Search

Mahubiri

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-5] Maana ya Injili halisi ya Kuzaliwa Upya tena (Yohana 3:1-6)

(Yohana 3:1-6)
“Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo jina lake Nikodemo mkuu wa Wayahudi. Huyo alimjia usiku akamwambia Rabi twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu akamwambia. Amin, amin nakuambia mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, awezaji mtu kuzaliwa akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa Maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilicho zaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.”
 

NINI MAANA YA KUZALIWA UPYA KULINGANA NA BIBLIA

Katika ulimwengu huu wapo wengi wenye kutaka kuzaliwa upya kwa njia ya kumwamini Yesu tu. Hata hivyo ningependa kukwambia awali kwamba kuzaliwa upya si takwa letu, au kwa maneno mengine si jambo ambalo litokanalo na matendo yetu pekee.

Je, kuzaliwa upya 
kunahusika na hisia na mabadiliko 
katika miili yetu?
Hapana, Kuzaliwa upya mara ya pili 
kwahusika na badiliko la kiroho. Ni kwa 
mwenye dhambi kuzaliwa upya 
kama asiye na dhambi.

Wakristo walio wengi hawafahamu upotofu juu ya jambo hili. Huamini ya kwamba wanauhakika kuwa wamezaliwa upya. Huamini hivyo kwasababu zifuatazo, Kati yao huchukulia wokovu kama namna ya kuwa na makanisa mengi mapya, wengine hujitoa kwa kuhubiri habari za kristo wakiwa wamisionari kwa wale ambao hawajafikiwa katika sehemu za mbali, na hata wengine hukataa swala la ndoa maishani mwao na kutumia nguvu zao zote katika kufanya kile wanachokiita kazi ya Mungu.
Hii haitoshi. Wapo wengine hutoa michango mikubwa ya kifedha katika makanisa yao, au labda hufagia makanisani na kufanya usafi kila siku, yote haya ni katika kujitolea muda wao na mali zao makanisani mwao. Na huamini kuwa juhudi hizi zote zitawapa tuzo ya uzima wa milele. Hutumaini kuwa Mungu atazikubali juhudi zao na hata kuwafanya wazaliwe upya.
Ukweli ni kwamba wapo watu wengi wanaojitolea ili waweze kuzaliwa upya. Wanaonekana mahala pote. Hujibidisha huku wakitarajia siku moja Mungu atawabariki na kuwaruhusu kuzaliwa upya. Watu wa aina hii utawakuta katika madhehebu mbalimbali na taasisi zake, seminari na mahospitalini. Inasikitisha kwamba hawajui ile kweli ya kuzaliwa upya.
Wote hawa hudhani juu ya matendo yao, “ikiwa nitafanya namna hii vyema nitakuwa nimezaliwa upya”. Hivyo huweka mkazo katika matendo yao wakiamini ya kwamba wanajenga msingi muhimu katika kuzaliwa upya na kufikiri ya kwamba “hata mimi nitazaliwa upya siku moja, kama Mchungaji Wesley!” Husoma katika Yohana 3:8, na kutafsiri mistari ya kuwa hakuna awezaye kusema ni wapi baraka ya kuzaliwa upya inatoka na ni wapi inakwenda.
Hivyo watakachoweza ni kujibidisha katika matendo yao huku wakitumaini ya kwamba Yesu atawaruhusu wazaliwe upya siku moja. Wapo wengi wenye kufikiri “ikiwa nitasimama hivi, Yesu atanikubali na kuzaliwa upya siku moja. Nitazaliwa upya tena bila hata kujitambua. Asubuhi moja nitaamka na kujikuta nimezaliwa upya na kujua ya kwamba nitakwenda mbinguni”. Imani hii na matumaini haya hayana matokeo ya kweli.
Kamwe hatutoweza kuzaliwa upya kwa jinsi hii! Hatutoweza kuzaliwa upya kwasababu tu tumeacha kunywa pombe na kuvuta sigara au kwa kuanza kwenda kanisani kikamilifu. Kama Yesu alivyosema yatupasa “kuzaliwa upya katika maji na Roho” tuweze kuingia ufalme wa Mungu. Maji na Roho ni kigezo pekee cha Mungu cha kuzaliwa upya mara ya pili.
Ikiwa mtu hatozaliwa upya kwa Maji na Roho, juhudi zake zote za kuwa mwenye haki mbele za Yesu zitakuwa njia panda. Mtu kamwe hawezi kuzaliwa upya kwa kutoa sadaka, michango au kujitoa kwa aina yoyote. Anaweza kudhani kwa kuwa Mungu ndiye pekee anayemjua aliyezaliwa upya mara ya pili, basi yeye hawezi kufahamu yakuwa amezaliwa upya au hapana.
Anaweza kufarijika kwa kudhani hivi, lakini kuzaliwa upya mara ya pili hakuwezi kufichika chini ya meza. Hakika ni lazima mtu atajitambua ndani yake na kwa wenzake kujua hili pia.
Pengine hutoweza kupata hisia za kimwili, lakini utahisi ndani ya roho. Waliozaliwa mara ya pili hakika ni wale tu waliozaliwa kwa kupitia neno la Mungu, neno la maji, damu na la Roho. Hata hivyo wale ambao hawajazaliwa upya hawatoweza kuelewa hili kama ilivyo kwa Nikodemo.
Hivyo yatupasa kusikiliza maneno ya kweli, ukombozi kupitia ubatizo na damu ya Yesu. Na tunaposikiliza na kujifunza neno la Mungu, ndipo tutakapoikuta hiyo kweli. Kwa maana hiyo ni muhimu kufungua akili zetu na kusikiliza kwa uangalifu sana.
“Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yohana 3:8).
Ikiwa mtu asiyezaliwa upya mara ya pili anaposoma kifungu hiki cha maandiko atafikiri, “ahaa! Yesu alisema sitoweza kuelewa ikiwa nimezaliwa upya au la! Hakuna awezaye kutambua!” Mawazo haya humpa faraja. Lakini huu si ukweli. Inawezekana tusijue upepo unakotokea au uendako, lakini Mungu ajua yote.
Hata kati ya waliozaliwa upya mara ya pili wapo baadhi wasiojua hili hapo awali. Hii inaeleweka. Lakini ndani ya moyo wa mtu ipo injili; neno la ukombozi kupitia ubatizo na damu ya Yesu.
Huu ni ushuhuda wa kuzaliwa upya. Wale waisikiayo injili na kugundua “Lo! Hivyo kumbe mimi sina tena dhambi. Kumbe basi nimekwisha okoka na kuzaliwa upya mara ya pili” wanapoamini na kudumu katika injili ya maji na Roho ndipo wanapokuwa wenye haki, wana wa Mungu.
Wengine mnaweza kuulizwa “Je, wewe umezaliwa upya?” na kujibu “Bado”. “Sasa basi umezaliwa upya?” “Ndiyo naamini nimeokoka” Hapa unatoa jibu lenye utata kwani unafikiri kwamba mtu anapozaliwa upya mara ya pili, anapaswa kubadilika mwili.
Watu kama hawa hudhani kuwa kuzaliwa upya ni kama jambo la kubadilika katika muundo wa maisha. Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawaelewi juu ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
Wapo wengi wasioelewa hili maana yake. Inasikitisha. Hii si kwa waumini wa kawaida tu, bali hata kwa wale viongozi wa makanisa ambao wamo katika upotofu huu. Mioyo ya wale wote tulio zaliwa upya kweli tunasikitika tunapowaona watu wa aina hii.
Ikiwa sisi tunajisikia namna hii, ni kwa kiasi gani basi naye Yesu Mungu wa Mbinguni analiona? Hebu basi nasi sote tuzaliwe upya mara ya pili kwa ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani.
Kuzaliwa upya mara ya pili na kuokolewa inamaana moja. Hata hivyo wapo wengi wasiojua ukweli huu. Kuzaliwa upya maana yake ni kwamba dhambi ndani ya moyo wa mtu inakuwa imesafishwa kwa kupitia kuamini injili ya maji na Roho. Maana yake pia ni kuwa mwenye haki kwa kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na kujitoa kwake msalabani.
Kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili, watu ni wenye dhambi, lakini baadaye wanakuwa wasio na dhambi hata kidogo, waliozaliwa upya kama watu wapya. Wanakuwa watoto wa Mungu kwa kuamini injili ya wokovu.
Kuzaliwa upya maana yake ni kuvaa vazi jipya la ubatizo wa Yesu kufa msalabani na Yesu na kufufuka naye. Ni kwamba mtu anakuwa ni mwenye haki kupitia maneno ya ubatizo na msalaba wa Yesu.
Mtu anapozaliwa toka tumbo la mamaye anakuwa moja kwa moja mwenye dhambi. Lakini anapoisikia injili ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho basi anakuwa amezaliwa upya na kuwa mwenye haki.
Kwa nje mtu wa aina hii haonekani tofauti lakini ndani yake amezaliwa upya kiroho. Na hii ndiyo maana ya kuzaliwa upya. Lakini wapo wachache wenye kujua ukweli huu; yapata moja kati ya kumi. Unaweza kukubaliana na mimi kwamba wapo wachache wenye kuelewa ukweli wa maana ya kuzaliwa upya mara ya pili?
Wale wenye kuamini injili ya maji na Roho na kuzaliwa upya mara ya pili wataweza kutofautisha kati ya ukweli juu ya kuzaliwa upya na kule kuwa Mkristo wa kawaida tu.
 

NI YESU ANAYETAWALA UPEPO

Nani awezaye kufahamu ya 
kuwa amezaliwa upya 
mara ya pili?
Ni waliozaliwa upya tu.

“Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia lakini hujui inakotoka wala inakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” Hapa Yesu alikuwa akizungumzia juu ya wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili. Waliozaliwa upya mara ya pili hufahamu yakua wamezaliwa upya mara ya pili, lakini Nikodemo yeye hakufahamu hili. Mungu anajua ni yupi aliyezaliwa upya, na ni yupi bado na hata aliyezaliwa upya hujua pia.
Hivyo basi wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili hawajui namna mtu anavyo zaliwa upya kama wasivyoelewa upepo unakotoka na unakokwenda. 
Je waweza kuelewa hili ni nani anayesukuma upepo? Mungu ndiye asukumaye. Ni nani aliyeumba upepo? Mungu wa mbinguni ndiye aliyeumba. Ni nani anayetawala hali ya hewa duniani, mikondo ya upepo na maji? Na ni nani aliyeweka pumzi ya uzima katika viumbe hai? Kwa maneno mengine ni nani aliyeweka uhai duniani na kufanya uendelee kuwepo? Si mwingine bali ni Yesu Kristo. Na Yesu ni Mungu.
Inapotokea kuwa hatufahamu maneno ya injili ya maji, damu na roho, kamwe hatutoweza kuzaliwa upya mara ya pili na hatutoweza kuwafundisha wengine kiroho pia. Yesu alituambia kamwe mtu asipo zaliwa kwa maji na kwa Roho basi hajazaliwa upya.
Yatubidi kuamini injili ya maji na Roho, yenye nguvu iwezayo kutufanya kuzaliwa upya mara ya pili. Roho huja na kukaa ndani ya mawazo ya wale wote wenye kuamini injili ya maji na Roho.
Yesu Kristo alibatizwa ili kubeba dhambi zote za wanadamu na kumwaga damu yake msalabani ili kulipia dhambi hizo. Amepandikiza wokovu wa kuzaliwa upya mara ya pili ndani ya mioyo ya wanadamu. Tunapoamini injili hii, Roho huja ndani yetu. Huu ndiyo wokovu katika kuzaliwa upya mara ya pili. Tunaamini katika kusafishwa dhambi zetu zote kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake ndipo tunapozaliwa upya hakika.
Katika Mwanzo 1:2 imeandikwa “nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji na Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji” Imeandikwa ya kwamba Roho wa Mungu alitulia juu ya uso wa maji. Roho wa Mungu alikuwa akitembea nje ya uso wa dunia.
Hii inamaana kwamba Roho hawezi kuingia ndani ya mioyo ya wenye dhambi. Moyo wa yule asiyezaliwa mara ya pili umejaa vurugu, umejaa giza la dhambi. Hivyo Roho wa Mungu hatoweza kukaa ndani ya moyo wa mtu wa aina hii.
Mungu ameshusha nuru ya Injili yake iangaze mioyo ya wenye dhambi. Mungu alisema “na iwe nuru” na ikawa nuru. Ndipo hapo basi Roho wa Mungu alipoweza kukaa ndani ya mioyo ya watu.
Hivyo basi ndani ya mioyo ya watu waliozaliwa upya mara ya pili, wale wenye kuamini injili ya maji na Roho humo hukaa Roho wa Mungu. Hii ndiyo maana ya kuzaliwa “upya mara ya pili.” Wamezaliwa upya ndani ya mioyo kwasababu wamesikiliza maneno ya wokovu wa maji na Roho na kuamini!
Ni kwa namna gani mtu aweza kuzaliwa upya? Yesu anaelezea hilo kwa Nikodemo mfarisayo na kusema “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu” Nikodemo akasema “Awezaje mtu kuzaliwa kwa maji na kwa Roho? Je, mtu aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Kwa vyovyote alichukulia moja kwa moja na kushindwa kufikiri namna mtu anavyoweza kuzaliwa upya.
Yesu alimwambia “Je! Wewe ni mwalimu wa Israel, na mambo haya huyafahamu?” Yesu alimwambia mtu asipozaliwa upya kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu hata kuuona.
Ni kweli kwamba wapo watu wengi wenye kuamini juu ya Yesu pasipo kuzaliwa upya. Wengi wa wakristo hivi leo wanafananishwa na Nikodemo kwa kutozaliwa upya mara ya pili.
Nikodemo alikuwa ni kiongozi wa kiroho katika Israel kwa nyakati hizo sawa na viongozi wa leo katika makanisa. Kwa usemi wa kileo alikuwa kama mbunge wa kitaifa. Kwa nafasi ya kidini alikuwa mwalimu, rabi wa Kiebrania, alikuwa mshika dini mzuri kiongozi wa Kiyahudi. Alikuwa mwanafunzi mhitimu.
Katika Israel nyakati hizo, hapakuwepo na taasisi zinazolingana na shule za nyakati hizi, hivyo watu wote iliwapasa kwenda hekaluni au katika masinagogi kwa nia ya kujifunza chini ya “aliye mwalimu”. Walikuwa ni walimu wa watu kama ilivyo nyakati hizi, palikuwepo na walimu waongo pia. Na walikuwa wakiwafundisha watu pasipo kuzaliwa upya wao wenyewe.
Pia nyakati hizi wapo viongozi wa kidini, viongozi wa makanisa, walimu, wahubiri, wazee wa kanisa na mashemasi ambao hawajazaliwa upya mara ya pili. Kama Nikodemo, hawajui kweli ya kuzaliwa upya mara ya pili. Wengi hudhani ya kwamba tutaweza kuingia tena katika matumbo ya mama mara nyingine katika kuzaliwa upya. Wanajua ya kwamba imewapasa kuzaliwa upya lakini hawajui ni kwa namna gani.
Na kwasababu ya upumbavu wao, kama kipofu apapasaye tembo ili kujaribu kuvuta hisia kwa kutumia mikono yake pekee, mafundisho yao yameelemea kwenye hisia zao na ujuzi. Wanahubiri maadili ya kidunia zaidi. Ondokana na hili basi, watu wengi waaminifu wanazuiliwa katika kuzaliwa upya mara ya pili.
Kuzaliwa upya mara ya pili hakuhusiani na maadili mema. Tunazaliwa upya kwa kupitia imani ya neno la maji, damu na Roho ambalo Mungu ametupatia. Ni injili ya Mungu ambayo inatubadilisha sisi wenye dhambi na kuwa wenye haki.
Yesu alisema maneno haya “Ikiwa nimewambia mambo ya dunia wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mabo ya mbinguni?” (Yohana 3:2) Hakika watu hawakuamini pale Yesu alipowaeleza ukweli kwamba upatanisho wa dhambi zote ulikuwa tayari umekamilika kupitia ubatizo wake. Hawakuamini nini? Hawakuamini ya kwamba upatanisho ulikwisha fanyika kwa kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Na hii ndiyo maana yake alipowaambia watu wasingeweza kumwamini ikiwa angewaambia juu ya “habari za mbinguni”.
Ili kututakasa na dhambi zetu zote, Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kufa msalabani na baadaye kufufuka toka wafu ili kusawazisha njia ya wokovu kwa watakaozaliwa upya.
Hivyo alimweleza Nikodemo kwa kunukuu maandiko katika Agano la Kale yasemayo, “wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni yaani Mwana wa Adamu. Na kama vile Musa alivyomuinua yule nyoka jangwani vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.” (Yohana 3:13-15). Kama Musa alivyomuinua nyoka jangwani, ndivyo hivyo ni lazima Mwana wa Mungu anapaswa kuinuliwa ili kuruhusu yeyote amwaminiye aweze kuwa na uzima wa milele.
Yesu alikuwa na maana gani aliposema haya yote “Na kama vile Musa alipomuinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa?” (Yohana 3:141) Alinukuu kifungu hiki katika Agano la kale ili kuelezea namna ya ubatizo wake na damu yake itakavyoleta upatanisho kwa dhambi zote za wanadamu.
Kwa Yesu kufa msalabani, kwake kuinuliwa ilimbidi kwanza azichukue dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji. Kwa kuwa Yesu hakuwa na dhambi, asingeweza kusulubiwa msalabani. Ili aweze kusulubiwa msalabani, ilimpasa kwanza abatizwe na Yohana Mbatizaji na ndipo hapo dhambi zote za ulimwengu zilipotwikwa juu yake.
Ni kwa kuzichukua dhambi zetu na kuzilipia kwa damu yake ndipo angeliweza kutuokoa sisi wenye dhambi toka hukumuni. Yesu ametupatia wokovu katika kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho.
Hivyo wale wote wenye kumwamini kuwa yeye ndiye Mwokozi moja kwa moja huvaa vazi la ubatizo wake, kifo chake na hivyo kuzaliwa upya naye. Na ndipo Nikodemo alipoelewa hili.
 

KAMA NYOKA ALIVYOINULIWA

Kwanini Yesu alisubiwa?
Kwasababu alibeba dhambi zote 
kwa kupitia ubatizo wake.

Je, unaifahamu habari ya Musa kumuinua nyoka wa shaba jangwani? Habari hii imeandikwa katika Hesabu 21. Inasema kwamba mioyo ya wana wa Israel ilivunjika baada ya kipindi cha safari kutoka Misri hivyo kusababisha kumlalamikia Mungu dhidi ya Musa.
Matokeo yake, Bwana alituma nyoka za moto kati ya watu, ambao waliingia ndani ya hema zao na kuwauma hadi kufa. Baada ya kugongwa na sumu za nyoka hao miili yao ilianza kuvimba na wengi walikufa.
Watu walipoanza kufa Musa, kiongozi wao alimwomba Mungu “Tafadhali Bwana tuokoe”. Mungu alimwambia atengeneze nyoka wa shaba na kumuweka juu ya mti. Akamwambia yeyote atakayemwangalia nyoka huyo wa shaba atapona. Musa akafanya kama alivyoagizwa na kuwatangazia maneno haya ya Mungu watu wote.
Yeyote aliyeamini maneno haya na kumuangalia nyoka yule alipona. Ndivyo hivyo kwa njia hii sisi nasi tunaponywa na sumu ya shetani. Watu wa Israel walimsikiliza Musa na kumuangalia nyoka wa shaba katika mti uliosimikwa na hivyo waliponywa.
Ufunuo wa nyoka huyu katika mti ulio simikwa ulikuwa ni hukumu ya dhambi za wanadamu iliyojuu yake Yesu Kristo kupitia ubatizo na kifo chake msalabani. Alibeba dhambi zetu juu yake ili aweze kulipa adhabu ya wale wenye dhambi ulumwenguni. Hivi ndivyo alivyoipokea adhabu ya dhambi zetu.
Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni ili kuokoa wale wote wenye hatima ya kifo tokana na “sumu ya nyoka”, vishawishi vya shetani. Ili kulipa dhambi zetu zote, ilimpasa abatizwe kwanza na afe msalabani kabla ya kufufuliwa ili kuokoa wale wote watakao mwamini.
Jinsi ile wana wa Israel katika Agano la Kale walivyookolewa kwa kumtazama nyoka wa shaba juu ya fimbo leo hii kwa wale wote wenye kumtumaini Yesu na kuamini kwamba alikwisha lipa deni la dhambi kwa kupitia ubatizo na damu yake basi wataweza bila shaka kuokolewa na kuzaliwa upya mara ya pili.
Yesu amekwisha lipa kikamilifu deni la dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo wa Yohana Mbatizaji katika mto Yordani, kifo chake msalabani na kufufuka kwake toka wafu. Hivyo wale wote wenye kumuamini watapata baraka ya wokovu kupitia huruma yake.
“Wala, hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni yaani, Mwana wa Adamu” (Yohana 3:13) Akiwa kama lipizi la dhambi zetu, Yesu alibatizwa na kumwaga damu msalabani hivyo kufungua lango la mbinguni kwa ajili yetu. “Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” amesema Yesu katika Yohana 14:6.
Hivyo basi kwa njia hii Yesu alibatizwa na kusulubiwa msalabani ili kufungua lango la mbinguni kwa ajili yetu wale wenye kuamini wokovu kupitia kwake. Yesu amekwisha lipia dhambi zetu zote, hivyo yeyote aaminiye ukweli wa maji, damu na Roho ataweza bila shaka kuingia ufalme wa mbinguni.
Yesu ametuokoa kwa injili ya maji na Roho. Kuzaliwa upya kunakuja kwa kuwa na imani na ubatizo na damu ya Yesu pia ukweli kuwa yeye ni Mungu.
“Na kama vile Musa alivyomuinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa” (Yohana 3:14). Nini maana ya kifungu hiki cha maandiko? Kwanini Yesu ilimpasa kusulubiwa? Je, alitenda dhambi yoyote? Je, alikuwa mwenye udhaifu kama tulivyo? Je, alikuwa si mkamilifu kama tulivyo? La hasha; hakuwa.
Sasa basi kwanini ilimpasa asulubiwe? Ilikuwa ni kutuokoa sisi na kulipia gharama ya dhambi zetu zote. Alibatizwa na kusulubiwa ili kutuokoa sisi sote tokana na dhambi zetu zote.
Huu ndiyo ukweli wa wokovu kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho. Yesu ametupa uzima mpya kwa wale wote wenye kuamini ubatizo wake na kifo chake msalabani amabacho ni malipizi ya dhambi zetu zote.
 

MAANA YA MAJI NA ROHO

Nini maana ya Maji 
na Roho?
Maji maana yake ubatizo wa Yesu 
na Roho maana yake 
yeye ni Mungu.

Biblia inatueleza ya kwamba tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, tunazaliwa upya mara ya pili. Kuwa mwana wa Mungu, kuzaliwa upya mara ya pili, kunawezekana kwa kupitia neno la Mungu, injili ya maji, damu na Roho amabyo ndiyo malipizi ya dhambi zetu zote.
Kulingana na biblia “maji” maana yake ni ubatizo wa Yesu (1 Petro 3:21) na “Roho” maana yake ni Yesu kuwa ni Mungu. Na huu ndiyo ukweli katika kuzaliwa upya mara ya pili, kwamba Yesu alikuja ulimwenguni katika mwili wa mwanadamu ili kulipa gharama ya dhambi zetu zote kupitia ubatizo na damu yake.
Alibeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo na kulipia mshahara wa dhambi kwa kufa msalabani. Kwa kubatizwa na kumwaga damu msalabani alituokoa sisi sote wenye kumuamini.
Yatupasa kuelewa kuwa, ubatizo na damu ya Yesu unawakilisha wokovu wetu na ndani yake inatuokoa na dhambi zetu zote. Wale tu waliozaliwa upya mara ya pili ndiyo watakaoweza kuingia ufalme wa mbinguni. Yesu ametuokoa kwa maji ya ubatizo wake, damu yake na Roho. Je una amini hili?
Yesu ni Kuhani Mkuu wa Mbinguni aliyeshuka ulimwenguni kulipia dhambi za dunia. Alibatizwa akamwaga damu yake msalabani na alifufuliwa, kwa hiyo amekuwa mwokozi kwa wote wenye kumwamini.
Yesu alisema katika Yohana 10:7 “mimi ndimi mlango wa kondoo”. Yesu anasimama mlangoni mwa mbinguni. Ni nani atufunguliaye mlango? Ni Yesu Kristo.
Hugeuza uso wake mbali na wale wenye kumwamini bila kujua ukweli wa wokovu wake. Hawaruhusu kamwe wale wasio uamini ubatizo, damu na Roho katika kuzaliwa upya. Hugeuza uso wake mbali kwa yeyote asiyeamini Neno lake, wale wenye kukataa utakatifu wake na wale wasio mtambua kuwa yeye ni Mungu.
Ukweli ulioandikwa ni huu, yeye alikuja ulimwenguni katika mwili, alibatizwa na kufa masalabani ili kufidia dhambi zote za ulimwengu, hata kufa msalabani ili apokee hukumu badala yetu na alifufuka siku ya tatu baada ya kusulubiwa. Yeyote akataaye kuamini ukweli huu hatafufuliwa naye, bali atangamia. Kama alivyoandikwa “Mshahara wa dhambi ni mauti.” (Warumi 6:23)
Hata hivyo, wale wote wenye kuamini katika baraka ya ukombozi kupitia ubatizo wake na damu yake, wale walio takaswa mioyoni mwao wameruhusiwa kuingia katika ufalme wa Mbinguni. Hii ni injili ya kweli katika kuzaliwa upya mara ya pili, injili ambayo ilikuja kwetu kwa maji, damu na kwa Roho. Uwezo wa kuzaliwa katika maji na damu ni injili ya Mbinguni.
Ni wale tu wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu ndiyo watakao zaliwa upya. Wale wenye kuamini injili ya maji, damu na Roho hawana dhambi tena mioyoni mwao, ni walio zaliwa upya mara ya pili kikamilifu.
Hivi leo kama alivyo Nikodemo ambaye hakujua juu ya ukweli huu, watu wengi humwamini Yesu pasipo kujua ukweli wa injili iliyo sahihi. Ni kwa vipi Nikodemo alionekana ni mtu wa daraja la juu katika jamii! Hata hivyo, aliweza kusikia injili toka kwa Yesu, na hapo baadaye Yesu aliposulubiwa alikuwa ndiye yeye tena aliyekuja kuuzika mwili wake. Kwa wakati huo Nikodemo alikuja kuamini.
Nyakati hizi wapo wengi wetu wasio ujua ukweli juu ya maji na Roho wa Yesu. Na zaidi wapo wengi wasio ukubali ukweli hata pale wanapopata nafasi ya kusikia injili ya kweli. Inasikitisha.
Yesu amewezesha kwetu sisi sote kuweza kuzaliwa upya mara ya pili. Nini kitufanyacho kuzaliwa upya mara ya pili? Ni maana ya maji, damu na Roho. Yesu alizichukua dhambi zetu zote alipobatizwa. Alikufa msalabani na kufufuka toka wafu.
Na amewapa wale wote wenye kumwamini yeye baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili. Yesu ni mwokozi mwenye kuwezesha kuzaliwa upya wote wenye kumuamini. Omba basi uweze siku zote kuwa na Yesu aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo.
Yohana 3:16 inasema “wale wote wamwaminio wasipotee bali wawe na uzima wa milele”. Tumepokea uzima wa milele kwa kumwamini Yesu. Tumezaliwa upya kwa kuamini maji na Roho. Ni kweli kwamba ikiwa tutaamini injili ya wokovu ubatizo na damu ya Yesu na kwamba Yesu ni mwokozi na ni Mungu tutaokolewa.
Lakini ikiwa hatutoamini ukweli huu, hakika tutatupwa motoni milele. Ndiyo maana Yesu alimwambia Nikodemo “Ikiwa nimewambia mambo ya duniani wala hamsadiki, mtasadiki wapi mambo ya mbinguni?” 
Mungu ametufanyia nini? Wokovu kupitia Yesu ametupatia kuzaliwa upya mara ya pili. Yesu ametuokoa toka ulimwenguni, kwa shetani na dhambi za ulimwengu. Ili kuokoa wenye dhambi hapa duniani toka hukumu ya dhambi, alibeba dhambi zetu kwa njia ya ubatizo wake, akasulubiwa msalabani na kufufuliwa kifoni. 
Ni chaguo letu ikiwa tutaamini wokovu huu au la. Wokovu wa kuzaliwa upya huja kwa imani ya wokovu utokanao na ubatizo na damu ya Yesu.
Inasemekana kwamba zipo baraka mbili ambazo Mungu ametuwekea wanadamu. Moja ni baraka ya jumla, ambayo imejumuisha vitu vyote vya asili kama vile jua na hewa. Hii inaitwa baraka ya jumla kwasababu imetolewa kwa watu wote, wawe wenye dhambi na wenye haki.
Sasa basi ni ipi baraka ya pekee? Baraka ya pekee ni kuzaliwa upya katika maji na Roho ambayo huokoa wenye dhambi wote.
 

BARAKA YA PEKEE

Nini maana ya baraka ya 
pekee ya Mungu?
Ni ile ambayo Mungu ametufanya tuweze 
kuzaliwa upya mara ya pili kwa 
kupitia ubatizo, kusulubiwa na 
kufufuka kwake Yesu.

Imeandikwa katika Yohana 3:16 “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele” Hii inaeleza juu ya baraka ya pekee ya Mungu. Yesu aliyeshuka duniani katika mwili wa mwanadamu na kutakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na kusulubiwa kwa ajili yetu. Hii ni baraka ya pekee ya Mungu, ukweli kwamba tumekwisha okolewa toka dhambini.
Ni kweli kwamba Yesu ametuokoa na kutubadilisha tukiwa wenye dhambi na kuwa wenye haki. Utaweza kuwa mwenye baraka hii ya pekee ya Mungu kwa kuamini ukweli tu. Je, unaamini? 
Imani yako itakuwa njia panda ikiwa utaikataa baraka hii ya pekee ya Mungu hata kama utakuwa mwaminifu maishani mwako.
Nahubiri mara kwa mara na sintosahau kuhubiri kwamba yakupasa uamini ubatizo wa Yesu na msalaba wake ambavyo ndivyo pekee vinavyowezesha kuzaliwa upya mara ya pili. Kitabu chochote katika biblia kimeonyesha baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kupitia Yesu ambayo ndiyo “baraka ya pekee kwa Mungu” tunayoieleza. Hakuna maelezo ya ziada katika baraka hii ya Mungu zaidi ya ule wokovu wa wenye dhambi kupitia ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake.
Ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake ndiyo baraka pekee kwa Mungu. Wahubiri walio laghai katika ulimwengu huu hawana la ziada juu ya hili. Hawa huja na sura za malaika wa nuru wakiwa wamejivika maadili ya kikristo na ubinadamu. Ndiyo hivi, ndivyo ilivyo! Miujiza waitendayo, uponyaji wa wagonjwa vyote ni uovu ikiwa hawana la kufanya juu ya baraka ya pekee ya Mungu.
Ni baraka hii ya pekee ya Mungu ndiyo itufaayo sisi wenye dhambi, injili ya upatanisho. Kwa baraka yake ya pekee Mungu ametuwezesha kuzaliwa upya mara ya pili. Ametufanya wapya kupitia ubatizo, damu, kifo na ufufuo. Ametufanya tuwe wana wake, kutuweka huru na dhambi. 
Je, unaamini haya? —ndiyo— Je, unabarikiwa? —ndiyo— Ubatizo wa Yesu na damu yake, kifo na ufufuo wake ni baraka ya pekee ya Mungu anayotupa kwa kupitia maji na Roho. Hii ndiyo injili yenye baraka pekee. Tumsifu Bwana kwa kutuokoa kupitia baraka yake ya pekee.
Inasikitisha kuona kuwa Wakristo wengi walio waaminifu katika nyakati hizi bado hawajaijua baraka hii maalumu ya Mungu, injili ya ubatizo na damu, ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Hujaribu kutafuta njia pasipo mwelekeo kwa kutumia theolojia na maadili ya dini zao. Huu ni ujinga!
Ukristo umekuwepo kwa muda mrefu na sasa yapata miaka mia tano tangu kipindi cha Mageuzi, lakini bado wapo watu wengi katika Korea na ulimwenguni pote ambao bado hawafahamu juu ya ukweli katika kuzaliwa upya na juu ya ile baraka maalumu ya Mungu.
Hata hivyo natumaini na kuamini kuwa Mungu atawawezesha kujua ukweli sasa kwasababu tupo karibu na mwisho wa dunia.
Wenye dhambi yawapasa kuzaliwa upya mara ya pili na kukubali ukweli juu ya maji na Roho ili kuweza kuwa wenye haki na kuingia ufalme wa mbinguni. Wakristo wengi wanajibidisha sana ili waweze kuzaliwa upa mara ya pili.
Hata hivyo ikiwa watajaribu pasipo kuelewa maana ya kweli ya kuzaliwa upya mara ya pili, imani yao itakuwa bure. Wanasema yakwamba wanapaswa kuzaliwa upya ili kuweza kuingia ufalme wa mbinguni, lakini hawana ufahamu juu ya ukweli wa namna ya kuzaliwa upya.
Wao hudhani kwamba kwakuwa wanaishika imani kikamilifu, kwakuwa huhisi moto ndani ya mioyo yao, basi wataweza kuzaliwa upya mara ya pili. Lakini kujaribu kuzaliwa upya kwa kutegemea hisia binafsi au kufuata matendo mema ya kidini ni kutupeleka kuwa na imani potofu.
 

NENO LA MUNGU LITUONGOZALO KWA HAKIKA KUZALIWA UPYA MARA YA PILI

Nini tofauti kati ya imani 
na udini?
Imani ni kuamini kile Yesu alichofanya 
katika kutuokoa, hali ya udini ni 
kutegemea mawazo na matendo 
binafsi ya kimwili.

Imeandikwa kwa uwazi katika 1 Yohana 5:4-8 ya kwamba tutaweza kuzaliwa upya mara ya pili ikiwa tu tutaamini juu ya maji, damu na Roho. Ikiwa yatupasa kuzaliwa upya mara ya pili, basi yatupasa kuweka akilini ya kwamba tutaweza kuzaliwa upya kupitia Neno la Mungu tu, neno la kweli. Yatupasa kuelewa kwamba maono, kunena kwa lugha au msisimko wa mwili kamwe hakuwezi kupelekea kuzaliwa upya mara ya pili.
Yesu alisema katika Yohana 3 kwamba mtu hawezi kuingia ufalme wa mbinguni ikiwa hatozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Ikiwa mtu anahitaji kuzaliwa upya basi kwa ujumla yampasa kumwamini Yesu kwa kupitia hatua mbili. Kwanza mtu humwamini Yesu kwa njia ya udini, kugundua dhambi ya moyo kupitia sheria ya Mungu. Kwa mara ya kwanza mtu anapomwamini Yesu ni kwa kupitia sheria ya Mungu na kuelewa kwamba ni mwenye dhambi. 
Tusimwamini Yesu kulingana na mitazamo ya dini na madhehebu ya ulimwengu huu. Ukristo siyo mojawapo ya dini kati ya dini za ulimwengu huu. Bali ni njia pekee ya kuupata uzima wa milele kupitia imani.
Yeyote amwaminiye Yesu kwa msingi wa kidini hakika ataishia mikono mitupu. Atabaki na moyo uliojaa dhambi, vurugu na utupu, je hii si kweli? Sidhani kama ungependa kuishia hivi kwa kuwa mnafiki kama walivyo kuwa mafarisayo katika biblia.
Kila mtu anahitaji kuwa Mkiristo aliye zaliwa upya mara ya pili. Hata hivyo mtu anapo amini ukristo kama dini, huishia kuwa mnafiki huku moyo ukiwa umejaa dhambi. Yatupasa kujua ukweli juu ya kuzaliwa upya.
Yeyote anayeamini ukristo kama dini nyinginezo pasipo kuzaliwa upya mara ya pili hakika ataishia katika kuchanganyikiwa na kuwa na moyo mkavu. Ikiwa mtu atamwamini Yesu hali akiwa hajazaliwa upya, imani yake ni batili. Hivyo ataishia kuwa mlaghai, kwa kujaribu kuonekana mtakatifu mbele ya kila mtu lakini hatimaye kushindwa vibaya. Kwa kuwa unaamini ukristo kama dini, basi utaendelea kuwa mwenye dhambi, mnafiki na kuishi kwa majuto siku zote. Ukitaka kuwekwa huru na dhambi yatupasa kuamini Neno la kweli, injili ya maji, damu na Roho.
 

KUTAFUTA SIRI YA UKOMBOZI KUPITIA UBATIZO WA YESU

Nini kitufanyacho kuzaliwa 
upya mara ya pili?
Ubatizo wa Yesu, kifo chake 
msalabani na ufufuo wake.

Biblia inatueleza kwamba, yeyote aweza kuzaliwa mara ya pili kupitia neno la Mungu ambalo halibadiliki. Hebu sasa na tuangalie maneno ya mtume Petro katika 1 Petro 3:21 “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi.”
Katika biblia imeandikwa ya kwamba, ubatizo wa Yesu ni mfano wa mambo hayo unaotuokoa. Wale wote wanao mwamini Yesu imewapasa kujua si juu ya ule ubatizo wetu bali ubatizo wa Yesu. Ubatizo wa Yesu unatupa wenye dhambi uzima mpya. Amini ubatizo huo wa Yesu utaweza kuzaliwa upya mara ya pili na kupata baraka ya wokovu.
Kwa kuelewa wokovu unapatikana kupitia kuamini ubatizo wa Yesu, basi tutaokolewa na kuwa wenye haki na kupata uzima wa milele. Kwa maneno mengine tunapoamnini ukweli kupitia ubatizo katika Neno la Mungu dhambi zetu hutakaswa mara moja na kwa siku zote.
Kuzaliwa upya ni kuzaliwa kwa mara nyingine. Wengi wetu mara nyingi tunaanza kumwamini Yesu kwa njia ya udini na baadaye tunazaliwa upya kupitia imani pindi tunapogundua ukweli. Jina la Yesu maana yeke “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21).
Tunapomwamini Yesu na kujua nini alichowafanyia wanadamu wote, basi tunawekwa huru na dhambi na kuzaliwa upya mara ya pili kama watu wapya. Kwanza tunamwamini Yesu kwa njia ya udini ndipo tena tunapoisikia na kuamini injili ya ubatizo wake na damu yake na hapo ndipo tunapo okoka.
Ukweli upi unao tuwezesha kuzaliwa upya mara ya pili? Kwanza kabisa ni ubatizo wa Yesu, pili damu yake aliyoimwaga pale msalabani na mwisho ufufuo wake toka kuzimu. Kuzaliwa upya mara ya pili maana yake ni kumwamini Yesu aliye Mungu wetu, mwokozi wetu. Hebu na tutazame namna ile watu wa Agano la Kale walivyoweza kuzaliwa upya.
 

MALIPIZI YA DHAMBI KATIKA AGANO LA KALE: KUWEKEA MIKONO NA SADAKA YA DAMU

Ni ipi injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika Agano la Kale? Kwanza hebu na tusome katika kitabu cha Walawi 1 na nini inasema juu ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Walawi 1:1-5, “Bwana akamwambia Musa na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania akamwambia Nena na wana wa Israeli, uwaambie, mtu wa kwenu atakapo mtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo katika ng’ombe na katika kondoo. Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu, ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe na Bwana. Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa ajili yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. Naye atamchinja huyo ng’ombe mbele ya Bwana kisha wana wa Haruni, hao makuhani wataileta karibu hiyo damu na kuinyunyuzia damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania.”
Mungu anatueleza katika Walawi namna ambayo wana wa Israel walivyoweza kuunganishwa na Mungu kupitia mpangilio wa matoleo ya sadaka. Ni kweli kwamba yatupasa nasi sote kujua na kuelewa hili. Hivyo basi hebu tutazame upya maneno haya.
Mungu alimwita Musa na kuongea naye mbele ya hema ya kukutania. Ilikuwa ni juu ya upatanisho wa dhambi kwa wana wa Israeli. Wana wa Israeli walipomtendea Mungu makosa ya kutotii sheria waliweza kupatanishwa tena kwa kutoa wanyama wasio na doa kwa Mungu.
Sadaka hii ya wanyama ilipaswa kuwa ni ile amabayo Mungu ameichagua na haikupaswa kuwa na doa. Pia ilipaswa kutolewa kwa namna ya kafara aliyoieleza Mungu. Taratibu ya utoaji ni kama ifuatavyo:
Ikiwa mtu yeyote ametenda dhambi katika kipindi kile cha Agano la Kale, ilimbidi kumtolea Mungui sadaka ya ondoleo la dhambi. Kwanza sadaka hiyo ilipaswa isiwe na doa, ndipo mwenye dhambi ataweka mikono yake juu ya hiyo sadaka ya mnyama ili kuitwika dhambi zake juu ya kichwa chake.
Baada ya kuchinjwa kwa mnyama huyo wa sadaka ndipo damu yake itawekwa katika zile pembe za madhabahu na iliyobaki kumwagwa ardhini. Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kutoa kafara katika madhabahu takatifu ambao Mungu aliwapa watu wake kama baraka ya ukombozi.
Sheria na amri za Mungu zilijumuisha vipengele 613 vya matamko yaliyoelezea nini “ufanye” na nini “usifanye”. Mungu aliwapa wana wa Israeli sheria na amri zake. Ingawa watu walijua ya kwamba sheria na amri za Mungu zilikuwa sawa, hata hivyo hawakuweza kuzifuata kwasababu wote walikuwa wamezaliwa wakiwa na aina kumi na mbili ya dhambi walizorithi toka kwa Adamu.
Hivyo walipoteza uwezo wa kutenda mema mbele za Mungu. Wana wa Israeli walipoteza uwezo wa kuwa wema na wenye haki mbele za Mungu. Kwa jinsi hiyo hawakuweza chochote zaidi ya kuendelea na dhambi hata pale walipojaribu kwa bidii kuishi pasipo dhambi. Na hii ndiyo hatima ya wanadamu wote hata leo tunazaliwa na kufa tukiwa wenye dhambi.
Lakini Mungu kwa huruma yake ya milele aliwapa watu wake utaratibu wa sadaka kupitia hiyo wataweza kupatanishwa naye tena. Aliwapa utaratibu wa kutoa kafara hii ya madhabahu takatifu ili watu wa Israeli na wale wengine wote ulimwenguni waweze kukombolewa na dhambi zao. Alionyesha hili kupitia mpangilio wa utoaji sadaka namna ya haki ya upendo wake kwa wanadamu wote. Alionyesha ulimwengu njia ya wokovu.
Mungu aliwapa watu mpangilio wa sadaka na kuamrisha nyumba ya Walawi kutumikia kazi ya utoaji wa sadaka. Kati ya makabila 12 ya Israel Walawi ndiyo pekee walioteuliwa kuhudumia utoaji wa sadaka kwa wana wa Israeli.
Musa na Haruni walitoka katika kabila la Walawi. Hivyo biblia inaelezea sheria na taratibu zinazo husu utoaji wa sadaka katika madhabahu takatifu yaani injili ya upatanisho kwa kuwekea mikono.
Kwa maana hiyo tunapoelewa kikamilifu namna ya utoaji kafara wa Walawi tutaweza kuzaliwa upya. Na ndiyo maana yatupasa kujifunza Neno la Mungu kwa kusoma juu ya sadaka ya madhabahu takatifu. Hii ni sehemu muhimu katika Agano la Kale. Mwisho tunapo rudi katika Agano jipya tuna baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
 

UPATANISHO WA DHAMBI KATIKA AGANO LA KALE

Ni zipi tabia za Mungu?
Haki na upendo.

Mungu alimwita Musa aliyekuwa kabila la Walawi aje mbele ya madhabahu takatifu iliyopo ndani ya hema ya kukutania aweze kumsimika ndugu yake Haruni kuwa Kuhani Mkuu. Haruni ilimpasa kutwika dhambi za watu wote juu ya sadaka ya dhambi.
Hivi ndivyo Mungu alivyomuagiza Musa kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Walawi “Nena na wana wa Israeli uwaambie, mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo katika ng’ombe na katika kondoo” (Walawi 1:2). Mungu anasisitiza hapa juu ya utoaji wa sadaka ya upatanisho. Mtu yeyote anayehitaji upatanisho kwa dhambi zake, ilimpasa kutoa sadaka ya ndama dume au kondoo toka kundi la mifugo yake.
Mungu pia aliwaeleza “matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana” (Walawi 1:3).
Sadaka hii ilikubalika mbele ya Mungu badala ya uhai wa mtu aliyepaswa kufa kwa dhambi zake. Waisraeli waliweza kutwika dhambi kwa kuwekea mkono juu ya kichwa cha mnyama huyo wa sadaka. Mnyama huyo wa sadaka alipaswa kutolewa kwa hiari. Sasa basi hebu tuone katika kifungu kifuatacho cha nne “kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa ajili yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake” Sadaka hiyo itakubalika na Mungu. Pale mwenye dhambi atakapoweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi basi dhambi zake zote zita twikwa juu ya mnyama huyo wa sadaka. Hivyo basi mwenye dhambi ilimpasa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha mnyama huyo mbele ya Mungu ili aweze kukubaliwa na kupata upatanisho kwa dhambi zake.
Mtu atatoa sadaka kwa kumchinja koo mnyama na kuweka damu yake katika pembe za madhabahu na kumwaga chini ya ardhi damu iliyobaki. Ili kulipia dhambi na kuwekwa huru, ilimpasa mtu kutoa sadaka hiyo kulingana na sheria alizoweka Mungu.
Imeandikwa katika Walawi 1:5 “Naye atamchinja huyo ng’ombe mbele ya Bwana, kisha wana wa Haruni hao makuhani wataileta karibu hiyo damu na kuinyunyuzia damu yake kandokando katika madhabahu iliyopo mlangoni pa hema ya kukutania” Ndani ya hema, pembezoni mwa mlango palikuwa na madhabahu ya kuteketeza kwa moto ambayo kingo zake nne ziliwekwa pembe.
Baada ya kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kumtwisha dhambi, mwenye dhambi ilimpasa kumchinja koo mnyama huyo wa sadaka na kuhani akishaichukua damu yake atainyunyizia katika pembe. Pembe zilizopo katika kingo za madhabahu ya kuteketezwa zinatafsiri hukumu ya dhambi. Hivyo kupekea mnyama yule wa sadaka amwage damu ili dhambi zile zilipiwe badala ya mwenye dhambi. Mungu anapoona damu kwenye pembe za madhabahu hufuta kabisa dhambi za anaye toa sadaka hiyo.
Kwanini sadaka hiyo ya dhambi ilipaswa kumwaga damu? Kwasababu “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) na pia uhai umo ndani ya damu. Hivyo imeandikwa katika Waebrania “na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). Kwa jinsi hii, kumwaga damu ya sadaka ya dhambi kunaitimiza sheria ya Mungu ambayo inasema mshahara wa dhambi ni mauti.
Kwa haki zote, damu itolewayo ilipaswa kutoka kwa mwenye dhambi lakini badala yake ilimwagika ya yule mnyama wa sadaka kwa upatanisho wa aliye na dhambi. Kuhani aliiweka damu hiyo kwenye pembe za madhabahu ya kuteketezwa ili kumaanisha kwamba mshahara wa dhambi umelipwa.
Tunaposoma katika kitabu cha Ufunuo 20:11-15 katika Agano Jipya tunaweza kuona pembe hizo zikimaanisha juu ya Kitabu cha Hukumu. Hivyo kuweka damu kwenye pembe ni kuweka damu katika kitabu cha hukumu. Nakushuhudia kwamba hukumu ya dhambi imetimizwa kwa kuwekea mikono na kumwaga damu ya sadaka ya dhambi.
 

DHAMBI ZOTE ZIMEWEKWA KUMBUKUMBU KATIKA SEHEMU MBILI KUU

Dhambi zote za wanadamu mbele ya Mungu zimewekwa kumbukumbu katika sehemu kuu mbili. Moja katika mbao za mioyo na nyingine katika kile kitabu cha Hukumu kilichofunguliwa na Mungu. 
Imeandikwa katika Yeremia 17:1 “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu.”
Walawi 17:11 imesema “kwakuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu” Damu ni uhai wa mwili na dhambi hulipwa kwa damu. Hivyo damu iliwekwa kwenye pembe zilizopo katika kingo za madhabahu ya kuteketezwa. Kulingana na sheria vitu vyote vilisafishwa kwa damu (Waebrania 9:22).
“Kisha atachuna sadaka ya kuteketeza na kuikata vipande vyake. Kisha wana wa Haruni watatia moto juu ya madhabahu na kuzipanga kuni juu ya moto. Kisha wana wa Haruni Makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu lakini matumbo yake na miguu yake ataiosha kwa maji na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu ili iwe sadaka ya kuteketezwa dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto ya harufu ya kupendeza kwa Bwana” (Warumi 1:6-9).
Ndipo basi kuhani atamkatakata vipande na kuviweka juu ya moto wa madhabahu. Kafara hii ilikuwa na maana ya kuwakilisha wenye dhambi mbele za Mungu, ambapo walipaswa kufa kwa njia hii na kumwaga damu kwa kutupwa motoni jehanamu. Kwahiyo hukumu ilitolewa kwa kupitia sadaka ya dhambi ili watu waweze kupatanishwa na dhambi zao.
Sadaka ya kuteketezwa ya wanyama ilikuwa ni kafara kwa ajili ya hukumu ya haki ya Mungu. Mungu alizihusisha sheria zake, yaani ile sheria ya haki na sheria ya upendo kuwa ni sadaka ya upatanisho kwa watu wake.
Kwakuwa Mungu ni mwenye haki ilimpasa basi kuitoa hukumu ya kifo kwa wenye dhambi. Lakini kwakuwa pia aliwapenda watu wake, aliwaruhusu kubebesha dhambi zao kwa sadaka ya dhambi. Katika Agano la Kale, kwakuwa Bwana ametupenda alibatizwa na kusulubiwa ili aweze kuwa sadaka halisi ya dhambi kwa ajili yetu sote. Ubatizo wa Yesu na kifo chake pale msalabani vimefuta dhambi zote ulimwenguni.
 

UPATANISHO WA DHAMBI ZA KILA SIKU KATIKA AGANO LA KALE

Sadaka ya mnyama asiye 
na doa katika Agano la Kale 
inamwakilisha nani?
Inamwakilisha Yesu Kristo.

Hebu tosome katika Walawi 4:27-31 “Na mtu awaye yote katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kusudia kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, naye atapata hatia, akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya. Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa. Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake na kutia katika pembe za madhabahu ya kuteketezwa na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu. Kisha atayaondoa mafuta yake yote kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupenda kwa Bwana na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake naye atasamehewa.”
Kizazi cha Adumu, wana wa Israel na wanadamu wote hapa ulimwenguni wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi. Kwa jinsi hii mioyo yetu sisi sote imefurika dhambi. Zimo kila aina ya dhambi ndani ya moyo wa mtu; mawazo mabaya, uzinzi, tamaa za mwili, uuaji, wizi, ulafi na upumbavu.
Mwenye dhambi anapotaka kupatanishwa na dhambi alizotenda kwa kila siku ilimpasa kuleta mnyama asiye na doa mbele ya hema takatifu. Ndipo ilimpasa kumwekea mikono juu ya sadaka hiyo ya mnyama ili kumtwika dhambi zake zote, kumchinja koo na kutoa damu kwa kuhani ili iweze kuletwa mbele ya Mungu. Kitakachofuata ni kuhani kumalizia hatua iliyobaki ili ikamilishe msamaha wa mwenye dhambi.
Pasipo sheria na amri za Mungu, watu wasingeweza kujua ikiwa kwamba wana dhambi au la. Tunapojichunguza wenyewe kupitia sheria na amri za Mungu tunagundua kwamba tunadhambi. Dhambi zetu hazikuhukumiwa kwa viwango vyetu, bali ni kwa sheria na amri za Mungu.
Watu wa kawaida katika Israel walitenda dhambi si kwasababu walipenda kutenda hivyo, bali kwakuwa walizaliwa wakiwa na dhambi za kila aina ndani ya mioyo yao. Mwenye dhambi huanguka kwasababu ya udhaifu unaoitwa makosa. Dhambi ni pamoja na makosa na uovu wa wandamu.
Watu wote si wakamilifu. Waisraeli hawakuwa wakamilifu, walikuwa wenye dhambi huku wakiendelea kutenda kila uovu. Makosa yao yote na uovu wao unaweza kuwekwa katika mafungu yafuatayo. Tunapokuwa na mawazo ya uovu ndani ya akili zetu yanaitwa ni dhambi na tunapotenda kulingana na mawazo hayo inaitwa uovu. Dhambi za dunia ni pamoja na yote haya ya aina hii.
Katika Agano la Kale, dhambi zilitwikwa juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kwa kuwekewa mikono. Na baadaye mwenye dhambi hakuwa tena na dhambi ndipo sadaka hiyo inapopaswa kuchinjwa na kufa badala ya mwenye dhambi. Mpangilio huo wa utoaji wa sadaka ya dhambi ni kivuli cha hukumu na upendo wa Mungu.
Kwakuwa Mungu ametuumba kutokana na udongo, hivyo basi sisi ni mavumbi tu. Kwa kuweka damu ile kwenye pembe za madhabahu na kumwaga iliyobaki chini ya madhabahu hii inamaana kwamba Waisraeli wamefidiwa kwa dhambi zao zote na kufutwa zote katika vibao vya mioyo yao.
“Kisha atayaondoa mafuta yake yote kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana” Mafuta katika biblia yanamaana ya Roho Mtakatifu. Hivyo, ili tuweze kupatanishwa kwa dhambi zetu zote yatupasa kufuata vile Mungu alivyoagiza ifanyike. Yatupasa pia kuchukulia ndani ya moyo wetu upatanisho wa dhambi zetu kwa namna Mungu alivyo iweka.
Mungu aliwaeleza wana wa Israel kwamba sadaka ya dhambi inapaswa iwe ni mwana kondoo, au mbuzi au ndama dume. Sadaka ya dhambi katika Agano la Kale ilipaswa kuchaguliwa kwa uangalifu mkubwa. Ndama aliye safi. Sababu ya sadaka ya dhambi kupaswa kuwa safi ni kwamba ilipaswa kuonyesha Yesu Kristo ambaye angezaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu wote.
Watu wa Agano la Kale walizitwika dhambi zao kwa kuweka mikono juu ya mnyama asiye na doa, kuhani alihudumia kwa sadaka hiyo ili kulipizia dhambi. Hii ndiyo namna ambayo Israeli ilivyo patanishwa kwa dhambi.
 

IBADA YA SIKU YA UPATANISHO

Kwanini watu wa Israel 
walihitaji kutoa sadaka katika 
siku ya upatanisho?
Kwasababu walikuwa wakiendelea kutenda 
dhambi hadi siku ya kifo. Sadaka ya 
dhambi za kila siku haikuweza 
kuwatakasa mbele za Mungu.

Hata hivyo kadri walivyoendelea kutoa sadaka kila siku waliendelea kutenda dhambi, sadaka hizo hazikuweza kukidhi hitaji la ondoleo la dhambi zao zote. Hivyo, hatua kwa hatua walianza kupuuzia. Ilikuwa kama juhudi isiyo na kikomo katika kupatanishwa na dhambi zao za kila siku na hivyo kuwafanya wajione kuwa wangeweza kuendelea pasipo ibada hii.
Haijalishi ni kwa namna gani tutajaribu, hakika hatutoweza kutoa sadaka ya upatanisho iliyobora kwa ajili ya dhambi zetu. Hivyo malipizi ya kweli ya dhambi zetu yanapaswa kutolewa kwa kupitia moyo uliojaa imani katika sheria ya wokovu Mungu aliyotutayarishia sisi sote.
Kwasababu ya udhaifu wetu, haijalishi ni kwa kiasi gani tunajibidisha kwa kuishi katika sheria ya Mungu, zaidi tunagundua ni jinsi gani tusivyowakamilifu na wadhaifu. Hivyo Mungu amewapa Waisraeli njia ya kupatanishwa kwa mara moja kwa dhambi zao zote (Walawi 16:17-22).
Imeandikwa katika Walawi “amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba siku ya kumi ya mwezi mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya aina yoyote mzalia na mgeni akaaye kati yenu. Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana. Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu ni amri ya milele” (Walawi 16:29-30).
Kwa jinsi hii watu wa Israel waliweza kuwa na amani mara moja kwa mwaka wakati kuhani alipohudumu siku ya upatanisho kwa kutoa sadaka ya dhambi siku ya kumi katika mwezi wa saba wa kila mwaka. Wakiwa wametakaswa na dhambi zao ndipo basi wakawa na amani katika siku hiyo.
Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba kuhani mkuu Haruni, akiwa mwakilishi wa Waisraeli ilimpasa kuhudumia katika utoaji wa sadaka ya upatanisho. Katika siku hiyo makuhani walio salia hawakuruhusiwa kuingia katika hema takatifu. Kwanza Haruni mwenyewe ilimpasa ahudumie katika kutoa sadaka ya upatanisho wa dhambi zake binafsi na za ukoo wake wa Walawi kabla ya kugeukia kutoa kwa ajili ya watu wote wa Israeli, kwasababu yeye na nyumba yake walikuwa na dhambi pia.
Alihudumu kwa ajili ya watu kwa kutoa sadaka kwa namna hii, “kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili kura moja kwa ajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruna atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana na kumtoa awe sadaka ya dhambi. Bali yule mbuzi aliyeangukia na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli” (Walawi 16:7-10).
Baadaya kutoa kafara hizo kwa ajili ya upatanisho wa nyumba yake na mwenyewe binafsi Haruni “atapiga kura juu yake wale mbuzi wawili kura” moja kwa ajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya yule wa kuachiliwa (Azazeli).
Kwanza, moja ya wale mbuzi wawili atatolewa kwa ajili ya Bwana. Hapa kuhani mkuu aliweka mikono yake juu ya mbuzi kwa niaba ya watu wote ili kumtwika dhambi walizotenda katika kipindi cha mwaka mzima.
Damu yake ilitolewa na kunyunyuziwa mara saba katika kile kiti cha rehema ndani ya patakatifu pa patakatifu. Watu wa Israel waliweza kusamehewa kwa dhambi zao zote kwa kipindi chote cha mwaka mzima. Badala ya watu wa Israel kufa kwa dhambi zao, kuhani Haruni alitwika dhambi zote juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kumwacha abebe. Na alimtoa sadaka yule mbuzi mwingine hai kwa Mungu. Hii ilikuwa ni sadaka inayotolewa kwa ajili ya watu.
 

KWA AJILI YA WATU
 
Akiwa mbele ya watu wote, Haruni aliweka mikono yake juu ya mbuzi yule wa sadaka na kukiri mbele za Mungu “Bwana, watu wa Israel wametenda dhambi ya kuua, uzinzi, wizi, ulafi, ulaghai……. na wameabudu sanamu. Hawakutunza Sabato takatifu, wameliitia jina lako bure na wamevunja vipengele vya sheria na amri zako” Ndipo basi atatoa mikono yake baada ya haya. Kwa yote haya, dhambi zote za watu kwa mwaka mzima zitawekwa juu ya mnyama huyo wa sadaka.
Hebu tuone katika Walawi 16:21 “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao naam dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kasha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.”
Mnyama huyo wa kuachiwa (Azazeli) atatangatanga jangwani hadi kufa na dhambi za watu wa Israel juu ya kichwa chake. “Azazeli” kiebrania maana yake “kuachiliwa”. Inamaana kwamba sadaka hiyo ya dhambi iliachiliwa kwa ajili ya Bwana kwa niaba ya watu wa Israeli.
Hivyo dhambi za Israeli zilitwikwa juu ya Azazeli kwa kupitia kuwekewa mikono na Haruni. Kwa njia hii Waisraeli walisamehewa dhambi zao. Walipokuwa wakimuona kuhani mkuu akiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na kumuachia jangwani, watu wote Israeli waliamini utoaji wa kafara hiyo kwa ajili ya upatanisho, walikuwa na uhakika kuwa wamepatanishwa kwa dhambi zao. Ibada hizi zote za kafara katika Agano la Kale zilikuwa ni vimvuli vya “injili ya kuzaliwa upya mara ya pili” katika Agano Jipya.
Katika Agano la Kale kuwekea mkono na damu ya mnyama wa sadaka ilikuwa ni injili ya wokovu wa dhambi. Kimsingi imebaki kuwa sawa na wakati huu wa Agano Jipya.
 

INJILI YA UKOMBOZI KATIKA AGANO JIPYA

Katika Agano Jipya ni kwa namna ipi dhambi zote za watu zilifutwa?
Imeandikwa katika Mathayo 1:21-25 “Naye atazaa mwana, naye mwana utamwita jina lake Yesu, maana yake ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yoye yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumla wa nabii akisema. Tazama Bikira atachukua mimba naye atamzaa mwana nao watamwita jina lake Immanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomuagiza; akamchukua mke asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe akamwita jina lake Yesu.”
Bwana wetu Yesu alishuka ulimwenguni kwa jina Imanueli ili kuokoa wanadamu wote na dhambi zao. Hivyo akaitwa Yesu. Yesu alikuja kubeba dhambi zote za dunia. Alikuja katika mwili wa mwanadamu ili awe mwokozi wa watu. Alitimiza wokovu na kutuweka huru na dhambi milele.
 

INJILI YA KUZALIWA UPYA MARA YA PILI

Ni kwa njia gani Yesu anatuweka huru na dhambi zetu zote? Amefanya hivi kupitia ubatiwzo wake. Hebu na tuangalie katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema mimi nahitaji kubatizwa na wewe nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwakuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwnangu mpendwa wangu ninayependezwa naye.”
Katika Agano Jipya, Yesu alipofikisha umri wa miaka 30 alikwenda kwa Yohana Mbatizaji katika mto Yordani. Alibatizwa naye na kubeba dhambi zote za wanadamu. Kwa kufanya hivyo alitimiza haki ya Mungu.
 

SABABU GANI YESU ALIBATIZWA YORDANI?

Nini kilichodhihiriswa 
katika injili?
Haki ya Mungu.

Hebu sasa natuangalie tukio lile wakati Kuhani Mkuu wa mbingu alipokutana na kuhani mkuu wa mwisho wa wanadamu. Hapa tunaweza kuona haki ya Mungu kupitia ubatizo ulio leta upatanisho wa dhambi zote za ulimwengu.
Yohana Mbatizaji aliye mbatiza Yesu alikuwa mkuu kati ya wote waliozaliwa na wanawake. Yesu alimshuhudia Yohana Mbatizaji katika Mathayo 11:11 “Amin nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji” Namna ile dhambi za watu zilivyoweza kufutwa wakati kuhani mkuu Haruni alipoweka mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi katika siku ile ya upatanisho, ndivyo hivyo katika Agano Jipya dhambi zote za ulimwengu zilivyoweza kufutwa pia pale Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji.
Injili ya kuzaliwa upya mara ya pili ni injili iliyo kamilisha ondoleo la dhambi zetu zote za zamani, za sasa na zijazo. Hivyo injili ya ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu ilikuwa ni injili ya Mungu iliyopangiliwa ili kutimiza haki yote, ambayo iliokoa watu wote duniani. Yesu alibatizwa kwa jinsi iliyo stahili ili kupatanisha dhambi za ulumwengu.
Nini maana ya kutimiza “haki yote”? Maana yake ni Mungu kusafisha dhambi zote za ulimwengu kwa njia inayostahili. Yesu alibatizwa ili kutakasa dhambi zote za wanadamu “kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hadi imani” (Warumi 1:17).
Haki ya Mungu imedhihirishwa katika uamuzi wa kumtuma mwana wake Yesu hapa duniani ili kutakasa dhambi za ulimwengu kupitia ubatizo wake kwa Yohana Mbatizaji na kwa kifo chake msalabani.
Katika Agano Jipya, haki ya Mungu imeelezwa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake. Tunakuwa wenye haki kwasababu Yesu alizibeba dhambi zetu zote sisi wanadamu kwa takribani miaka elfu mbili iliyopita katika mto Yordani. Tunapoukubali wokovu huu wa Mungu ndani ya mioyo yetu haki ya Mungu inatimizwa kwa uhakika.
“Yesu akajibu akamwambia kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini, na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye” (Mathayo 3:15-17).
Ujumbe huu unatuonyesha kwamba Mungu mwenyewe alishuhudia juu ya ukweli wa ubatizo wa mwanawake ulio itimiza haki ya wokovu. Mungu alikuwa anatuambia “Yesu huyu aliyebatizwa na Yohana Mbatizaji, sasa amekuwa hakika ni mwana wangu” Mungu alishuhudia kwamba mwana wake Yesu Kristo alibatizwa ili kuleta upatanisho wa wanadamu. Alifanya hivyo ili kazi takatifu ya mwanawake Yesu isiwe bure.
Yesu ni mwana wa Mungu na pia mwokozi wa wenye dhambi ulimwenguni. “Ninayependezwa naye” alisema Mungu. Ni kweli kwamba Yesu alitii mapenzi ya Baba kwa kubeba dhambi za wanadamu wote kupitia ubatizo wake.
Neno ubatizo maana yake “kusafisha, kutwika, kuzikwa”. Kwakuwa dhambi zote alitwikwa Yesu alipobatizwa tunalohitaji basi ni kuamini injili ya wokovu wa dhambi zote za ulimwengu.
Kutimia kwa unabii wa wokovu katika Agano la Kale kulihitimishwa kwa njia ya ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya. Hivyo unabii wa Agano la Kale hatimaye ulipata mwenzake katika Agano Jipya. Vile watu wa Israel walivyopatanishwa kwa dhambi zao mara moja kwa mwaka katika Agano la Kale, ndivyo ilivyo sasa dhambi za watu wote ulimwenguni zilivyo twikwa kwa Yesu na kufutiliwa mbali milele katika Agano Jipya.
Walawi 16:29 ni mfano wa Mathayo 3:15. Yesu alibatizwa ili azibebe dhambi zote za ulimwengu. Nashukuru kwa ubatizo wake, wale wote wenye kuuamini msamaha wake wa milele wameokolewa; dhambi zao zote zilifutwa katika mbao za mioyo yao.
Ikiwa hukubali na kuamini hili moyoni mwako juu ya huu ukweli wa ubatizo wa Yesu na kifo chake pale msalabani kamwe hautoweza kutakaswa na dhambi zako hata kama wewe unaishi maisha ya utakatifu kwa kiwango kikubwa. Ni kwa njia ya ubatizo tu wa Yesu ndipo neno la Mungu litatimia na dhambi zetu kufutwa. Wokovu wa kweli hupatikana kwa kupitia ukombozi wa dhambi zetu zote, au kwa maneno mengine kupitia ubatizo wa Yesu. 
Kwa kuelewa hivyo, Je, utafanya nini? Je, utakubali huu wokovu kwa moyo wako wote? Au utakataa? Hakika jambo hili si hadithi ya mtu, bali ni Mungu mwenyewe. Yesu alikufa msalabani kwasabu alibeba dhambi zako zote kwa ubatizo wake. Je, unakubali kwamba kusulubiwa kwa Yesu ni matokeo ya ubatizo wake?
Imeandikwa katika Warumi 8:3-4 “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwasababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.” 
Kwakuwa sisi ni wanadamu tusio weza kamwe kufuata sheria na amri za Mungu kutokana na udhaifu wa miili yetu, Yesu alibeba dhambi zetu zote juu yake. Huu ni ukweli wa ubatizo wake. Ubatizo wa Yesu ulitabiri kifo chake pale msalabani. Hii ni hekima halisi ya Injili ya Mungu.
Ikiwa umekuwa ukiamini kifo cha Yesu masalabani pekee, sasa nakusii ugeuke na ukubali kwa moyo wako wote injili ya wokovu kupitia ubatizo wa Yesu. Ndipo sasa utaweza kuwa kweli mtoto wa Mungu.
 

INJILI HALISI 

Ni ipi injili halisi?
Injili ya Maji na Roho.

Injili halisi ni ile injili ya upatanisho wa dhambi. Injili hii ni ya ubatizo wa Yesu, kifo chake na ufufuo ambao Mungu ametuonyesha. Yesu Kristo ametakasa dhambi zetu zote kwa wakati mmoja kwa kubatizwa katika mto Yordani na kwa njia hii ametupatia wokovu kwa wote wenye kuamini ukweli huu. Kwa imani yetu dhambi zetu zote tutakazo tenda mbeleni zimetakaswa pia.
Sasa, yeyote atakayeamini ubatizo wa Yesu na damu yake masalabani ameokolewa na dhambi zake zote daima milele. Je unaamini? Ikiwa ndiyo, basi hakika utakuwa ni mwenye haki.
Hebu na tusome kwa ufupi kilichotokea baada ya ubatizo wa Yesu katika Yohana 1:29 imeandikwa “Tazama! Mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”
Yohana Mbatizaji alishuhudia kwamba Yesu alikuwa ni Mwana-Kondoo wa Mungu aliyeichukua dhambi ya ulimwengu. Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu pale alipombatiza Yesu katika mto Yordani. Kwa nyongeza kwa kuwa Yohana Mbatizaji ndiye aliyembatiza Yesu basi alikuwa na nafasi ya kumshuhudia, “Tazama! Mwana—kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” Yesu alibatizwa na kuibeba dhambi ya ulimwengu, hakika hii ndiyo injili yenyewe ya kuzaliwa upya mara ya pili.


“Tazama! Mwana—kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29) Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake.
Dhambi ulizotenda toka kuzaliwa hadi kufikisha umri wa miaka kumi zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu. Je unaamini kuwa dhambi zako zote alizibeba Yesu? —Ndiyo naamini.— Je, na makoso yako tangu ukiwa na umri wa miaka 11 hadi 20? Unaamini kuwa nayo alibeba Yesu? —Ndiyo naamini.— Je, na zile dhambi utakazotenda siku zijazo pia nazo zimo katika dhambi za ulimwengu? —Ndiyo pia zimejumuishwa.— Alizibeba Yesu? —Ndiyo alibeba.— Je, hakika unaamini kwamba dhambi zako zote alijitwika Yesu? —Ndiyo naamini.— Je, unaamini kuwa alijitwika kwa kupitia ubatizo wake? —Ndiyo naamini.—
Je, hakika unapenda kuokolewa tokana na dhambi za ulimwengu? Ikiwa unakubali, basi amini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Utakapo amini tu, utakuwa umeokolewa. Je, unaamini hilo? Huu ni wokovu wa kweli katika kuzaliwa upya mara ya pili. Ubatizo wa Yesu na damu yake ndiyo injili halisi katika kuzaliwa upya mara ya pili. Ni baraka ya Mungu kwa wale wote wenye dhambi ulimwenguni.
Kuamini wokovu wa kuzaliwa upya mara ya pili kwa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, kutazamia upendo wake ndiyo namna ya kuwa na imani na kuzaliwa upya kwa hakika. Alama ya kuzaliwa upya ni maji na damu ya Yesu. Yakupasa ukubali maneno ya kweli yaliyo andikwa katika Biblia.
 

IMANI HALISI

Tunaushuhuda gani ndani ya 
mioyo ya waliozaliwa upya?
Ya kwamba Yesu ametuondolea 
dhambi zetu zote kwa ubatizo 
na damu yake.

Maana ya udini ni kumwamini Yesu kulingana na vile uonavyo kwa mawazo yako, kukataa neno halisi la Mungu. Hata hivyo, wokovu wa dhambi ni mbali na mawazo binafsi. Imani ni kuchukulia maneno ya Agano la Kale na Jipya, kukataa mawazo binafsi. Ni kuchukulia kama ilivyoandikwa katika biblia na kukubali wokovu kupitia maji na damu; ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Mtu ataweza kuokolewa kwa kuchukulia moyoni hekima ya injili halisi.
Pasipo ubatizo wa Yesu, hakuna kubebeshwa dhambi zetu kwa Yesu, na pasipo kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi. Dhambi zetu zote alitwikwa Yesu kabla ya kupelekwa msalabani na kumwaga damu yake hapo. Tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani katika kuzaliwa upya mara ya pili tunawekwa huru kwa dhambi zetu zote za dunia.
Imani ya kweli ni kumuamini Yesu Kristo moja kwa moja, alitusafisha kwa dhambi zetu zote alipobatizwa; ni kuamini kwamba alibeba hukumu ya dhambi zetu zote msalabani. Yatupasa kuamini haki ya wokovu wa Mungu. Mungu alitupenda sisi sote kwa kiwango kikubwa hata kutuokoa kwa kupitia ubatizo wa Yesu na damu mslabani. Tunapoamini injili hii, tunaokolewa kwa dhambi zetu zote, kuwa huru na hukumu na kufanyizwa kuwa wenye haki mbele ya Mungu.
“Bwana ninaamini, sikustahili wokovu huu lakini ninaamini injili ya ubatizo wa Yesu kusulubiwa na kufufuka kwake” Yatupasa kumshukuru Bwana kwa baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili. Kuamini injili iliyohalisi ya kuzaliwa upya mara ya pili ndiyo imani ya kweli.
Ukeli wa kuzaliwa upya mara ya pili ndiyo huu, “Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia kuja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). “Tena mtafahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). “Yatupasa kujua kweli na kuamini juu ya maji, damu na Roho ambavyo hushuhudia hiyo kweli” (1 Yohana 5:5-8).
“Nayo hiyo kweli itawaweka huru” Haya ni maneno ya Yesu juu ya maji na damu. Je, umekwisha wekwa huru? Je, wewe ni mwenye udini au imani? Yesu anawahitaji wale tu walio na imani juu ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
Ikiwa unaamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, wewe si mwenye dhambi tena moyoni. Ingawa ikiwa utamwamini Yesu kwa jinsi ile ya kidini tu, wewe bado unaishi na dhambi kwasababu hujawa na imani iliyo kamili ya wokovu wa Yesu. Watu wa udini hujaribu kujipatia ukombozi wa dhambi zao kwa njia ya toba za mara kwa mara. 
Kwa namna hii, watu wa aina hii hawatoweza kamwe kuondolewa dhambini mara moja. Hata ikiwa wataendelea kutubu maishani mwao haitoweza kuchukua nafasi ya msamaha kamili wa dhambi upatikanao kwa ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Hebu na tuokoke kwa kuamini injili ya Yesu ambayo imetakasa dhambi zetu zote za ulimwengu, hata zile zijazo mbeleni.
Nakwambia kweli tena, kutubu kila siku kamwe hakutoweza kuchukua nafasi ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili. Wakristo wote yawapasa kuamini ondoleo la dhambi kupitia injili ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Haitowezekana kutubu dhambi zote kikamilifu. Toba ya uongo haitoweza kutuongoza kuelekea mbele ya Mungu bali zaidi itaridhisha nafsi zetu tu. Toba isiyo ya kweli ni kukiri kwa upande mmoja ambapo kamwe hakujali mapenzi ya Mungu. Na hii sivyo Mungu anavyohitaji tuwe.
Ni ipi basi toba ya kweli? Ni kumgeukia Mungu kurudi katika neno la wokovu wa Yesu na kuamini vile neno lilivyoandikwa. Injili inayotuokoa ni ile ya ubatizo wa Yesu, kusulubiwa na kufufuka. Tunapoamini injili kikamilifu ndipo tunapo okolewa na kupokea uzima wa milele.
Hii ndiyo hekima ipatikanayo katika injili ya kuzaliwa upya mara ya pili, ni kuamini ubatizo wa Yesu na damu pamoja na habari njema ya ufalme wa Mungu inayotuwezesha kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho, na maana ya kuzaliwa upya katika ubatizo wake na damu yake pale msalabani. Ndipo tutakapoweza kuingia na kukaa katika ufalme wa Mungu. Yatupasa kuamini neno la Mungu. Mambo haya mawili hushuhudia ondoleo la dhambi, yaani ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo maneno yatuwezeshayo kuzaliwa upya mara ya pili.
Je, unaamini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili na ondoleo la dhambi? Imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani huokoa dhambi zote duniani. Tutaweza kuzaliwa upya mara ya pili kwa imani. Ikiwa Biblia inatuambia ya kwamba Yesu anasafisha dhambi zote za waovu duniani, basi ni kwanini tusiamini na kuweza kuzaliwa upya mara ya pili?
Wale wenye kuamini mambo haya mawili ambayo yanashuhudia juu ya kuzaliwa upya upya mara ya pili, ubatizo wa Yesu na kusulubiwa ndiyo waliozaliwa upya hakika. Na yeyote mwenye kumwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huu ndani yake (1 Yohana 5:3-10). Unapomwamini Yesu haipaswi kuikataa injili ya maji na damu na Roho.
Kama vile Jemedari Naamani alivyotakaswa katika mto Yordani mara saba ili kuponywa kabisa ukoma (2 Wafalme:5) nasi pia yatupasa kumwamini Yesu kuwa ametutakasa na dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote pale mto Yordani na matokeo yake ametupa wokovu wa milele. 
Kwakuwa Yesu anatupenda basi tutaweza kuokolewa na dhambi zetu ulimwenguni na kupokea uzima wa milele kwa kuamini injili ya ondoleo la dhambi. Hebu basi na tuamini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili na kupokea wokovu wa Mungu.