Search

Mahubiri

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-4] Ubatizo Wa Yesu Ni Mfano Wa Wokovu Kwa Wenye Dhambi (1 Petro 3:20-22)

(1 Petro 3:20-22)
“Watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja siku za Nuhu, Safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache; yaani watu wanane, walio okoka kwa maji. Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni. Malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiisha chini yake.”
 

Kwa njia gani tutaweza
Kuwa wenye haki?
Kwa Neema ya Mungu.

Mungu alitutambua kabla ya kuzaliwa kwetu hapa duniani. Alitambua ya kwamba tutazaliwa tukiwa wenye dhambi na kutuokoa wote wenye kuamini kupitia ubatizo wake uchukuao dhambi zote za ulimwengu. Aliokoa wote wenye kuamini na kuwafanya kuwa watu wake.
Haya yote ni matokeo ya Neema ya Mungu. Kama inavyosema Zaburi ya 8:4 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie?” Waliokombolewa na kuokolewa toka dhambini ni wapokeaji wa upendo wake wa pekee. Ni watoto wa Mungu.
Tulikuwa vipi hapo awali sisi wenye kuamini damu tu na Roho kabla ya kuwa watoto wa Mungu kabla ya kufanywa wenye haki na kuokolewa kwa kupewa haki ya kumwita Baba? Tulikuwa wenye dhambi, wenye dhambi tu, tuliozaliwa ili tuishi duniani miaka 70 au 80 kama tutakuwa na afya.
Kabla ya kuoshwa dhambi zetu, na kabla ya kuwa na Imani juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake tulikuwa watu wasio haki na wenye uhakika wa kuangamia.
Mtume Paulo alisema ilikuwa ni neema ya Mungu kwake yeye kuwa alivyo sasa. Tunamshukuru Mungu kwa neema yake. Muumba alikuja duniani na kuokoa kutufanya watoto wake, watu wake. Tunamshukuru kwa neema ya wokovu wa maji na Roho.
Nini sababu inayoruhusu sisi kuwa watoto wake, wenye haki? Je, ni kwa sababu ya uzuni wetu? Je, ni kwa kuwa ni wenye thamani? Au ni wema sana? Hebu na tufikiri jambo hili na kushukuru pale panapo hitajika.
Sababu ni kwamba Mungu alituumba ili tuwe watu wake na kuturuhusu tuishi katika Ufalme wa Mbinguni pamoja naye. Mungu ametufanya kuwa watu ili kuturuhusu tuishi naye milele. Na hii ndiyo sababu pekee Mungu kutubariki na uzima wa milele. Hakutufanya kuwa watu wake kwa kuwa tu wazuri, wenye thamani au muhimu zaidi ya viumbe wake. Sababu pekee ni kwamba ametupenda.
“Mfano wa mabo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1 Petro 3:21). “Watu wanane waliokoka kwa maji” (1 Petro 3:20).
Ni watu wachache, mmoja mjini na wawili katika familia moja ndiyo walio okoka. Je, walikuwa ni wenye thamani zaidi ya wengine? Hata kidogo! Sisi sote si wenye thamani, bali tumeokolewa kwa njia nyingine kupitia imani katika maji kwa Roho.
Huu ni muujiza kati ya miujiza kwa kuokolewa na ni zawadi isiyo na pingamizi, zawadi ya Mungu kuweza kumwita yeye ni Baba, Bwana wetu. Hatuwezi kukataa hili. Tunaweza vipi kumwita yeye kuwa ni Baba au Bwana ikiwa bado ni wadhambi?
Tunapofikiri ukweli huu kwamba tumeokolewa tunajua kwamba Mungu alitupenda pasipo kikwazo Je, hatuwezi kumshukuru kwa hilo? Tungeweza kuzaliwa na kufa bila tegemeo lolote maishani mwetu na kuishia motoni kama si upendo na baraka yake. Tunamshukuru Mungu tena na tena kwa baraka na upendo uliotufanya wenye thamani kuwa watoto wake mbele ya macho yake.
 

Tuliupata Wokovu huu wenye thamani kupitia ubatizo wa Yesu

Kwa nini watu wale wa
Kipindi cha Nuhu waliangamia?
Kwa sababu hawakuamini maji
(ubatizo wa Yesu).

“Mfano wa mambo haya ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi.” Imeandikwa katika 1Petro na roho nane tu ndizo ziliokoka kwa maji. Ni watu wangapi walikuwepo kipindi hicho cha Nuhu? Hatuna njia ya kujua ni wangapi, lakini hebu tufikiri ikiwa walikuwa kiasi cha milioni. Watu 8 tu katika familia ya Nuhu kati ya mamilioni ndiyo walio okoka.
Kwa kuonyesha ni sawa na nyakati hizi. Wanasema leo kuna zaidi ya watu bilioni 6 ulimwenguni. Ni watu wangapi walio takaswa dhambi zao kati ya wale wenye kumwamini Yesu leo. Ikiwa tulipaswa kuangalia mji mmoja, basi wapo wachache kati yao.
Katika mji wangu wenye watu 250,000 ni wangapi waliokombolewa toka dhambini? Labda 200? Sasa uwiano utakuwa vipi? Itakuwa na maana kwamba pungufu ya mtu mmoja kati ya elfu moja ndiyo pekee walio pokea bara ya ukombozi.
Inakadiriwa kwamba, wapo watu milioni 12 walio Wakristo hapa Korea, pamoja na Wakatoliki. Kati ya hawa ni wangapi kati yao waliozaliwa upya katika moji na Roho? Tunapaswa kukumbuka kwamba wapo watu 8 tu walio okoka kati ya idadi ya watu wote duniani kwa kipindi kile cha Nuhu. Yatupasa kujua na kuamini kwamba Yesu alichukua dhambi zote za wale wenye kuamini ubatizo wake.
Ni watu wachache wenye kuamini kwamba Yesu ametukomboa sisi sote kwa ubatizo wake na damu yake msalabani. Hebu jaribu kuangalia picha maarufu ya ufufuko wa Yesu. Ni watu wangapi wali onyeshwa wamefufuka? Unaweza kuona wakishuka toka jumba la Yerusalemu kuelekea aliko Yesu aliyenyosha mikono kuwapokea. Jaribu kufikiri ni wanatheologia au watumishi.
Leo hii wapo wanatheologia wengi ulimwenguni, lakini tunapata wachache wenye kuelewa na kuamini juu ya ubatizo wa Yesu kama nyenzo muhimu ya ukwe wa ukombozi. Wengine husema alibatizwa ili kuweza kufanana nasi zaidi sisi wanadamu.
Lakini imeandikwa katika Biblia kwamba Mitume wote pamoja na Petro na Yohana, walishuhudia juu ya ubatizo wa Yesu kama kuhamisha dhambi zetu kwake na tunaamini hivyo pia.
Mitume wanashuhudia maandiko ya kwamba dhambi zetu zilihamishiwa kwame Yesu kwa ubatizo wake. Huu ni ushuhuda wa ajabu wa neema ya Mungu kwamba tunaweza kombolewa kwa kuamini hilo tu.
 

Hakuna neno “Labda” juu ya habari ya Ubatizo wa Ukombozi

Ni nani apokeaye upendo
Usio na mipaka kwa Mungu?
Yule anaye amini ubatizo wa
Yesu na Damu yake.

Watu huona ni sawa kumwamini Yesu ili tu waokoke. Madhehebu yote hukubali juu ya wokovu katika imani za aina yao, na wengi hudhani ubatizo wa Yesu ni sehemu tu ya mafundisho ya kanuni ya jamii ya Kikristo. Lakini hii sivyo. Kati ya maelfu ya vitabu, vichache nilivyobahatika kusoma sikuweza kupata kitabu chochote juu ya wokovu unaozingatia kwa kina uhusiano kati ya ukombozi katika ubatizo na damu ya Yesu na wokovu wa Mungu.
Ni watu 8 tu ndiyo walio okolewa kipindi cha Nuhu. Sijui ni wangapi katika nyakati hizi, lakini nafikiri si wengi. Wale walio okolewa ni wale walioamini ubatizo wa Yesu na Damu yake. Nilipo tembelea Makanisa mengi, niligundua tena kwamba wapo watu wachache wenye kuhubiri Injili ya ubatizo wa Yesu, ambayo ndiyo injili ya kweli.
Ikiwa hatutaamini ukombozi wa ubatizo na damu ya Yesu, bado sisi ni wadhambi na hatujaokoka, haijalishi uaminifu wetu kuhudhuria ibada Kanisani. Tunaweza kuwa waaminifu kwa kwenda Kanisani katika maisha yetu yote, bado tu wadhambi.
Ikiwa tumekwenda miaka 50, bado tu wadhambi mioyoni imani yetu ya miaka 50 si kitu bali unafiki. Ni vema zaidi kuwa na siku moja ya ukweli. Kati ya wale wenye kumwamini Yesu, ni wale tu wenye kuamini ukweli juu ya ubatizo wake na Damu yake wataingia katika ufalme wa Mbinguni.
Imani ya kweli ni kuamini ukweli kwamba Mwana wa Mungu alishuka ulimwenguni na alibatizwa ili kuchukuwa dhambi zote za ulimwengu. Na hii ndiyo imani ituongozayo kwenda katika ufalme wa Mbinguni. Yatupasa pia kuamini Yesu alitoa damu yake msalabani kwa ajili yako na yangu. Yatupasa kuelewa mpangilio huu ili tuweze kumshukuru na kumtukuza Mungu.
Sisi ni nani? Ni watoto wa wanadamu ambao walio okolewa kwa ubatizo na damu ya Yesu. Kwa nini tusimshukuru yeye? Yesu alibatizwa mto Yordani alipo kuwa na umri wa miaka 30 ili kutuokoa. Kwa hili, alizichukuwa dhambi zetu zote na kupokea hukumu yetu pale msalabani.
Tunapowaza juu ya hili, hatuna na ziada bali ni kunyenyekea kwa kumshukuru. Yatupasa kuelewa yote Yesu aliyo yafanya ulimwenguni ni kwa ajili ya Wokovu wetu. Kwanza alikuja ulimwenguni. Alibatizwa akasulubiwa msalabani, alifufuka kutoka wafu baada ya siku tatu na amekaa mkono wa kuume wa Mungu Baba.
Ukombozi wa Mungu ni wa kila mtu bila upendeleo. Wokovu wa Yesu ni wa wote, mimi na wewe Tunamsifu Mungu kwa upendo wake na baraka.
Upo wimbo usemao “♫Ipo habari njema, kati ya watu, ulimwenguni, mimi ni mmoja wao niliye na upendo na wokovu wa Mungu. Ni upendo wa ajabu. Upendo wake kwangu. Ipo habari njema ulimwenguni, mimi ni mmoja wao niliye okolewa, nimefanya kuwa wake, nimevishwa upendo wake. Oh! Upendo wa Mungu neema ya Mungu. Ni upendo wa ajabu. Upendo wake kwangu. ♫”
Yesu alishuka kutuokoa, wewe na mimi na ukombozi wa ubatizo wake ni kwa ajili yetu sote. Injili hii si visa na ngano (hadithi, simulizi za kale) ni ukweli uliotuletea uhai toka magumu ya ulimwengu kuelekea ufalme mzuri wa Mungu. Yakupasa uelewe kwamba imani ni mahusiano kati yako na Mungu.
Yesu alishuka ulimwenguni ili kutuokoa. Alibatizwa na kupokea hukumu ya msalaba ili kututakasa dhambi zetu.
Ni baraka ya namna gani kwa aliye mwaminifu, kuliita jina la Mungu Baba. Tunaweza vipi kuamini katika Yesu kama Mwokozi wa kuokolewa kutoka dhambini kwa imani? Ni rahisi kwa kuwa anao upendo usio na mpaka kwetu. Tumeokolewa naye aliye tupenda kabla ya kunipenda.
 

Yesu alizitakasa dhambi zetu zote kwa mara moja na kwa wakati wote

“Kwa maana Krsito naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1 Petro3:18). Yesu Kristo alibatizwa kwa ajili ya ukombozi wetu na kufa mara moja msalabani ili kutuokoa, tusio haki.
 
Je, tumeokolewa mara
moja au kwa hatua?
Mara moja na kwa wakati
wote.

Alikufa mara moja hapa duniani ili kutukinga na hukumu ya Mungu. Ili tuweze kuingia katika ufalme wa Mbinguni na kupata uzima wa milele, alishuka duniani katika umbo la mwanadamu na kutakasa kabisa dhambi zetu zote kwa mara moja kwa ubatizo wake, kifo na ufufuo.
Je, unaamini kuwa Yesu Kristo ametuokoa kwa ukamilifu wote katika ubatizo wake na damu yake? Ikiwa hujaamini Injili ya ubatizo na damu yake, hujaokolewa bado. Kwa kuwa sisi ni wenye udhaifu hatuwezi kuzaliwa upya ikiwa hatutoamini kwamba Yesu alizisafisha dhambi zetu zote kwa mara moja na wakati wote kwa ukamilifu wote. Kwa ubatizo wake na damu yake.
Alibatizwa ili kuzichukua dhambi zetu zote na kuhukumiwa msalabani kwa ajili yetu sote. Alitakasa dhambi zote mara moja na kwa wakati wote kwa ukombozi wetu sisi wanadamu katika ubatizo na damu yake.
Haiwezekani kwa wanadamu kukombolewa ikiwa tutaendelea kutubu kila wakati tunapotenda dhambi, kuwa wema na wenye fadhila nyakati zote kwa kutoa, sadaka na mali zetu Makanisani na penye huduma.
Hivyo, imani katika ubatizo wa Yesu ni lazima kwa ajili ya ukombozi wetu. Inatulazimu kuamini juu ya maji na damu. Kwakufanya matendo mema pekee hakuhusiani na ondoleo la dhambi zetu.
Haiwezi kuleta jambo jema katika wokovu wetu ikiwa tutagharamia kununua nguo nzuri kwa ajili ya maskini au kuandalia chakula kizuri wachungaji. Yesu ametuokoa kupitia ubatizo wake na damu yake. Ikiwa tutaamini kwamba Mungu ametuokoa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake kwa mara moja na kwa wakati wote, basi hakika tumeokolewa.
Wengi wataweza kudhani kwamba ingawa Mungu alisema hivyo katika Biblia, itawabidi wafikiri zaidi. Hili ni shauri lao, lakini yatupasa kuamini Neno lake kama ilivyo andikwa.
Katika Waebrania 10:1-10 imeandikwa kwamba Yesu ametuokoa mara moja. Ni kweli kwamba Mungu ametuokoa mara moja. Ni kweli kwamba Mungu ametuokoa sisi tulioamini ubatizo wa Yesu na damu yake mara moja. Tuamini hili. “♫ Alikufa mara moja, alituokoa sote mara moja, Ndugu amini na ukombolewe. Utue mzigo wako katika ubatizo wa Yesu. ♫” Huu ni wimbo wetu siku zote. Yesu alituokoa kwenye uhasi na dhambi mara moja na kwa wakati wote kwa kubatizwa kwake mara moja na kwa damu yake msalabani.
“Mwenye haki kwa ajili yao wasio haki” (1 Petro 3:18). Yesu ni Mungu asiye na dhambi, na hakutenda dhambi kamwe Alishuka kwetu katika mwili ili kuokoa watu wake na dhambi zao. Alibatizwa na kuchukua dhambi zote alikutokoa dhambini.
Dhambi za watu wote toka kuzaliwa kwao hadi mwosho wa kifo zilitwikwa kwake Yesu alipobatizwa na wote wameokolewa hukumuni alipo toa damu yake msalabani. Alibatizwa kwa ajili ya wenye dhambi na kufa kwa ajili yao kama kafara.
Upo ukombozi katika ubatizo wake. Yesu alituokoa sisi sote, wote tulio wadhambi, mara moja na kwa wakati wote. Ni kwa kiasi gani tulivyo dhaifu! Yesu alitukomboa sisi sote toka kuzaliwa kwetu hadi kifo kwa kujito yeye mwenyewe kwa hukumu ile ya msalaba sisi wenye kumwamini Yesu yatupasa kuamini kwamba ametuokoa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wake na damu yake.
Sisi ni dhaifu, lakini Yesu si dhaifu. Sisi si waaminifu, lakini yeye ni mwaminifu. Mungu alituokoa mara moja na kwa wakati wote. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Mungu alitupa mwanae wa pekee. Alimbatiza ili azibebe dhambi zote za ulimwengu ili aweze kupokea hukumu za wanadamu wote.
Huu ni ukombozi wa ajabu. Ni upendo wa ajabu. Tunamshukuru Mungu kwa upendo wa wokovu wake. Yeye huokoa wale wote wenye kuamini maji na damu ya Yesu; Ubatizo na damu aliyotoa Yesu na ukweli ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. 
Wenye kumwamini Yesu wataweza kuokolewa kwa kuwa wameamini ukweli wa ubatizo wake na damu yake ni kuweza kuwa na uzima wa milele kama haki yao. Yatupasa sote tuone hili.
Ni nani aliye tuokoa? Je, ni Mungu, au ni moja kati ya alivyo viumba ndivyo huokoa? Ni Yesu, aliye Mungu, ndiye aliye tuokoa. Tumeokolewa kwa kuwa tumeamini ukombozi wa Mungu na huu ndio wokovu wake.
 

Yesu ni Bwana wa Wokovu

Nini maana ya “Kristo”?
Kuhani, mfalme na Nabii.

Yesu Kristo ni Mungu. Yesu maana yake ni Mwokozi na Kristo “Mpakwa mafuta”. Kama vile Samweli alivyo mpaka mafuta sauli katika Agano la Kale, Wafalme walipakwa mafuta, makuhani na manabii ili kuhudumia kazi, walipaswa kupakwa mafuta.
Yesu alikuja duniani na kupakwa mafuta kwa kazi tatu, ile ya ukuhani, ufalme na unabii. Ikiwa kuhani wa mbinguni, alibatizwa ili kubeba dhambi zote za wanadamu.
Kwa kutii mapenzi ya Baba yake, alijitoa kuwa sadaka ya upatanisho mbele ya Baba. “mimi ndimi njia, kweli na uzima, Mtu haki kwa Baba bila kwangu” (Yohana 14:6). Yesu anaokoa sisi wale wenye kumwamini kwa kuzichukua dhambi zote kupitia ubatizo wake na kwa kusulubiwa kwake.
“Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu” (Walawi 17:11). Yesu alimwaga damu yake msalabani baada ya ubatizo wake, hivyo alitoa mwili wake mbele ya Mungu kama mshahara wa dhambi zetu ili wale tunao mwamini tuweze kuokolewa.
Alifufuka siku ya tatu baada ya kufa msalabani na alikwenda kuhubiri Injili kwa roho zilizo fungwa jela. Wale ambao bado hawajakombolewa wanafananishwa na wafungwa wa kiroho katika jela ya dhambi, na kwao Yesu anahubiri injili ya kweli injili ya maji na damu. Mungu ametupa Injili ya maji na roho ili kutuokoa. Kwa yeyote mwenye kuamini atazaliwa upya.
 

Ubatizo na Damu ya Yesu unaokoa wenye dhambi

Kwa vipi unaweza kuwa 
na Dhamira njema 
Mbele za Mungu?
Kwa kuwa na imani katika ubatizo 
na Damu ya Yesu. 

Yesu Kristo ni mwokozi wetu na imethibitishwa katika 1 Petro 3:21 “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu).” Ubatizo wa Yesu kwa maji ni lazima uwe we wokovu kwa wenye dhambi.
Yesu amesafisha dhambi zetu kwa kuzibeba yeye mwenyewe kwa kupitia ubatizo wake. Je, unaamini ubatizo wa Yesu? Je unaamini ya kwamba mioyo yetu alisafishwa na kuwa safi kwa dhambi zetu zote kupitia ubatizo wa Yesu? Mioyo yetu ni safi kwa kusafishwa dhambi zote, lakini bado miili yetu inatenda dhambi.
“Kuzaliwa upya” haina maana kwamba mtu hatotenda dhambi tena. Sisi tulizaliwa upya, pia hutenda dhambi lakini mioyo yetu ni safi kwa sababu imani yetu ipo katika ubatizo. Kwa kifungu hicho kisemacho “siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu” (1 Petro 3:21).
Ikiwa Yesu alizisafisha dhambi zangu, na ikiwa Mungu ameikubali hukumu badala yangu, basi ni kwa vipi nisimwamini Yesu? Kwa kujua ya kwamba Yesu, aliye Mungu, aliniokoa kwa ubatizo wake na damu yake, ni kwa vipi nisimwamini? Tumeokolewa mbele ya Mungu na sasa dhamiri (mioyo) ni safi. Hatuwezi kamwe kusema mbele ya Mungu kwamba Yesu hakuzisafisha dhambi zetu zote kama vile pia hatuwezi kusema Mungu hatupendi.
Dhamira zetu zimekuwa mbali zaidi na hisia ya dhambi baada ya kuzaliwa upya na hutuambia kila tunapo tenda dhambi. Ikiwa dhamira zetu zitatusuta hata kwa jambo dogo, hatuwezi basi kuwa huru kikamilifu kwa dhambi hadi pale tutakapo jikumbusha juu ya nguvu ya ubatizo wa Yesu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwwa na dhamira njema.
Dhamira yetu inapotusuta, maana yake lipo jambo baya. Maji ya ubatizo wa Yesu hutakasa uchafu wote wa dhambi. Yesu alizichukuwa dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kututakasa hata dhamira zetu. Hakika tunapo amini hili, dhamira zetu zaweza kweli kutakaswa. Ni vipi dhamira zetu zaweza takaswa? Kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Kila mtu ana uovu na dhamira chafu toka kuzaliwa kwake, lakini tunapo amini hili, dhambi zetu zote hutwikwa kwake Yesu na kuondoa doa hili.
Hii ndiyo imani ya waliozaliwa upya. Siyo jambo ambalo huongozwa kwa fikra ndani yako kwa kitu Fulani ili udhamirie kwa kukubali. Je, dhamira yako ni safi? Ni safi kwa kuwa umeishi kwa matendo mema au ni safi kwa kuwa dhambi zako zote alizibeba Yesu na unamwamini yeye? Ni kwa imani pekee ndipo unapo pata dhamira safi.
Yapo maneno yenye uhai na yasiyo na uhai. Ni kwa namna gani dhamira zetu zaweza kutakaswa? Njia pekee ambayo tunaweza kuwa wenye haki na kuwa na dhamira safi ni kwa kuamini ukombozi wa Yesu kikamilifu.
Tunapo amini ubatizo wake unaotutakasa, haina maana kwamba uchafu wa miili yetu umeondokana nasi bali dhamira zetu ndizo safi mbele ya Mungu! Kwa hilo Yesu alikuja kubatizwa, kufa msalabani na alifufuka toka kifoni na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Siku itakapo wadia atarudi ulimwenguni tena “atatokea mara ya pili, pasipo dhambi kwa hao wamtazamiao kwa wokovu” (Waebrania 9:28). Tunaamini atakuja kutuchukuwa, sisi wale tumtazamiao, na tusi na dhambi kwa kuamini Ubatizo wa Yesu na damu yake.
 

Jaribio la Uchunguzi wa Imani

Je, tunaweza kuokolewa 
bila ya Ubatizo wa Yesu?
Kamwe hatuwezi.

Tulifanya uchunguzi na jaribio la ghafla katika Kanisa letu hapa Daejeon.
Mchungaji Park wa Kanisa hilo aliwaeleza waumini ya kwamba hakuna dhambi ulimwenguni bila ya kuelezea maana ya ubatizo wa Yesu. Wanaume husinzia wakati wa mahubiri wanapokuwa wanahudhuria makanisa mengine kwa sababu wachungaji wote walihubiri Injili isiyo na ukombozi utokanao na ubatizo wa Yesu, hivyo hulazimika kutubu kila siku.
Lakini sisi hapa Kanisani petu Taejon, husikiliza mahubiri macho yao yote yakiwa maangavu, kwa sababu wameelezwa ya kwamba dhambi zao zote alizibeba Yesu. Inakuwa ni rahisi sana kwa wanawake zao kuwashawishi kuja Kanisani nao.
Siku moja mmoja wao alikuwa amekaa Kanisani na aliposikia Warumi 8:1 “Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Ghafla aliwaza “Ahaa! Ikiwa mtu atamwamini Yesu hawezi kuwa na dhambi tena. Hivyo hata mimi sina dhambi.”
Hivyo alimpigia simu shemeji yake na marafiki wengine moja baada ya mwingine na kuwaeleza “Je, unayo dhambi moyoni mwako? Basi imani yako si sahihi.” Kwa hili, Mchungaji Park alikuwa amepotea Wanaume hawakujua juu ya ubatizo wa Yesu ila yeye aliwasisitiza ya kwamba hawana dhambi.
Hivyo waumini wakaanza kuwa na tabu. Wanawake waliokuwa washika dini, lakini ndani ya mioyo yao wana dhambi, waume zao waliendelea kusema hawana dhambi. Waume hao walihudhuria ibada mara chache lakini tayari hawakuwa na dhambi mioyoni mwao. Wanawake waliamini ya kwamba wao wote na waume zao walikuwa bado ni wenye dhambi mioyoni mwao. Walianza kubishana juu ya hili. Waume waliendelea kusisitiza hawakuwa na dhambi kwa sababu “hakuna hukumu ya dhambi juu yao walio katika Kristo.” Na wake walibisha, na kusema bado wenye dhambi mioyoni mwao.
Siku moja mmoja wa wanawake hawa alikerwa na jambo hili na kuamua kwenda kumuulizia Mchungaji Park alikuwa na maana gani anaposema dhambi zote alitwikwa Yesu.
Hivyo siku moja, baada ya Ibada, alimwacha mume arudi nyumbani yeye alibaki kumuuliza Mchungaji Park swali lake. Alisema “Najua unajaribu kutueleza jambo Fulani, lakini naamini lipo jambo muhimu lililofichika. Tafadhali nieleze.” Basi Mchungaji Park alimwambia juu ya kuzaliwa upya katika maji na Roho.
Na aligundua mara moja, kwa nini imeandikwa katika Warumi 8:1 “hakuna ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Aliamini mara moja na aliokolewa hatimaye aligundua kwamba dhambi zetu zote alitwikwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake na kwa wale wote walio katika Kristo hawahukumiwi tena.
Alianza kuelewa juu ya andiko hili. Hatimaye aligundua ufunguo wa ukombozi wake ulikuwa ni ubatizo wa Yesu na kwa hiyo tunaweza kuwa wenye haki kupitia ukombozi wa ubatizo wa Yesu.
Kwa kweli mume wake hakwenda nyumbani bali alikuwa akimsubiri nje. Alisikiliza ushuhuda wake ya kwamba dhambi zake zote zimetakaswa na kwa furaha alimuuliza “sasa umekombolewa?”
Lakini aliposikia juu ya Mchungaji alichomwelezea mkewe, alichanganyikiwa. Hakuwa amesikia bado juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu. Alikuwa na uhakika kwamba hakuwa na dhambi moyoni hata kama haamini ubatizo wa Yesu. Kwa mara nyingine tena wakaanza kubishana.
Kwa mara nyingine tena mambo yalikuwa kinyume. Mke alimwuliza ikiwa mumewe alikuwa na dhambi moyoni au la! Alimuuliza ni kwa vipi hawezi kuwa na dhambi ikiwa bado hajaamini ubatizo wa Yesu. Alimsihi achunguze dhamira yake kwa makini ndipo alipogundua katika ugunduzi wake kwamba bado anayo dhambi moyoni mwake.
Hivyo, mume huyo alikwenda kwa Mchungaji Park na kukiri anayo dhambi moyoni. Aliuliza “Walipokuwa wakiweka mikono juu ya kichwa cha yule mnyama wa kafara, ilikuwa ni kabla ya kuchinjwa, au baada ya kuchinjwa?” Hakuwa amesikia juu ya Injili ya maji na kwa Roho, hivyo alijawa na hofu.
Na hii ndiyo maana ya uchunguzi huu wa kiroho. Ilimbidi Yesu abatizwe ili azibebe dhambi za ulimwengu. Hivyo abatizwe ili azibebe dhambi za ulimwengu. Hivyo ilibidi pia afe msalabani kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.
“Je, waliwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kabla au baada ya kuuwawa? Aliuliza hili kwa kuwa hakuelewa juu ya kuwekea mikono na juu ya ubatizo wa Yesu. Hivyo Mchungaji Park alimwelezea juu ya Ukombozi katika ubatizo wa Yesu kwa undani zaidi.
Kwa siku hiyo, Mume huyo alisikia kwa mara ya kwanza Injili ya maji na Roho na alikombolewa. Alisikia mara moja na kukombolewa mara moja.
Hili ndilo jaribio litokanalo na kuondoa ubatizo wa Yesu. Tunaweza kusema hatuna dhambi, lakini hakika tuna dhambi ndani ya dhamira zetu bila ya ubatizo wa Yesu. Watu mara nyingi husema kwamba, Yesu alisafisha dhambi zote kwa kufa kwake msalabani, lakini ni kwa wale tu wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu ndiyo wanao weza kusema kweli kwamba hawana dhambi mbele za Mungu.
Mchungaji Park alithibitsha kwa wanandoa hawa katika Kanisa hili kwamba hawawezi kupata ukombozi wa kweli katika dhambi zao bila kuwa na Imani juu ya ubatizo wa Yesu.
 

Mfano wa Wokovu: Ubatizo wa Yesu

Ni upi mfano wa 
Wokovu?
Ubatizo wa Yesu.

“Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi.” Yesu alishuka duniani ili kusafisha dhambi zote na kufanya dhamira zetu kuwa nyeupe kama theluji. Tumetakaswa na dhambi zetu zote kwa kuwa Yesu alizichukua yeye mwenyewe kupitia ubatizo wake na damu yake. Hivyo, viumbe wote yawapasa kupiga magoti mbele yake.
Tukimwamini Yesu tutaokoka. Tunakuwa watoto wa Mungu na kwenda mbinguni kwa kumwamini Yesu. Tunafanywa kuwa haki kwa kumwamini Yesu. Sisi ni uzao wa kuhani. Tuna haki ya kumwita Mungu kuwa Baba yetu. Tunaishi duniani tukiwa wafalme.
Je, hakuka unaamini kwamba Mungu amewaokoa wale kati yetu wenye kuamini katika ukombozi wa maji na Roho? Ukombozi wetu hautoweza kamwe kukamilika bila ya ubatizo wa Yesu. Imani ambayo Mungu Baba anaikubali kuwa ya kweli ni ile imani ya Injili ya ubatizo wa Yesu Kristo, msalaba wake na Roho ambayo imetuokoa kwa ukamili wote. Hii ndiyo imani ya kweli.
Dhambi zetu zimetakaswa kabisa pale Yesu alipozibeba kwa ubatizo wake, na zililipiwa pale alipo toa damu yake msalabani. Yesu Kristo alituokoa kwa maji na Roho. Ndiyo! Tunaamini!