema ya ukombozi ndiyo wenye kutambuliwa kuwa wenye haki na Mungu. Ni walio na imani sahihi, moja kwa moja wanaamini yote Yesu aliyotufanyia. Wanaamini kuwa Yesu alikuja, alibatizwa ili kuchukua dhambi zetu zote, alihukumiwa kwa ajili yetu na kufa msalabani na akafufuka kutoka mauti.
Yote haya yalifanyika kwa upendo wa Mungu Yesu alikuja ulimwenguni akitokea mbinguni “Njooni kwangu ninyi, nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Alifanya haya kwa kuyachukua madhambi yetu yote.
Mungu hawatambui wale wenye kuamini damu ya Yesu pekee. Wale wenye kuamini damu ya Yesu bado wana dhambi mioyoni mwao. Ni nani Yesu huwatambua kuwa wamekombolewa?
Amini ubatizo wa Yesu, damu yake na ukweli kwamba yeye ni Mungu yote haya ni muhimu kwa wokovu “Nimechukua dhambi zako zote nilipo kuja ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Nashuhudia kwamba dhambi zote za dunia zimetwikwa kwangu. Nimelipa dhambi hizo msalabani. Kwa hayo nimekuokoa.”
Kwa wale wenye kuamini mambo haya matatu Yesu anasema “Ndiyo umeokoka. Ni mwenye haki na mtoto wa Mungu” wewe nawe waweza kuokoka ikiwa utaamini ubatizo wa Yesu damu yake na Roho kwa pamoja. Wenye kuamini damu na Roho pekee bado wanadhambi mioyoni.
Katika ufalme wa Mungu upo ukweli tu. Ipo haki, ukweli, upendo na ukarimu. Hakuna kusema uongo. Uongo na hila haupo Mbinguni.
Ni nani asiyetenda haki?
Yule asiye amini ubatizo
wa Yesu.
“Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?” (Mathayo 7:22).
Mungu hawatambii kazi hizo za watu kuwa ni halali kuingia katika ufalme wake “Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:23).
“Ninakutolea nyumba mbili. Nimekutolea maisha yangu. Sijakukana maishani mwangu hadi mwisho wa pumzi ya mwisho. Hukuniona?”
“Je, una dhambi moyoni?”
“Ndiyo, Bwana. Nina ninazo kidogo.”
“Basi, uondoke mbele zangu! Hapana mwenye dhambi aliye ruhusiwa kuwa mbele zangu.”
“Lakini nilikufa kama shahidi mfia dini kwa kukuamini wewe Bwana!”
“Una maana gani kufia dini? Ulikufa kwa huo moyo wako mgumu na ubishi Je, uliutambua ubatizo wangu na damu? Je, sikukushuhudia moyoni mwako kuwa wewe ni mtoto wangu? Huamini ubatizo wangu na sikukushuhudia kuwa wewe ni mwanangu, na ndiyo maana uling’ang’ana kwa imani yako na kufa kwa hiyo. Je, nilikushuhudia? Uliyaleta kwa nafsi yako unayo amini. Ulijaribu kufanyiza ukombozi wa aina yako mwenyewe. Je, unaelewa? Sasa endelea na njia zako.”
Yesu alituambia tuamke na tuangaze. Waliokombolewa wanaweza kuogopa madhehebu mengi ya Ukristo wa majina na manabii wa uongo, hivyo kushindwa kuangaza vizuri. Lakini dini ya moto yaweza kuanzisha moto mkubwa. Ikiwa mtu atasimama kwa ujasiri na kushuhudia ukweli, dunia yote itaangaziwa.
Katika Isaya 60:1-2 inasema. “Ondoka, uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia, maana, tazama, giza litakufunika dunia na giza kuu litazifunika kabila za watu, bali Bwana atakuzukia wewe na utukufu wake utaonekana juu yako.”
Mungu anatuamrisha kuondoka na kuangaza na kuwa nuru. Kwa kuwa giza la uongo, yaani Injili isiyo ya kweli imefunika ulimwengu wote. Ni kwa wale wenye kumwamini Yesu wataweza kumpenda. Wasiokombolewa hawawezi kunipenda ikiwa hawataweza kuamini ukweli wote.
Yapo Mambo Matatu yenye kushuhudia juu ya Wokovu wa wenye dhambi
Ni upi ushuhuda wa wokovu
Ndani ya moyo wetu?
Ubatizo wa Yesu.
“Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na damu; na watatu hawa hupatikana kwa habari moja.” Yesu alikuja ulimwenguni na alifanya kazi yake kwa maji na damu. Alifanya haya na kutuokoa.
“Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima asiye na Mwana wa Mungu hana huo uzima” (1 Yohana 5:9-12).
Wale waliozaliwa upya hupokea ushuhuda wa wanadamu. Tunatambulika kama wenye haki. Waliozaliwa upya, walio kombolewa, wanaponena ukweli juu ya ukombozi, watu hawawezi kupinga. Hukubaliana nalo. Husema kuwa wameamini vema na wako sahihi kwa imani yao. Tunapowaeleza ni kwa namna gani wamezaliwa upya hakuna awezaye kusimama kinyume na Injili ya kweli tunayo shuhudia. Husema tupo sahihi. Tunapokea ushuhuda wa wanadamu.
Lakini kifungu hicho kusema “ushuhuda wa Mungu mkuu zaidi kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu.” Hapa inasema ushuhuda wa Mungu ni wa Mwana wake. Je, ni sawa? Ni upi ushuhuda wa Mwana wa Mungu? Ushuhuda wa Munngu alituokoa ni ule wa Yesu aliyekuja kwa Roho; kwa maji ya ukombozi na kwa damu yake msalabani. Ushuhuda wa Mungu kwamba hii ndiyo njia aliyotuokoa na ya kwamba sisi ni watu wake kwa kuwa tuna iamini njia hiyo.
“Yeye amwaminiye mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia mwanawe.”
Kifungu hiki kinatueleza zaidi ni yupi aliye kombolewa. Kinasema ni yule amwaminiye Mwana wa Mungu na kuwa na ushuhuda ndani yake. Je, unao ushuhuda ndani yako? Umo ndani yetu sote Yesu alikuja duniani kwa ajili yetu sote (Alikuja katika mwili kupitia mwili wa Mariamu kwa Roho Mtakatifu) Alipokuwa miaka 30, alibatizwa ili kuchukua dhambi zetu zote na akiwa nazo zote, alihukumiwa msalabani alifufuliwa siku ya tatu ili kutupatia uzima wa milele. Hivi ndivyo Yesu alivyo tuokoa.
Ingekuwa vipi ikiwa asingefufuka? Angeshuhudia vipi kwangu akiwa kaburini? Na ndiyo maana ni mwokozi wangu. Hivi ndivyo tuaminivyo.
Kama alivyosema, alituokoa kwa ubatizo wake na kwa kuwa tunaamini, mimi na wewe tumeokoka ushuhuda umo ndani yangu na ndani yako. Waliokombolewa hawawezi kudharau “maji” ya ubatizo wa Yesu. Hatuwezi kamwe kuondoa mambo aliyofanya ili kutuokoa.
“Hivi ndivyo itupasavyo kutimiza hako zote” (Mathayo 3:15). Kamwe hatuwezi kukana yale yote Yesu aliyofanya ili kubeba dhambi zetu zote katika Mto Yordani alipobatizwa na Yohana Mbatizaji waliokombolewa hawawezi kuyakana “maji” ya ubatizo wa Yesu.
Wenye kuamini, lakini Bado hawajakombolewa, hukana ubatizo wa Yesu hadi mwisho
Ni nani amfanyaye
Mungu kuwa mwongo?
Yule asiye amini juu
Ya ubatizo wa Yesu.
Alisifu vipi Mtume Yohana aliposema “Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo.” Ikiwa Mtume Yohana angekuwepo leo, angetueleza nini Wakristo? Bila shaka angetueleza ikiwa kwa kupitia ubatizo wa Yesu dhambi zetu alitwaa au la.
Je, Yohana Mbatizaji naye pia hushuhudia juu ya Injili juu ya Yesu kutukomboa kwa ubatizo wake? “Je, dhambi zenu hukujitwika. Yesu na hakuzibeba alipobatizwa nami? Hivi ndivyo ukweli ulivyo anapo mshuhudia Yesu aliyebatizwa nami?” Hivi ndivyo ukweli ulivyo anapomshuhudia Yesu aliyebatizwa ili kutuokoa sisi sote (Yohana 1:29, 1 Yohana 5:4-8).
Wale wasiomwamini Mungu kwa maneno mengine wale wasio amini yote aliyofanya kutuokoa humfanya kuwa mwongo. Tunaposema Yesu alichukua dhambi zetu zote alipobatizwa, wao husema “Hapana! Asingeweza chukua zote! Bali alichukua ile dhambi ya asili tu, hivyo zile zote za kila siku bado ninazo.”
Hivyo huendelea kusisitiza kwamba inawapasa kuomba sala ya toba ili kuomba msamaha wa dhambi za kila siku ili kuombolewa. Hivi ndivyo walivyo amini. Je, na wewe unaamini hivyo? Yeyote mwenyekuamini ya kwamba dhambi zetu zote hazikutakaswa katika ubatizo wa Yesu anamfanya Mungu ni mwongo.
Yesu ametukomboa kwa mara moja na kwa wakati wote alipobatizwa na kutoa damu yake Msalabani
Ni nani aliye Mwongo?
Yule asiye amini Juu ya
ubatizo wa Yesu.
Yesu alibatizwa na kuzichukua dhambi zetu zote kwa mara moja na wakati wote. Mungu huwaokoa wale wote wenye kuamini ubatizo na damua ya Yesu bali huwa mbali na wale wasio amini. Hawa watakwenda motoni. Hivyo, ukiokoka na usipo okoka hutegemea ni lipi unaloamini. Yesu aliukomboa ulimwengu kutoka dhambini. Wenye kuamini wameokolewa wasioamini bado hawajaikolewa na wanamfanya Mungu kuwa mwongo.
Watu hawaendi motoni kwa madhabahu yao, bali kwa kutoamini “Asiyeamini Mungu amemfanya kuwa mwongo” (1 Yohana 5:10) wasioamini ya kuwa dhambi zao zote alibeba Yesu bado watabaki na dhambi mioyoni mwao. Hawawezi kusema hawana dhambi.
Siku moja nilikutana na Shemasi Fulani, na kumuuliza “Shemasi, je, dhambi zako zote zilitoka moyoni mwako ulipomwamini Yesu?”
“Bila shaka, zilitoka” alijibu.
“Hivyo tangu Yesu azichukue dhambi za ulimwengu na kusema imekwisha umeokolewa je, hivi ndivyo?”
“Ndivyo.”
“Hivyo huna tena dhambi?”
“Ndiyo, sina.”
“Sasa inatokea nini ukitenda dhambi tena?”
“Sisi ni wanadamu tu. Itawezekana vipi tusitende dhambi? Hivyo inatubidi tutubu kwa kuzisafisha kila siku dhambi hizo.”
Shemasi huyu bado anazo dhambi moyoni kwa kuwa, hajatambua juu ya ukombozi ulio wa kweli.
Watu wa aina hii humfanya Mungu mjinga na mwongo. Je, Yesu aliye Mungu alishindwa kuziondoa dhambi zote za dunia hii? Inasikitisha kwa kweli! Ikiwa Yesu hakuziondoa dhambi zote, basi ataweza vipi kuwa Mungu wa Wokovu? Angeweza vipi kutueleza tumwamini yeye? Je, utakwenda kumfanya yeye kuwa mwongo? Nakushauri usifanye hivyo!
Biblia inatuonya tusimdhihaki Mungu. Maana yake tusimfanye kuwa mwongo na kujaribu kumlaghai. Sivyo alivyo tulivyo sisi.
Mtume Yohana anatueleza kwa hakika juu ya Injili ya ukombozi. Wengi hawaamini Mungu aliyoyafanya kwetu – ukweli wa Yesu Kristo kuja kwa maji, kwa damu na kwa Roho.
Yapo makundi mawili ya Wakristo; wale wasio amini Biblia isemavyo na kusema “mimi ni mwenye dhambi” na wale wenye kuamini yote Mungu aliyoyafanya kwao kwa kusema “Mimi ni mwenye haki.” Je, ni kundi lipi husema kweli?
Wale wasio amini yale Mungu aliyotafanya kwa usema mwingine, wasio amini ushuhuda wa maji, damu na kwa Roho ni waongo. Wana imani isiyo ya kweli. Wasio amini humfanya Mungu mwongo.
Usimfanye Mungu kuwa mwongo. Yesu alikuja Mto Yordani na hivyo (kwa kubatizwa) alitimiza haki yote (kwa kuchukua dhambi zote za ulimwengu).
Wasioamini huukana ubatizo wa Yesu na Utukufu wake
Ni kipi shetani
Anacho kikana?
Ubatizo wa Yesu.
Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Wale waliozaliwa upya huamini kwamba dhambi zao zilitwikwa kwa Yesu alipobatizwa na walikombolewa kwa maji na damu ya Yesu. Huamini kwamba Yesu alizaliwa duniani kupitia Bikira Mariamu, na alibatizwa Yordani kabla ya kufa kwake msalabani na alifufuka.
Wenye haki wanao ushuhuda huu mioyoni mwao. Ukweli wa wokovu umo ndani ya imani juu ya Yesu, aliyekuja kwa maji, damu na Roho ushuhuda umo ndani yako. Nakushauri uwe na ushuhuda ndani yako. Hakika nakueleza. Utakuwa si wokovu ikiwa hakuna ushuhuda, ukweli wa wokovu ikiwa hakuna ushuhuda, ukweli wa wokovu ndani yako.
Mtume Yohana alisema “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yaki” (1 Yohana 5:10). Je, kuamini damu yake msalabani tu ndiyo kuwa na ushuhuda? Au maji bila damu? Yakupasa kuamini mambo yote matatu ili utambuliwe na Mungu.
Ni Yesu pekee aweza kukushuhudia kuwa umeokoka J, unasema waweza kuwa na ushuhuda wa mambo mawili kati ya matatu? Hii ni kuamini Mungu kwa njia yako. Ni ushuhuda wa nafsi yako.
Wapo wengi wa aina hii wapo wengi duniani wenye kuamini mawili kati ya yale matatu. Hushuhudia ya kwamba wameokoka na hata kuandika vitabuni juu yake. Ni kwa namna gani walivyo na ulaghai. Ina leta mtafaruku. Hujiita Wainjilisti. Hudhani kuwa si hivyo tu bali pia ni wenye kushika dini” Hawaamini juu ya “maji” na bado hajigamba juu ya wokovu! Wanaweza kueleweka, lakini bado hawana ushuhuda wa Mungu moyoni mwao. Ni wanafiki.
Unaweza vipi kuuita ni wakovu? Wale tu wenye kumwamini Yesu, aliye kuja kwa Roho, maji na damu ndiyo wenye ushuhuda wa Mungu na wanadamu.
Mtume Paulo alisema “ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali katika nguvu na katika Roho Mtakatifu na uthibitifu mwingi” (1 Wathesalonike 1:5). Shetani hupendezwa watu wanapo amini damu ya Yesu pekee. Lo! Nyie wajinga sana nimewalaghai!” Wapo wengi wenye kuamini kwamba wanapoisifu damu ya Yesu shetani hukimbia. Hufikiri Shetani huogopa msalaba pekee. Yakupasa uelewe shetani hugeuka kivuli tu, na yakupasa usidanganyike na hilo.
Mtu aliyepagawa na mapepo hutoa povu mdomoni. Si jambo gumu kwa shetani kufanya atakalo juu ya mtu huyo kwa kuwa anayo nguvu juu yake. Atatumia ujanja kidogo tu. Mungu alimpa shetani nguvu aina zote, isipokuwa nguvu ya kuua shetani anaweza kumfanya mtu atetemeke kama unyasi, kupiga mayowe, kutoa povu mdomoni.
Sasa yote haya yanapotokea, waumini hukemea “Toka! Katika jina la Yesu!, Toka! Katika jina la Yesu!” Na mtu huyo anaporudia fahamu zake na kuwa kawaida, humwambia ilikuwa ni kwa nguvu ya damu ya Yesu pekee iliyokuwa na nguvu ya kumuokoa na kumponya. Lakini hii sivyo si damua ya Yesu pekee. Ni shetani anafunika kwa kivuli tu.
Shetani anawaogopa sana wale tu wenye kumwamini Bwana Yesu, walio safishwa na kuwa safi kwa ubatizo wake, na kuchukua hukumu zao kwa damu yake na baada ya siku tatu alifufuka. Shetani hawezi kuwa karibu na ushuhuda wa ubatizo wa Yesu na wokovu wa damu.
Kama ninavyoelewa Mapadre wa Kikatoliki mara nyingine hufanya huduma ya kutoa pepo wachafu kwa namna hii. Tumeona katika sinema, kwa jina “THE OMEN”, Padre aliyebeba msalaba mdogo wa mbao na kuutikisa, hatimaye alikufa. Aliyezaliwa upya (aliye okoka katika damu na maji) hawezi kushindwa namna hii hata kidogo!
Aliyezaliwa upya ana uhakika anapotaja damu na maji katika Yesu. Shetani anapojaribu kumwogopesha, atamwambia “Je, unajua Yesu alizichukua dhambi zangu zote?” Ndipo shetani atakapokimbia kwani hapendi hata siku moja kukaa karibu na walio okoka. Aliye okoka akiwa hapo, shetani atajaribu kwa njia zote kumkimbia. Inasemekana wale wasio mwamini Mungu wamemfanya kuwa mwongo. Hawaamini ushuhuda wa mwana wake, juu ya maji na damu yake.
Ushuhuda wa Mwana
na Mungu ni upi?
Ubatizo wake, Damu yake
na kwa Roho.
Ni upi ushuhuda wa Mwana wa Mungu? Nao ni huu, alikuja kwa Roho, na kuchukua dhambi zetu zote kwa maji. Alichukua dhambi zote za ulimwengu na kutoa damu yako msalabani kwa dhambi zote. Je, huu siyo ukombozi wa damu, maji na kwa Roho?
Watu husema uongo mbele za Mungu kwa sababu hawaamini Injili iliyo ya kweli katika maji na damu, Injili ya ukombozi kamili. Injili nyingine zaidi ya hii ni ulaghai mtupu! Imani zao ni potofu, na hueneza Injili ya ulaghai bila malengo.
Hebu na turudi katika 1 Yohana 5, mstari wa 11 unasema “Na huu ndio ushuhuda ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.” Inasema Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu upo kwa yule mwenye kuupokea tu! Nao upo kwa mwanawe.
Wale wenye kupokea uzima wa milele ni wale walio kombolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Wamepokea uzima wa milele ni wale walio kombolewa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Wamepokea uzima wa milele na kuishi milele pia. Je, wewe umeupokea?
Katika mstari wa 12 “Yeye aliye naye mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima” kwa namna nyingine, yule anaye amini mambo mwana wa Mungu hana huo uzima.” Kwa namna nyingine, yule anayeamini mambo mwana wa Mungu aliyofanya hapa duniani – Ubatizo wake, kifo chake msalabani na ufufuko wake – unao huo uzima wa milele. Lakini yule anayeondoa hata moja kati ya haya hakika hawezi kupata uzima wa milele na pia ukombozi.
Mtume Yohana aliwatofautisha watu wa Mungu kwa msingi wa Imani ya mambo Yesu aliyofanya maji, damu na kwa Roho; Haya mambo hutuelezea ikiwa wanalo Neno ndani yao au la! Alibainisha ukombozi kwa imani zao juu ya maji ya ubatizo wa Yesu, damu yake na kwa Roho.
Wasiozaliwa upya hawawezi kutambua kondoo kati ya Mbuzi
Nani awezaye
kutambua Waliokombolewa
na wasiokombolewa?
Aliyezaliwa upya.
Mtume Yohana kwa uwazi alionyesha wenye haki waliokombolewa. Mtume Paulo pia. Ni vipi Mtumishi wa Mungu kwa umakini anaweza kutofautisha kati ya watumishi wa Mungu na walaghai? Wale waliokombolewa kwa kuamini katika maji na damu ya Yesu hupokea nguvu ya utambuzi.
Hata ikiwa mtu ni Mchungaji, Mwinjilisti au Mzee wa Kanisa ikiwa anashindwa kumgundua aliyekombolewa au kutofautisha kati ya kondoo na mbuzi, hakika yeye binafsi hajazaliwa upya bado na hana uzima ndani yake. Lakini wale waliozaliwa upya kweli wanaweza kwa hakika kutofautisha wasio na uzima hawawezi kuona tofauti na hata kutambua.
Ingawa hatuwezi kutofautisha rangi gizani, kijani, nyeupe itabaki nyeupe. Lakini pia unapofumba macho, huwezi kuona wala kutambua rangi.
Bali, wale wenye kuangaza macho yao wanaweza bila shaka kuona hata tofauti ndogo ya aina za rangi. Wataweza kutaja ipi kijani na ipi nyeupe. Vile vile upo wazi tofauti kati ya waliokombolewa na wale wasiokombolewa.
Yatupasa kuhubiri Injili ya ukombozi, Injili ya maji, damu na kwa Roho. Yatupasa kuamka na kuangaza. Tunapo kusanya watu na kueneza imani ya kweli, hatuneni maneno yetu. Katika Biblia 1Yohana 5 inatuelezea maana yake. Yatupasa kuelezea hatua kwa hatua ili kusewepo na mkanganyiko.
Neno tunalo hubiri, yaani Neno la maji, damu na kwa Roho la Yesu ni nuru ya ukombozi. Kufanya “maji” ya Yesu kujulikana kwa watu wote yatupasa tuangaze. Kufanya “damu ya Yesu” ijulikane ni kuangaza. Yatupasa kuifanya ieleweke wazi ili pasiwepo na yeyote duniani asiyefahamu ukweli huu.
Ikiwa walio okoka hawajaamka na kuangaza, basi watu wengi watakufa bila ukombozi na haitamfurahisha Mungu. Atatuita kuwa ni watumishi wavivu. Ni lazima tueneze Injili ya maji na damu ya Yesu.
Unajua kwa nini narudia rudia haya mara nyingi, ni kwa sababu ubatizo wa Yesu ni muhimu sana kwa wokovu wetu. Tunapoongea na watoto wetu yatupasa kuwaelezea mambo kwa kurudia rudia, kupitia kila jambo muhimu ili wawe na uhakika wa kuelewa.
Ikiwa tunamfundisha mtu asiyejua chochote, yaani mbumbumbu, asiyefika shule, yatupasa kuanza herufi moja baada ya nyingine. Na ndipo kwa hatua tutaweza kumfundisha jinsi ya kuandika maneno kwa herufi. Anapoweza kuweka maneno pamoja kama vile “HUKUMU,” basi tuanze kumueleza nini maana ya neno hilo. Na hii ndiyo sawa na jinsi ya kuwaelezea watu juu ya Yesu ili kuhakikisha wanaelewa kweli.
Yatupasa kwa uwazi kuelezea juu ya ubatizo wa Yesu. Alikuja duniani kwa maji, damu na kwa Roho. Nakuombea ili umwamini Yesu kama Mwokozi na kukombolewa.
Ukombozi wa maji na Roho hububujika toka katika imani juu ya ubatizo wa Yesu, Damu yake katika msalaba, na kwa imani kwamba Yesu ni Mungu na Mwokozi wetu.