Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 6-2] Maana halisi ya ubatizo wa Yesu (Warumi 6:1-8)

(Warumi 6:1-8)
“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tulio batizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake, tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubatilike tusitumikie dhambi tena kwa kuwa yeye aliye kufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye.”
 

Ubatizo una maana gani?
 
Tunamwita Yohana, aliyembatiza Yesu, Yohana Mbatizaji. Sasa, nini maana ya ubatizo? “Ubatizo” kwa Kiyunani “babtizo” maana yake “βάφτισμα” na maana kuu iliyo muhimu ya ubatizo ni “kubeba dhambi na kifo”.
Usemi “kuzamisha” unamaanisha kifo. Dhambi zote za dunia zilihamishwa juu yake Yesu pale Yohana alipo mbatiza Yesu na hivyo alibeba dhambi hizo na kufa msalabani kulipia msharahara wa dhambi hizo zote. Yesu alikufa kwa niaba yetu. Kifo maana yake ni matokeo ya dhambi kwa sababau ya “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23).
Ubatizo pia maana yake, “kutakaswa.” Dhambi zetu zote zilisafishwa pasipo kuacha hata kidogo kwa kuwa Yesu alibeba dhambi zote duniani juu ya mwili wake kupitia ubatizo wake. Dhambi zote katika moyo wa mwanadamu zinasafishwa kwa sababu zilitwikwa juu yake kupitia ubatizo.
Ubatizo unamaana sawa ya “kuwekewa mikono.” Tendo la “kuwekewa mikono” maana yake “kutwika” Tendo la Yesu kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji lilikuwa ni kubeba dhambi zote za dunia. Lilikuwa ni sheria ya milele katika wokovu wa Mungu ambapo kuhani aliweka mikono juu ya sadaka ya dhambi ili kuitwika dhambi ya Israeli yuu yake katika siku ya kumi, mwezi wa saba.
Warumi 16:21-22 inatamka “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli na makosa yao, naam, dhambi zao zote, naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliya tayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka chini isiyo watu naye atamwacha mbuzi jangwani.” Wakati Haruni anapo weka mikono juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai, mbuzi huyo hubeba dhambi zote za Israeli na kuchinjwa kwa ajili ya watu.
 

“Kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya Dhambi ni” katika Agano la Kale humaanisha “Ubatizo” katika Agano Jipya.
 
Maana ya ubatizo ni “kuzamishwa.” Linajumuisha “kuzikwa, kutakaswa au kutwika.” Watu katika Agano la Kale walimleta mbuzi au kondoo asiye na doa na kumwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka hiyo ili kumtwika dhambi zao juu yake. Tendo hili ni sawa na ubatizo katika Agano Jipya. Mbuzi huyo alibeba dhambi kwa kupitia “kuwekewa mikono” na hatimaye kuchinjwa. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji aliye kuwa ni mwakilishi wa wanadamu, ili aweze kubeba dhambi zote za dunia na alisulubiwa.
Haruni, Kuhani Mkuu na mwakilishi wa Israeli aliweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi ili kumtwika dhambi za Waisraeli juu yake, alimchinja mbuzi huyo na kuchukua damu yake kwa vidole vyake na kuweka juu ya pembe za madhabahu ya kuteketezwa kwa moto. Kwa hiyo Luka alisema kwamba Yohana Mbatizaji, aliyekuwa amezaliwa katika familia ya Haruni alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu kama ilivyo Haruni Kuhani Mkuu alivyo kuwa mwakilishi wa Waisraeli wote.
Biblia inasema “Amini nawaambieni Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake laiye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye” (Mathayo 11:11). Yohana Mbatizaji alikuwa na haki ya kumtwika dhambi zote za dunia Yesu kwa njia ya ubatizo mara moja na kwa wakati wote akiwa kuhani wa dunia kulingana na agano la Mungu la milele. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye kuhani Mkuu wa mwisho duniani. Ninapo sema kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ni Kuhani Mkuu, baadhi ya watu husema “Imeandikwa wapi kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni kuhani Mkuu katika Biblia?” Je, haikuandikwa? Mtu aliyezaliwa na Zakaria alikua ni Yohana Mbatizaji, Kuhani Zakaria wa zamu ya Abiya, mjukuu wa Haruni Kuhani Mkuu, alikuwa kwa uwazi ni familia au ukoo wa Haruni.
Biblia inatuambia juu ya zamu ya makuhani ambapo wote ni ukoo wa Haruni na kizazi chake katika 1 Mambo ya Nyakati 24. Katika siku za mwisho za Daudi, palikuwepo na makuhani wengi hivyo kuhitaji kupangiwa zamu. Kwahiyo walipangwa kwa makundi ya zamu yapatayo 24 kulingana na idadi ya wajukuu 24 wa Haruni. Kundi la 8 lilimwangukia Abiya. Kila kundi lilitumikia madhabau na nyumba ya Bwana kwa siku 15. Na Zakaria alikuwa ni wa kundi la Kuhani Abiya aliyechaguliwa na Mungu kuwa Kuhani wa zamu katika kundi lake.
Luka 1:9 inatamka, “Kama ilivyo desturi ya ukuhani kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.” Inatuonyesha kuwa Yohana Mbatizaji alizaliwa katika familia ya Haruni, Kuhani Mkuu ambaye yeye Yohana, alikuja kuwa mwakilishi wa wanadamu wote (Mathayo 11:11, 3:13-17). Ni yulie tu aliye zaliwa katika ukoo wa Kuhani Mkuu kulingana na sheria. Ni simba tu awezaye kuzaa watoto wa simba Yohana Mbatizaji alibeba mamlaka za kikuhani toka kwa Haruni mzazi wake wa kwanza.
 

Mitume wa Yesu walishuhudia juu ya ubatizo wa Yesu.
 
Mitume wote, hasa Paulo, Petro, Mathayo na Yohana walishuhudia juu ya ubatizo wa Yesu. Hebu tuone ushuhuda wa Mtume Paulo ulioandikwa katika ujumbe wa leo. “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tulio batizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake, tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubatilike tusitumikie dhambi tena kwa kuwa yeye aliye kufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye” (Warumi 6:1-8).
Wagalatia 3:27 nayo inatamka “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvua Kristo.” Hebu pia tuone ushududa wa Petro. 1 Petro 3:21 inatamka “mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unao waokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.”
Mtume Yohana anasema katika 1 Yohana 5:5-8 “Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo, si katika maji tu bali katika damu, naye Roho ndiye anaye shuhudia, kwa sababu Roho ndiye kweli, kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba na neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja, kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na damu na watatu hawa hupatana na kwa habari moja.”
Ushuhuda wa Mathayo umeandikwa katika Mathayo 3:13-17 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe, lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini, na tazama, mbinguni zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu ninaye pendezwa naye.”
Yesu alibeba dhambi zote za dunia kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. “Ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji ambapo ilikuwa ndiyo njia inayo stahili. Mungu mwenyewe anashuhudia. “Mara akapanda kutoka majini, na tazama, mbinguni zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema huyu ni Mwanangu mpendwa wangu ninaye pendezwa naye.” Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, alishuhudia Injili ya maji na Roho kwa miaka mitatu, akasulubiwa kifo na kufufuka tena toka kifoni katika siku ya tatu. Kwa sasa ameketi kuume kwa Mungu.
Yesu atakuja tena kwao wale wote wanao msubiri, wasio na dhambi. Waebrania 9:28 inatamka “Kadhalika Kristo naye, akisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi, atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwao wao wamtazamiao kwa wokovu.” Mungu mwenyewe alisema “Huyu ndie mwanawangu mpendwa wangu ninaye pendezwa naye” na Roho Mtakatifu alishuhudia hili kwamba Mtu aliye chukua dhambi zote za dunia alikuwa ni Yesu, Mwokozi. Hata hivyo watu hawaelewi Biblia kwa sababu macho yao ya kiroho yamepofuka. Macho yao ya kiroho yamepaswa kufunguka na imewapasa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho (Yohana 3:5).
Kwa hiyo, watu hawa hudhani kwamba ni Yesu pekee ndiye aliye hudumu wokovu wa wanadamu. Lakini katika ukweli, ni kwamba, Yesu alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu na Yohana Mbatizaji ndiye aliyekuwa mwakilishi wa wanadamu. Yohana ndiye aliye ruhusiwa kutwika dhambi zote za dunia juu yake, Yesu, kwa mfano wa Haruni, Kuhani Mkuu aliyeweka mikono yake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi, (mbuzi aliye hai) na kumtwika dhambi zote za Waisraeli juu yake kwa kumwekea mikono juu ya kichwa chake. Kwa jinsi hii Haruni aliwaweka huru kwa dhambi zao kwa kumchinja sadaka huyo. Hivyo Mungu alimtuma Mjumbe wake kabla ya Yesu.
 

Yohana Mbatizaji ni nani?
 
Yohana Mbatizaji ni mjumbe wa Mungu aliyetabiriwa katika Malaki 3:1-3. Bwana alimhitaji mjumbe Yohana Mbatizaji, atakaye wakilisha wanadamu wote. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, alizichukua dhambi za milele za wanadamu wote kupitia Yohana Mbatizaji na alisulubiwa. Ikiwa mshahara wa dhambi ni mauti katika Agano Jipya, wakati wa Agano la Kale kondoo alipochukua dhambi za kipindi maalumu kilicho pangwa katika muda hivyo pia Yesu aliokoa watu wote kwa dhambi zao zote.
Matukio makuu mawili yalitokea kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, moja ni Mariamu kutunga mimba ya Yesu, na lingine lilikuwa kwa Yohana Mbatizaji kuzaliwa katika zamu ya koo wa Abiya. Matukio haya mawili yalitokea kwa nguvu ya mpango wa Mungu. Ilikuwa ni mpango mahususi wa Mungu. Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji duniani miezi sita kabla ya Yesu na ndipo kumtuma Mwana wake wa pekee ili atuweke huru toka taabu na maumivu. Je unaelewa? Hebu basi tuangalie kwa undani zaidi katika Biblia.
Hebu tuangalie Mathoyo 11:7-14 inavyo shuhudia kuhusu Yohana Mbatizaji “Na hao walipokwenda zao Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii. Hivyo aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakaye itengeneza njia yako mbele yakeo. Amini nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wana wake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Na ikiwa mnataka kukubali yeye ndiye Eliya atakayekuja.”
Watu walikwenda nyikani kumwangalia Yohona Mbatizaji aliye kuwa akipaza sauti “Tubuni kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia!” (Mathayo 3:2) Yesu aliwaambia “Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Mtu aliyevikwa mawazi mororo? Tazama watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia na aliye mkuu zaidi ya nabii.”
Katika nyakati za Agano la Kale, mfalme hakuwa na nguvu zaidi ya mtume. Wafalme walitii mitume waliyo sema. Ni nani aliye mkuu kuliko wafalme wote na mitume katika Agano la Kale? Alikuwa ni Yohana Mbatizaji. Yesu mwenyewe alishuhudia hili. Ni nani aliyekuwa mwakilishi wa wanadamu wote aliyekuwa na mwili isipokuwa Yesu? Yote, alikuwa ni Yohana Mbatizaji aliyekuwa ni Kuhani Mkuu wa duniani kwa wanadamu wote. Alichaguliwa na Bwana mwenyewe na kutumwa duniani ili atekeleze jukumu lake.
“Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona babii? Naam nawaambia na aliye mkuu zaidi ya nabii. Huyo aliye andikiwa hayo, Tazama mimi na mtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakaye itengeneza njia yako mbele yako.”
Isaya alitabiri hili kwamba taabu na vita katika Yerusalemu itafikia kikomo. Twaweza kuona kuwa utabiri huu uliweza kugundulika wakati Yohana Mbatizaji alipo sema “Tazama, mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). Yohana Mbatizaji alishuhudia kuwa Yesu ndiye Mwana wa Mungu na ndiye aliye ibeba dhambi ya dunia.
Kwa upande mwingine, Yesu alimshuhudia Yohana Mbatizaji ndiye mjumbe aliye teuliwa na Mungu aliye kuja. Mathayo 11:11 inatamka “Amini nawaambieni hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji” maana yake ni Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye mwakilishi wa watu wote duniani. Ndiye Kuhani Mkuu kwa sababu alizaliwa katika ukoo wa Haruni.
 

Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa watu wote duniani.
 
Je, unaweza kuamini kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa watu wote duniani na ni Kuhani Mkuu aliye mtwika dhambi zetu zote Yesu, ukijua kwamba Mungu alimchagua Haruni na uzao wake ili kuhudumu ukuhani daima katika Agano la Kale?
Ni nani aliye mwakilishi wa wanadamu wote? Na nani aliye kuwa mwakilishi wa watu aliye na mwili ukiacha Yesu tu? Alikuwa Yohana Mbatizaji aliye mbatiza Yesu.
“Naam, nawaambia na aliye mkuu zaidi ya nabii huyo ndiye aliye andikiwa haya”, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29) alikuwa ni Yohana Mbatizaji.
Yesu alisema “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wautaka. Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:12-13) kifungu hiki kinatuonyesha kwamba Yesu alibeba dhambi zote za dunia kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji na hatimaye kuwa Mwokozi wa wanadamu wote. Pia ina onyesha kuwa Yohana Mbatizaji alimtwika dhambi zote za dunia Yesu. Yesu mwenyewe ndiye atamkaye hayo. Hii maana yake ni kwamba Yohana Mbatizaji alimtwika dhambi zote za dunia Yesu, na kila atakaye amini ukweli huu ataokolewa na dhambi zake zote na kuingia Ufalme wa Mbinguni. Je, ndivyo au sivyo? Hakika ni kweli kulingana na maneno ya Mungu, na hivyo basi sisi wahubiri wa kweli ya kibiblia tutaweza kuhubiri hili kwa heshima kuu na atakaye amini ukweli huu ndiye atakaye ingia Ufalme wa Mbinguni.
 

Yohana Mbatizaji alimtwika dhambi za dunia Yesu akiwa kama Kuhani Mkuu wa mwisho katika Agano la Kale.
 
Zakaria baba yake Yohana Mbatizaji alisikia toka kwa Malaika wa Bwana. Hebu tuchunguze ushuhuda wa Zakaria kwa mtoto wake anasema nini juu yake. Je, ushuhuda huu ni zaidi ya kile kilicho cha kweli? Hebu basi na tusome ushuhuda wake alio imba katika mahadhi ya zaburi, “Na Zakaria baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu akatabiri, akisema. Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa, Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi, mtumishi wake kama alivyo sema tangu mwanzo kwa kinywa cha nabii wake watakatifu, Tuokolewe na adui zetu na mikononi mwao wote wanatuchukia. Ili kuwatendea rehema baba zetu na kulikumbuka agano lake takatifu uapo alimwapia Ibrahimu baba yetu ya kwamba atatujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu na kumwabudu pasipo hofu, kwa utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote. Nawe mtoto utaitwa nabii wake aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake, uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao kwa njia ya rehema ya Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti na kuingoza miguu yetu kwenye njia ya amani. Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni akakaa majagwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli” (Luka 1:67-80).
Baba yake alitabiri vile Yohana atakavyo kuwa nabii na Kuhani. Tuone alivyo mtabiria mtoto wake “Nawe mtoto utaitwa nabii wake Aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake, uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao kwa njia ya rehama ya Mungu wetu, ambozo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia kuwaangazia wakaao katika giza na uvuli wa mauti na kuwaongoza miguu yetu kwenye njia ya amani” (Luka 1:76-79).
Hapa Biblia inatamka wazi “awajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao kwa njia ya rehema ya Mungu wetu.” Ni nani ajulishaye juu ya wokovu? Luka 1:76 inaonyesha kwamba ni Yohana mbatizaji. Tunakuja kumwelewa Yesu na hatimaye kumwamini kwa sababau ya Yohana Mbatizaji kushuhudia kwamba Yesu Kristo aliokoa wenye dhambi kutokana na dhambi zao kwa njia ya ubatizo alio upokea toka kwake Yohana ili dhambi hizo zichukuliwe naye, ambapo tendo hili lilifanyika kwa namna ipasavyo na kwa halali. Yonana Mbatizaji “alikuja kwa ushuhuda ili aishihudie ili nuru wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru” (Yohana 1:7-8).
 

Ni lazima tuokolewe.
 
Yatupasa kukombolewa kwa kuamini kwamba Yesu aliokoa watu wote duniani kupitia njia iliyo halali na namna iliyo sahihi, kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. Haki ya Mungu hutamka kwamba, Yesu alikuja duniana kwa mfano wa umbile la mwanadamu akaokoa wenye dhambi wote na dhambi zao zote kwa namna iliyo halali na haki kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji na alifanywa kuwa hai tena baada ya kufa kwa kusulubiwa. Haki ya Mungu imefichika katika Injili ya maji na Roho.
Haki ya Mungu yenye kudhihirika katika Injili inatufundisha kwamba Yesu alitumwa akiwa kama mwanadamu, akabatizwa, kasulubiwa na kufufuka tena toka kifoni siku ya tatu. Tunakuja kumwamini Yesu kupitia ushuhuda wa Yohana mbatizaji na tunaokolewa kutokanana na dhambi zetu kwa kuamini haki ya Yesu. Dhambi za watu wote zilifutwa na wana uzima wa milele kwa imani katika Yesu kupitia Yohana Mbatizaji. Wamepokea Roho Mtakatifu ambaye yeye hushuhudia ndani yetu kuwa sisi ni watoto wa Mungu, akiwa ni zawadi.