Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 7-3] Sababu Inayotufanya Tumsifu Bwana (Warumi 7:5-13)

(Warumi 7:5-13)
“Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko. Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema Usitamani. Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua. Basi torati ni takatifu, ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.”
 

Ninamsifu Bwana Ambaye Ameniongoza Hadi sasa
 
Ninamsifu Bwana ambaye ameniongoza hadi kuonana na ninyi watu wa Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwa kunibariki na kunifanya niishi maisha yenye furaha hadi leo hii. Mungu ameendelea kuwa pamoja nami na amekuwa akinihurumia ingawa kulikuwa na nyakati ambazo nilikuwa najisikia kukatishwa tamaa, nyakati ambazo nilikutana na magumu na kupata udhaifu ndani yangu katika vipindi mbalimbali. Mungu amekuwa makini na amekuwa upande wangu katika maisha yangu yote katika shida na katika furaha. Hakukuwa na wakati wowote ambapo Mungu aliniacha hata kwa sekunde moja. 
Mungu ametubariki kwa kiasi kikubwa sana! Ikiwa Mungu angalikuwa kama sisi basi bila shaka angalituonea huruma mara mbili au tatu na hatimaye angepoteza kabisa uvumilivu wake. Lakini Mungu si mwanadamu na uvumilivu wake hauna mpaka wala ukomo. Mungu anaendelea kutupatia rehema zake zisizokwisha bila kujalisha ikiwa tunatenda mazuri au tunatenda mabaya, bila kujalisha kuwa tunalitii au hatulitii Neno lake. Kwa kweli hali tukiwa na Mungu mwenye upendo kama huyo basi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumsifu, kumwabudu na kumtumikia. Mfalme Daudi alimsifu Bwana katika maisha yake yote hali akimshukuru kwa kumtunza na kumlinda kila wakati alipoingia katika matatizo kwa kupitia magumu katika maisha yake. Daudi alikiri kuwa “Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta” (Zaburi 18:29).
Mungu ametubariki kwa kiasi kikubwa sana! Kwa kweli hatuwezi kumsifu yeye vya kutosha. Je, tunaweza kutosheka ikiwa tutajenga kanisa kubwa kama ulimwengu mzima? Je, tunaweza kutosheka ikiwa tutajenga kanisa ambalo linafika hadi mawinguni? Kwa kweli sio kweli! Tunaweza kujenga kanisa kubwa na zuri kuliko yote kama tunavyodhania, lakini kinachojalisha si ukubwa na uzuri wa kanisa bali ni ule ukweli kuwa Mungu anafanya kazi kwa thamani kubwa katika kuziita nafsi za watu na kuzifanya zilisikie Neno lake na kuwaruhusu kuzaliwa tena upya na kuamini katika Neno lake. Na kwa sababu hiyo hakuna tunachoweza kukifanya zaidi ya kumsifu Bwana wetu kwa baraka hizo zote. Tunatoa shukrani kwa Mungu kwa kuturuhusu kumtumikia, hali tukizaa matunda ya kazi yake. 
Je, humshukuru Mungu kwa kukuruhusu kuketi katika sehemu hii mpya ya utulivu? Mungu wetu ametubariki kwa neema yake isiyofungwa na ametufanya sisi kuwa mboni ya jicho lake. Sisi ni akina nani na tumefanya nini hata tukastahili upendo wake huu? Sisi si kitu na hatujafanya lolote. Lakini bado Mungu ametufanya sisi kuwa wa thamani mbele zake, ametufanya kuwa wa thamani si kwa sababu tumefanya lolote la kuweza kulionyesha bali kwa sababu tumezaliwa tena upya. Kabla ya kukutana na Yesu Kristo sisi tulikuwa si kitu chochote. Mungu alitufanya sisi tuliokuwa katika matope, tuliokuwa tukitangatanga jangwani, tuliokuwa tumepangiwa kufa na kupotea katika mavumbi na majivu tume kuwa watoto wake. 
Upendo wa Mungu aliotupatia ni mzuri na mkubwa sana! Bwana Asifiwe! Miongoni mwa nafsi nyingi katika ulimwengu huu, Mungu ametuokoa sisi kwa upendo wake usio na masharti katika haki yake. Kwa kweli ni wokovu mkamilifu na si ukombozi tu. Hii ina maanisha kuwa kwa sasa nafsi zetu zina uhusiano pamoja na Mungu. Hii ina maanisha kuwa upendo wa Mungu ni wetu. Pia inamaanisha kuwa hata baraka zake pia ni zetu na tunaweza kuzidai. 
Ni kwa kupitia mwongozo wa kushangaza wa Mungu ndio maana tunaweza kujikuta sisi wenyewe tupo katika Kanisa lake. Ikiwa Mungu angekuwa hajatuweka hapa basi tungewezaje kuwa hapa? Ikiwa Mungu angekuwa hajatupenda na kutubariki basi tungewezaje kuihubiri injili na kumtumikia Mungu? Sisi tunaweza kumtumikia Mungu kwa sababu yuko hai, yuko pamoja nasi, na ametubariki. 
Ikiwa Bwana angekuwa hajatutunza wala kutubariki basi kwa hakika tusingeweza kumsifu hapo kabla au hata sasa. Mungu ametubariki, ametupenda, ametutia moyo, na ametufunika kwa mikono yake yenye rehema ili tuweze kumtumikia, kumfuata, kumsifu na kumwabudu yeye. Je, hii si kweli? Kwa kweli sisi tunamsifu Bwana kwa mioyo yetu yote kwa kazi zake za kushangaza na upendo wake usiokwisha kwetu. 
Mungu amefanya mambo mengi kwa wale ambao amewaokoa. Kule kusema kuwa Mungu ametukomboa, na kwamba anaendelea kuiimarisha imani ya watakatifu waliozaliwa tena upya ni uthibitisho kuwa Mungu anatushikilia na kwamba anatulinda. Mungu anatenda na kuyatimiza mapenzi yake kwa kupitia kwetu. 
Ninaamini kuwa Mungu ameyabariki makanisa yake yote, ambayo ni makusanyiko ya waliozaliwa tena upya duniani pote na ataendelea kuwabariki milele. Sisi tumekutana na magumu mengi lakini Mungu ameendelea kuwa pamoja nasi, ametufanya sisi kuvumilia na kuendelea kuifanya kazi yake, amezi imarisha roho zetu na ameiandaa mioyo yetu kuwa na imani inayohitajika ili kuweza kupokea baraka zaidi. Neema yake ni kubwa sana! Kwa kweli ninatoa shukrani kwa Bwana kwa mara nyingine tena. 
 

Tunaweza Kumsifu Bwana Kwa Mioyo Yetu Yote 
 
“Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko” (Warumi 7:5-6). Biblia inasema kuwa tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za mwili zilizoamshwa na torati zilikuwa katika viungo vyetu ili kuizalia matunda mauti. Hata hivyo, Biblia inasema, “Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.”
Je, mwili unaweza kukombolewa toka katika tamaa mbaya ya dhambi? Mwanadamu ana sehemu mbili za uwepo. Moja ni mwili na nyingine ni moyo. Mwili hauwezi kuifikia haki ya Mungu hata kama ukijitahidi kiasi gani. Pia hauwezi kuitunza na kuishika Sheria ya Mungu. Mwili wetu hauwezi kuitunza na kuishika Sheria ya Mungu hata baada ya kuzaliwa upya hata kama tukijitahidi kiasi gani. Ndio maana Mtume Paulo anasema, “Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga.”
Warumi 4:15 inasema, “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Ni lazima tumsifu Mungu wetu katika mioyo yetu. Mungu alituumba ili tumsifu katika upya wa Roho, na wala si katika hali ya zamani ya andiko, kwa kuwa sisi tuliokuwa tumeshikiliwa na Sheria tulikuwa tumelaaniwa tayari na hasira ya Torati. 
Mwili ni tofauti na moyo. Mwili una ukomo lakini moyo unaweza kupokea Neno la Mungu na kumsifu kwa imani. Moyo unaweza kukombolewa toka katika dhambi. 
Sisi tumeifia Sheria. Mimi ni mfu kwa sababu nimeifia ile iliyokuwa ikinishikilia. Miili yetu imemfia Mungu tayari. Kwa mwili, hatuwezi kuifikia haki yake wala hatuwezi kuhesabiwa haki mbele ya Sheria ya Mungu. Mwili hauwezi kukwepa kuhukumiwa. Lakini Mungu Baba alimtuma Mwanae pekee Yesu Kristo na akaipitisha hasira na ghadhabu yote ya Torati juu yake, na kisha akasulubiwa kwa ajili yetu. Kwa hiyo Mungu ametuwezesha sisi kumtumikia Bwana kwa imani katika upya wa Roho na wala si katika hali ya zamani ya andiko, ambayo ilikuwa imetushikilia kwa Torati na chini ya ghadhabu ya Torati hiyo. 
Sasa tunaweza kumsifu Mungu kwa imani. Pamoja na kuwa bado tunao mwili, moyo unaweza kumsifu Bwana. Mioyo yetu inaweza kuamini kuwa Bwana anatupenda sisi. Tunaweza kumsifu Bwana wetu kwa kuwa tunaamini kuwa sisi tu wafu katika Kristo. Mungu ametuokoa toka katika hasira na ghadhabu ya Torati. Mungu Baba alimtuma Mwanae pekee kwa ajili yetu sisi ambao tulikuwa tumeshikiliwa na laana ya Sheria na hukumu ya Mungu, na utimilifu wa wakati ulipowadia, Mungu alizipitisha dhambi zetu zote na ghadhabu ya Sheria katika Mwana wake. Hivyo, Mungu amewaokoa wale ambao wanaupokea upendo wake na wanao mwamini Mungu toka katika dhambi zao, toka katika hukumu ya Mungu, na toka katika ghadhabu ya Sheria. Sisi tunamsifu Bwana kwa kutuokoa kikamilifu toka katika dhambi zetu zote. 
Tunaamini kwa moyo wote kuwa Mungu ametuokoa sisi katika haki yake. Tunatoa shukrani zetu, tunamsifu na kumtukuza Mungu kwa mioyo yetu yote kwa upendo wake. Lakini je, tunaweza kuyafanya mambo haya yote kwa miili yetu? Hapana. Wakati tulipokuwa katika mwili tamaa mbaya ya dhambi iliyokuwapo kwa Torati ilitenda kazi ndani ya vioungo vyetu ili kuizalia matunda mauti. Mwili unadumu na kutenda chini ya hasira ya Mungu. 
Sasa tumekombolewa toka katika hasira hii ya Torati kwa imani. Mungu alitufanya sisi tumtumikie yeye kwa imani yetu katika upendo wake na wokovu wake na wala si kwa hali ya zamani ya andiko na wala si chini ya Sheria ya hasira ya Mungu hata kama tutakuja kuhukumiwa kwa Sheria. 
Hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kumtumikia Bwana kwa matendo yetu. Pamoja na kuwa tumezaliwa tena upya, kwa kweli hatuwezi kumtumikia Mungu kwa miili yetu. Je, kuna yeyote miongoni mwetu ambaye amekatishwa tamaa wakati akijaribu kumtumikia Mungu kwa mwili? Kwa kweli hatuwezi kumtumika Mungu kwa Mwili. Tamaa mbaya ya dhambi inautawala mwili wakati wote. Hatuwezi kumtumikia Bwana kwa miili yetu hata baada ya kuzaliwa tena upya. Tunaweza kumsifu Mungu na kumtumikia yeye kwa mioyo yetu tu kwa imani. Hivyo, unapomsifu Mungu, amini kwa moyo wako wote na umpe Mungu shukrani kwa upendo wake. Basi ukifanya hivyo, mwili utakuwa ni kama chombo kinachoifuata imani. 
Ninamsifu Bwana ambaye ametuokoa sisi toka katika ghadhabu ya Torati, kwa kuwa ninamwamini Bwana kwa moyo wangu wote. Ninamtolea Bwana shukrani zangu. Bwana ameniokoa mimi kikamilifu. Bwana amenikomboa mimi toka katika dhambi zangu za kila siku na toka katika laana ya Torati. Hivyo kusiwe na shaka tena, maana Bwana ametuokoa. Pamoja na madhaifu na mapungufu yetu yote, Bwana ametuokoa kwa kuwa anatupenda. Ni jambo la kufurahisha kiasi gani kuona kuwa Mungu ametufanya sisi kuwa wenye haki hata pale ambapo tumejawa na mapungufu? Ni jambo la kushangaza kiasi gani kuona kuwa Mungu ametufanya sisi kuwa watumishi wake? 
Tunaweza kumsifu Mungu kwa sababu ametuokoa toka katika ghadhabu ya Torati. Sisi tunaweza kumtumikia Bwana kwa Roho na kwa mioyo yetu. Tunaweza kumfuata Bwana. Tunamtolea Bwana shukrani zetu ambaye ametukomboa toka katika dhambi zetu na hasira yake. Je, unamtolea Bwana Shukrani? Je, wokovu wetu haudhihirishi jinsi tulivyokuwa dhaifu? Ni mara ngapi ambapo tumeshindwa kuishi kwa kufuata mapenzi yake ingawa tumejaribu kwa kadri tuwezavyo kufanya hivyo? Ni mara ngapi tumekuwa watu wenye kujisifu? Je, tuna madhaifu mangapi? Kwa kweli hatuwezi kumsifu Mungu kamwe kwa miili na matendo yetu, si tu kwa sasa bali hata kwa wakati ujao. Tunamsifu Mungu kwa kile alichokifanya kuhusiana na mioyo yetu. Ni kwa mioyo yetu tu na kwa imani yetu tu ndipo tunapoweza kumsifu Bwana. 
 

Hatuwezi Kumsifu Bwana Kwa Mwili
 
Haki yetu binafsi inafikia hatua ya kuvunjwavunjwa katika vipande tunapokuwa tukimfuata Bwana. Ulimwengu wa fikra na akili na ulimwengu wa mwili ni lazima vitenganishwe. Na huku ndiko kuitenganisha roho toka katika mwili. 
Je, unaamini hivi? Kwa kweli ni jambo lisilo na maana kwetu kujaribu kwa mwili. Tunapoimba, kufurahia, kusifu, kuamini, kufuata na kutoa shukrani kwa mioyo yetu, basi miili yetu inaweza kumtumikia Mungu hali ikiifuata mioyo yetu. Sisi tunamsifu Bwana na kumtolea shukrani kwa ajili ya wokovu wetu hali tukiimba, “♫Dhambi zangu zote zimetoweka, kwa sababu ya Kalvari; Maisha yamejawa na nyimbo, yote ni kwa sababu ya Kalvari; Kristo anaishi ili kuniweka huru toka katika dhambi; Siku moja atakuja Ooh kwa kweli itakuwa ni siku ya baraka! Yote hii ni kwa sababu ya Kalvari. ♫” Lakini wakati mwingine tunajikwaa kwa sababu ya mwili. Ndipo tunapojifikiria, “kwa nini mimi ni dhaifu kiasi hiki pamoja na kuwa sina dhambi?” Ndipo tunapojishangaa wenyewe, “‘♪Dhambi zangu zote zimetoweka ♪’—hiyo ni sawa—‘♪Maisha yamejawa na nyimbo ♪’—hiyo pia ni sawa— ‘♪Yote ni kwa sababu ya Kalvari ♪’—hiyo ni sawa, lakini kwa nini mimi ni dhaifu kiasi hicho? Ninapaswa kutoa shukrani na kumfuata Bwana kwa furaha zaidi na kwa wakati, lakini kwa nini nimejawa na mapungufu? Aah mwili wangu wa kusikitisha!”
Tunapojisikia kuwa tuna huzuni, Mungu anasema nasi, “Kwa nini unahuzunika, ee nafsi yangu? Je, hufahamu kuwa mimi ni mwokozi wako? Nimekufanya kuwa mwenye haki.” Kwa kweli hatuwezi kumtumikia wala kumfuata Mungu kwa mwili. Tunaweza kumtumikia Mungu kwa kuamini katika kile alichokifanya ili kutuokoa sisi, kwa kumpenda, kwa kumpatia shukrani na kwa kumtukuza kwa mioyo yetu. 
Ninahitaji umsifu Mungu kwa moyo wako. Pia ninataka uamini na kumtolea shukrani Mungu kwa moyo wako. Mambo haya yanawezakana kwa kupitia katika mioyo yetu tu. Mambo haya hayawezekani kwa mwili. Wakati wote mwili unabakia kuwa usiobadilika hata baada ya kuwa tumeokolewa. Kile ambacho Mtume Paulo anakisema katika kifungu hicho hapo juu kinajumuisha hali zote kabla na baada ya kuokolewa. Neno la Mungu ni moja kwa wale waliookolewa na kwa wale ambao bado hawajaokolewa. 
 

Je, Umeendelea Kumpendeza Mungu kwa Mwili Baada ya Kuokolewa? 
 
Je, umeendelea kumpendeza Mungu kwa mwili baada ya kuokolewa? Je, unafikiri kuwa unaweza kumpendeza Mungu ati kwa sababu wewe ni tofauti na wengine na kwamba unamtumikia Mungu zaidi kuliko hao wengine? Wale ambao wamejazwa na haki yao binafsi kuna siku moja wataangukia katika shimo. Kuna baadhi ya watu ambao wana uzoefu wa kuanguka katika shimo. 
Kuna dada mmoja aliangukia katika shimo la mbolea katika kipindi cha Mkutano wa Biblia wa Kiangazi. Ninamaanisha kuwa aliangukia katika shimo halisi lililokuwa nje ya nyumba ambalo lilikuwa bado halijatumika kama choo. Ingelikuwa kuna mtu amelitumia basi kwa kweli dada huyu angekuwa katika wakati mgumu sana. Tulikuwa tumechimba mashimo marefu na tulikuwa tumeyajengea vibanda katika kilima chenye miti ya kijani wakati tulipokuwa tukiuandaa mkutano huu. Kisha tukaweka sehemu ya kuwekea miguu katika kila choo, lakini tulikuwa hatujakaza vizuri sehemu hizo za kuwekea miguu, hivyo huyu dada aliteleza na kuangukia katika shimo. Mungu amechimba mashimo ya jinsi hiyo kwa wale ambao wamejazwa na haki yao binafsi. Mungu anatuhitaji sisi tumtukuze yeye tu. 
Nafsi yangu inajisikia kutokuwa na raha wakati ninapochepuka toka katika njia sahihi baada ya kuwa nimeokolewa. Ninapotafakari kuwa ni kwa nini ninajifikiria hivi, ndipo ninapotambua kuwa mavazi yangu yametiwa doa na uchafu. Ndipo ninapotambua kuwa sipaswi kuenenda kwa jinsi hiyo, lakini baada ya muda mfupi ninasahau. Mara ninapotambua hivi ninatubu kwa kusema, “sipaswi kufanya jambo hili. Nilikuwa nawaza nini? Aah, Bwana. Ninakusifu kwa kuzioshelea mbali dhambi zangu zote.” Lakini baada ya muda mfupi ninatenda dhambi tena. Wakati fulani ninakuwepo na kuishi katika neema ya Mungu na ghafla ninaangukia katika dhambi. Kisha, ninajikuta nikiikwepa dhambi kwenda katika neema ya Mungu. Ninayumba mbele na nyuma. Ndipo mwishowe ninashusha pumzi kwa huzuni nikifikiri juu ya uwepo wangu. 
Nilifikia hatua ya kutambua jinsi nilivyo mchafu baada ya dhambi zangu zote kusamehewa. Ndipo nilipofikia kutambua kwa kina na kuwaza, “Ni mbaya sana. Pamoja na kuwa ninakuamini wewe Mungu, kwa nini mimi ni mnyonge na mdhaifu kiasi hicho?” Tamaa mbaya za dhambi ambazo zinaamshwa kwa Torati zinafanya kazi katika viungo vyetu. Nilitambua kuwa kadri nilivyojitahidi kuishi kwa mujibu wa Sheria, ndivyo mwili wangu ulivyozidi kuangukia katika tamaa mbaya za dhambi. Nilifikia hatua ya kutambua kuwa mwili hauwezi kamwe kumfuata Mungu. Nilifikia hatua ya kumtumikia Bwana kwa kuutoa mwili wangu kama chombo cha haki ya Mungu na nilikisifu kile ambacho Mungu amekibariki baada ya kumwamini yeye katika moyo wangu. 
 

Mwili ni Lundo la Tamaa za Dhambi
 
Wale wasiotambua kuwa wao ni lundo la tamaa za dhambi mara nyingi wanashangazwa jinsi wanavyoteleza na kuangukia katika dhambi hasa pale wanapoacha kumtumikia Bwana kwa kitambo fulani. Ni lazima tumwamini Bwana, tumsifu yeye, tumtukuze na kumfuata yeye kwa mioyo yetu yote. Kumfuata Mungu kwa moyo ni baraka ya neema ya Bwana. Tunaweza kumfuata Mungu pale tunapo mwamini yeye kwa mioyo yetu yote. Tunapokuwa katika mwili, tamaa za dhambi, ambazo zilikuwa zikiamshwa na Torati zinafanya kazi katika viungo vyetu ili kuizalia matunda mauti. Tunapokuwa hatumsifu au hatumfuati Bwana kwa mioyo yetu, basi miili yetu inaanguka kwa haraka katika tamaa za dhambi. Sisi sote tuna tatizo la aina hii ambalo hata Mtume Paulo alikuwa nalo. 
Paulo aliishi akiwa mseja maisha yake yote hali akiihubiri injili. Lakini alifikia hatua ya kutambua kuwa dhambi iliamshwa kwa kupitia tamaa mbaya za mwili. Bila shaka alifikiria kuwa, “Ninaogopa. Nilikuwa nimejawa na furaha muda si mrefu uliopita, lakini kwa nini sasa ninasononeka? Nina tatizo gani? Nilikuwa mtu wa kiroho sana muda mfupi uliopita lakini sasa ninajisikia kuwa ni kama pipa la taka.” Baada ya kufikiria tena na tena, Paulo alikuja kutambua kuwa hawezi kumtumikia Bwana pasipo kuutenganisha mwili toka katika Roho. “O maskini mimi! Siwezi kufanya mema kwa mwili.” 
Wakati tunamsifu na kumfuata Mungu kwa mioyo yetu basi mwili unautii moyo. Paulo aliutambua ukweli huu. Sisi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi. Je, unalitambua jambo hili? Wakati wale wasio na dhambi wanapomsifu Bwana kwa mioyo yao, basi miili itaufuata moyo. Mtu anaweza kufikiria kwa mara ya kwanza, “Nimeokolewa toka katika dhambi zangu zote. Halleluya. Ninafuraha sana.” Lakini tamaa mbaya zinazidi kujifunua zaidi na zaidi ndani ya mtu huyo katika kipindi fulani. Wale ambao wamejazwa na haki yao binafsi ndio wanaokatishwa tamaa kwa urahisi zaidi kadri tamaa mbaya zinavyozidi kujitokeza kidogo kidogo. Ingawa wanaweza wasifikirie hivyo ukweli ni kuwa wao ndio wanakuwa wabaya zaidi kuliko wanavyoweza kujifikiria. 
Ni lazima tutambue kuwa miili yetu ni lundo la tamaa za dhambi. Hatuna ujasiri katika mwili; na kamwe usiutegemee mwili. Badala yake, amini katika neema ya Mungu, mtukuze Bwana, na umfuate kwa moyo wako wote. Mambo haya yanawezekana tu kwa kupitia katika moyo. Msifu Bwana, kwa kuwa ni neema ya Mungu inayoniruhusu mimi, ambaye nilikuwa mbaya katika kuongea na niliyekuwa nimejawa na haki yangu binafsi ili kuihubiri injili! Ninawezaje kufanya hivyo pasipo neema ya Bwana? Ninaweza kumsifu Bwana wangu. 
 

Ninamshukuru Bwana Aliyeniwezesha Kumsifu
 
Ninatoa shukrani kwa Bwana aliyezioshelea mbali dhambi zetu zote na aliyetupatia Roho Mtakatifu ili kutufanya sisi tuweze kumsifu yeye kwa mioyo yetu na si kwa miili yetu. Tunaweza kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sababu tunamwamini yeye kwa mioyo yetu yote. 
“Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana” (2 Wakorintho 5:6). Ninamsifu Bwana aliyetuokoa toka katika dhambi zetu zote. Ninamsifu na kumshukuru Bwana. Ninamtukuza na kumwamini Bwana. Bwana ametuokoa toka katika dhambi zetu zote, hata pale tulipokuwa tumepangiwa kufa baada ya kuwa tumeishi kwa tamaa za dhambi. Mungu alituruhusu kuokolewa kwa kumwamini Mungu kwa mioyo yetu. Alitufanya sisi tumsifu yeye na akatupatia furaha. 
Usijaribu kumtumikia Mungu kwa mwili—kwa kuwa haiwezekani. Usijaribu kuipata hali ya kimungu kwa mwili—kwa kuwa hali hiyo haiwezi kupatikana. Jitahidi uache juhudi hizo za kimwili. Je, tutafanyaje basi katika kumfuata Mungu? Tutamfuata Mungu kwa mioyo yetu. Tunaweza kumtumikia Mungu kwa moyo katika upya wa Roho. Mungu wetu ametuokoa sisi, hivyo mfuate Mungu kwa moyo wako uliokuwezesha kuupokea wokovu. 
Ninamsifu Mungu. Je, ni watu wangapi ambao wana jiombolezea wao wenyewe? Wanashusha pumzi kwa uchungu na wanajiumiza wao wenyewe hali wakisema, “Kwa nini ninafanya kama hivi?” Usiwe kama wao. Kwa kweli haiwezekani kwa wewe kutotenda dhambi hali ukiwa na mwili. Usijaribu kulifanya lisilowezekana kuwa linalowezekana. Ninataka uamini katika Mungu na umsifu yeye katika moyo wako. Kisha mwili utaufuata moyo. Je, umejaribu kumfuata Bwana kwa mwili wako kwa muda mrefu baada ya kuwa umeokolewa? Je, una tatizo kuhusiana na lile ambalo ungepaswa kulitenda? Ikiwa ndivyo, basi tatizo ni kuwa unajaribu kumtumikia Mungu kwa mwili wako na wala si kwa moyo wako. Je, unafahamu kile ambacho wanachokisema wale ambao wananidharau mimi? Wananicheka huku wakining’ong’a. Lakini mimi ninatoa tabasamu kwao kwa kuwa ninafahamu kuwa hawatambui kile kinacho endelea ndani yangu. 
Mimi ninaweza kuihubiri injili kwa sababu Bwana amekwisha ziosha mbali dhambi zangu zote. Ikiwa Bwana angekuwa hajaziosha mbali dhambi zangu basi kwa hakika ningekuwa nimesha hukumiwa kufa na Mungu. Mungu ametufanya sisi kuwa wakamilifu kwa kutufanya sisi kuwa wamoja kwa Roho. Mungu ametufanya sisi kuwa ni wale tunaomsifu yeye. Ametufanya sisi kuishi kwa akili zenye shukrani. Ametufanya sisi kuzifurahia baraka zake. Mungu asifiwe! Bwana Asifiwe aliyetufanya sisi kuwa watoto wake! Utukufu wote na uwe wake!
Kwa kweli bado hatujachelewa. Usiweke tumaini katika mwili wako. Tamaa za dhambi zinatoka ndani yetu mara moja na katika fursa ndogo inayopatikana. Mara nyingi mwili unataka kujifanya kuwa ni kipaumbele badala ya mapenzi ya Mungu. Hii ndio sababu kuyafuata mapenzi ya Mungu inawezekana kwa imani tu. Kwa kweli kwa mwili haiwezekani. Usijaribu kujidanganya wewe mwenyewe hata baada ya kuwa umeokolewa. Pamoja na wokovu wetu, chini ya utawala wa mwili bado inawezekana kabisa kwetu sisi kuanguka kwa sababu tunafahamu wazi kuwa mara zote mwili si mkamilifu na ni mdhaifu. 
Sisi ni watu wa Roho, ni watu wa imani. Hivyo usiweke matumaini yako katika mwili. Nifuatishe mimi: “Mwili wangu ni kama pipa la takataka.” Ninataka ukumbuke hili. Usijiamini sana wewe mwenyewe. Ni lazima tuamini na kumfuata Mungu kwa mioyo yetu. Ninatoa shukrani kwa Bwana na ninamsifu kwa kutuokoa toka katika ghadhabu yote ya sheria ya Mungu. Halleluya!