Search

Mahubiri

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-6] Tohara ya kweli ya Kiroho (Kutoka 12:43-49)

(Kutoka 12:43-49)
“Bwana akawaambia Musa na Haruni, Amri ya Pasaka ni hii, mtu mgeni asimle, lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri ndipo hapo atamla pasaka. Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle pasaka. Naaliwe ndani ya nyumba moja. Usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote; wala msivunje mfupa wake uwao wote. Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka, naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi, lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle. Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni aliaaye kati yenu ugenini.”
 

Sharti lipi lisiloepukika kwa 
Waisraeli kuweza kuwa wana wa 
Mungu katika Agano la Kale?
Walipaswa kutahiriwa.

Maneno ya Mungu katika Agano la Kale na Jipya ni muhimu na yenye thamani kwetu sisi tunaomwamini Mungu. Hatuwezi kupuuzia hata mstari mmoja wa maneno kwa kuwa maneno ya Mungu ni maneno ya uzima.
Fungu la leo linatueleza kuwa yeyote aliyetaka kuitimiza Pasaka ilimpasa kutahiriwa kabla. Yatupasa kufikiri juu ya sababu ya Mungu anatueleza hili. Ikiwa mtu hatotahiriwa asingeweza kuila Pasaka.
Ikiwa tunataka kumuamini Yesu, yatupasa kuelwa, kufahamu, kuamini Mungu ametupa tamko hili. Kutahiri ni kuondoa sehemu ya ngozi ya kiungo cha uzazi cha mwanaume (uume). Kwa nini sasa Mungu alimwambia Ibrahimu na kizazi chake kutahiriwa? Sababu ni kwamba Mungu alitoa ahadi ya kwamba atawafanya kuwa watu wake watakao kubali kutahiriwa.
Na ndiyo maana anawaambia watu wa Israeli katika Agano la Kale watahiriwe. Ilikuwa watu wa Mungu, wa Israeli iliwapasa kutahiriwa. Ilikuwa ndiyo taratibu yake, kwa msingi wa utakaso na akawa Mungu wa wale wote waliozikata dhambi zao kwa imani kupitia tohara. Kwa nyongeza, katika Agano Jipya amekuwa Mungu wa wale walio ziondoa dhambi zao kwa imani.
 

PASAKA

Pasaka ilikuwa ni nini?
Ilikuwa ni siku ya Waisraeli kukumbuka 
na kumshukuru Mungu 
kwa kutolewa Misri.

Sikukuu iliyo muhimu kwa Waisraeli ilikuwa ni Pasaka. Ilikuwa ni siku ya kukumbuka na kumshukuru Mungu kwa kutoka Misri, ambapo waliishi wakiwa watumwa takribani miaka 400. Mungu alileta mapigo 10 ili kuondoa moyo wa Farao uliokuwa mgumu. Ilikuwa kwa njia hii ndipo alipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri kwenda nchi ya Kanaani.
Watu wa Israeli walipokelewa na kifo cha mzao wa kwanza, pigo la mwisho kwa kupitia damu ya kondoo wa sadaka na kutahiriwa. Hivyo, Mungu aliwaambia kutunza Pasaka kwa kizazi chao chote kama ukumbusho wa huruma yake.
 

NINI KILICHOTAKIWA KUFANYWA NA WAISRAELI ILI KUITUNZA PASAKA?

Nini kilichotakiwa kufanywa na 
Waisraeli ili kuitunza Pasaka?
Iliwapasa kutahiriwa.

Yatupasa kuelwa ya kwamba ili kuitunza Pasaka kiroho, yatupasa kutahiriwa mioyo yetu. Hata Waisraeli iliwapasa kutahiriwa ili kutunza Pasaka. 
Imeandikwa katika Kutoka 12:43-49 “Bwana akawaambia Musa na Haruni, amri ya Pasaka ni hii, mtu gani asimle, lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliye nunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri ndipo hapo atamla pasaka. Akaaye kwenu hali ya ugeni na mtumishi aliyeajiriwa wasimle pasaka. Na aliye ndani ya nyumba moja, usiichukue nje ya nyumba nyama yake yoyote, wala msivunje mfupa wake mwao wote. Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote. Na mgeni atakapoketi pamoja nawe na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi, lakini mtu yeyote asiyetahiriwa asimle. Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.” Hivi ndivyo alivyowaambia Waisraeli kuitunza pasaka baada ya kutahiriwa.
Ni watu gani waliruhisiwa kuila nyama ya kondoo wa pasaka na kuitunza pasaka? Ni wale tu waliotahiriwa ndiyo walioruhusiwa.
Mwana kondoo wa pasaka pia anajulikana kama ndiye Yesu Kristo aliye ichukua dhambi ya ulimwengu.
Hivyo basi nini maana ya tohara katika Agano la Kale na Agano Jipya? Tohara maana yake kuondoa kwa kuikata sehemu ya ngozi ya uume. Yesu Kristo alitahiriwa baada ya siku nane kuzaliwa duniani. Mungu aliamrisha kwa wale wote watakao shiriki kafara ya pasaka iliwapasa kutahiriwa na kuweka wazi kwamba yeyote asiyetahiriwa asingeweza kushiriki kuila Pasaka.
Hivyo kila mtu ilimpasa kutahiriwa kwa amri ya Mungu. Unapomwamini Yesu unapaswa kuelewa maana ya kutahiriwa katika Agano Jipya.
 

NI KAFARA YA AINA GANI YA TOHARA MUNGU ALIMWAMURU IBRAHIMU 
KUIFANYA?

Kwa namna gani Ibrahimu 
na uzao wake waliweza kuwa 
watoto wa Mungu?
Kwa kutahiriwa.

Katika Mwanzo, Mungu alimjia Abraham na kufanya naye Agano pamoja na uzao wake. Katika sura ya 15, Mungu aliahidi kuwa uzao wa Ibrahimu utaongezeka kama nyota angani na atawapa nchi ya Kanani kama urithi.
Na sura ya 17 alimwambia Ibrahimu kwamba ikiwa yeye na uzao wake watakapoingia katika agano na kutahiriwa atakuwa Mungu wao na watakuwa watu wake. Ilikuwa ni agano la Mungu na watu wake. Mungu aliahidi kwamba pale watakapoamini agano lakena kutahiriwa, itakuwa na maana kuwa wamekwishakuwa watu wake, na hakika atakuwa Mungu wao.
Mwanzo 17:7-8 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako na vizazi vyako, kuwa agano la milele kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.”
Tohara ilikuwa ni alama ya agano la Mungu kwa Ibrahimu pamoja na uzao wake.
 

NINI MAANA YA NJIA YA TOHARA YA KIROHO?

Tohara ya kiroho ni nini?
Ni kuondolea mbali dhambi zilizomo 
ndani ya mioyo yetu kwa kuamini 
ubatizo wa Yesu.

Kwa kuwa Ibrahimu aliamini neno la Mungu, naye Mungu alimfanya kuwa mwenye haki na mtoto kwake. Ni tohara ndiyo iliyokuwa alama ya agano kati ya Mungu na Ibrahimu.
“Hili ndilo agano langu utakalolishika kati ya mimi na wewe na uzao wako baada yako. Kila mwanamume wa kwenu atathiriwa” (Mwanzo 17:10).
Tohara ya mwili ni kukatilia mbali ngozi ya mbele ya uume; kiroho pia humaanisha kutwika dhambi zetu zote juu ya Yesu kupitia imani yetu kwa ubatizo wake. Kiriho tumetahiriwa pale tunapokatilia mbali dhambi zetu kwa kukubali wokovu wa ubatizo wa Yesu. Tohara katika Agano Jipya ni kukatilia mbali dhambi kupitia ubatizo wa Yesu.
Hivyo tohara katika Agano la Kale ni sawa na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya, na vyote kwa pamoja ni maagano ya Mungu yanayotufanya kuwa watu wake. Hivyo tohara katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ni moja na ni sawa.
Kama ilivyo kwa uzao wa Ibrahimu kuwa ni watu wa Mungu pale walipokatilia mbali magovi yao, nasi tunakuwa watoto wa Mungu pale tunapokatilia mbali dhambi za mioyoni mwetu. Tunafanya hivi kwa kuamini kwamba hakuna tena dhambi ulimwenguni kwa sababu Yesu alizichukua pale alipobatizwa na Yohana Mbatizaji.
Ubatizo wa Yesu unawafanya wenye dhambi wote kuwa wenye haki kwa kukatilia mbali dhambi zao zote. Kwa jinsi ile govi lilivyokuwa likiondolewa katika hatua ya tohara, ndivyo sisi wote wanadamu dhambi zetu zinavyoondolewa ndani ya mioyo yetu pale tunapoamini kuwa Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto Yordani. Wale wote wenye kuamini hivi wataweza kupata tohara ya kiroho na kuwa watoto wa Mungu wenye haki.
 

IMANI BANDIA YENYE KUFANYA WATU WAWE MBALI NA MUNGU

Nini kilichowafanya Waisraeli 
kujitoa mbali na Mungu?
Kutotahiriwa.

Mungu alimwambia Ibrahimu kwamba, mtu asiyetahiriwa ataondolewa mbali na watu. Hivyo nini maana ya tohara? Na nini maana ya tohara ya kiroho? Ikiwa tohara ya mwili ni kukatilia mbali govi toka mwilini, tohara ya kiroho ni kukatilia mbali dhambi zote mioyoni mwetu na kumtwika Yesu kupitia ubatizo wake.
Ubatizo wa Yesu ni tohara ya kiroho kwa wandamu, amabyo dhambi zote za ulimwengu zilikatiliwa mbali kwetu na kutwikwa kwa Yesu. Sababu Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji ilikuwa ni kuokoa wanadamu kupitia tohara ya kiroho iliyochukua dhambi zetu zote.
Dhambi zote za wanadamu zilitwikwa kwa Yesu Mungu ili awe Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo na Mungu wa vizazi vyao. Aliweka agano kwa Ibrahimu na vizazi vyake na kuwataka kukatilia mbali magovi yao kwa kutahiriwa.
Tohara inayoondolea mbali magovi ni ipi? Ni lile agano la Mungu kwa Ibrahimu na kwa wote waliozaliwa upya kwa kuamini ubatizo wa Yesu na kifo chake juu ya msalaba. Kwa njia hii, ametupa haki ya kuwa watoto wa Mungu. Hivyo ni Mungu wa wote walio tahiriwa.
Mungu alinena na Ibrahimu “Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanaume katika vizazi vyenu mzaliwa nyumbani na mnunuliwa kwa fedha kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani kwako na mnunuliwa kwa fedha lazima atahiriwe, na agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele. Na mwanaume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake, amelivunja agano langu” (Mwanzo 17:12-14).
Yeyote anayetaka kuja kwa Yesu pasipo tohara ya kiroho atatengwa na watu wa Mungu. Tohara ya kiroho ni ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya kupitia huo ndipo dhambi za ulimwengu zilitwikwa kwake.
Mtu anayemwamini Yesu yampasa pia kuamini tohara ya Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ili aweze kupokea Roho, kuokolewa na dhambi zote, na kuwa mtoto wa Mungu. Kwetu sisi tunaoamini ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya na tohara katika Aganola Kale vyote hivi ni sawa.
Tunaposhindwa kuelewa maana halisi ya tohara au kukataa mioyoni mwetu wokovu kupitia tohara inayowezesha kuzaliwa upya mara ya pili, basi imani yetu itakuwa njia panda na bure. Tunaweza kudhani sisi ni waamninifu kwa Mungu, lakini ni sawa na kujenga nyumba ya imani yetu juu ya mchanga.
Mungu anawaasa wale wote wenye kumwamini watahiriwe, kuamini ukombozi kupitia ubatizo wa Yesu, tohara ya kiroho. Pasipo tohara, hatutoweza kuwa watu wake. Pasipo tohara tutatengwa toka tabaka la watu wake. Hivyo Mungu anatoa amri kwamba, mtu yeyote, awe amenunuliwa kwa fedha au kuwa mgeni imempasa kutahiriwa kabla ya kushiriki karamu ya Pasaka.
Hata pia wale wakazi wa Israeli wangetengwa mbali na watu wake ikiwa hawakutahiriwa. Agano la Mungu kwa watu wa Israeli itakuwa pia kwa wale wote wenye kumwamini Yesu.
Katika Kutoka sura ya 12 watu wa Israeli waliokula Pasaka na mboga iliyouchungu wawe wametahiriwa kabla. Haki ya kula nyama ya Pasaka ilipewa kwa wale watu waliotahiriwa.
Ni muhimu kwetu kujua kwamba wakati watu wa Israeli wakila nyama ya Pasaka na kupaka damu ya kondoo katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu walikuwa tayari wamekwisha tahiriwa.
Kwa amri ya Mungu, ikiwa mtu hakutahiriwa ametengwa na watu wa Mungu na kupoteza haki ya kuwa mtoto wa Mungu. Hii inamaana kwamba wale wote walio pata tohara ya kiroho kupitia ubatizo wa Yesu ndiyo watakuwa wameokolewa.
“Mfano wa mambo hayo ni ubatizo utuokoao sisi sote” (1Petro 3:21). Je unaamini kweli kwamba dhambi zako zote alitwikwa Yesu kupitia ubatizo Yordani? Ikiwa kweli unaelewa na kuamini ukweli, ubatizo wa Yesu na damu yake, utagundua kuwa kiroho umepokea tohara ya kiroho na kuwa mwenye haki. Na pia utakuwa na imani katika ukweli wa kiroho kuwa damu ya Yesu msalabani ingekuwa hainamaana pasipo ubatizo wake.
Iwapo ungeamini msalaba wa Yesu pasipo kupata tohara ya kiroho kupitia imani katika ubatizo wa Yesu utajikuta ukitupiliwa mbali na rehema ya Mungu. Bado utajikuta unaendelea kuwa na dhambi moyoni.
Yatupasa kuamini ukweli wa ukombozi wa Mungu ulioanzia kwa ubatizo wa Yesu Kristo na kuhitimishwa kwa damu yake msalabani. Kwa kufanya hivyo, yatupasa kuchukulia kwa moyo wetu maneno ya kweli, ubatizo wa Yesu na damu yake kuwa ndiyo wokovu wetu.
Kwa imani hii, tutaweza kukombolewa kutokana na nguvu za giza na kuwa wana wa nuru. Imani hii kiroho hutenganisha wale wote waliozaliwa kweli mara ya pili kwa tabaka la waumini wa kawaida.
Bwana wetu, Yesu anatueleza kuwa tumtegemee yeye. Amekwisha takasa kabisa dhambi za ulimwengu kwa ubatizo na damu yake. Hivyo kuweka alama ya kuwa ni watu wa Mungu, yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu. Tutakaposhindwa kufanya hivyo, tutatengwa naye.
Wokovu wa ukombozi si mwingine zaidi ya ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya na tohara katika Agano la Kale. Wokovu umekamilika ikiwa tu tunaimani katika mambo yote mawili, ubatizo wa yesu (tohara ya kiroho) na damu yake msalabani (damu ya mwana kondoo wa Pasaka).
Tohara ya mwili katika Agano la Kale inahusishwa na ubatizo wa yesu Kristo katika Agano Jipya. Isaya 34:16 inatueleza kuwa maneno yote katika Biblia yanawenzake kwa upande mwingine. “Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake, kwa maana kinywa changu kimeamuru na roho yake imeyakusanya.”
Kila neno katika Agano la Kale linauhusiano na neno katika Agano Jipya. Hakuna hata moja linalo mkosa mwenzake.
 
 
VIPI WALE WENYE KUAMINI PASIPO UANGALIFU KATIKA NAMNA ISIYO SAHIHI

Ni watu gani watakaokwenda 
motoni kati ya waumini 
wa ulimwengu huu?
Ni wale wasio amini 
tohara ya kiroho.

Leo hii wapo wengi wanaoamini damu ya mwana kondoo wa Pasaka tu. Wanauliza “Inamaana gani tohara? Ilikuwa ikifanyika kwa Wayahudi tu wakati wa Agano la Kale. Hatupasi kuondoa magovi yetu katika nyakati hizi za Agano Jipya.”
Bila shaka ni kweli. Sitoi ushauri kwamba imetupasa kutahiriwa kimwili. Mtume Paulo aliainisha juu ya tohara ya kiroho vyema na ni tohara ya moyo amabayo nami nazungumzia.
Siwaambii juu ya kutahiriwa kimwili. Tohara ya mwili haina maana kwetu, ila imetupasa kuja kwa Yesu na kupata tohara kwa kuamini ubatizo wa Yesu ili tuokolewe kwa dhambi zetu zote.
Ili mtu aweze kuzaliwa upya mara ya pili imempasa kutahiriwa kiroho. Yeyote anayemwamini Yesu yampasa kutahiriwa kiroho. Ndiyo njia pekee ya kuondolea mbali dhambi zetu zote, njia pekee ya kuwa mwenye haki, ni baada tu ya tohara ya kiroho ndipo tutakapokamilika pasipo dhambi. Hivyo yatupasa kuikubali kwa moyo tohara ya roho kwa kuamini ubatizo wa Yesu.
Mtume Paulo pia aliamini umuhimu wa tohara ya kiroho. Alisema “tohara ni ile ya moyo” (Warumi 2:29). Kila mmoja wetu imempasa kutahiriwa kiroho kuweza kuwa huru na dhambi.
Je, dhambi zako umemtwika Yesu kweli baada ya kuziondolea mbali? Hata katika Agano Jipya, aliye mwamini Yesu, ilimpasa atahiriwe moyoni kwa kuamini ubatizo wa Yesu.
Mtume Paulo aliweka hili wazi katika Barua zake. Mungu amewaokoa wanadamu kwa dhambi za dunia kuwafanya kuwa watu wake. Watu wa Israeli wamekuwa watu wa Mungu kwa kuondoa magovi yao na sisi pia tumekuwa watoto wake pale tunapomtwika Yesu dhambi zetu zote kwa kuamini ubatizo wake.
Mungu anatukubali sisi kuwa ni watu wake pale tu anapoangalia imani yetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Imani hii inatufanya kutahiriwa kiroho na kutuongoza katika wokovu.
 

WOKOVU UPO KWA WENYE DHAMBI KUPITIA UBATIZO WA YESU NA DAMU YAKE

Ni kwa namna ipi wokovu 
ulikamilishwa na Yesu?
Kupitia ubatizo wake na kifo 
chake msalabani.

Yesu Kristo alioukamilisha wokovu kupitia maji ya ubatizo na damu yake msalabani ni kwa wote wale wenye dhambi. Damu ya Mwana-kondoo ilikuwa ni kwa hukumu na ubatizo wa Yesu ni kwa tohara ya kiroho ambayo ilibadilisha wale wote wenye dhambi kwake.
Makanisa ya Kikristo nyakati hizi yanapaswa kuweka bayana imani ya tohara ya kiroho, ingawa tohara katika Agano la Kale inamaana ndogo kwetu sisi nyakati hizi, ubatizo wa Yesu haupaswi kamwe kupuuziwa.
Nimewaeleza ya kwamba dhambi zetu zote zimechukuliwa kwa ubatizo wa Yesu na ubatizo wa Yesu umekuokoa na dhambi zako zote. Je, unaamini? Ukipuuzia ubatizo wa Yesu, kamwe hutoijua injili ya kweli ya kuzaliwa upya mara ya pili, injili ya ukombozi ulio kamili kupitia ubatizo wa Yesu.
Tutawezaje kupuuzia ubatizo wa Yesu tohara ya kiroho ambayo Mungu ametuelezea? Ikiwa utasoma Biblia utaweza kuona kwamba tohara na damu ya mwana-kondoo wa Pasaka ni vitu vyenye uhusiano wa karibu. Hii ni siri ya tohara ya kiroho, ubatizo wa Yesu.
Injili iliyo hubiriwa na mtume Yohana haikuwa nyingine zaidi ya ile injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Alisema katika 1Yohana 5:6 “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.”
Alisema kwamba, Yesu alikuja kwa maji, damu na kwa Roho. Si kwa maji tu, na si kwa damu tu bali kwa maji, damu na kwa Roho vyote kwa pamoja. Mambo haya matatu ubatizo wa Yesu, damu ya Yesu, msalaba na ufufuko toka kifoni ni mambo ya pamoja, uthibitisho wa wokovu wetu.
 

KWA NINI BIBLIA INAZUNGUMZIA JUU YA UBATIZO WA YESU NA DAMU YAKE?

Je watu wa Israeli
waliokolewa kwa damu ya mwana 
kondoo wa Pasaka tu?
Hapana. Walikuwa tayari wamekwisha 
tahiriwa kabla ya kuila Pasaka.

Ubatizo wa Yesu na damu yake ndivyo vitu vituwezeshavyo kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Kutoka sura ya 12 inasema “Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu katika zile nyumba watakazo mla, nami nitakapoiona ile damu nitapita juu yenu lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.”
Kwa kuelewa hili, je, ni rahisi kweli kuokolewa kwa dhambi zetu zote kwa kuamini damu ya mwana kondoo wa Pasaka tu? Sasa, kwa nini ubatizo wa Yesu umezungumziwa mara nyingi katika Agano Jipya? Mitume walisema “mkazikwa pamoja naye katika ubatizo” (Wakolosai 2:12), “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27), “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1Petro 3:21).
Mtume Petro na Paulo na wale wote waliokuwa wafuasi wa Yesu Kristo walizungumzia juu ya ubatizo wa Yesu. Ni ubatizo wa Yesu pale Yordani ambao walikuwa wanamaanisha na ni imani ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo ukweli wa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Kusema ukweli, mimi nilimwamini Yesu hapo nyuma lakini kwa damu tu, zaidi ya miaka 10 pasipo kujua na kutambua ubatizo wa Yesu. Kwa hilo halikuweza kuondoa dhambi moyoni mwangu. Nilimwamini Yesu kwa moyo wangu wote, lakini ndani yangu nilijawa na dhambi nyingi.
Baada ya miaka hiyo 10 niligundua maana ya tohara ya kiroho (ubatizo wa Yesu) na ndipo nilipoweza kuzaliwa upya mara ya pili. Na ndipo tu nilipogundua ukweli wa tohara katika Agano la Kale ilimaanisha ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya. Naamini hivyo na ninaendelea kuamini.
“Katika Agano Jipya, ni imani sahihi kuamini katika yote mawili, damu ya Yesu na ubatizo wake? Je, imani yangu ni sahihi kulingana na Biblia?” Baada ya kuzaliwa upya mara ya pili nilitangatanga kimawazo juu ya mambo haya.
Ingawa niliamini ujumbe wa ubatizo wa Yesu na damu yake, swali lilibaki katika mawazo yangu, “ni sahihi kuamini ukweli kwamba dhambi zangu zote zilitwikwa juu ya Yesu pale alipobatizwa au ni sahihi kuamini kwamba Yesu alituokoa kupitia kifo chake msalabani tu. Je, inatosha kuamini kwamba Yesu ni Mungu wangu na mwokozi tu?” Niliwaza sana hili huku nikisoma Kutoka sura ya 12.
Watu wengi nyakati hizi husoma kitabu cha Kutoka sura ya 12 na hawafikirii mara mbili juu ya kutamka kwamba Yesu Kristo alikufa msalabani kama mwokozi wao. Hudhani kuwa ni sahihi kuiamini damu ya Kristo na kushuhudia ukweli wa dhamiri zao. Wanaweza kuamini pasipo hofu na kusema kwamba Bwana ni Kristo na ni Mwana wa Mungu lakini bado wanadhambi. Wanafikiri kwamba ikiwa watamwamini Yesu Kristo kuwa ni mwokozi, wataokolewa hata ikiwa wataendelea kuwa na dhambi mioyoni mwao.
Imani hii si imani sahihi. Imani hii pekee haitoweza kuwasaidia kuzaliwa upya mara ya pili. Ni ubatizo wa Yesu na damu yake pekee ndivyo vitatufanya kuwa wenye haki.
Sasa basi, Kutoka sura ya 12 inamaana gani? Nilipo tazama katika Biblia nikidhani “je kuna tatizo nikiamini damu ya Yesu tu na kuachana na ubatizo wake?” Hata kabla sijamaliza kusoma Kutoka, niligundua ukweli kwamba, wokovu si damu ya Kristo pekee bali pia ubatizo wake. Kupitia Biblia, nilihakikishiwa kwamba tumetahiriwa mioyoni mwetu kupitia ubatizo wa Yesu pamoja na damu yake msalabani.
 
Kwa nini wakristo walio wengi 
bado ni wenye dhambi?
Kwa sababu hawaamini juu ya 
ubatizo wa Yesu.

Niligundua katika Kutoka 12:47-49 kwamba kabla mtu kuruhusiwa kuila ile nyama ya Pasaka, ilimpasa kutahiriwa. Ni kwa sababu hiyo basi Mungu anasema katika mstari wa 49 “sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.”
Hivyo, yeyote yule asiye tahiriwa asingepaswa kula nyama ya Pasaka. Na huu ndiyo ukweli niliougundua. Ni sawa pia tunapomwamini Yesu kama mwokozi, yatupasa kwanza kukubali ukweli kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa kwake Yesu kupitia ubatizo wake pale Yordani na ndipo pia kukubali ukweli kwamba Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya hizo dhambi.
Nilipogundua kwamba Yesu alikufa msalabani ili kupokea hukumu kwa dhambi alizobeba katika ubatizo wake niligundua pia maana ya tohara ya kiroho ambayo imetuokoa kwa dhambi zetu zote na uovu wa ulimwengu.
Kwa wakati huo niligundua kwamba dhambi zangu zote zimefutika! Moyo wangu ukawa mweupe kama theluji na mwishowe nilipokea kwa moyo wangu wote injili ya maji, damu na Roho.
Niligundua ya kwamba yapo mambo mawili yanayotuokoa, tohara na damu ya mwana kondoo katika Agano la Kale na tendo la kumtwika Yesu dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake na damu yake pale msalabani na ubatizo wa yesu katika Agano Jipya hakika ni sawia.
Yesu Kristo alihukumiwa kwa sababu alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni kupitia ubatizo wake.Wale wote wenye kuamini ya kwamba. Yohana Mbatizaji ni mwakilishi wa wanadamu, aliye mbatiza Yesu na kumtwika dhambi zote za ulimwengu pia wanaamini vyote, ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Kwa nini basi watu wengi wanaukana ubatizo ingawa umeelezwa mara kwa mara katika Biblia? Kwa kufanya hivyo bado ni wenye dhambi ikiwa watamwamini Yesu. Wanaweza kumwamini Yesu lakini wametengwa mbali na Mungu. Ni wenye dhambi wanao sikitisha ambao watakwenda motoni hata ikiwa wanamwamini Yesu.
Watawezaje kuendelea kuwa wenye dhambi ikiwa wanamwamini Yesu? Kwa nini wanaishi wakiwa wenye dhambi? Kwa nini wanaelekea njia ya kuangamia? Inasikitisha sana. Wataendelea kuwa wenye dhambi kwa sababu hawaamini ukweli kwamba dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa kwake Yesu Kristo ambaye ameleta wokovu wa milele kwa watu wote kupitia ubatizo wa kiroho.
Watu hudhani wamekombolewa kwa kuamini damu ya Yesu, lakini imani hii kamwe haijakamilika. Kwa nini? Kwa sababu wameshindwa kumtwika Yesu dhambi zao!
Tutaweza kuokolewa ikiwa tu tutaamini maji (ubatizo wa Kristo) na damu yake katika njia aliyoamrisha Mungu; wokovu wa tohara ya kiroho. Ndipo pekee tutaweza kuwa wana wa Mungu.
Yatupasa kujiuliza “ikiwa tunaamini damu ya Yesu pekee kama tohara ya kiroho, dhambi zetu zote zitatakaswa kweli?” Yatupasa kuangalia kwa kina ndani ya mioyo yetu kutafuta jibu.
Katika Agano la Kale, watu waliokolewa kupitia tohara na damu ya Mwna-kondoo kama ilivyo kwetu pia tunapata wokovu kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Kwa njia hii tuliokolewa na hukumu ya Mungu na uovu wa dunia hii. Wale wote wenye kuamini wamefanywa kuwa wana wa Mungu na Mungu amekuwa Baba kwao.
Mtu ameokolewa na kuwa moja ya mali ya Mungu kwa kuamini mambo mawili, tohara na damu ya mwana-kondoo wa Pasaka, yaani ubatizo wa Yesu na damu yake. Huu ni ukweli kulingana na Yesu. Hii ndiyo maana ya kweli katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji, damu na kwa Roho.
 

NINI MAANA YA UKOMBOZI WA MAJI NA ROHO ULIOTAJWA KATIKA BIBLIA?

Je, mwenye dhambi ataweza 
kuwa mwenye haki kwa kuamini 
damu ya Yesu Pekee?
Kamwe. Haiwezekani.

Yesu aliuacha utukufu wake mbinguni na kushuka hapa duniani. Alibatizwa na Yohana Mbatizaji akiwa na umri wa maka 30 kuzibeba dhambi za ulimwengu.
Damu ya Yesu msalabani ilikuwa ni kwa hukumu ya dhambi za ulimwengu. Yesu Kristo alikuja akiwa ni mwokozi katika dunia na kuokoa wale wote wenye dhambi kwa maji na kwa damu.
Je, tumeokolewa kwa damu pekee? Kamwe. Tumeokolewa na dhambi kwa ubatizo wa Yesu na damu yake. Ningependa kuuliza swali kwa wale wote wenye kuamini damu ya Kristo tu “je, mwenye dhambi ataweza kuwa mwenye haki kwa kuamini damu ya Kristo pekee, au ni kwa mambo yote mawili, ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani? Je, si kwa kuamini juu ya kumtwika dhambi zetu Yesu kupitia ubatizo na damu au kupitia damu yake? Ukweli ni upi nauliza?”
Kuweza uzaliwa kwa uhakika katika maji na Roho yatupasa kutimiza yafuatayo. Yatupasa kumwamini Yesu alikuja duniani katika mwili, alibeba dhambi zote za ulimwengu juu yake katika mto Yordani kwa ubatizo wake na kuhukumiwa maslabani kwa dhambi hizo. Kwa kumwamini yesu Kristo, mwokozi wetu wa kweli kwa njia hii tutaweza kuzaliwa upya mara ya pili kiuhakika.
Nauliza tena. Ni imani ipi iliyoelezewa katika biblia? Ni imani ya damu ya Yesu, au ni vyote viwili ubatizo wa Yesu na damu yake?
Imani katika damu ya Yesu ni kama ifuatavyo: Yesu alihukumiwa na kuuwawa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Kwa kuwa alipigwa na kujeruhiwa kwa ajili ya dhambi zetu tumeokolewa toka hukumuni. Lakini huu ni ukweli usio kamilika. Kabla ya kukubali fundisho hili yatupasa kuweka bayana jambo moja. Kwa nini Yesu ilimpasa asulubiwe masalabani?
Biblia inaweka wazi kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. Yesu hakutenda dhambi yoyote hapa duniani. Alikuja akiwa na mwili wa mwanadamu kupitia Mariamu, lakini alikuja akiwa kama mfano wa umbo la watu wake akiwa Mwana wa Mungu, Mtakatifu na Mwokozi wa wenye dhambi. Na hii ndiyo maana ilimpasa abatizwe na Yohana Mbatizaji kabla ya kufa msalabani. Alipo kuwa akibatizwa, ndipo alipobeba dhambi zote juu yake. Kwa hivyo, pasipo ubatizo, asingeweza kuhukumiwa kumwaga damu yake msalabani.
 

MPANGILIO WA SADAKA KATIKA AGANO LA KALE

Ni vigezo gani muhimu 
katika utoaji wa sadaka?
(1) Mnyama hai asiye na doa
(2) Kuwekea mikono
(3) Damu ya mnyama huyo

Hebu tutazame ukweli huu kupitia mpangilio wa utoaji wa sadaka katika Hema takatifu. Katika Agano la Kale, ama mwenye dhambi au kuhani aliwekea mikono juu ya sadaka ya kondoo au mbuzi kumtwika dhambi zake au dhambi za watu wote wa Israeli juu yake. Na baadaye sadaka hiyo kuchinjwa koo na kutolewa mbele. Kwa Agano Jipya, Yesu Kristo ndiye aliyekuja kuwa sadaka ya mwanakondoo wa Mungu aliyeahidi kumtuma.
Ni lini ninyi nyote mlipomtwika Yesu dhambi zenu zote? Napenda ufikiri juu ya hili na kijibu swali hili. Katika Agano la Kale, Waisrael wasingeweza kuchinja wale wanyama wa sadaka pasipo kuwa wekea mikono yao. (kuwekea mikono maana yake kutwika dhambi juu ya sadaka ya dhambi). Kabla ya sadaka ya dhambi kutolewa, zililetwa mbele ya madhabahu kuwekewa mikono kitendo hiki kilipaswa kifanyike ili kuweza kutwika dhambi zote juu ya mnyama huyo.
“Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa” (Walawi 1:4). Imeandikwa katika Walawi kwamba sadaka zote zilihitaji kuwekewa mikono. Kwa kuwekewa mikono juu ya kichwa cha sadaka, watu wa Israeli waliweza kutwika dhambi zao juu yake, na kutoa damu yake na nyama kwa imani mbele ya Mungu, waliweza kuokolewa kwa dhambi zao zote. Waisraeli pia waliokolewa kwa imani katika nyakati zile za Agano la Kale.
Sadaka ya kuteketezwa ilipotolewa mbele ya Mungu, mwenye dhambi ilimpasa kumwekea mikono juu ya kichwa ili kuitwika dhambi sadaka hiyo. Sadaka hiyo ilichinjwa koo kwa niaba ya mwenye dhambi. Damu yake ilinyunyizwa katika pembe nne katika kingo za madhabahu na iliyobaki kumwagwa chini ya madhabahu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wenye dhambi kukombolewa.
Katika Agano Jipya, wenye dhambi wanakombolewa kwa dhambi zao zote kupitia imani katika maji na damu ya Yesu. 1Yohana 5:1-10 inasema kwamba mwenye dhambi amekwisha kombolewa pale anapoamini ubatizo wa Yesu na damu ya mwana kondoo (msalabani).
Hivyo mwenye dhambi yeyote ataweza kukombolewa ikiwa ataamini kwa pamoja ubatizo wa Yesu na damu ya Yesu msalabani. Ubatizo wa Yesu na damu yake, kwa pamoja na Roho Mtakatifu ni mambo yasiyowekwa kando katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na Roho.
Wapendwa, je, mtaweza kukombolewa kwa kuamini damu ya Yesu pekee? Wenye kudhani kwamba wataweza kuzaliwa upya mara ya pili kwa kuamini damu ya msalaba bado ni wenye dhambi mioyoni. Hivyo tutaweza kuokolewa kwa dhambi zetu zote kwa kuamini ubatizo wa Yesu ikiwa ni tohara ya kiroho katika Agano Jipya, ambapo ni sawa na tohara iliyokuwepo hapo awali katika Agano la Kale.
Madhehebu yote yanamafundisho yake pekee. Tunajua kuwa yote yataangamia motoni ikiwa hayataacha imani potofu. Kanisa la Kipresbiterian linasisitiza mafundisho ya kuchaguliwa tangu asili; Kanisa la Methodisti linasisitiza mafundisho ya ubinadamu (uungwana/utu); Kanisa la Baptisti na Kanisa la Holyness husisitiza juu ya maisha matakatifu; yote haya yamekwepa ukweli wa Neno.
Lakini, ni neno gani la kweli katika Biblia linaloongelea juu ya kuzaliwa upya mara ya pili? Biblia inasema kweli hupatikana katika ubatizo wa Yesu na damu yake. Yeyote anayeamini na kufuata neno la Mungu na kuwa na imani ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho atapokea ukombozi.
 

NINI SIRI YA UBATIZO WA YESU?

Nini maana ya tohara 
katika Agano Jipya?
Ni ubatizo wa Yesu.

Ubatizo wa Yesu ni tohara ya kiroho. Katika Agano la Kale. Mungu alisema kwamba, mtu yeyote asiye tahiriwa angetengwa mbali na watu wa Mungu.
Yatupasa kujua na kuamini kwamba tohara ya kiroho katika Agano Jipya ndiyo ubatizo wa Yesu haswa kwa sababu Yesu alibatizwa na Yohana mbatizaji mwanzo wa huduma yake hadharani, nasi tutaweza kutahiriwa kiroho kwa kuamini ubatizo wake. Yatupasa kuwa makini kufikiri sababu gani Yesu alibatizwa na Yohana mbatizaji.
“Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, alisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali” (Mathayo 3:13-15).
Yesu alibatizwa na Yohana mbatizaji katika mto Yordani, “mto wa mauti.” Aliweka mikono juu ya kichwa cha Yesu na kumzamisha kabisa. Hivi ndivyo sahihi kubatizwa (Ubatizo:kuzamishwa kwenye maji) Ili Yesu aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu ilimpasa kubatizwa kwa namna ile ya kuwekewa mikono iliyokuwepo katika Agano la kale.
Ubatizo wa Yesu ni tohara ya kiroho kwa wale wote wanaomwamini Yesu “Kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15) Ilimpasa Yesu kubeba dhambi zote za ulimwengu na kuwa Mungu na mwokozi wetu. Kwa njia hii, ilimpasa, kama ilivyo andikwa, kwake kufa msalabani kwa dhambi zetu zote juu yake.
Ubatizo wa Yesu unanguvu ya kuwafanya wenye dhambi wote kuzaliwa upya mara ya pili. Ni siri ya injili ya maji na Roho.
Jambo la kwanza Yesu kufanya katika huduma yake hadharani kwa wenye dhambi kuokolewa ilikuwa ni kubatizwa na Yohana mbatizaji. Ubatizo maana yake “kutakaswa,kuzikwa,kutwika”.
Kwa kubatizwa namna ile Mungu aliyoiweka, Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu juu yake “Tazama mwana kondoo aichukuaye dhambi ya dunia” (Yohana 1:29). Ubatizo wa Yesu maana yake watu wote ulimwenguni wenye kumwamini wanatahiriwa kiroho.
Baadaye, alikwenda msalabani kama mwanakondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu na kukubali hukumu badala ya wenye ndambi wote.
Kwa hivyo, ameokoa wanadamu wote kwa dhambi. Hivyo wale wote wenye kuamini ubatizo wake Yesu Kristo, tohara ya Agano la kale, na damu yake msalabani kama wokovu wa dhambi zao, wameokolewa. Yesu Kristo ameokoa wale wote wenye dhambi kwa ubatizo na kwa damu yake. Huu ni ukweli wa tohara ya kiroho.
 

JE WOKOVU NI KWA DAMU PEKEE? HAPANA

Yesu amekuja duniani 
kwa namna gani?
Kwa maji na kwa damu.
 
1Yohana 5:4-9 inasema “kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu, na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye kwa sababu ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho na maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.”
Wapendwa wakristo upi ni ushuhuda wako kwake Yesu Mwokozi? Si mwingine ila ni imani katika Mwana wa Mungu aliye kuja kwa maji na kwa damu.
Ni ushindi gani unao ushinda ulimwengu? Si mwingine ila nguvu ya imani katika maji na damu. Ni Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na kwa damu.Na ni Roho ndiye ashuhudiaye kwani Roho ni kweli.
Wapo watatu washuudiao duniani, maji, damu na Roho. Nao wanapatana kwa jambo moja. Yesu alikuja ulimwenguni akiwa mwili, akabatizwa na kufa masalabani kutuokoa kwa hukumu ya milele.Ushahidi kuwa Mungu, Muumba wetu alikuwa nimwokozi wetu sisi wote wenye dhambi upo katika injili ya maji na Roho yenye kutuokoa sisi sote.
Ni ushahidi wetu kuwa Yesu aliyekuja duniani akiwa Roho ndani ya mwili alibatizwa Yordani kuchukua juu yake dhambi zetu, kutoa damu yake msalabani kwa kukubali hukumu kwa ajili yetu. Kwa hiyo ametuokoa sisi sote wenye kumwamini. Hii ndiyo injili halisi ya maji na Roho.
 

NINI MAANA YA MAJI NA DAMU YENYE KUSHUHUDIA WOKOVU WA MUNGU?

Ni upi mfano wa tohara yenye 
kuelezewa katika Agano la Kale?
Ni ubatizo wa Yesu.

Maji humaanisha ubatizo wa Yesu Kristo. Katika Agano la Kale, ubatizo wa Yesu ulimaanisha tohara. Mfano wa tohara katika Agano la Kale ni ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya. Ushahidi kwamba dhambi zote za ulimwengu alitwikwa Yesu upo katika ubatizo wake.
Yeyote anayeamini ukweli huu anaouwezo wa kusimama mbele ya Mungu na kusema kwa dhamiri safi “wewe ni mwokozi wangu, Bwana wangu kwa sababu ninaamini ubatizo na damu yako, injili ya maji na Roho. Hivyo, sina dhambi moyoni. Ni mwana wa Mungu na wewe ni mwokozi wangu” Tunao uwezo wa kutamka haya kwa imani ya kweli. Sababu ya kuweza kusema yote haya ni kwa kuwa tunayo imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake.
Ni neno gani lenye kutuwezesha kuzaliwa upya mara ya pili? Ni ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, ndiyo ulio ushahidi wetu wa wokovu mioyoni mwetu. Hii ni injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Wapendwa wakristo, Nauliza tena, “Je, mwenye dhambi aweza kweli kiurahisi kuokolewa kwa kumini damu ya Kristo pekee?” La hasha! Wokovu unamhitaji siyo tu kuamini kifo cha Yesu msalabani. Ni kwa kuamini vyote viwili maji na damu—injili ya maji na Roho—amabayo wenye dhambi wanazaliwa upya mara ya pili. Hebu nirudi katika Biblia ambayo inazungumzia juu ya maji au kwa maneno mengine ubatizo wa yesu.
1Petro 3:21-22 inasema “mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu amekwenda zake mbinguni na malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.”
Mtume Petro alishuhudia juu ya ubatizo wa Yesu kuwa ni mfano wa wokovu wetu, na pia ni uthibitisho wa wokovu wa dhambi. Ubatizo wa Yesu ni sawa na tohara katika Agano la Kale. Kama vile jinsi Waisraeli walivyo amini neno la Mungu na kukubali kukata magovi yao hivyo kuwa watoto wa Mungu, katika Agano la Kale ubatizo wa Yesu unatuokoa nasi pia kwa dhami zetu zote wakati huu wa Agano Jipya.
Hivyo basi tohara katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ni kitu kimoja na cha kufanana. Je, wote sasa mnaamini ubatizo wa Yesu ndio hiyo tohara? Kama ilivyoandikwa katika 1Petro 3:21 mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi siku hizi. Je, utawezakubishana na neno la Mungu?
Inakuwaje sasa, sisi tunaoishi duniani, tunaweza kuwa huru kwa dhambi? Ni pale tu Yesu Kristo alipobatizwa ili kuitimiza haki yote ndipo wokovu toka dhambini unapokuwepo kwetu. Mathayo 3:15 inasema “hivi ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”
Kwa kuwa dhambi zote ulimwenguni alitwikwa Yesu, wale wote wenye kumwamini hawana dhambi tena. Tutaweza sote kuwa wenye haki kwa kukubali ukweli kwamba dhambi zetu zote alitwikwa Yesu kupitia ubatizo wake. Yesu Kristo alichukua dhambi zetu zote na kufa msalabani ili kutuokoa na hukumu.
Rafiki wapendwa, vitu viwili ndivyo vinaokoa wote wale wenye dhambi kwa dhambi zao, navyo ni maji na damu. Kubeba dhambi zetu na kufa nazo msalabani ni mambo makuu mawili ambyo Yesu Kristo alifanya kwa ajili yetu sisi sote katika kipindi cha miaka 3 ya huduma yake hadharani hapa ulimwenguni.
Yohana 1:29 inasema “Tazama! Mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” Yesu Kristo alibatizwa ili aichukue dhambi ya ulimwengu na kufa msalabani ili aweze kutupatanisha kwa makosa yetu. Yesu ni mwana wa Mungu na Muumba aliyetimiza agano la tohara ambalo Mungu Baba aliweka katika Agano la Kale kwa kuondoa dhambi zote za ulimwenguni.
Kila mtu aaminiye moyoni mwake Injili ya Ubatizo wa Yesu, maji na damu atazaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Na Bwana atakuwa Mwokozi kwa wote walio amini. Asante Bwana, Haleluya! Yesu alitimiza wokovu wetu kama vile Mungu alivyo kuwa ameahidi, na alituokoa kutoka kwa dhambi zote za ulimwengu. 
 

SIYO KUWEKEA MBALI UCHAFU WA MWILI

Je, mwili unatakasika kwa muda?
Hasha! Mwili huendelea kukusanya 
dhambi hadi siku ya kifo chetu.

1Petro 3:21 inasema “mfano wa mambo hayo ni ubatizo unaowaokoa ninyi pia siku hizi, (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Wakati mtu anapomwamini Yesu Kristo kuwa mwokozi hainamaana kuwa ataacha kutenda dhambi za mwilini. Tutaweza kutenda dhambi lakini tukiamini ubatizo wa Yesu, tutaweza kutwika dhambi zetu zote za dunia juu yake aliye zilipia kwa damu yake msalabani. Kwa kuamini mambo haya mawili muhimu yasiyotenganishwa katika wokovu wetu, ndipo tunapookolewa kwa dhambi zetu.
Kuzaliwa upya mara ya pili maana yake ni kumkaribisha Yesu ndani ya mioyo yetu kuwa mwokozi wa wanadamu. Msamaha wa dhambi pia hupatikana mioyoni mwetu. Tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake maslabani, mioyo yetu huzaliwa upya mara ya pili. Lakini bado tungali kutenda dhambi na uovu kwa miili yetu. Lakini dhambi zetu zote za mwili zilikwisha kusamehewa.
Ubatizo wa Yesu ni ushuhuda wa wale wote waliokolewa. Hatuwezi kuwa na dhambi tena ikiwa tutaamini msamaha wa dhambi kupitia ubatizo wa Kristo. Tumezaliwa upya mara ya pili pale tunapoukubali kwa moyo wetu wote ukweli wa wokovu kupitia ubatizo wa Yesu na tunakuwa wenye haki kupitia injili ya maji na Roho.
Hii ni imani ya Ibrahimu katika Agano la Kale, imani ya kuwa mwenye haki ambayo Mtume Paulo aliizungumzia na mfano wa wokovu ambao pia Mtume Petro aliutaja.
Kama ilivyokuwa Ibrahimu aliposikia na kuamini Neno la Mungu na kufanywa kuwa mwenye haki sisi nasi tumeokolewa tunapoamini ubatizo wa Yesu na kifo chake pale msalabani.
Yohana 1:12 inasema “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” Je, unamwamini Yesu Kristo, yule aliyetuokoa kwa dhambi zetu zote kupitia ubatizo na damu yake akiwa ni mwokozi wetu?Yatupasa kupokea wokovu uliotolewa kupitia maji na damu ya Mwana wa Mungu.
Je, wokovu ni kwa damu ya Yesu Kristo tu? Hapana ni wa maji na damu ya Yesu. Katika Biblia imeandikwa wazi kuwa wokovu si kwa damu ya Yesu pekee. Ni kwa ubatizo wa yesu na damu yake.
Ubatizo wa Yesu ni tohara ya kiroho katika Agano Jipya. Ni ukweli wa wokovu unao ondolea mabli dhambi kwetu. Ukweli kwamba alihukumiwa kwa dhambi za ulimwengu maana yake alihukumiwa kwa ajili yetu, mimi na wewe.
Kwa kupokea injili ya msamaha wa dhambi ubatizo wa yesu na damu yake, tunamaanisha kuwa huru na hukumu ya dhambi zetu zote. Kwa imani yetu tumeokolewa kwa dhambi zote tunazotenda hapa duniani. Tunapouchukulia ubatizo wa Yesu na damu yake kuwa ni wokovu kwetu, dhambi zetu zote mioyoni hutakasika. Je, unaamini na kuelewa hili kuwa ni kweli? Kwa uaminifu natumaini utaamini injili ya maji na Roho. Amini na upate uzima wa milele.
Mtume Paulo alisema “na tohara ni ya moyo katika roho” (Warumi 2:29). Tunapotaja tohara katika mioyo yetu. Tunaweza kutahiriwa kiroho tu pale tunapoamini kuja kwake Kristo Yesu hapa duniani katika mwili, kuamini ubatizo wake uliochukua dhambi zote za ulimwengu kifo chake msalabani kwa ajili yetu, na ufufuko wake toka kifoni.
Mtume Paulo alisema kuwa tohara ni ile katika moyo. Tohara katika moyo maana yake ni kuuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Ikiwa unataka kutahiriwa moyoni yakupasa uchukue ndani ya moyo wako injili ya ubatizo wa yesu na damu yake. Ndipo utakapoweza kuwa kweli mtoto wa Mungu hakika.
 

JE YOHANA MBATIZAJI ALITUMWA NA MUNGU?

Yohana Mbatizaji alikuwa ni nani?
Alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu na 
Kuhani Mkuu wa mwisho kutokana 
na kizazi cha Haruni.

Hapa tunahitaji kujiuliza kwamba Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu Kristo alikuwa ni nani hasa? Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu wote. Mathayo 11:11-14 inasema “Amin, nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji walakini aliyemdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali yeye ndiye Eliya atakayekuja. Mwenye masikio na asikie.”
Wapendwa wakristo, Yesu alisema kwamba hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliyemkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji katika kipindi cha agano la kwanza la Mungu, ndipo kipindi cha Agano la Kale kilihitimishwa. Kilihitimishwa kwa kuwa Yesu Kristo aliyetimiza agano la Mungu mwishowe alikuja.
Walikuwa ni akina nani basi ambao wangetimiza agano la Mungu? Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji alimtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu. Nani aliyekuwa Kuhani Mkuu katika Agano la Kale? Ni nani aliyekuwa uzao wa Haruni? Yesu Kristo alishuhudia kwamba, hakuwa mwingine bali ni Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu Mkuu kati ya wote waliozaliwa na wanawake.
Hebu tufikiri zaidi juu ya huu ukweli tulionao. Musa, Ibrahimu, Isaka na Yakobo wote hawa walizaliwa na wanawake. Lakini kati ya watu katika Agano la Kale na Jipya ni nani aliyemkuu kuliko wote hawa aliyezaliwa na mwanamke? Ni Yohana Mbatizaji.
Yohana Mbatizaji akiwa nabii wa mwisho katika Agano la Kale na uzao wa Haruni, alimbatiza Mwana kondoo wa Mungu katika Agano Jipya kwa namna ile ile ambayo Haruni aliweka mikono juu ya sadaka ya dhambi katika siku ile ya upatanisho wakati wa Agano la Kale. Alimbatiza Yesu Kristo na kumtwika dhambi zote za ulimwengu juu yake. Alikuwa ni mtumishi wa Mungu. Alitimiza tohara ya mioyo ya wanadamu kwa kumbatiza Yesu Kristo.
Pamoja na ubatizo wa Yesu, yatupasa kuiamini damu yake pia ukiwa ni ushuhuda wa wokovu wetu. Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo na alihukumiwa kwa ajili ya hizo dhambi. Na kitu pekee kwetu kufanya ni kuamini tu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba tuamini kile Yesu alichofanya.
Unapopokea hili moyoni mwako, injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho, moja kwa moja unakuwa uzao wa Ibrahimu na pia mtoto wa Mungu. Wapo wachache walio katika Kristo hali wapo wengi amabo bado hawajakubalika naye katika mioyo yao. 
Siku zimekwisha na giza limetanda. Amini ubatizo wa Yesu na kubali aingie moyoni mwako. Imani yako katika ubatizo wa Yesu na damu yake itakufanya ubarikiwe kwa wokovu wa kiroho.
Kumbuka mara zote upako wa Kristo huja pale tu unapoamini injili ya wokovu, injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Nataka uelewe kwamba utaweza kutayarisha taa yako ya kiroho (kanisa) na mafuta (Roho Mtakatifu) na kama wale wanawali (Mathayo 25:4) kwa kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Wale wenye kumuamini Yesu huenda kanisani na Roho Mtakatifu ndani yao. 
 

YESU ALIBATIZWA NA NANI?

Yesu alibatizwa kwa sababu ipi?
Ili kutakasa dhambi zote za 
wandamu wote.

“Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akamjibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote; Basi akakubali” (Mathayo 3:14-15).
Yesu alibatizwa ili kutakasa dhambi zote za wanadamu. Yesu Kristo ni mwana wa Mungu aliyetuumba sisi. Yesu Kristo alikuja kwa mapenzi ya Mungu Baba ili kutufanya watu wake.
Ni nani aliyezungumziwa na manabii wa Agano la Kale? Manabii walizungumza juu ya Yesu Kristo. Manabii wote wa Agano la Kale walizungumzia juu ya ujio wa Yesu hapa duniani kuja kuchukua dhambi zote na kutuweka huru milele.
Yesu alishuka duniani kama ilivyotolewa unabii katika Agano la Kale na kubeba dhambi zote za wanadamu kuanzia Adamu na Hawa hadi yule mtu wa mwisho hapa duniani.
Sasa, kubali kwa moyo wako wokovu kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake. Je, bado una uhakika na ukweli huu? Je, bado unadhambi moyoni? “Kwa kuwa ndivyo itupasavyokuitimiza haki yote.” Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili kuitimiza haki yote. 
Neno “ubatizo” peke yake lina maana ya “kusafishwa”. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji kwa njia ya kuwekewa mikono kama ilivyo ainishwa katika Agano la Kale.
Alijitumbukiza mwenyewe mto Yordani na kubeba dhambi zote za wanadamu. Mto Yordani humaanisha kifo na hukumu kwa wenye dhambi. Kuzama kwa Kristo katika mto kunaashiria kifo chake msalabani. Kuibuka toka kwenye maji kunasimama badala ya ufufuko wake. Yesu alifufuka katika siku ya tatu baada ya kufa msalabani.
Yesu ni Mungu na mwokozi wetu. Ukweli ni kwamba Yesu alikuja duniani ili kubatizwa, kumwaga damu yake msalabani, alifufuka siku ya tatu na sasa ameketi kuume kwa Mungu ni udhihirisho tosha kuwa ameokoa wanadamu kwa dhambi zao. Je, kweli unaamini juu ya ukweli huu?
Ubatizo wa Yesu ni tohara ya kiroho katika Agano Jipya. “Tohara ya moyo.” Hii hukamilishwa pale tunapoamini ubatizo wa Yesu, ukweli juu ya kutwika dhambi zote kwake Yesu. Tohara ya moyo ni kukiri juu ya ubatizo wa Yesu kupitia huo dhambi zote alitwikwa Yesu.
Je wewe umekwisha tahiriwa moyo wako? Ikiwa utaamini tohara ya moyo, dhambi zako zote zitatakaswa mara moja na kwa wakati wote. Kwa sababu hiyo Yesu alitimiza haki yote na kutuhakikishia wokovu wa wenye dhambi wote.
Wapendwa wakristo, pokea uhakika wa wokovu ndani ya moyo wako na akilini mwako. Hili ni kweli pale utakapochukua ndani ya moyo wako wokovu wa Yesu, utakuwa huru kwa dhambi zako zote. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waaminio jina lake” (Yohana 1:12).
Je, unaweza kuona ni kwa nini Yesu ilimpasa kuja duniani ili kubatizwa? Je, unaamini sasa? Yesu alibatizwa ili achukue dhambi za wanadamu. Ni ubatizo wa tohara. Ubatizo wa Yesu unatupatia tohara ya kiroho. Hii ndiyo maana mtume Paulo anatuasa sisi leo kutahiriwa mioyoni mwetu. Yesu ametuokoa bayana kwa ubatizo wake na damu yake hivyo hatuna uchaguzi bali ni kuamini kwa moyo wetu wote. Inatupasa kusema “Ndiyo. Amina” kwa neno la Mungu mioyoni mwetu. Ni kweli? Unaamini hilo?
 

JE UNAAMINI HILI NDANI YA MOYO WAKO?

Yatupasa kufanya nini kabla 
ya kumuabudu Yesu?
Yatupasa kupokea kwa moyo wetu 
wote ukweli wa maji 
na damu yake.

Takribani miaka 2000 imekwishapita tangu kuja kwa Yesu hapa duniani. Katika siku hizi na nyakati za neema ya Mungu yatupasa kuchukua ndani ya mioyo yetu ukweli, maji na damu ya Yesu. Hakuna kingine tuwezachokufanya.
“Tohara ni ile ya moyo.” Yatupasa kutahiriwa kupitia imani zetu katika mioyo. Tutaweza kuokolewa kwa neema tu. Katika Agano la Kale, Waisraeli waliokolewa kupitia tohara na damu ya Pasaka ambayo iliwekwa katika miimo ya milango na vizingiti vya nyumba zao.
Wale waaminio ubatizo wa Yesu na damu yake kuwa ni wokovu wao hawana hofu ya hukumu ya Mungu kwa kuwa itapita juu yao. Lakini hukumu ya Mungu itaanguka juu ya wale wote wasiokubali ukweli huu moyoni. Wapo wengi wanaomwamini Yesu wakiwa njia panda na hivyo kuendelea kuwa watumwa wa dhambi zao.
Je, wamefikia hatua hiyo? Kwa nini bado wanaendelea kuteseka kwa dhambi? Ni kwa sababu hawajui ukweli juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Wao huamini damu ya Yesu pekee, huiacha au kutotilia maanani ubatizo wake.
Je, wokovu hupatika kwa njia rahisi za kiimani katika damu ya Yesu pekee? Je, Biblia inatuelezea kufanya hivyo? Mambo gani Agano la Kale na Jipya yanatueleza juu ya hili? Kulingana na Biblia si kwa damu ya Mwana kondoo wa Mungu tu bali pia kwa ubatizo wa Yesu ndipo wokovu unapatikana (1Yohana 5:3-6).
Je, wewe nawe unaamini damu ya Yesu pekee? Wale wenye kuendelea kuamini hivyo bado wanadhambi mioyoni mwao. Yawapasa kuachana na imani isiyo sahihi na kurudi katika injili ya kweli.
Wale wasioamini ni lazima wakiri sasa kwamba walikuwa wamepotea, pasipo kujua kwamba Yesu alizichukua dhambi zote pale Yordani kupitia ubatizo wake. Yawapasa kukubali kwamba walitenda kosa la kudharau katika kukubali ubatizo wa Yesu. Yawapasa kujua moyoni kwamba, Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu kupitia ubatizo wake. Wokovu hupatikana pale tu tunapoamini yote mawili ubatizo na msalaba wa Yesu. Kwa maneno mengine, ni kwa injili ya maji na Roho tu ndipo tunaweza kupata uzima wa milele.
Wapendwa wakristo, mpaka leo umekuwa ukiishi kwa kutegemea imani ya damu ya Yesu pekee? Ikiwa ndivyo, hakika unadhambi moyoni. Ukitenda dhambi basi unayodhambi moyoni. Ukidhani uko huru kwa dhambi unapofuata sheria ya Mungu, hizi ni fikra zako binafsi zitokanazo na hisia tu. Uhakika huu hutokana na neno la Mungu.
 

HUJACHELEWA BADO

Kwa namna gani 
tupo huru kwa dhambi?
Kwa sheria ya dhambi na kifo.

Hujachelewa bado unachopaswa kufanya ni kuamini ubatizo wa Yesu na damu na utakuwa na tohara ya moyo na kuwa huru kwa dhambi zako zote. Kuwa huru kwa dhambi maana yake kuokolewa kwa kuamini injili ya ubatizo wa yesu na damu yake. 
Je, upo tayari na una hiari ya kuuamini ubatizo wa Yesu na damu yake kwa wokovu wa dhambi zako? Utakapoaamini tu utagundua nini maana ya wokovu. Utapokea amani ya moyo. Hapo ndipo utakuwa mwenye haki si kutokana na matendo yako bali kupitia imani yako katika neno la Mungu. Ikiwa mtu yeyote bado anaamini na kutegemea damu ya Yesu pekee kwa wokovu, napenda kumsihi kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake kwa pamoja.
Wapendwa wakristo, wokovu uliokamilika kwa wanadamu tokana na dhambi zao ulikamilishwa kupitia injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Roho ni Mungu. Mungu alishuka duniani katika mwili wa mwanadamu.
Mungu alisema kupitia manabii kwamba yatupasa kuliitia jina la Yesu, kwa kuwa yeye ndiye aokoaye watu wake na dhambi zao. Mungu alisema “tazama bikira atachukua mimba naye atazaa mwana, nao watamwita jina lakeImanueli” (Mathayo 1:23).
Mungu alikuja duniani kuokoka wenye dhambi. Alibatizwa ili kubeba dhambi zote za dunia na hivyo kuokoa wenye dhambi wote. Huu ni ukweli na wokovu wa maji na damu. Nipo hapa kukwambia juu ya hili. Je, tumeokolewa kwa damu ya Yesu pekee? Bila shaka hapana. Tumeokolewa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Wapo manabii waongo wengi na wazushi leo hii wasio amini ubatizo wa Yesu. Yesu alisema “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).
Yatupasa kufahamu kweli. Lazima tujue kwa nini Yesu alizungumzia juu ya ubatizo wake, na kwa nini tuamini. Yatupasa kujua kwa nini Mungu aliwaambia Waisraelii kutahiriwa katika Agano la Kale na kwa nini anazungumzia juu ya damu ya Mwana kondoo wa Pasaka?
Tutakapoelewa sehemu tu ya habari hii kwamwe hatutojua ukweli. Yesu alisema “Yesuakajibu amin, amin nawaambia, mtu asipozaliwa upya kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5).
 

KUBATIZWA KATIKA KRISTO

Tutaweza kuunganishwa 
vipi na kifo cha Kristo?
Kwa kutwika dhambi zetu zote
juu ya Yesu kupitia 
ubatizo wake.

Biblia inashuhudia siri ya wokovu. Je, ni kwa damu pekee? Hapana. Ni kwa ubatizo na kwa damu pamoja. Mtume Paulo alizungumzia juu ya hili mara nyingi katika Warumi sura ya 6 na pia katika nyaraka nyinginezo.
Hebu tusome Warumi 6:3-8 “hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake mkijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena. Kwa kuwa yeye aliyekufa maehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye.”
Hebu tuangalie mstari wa tano “kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake kadhalika mtuaunganika katika mfano wa kufufuka kwake.”
Kifo chake kilikuwa ni kifo chetu kwa sababu dhambi zetu zote zilitwikwa kwake kupitia ubatizo wake. Hivyo ubatizo wa Yesu unahusika na damu yake msalabani kwetu sisi.
Imani yetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake inaturuhusu kuungana naye. “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Hivyo alibatizwa ili kubeba dhambi zetu zote juu yake. Kwa kuamini ukweli huu ni sawa na kuungana na Yesu Kristo Mwokozi wetu.
 

HATUPASWI KUMUAMINI YESU KAMA SEHEMU YA NJIA YA MAISHA YA KIDINI

Nini maana ya “yeye ni 
mwaminifu na wa haki”?
Maana yake Yesu alitakasa dhambi 
zote mara moja na kwa wakati 
wote na kuokoa wale wote 
wenye kuamini ukweli.

Wengi humuamini Yesu kama sehemu ya njia ya maisha ya kidini, hivyo huenda kanisani na kulia machozi kwa kusali na kutubu. Hukiri dhambi zao na kuomba msamaha kila wakati. Huomba “Yesu naelewa nakuamini kuwa umekufa msalabani kwa ajili yangu. Ndiyo naamini.”
Kwa uwazi hawaelewi mstari huu “tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolea dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:9). Hudai kuwa imewapasa kusamehewa dhambi kila siku kwa kutubu. Lakini dhambi inayozungumziwa hapo haina maana ya makosa ya kila siku. Maana ya mstari huu ni kwamba, tunasamehewa dhambi mara moja na kwa wakati wote pale tunapokiri kwamba hatukuokoka.
“Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).
Wapendwa wakristo, ukweli upo wazi. Ikiwa unaamini Yesu alikufa msalabani pasipokuchukua dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake Yordani, imani yako ni bure. Ikiwa mkristo yeyote anataka kuokolewa kutoka dhambi zote, ni lazima aamini kwamba dhambi zake alibeba Yesu kupitia ubatizo wake Yordani mara moja na kwa wakati wote na kubeba hukumu ya dhambi hizo msalabani. Kwa maneno mengine yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake.
“Hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu tulipasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Yesu Kristo alibeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo na hivyo kuwa mwokozi wetu. Yesu alikuja kwa maji na damu kutuokoa kwa adhabu ya milele. “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10). Je, wewe ni mwenye dhambi, au mwenye haki?
Wagalatia 3:27 inasema “maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” Mstari huu unatuelezea ukweli kwamba, Yesu alisulubiwa baada ya kuzibeba dhambi zetu zote duniani. Kupitia ubatizo wake, alifufuka toka kuzimu baada ya siku 3 na sasa amekaa kuume kwa Mungu. Amekuwa Bwana wa Wokovu kwa wale wote wanaomwamini.
Ikiwa Yesu asingebatizwa, kama asingemwaga damu yake mslabani kwa ajili yetu, basi asingeliweza kuja kuwa mwokozi wetu. Tutaweza kuokolewa ikiwa tu tutaamini injili ya maji na Roho. 
 

HATA PAMOJA NA MTOTO WA MUSA

Kwa nini Mungu alitaka 
kumuua mtoto wa kiume wa Musa 
walipokuwa wakielekea Misri?
Kwa sababu hakuwa amemtahiri 
mtoto huyo.

Ndugu wapendwa, hapa unasikiliza siri ya ukombozi wa dhambi zako zote kupitia maji na damu ya Yesu. Ni baraka ya ajabu kuweza kusikia maneno haya ya Mungu.
Je, ni damu ya Yesu tu? Nyakati za Agano la Kale watu waliweza kuwa kizazi cha Ibrahimu kupitia tohara na damu ya Mwana kondoo wa Pasaka. Na leo hii tunakuwa watu wa Mungu kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Mungu ametuonyesha ukweli wa Agano la Kale kupitia Musa.
Ili kuokoa watu wa Israeli Mungu alinena na Musa na kumwambia awalete watu wake toka Misri. Hivyo Musa kwa mapenzi aliyokuwa nayo kwa baba mkwe wake Jethro ilimbidi aiache nchi ya Midia na kwenda Misri akiwa na mkewe na watoto wake wa kiume. Alipoipandisha familia yake juu ya punda, Bwana alikutana naye katika kambi ya kupumzikia na kutaka kumuua.
Lakini mkewe Sipora alikwisha kujua sababu ya hili. Aliokota jiwe lenye makali na kukata govi la mtoto wake wa kiume na kumtupia Musa miguuni pake huku akisema “hakika wewe ni bwana harusi wa damu kwangu mimi.” Hivyo Mungu akamruhusu kuendelea.
Hii ilikuwa njia ya Mungu kusema kwamba, hakika angemuua yeyote yule, hata pamoja na mtoto wa Musa ikiwa kama asingetahiriwa. Kwa watu wa Israeli, tohara ilikuwa ni alama ya agano la Mungu. Walijua kwamba Mungu angeliwatenga mbali na watu wake, hata kama angelikuwepo mtoto wa kiume wa kiongozi asiyetahiriwa. Hivyo ili kuzuia mtoto wake asiweze kutengwa mbali, Mungu alimpa ishara Musa kwa njia hii.
Biblia inasema kwamba, sababu ya Sipora kukata gavi la mtoto wake wa kiume na kutupa miguuni pa Musa na kusema “hakika wewe ni Bwana harusi wa damu kwangu mimi” (Kutoka 4:26).ilikuwa ni kutimiza hitaji la Mungu la tohara.
Yeyote asiyetahiriwa kati ya Waisraeli ilimpasa kuondolewa mbali na watu. Ni wale tu waliotahiriwa waliruhusiwa kula nyama ya mwana kondoo wa pasaka na kujiunga katika huduma wakiwa watu wa Mungu.
Mtume Paulo alikuwa ni Mwebrania. Alitahiriwa siku ya 8 baada ya kuzaliwa, alikuwa mwanafunzi chini ya Mwalimu (Rabi) mashuhuri Gamalieli, na alielewa vyema kwa nini Yesu Kristo alibatizwa katika Yordan na kwa nini alisulubiwa. Hivyo Mtume Paulo aliandika juu ya ubatizo katika nyaraka zake zote.
Mtume Paulo pia alizungumzia mara nyingi juu ya damu ya Yesu kama hitimisho la wokovu wetu. Damu ilikuwa ni hatua pekee ya mwisho katika ukombozi hali ukweli wa tohara ya kiroho ilikuwa ni ubatizo wa Yesu. Hakutokuwa na maana kusisitiza juu ya damu ya Yesu pasipo ubatizo wa Yesu.
Mtume Paulo alizungumzia mara nyingi juu ya msalaba wa Yesu moja kwa moja. Kwa nini ilikuwa hivyo? Kwa sababu ni uthibitisho wa hatua ya wokovu wetu. Ikiwa Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu juu yake lakini akashindwa kumwaga damu yake msalabani ili kupokea hukumu kwa niaba yetu, hakika tusingeweza kuokolewa kwa ukamilifu. Hii ndiyo maana Mtume Paulo alizungumzia juu ya msalaba mara nyingi. Msalaba ni hatua ya mwisho ya wokovu wetu.
Ikiwa ukweli wa wokovu ungeshushwa kwa ajili ya kizazi hiki pasipo kubadilisha maana, leo hii wangekuwepo watu wengi wasio na dhambi mioyoni mwao. Lakini kwa bahati mbaya ukweli huu umepotea muda mrefu na watu wengi wanachofahamu ni msalaba bila kuelewa ukweli wa maana ya ubatizo wa Yesu.
Kwa kuwa wanaimani ndani ya ganda tupu la injili, hivyo watabaki kuwa wenye dhambi hata ikiwa ni kwa miaka mingapi watakuwa wanamwamini Yesu kwa dhati. Watakuwa wenye dhambi baada ya miaka 10, hata miaka 50 ya maisha ya udini.
 

USHUHUDA WANGU

Je, Mungu huwachukulia wenye 
dhambi kuwa wenye haki?
Hapana. Mungu ni wa haki. Wenye haki 
ni wale tu walio huru kwa dhambi, 
wakiwa wamemtwika dhambi zao 
Yesu kupitia ubatizo wake.

Nilianza kumuamini Yesu nilipokuwa na umri wa miaka 20. Kabla ya kipindi hicho, nilielewa kwa kiasi gani nimekwisha tenda dhambi maishani kwa sababu sikujua sheria ya Mungu. Nilikuwa nimeishi maisha ya uasi pasipo kumjua Mungu.
Ndipo nilipougua sana. Hivyo niliwaza kuwa ningelikufa. Hivyo niliamua kwamba yanipasa walau nikombolewe kwa dhambi zangu zote kabla ya kufa. Kwa sababu nilisikia kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi kama mimi, niliamua kumwamini yeye, mwanzo nilijawa na furaha kubwa na shukrani. Lakini hisia ilianza kupotea taratibu baadaye. Baada ya miaka michache, nilishindwa na kuanza tena kutenda dhambi kila siku. Nikawa mwenye dhambi tena na tena. Baada ya miaka 10 nilikuwa bado mwenye dhambi, hakika mwenye dhambi kuliko hapo mwanzo. Nilimwamini Yesu kwa takribani miaka 10 na kwakweli nilikuwa mwenye dhambi kamwe sikubadilika. Nilikuwa vyote, mwenye kuamini na mwenye dhambi.
Ingawa niliimba “♪kulia hakutonisaidia! Ingawa uso wangu umefurika machozi, huku kusingeondoa hofu yangu, kusingetakasa dhambi zangu za mwaka mzima! Kulia hakutoniokoa!♪” Nililia kila nilipoanguka dhambini.
“Mungu wangu tafadhali nisamehe kwa dhambi hii. Nisamehe hii tu na sinto rudia kamwe” nilipotenda dhambi nilizoea kuomba kwa takribani siku tatu. Nilijifungia na kuketi kiwambazani mwenyewe ndani ya chumba na kufanya maombi ya kufunga kwa siku tatu. Kwa kuwa dhamiri yangu ilikuwa inanisuta nililia sana na kuomba msamaha wa Mungu. Baada ya siku tatu ndipo ninapojisikia nafuu na kudhani kuwa nimesamehewa katika uwepo wa Mungu.
“Sasa tena nimekwisha samehewa dhambi zangu Haleluya!” Nilitoka na kuishi maisha ya uadilifu kwa muda. Lakini punde nilitenda dhambi tena na kukata tamaa kulichipuka. Hivyo niliendelea kurudia njia hii isiyo na matumaini tena na tena. Inaleta hisia nzuri pale tu unapoanza kumuamini Yesu kwa siku za kwanza, lakini kadri nilivyoendelea kumuamini, ndipo dhambi zangu zilipojilundika kwa wingi kama vumbi katika chumba kisichotumika.
Baada ya miaka 10 nilijikuta mwenye dhambi kupindukia kuliko ilivyokuwa mwanzo. “Kwa nini nilimwamini Yesu mapemapema hivi? Ingekuwa rahisi zaidi kama ningemwamini kwanza kwa kusubiri nifikishe umri wa miaka 80 punde tu kabla sijafa. Hivyo nisingeweza kuwa na hisia ya dhambi na nisingehitaji kutubu kila siku” Nilidhani kwamba ningeweza kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu, lakini ilikuwa si rahisi. Nilihisi kwamba nitapata uwendawazimu!
Nilianza kutafuta njia mbalimbali za Mungu. Nilitumia muda mwingi kujifunza theologia lakini baada ya miaka michache moyo wangu ukawa hauna matunda zaidi na zaidi. Kabla sijaanza kusoma vitabu vya kanuni za dini, nilikuwa nimezoea kusema kuwa ningependelea kuishi kama Mtakatifu Damiani, ambaye kamwe hakulala kwenye kitanda kizuri. Niliweka nadhiri kwamba sinto jiingiza kwenye anasa (ukwasi) badala yake nitajitolea kwa wenye mahitaji.
Nilisoma juu ya maisha ya Mtakatifu huyu nikaweka nadhiri kuishi kama yeye. Nilijaribu kujiundia maisha ya upweke. Nilipiga magaoti kwenye sakafu ngumu na kuomba kwa saa nyingi kwa wakati mmoja. Ndipo basi nilijihisi sala zangu zilikuwa ni zenye maana kubwa na nilijiona bora kila siku. 
Lakini baada ya miaka 10 sikuweza kuendelea tena. Hivyo niliomba kwa Mungu, “Mungu wangu wewe uliye mbinguni tafadhali niokoe. Ninakuamini kwa moyo wangu wote. Nafahamu kuwa sintoweza kubadilisha utawa wangu kwako hata kama nitawekewa kisu kooni. Lakini ingawa nakuamini kwa moyo wangu wote, kwa nini basi ninaendelea kuhisi utupu ndani yangu? Kwa nini nimechanganyikiwa sana? Kwa nini ninaendelea kuwa mwenye dhambi zaidi kuliko mwanzo? Sikuwaza juu ya dhambi kamwe hapo awali. Nilikuamini na sasa nashangaa kwa nini nimekuwa taabani baada ya kuwa na imani kwako kwa muda wote. Ninatatizo gani?”
Ilikuwa katika kiwango hiki ndipo nilipokuja kupata sababu. Nilimwamini Mungu hapo awali pasipo kuokolewa kwa dhambi zangu. Sikujua kweli kwa wakati huo na ilitosha kabisa kunifanya nichanganyikiwe.
Nikiwa na dhambi moyoni ningeweza vipi kuwaeleza wengine juu ya ukombozi wa neema ya Mungu? Ningewaeleza vipi wengine wamwamini Yesu? Nilisali tena na tena. “Mungu wangu hivi punde tu nitahitimu shule ya dini na kusimikwa kuwa mtumishi. Lakini ikiwa nitakuwa mtumishi aliyefurika kwa dhambi, kwa namna gani basi nitaweza kuwaeleza wengine juu ya ukombozi? Mimi ni mwenye dhambi na kila ninaposoma nyaraka za Mtume Paulo nakuta kwamba ikiwa mtu yeyote hana roho wa Kristo si mwana wa Mungu. Lakini hata ikiwa nitakutafuta kwa bidii kubwa Roho hayupo ndani yangu. Nahisi kuwa ndipo hapo palipo mwanzo kwangu lakini mara kunatoweka. Nini kimetokea? Tafadhali hebu niambie Bwana!”
Ukweli ni kwamba, sababu yake nilikwisha jidanganya ndani yangu kwa kufikiri kuwa nilikwisha kukombolewa kupitia imani rahisi katika Yesu. Niliteseka kwa hili takribani muda mrefu.
Mungu aliahidi kujitolea mwenyewe kwa wale tu waliomtafuta kwa dhati. Alinikutanisha na ukweli wake hatimaye. Nilikuwa bado nimwenye dhambi kwa miaka 10 baada ya kumwamini Yesu na damu yake ndipo nilipogundua maana ya tohara katika Agano la Kale na tohara ya kiroho katika Agano Jipya, nilipogundua na kuamini siri ya wokovu kupitia ubatizo wa Kristo, mateso yangu yote yalikwisha. Moyo wangu ukawa mweupe kama theluji.
Itakuwa kama hivyo kwako. Ikiwa hautaiamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, utakuwa pia usiye na dhambi. Yawezekana kabisa usiwe mkamilifu lakini utakuwa ni mwenye haki. Unapopokea ukweli huu moyoni mwako na kufanya ueleweke kwa wengine nao pia wataokolewa na kumsifu Mungu, shangilia “Haleluya!”
Napenda kuwapongeza wale kaka zangu na dada zangu waliokwisha kukombolewa. Namsifu Yesu kwa kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Haleluya! Tumefurahi kukombolewa kwa dhambi zetu zote.
Ni baraka kuu kiasi cha kushindwa kuelezea furaha yetu yote kwa maneno ya kawaida. Hebu na tuimbe wimbo huu kwa pamoja “♪Jina lake limekuwa ni siri, kwani hatukuitangaza siri kwa kila kiumbe. Alitupiliwa mbali kama jiwe alilolikataa mwashi, lakini jina lake limegeuka kuwa madini ya thamani moyoni.♪”
 

UBATIZO WA YESU NA DAMU YAKE VINATOSHA KABISA KUOKOA WALE WOTE WENYE DHAMBI

Nini kinacho ondoa dhambi 
zote mioyoni mwetu?
Ubatizo wa Yesu.
 
Yesu Kristo alitakasa dhambi zote za dunia kupitia ubatizo na damu yake. Alitutahiri sisi sote na kutufanya kuwa watu wake. Ni Mungu wa waliozaliwa upya.
Ipo hukumu ya dhambi siku zote. Lakini Yesu alibatizwa na kuhukumiwa msalabani kutuokoa. Kwa damu yake, alituokoa sisi sote na alifufuka baada ya siku tatu. Ni Mungu Baba ndiye aliyemfufua toka kifoni.
Uhai wa Yesu ni uhai wetu na ni alama ya kuwepo kwetu tukiwa watoto wa Mungu. Ubatizo wake ulizichukua dhambi zetu zote na damu yake Yesu msalabani ni ushuhuda kwamba aliibeba hukumu kwa niaba yetu.
Rafiki wapendwa mnao ushuhuda wa ubatizo wa Yesu na damu yake mioyoni mwenu? Nauliza tena. Je wokovu wetu unakuja kwa kupitia damu ya Yesu pekee? Hapana. Unakuja kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake kwa pamoja.
 

NI NANI ALIYE MZUSHI?

Ni nani aliye mzushi?
Ni yule mtu anaye jihukumu hatia 
yeye mwenyewe kwa kushindwa 
kuamini ubatizo wa Yesu.

Ndugu marafiki, je, bado una dhambi ingawa bado unakiri imani kwa Yesu kila siku maishani? Ikiwa bado unadhambi huku ukimwamini Yesu basi ni mzushi. Uzushi nikutokuamini ukweli wa Mungu. Tito 3:10-11 inazungumzia juu ya wazushi “mtu aliyemzushi baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili mkatae, ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotea tena atenda dhambi, maana anajihukumu hatia yeye mwenyewe.”
Anaye jihukumu hatia husema “Mungu wangu! Mimi ni mwenye dhambi. Nakuamini, lakini bado ni mwenye dhambi. Hata iweje yeyote asemaye kuhusu mimi, bado mimi ni mwenye dhambi na naelewa kuwa hivi ni kweli”
Mungu atamwambia “Bado wewe ni mwenye dhambi na si mwanangu? Hivyo, wewe ni mzushi na utatupwa katika moto wa ahera.”
Ikiwa unamwamini Yesu pasipo kuamini injili ya ubatizo wa Yesu moyoni mwako, ikiwa unajihukumu hatia kuwa wewe ni mwenye dhambi na kukiri kwa Mungu roho yako ina dhambi, basi wewe ni mzushi mbele ya Mungu.
 

WAUMINI GANI WALIO WA KWELI?

Mungu hushuhudia 
nini juu ya wokovu?
Maji, damu na Roho.

Wale wote wenye kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, wale wote waliokuwa watu wa Mungu na wale wote ambao dhambi zao zimetakaswa ndiyo walio na haki mbele ya Mungu. Utawezaje kuwa mwenye dhambi hali ukimwamini Yesu? Mwenye dhambi kamwe hatoingia ufalme wa Mungu.
Wale walio na haki kwa kumuamini Yesu wanaushuhuda wa Mungu mioyoni mwao. Ushuhuda huo ni ubatizo wa Yesu na damu yake. Kazi hii ya wokovu ndiyo Yesu Kristo aliyoifanya hapa ulimwenguni.
Hivyo yeyote yule anayekataa kuamini injili ya ubatizo kwa kupitia huo ndipo Yesu alizibeba dhambi zetu zote hakika atafutiliwa mbali na Mungu.
Wapendwa kaka na dada zangu katika imani, je, unaamini kwa moyo wako injili ya wokovu wa wenye dhambi si kwa damu ya Yesu pekee bali pia kwa maji ambayo ni ubatizo wa Yesu?
Yeyote anayeamini katika kazi ile Yesu aliyoifanya hapa duniani, na yeyote nayekubali juu ya maji, damu na Roho ataokolewa kwa dhambi zake zote. Huu ni ukweli na hekima ya injili ya maji, damu na Roho. Yesu ametutakasa kikamilifu kwa dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake ili wanadamu wote waweze kuokolewa kupitia kwake. Sasa basi ikiwa kweli unamwamini Yesu, hakuna njia nyingine kwako ya kuwa ni mwenye dhambi.
Yesu alifufuka kutoka kifoni. Ameokoa roho zote zilizoangamia na kuwa mbali na Mungu kwa kudanganywa na shetani. Yesu anataka kuzitafuta roho zote zilizopotea. Mungu anatenda kazi ndani ya Yesu kupitia injili ya maji na damu na Roho. Ametuita nasi tutaweza sasa kukombolewa na kuokolewa naye.
Je, unaamini ukweli huu uliothibitika? Nawaeleza kwamba, wokovu si swala la damu tu bali kwa yote mawili, ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Wale wanaosema wameokolea kwa damu tu yawapasa kuelewa kwamba wanadhambi mioyoni mwao.
Nasi pia tulidhani namna hiyo kuwa inatosha kwa wokovu wetu kwa kuamini damu ya Yesu pekee. Tulifikiri hivyo hapo mwanzo, lakini leo hii yatupasa kuelewa kwamba haitoshi. Tumeokolewa na kuzaliwa upya kwa kuamini juu ya Yesu Kristo aliye kuja kwa maji, damu na Roho.
Kila mwenye dhambi ataweza kuzaliwa upya mara ya pili kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake (1Yohana 5:5-10). Hebu basi na tumsifu Mungu. Haleluya!