Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 6-3] Vitoeni viungo vyenu kuwa silaha za haki (Warumi 6:12-19)

(Warumi 6:12-19)
“Basi, dhambi isiwatawale ndani ya miili yenu ipatikanayo mauti hata mkazitii tamaa zake, wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi bali jitoeni wenye kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamui chini ya sheria bali chini ya neema. Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii kwamba ni utmishi wa dhambi uletao mauti au kwamba ni tumishi wa utii uletao haki. Lakini Mungu na ashukuriwe kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi lakini mlitiii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekea chini yake na mlipo kwisha kuwekwa huru mbali na dhambi mkawa watumwa wa haki. Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu kwa kuwa kama mlivyo vitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.”
 

Hatuwezi kuendelea kutenda dhambi ili neema iongezeke.
 
Mtume Paulo anatuambia namna ya mwenye haki impasavyo kuishi baada ya kuokolewa toka dhambini katika Warumi sura ya 6. Ameainisha “Imani” pamoja tena na ubatizo wa Yesu. Dhambi zetu zilisamehewa mara moja na kwa wakatika wote kupitia imani ya ubatizo, msalaba na ufufuko wa Yesu. 
Hatuwezi kujawa na haki ya Mungu na wokovu wake pasipo ubatizo wa Yesu. Ikiwa Yesu hakuzichukua dhambi zetu zote alipobatizwa basi tusingeweza kusema kwamba sisi ni wenye haki baada ya kupokea ondoleo la dhambi.
Kwa uhakika hatuwezi kusema kwamba sisi ni wenye haki kwa sababau dhambi zetu zote zilitwikwa juu yake Yesu na kwa kuwa alisulubiwa na kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu zote. Warumi sura ya 6 inatufundisha yote mawili katika wokovu kwa imani na maisha ya kila siku ya mwenye haki. Amesema “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?” (Warumi 6:1). Anasema katika vifungu vilivyo pita “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana, na dhambi ilipozidi neema kuwa nyingi zaidi, ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 5:20-21). Dhambi za dunia kamwe haziwezi kuzidi upendo wa Mungu na haki yake, ingawa zaweza kuwa kubwa kupita kiasi. Dhambi zetu zilisamehewa kwa upendo wa Mungu na haki yake kupitia imani ya neno la kweli.
Biblia inasema kwamba hatuwezi kuendelea kutenda dhambi ili kwamba neema izidi ijapoluwa sisi tunaoishi katika mwili tumekwisha pokea ondoleo la dhambi zetu zote “Hasha! Sisi tuliofia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tulio batizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, na sisi tuenende katika upya wa uzima” (Warumi 6:2-4).
 

Tumezikwa na Yesu kupitia ubatizo katika kifo.
 
Utu wetu wa kale ulisulubiwa na Yesu. Hii maana yake tumekufa kwa dhambi. Dhambi zetu zote zilitwikwa juu yake Yesu na alikufa kwa niaba yetu. Hivyo basi mauti ya Yesu ni mauti yetu kwa dhambi “Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake” utu wetu wa kale ulizikwa naye kupitia ubatizo katika kifo.
Bwana alibeba dhambi zetu juu yake kupitia ubatizo na kufa msalabani kwa niaba ya wenye dhambi. Yeye hakuwa na dhambi kwa asili. Hata hivyo, alichukua dhambi zote za watu juu yake na alihukumiwa kwa niaba yao. Je, unaamini hili? Yeye binafsi hakuhitaji kuhukumiwa lakini sisi wenye dhambi tulihukumiwa katika yeye, kwa maana tulibatizwa katika Yesu Kristo.
Mtumie Paulo alisisitiza juu ya ubatizo wa Yesu. Sisi nasi tunahubiri juu ya huo ubatizo wa Yesu pia. Siyo kosa kuhubiri juu ya ubatizo wake kwa mtazamo ulio wa uaminifu na kweli. Yesu alichukua dhambi za waovu kupitia ubatizo wake na kufa kwa ajili yao kama vile mwenye dhambi alivyo mtwika juu yake yule mnyama wa sadaka ya dhambi kwa kumwekea mikono kichwani na kumchinja katika nyakati za Agano la Kale.
Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu, Mwanakondoo wa Mungu. Alibeba dhambi zote za ulimwengu juu yake pale alipo batizwa akiwa kama sadaka ya dhambi. Hivyo kifo chake kilikuwa ni kifo chetu na pia kwa wale wote wanao amini. Wale wote walio kwisha batizwa katika Kristo Yesu walizikwa pamoja naye. Wale ambao bado, kamwe hawato weza kuokolewa, kuamini, kujikana nafsi zao au hata kuushinda ulimwengu.
Ni yule tu anaye aamini ubatizo wa Yesu Kristo ndiye anaye fahamu kwamba amekufa msalabani kwa ajili yake. Mtu huyu hutawala na kuushinda ulimwengu akijikana mwenyewe. Ataweza kutegemea neno la Mungu na kuliamini. Ni wale wanao amini kwamba ubatizo wa Yesu ni jambo lisiolo weza kuwekwa kando. Kwa Yesu kubeba dhambi zote za dunia hupelekea ondoleo la dhambi yaani ule wokovu wake kamili.
Maana kuu ya wokuvu kupitia ondoleo la dhambi ni ubatizo na damu ya Yesu. Ikiwa Yesu asingelibeba dhambi za waovu wote kwa ubatizo wake, kifo chake kisingelikuwa na maana katika wokovu. Undani wa wokovu ni ubatizo wa Yesu. Dhambi zote za dunia ziliweza kutwikwa juu yake Yesu pale alipo batizwa na Yohana Mbatizaji.
 

Tumefikia kuishi na Mungu na kutembea katika upya wa uzima.
 
Mtume Paulo anasema “tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake” (Warumi 6:4) pia wale waliobatizwa katika Yesu Kristo wana ukombozi kwa imani, wali zikwa naye na kuwa na uzima mpya ndani yake. Imani hii ni imani iliyo kuu. Imani katika ubatizo ni imani ambayo iliyosimikwa katika mwamba imara.
“Basi tulizikwa pamojana naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utufufuo wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa kufufuka kwake” (Warumi 6:4-5). Twaweza kuungana na Mungu kwa imani katika ubatizo wa Yesu.
Hivyo sasa wale wanao amini katika Yesu Kristo wataweza kuenenda katika upya wa uzima. Utu wetu wa kale ulio kuwepo hapo mwanzo kabla ya kuzaliwa upya hufa na hivyo tunakuwa na utu mpya tena na hivyo tunaweza kutenda kazi mpya, tukiishi katika njia mpya kwa imani mpya. Mtu aliye zaliwa upya haishi kwa namna ya kale tena na hata namna ya kufikiri. Sababu ya kuzikana njia za kale katika kufikiri ni kwa kuwa utu wetu wa kale ulikufa msalabani na Yesu Kristo.
2 Wakorintho 5:17 inatamka “Amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya.” Bwna alibatizwa mto Yordani ili kubeba dhambi zetu, alisulubiwa na kufufuka tena toka kifoni. Kwa njia hii aliokoa waovu wote kutokana na dhambi zao ili kuwafanya waweze kutembea katika uzima mpya. Mambo yetu ya kale mateso, taabu, uchungu na mioyo yenye kutanga tanga yamekwisha sasa. Hivyo sasa uzima mpya umekwisha anza. Kuokolewa ni mwanzo wa safari ya uzima mpya.
Mungu aliwaambia wana wa Israeli kuifuata Pasaka baada ya kukombolewa toka Misri. Hii kwetu inatuashiria kuokolewa toka dhambini. Mungu aliwaambia watu wa Israeli, “Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa mwezi kwenu utakuwa ni mwezi wa kwanza na mwaka kwenu. Semeni na mkutanapo wote wa Israeli, mkawaambia, siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana kondoo kwa watu wa nyumba moja na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu yawatu; kwa kadiri ya mtaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyo fanya hesabu yenu kwa yule mwana kondoo. Mwana kondoo wenu atakuwa hana hila, mume wa mwaka moja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule, na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu katika zile nyumba watakazo mla, watakula nyama yake usiku ule ule imeokwa motoni pamoja na mkate usiotiwa chachu, tena pamoja na mboga zenye uchungu. Msiile mbichi wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni, kichwa chake pamoja na miguu yake na nyama zake za ndani. Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakacho salia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. Tena mtamla hivi mtakula mmefungwa viuno vyenu mmevaa viatu vyenu miguuni na fumbo zenu mkononi mwenu; nanyi mtawala kwa haraka ni pasaka ya Bwan” (Kutoka 12:1-11). Yakupasa kukumbuka kwamba Mungu aliwaamuru waile nyama ya mwana kondoo pamoja na mkate usio chachuka na mboga chungu katika Pasaka.
Yapo mambo mengi yajayo baada ya kuokoka toka dhambini. Mboga chungu huwakilisha kujitoa nafsi. Hapa bila shaka ni pagumu, hata hivyo yatupasa kukumbuka kwamba tumezikwa na Kristo. “Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kuke kuishi kwake amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi jehesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu” (Warumi 6:10-11).
Huu ndiyo moyo wa kuungana na Yesu. Tuna ungana na Yesu kwa kuamini ubatizo wake, msalaba na ufufuko ambao alikamilisha yote. Huduma yake ni pamoja na kuzaliwa kwake, kupokea ubatizo toka Yohana, kusulubiwa kufufuka, kupaa na kuja kwake mara ya pili katika kuhukumu wazima na wafu. Kuamini yote haya ndiyo imani ya kweli, ambayo ni imani ya wokuvu, kuhukumu kwa haki ya Mungu.
Warumi 6:10 inatamka “Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake amwishia Mungu.” Yesu hakusafisha dhambi zetu katika vipindi viwili tofauti. Yesu alifuta dhambi zote za dunia mara moja. Warumi 6:10-11 inatamka “Lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi hehesabuni wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.” Hakika tumekufa kwa dhambi lakini tuko hai kwa Mungu. Tuna uzima mpya na tu viumbe wapya.
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni; wenyewe kwa Mungu kuwa hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki kwa maana dhambi haita watawala ninyi kwa sababau hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema” (Warumi 6:12-14).
“Kwa maana dhambi haita watawala ninyi kwa sababu hamwi chini ya sheria bali chini ya neema.” Hakuna tena dhambi baada ya kukombelewa, haijalishi udhaifu wa aina gani ujitokezao katika maisha yetu. Bila shaka tuna udhaifu kwa sababu bado tunaishi na mwili. Hata hivyo, dhambi haitoweza kuwa na mamlaka juu yetu hakuna tena hukumu kwetu kwa sababu tulipokea ondoleo la dhambi kwa njia ya imani katika ubatizo wa Yesu na hukumu yake kwa njia ya damu yake ingawa bado tuna udhaifu. Ingawa uovu wetu ni dhambi pia.
Ni kweli kwamba dhambi haiwezi kuwa na mamlaka juu yetu. Mungu aliwafanya wenye dhaki kuitawala dhambi. Bwana bila shaka alisafisha dhambi zetu zote kupitia ubatizo wa Yesu mara moja na kwa wakati wote ili dhambi isiweze kututawala ingawa tu wadhaifu. Alilipa mshahara wa dhambi katika msalaba. Hawa ndiyo wanao amini kuwa hawana tena dhambi kwa sababu Bwana tayari amekwisha lipa mshahara wa dhambi.
Wenye haki huona kwamba udhaifu mwingi na uovu hujitokeza ndani yao, lakini bado dhambi haitoweza kuwatawala na hakuna hukumu kwao pale wanapo kuwa na imani ya kweli kwa Bwana. Hivyo wakati wote twaweza kutembea katika uzima mpya.
 

Vitoene viungo vyenu kama silaha ya haki ya Mungu.
 
Bwana alikwisha kubariki wenye haki katika kuishi uzima mpya kila siku. Hata hivyo, je, wataweza kuendelea kutenda dhambi? Bila shaka hapana. Warumi 6:13 inatamka “Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhaluma bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.”
“Lakini Mungu na ashukuruwe kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi” Tulikua watumwa wadhambi kwa asili na tulikuwa hodari katika hilo lakini biblia inasema “Lakini mliitii kwa mioyo yenu ili namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki” (Warumi 6:17-18).
Sisi tulio wenye haki tumekwisha wekwa huru toka dhambini nakuwa watumwa wa haki ya Mungu kwa neema. Tume kuwa wenye haki ili tuweza kutenda kazi ya haki.
Lakini sasa tufanye nini na miili yetu baada ya kukombolewa? Tuwe na tabia gani katika miili yetu baada ya kukombolewa? Biblia inasema “sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa” (Warumi 6:19). Mwili hufanya nini ingawa tumeokolewa? Mara nyingi mwili huanguka dhambini ingawa hatuna tena dhambi mioyoni. Kwa hiyo twaweza kukwepa kuanguka katika dhambi ikiwa pale tuta vitoa viungo vyetu kuwa mtumwa wa haki. Hii pia inamaana kwamba imetupasa kuvitoa viungo vyetu kwa kazi ya haki kwa sababu tumekwisha kufanywa kuwa haki.
 

Tunahitaji kujituma katika utauwa.
 
Je, sisi hatuna dhambi, ingawa mwili ni dhaifu, baada ya kuokolewa? Bila shaka kwao wale wanao amini ubatizo wa Yesu, Msalaba, ufufuko, kuja kwake mara ya pili na hukumu ya Yesu, hawana dhambi. Hawana tena dhambi mioyoni. Yatupasa kutoa miili yetu kwa kazi ya haki na mioyo yetu pia hutaka kuenenda kwa haki. Ingawa miili haiwezi kufanya kazi ya haki ya Mungu, 1Timotheo 4:7 inatamka “ujizoeze kupata utauwa” Yatupasa kujizoeza katika utauwa.
Haifanyiki kwa muda mfupi. Tunapo gawa vijitabu vya Injili kwa watu, kwa mara ya kwanza tunaweza kuona aibu tunapo kutana na watu wanao tufahamu. Tunaweza kujificha na hata kurudi nyumbani kwa kuona haya. Hata hivyo, tunapo jaribu tena mara kwa mara tukiwaza “utu wangu wa kale umekwisha kufa” na hata kuwa na ujasiri kwa kuwaonya “utakwenda jehanamu ikiwa kama huna ukombozi, kwa hiyo pokea vijitabu hivi na usome ili uongozwe kupata ukombozi!” unapo fanya hivi, basi unaweza kuutoa mwili wako kwa haki.
Warumi sura ya 6 inatuambia “kutoa viungo vya mwili kuwa watumwa wa haki na utakaso”. Lazima tuvitoe viungo vyetu kuwa watumwa wa haki. Yatupasa kufanya hili mara kwa mara. Haitowezekana kwa muda mfupi. Yatupasa kujaribu mara kwa mara. Baadaye tutakuja kuelewa namna ilivyo vyema katika kuhudhuria kanisani kama tutaanza kwenda. Tusiwaze kuwa “Naamini hili, lakini ningependa kuamini kila kitu nikiwa nyumbani. Kwa kuwa najua ni kitu gani Mchunguaji ata fundisha.” Vyote viwili, mwili na moyo lazima viwe kanisani. Imani hukua ndani ya moyo ikiwa tu utatoa viungo vya mwili kuwa utumwa wa haki.
Yatupasa kuvitoa viungo vyetu kwa kazi ya haki. Je, unaona kile ninacho maanisha? Tusijitenge mbali na mikusanyiko na mikutano ya viongozi. Unapo kwenda sokoni au dukani, ni vyema kwanza ukafika kanisani na ufungue mlango ukisema “jamani napita kuelekea sokoni vipi hamjambo hapo!” Kufika kanisani mara kwa mara ni kuvitoa viungo vya mwili kuwa mtumwa wa haki.
Viongozi wataweza kukwambia kwa mfano, “Dada yetu, samahani, je, unaweza kusafisha mahala hapa?” 
“Sawa.” 
“Na pia tafadhali urudi kuhudhuria kipindi cha jioni.” 
“Kwa ajili gani?” 
“Tutakuwa na ushirika wa vijana.” 
“Sawa nitarudi.”
Tunashughuli nyingi duniani, lakini ni wapi yatupasa kuvitoa viungo vya miili yetu kwanza wakati watu wadunia wanatuhitaji kuhudhuria mikutano yao?
Yatupasa tujitoe kwa kanisa. Yatupasa kuhudhurua kanisani ingawa tunahitajika kutembea na marafiki zetu. Tusi ache miili yetu kushinda migahawani ingawa mioyo iko kanisani. Tunapo fanya miili yetu kukwepa dunia na kuielekeza kanisani basi vyote mwili na moyo utapata tulizo.
Unafikiri nini? Ikiwa mwili wako huvutiwa zaidi na baadhi ya sehemu za starehe. Basi utaweza kuwa adui wa Mungu na mapenzi yako ingawa moyo wako unataka kuungana na kanisa.
 

Yatupasa kuufanyia mwili na roho mazoezi.
 
Yatupasa kuutoa mwili na kuwa mtumwa wa haki, lakini haina maana kwamba mwili ni mkamilifu. Lazima tuvitoe viungo vyetu kwa kazi ya haki mara kwa mara ingawa mwili hupenda kufuata yake. Mara kadhaa hujikuta tukipotoka. Inategemea ni kwa jinsi gani tunavyo utoa mwili kuwa mtumwa.
Mtume Paulo anasema “Vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Vitoeni viungo vyenu kuwa silaha ya haki ya Mungu.” Inategemea namna ipi unauelekeza au kuufuata. Matokeo yake unakimbilia kwenye baa wakati ukiwa unahitaji kwenda kanisani. Ikiwa utakaa katika baa moyo wako utahisi maumivu. Lakini ukiwa kanisani moyo wako utafurahia ingawa mwili utapata uchungu.
Mwili nao una uamuzi. Mwili hutegemea vile utakavyo elekezwa na moyo. Mwili husema “napenda pombe” pale unapo endelea kunywa. Lakini utakapo kosa pombe mwili utasema “sipendi namna hii”, kwa nini? Kwa sababu mwili hauongozwi. Itategemea vile tunavyo uongoza mwili kwa kuuzoeza ingawa moyo umetakaswa. Roho Mtakatifu huutunza moyo. Yeye bado hututunza ingawa wakati mwingine tuna liacha kanisa. Hata hivyo yatupasa kuutoa mwili wetu kuwa watumwa wa haki kwa ajili ya kutakaswa. Hivyo hudhuria kanisani mara kwa mara.
Wale waliokwisha kuokolewa yawapasa kujizoeza katika utauwa. Biblia inatuelekeza kutii neno la Mungu na hata kuongozwa nalo. Sababu ya kuongozwa na neno la Mungu ni kwamba wakati wote hupenda kufuata kile mwili inacho fanya, tukidhani kuwa miili yetu ni mali yetu. Kwa sababu tuna kwenda kununua vitu dukani, kucheza muziki na kunywa vile tutakavyo, ni vigumu kwetu kukaa chini na kuchukua muda zaidi katika kuongozwa na kuelekezwa, huku tukishurutishwa kwa kuambiwa, “Tafadhali hebu kaa kitako na usikilize neno la Mungu kwanza. Sawa?”
Yatupasa kuwa wavumilivu ingawa tutachoka kusikiliza mahubiri tukiwaza “Nataka nikae mahala hapa kwa subira. Lakini nikwa sababu gani pananichosha hali naweza kukaa baa hata zaidi ya saa 3? Kwa nini nashindwa kukaa hata saa moja? Ni saa moja sasa limepita nikiwa nasikiliza mahubiri! Nimekwisha wahi kulewa kwa saa 5 katika baa na hata kucheza michezo kwa zaidi ya saa 20 pasipo kupumizika.”
Yote haya hutegemea vile unavyo ushurutisha mwili. Mwili ambao mara nyingi hukaa kanisani hauto penda kwenda baa. Hali mwili ulio zoezwa baa ni vigumu kukaa kanisani kwani hugeuka kuwa jehanamu. Nataka uvumilie kwa siku kadhaa chache na ndipo hapo utakapo jifunza kujizoesha. Ni vigumu sana hadi pale utakapo uzoesha mwili wako. Lazima tutumie muda wetu kanisani tunapo hitajikufanya mambo mengine kwa muda wetu.
Tunatumia muda wetu kanisani, tukiongea na viongozi wetu kaka na dada zetu ilikujizoesha. Nina jisikia furaha zaidi ninapo kuwa kanisani na hakuna kinacho nitia tamaa hapo. Hata hivyo ninapo toka kwenda mitaani vitu vingi vinanitia tamaa! Yapo majaribu mengi ya kutamanisha kama vile nguo nzuri katika maduka, inanichukua saa 2 kwenda nyumbani ninapo tembea kuangalia kila kile macho yanacho taka kuona na hatumaye napotoka kimawazo.
Naweza kwenda kuangalia jambo fulani la ajabu mahala fulani. Baadaye nagundua na kujiuliza “He!nitafika nyumbani saa ngapi? Napenda mtu anitie msukumo niende” kwa hiyo usipende kuzurura hovyo unapokuwa njiani kuelekea nyumbani. Jitahidi urudi nyumbani moja kwa moja baada ya ibada, panda basi la kanisani na uende moja kwa moja kwako. Ikiwa utasema “usije kunifuata kwenda kanisani, nitakwenda mwenyewe nina miguu iliyo imara kutembea kwa hiyo, hakuna sababu yakutumia basi la kanisani” huku ukiwa huna shaka juu ya mambo yasiyo na maana njiani. Ni vyema zaidi ukachukua Biblia yako na kujisomea ukisali na kwenda kitandani kulala punde unapo rudi nyumbani.
Ni vyema kwako angalau kuishi namna hii. Mtu anaweza kufikiri kuwa “Mimi nina imani madhubuti sina dhambi. Nita jihakiki binafsi, sinto kunywa pombe hata kama nitakwenda baa. Dhambi ikiwa nyingi neema huzidi zaidi” Kama una mawazo ya aina hii na hatimaye kwenda baa rafiki zako wata kwambi, “Haloo! hebu pata kinywaji na wewe” utajibu 
“Hapana, ulikwisha wahi kuniona tena nikinywa pombe? Nimeacha!” 
Watakujibu, “Aah! hata hivyo kunywa kidogo tu!” 
“Hapana.” 
“Kwa nini usinywe divai kidogo tu?” 
Ndipo watakapo kumiminia katika bilauri, kidogo tu na kukupa. Lakini ataweza kusema “Nakunywa soda badala yake, ingawa umenijaribu ili ninywe pombe.” Hapo ndipo yanapo kuja mawazo ya hapo awali ulivyo kuwa ukipenda pombe jinsi ilivyo kuwa murua na kuanza kuwaza moyoni “Lo, ilikuwa ni tamu sana.” “Kwa nini msinipe kwa mara nyingine tena divai? Nitakunywa kidogo tu kwa leo.” Kama ulikuwa unakunywa soda utaimaliza haraka ili upate divai.
Ndipo rafiki zako watakapo gundua kwamba ungependa zaidi na hatimaye kumiminia 
“Oh ni muruwa sana.Unaweza kuchanganya na soda tu” 
Utajibu kwa unafiki, 
“Hapana. Si pendi pombe. Haujui kwamba nina mwamini Yesu na mimeokoka siku hizi?” 
Ingawa hatimaye atakunywa bilauri moja ya divai huku rafiki zako wakijua ni mnywaji mzuri wakikubembeleza, 
“Sasa rafiki yetu, kunywa leo tu!” 
“Sawa ni leo tu, lakini na ninyi pia lazima mumwamini Yesu na muokoke, sawa? Mimi mwenzenu sina tena dhambi ingawanimekunywa pombe hii. Lakini nyinyi mnadhambi? Imewapasa kuokolewa kutokanana na dhambi zenu.”
 

Jambo muhimu ni kuwa, mwili wako unauzoeza nini.
 
Wanadamu ni wajinsi hii. Hawana la kutegemewa. Jambo muhimu ni vile tulivyo utoa mwili wetu kuelekea wapi. Vitoe viungo vyako kama mtumwa wa haki katika kutakaswa. Utoe mwili wako kwa utakasao kwa sababu ni mchafu. Nilizoea ulevi na mimi kama mfano. Lakini yapo mengine kama haya. Inategemea vile unavyo uelekeza mwili wako.
Tumeokolewa kwa imani katika pumzi moja na hatimaye milele, lakini utauwa wa mioyo yetu na miili yetu hutegemea vile tunavyo utoa mwili. Tuna hisi kwamba moyo pia nao huchafuka pale tunapo toa miili yetu katika hasira, ingawa moyo ni safi. Ndipo tunapoiacha imani, kwenda kinyume na kanisa kulidhalilisha jina la Mungu bure na hatimaye kupotea mbali na uwepo wa Mungu. Tukidanganywa na shetani hatimaye tunakuja kuangamia.
Kwa hiyo jichunge ili usingamie. Uwe mwangalifu sana. Tutawezaje kuzikabili dhambi zetu za kila siku baada ya kuokolewa? “Dhambi inapokuwa nyingi neema huongozeka zaidi.” Bwana pia amefuta kabisa dhambi zako za kila siku ili kwamba tusiwe wenye dhambi tena ingawa tunaweza kuanguka mara mora.
Hata hivyo tunaweza kuwa na shida ikiwa mwili una kimbilia uovu zaidi kila mra. Tuutoe wapi mwili huu? Mwili unapaswa uelekee njia yake iliyo pangiwa. Nimekwisha sema hadi sasa ili uweze kuelewa ni wapi.
Mwili unakuwa umetakaswa kadiri moyo unavyo kuwa safi na unakuwa mtumwa wa haki mbele ya Mungu tunapo utoa kwa utumwa wa haki. Yatupasa maisha yetu kuyaelekeza kanisani hasa baada ya kuokoka. Biblia inasema kwamba kanisa ni kama mgahawa. Tuna kunywa maji, tunakula vyakula vya kiroho na kuendelea na ushirika kama vile ilivyo katika mgahawa.
Kanisa ni sawa na mgahawa. Tunaingia na kuwa na ushirika na wengine tukiongea na kila mmoja. Hivyo imetupasa kwenda kanisani hata bila shaka. Mtu ambaye ana mazoea ya kwenda kanisani mara kwa mara hugeuka na kuwa ni mtu wa kiroho ambaye mara nyingi, na yule asiyependa hawezi kuenenda na Roho ingawa labda hapo mwanzo alikuwa ni mtu mwenye imani kubwa. Mtu anaye hudhurua kanisani mara kwa mara hustawi zaidi kiroho ingawa anawezakuwa dhaifu kimwili. Ni kwa sababu ya ushirka wa kiroho baada ya kupata ukombozi.
Hakuna sehemu nzuri zaidi ya kanisani kwa ajili ya kukaa. Napenda kuwaalika mje katika kanisa la Mungu mara kwa mara na kuendelea na ushirika na watu wa Mungu. Njoo na upitie kanisani kila mara na uhudhuria ibada, sikiliza neno la Mungu napata ushauri toka kwa viongozi wako wa kiroho walio wa kweli katika Neno la Mungu kwa kila unalo panga maishani.
Lazima tuyaweke kati maisha yetu kwa neno la Mungu na kujipanga. Ndipo tutakapo fanikiwa maishani kwa imani bila kutetereka. Tunaweza kutumika kwa uthamani na kubarikiwa na Bwana. Napenda mtoe miili yenu na mioyo yenu kama silaha ya haki ya Mungu.