Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-8] Rangi ya Lango la Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)

Rangi ya Lango la Ua wa Hema Takatifu la Kukutania
(Kutoka 27:9-19)
“Nawe utaufanya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Kwa upande wa Kusini kuelekea Kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani safi yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia. Na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini na vitako vyake vitakuwa ishirini na vitakuwa vya shaba. Kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. Na vivyo hivyo, upande wa Kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba, na kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. Na kwa upande wa magharibi, upande wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi na vitako vyake kumi. Upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini. Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa na upana wa dhiraa kumi na tano; nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu. Na kwa upande wa pili ni vivyo hivyo, chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu na vitako vyake vitatu. Na kwa lile lango la ua kutakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa na nguo ya rangi ya bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa, kazi ya mshona taraza; Itakuwa na nguzo nne na vitako vyake vinne. Nguzo zote za ule ua ziuzungukazo pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha na vitako vyake vya shaba. Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano, uwe wa nguo ya kitani safi na vitako vyake vitakuwa vya shaba. Vyombo vyote na vigingi vyake vyote vitumikavyo katika Hema Takatifu la Kukutania, na vigingi vyote vya ule ua vitakuwa vya shaba.”
 
 
Lango la mahakamaKuna tofauti za wazi kati ya imani ya wale waliozaliwa upya na ile ya wakristo wa mazoea: imani ya wale waliozaliwa upya inafahamu na kuamini kuwa Mungu amezifuta dhambi zao zote, na imani ya wakristo wa mazoea inamwamini Yesu kwa kuyategemea mawazo yao binafsi, ni kama suala la kidini tu. Pamoja na hayo wale wanaomwamini Mungu kama sehemu ya masuala ya kidini wanafanikiwa sana kiasi kuwa wale wanaohubiri ukweli halisi wanaumizwa moyo pale wanapowaona watu hawa wenye imani potofu wakiyaeneza mafundisho yao ya uongo huku wakifanikiwa. Wanaumizwa mioyo kwa sababu wanafahamu wazi kuwa Wakristo wengi sana wanaletwa katika dini hiyo ya uongo na udanganyifu.
Mimi pia niliumizwa moyo na jambo hili kwa muda. Kwa sababu nilikuwa nimezaliwa upya kweli kweli kwa kukutana na ukweli, na kwa kweli ninamshukuru Mungu kwa kunitumia kama chombo kwa kazi yake, na kwa sababu moyo wangu ulitamani sana kuona kweli ya Mungu inaenezwa mbali na kwa mapana, nilipowaona watu wengi sana wakiyaongoza maisha yao ya kidini hali wakiwa wamedanganywa kwa uongo, sikuweza kufanya chochote bali nilihuzunishwa mno.
Hata hivyo, kilichowazi ni kuwa Roho Mtakatifu yuko ndani ya moyo wangu, na kwamba pamoja na mapungufu yangu, moyo wangu hauna dhambi. Kwa hiyo, katika moyo wangu inapatikana shukrani, na siionei haya injili ambayo ninaiamini. Ninapoihubiri injili hii kwa watu ulimwenguni pote, ikiwa wanalisikia Neno hili la kweli na kuliamini, wao pia wanaweza wasiwe na aibu mbele za Mungu na watu, kwa kuwa wanapouamini ukweli huu, wote wanafanyika kuwa wana wa Mungu.
Wewe pia unaweza kuwa na baraka kama hizo kwa imani. Ingawa haujasomea theolojia, ikiwa unauamini ukweli wa injili hii ya maji na Roho, utapokea ondoleo la dhambi zako, utafanyika mwana wa Mungu, na utapokea Roho Mtakatifu katika moyo wako, na kwa huyo Roho Mtakatifu unaweza pia kutembea na watumishi wa Mungu. Huu ndio ukweli halisi na kuamini hivyo ni imani ya kweli.
Ingawa ninaishi katika ulimwengu uojaa uongo, na kwa sababu ndani ya moyo wangu kuna imani hii ya kweli, nimeweza kuendelea kuihubiri injili ya kweli hadi sasa. Tangu nilipoanza kulihubiri Neno katika mada ya Hema Takatifu la Kukutania, ndipo nilipoweza kufahamu vizuri juu ya mipango ya waongo, na kwa hiyo niliweza kutambua kati ya ukweli na uongo. Hii ndiyo sababu nimekuwa nikiushuhudia ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Ukweli huu unanipatia furaha kuu kwamba kwa kuueneza ukweli halisi kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania, watu wameweza kutambua kati ya ukweli na uongo.
Katika kukiandika kitabu hiki juu ya Hema Takatifu la Kukutania, jambo gumu sana kwangu lilikuwa ni kujaribu kuishughulikia misamiati yake. Nimetumia kiwango kikubwa cha uangalifu katika jambo hili, hali nikiangalia maandiko ya asili, ili kuhakikisha kuwa ufafanuzi na tafsiri yake vinavyohusiana na Hema Takatifu la Kukutania havitaleteleza katika kutoa ujumbe potofu au hali ya kupokea ujumbe uliopotoshwa kwa wasomaji. Pamoja na ufahamu wangu wa Hema Takatifu la Kukutania, kwa sababu ya mitindo katika Hema Takatifu la Kukutania na maana yake ya kiroho iliyofichika basi inahitajika kuelezewa vizuri kwa wale ambao ufahamu wao ni mdogo, kwa kiwango fulani nilikuwa ninafikiria sana kuhusiana na jukumu hili, sikuwa na hakika jinsi ambavyo ninaweza kuelezea kwa usahihi na kwa uhakika kuhusu umuhimu wa Hema Takatifu la Kukutania.
Kwa kweli itakuwa vizuri ikiwa watu wataelewa na kuamini mara watakapousikia ujumbe wa kweli. Lakini mji wa Roma haukujengwa kwa siku moja; vivyo hivyo, na kama ilivyo kwa mambo mengine yote, kuueneza ukweli na imani ya kweli hakuwezi kukamilishwa kwa siku moja, bali kutakamilika kwa hatua kadri tunavyozidi kuchimba ndani ya kiini cha ukweli kidogo kidogo. Kwa hiyo kama ningalivutwa zaidi kuanza kuchimba kwa kina tangu mwanzoni, basi bila shaka si kila mmoja angeweze kuelewa, hali hii ilikuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa nilizozipata nilipokuwa ninaandika kitabu hiki.
Hata hivyo, kwa msaada wa Mungu, hatimaye kitabu hiki kimetoka pasipo kuwa na matatizo mengi. Sihitaji kusema sana, kwa kweli nina furaha na ninamshukuru Mungu kwa kitabu hiki. Kwa kupitia kitabu hiki, na kwa kuutambua ukweli baina ya uongo, nitaufunua jinsi ambavyo ni wa thamani, kwa waamini wa leo wa injili ya maji na Roho jinsi ambavyo wameokolewa, na pia nitaonyesha kinyume chake yaani jinsi ambavyo dini inawapofusha waamini wa injili nyingine ambayo si injili hii ya maji na Roho. Kwa hiyo, zaidi ya yote ninamshukuru Mungu kwa kuniokoa toka katika dhambi zangu.
Siku hizi, kuna watu wengi wanaojiita wainjili, ambao wanakubali pasipo utaratibu kuwa hawana dhambi ati kwa sababu tu wanamwamini Yesu. Mioyo yao imejawa na imani potofu zenye msingi mbaya. Tunapojifunza juu ya Hema Takatifu la Kukutania, ndipo nimeweza kutambua kwa wazi jinsi ambavyo imani yao ni ya uongo na isiyo na kitu, na kwa sababu ya kutambua hivi, basi ninamshukuru Mungu zaidi kwa moyo wangu wote kwa wokovu wangu.
 

Lango na Uzio wa Ua wa Hema Takatifu la Kukutania
 
Nguzo za ua wa Hema
Toka katika kifungu kikuu cha maandiko katika mada hii, tunaweza kuona ukweli kuwa urefu wa ua wa mstatiri wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni mita 45 na upana wake ulikuwa mita 22.5 (futi 75), kwa kuwa dhiraa ni kipimo cha urefu ambacho ni sawa na mita 0.45 (futi 1.5); kwamba ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulizungukwa kwa nguzo 60 katika pande zote, kimo cha nguzo kilikuwa mita 2.25 (futi 7.5); kwamba katika upande wake wa mashariki kulikuwa na lango, lililokuwa na upana wa mita 9; na kwamba maeneo mengine ya uzio yaliyobakia (kiasi cha mita 126 (yadi 115) kati ya mita 135 (yadi 123) ulizungukwa kwa mapazia ya kitani safi nyeupe.
Lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na lilikuwa na upana wa mita 9 na urefu wa mita 2.25 (futi 7.5) kwa kimo. Kwa maneno mengine, aina hizi nne tofauti za nyuzi zilifumwa kutengeneza kisitiri chenye vipimo vya mita 9 (futi 30) kwa mita 2.25 (futi 7.5). Nyuzi za bluu zilifumwa kwanza katika urefu na upana kamili katika kitani safi ya kusokotwa, na kisha nyuzi za zambarau zilifumwa kwa kimo cha mita 2.25, na kisha nyuzi nyekundu zilifumwa kwa kimo cha mita 2.25 (futi 7.5), zikafuatiwa na kufumwa kwa nyuzi nyeupe, ili kufanya kisitiri kinene na chenye nguvu, kilichosokotwa kama zulia, hicho kilikuwa na kimo cha mita 2.25 (futi 7.5). Kwa njia hii, kisitiri kilichosokotwa chenye vipimo vya mita 2.25 (futi 7.5) kwa kimo na mita 9 (futi 30) kwa upana, ambacho kiliwekwa katika nguzo nne za ua wa Hema Takatifu la Kukutania katika upande wake wa mashariki.
Kwa hiyo, ili kuingia katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania, watu walitakiwa kulivuta zulia kama kisitiri kwa kuinuka. Kinyume na malango mengine, lango la Hema Takatifu la Kukutania halikuwa la mbao. Ingawa nguzo zake ziliundwa kwa mbao, lango ambalo lilining’inizwa katika nguzo hizi lilikuwa ni kisitiri kilichofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Bila shaka umekwenda katika maonyesho ya sakarakasi hapo kabla, na bila shaka umeona jinsi ambavyo hema la sarakasi linavyojengwa. Kwa kawaida mlango wake umetengenezwa kwa vitambaa vinene. Lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulifanana kidogo na mlango huu wa hema la sarakasi. Kwa kuwa ilitengenezwa kwa vitambaa vinene, haukufunguliwa kwa kufungua au kusukuma kama ilivyo kwa milango migumu, bali ili kuingia mlango ulivutwa tu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania na pia kwa malango ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu ndani ya Hema Takatifu la Kukutania.
Kwa nini Mungu aliwaeleza waisraeli kutengeneza malango yote matatu ya ua wa Hema Takatifu la Kukutania, Mahali Patakatifu, na Patakatifu pa Patakatifu kwa kuyafuma kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa? Ni lazima tuchunguze vizuri kuwa kwa nini Mungu aliagiza amri hii ili tuweze kufahamu mapenzi yake kwa agizo hili. Kitabu cha Waebrania kinatueleza sisi kuwa mambo yote mazuri ya Agano la Kale yalikuwa ni kivuli-tangulizi cha yale mambo halisi yatakayokuja, ambayo ni Yesu Kristo (Waebrania 10:1).
Vivyo hivyo, lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania linafanana kiutatanishi na ubatizo wa Yesu Kristo, kifo chake Msalabani, na utambulisho wake binafsi. Kwa hiyo, pale tunapokuwa na shinda ya kulifahamu Agano la Kale, tunaweza kuufikia ufahamu huu kwa kuliangalia Agano Jipya. Bila kukiona kitu halisi, ni vigumu sana kufikiria juu ya kivuli chake, lakini tunapoona kuwa ni kitu gani au ni nani anayetoa kivuli, ndipo tunapoweza kutambua suala zima kwa uwazi. Ni lazima sisi sote tutambue kwa wazi kuwa yupi ni mwokozi wa wenye dhambi ambaye Mungu amemwandaa toka katika Agano la Kale, tumfahamu yeye kuwa ndiye kiini halisi cha Hema Takatifu la Kukutania, na kisha tuamini kuwa kazi zake zimetuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote.
Je, ni nani hasa ambaye ndiye kiini cha Hema Takatifu la Kukutania, je, ni yeye aliyefanyika Mwokozi wa wenye dhambi? Si mwingine bali ni Yesu Kristo. Tunapochunguza jinsi ambavyo Yesu Kristo, Mwokozi wetu, alivyokuja hapa duniani na jinsi alivyotuokoa toka katika dhambi zetu, basi ndipo tunapoweza kuuona ukweli kwamba ametuokoa sisi wenye dhambi kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Kuufahamu na kuuamini ukweli uliodhihirishwa katika rangi za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutani ni muhimu sana katika kuufahamu wokovu wa Yesu kwa wenye dhambi. Tunapolichunguza Hema Takatifu la Kukutania, kitu cha kwanza ambacho ni lazima tukitambue ni kuwa lango la ua liliundwa kwa nyuzi nne. Na tunapolitatua fumbo la lango hili, basi ndipo tunapoweza kuja kupata ufahamu imara wa kazi zote za Yesu Kristo. Kwa kuliangalia lango la kisitiri lililofumwa kwa nyuzi hizi nne, ndipo tunapoweza kufahamu kwa wazi jinsi ambavyo inavyotupasa kumfahamu na kumwamini Yesu, pia tutaweza kufahamu juu ya imani ya kweli na imani ya uongo.
Ua wa nje wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kweli unatukumbusha juu ya zizi la kondoo. Yesu, Masihi wetu, ndiye mlango wa zizi la Mungu, na pia amefanyika kuwa Mchungaji mwema (Yohana 10:1-15). Tunapozifikiria zile nguzo zilizouzunguka ua, kwa hakika tunakumbushwa juu ya Masihi, ambaye amefanyika kuwa mlango na Mchungaji mwema wa kondoo zake, ambao ni watakatifu waliozaliwa upya.
Kwa kweli Mchungaji ameweka nguzo kulizunguka zizi ili kuwalinda kondoo wake na ameufanya mlango pale, na kwa kupitia mlango huu, anawaelekeza kondoo wake. Kwa kupitia mlango huu Mchungaji ana uhusiano wa karibu na kondoo zake na anawalinda kondoo. Kusema kweli, wale wote ambao si kondoo wake hawaruhusiwi kuingia kwa kupitia mlango huu. Mchungaji anaweza kutofautisha kati ya kondoo na mbwa mwitu. Hii ndiyo sababu kondoo wanahitaji Mchungaji.
Lakini inawezekana kuwa kuna baadhi kati ya hawa kondoo ambao wanakataa kuongozwa na Mchungaji. Kondoo wa jinsi hiyo wanaweza kuingia katika njia ya kifo, wakidhani kuwa ni njia nzuri na ya kupendeza ilhali njia hiyo ni ya uhaini na ya hatari, kwa kuwa hawajaisikiliza sauti ya Mchungaji na wakakataa kuongozwa naye. Kondoo hawa wanaweza wakaruhusiwa kuishi na wakaendelea kulishwa na Mchungaji, na wanaweza wakaendelea kuishi vizuri kwa sababu ya Mchungaji. Kwa kweli, Mchungaji wetu, ni Yesu Kristo, ambaye amefanyika kuwa Masihi wetu.
 
 
Yesu Kristo Alituonyesha Sisi Rangi Nne za Lango la Hema Takatifu la Kukutania
 
Kisitiri ambacho kiliwekwa kama lango la Hema Takatifu la Kukutania kilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Nyuzi hizi za rangi nne tofauti zilitumika kutengeneza lango la Hema Takatifu la Kukutania. Zilionyesha huduma nne ambazo Masihi, kwa kuja hapa duniani, alizitimiza ili kuwaokoa kondoo waliokuwa wamepotea—ambao ni waisraeli wa kiroho ulimwenguni kote—toka katika dhambi zao ili kuwageuza kuwa watu wa Mungu wasio na dhambi.
Ikiwa kweli tutamtambua Masihi wetu aliyekuja kwetu kwa huduma zake nne, basi, tumeoshwa dhambi zetu zote kwa imani hii, tumeyatoa maisha yetu yaliyosalia kwa kuihubiri injili ya maji na Roho, na tutaingia mbinguni kwa kupitia imani hii. Hivyo, kwa kweli kila mtu ni lazima alifahamu Neno la kweli kuwa Masihi amekuja kwetu kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na ametuokoa toka katika dhambi zetu zote.
Je, unapenda kupokea ondoleo la dhambi zako kwa kuziamini huduma nne za Masihi? Basi, hebu tujifunze kuhusu Hema Takatifu la Kukutania. Wale ambao wanazifahamu huduma hizi nne kwa hakika watafanyika wenye haki kwa kupokea ondoleo la dhambi lililofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Watu wa Israeli walipoliangalia lango la Hema Takatifu la Kukutania lililofumwa kwa nyuzi za rangi nne tofauti, waliamini kuwa kwa hakika Masihi atakuja baadaye ili kuzitimiza huduma hizi nne.
 

Ukweli Ambao Kila Mwenye Dhambi ni Lazima Auamini
 
Ikiwa tungeyaangalia mapazia ya kitani safi ya ua wa Hema Takatifu la Kukutania, tungetambua uhitaji wetu wa kuwa na Mwokozi kwa kutambua jinsi ambavyo Mungu ni mtakatifu. Kwa kweli kila mtu anayekuja kuufahamu utakatifu wa Mungu, hakuweza kufanya lolote zaidi ya kukiri kuwa, “Mungu, ninatambua kuwa nimefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zangu, kwa kuwa mimi ni umati wa dhambi.” Tukiziangalia kitani nyeupe zikiwa zimezifunika nguzo za ua, na kwa sababu ya usafi wake na utukufu itaonekana vizuri sana, watu watakuwa walizitambua dhambi zilizopatikana katika mioyo yao na wakatambua kuwa hawafai kabisa kuishi na Mungu. Inapotokea kuwa wale ambao mioyo yao haiko safi wanapojaribu kwenda mbele za Mungu, kwa kawaida dhambi zao zinafunuliwa. Kwa hiyo, watu wanakataa kwenda mbele za Mungu, kwa kuwa wanaogopa kuwa dhambi zao zitafunuliwa.
Lakini watu wa jinsi hiyo wenye dhambi wanapotambua kuwa Mwokozi wao ametatua tatizo lao la dhambi kwa nyuzi za bluu na nyekundu, ndipo wanapoweza kwenda mbele za Mungu kwa ujasiri kwa uhakika wa wokovu katika mioyo yao.
Ukweli wa aina nne unaoonekana katika lango la Hema Takatifu la Kukutania unatueleza sisi kuwa Masihi alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana, na akaimwaga damu yake Msalabani. Wale ambao kwa kupitia injili ya maji na Roho wanafahamu na kuamini katika ukweli wa rangi nne za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania basi wanaweza kupokea ondoleo la dhambi la milele. Ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake, ukweli kuwa Kristo alituokoa kikamilifu toka katika dhambi zetu kwa ubatizo wake na kwa damu yake Msalabani, ni wokovu kama zilivyo rangi nne za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kwa kweli zinatuonyesha juu ya huduma ya Masihi iliyowaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao zote. Ukweli wa wokovu ambao Mungu amewapatia wanadamu umefunuliwa katika nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Kwa kweli wale ambao wana dhambi katika mioyo yao, wamesamehewa dhambi zao zote kwa kuuamini ukweli wa wokovu uliofunuliwa katika injili ya maji na Roho.
Dini nyingi zimezuka hapa ulimwenguni. Dini hizi zote za kidunia zimekuja na mafundisho yao yaliyoundwa kwa mawazo ya binadamu, wakijaribu kuwafanya watu kuufikia utakatifu. Lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kuoshwa dhambi zake kwa kupitia dini hizi za kidunia. Hii ni kwasababu dini hizi zinaamini katika mafundisho yao ya wokovu yanayotokana na mawazo yao binafsi bila kutambua kuwa wamejazwa na dhambi. Kwa sababu kila mmoja ni lundo la dhambi, hivyo mtu hawezi kuwa mtakatifu kwa kuitegemea haki yake binafsi, haijalishi ni kwa kiwango gani mtu anafanya jitihada ili kujitoa katika msingi wa asili wa dhambi, hakuna hata mmoja anayeweza kufanikiwa katika hili. Hii ndio maana kila mmoja kwa hakika anamhitaji Mwokozi ambaye atamwokoa toka katika dhambi—na hii ni kusema kuwa, kila mmoja anamhitaji Yesu. Ni lazima utambue kuwa wanadamu hawana Mwokozi wa kweli zaidi ya Yesu Kristo.
Kwa sababu Sheria ya Mungu haiwaruhusu wenye dhambi kuingia katika nyumba ya Mungu, hivyo ni lazima tufahamu na tuamini kwamba kwa hakika Masihi ameziondoa na kuzifuta dhambi zetu zote.
Injili ambayo imezisamehe dhambi za mwanadamu mara moja na kwa wote si nyingine bali ni injili ya maji na Roho. Kuiweka imani ya mtu katika mafundisho ya dini za kidunia kutampeleka mtu wa jinsi hiyo katika shida kubwa hasa kuhusiana na masuala ya dhambi zake, kwa kuwa Mungu wetu Mtakatifu anakemea na kuadhibu kila kosa la wenye dhambi pasipo kushindwa.
Ukweli uliofunuliwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ulitimizwa kwa injili ya maji na Roho katika kipindi cha Agano Jipya. Je, umewahi kumsikia mtu akidai kuwa lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa nyuzi nyekundu tu au kwa nyuzi za zambarau na nyekundu tu? Kama ndivyo, ni lazima utambue sasa kuanzia sasa kuwa, kwa hakika lango la Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Mungu aliwaamuru waisraeli kulifanya lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kisitiri kilichofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizofanywa na fundi mshona taraza.
Hata hivyo, kwa sababu watu wengi wamefikiria kimakosa kuwa lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi nyekundu tu, hivyo wameshindwa kulitatua fumbo la huduma nne za Bwana wetu. Hii ndio sababu wana dhambi katika mioyo yao hata pale wanapomwamini Yesu. Tambua sasa kuwa Kristo aliziondoa dhambi zako zote kwa kupitia huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kisha uuamini ukweli huu. Kazi ya wokovu iliyotimizwa kwa nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa kwa hakika zimekuokoa toka katika dhambi zako zote. Ni lazima utambue kuwa Yesu alizichukua dhambi zako zote kwa huduma hizi nne. Kwa maneno mengine, kujiwekea viwango vyako binafsi vya ondoleo la dhambi hali ukibaki bila kuufahamu ukweli huu kwa hakika ni makosa.
Baadhi ya watu, hata pale wanapokuwa hawatambui juu ya maana ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, wanaendelea kudai kimakosa kuwa mtu anaweza kuokolewa bila masharti kwa kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi. Kwa kweli, tunapowauliza viongozi wa jumuia za Kikristo juu ya huduma nne za Yesu, ndipo tunapotambua kuwa wengi wao hawazifahamu huduma hizo. Wanasema kuwa wanaiamini huduma ya nyuzi nyekundu tu. Ikiwa wanaamini zaidi ya huduma moja, basi wanaweza kusema kuwa wanaiamini pia huduma ya nyuzi za zambarau. Hata hivyo, kwa kweli Bwana wetu aliyatimiza majukumu yote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa hiyo, ni lazima tuamini kwamba Bwana wetu alizichukua kwa ajili yetu huduma zake nne za wokovu. Yeyote aliye na moyo unaotamani kuufahamu ukweli uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa za lango la Hema Takatifu la Kukutania kwa kweli anaweza kuufahamu na kuuamini ukweli huo.
“Je, ninawezaje kuifahamu maana ya kweli ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa?” Ikiwa ungemuuliza swali hili mtu fulani katika hali ya kuutafuta ukweli wa nyuzi hizi na kitani, bila shaka unaweza kukemewa, “Ni lazima usijaribu kuifahamu Biblia kwa undani sana; inaweza kukuletea madhara,” na kwa hiyo udadisi wako unaweza kudharauliwa. Hali wakiwa wamevunjwa moyo, watu wengi wanapoteza ule udadisi wao kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Na kwa hiyo huwezi kukutana na Masihi kamwe ambaye amefunuliwa kwa uwazi na undani kupitia lango.
Kusema kweli, wale wanaojaribu kuonana na Masihi pasipo kutambua wajibu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, ni watu wa dini tu ambao wanauamini Ukristo kama moja ya dini za ulimwengu huu. Ili kuingia katika Nyumba ya Mungu, ni lazima tuufahamu kikamilifu ukweli wa huduma nne za wokovu wa Mungu zilizofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Na wale walioupata ukweli huu ni lazima watambue kuwa Bwana alizitimiza huduma hizo kwa injili ya maji na Roho katika kipindi cha Agano Jipya.
Mungu alimwamuru Musa kulisokota lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Je, nini maana ya kiroho kwa jambo hili? Kila rangi ya bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa iliyotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania ni kazi ya Yesu aliyoifanya ili kuzifanya dhambi zetu kutoweshwa. Nyuzi hizi na kitani kwa kweli zinahusiana. Kwa hiyo, wale wanaoweka umakini wao katika kuiamini injili ya maji na Roho wanaweza kuamini juu ya ondoleo lao la dhambi la milele kuwa ni huduma nne za Yesu.
Pamoja na hayo, kutojaribu kuufahamu ukweli na kuudharau ukweli wa wokovu uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyekundu, ni ufafanuzi wa wazi juu ya utofauti alionao mtu fulani kwa Masihi na hiyo ni sawa na kuwa adui aliye kinyume na Masihi. Kwa kweli, watu wengi wanabaki kuwa kinyume na ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na kwa hiyo wanaugeuza Ukristo kuwa ni moja ya dini za kidunia tu. Ikiwa watu hawa wanazichukulia huduma nne za Yesu kitofauti, basi huu ni uthibitisho kwamba wao ni matunda ya wanadini wa kidunia wanaosimama kinyume na Kristo. Hata hivyo, kwa bahati, bado kuna tumaini kwetu, kwa kuwa katika ulimwengu huu watu wengi bado wanaitafuta injili ya maji na Roho.
Wakati watu wana ufahamu wa kiroho wa kweli wa ondoleo la dhambi unaofunuliwa na lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, basi ndipo wanapoweza kupokea baraka zote za kiroho za mbinguni. Kwa sababu imani hii ndio imani hasa inayotakiwa na ambayo mtu anatakiwa kuifahamu na kuiamini ili aweze kuonana na Masihi, hivyo ni lazima tukae katika imani hii daima. Ikiwa kweli wewe ni Mkristo, ni lazima uuzingatie ukweli huu.
Yeyote anayetaka kuingia katika nyumba ya Mungu ni lazima autambue ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na amsifu Mungu kwa jambo hilo.
 

Masihi Aliyekuja Kama Mtimizaji wa Unabii
 
Mungu alitabiri kwa Neno lake kwamba Masihi atazaliwa kupitia mwili wa bikira. Isaya 7:14 inasema, “Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Immanueli.” Kwa upande mwingine, Mika 5:2 inaeleza kuwa Masihi atazaliwa katika Bethlehemu: “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; Kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; Ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Kwa kweli Masihi alikuja hapa duniani kikamilifu kama ilivyotabiriwa kwa Neno hili la Agano la Kale. Alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu kama kuutimiza unabii kwa mujibu wa Neno la Mungu. 
Je, ni wakati gani katika historia ya mwanadamu ambapo Masihi alikuja? Je, ni lini ambapo Yesu Kristo alikuja hapa duniani? Yesu alikuja hapa duniani katika kipindi cha utawala kwa Kaisari Agusto wa dola ya Warumi (27 K.K – 14 B.K). Yesu alikuja hapa duniani kutukomboa wewe na mimi toka katika dhambi zetu zote na adhabu kwa kuupokea ubatizo toka kwa Yohana na kwa kusulubiwa na kumwaga damu Msalabani.
Yesu alikuja kama ni Mwokozi wa wanadamu katika kipindi ambacho Israeli ilikuwa imegeuzwa kuwa koloni la Dola ya Rumi na katika kipindi ambacho Agusto alikuwa akitawala kama Kaisari. Kwa sababu Israeli lilikuwa ni koloni la Warumi, lilikuwa likifuata amri za Rumi. Katika kipindi hiki, Kaisari Agusto alimwamuru kila mmoja katika dola yote ya Warumi kurudi katika mji wake ili apate kujiandikisha katika sensa ya watu. Kufuatia amri ya Agusto, sensa hii ilianza mara moja. Kwa sababu sensa ililenga kupata habari za kila mtu aliyeishi katika dola hiyo, wakiwamo wale walioishi Israeli, basi waisraeli wote iliwapasa kurudi katika miji yao ya asili. Tangu kipindi hiki, Yesu Kristo alikuwa tayari anafanya kazi katika historia ya mwanadamu.
 

Tazama Juu ya Kutimia Kwa Neno la Agano la Kale!
 
Katika kipindi hicho, katika nchi ya Yuda, Masihi alikuwa amekwisha chukuliwa mimba katika tumbo la Bikira Maria. Huyu Maria alikuwa amechumbiwa na Yusufu. Maria na Yusufu wote walikuwa wanatoka katika kabila la Yuda, kama ambavyo Mungu aliahidi kwamba kati ya makabila kumi na mbili ya Israeli, wafalme wataendelea kuzaliwa katika kabila la Yuda.
Kwa hiyo wakati Kaisari Agusto alipotoa amri ya sensa kufanyika, Maria wa kabila la Yuda alikuwa tayari amembeba mtoto katika tumbo lake. Wakati muda wake ulipowadia na alipokuwa karibu kuzaa, kwa sababu ya amri ya Kaisari, alitakiwa kwenda katika mji wa asili wa Yusufu ili akajiandikishe katika sensa. Kwa hiyo, Maria akaenda Bethlehemu akiwa na Yusufu pamoja na kuwa alikuwa akitegemea kuzaa wakati wowote. Wakati Maria alipopata uchungu wa kuzaa, walihitaji kutafuta chumba kwa ajili yake, lakini hawakuweza kupata chumba chochote mjini. Hivyo iliwalazimu kutumia mahali popote palipopatikana kwa ajili yao, pamoja na kuwa waliishia katika hori la ng’ombe. Na Maria akamzaa mwanawe Yesu katika hori la ng’ombe.
Katika mwaka 1 B.K, Yesu alizaliwa na akawekwa katika zizi la kulishia ng’ombe. Mungu Mwenyezi alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu. Mwokozi wa wanadamu alikuja mahali ambapo wakati fulani wanyama walikuwa wakiishi. Hii inamaanisha kuwa Yesu alizaliwa katika mahali hapa pa chini ili kuwa Masihi wetu, na mambo haya yote yaliandaliwa na kupangwa na Mungu hata kabla ya uumbaji. Ingawa watu huenda walifahamu kuwa Mungu Yahwe anaiongoza historia ya mwanadamu, hakuna aliyeweza kutambua kuwa Mungu mwenyewe atakuja hapa duniani ili kuwaokoa. Kwa hiyo, Mungu, alifanya iwezekane kwa kila mtu kutambua kuwa atamwokoa kwa kujishusha yeye mwenyewe na kuzaliwa hapa duniani katika mwili mnyenyekevu wa mwanadamu ili kuwakomboa wanadamu wote toka katika dhambi zao.
Kwa nini basi, Yesu alizaliwa Bethlehemu? Pia tunaweza kushangaa kuwa ni kwa nini alizaliwa katika hori la kulishia ng’ombe, na kwa nini alizaliwa katika kipindi ambacho waisraeli walikuwa chini ya ukoloni wa Warumi? Lakini tutatambua mara kuwa mambo haya yote yalikuja kwa mpango wa Mungu uliopangwa kwa uangalifu ili kuwakomboa watu wake toka katika dhambi zao.
Wakati Yusufu na Maria walipojiandikisha kwa ajili ya sensa katika mji wao wa asili, iliwapasa kutoa ushahidi unaothibitisha kuwa wanatoka katika mji huu, na wakatoa vitambulisho vyao sahihi. Waliweza kusajiriwa kwenye sensa pale walipoweza kutoa vithibitisho muhimu ili kuthibitisha kuwa wazazi wao waliishi Bethlehemu kwa vizazi. Hivyo walipaswa kutaja mababu zao waliopita na kuwa walitoka katika nyumba gani na waliandika habari zao zote za kiukoo katika sensa. Kwa kuwa hakuna kati ya historia hii iliyoondolewa na kwa sababu historia ilirekodi vizuri utambulisho wa Yusufu na Maria, Mungu alihakikisha kuwa historia ya mwanadamu itathibitisha juu ya kuzaliwa kwa Yesu (Mathayo 1:1-16, Luka 3:23-38). Haya yote yalikuwa ni kazi za Mungu alizozifanya ili kuutimiza unabii wa Neno la Agano la Kale.
Mika 5:2 inasema, “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; Kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; Ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Kwamba siku ya kuzaliwa ilifika na Mwokozi alizaliwa katika mji uliotabiriwa wa Bethlehemu kwa kumfanya Yusufu na Maria kufika katika huo mji kunamaanisha kuwa Mungu aliifanya kazi hii ili kuutimiza unabii wa manabii wake. Kwa hakika Mungu alipanga mafanikio ili kuziondosha mbali zambi zote za mwanadamu. Kwa Yesu atazaliwa katika mji mdogo wa Bethlehemu kulikuwa ni kutimiza Neno la unabii la Agano la Kale.
Mamia ya miaka kabla Yesu Kristo hajazaliwa katika mji mdogo wa Bethelehemu, Mungu alikuwa ameshalitoa Neno lake la unabii kupitia kwa nabii wake Mika kama ilivyonukuliwa hapo juu (Mika 5:2). Pia, nabii Isaya alikuwa ametabiri takribani miaka 700 kabla ya kuja kwa Bwana wetu jinsi ambavyo Masihi atakavyokuja kwa watu wake ili kuwa Mwokozi wa wenye dhambi (Isaya 53). Kama ambavyo Yesu Kristo alizaliwa Bethlehemu kwa usahihi kama Mungu alivyotabiri kupitia Nabii Mika, kwa kawaida alitimiza Neno lake lote la unabii.
Unabii huu ulitimizwa kama ukweli wa kihistoria wakati ule Maria na Yusufu walipokwenda katika mji wa baba zao kujisajili kwa ajili ya sensa. Mungu alilitimiza Neno lake kwa kuhakikisha kuwa wakati wa mtoto kuzaliwa utafikia wakati ambapo Maria atafika Bethlehemu, ili kwamba asiwe na chaguo zaidi ya kuzaa katika mji huu.
Hapa tunatambua kuwa Mungu wetu ni Mungu anayeliongea Neno lake la unabii kwetu na analitimiza Neno hilo kama alivyopanga. Kutoka katika hili, tunawe kuona kuwa “kitani safi ya kusokotwa” iliyotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania inamaanisha kuwa ni usahihi na ukamilifu wa Neno la Mungu. Mungu alipanga kwa uangalifu wokovu wa mwanadamu hata kabla ya uumbaji, na ameyatimiza haya bila kushindwa kulingana na Neno lake la unabii. 
Kwa hiyo, tunaweza kutambua kwamba Neno la Agano la Kale kwa hakika ni Neno la Mungu, na kwamba Neno la Agano Jipya pia ni Neno la Mungu. Pia tunaweza kutambua na kuamini kwamba kwa hakika Mungu anaitawala historia nzima ya ulimwengu na dunia hii. Kwa maneno mengine, tunaweza kufahamu kuwa kama vile Mungu alivyouumba ulimwengu mzima, ametuonyesha sisi kuwa anawatawala watu wote, historia zote, na kila hali ya mtu kwa upana. Kwa hiyo, Mungu anatuonyesha sisi kuwa hakuna kinachoweza kufanyika kwa mapenzi ya mtu binafsi bila kujali jinsi kilivyo, labda yeye Mungu awe amekiruhusu.
Wakati mtoto Yesu alipozaliwa na kuja hapa duniani, hakujiweza zaidi ya kuzaliwa katika mahali pa kulishia wanyama, kwa kuwa hakukuwa na nafasi katika nyumba za wageni. Kwa kweli yeye mwenyewe alizaliwa katika mji wa Bethlehemu. Ni lazima tutambue kuwa haya yote yalikuwa ni mafanikio makubwa ya unabii wa Mungu kulingana na uaminifu wake.
Kwa hiyo, ni lazima tuamini kwamba yule anayeitawala historia ya ulimwengu ni Mungu wetu, Mwokozi aliyetuokomboa toka katika dhambi zetu. Ukweli huu ni Neno la Mungu ambalo linatuonyesha kwamba Mungu anatawala juu ya yote, kwa kuwa Mungu ni Bwana wa wote.
Kwa sasa imethibitika kuwa kuzaliwa kwa Yesu katika mji mdogo wa Bethlehemu halikuwa ni jambo la kubahatisha, wala hakikuwa ni kitu kilichoundwa kimakosa ili kulitawala kimakosa Neno la Biblia. Hivi ndivyo ambavyo Mungu mwenyewe alisema, na ndivyo ambavyo Mungu mwenyewe alilitimiza kupitia Yesu. 
Ni lazima tulifahamu na kuliamini jambo hili. Ni lazima tulibebe katika mioyo yetu na kuamini kuwa wokovu wa Masihi wetu ni ukweli uliotimizwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Mungu ametuonyesha sisi ondoleo la dhambi, jambo hili pia si kitu kilichofanyika kwa bahati, bali kimefanyika kwa kupitia huduma nne za Yesu zilizoandaliwa kwa majaliwa ya Mungu.
Kwa nyongeza hii inatuonyesha kuwa Ukristo si moja ya dini za kidunia. Mwanzilishi wa dini ya kidunia kwa kawaida ni mtu anayeharibika na kufa, lakini mwanzilishi wa Ukristo ni Mwokozi wetu Yesu, na Mungu ametuonyesha sisi kuwa ukweli wa Ukristo unaanzia katika ukweli kuwa huyu Mwokozi wetu ni Mungu mwenyewe. Kwa maneno mengine, Mungu anatushuhudia sisi kwamba Ukristo tunaouamini kwa kweli si dini ya kidunia. Tofauti na dini nyingine za kidunia, Ukristo umeanzishwa kwa neema yote iliyotolewa na Mungu. Kama ilivyoandikwa katika Warumi 11:36, “Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina,” Mungu alitupatia Mwana wake pekee kuwa Mwokozi wetu, injili ya maji na Roho kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, uwepo wa Roho Mtakatifu, na Ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo, ni lazima sisi sote tufahamu na kuamini katika mioyo yetu kwamba ni lazima tumheshimu na kumwogopa Mungu na Neno lake kwa mioyo yetu yote.
Kuzaliwa kwa Masihi katika dunia hii kulikuwa ni kwa mujibu wa mpango wa wokovu ulioazimiwa na Mungu Baba hata kabla ya uumbaji. Wokovu wetu umepangwa kwa uangalifu na uzuri. Mungu ameturuhusu kutambua kwa wazi kuwa ukweli huu ni kiini halisi cha nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa hiyo, ni lazima tuutambue wokovu ambao umekuja kwetu kupitia injili ya maji na Roho kama ondoleo la dhambi zetu na kuamini hivyo. Ni kwa kupitia imani hii kwamba wewe na mimi tumeweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote. Ni lazima tuamini kwamba ukweli huu wa rangi nne, pia unafanywa kuwa kamili kwa imani yetu katika Neno la injili ya maji na Roho.
 


Yesu Kristo, Mwokozi Aliyetuokoa Sisi Kwa Nyuzi Zake za Bluu, Zambarau, na Nyekundu na Kitani Safi ya Kusokotwa

 
Kazi ambazo kwa hizo Yesu Kristo amewaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao zipo katika namna nne: nyuzi za bluu (Ubatizo wa Yesu); nyuzi za zambarau (Yesu ni Mfalme wa wafalme—kwa maneno mengine ni Mungu mwenyewe); nyuzi nyekundu (damu ya Yesu); na kitani safi ya kusokotwa (utimilifu wa wokovu wa wenye dhambi wote toka katika dhambi zao kupitia Neno la Mungu la Agano Jipya na Agano la Kale). Yesu amefanyika kwa hakika kuwa Mwokozi kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa.
Ni lazima tutambue kuwa ni mpaka pale tutakapoamini kuwa Yesu aliyekuja kwetu kwa kupitia maji na Roho ametuokoa toka katika dhambi zetu kwa nyuzi za bluu (ubatizo wa Yesu), nyuzi za zambarau (Yesu ni Mungu), Nyuzi nyekundu (damu ya Yesu), na kitani safi ya kusokotwa (Yesu aliyekamilisha wokovu kwa Neno la Agano la Kale na Agano Jipya), ndipo tunapoweza kukombolewa toka katika dhambi zetu na adhabu ya dhambi hizi. Kwa hiyo pasipo kutuokoa toka katika dhambi zetu na adhabu, Bwana wetu asingelifanyika Mwokozi mkamilifu.
Ni lazima tutambue kiroho sababu iliyofanya pazia la lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kufumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilitengenezwa kwa nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ili kwamba kila mtu aweze kulitambua lango na kulipata kiurahisi. Kwa kupitia lango hili, Mungu alimruhusu kila mtu kuingia katika nyumba yake ya kung’aa.
Hema Takatifu la Kukutania ni nyumba inayong’aa ya Mungu. Hakuna hata mmoja aliyehitaji kuingia katika nyumba ya Mungu aliweza kufanya hivyo pasipo kuutambua ukweli wa wokovu uliodhihirishwa katika uzio na lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Mungu alisema kuwa wale ambao wanaudharau utakatifu wa pazia la kitani nyeupe iliyoifunika Hema Takatifu la Kukutania hawaingii katika Hema Takatifu la Kukutania kwa kupitia mlango, bali wanaparamia njia nyingine, na hao wote ni wezi na wanyang’anyi. Lango la wokovu linamaanisha Yesu Kristo (Yohana 10).
Biblia inaposema kuwa lango hili limefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, Mungu anatuonyesha wazi kupitia Neno lake la kweli la Agano la Kale na Agano Jipya, kuwa Yesu Kristo alikuja hapa duniani kama Mwana wa Mungu, alibatizwa na Yohana, alikufa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Masihi wetu. Kwa hiyo tunaweza kulifahamu fumbo la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni lazima tuamini kuwa Mungu ameturuhusu kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu aliyekuja kutuokoa katika hukumu ya dhambi za ulimwengu huu, na kwamba yeye ni Mwokozi ambaye ameutimiza wokovu wa mwanadamu kupitia Neno la Agano la Kale na Agano Jipya.
Ni lazima tuweze kutambua kwa hakika kuwa ni kwa nini lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Je, nyuzi za bluu zinatueleza nini? Je, nyuzi za zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa vinatueleza nini? Tunapoutambua mpango wa Mungu, ndipo tutatambua kuwa kazi ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni mpango wa Mungu wa wokovu kwetu na ukweli wa uzima wa milelele, na kwamba tunaweza kuingia katika Ufalme wake kwa kupitia imani yetu ya ondoleo la dhambi.
Tunaposema kuwa tunazifahamu na tunaziamini nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, ina maanisha kuwa tunatambua vizuri sababu iliyomfanya Yesu akabatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake Msalabani, ambaye ni Masihi, ambaye ni mafumbo yote ya utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa wa Agano la Kale, na injili ya maji na Roho ya Agano Jipya.
Inaweza kuonekana kuwa watu wengi wanaufahamu mzuri kuhusu Hema Takatifu la Kukutania, lakini kwa kweli hivi sivyo. Kwa kweli watu wengi hawajui maana ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizofumwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Kama ambavyo fumbo la nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni gumu kueleweka, watu wengi wana hamu ya kweli ya kujifunza na kuziamini hizo nyuzi. Hata hivyo, kwa sababu fumbo hili haliwezi kufahamika kwa kila mtu tu, watu wengi wameishia kulitafsiri fumbo hilo kimakosa wakijenga msingi katika maoni yao binafsi. Kwa kweli viongozi wengi wa kidini wameutafsiri vibaya na hawajauelewa ukweli huu katika njia ambazo walifikiri ndivyo, wameutumia ukweli huo kwa mambo yao ya kidini. Lakini Mungu hakuruhusu wakristo waendelee kudanganywa na waongo hawa. Hivyo aliamua kuelezea kwa wazi maana ya ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, na kwa hiyo amewaokoa toka katika dhambi zao zote.
Waraka wa 1 Yohana 5:6-8 toka katika Agano Jipya unasema, “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu; na watatu hawa ni umoja. Na kisha kuna watatu washuhudiao duniani: Roho, na Maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Kifungu hiki kinaeleza kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake, na akatuokoa kwa kuimwaga damu yake. Hii ndiyo sababu lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa lote kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Kwanza, nyuzi za bluu zinatuonyesha nini? Zinatuonyesha sisi sehemu ya ukweli kuhusu Yesu, ambaye alifanyika Masihi halisi wa wenye dhambi, alikuja hapa duniani na akazichukua dhambi za ulimwengu kwa kuupokea ubatizo wake toka kwa Yohana. Kwa kweli, ubatizo huu ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana katika Mto Yordani ni ukweli wa Yesu wa kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote. Kwa kweli Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu katika mabega yake kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, ambaye ni mwakilishi wa wanadamu wote. Kwa sababu dhambi zote za wanadamu zilipelekwa katika kichwa cha Kristo mwenyewe, wale wanaouamini ukweli huu hawana dhambi katika mioyo yao.
Pili, nini maana halisi ya nyuzi za zambarau zilizofumwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania? Zinatueleza kuwa Yesu ndiye Mfalme wa wafalme. Kwa kweli, Yesu, ndiye aliyeuumba ulimwengu, yeye ni muumbaji mwenyewe, na yeye si sehemu ya uumbaji, na pia ni Masihi halisi aliyekuja hapa duniani. Yeye, Masihi, alikuja hapa duniani katika mfano wa mwili wa mwanadamu. Na kubeba dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana, na kwa kifo chake cha kusulubiwa na kufufuka kwake, Yesu amewaokoa watu wake wote, ambao wametambua, wameogopa, na wamemwamini Masihi wao, toka katika dhambi zao zote na hukumu ya dhambi.
Kwa kweli Yesu ni Mungu wetu kamili na Masihi wetu kamili. Pia yeye ni Mwokozi wetu kamili. Kwa sababu Yesu alizichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake, kuimwaga damu na kufa Msalabani na kwa kufufuka toka kwa wafu, yeye Yesu hakuzisafisha dhambi zetu zote tu, bali alipokea hukumu ya haki kwa niaba yetu.
Tatu, nyuzi nyekundu zinaonyesha damu ambayo Yesu aliimwaga Msalabani, na maana yake ni kuwa Kristo ametupatia maisha mapya kwetu sisi tunaoamini. Ukweli huu wa nyuzi nyekundu unatueleza kuwa Yesu Kristo sio kwamba aliipokea hukumu ya dhambi zetu tu kwa kuzipokea dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana, bali pia alitoa maisha mapya kwa waamini kwa kuwapatia imani inayotoa maisha na uhai kwa wale ambao wamezifia dhambi. Kwa hakika Yesu amewapatia maisha mapya wale wanaouamini ubatizo wake na damu aliyoimwaga.
Je, kitani safi ya kusokotwa inamaanisha nini? Ina dhihirisha kuwa kwa kutumia Agano Jipya, Mungu aliitimiza ahadi yake ya wokovu iliyoandikwa katika Agano la Kale. Na inatueleza kuwa wakati Yesu alipozichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake na akahukumiwa kwa dhambi zetu Msalabani katika Agano la Jipya, aliutimiza wokovu ambao Mungu aliuahidi kwa waisraeli na kwetu kwa Neno lake la agano.
Mungu Yahwe alisema katika Isaya 1:18, “‘Haya, njooni, tusemezane, asema BWANA, ‘Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; Zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.’” Pia, utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa wa Agano la Kale ulioratibu jinsi ambavyo sadaka za kuteketezwa zilivyokuwa zikitolewa katika Hema Takatifu la Kukutania, ambao kwa huo dhambi za watu wa Israeli zilipelekwa kwa mwanakondoo wa sadaka kwa kuwekewa mikono kichwani, ni ahadi ambayo Mungu aliifanya kwa waisraeli na kwetu sisi. Huu ulikuwa ni ufunuo wa Mungu wa ahadi kwamba atawaokoa watu wote wa ulimwenguni toka katika dhambi zao za kila siku na za kila mwaka kwa kupitia Mwanakondoo wa Mungu hapo baadaye.
Hii ilikuwa pia ni ishara ya kuja kwa Masihi aliyeahidiwa. Kwa hiyo, katika kipindi cha Agano Jipya, wakati Yesu alipozichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kuupokea ubatizo wake kwa mujibu wa utaratibu wa Agano la Kale, hiyo ilikuwa ni kulitimiza agano la Mungu. Baada ya kutupatia sisi sote Neno lake la ahadi, Mungu ametuonyesha sisi kuwa kwa kweli amelitimiza Neno lake lote kwa usahihi kama alivyoahidi. Ubatizo ambao Yesu aliupokea unadhihirisha ukweli huu, kwamba Mungu wa agano ameyatimiza maagano yake yote.
 


Yesu Kristo Aliyekuja Kwa Maji, na Damu, na Roho Mtakatifu

 
Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana? Ni kwa sababu alihitaji kuzichukua dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake, na kuipokea hukumu ya dhambi kwa niaba yetu. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, akaenda Msalabani, na akamwaga damu yake na kufa Msalabani, ili kuzifanya dhambi za wanadamu wote kutoweshwa na kufanyika Mwokozi wetu wa kweli. Kwa kufanya hivyo hakuziosha dhambi zetu zote tu, bali aliipokea hukumu yote ya dhambi hizi badala yetu, na kwa hiyo amefanyika Mwokozi wetu wa milele. Dhambi zetu zote zilipelekwa kwa Yesu pale alipobatizwa na Yohana, na akazibeba dhambi hizi za ulimwengu Msalabani. Ni kwa sababu Kristo alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake, na kwa sababu alizibeba dhambi hizi za ulimwengu Msalabani, ndio maana aliweza kusulubiwa, kuimwaga damu yake, na kufa badala yetu.
Isaya 53:5 inasema, “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Kwa kupitia ubatizo wa Bwana wetu, dhambi zetu za asili ambazo zilirithishwa kwetu na baba yetu Adamu na dhambi zetu halisi ambazo tunazifanya kila siku katika maisha yetu zote zilipelekwa kwa Yesu. Na alihukumiwa kwa dhambi hizi zote. Na kwa hiyo, Bwana wetu amezifanya dhambi zetu zote kutoweshwa kwa kuja kwetu kwa maji na kwa damu (1 Yohana 5:5-8).
Basi huyu Yesu Kristo, Mwokozi wetu na Masihi ambaye alizishughulikia dhambi zetu zote na akazifanya zitoweshwe ni nani? Mwanzo 1:1 inaeleza, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Je, ni nani huyu Mungu mwenyezi ambaye aliuumba ulimwengu kwa Neno lake? Si mwingine bali ni Masihi wa wenye dhambi, yeye ambaye alikuja kwa maji ya ubatizo wake kukuokoa wewe na mimi toka katika dhambi zote za ulimwengu, aliyekuja kama Mwokozi aliyemwaga damu Msalabani na kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi zote za ulimwengu. Kwa kupitia maji, na damu, na Roho, Yesu ametuokoa toka katika dhambi zetu na hukumu. Bwana wetu alikuja kwetu kama Mwokozi kuzichukua dhambi zetu zote na akahukumiwa kwa dhambi hizi kwa niaba yetu.
Kwa kweli, Yesu Kristo, ni Mwana wa Mungu na Mungu mwenyewe, kwa kuwa Masihi ni Mungu wetu wa kweli. Jina “Yesu” maana yake “Mwokozi ambaye atawaokoa watu wake toka katika dhambi zao” (Mathayo 1:21). Kwa upande mwingine, neno “Kristo,” “Basileos” katika Kiyunani linamaanisha “Mfalme wa wafalme.” Yesu ni muumbaji aliyeuumba ulimwengu wote, mtawala wa wote, Mwokozi wa wenye dhambi, na Mfalme wa wafalme anayemhukumu Shetani.
Kwa kweli Mungu huyu mkamilifu alimuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake. Hivyo, sisi ambao ni uumbaji wake, tulipoanguka katika dhambi na ikawa inatupasa kuupata uharibifu kwa sababu ya udhaifu wetu, huyu Mfalme wa wafalme alituahidi sisi kutuokoa toka katika dhambi zetu, na ili kuitimiza ahadi hii alikuja kwetu. Bwana wetu alikuja kwetu kwa maji, na damu na Roho ili kutufanya sisi kuwa watu wa Mungu wakamilifu na wasio na dhambi.
Masihi, ambaye ni Mwokozi, kwa hakika alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu ili kuzifanya dhambi zetu zote kutoweshwa, na akazichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kuupokea ubatizo toka kwa Yohana katika Mto Yordani. Na kwa kufa Msalabani, alihukumiwa kwa dhambi zetu zote badala yetu. Kwa sababu Yesu alikuwa ni Masihi halisi kwetu, na kwa sababu ni Mwokozi wetu na Bwana wa maisha yetu, tunaweza kupata maisha mapya na ya milele kwa kumwamini yeye. Kwa hiyo, kwa kweli Masihi amefanyika kuwa Mungu wetu. Hii ndiyo sababu lango la Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, kwa kuwa hili lilikuwa ni fumbo la maji na Roho vinavyotuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote na hukumu ya dhambi zetu.
Ukweli kuwa Bwana wetu ametuokoa sisi kwa uhakika toka katika dhambi zetu ni jambo lisilo na shaka. Bwana wetu hakutuahidia wokovu wake bila mpangilio, na hakuutimiza wokovu huo ovyoovyo, na hawezi kuikubali imani ya wale ambao wanamwamini kwa mashaka, mbali na ukweli wake imara kuwa ametuokoa sisi kwa kupitia maji yake na damu yake. Kwa hiyo Bwana wetu aliwaeleza wale ambao wanamwamini kwa mazoea, “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).
Walimu wa uongo wanakazia kuwa wanawafanya watu wapokee Roho Mtakatifu katika jina la Yesu, wanawatoa mapepo kwa jina la Yesu, na wanafanya maajabu mengi kwa jina lake. Lakini Mungu anawaeleza katika Mathayo 7:23, “Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!” Hii inatueleza sisi kuwa miongoni mwa wakristo wapo wengi ambao kwa kweli wanabakia ni wenye dhambi, ambao watahukumiwa kwa dhambi zao katika siku ya hukumu, na kisha wakatupwa kuzimu.
Kwa kweli, kuna wakristo wengi ambao wanakiri kwa wazi kuwa, “Yesu ni Mwokozi wetu. Yesu ametuokoa mara moja toka katika dhambi zetu zote.” Lakini, pamoja na kudai hivyo, hawajaribu hata kujifunza ukweli kuwa Masihi alizichukua dhambi zao kwa ubatizo wake, na kwamba kwa hakika alizibeba dhambi zao na hukumu ya dhambi hizi kwa kuimwaga damu yake Msalabani. Watu hawa wataenda wote mbele za Mungu hali wakiwa bado ni wenye dhambi, kwa kuwa wanaamini kwa mazoea tu, kana kwamba wanaigiliza moja ya dini za kidunia.
Kwa hiyo, kwa sababu hawaamini kwa mujibu wa ukweli kwamba Bwana wetu amesema, “Mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru,” basi hawajapokelewa na Mungu. Kwamba watu wanamwamini Yesu au hapana, wale walio na dhambi katika mioyo yao hawawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu, ambako hakuna dhambi, kwa sababu hawana sifa za kuuingia ufalme huo. Hivyo, ni lazima wahakikishe kuwa wanakuwa na sifa za kuingia mbinguni kwa kuuamini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu wakiwa hapa duniani. Kulitengeneza lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi hizi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa yalikuwa ni majaliwa ya Masihi. Wale ambao wanaelekea kuzimu kwa sababu ya dhambi ni lazima waamini katika ukweli huu.
Kwa sababu watu hawa hawaufahamu ukweli, na kwa sababu wanamwamini Yesu kwa ufahamu wao wenye makosa uliopatikana kwa juhudi zao, bado watabakia ni wenye dhambi. Bado wana dhambi kwa sababu, badala ya kuamini kwa mujibu wa ukweli uliofichika katika vifaa vya Hema Takatifu la Kukutania, wao wameendelea kumfikiria Mwokozi kwa njia zao na wamejifanyia mafundisho yao binafsi ya wokovu yenye msingi katika mawazo yao binafsi, hali wakiamini kuwa wokovu unapatikana kwa juhudi zao binafsi kwa kufanya maombi ya toba kwa Mungu hali wakijaribu kuufikia utakaso wao unaokua na kuongezeka taratibu.
Wapo wengi katika ulimwengu huu wanaodai kuwa wanamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao, ilhali hawauamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Wapo wengi katika ulimwengu huu ambao badala ya kuamini nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kuwa ni wokovu wao, wanafikiri kuwa wanaweza kuuingia Ufalme Mtakatifu wa Mungu kwa kuiamini damu ya Yesu tu, hata kama wanabakia ni wenye dhambi.
 

Kulingana kwa Agano la Kale na Agano Jipya
 
Mungu anatueleza sisi katika Isaya 34:16 kwamba kila Neno la Mungu lina jozi ya kufanana nayo. Kwa maneno mengine, Neno la Mungu linalingana lote. Mungu alisema tuangalie na kujionea sisi wenyewe ikiwa Neno lake la Agano la Kale linafanana na Neno lake la Agano Jipya. Kile kilichoandikwa katika Agano la Kale kina Neno linalohusiana katika Agano Jipya. Kwa mfano, katika Agano la Kale, wakati waisraeli walizipitisha dhambi zao kwa mwanakondoo wa kuteketezwa kwa kumwekea mikono mwanakondoo huyo, katika Agano Jipya jambo hili linalinganishwa na kubatizwa kwa Yesu Kristo ili kuzichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake, na kwa hiyo kuzipitisha dhambi zetu zote kwa Yesu.
Kwa kupitia maji na damu yake, Yesu alikuja hapa duniani kama sadaka ya kuteketezwa na Mwokozi wa wenye dhambi. Ikiwa hangezichukua dhambi za ulimwengu kwa kuupokea ubatizo, kusingekuwa na sababu ya yeye kufa Msalabani. Bwana wetu amezifanya dhambi zetu zote kutoweshwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Hili pia liliahidiwa na Mungu kwa Neno lake, ambapo Bwana wetu alikuja kwetu kwa kupitia Neno hili na akaziosha dhambi zetu nyekundu, akizigeuza kuwa nyeupe kama theluji.
Kwa kweli, kabla ya kuutambua ukweli huu, bila shaka tulikuwa tukielea kwa dhambi zisizoisha. Kwa hiyo hatuna kitu cha kujisifia mbele za Mungu. Si kwamba hatuna kitu cha kujisifia tu mbele za Mungu, bali hatuna chochote cha kutufanya tuwe na ujasiri mbele zake. Kwa maneno mengine, hakuna kitu kinachoweza kuturuhusu hata kujifanya kuwa tuko watanashati. Tunachoweza kukisema mbele za Mungu ni “Ndiyo, uko sahihi.”
Ikiwa Mungu anasema, “Wewe ni mbegu ya makosa,
umefungwa kuzimu.”
“Ndio, uko sahihi; tafadhali niokoe mimi.”
“Nimekuokoa wewe kwa njia hii, kwa kupitia maji, na damu na Roho Mtakatifu.”
“Ndio, Bwana! Ninaamini!”
Tunachoweza kusema ni “Ndiyo” wakati wote. Tukiwa tumesimama mbele za Mungu hatuwezi kumwambia, “Nilifanya jambo hili na lile; Nililitumikia Kanisa langu vizuri; kwa kweli nilimwamini Yesu kwa moyo wangu wote; niliilinda imani yangu kwa ukaidi na ugumu kiasi kuwa hakuna yeyote anayeweza kuwazia hivyo!”
Bwana wetu alifanyaje hasa ili dhambi zetu zitoweke? Ametuonyesha sisi kuwa alizifanya kutoweka kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kwa kupitia Neno la Agano la Kale na Neno la Agano Jipya. Katika Agano la Kale, alizifanya dhambi zetu kutoweka kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, ilhali katika Agano Jipya, Yesu alifanyika kuwa Mwokozi wetu kwa kuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, kwa kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, na akazishughulikia dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi hizi kwa kuimwaga damu yake Msalabani. 
Kwa kubatizwa, Bwana wetu alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu mara moja (Mathayo 3:15). Dhambi zetu zote za kidunia zilipitishwa katika mabega ya Yesu. Kwa hiyo, baada ya kuzichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake, akazibeba dhambi hizi kwenda Msalabani, alisulubiwa, akaimwaga damu yake, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo akazifanya dhambi zetu kutoweka. Hivyo, kwa hakika Yesu Kristo amefanyika kuwa Mwokozi wetu.
Haki ya Mungu ambayo tumeipokea ni haki inayopatikana kwa kumwamini Yesu Kristo aliyekuja hapa duniani kwa kupitia maji, na damu, na Roho. Huu ndio wokovu halisi tulioupokea toka kwa Mungu, na si kitu ambacho tumekipata kwa jitihada zetu binafsi. Hakuna kitu tunachoweza kujisifia mbele za Mungu.
Kwa kweli, tunaokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kumwamini Yesu Kristo ambaye amefanyika Mwokozi wetu halisi. Kwa maneno mengine, sisi ambao tulikuwa ni wenye dhambi kwa kweli tumepokea ondoleo la dhambi kwa kuuamini wokovu, ubatizo wa Yesu, na damu aliyoimwaga kwa ajili yetu. Ikiwa kazi ya Yesu ya wokovu ingekuwa imefanyika walau kwa asilimia 70, na halafu asimilia nyingine 30 ikatakiwa tuifikie kwa jitihada zetu za kutokufanya dhambi, ili tuweze kutakaswa taratibu na kuukamilisha wokovu wetu kidogo kidogo, kwa hakika ingetupasa kukesha usiku kucha tukiomba kwa nguvu, tungeitumia kila siku kutoa maombi yetu ya toba, tungeihudumia jamii, au vinginevyo tungejaribu kufanya kila linalowezekana na kila kinachowezekana!
Lakini Mtume Paulo anasema katika Warumi, “Ole wangu, maskini mimi, Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?Ninamshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu! Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 7:24-8:1). Kama ambavyo Paulo alikiri, sisi pia ni lazima tumwamini Yesu Kristo kama alivyofanya. Maandiko yanatueleza sisi kuwa, Yesu Kristo ametuokoa kikamilifu toka katika mwili huu wa mauti, kwa asilimia 100. Ni nani basi atakayetuhukumu adhabu? Hakuna hata mmoja atakayetuhukumu sisi, kwa kuwa Yesu Kristo amekwisha tuokoa kwa asilimia 100 bila kujali udhaifu wetu.
 

Wewe na Mimi Pia Tulikuwa Mafarisayo wa Kiroho
 
Baadhi yenu mnaweza kuwa mmemfahamu na kumwamini Yesu taratibu taratibu kwa muda mrefu. Kwa maneno mengine, umemwamini Yesu kuwa ni Mwokozi hata kabla hujakutana na injili ya maji na Roho. Mimi pia nimekuwa Mkristo pasipo kuzaliwa upya kwa takribani miaka kumi.
Wakati tulipoamini kwanza katika Yesu kuwa ni Mwokozi wetu, ilikuwa ni uzoefu wenye kufurahisha. Mwanzo ulikuwa ni mzuri sana na tulidhani kuwa tutaokolewa pasipo kanuni kwa kumwamini Yesu tu kuwa ni Mwokozi, hata kama tungebakia wajinga na kutofahamu ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Mara ya kwanza nilipomwamini Yesu, kwa kweli moyo wangu ulijawa na furaha. Kwa hiyo nilifurahi sana nilipomwamini Yesu kwa mara ya kwanza, lakini baada ya miaka mitano, nilikuja kujitazama mwenyewe, na nikatambua kuwa nimekuwa nikifungwa na dhambi moja kwa moja ambazo nimekuwa nikizifanya, ndipo nikatambua kuwa bado sikuwa huru. Je, unafikiri nilifanya dhambi, au unafikiri sikufanya dhambi yoyote katika hiyo miaka mitano ya mwanzo ya maisha yangu ya Ukristo? Ikiwa unanifahamu au hunifahamu, jibu liko wazi: kwa kweli nilifanya dhambi. Katika kipindi hiki, wakati ambapo nilikuwa siijui kweli, kwa kweli nilisumbuliwa sana kila nilipofanya dhambi, na ili kujinasua kutokana na hilo nilikuwa ninafanya maombi ya toba, na wakati mwingine nilikuwa ninafunga hata kwa siku tatu. Basi hapo ndipo mzigo wa moyo wangu ulikuwa mwepesi kidogo, na ikaniruhusu kumsifu Mungu, “♫Neema ya kushangaza! ♫Ni ya sauti ya ajabu, iliyoniokoa mwenye dhambi kama mimi! ♪” Lakini, kwa kweli, bado niliishia kufanya dhambi tena. Kwa sababu nilikuwa na mapungufu mengi na nilikuwa na malaumu mengi, kila siku nilifanya dhambi, hata pale nilipokuwa ninachukia kufanya hivyo. Hakuna hata mara moja nilipoweza kutatua tatizo langu la dhambi daima.
Miaka mingine mitano ilipita katika mazingira kama haya, na pale nilipokuwa nimekuwa Mkristo kwa miaka karibu kumi, kwa ghafla, nilishtushwa kutambua jinsi ambavyo nilitenda dhambi nyingi sana katika miaka hiyo yote. Nilipojiangalia nikifanya dhambi hizo kubwa kila siku, kwa kweli nilihuzunika sana na nilikatishwa moyo sana. Na niliposimama mbele ya Sheria, pia nikatambua jinsi ambavyo mimi ni mwenye dhambi. Hivyo hali ikazidi kuwa ngumu kwa mimi kusimama mbele za Mungu, na mwishowe nikaishia kuwa mwenye dhambi ambaye sikuweza hata kulalamika, katika dhamiri safi, kumfahamu na kumwamini Yesu vizuri. Hivyo katika mwaka wa kumi kama Mkristo sikuweza kufanya lolote zaidi ya kukiri hali ya udhambi katika nafsi yangu.
Nilipomwamini Yesu kwa mara ya kwanza, kwa kweli nilidhani kuwa nilikuwa ni Mkristo mzuri. Lakini kadri muda ulivyokwenda nilizidi kutambua zaidi na zaidi kuwa sikuwa na kitu cha kujidaia mbele za Mungu. Nilitambua, “kwa hakika mimi ni Farisayo. Mafarisayo hawapatikani tu katika Biblia, kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa Farisayo wa leo!”
Mafarisayo ni aina ya watu ambao wapo katika utakatifu wao wa kujifanya au wa kuigiza. Kila Jumapili wanakwenda kanisani na Biblia zao, wanawapigia kelele Wakristo wenzao, “Habari ya asubuhi! Halleluya!” Na wanapoabudu, wanasikia kila wakati mtu mmoja akizungumza juu ya Msalaba, mwishowe wanaishia kulia. Mimi pia niliwahi kumwaga machozi yangu nilipokuwa nikiifikiria damu ya Yesu. Nilidhani kuwa huku ndiko kuabudu kwa kweli kunakotakiwa. Lakini kadri tunavyoishi katika ulimwengu huu, hatimaye kila mtu anakuja kuigundua hali yake ya ndani, ya kufanya dhambi moja baada ya nyingine. Hivyo, watu kwa mara nyingine wanaishia kutoa maombi ya toba. Kwa kweli wanaweza wakajisikia vizuri kwa muda kidogo, lakini baadaye tena, wanakimbilia tena kwenye maombi ya toba kwa sababu kuna dhambi nyingi sana ambazo wamezifanya. Baadhi ya watu wananena hata kwa lugha na baadaye wanaona hata maono, lakini haya yote hayasaidii kitu. Haijalishi ni kiwango gani cha majaribio wanakuwa wamekifanya, kwa kweli haisaidii kwa wao kujaribu kutatua tatizo la dhambi katika mioyo yao.
Ikiwa hatimaye watatambua kuwa wao ni viumbe wasio na maana mbele za Mungu na wakatambua kuwa wamefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zao, hata kama utambuzi huu unakuja baadaye kwa kuchelewa, kwa kweli utakuwa ni utambuzi wenye matokeo ya bahati. Kwa kweli, kadri tulivyomwamini Yesu kwa muda mrefu ndivyo tunavyozidi kutambu jinsi tulivyokuwa wenye dhambi. Lakini Mafarisayo ni wazuri katika kuficha ukweli huu. Ni wazuri sana kwa kuzificha dhambi za mioyo yao na kucheza mchezo wa unafiki kiasi kuwa wanathibitishwa hata na wale wanaowazunguka kwa utakatifu wao.
Wanadini wa ulimwengu huu wanaheshimiana sana. Lakini bila kujali jinsi wanavyoheshimiana, wanaposimama mbele za Mungu, wao wote ni lundo tu la dhambi.
Tulipokuwa hatuufahamu ukweli, sisi nasi pia tulizoea kutoa maombi ya toba kwa juhudi. Lakini baada ya muda, tunachoka na mwishowe tunaishia kuomba, “Bwana, fanya lolote ambalo unapenda kulifanya. Nina dhambi nyingi sana. Bado nimefanya dhambi tena. Sasa linakuwa ni jambo la kuudhi kwangu kuendelea kukueleza kuhusu dhambi hizi.” Japokuwa ni jambo la kuudhi, kwa sababu tuliambiwa kuwa Mungu atafurahishwa kila tunapozikiri dhambi zetu, na kwamba atatusamehe dhambi zetu kwa haki yake na atatutakasa toka katika madhambi yote, basi ndipo tuliendelea kumwomba Mungu, “Bwana, nimetenda dhambi. Tafadhali nisamehe, Bwana!” Hata hivyo, bado dhambi zetu zilibakia katika mioyo yetu.
Kila wakati watu wanapoinamisha vichwa vyao na kumwomba Mungu, dhamiri zao zinawakumbusha juu ya dhambi zao na hiyo dhamiri inaitafuna mioyo yao. Dhamiri zetu zinaisumbua mioyo yetu zikitueleza, “Unadiriki vipi kusali kwa Mungu ilhali una madhambi mengi uliyoyafanya?”
Kwa hiyo, baada ya kitambo, kwa kuwa hatukuwa hasa na maneno ya kusema, ndipo tunaishia tukilia, “Bwana, Bwana!” Mara kwa mara tumejikuta tukienda mlimani na kuliitia jina la Bwana. Ili kuepuka usumbufu utakaowafanya watu wastuke, mara nyingi tumepanda mlimani kuomba nyakati za usiku wa manane, tukaingia katika pango mahali fulani, na huko tukalia na kuliitia jina la Bwana. Lakini jambo hili pia, lilikuwa ni kujiridhisha sisi wenyewe na dhambi zetu zilibaki pamoja nasi.
Pia tulijaribu kuzituliza dhamiri zetu, hali tukijieleza kuwa sisi hatuna dhambi kamwe, “Mungu ni wa huruma sana kiasi kuwa amezifanya dhambi zangu kutoweka. Nimefunga na kuomba kwa siku tatu. Nini cha zaidi, ninafikiri kuwa sijatenda dhambi kiasi hicho. Je, Mungu wetu wa huruma si atanisamehe?”
Lakini, je tungeweza hasa kujidanganya sisi wenyewe, hata kama tungelimsifu Mungu kwa rehema zake? Je, tungeliweza kudiriki kuidanganya mioyo yetu wenyewe hali tumebakia wenye dhambi mbele za Mungu? Hatungeweza kufanya hivyo! Haijalishi tumepanda cheo kiasi gani katika safu za uongozi katika makanisa yetu, haijalishi ni kiasi gani tulisifiwa na kutukuzwa na wengine, kadri tulivyoendelea kutenda dhambi katika nafsi zetu, hatukuweza kamwe kuwekwa huru toka katika dhambi hizi, hivyo mwishowe tuliishia kuwa wanafiki.
Matamanio ya dhambi yaliendelea kukua katika mioyo yetu. Ingawa tulizungumzia juu ya damu ya Yesu Msalabani mara nyingi, japokuwa tulimwaga machozi mengi kwa kuifikiria damu ya Yesu Msalabani, na ingawa tumekuwa wakristo wazuri, bado tulibaki ni wenye dhambi hadi pale tulipokutana na injili sahihi ya maji na Roho. Pamoja na kuishi kwa mujibu wa taratibu na desturi zote za Ukristo, bado tulikuwa na dhambi. Hii ndiyo iliyokuwa dini ya Mafarisayo. Bado kuna watu wengi katika ulimwengu huu ambao wana aina hii ya imani, na wanapatikana hata katika jamii zetu za Wakristo.
 


Dhambi Zetu Zote Zilitoweshwa Kwa Kuiamini Injili ya Maji na Roho

 
Kabla ya kuifahamu injili ya maji na Roho, na kabla ya kuiamini injili hii, sisi sote tulikuwa na dhambi katika mioyo yetu. Kabla hatujauamini ukweli huu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, dhamiri zetu zilikuwa na dhambi. Kwa kweli, sisi sote tulikuwa ni wenye dhambi mbele za Mungu, na tulifungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, kwa kuwa Biblia inatueleza kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti”. Kwa hiyo tulisumbuliwa sana kwa sababu ya dhambi. Na tulifungwa kuzimu kimwili na kiroho kwa sababu ya hukumu ya Mungu juu yetu kwa sababu ya dhambi zetu.
Tuliwafanya watu wengi kuingia katika Ukristo na tuliwafundisha. Lakini tulifanya kazi wakati ambapo hatukuweza hata kuzisafisha dhamiri zetu wenyewe. Hatukuweza kulikana hili mbele za Mungu. Tulitambua mbele za Mungu kwamba mioyo yetu ni yenye dhambi na tumefungwa kuzimu.
Kwa kweli mara zote nilikuwa na maswali yasiyo na majibu: “Kwa nini Bwana wetu alibatizwa alipokuja hapa duniani?” Nilipenda kufahamu kwa nini Yesu aliupokea ubatizo. Kwa nini, na kwa madhumuni gani Yesu alibatizwa? Niliweza kuufahamu ubatizo wetu wa maji kuwa ni alama au ishara ya imani yetu katika Yesu, lakini sikuweza kufahamu kabisa kuwa ni kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji. Kwa nini Yesu alibatizwa? Kwa nini?
Basi nikawauliza viongozi baadhi katika jumuiya za Kikristo, “Mheshimiwa, nina swali. Unaniruhusu kuuliza?” Wakaniambia endelea na swali lako, kwa hiyo nikawauliza. “Swali linahusu Biblia. Ni wazi kuwa Yesu aliupokea ubatizo toka kwa Yohana katika Agano Jipya. Lakini sina hakika kuwa ni kwa nini Yesu alibatizwa. Je, Mheshimiwa, unafahamu ni kwa nini Yesu alibatizwa?” Kisha wakatabasamu, wakaniambia, “Haulifahamu hata hilo? Ni kitu ambacho hata watoto wetu wa Shule ya Jumapili wanakifahamu! Kinapatikana katika maandiko ya Biblia ya asili, na pia habari hiyo inapatikana katika Kamusi za Biblia. Je, Yesu hakubatizwa ili kutuongoza sisi na kutuonyesha mfano, na kutuonyesha sisi unyenyekevu wake?” Basi nikasema, “Lakini Mheshimiwa, ikiwa jibu lingekuwa rahisi hivyo, kiasi kuwa hata watoto katika shule ya Jumapili walifahamu kwa hakika. Nimelichunguza jambo hili katika maandiko ya asili na katika historia, ninaona kuwa ubatizo wake haumaanishi hivyo. Je, hakuna sababu nyingine iliyomfanya Yesu akabatizwa na Yohana?”
Niliendelea kuuliza. Nilianza kulitafuta jibu mara baada ya kuwa Mkristo. Sikuwa na uchaguzi zaidi ya kujitolea miaka kadhaa katika kulitafuta jibu la swali hili. Niliziangalia kazi zote za wanazuoni kuhusu swali hili. Pamoja na kuwa nilitafuta, sikuweza kupata popote palipoelezea kuhusu ubatizo wa Yesu kwa wazi na kwa usahihi. Nilijitahidi kulitafuta jibu la mwisho hadi pale Bwana aliponipa maarifa ya injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Wakati nimetekwa na fumbo la ubatizo wa Yesu ambalo sikuwa nimelipata jibu lake, ndipo nikapata nafasi ya kusoma kwa makini injili ya Mathayo 3:13-17: “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’”
Nilipolisoma Neno hili, mwishowe nilitambua, “Kwa hiyo hivi ndivyo! Sababu iliyomfanya Yesu akabatizwa ni kwa sababu alikuwa ni sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale! Huu ni ukweli wa wokovu wake uliofichika katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa!”
Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye Eliya ambaye Mungu aliahidi kumtuma katika Agano la Kale. Mungu alisema katika Malaki 4:5 kuwa atamtuma Eliya kabla ya siku ya hukumu, na Mathayo 11:14 inatueleza kuwa Eliya ambaye Mungu aliahidi kumtuma kwetu si mwingine bali ni Yohana Mbatizaji. Kwa hiyo niliweza kufahamu kuhusu Eliya, lakini bado sikuwa na hakika kuwa ni kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji Ndipo nikarudia tena kusoma Mathayo 3:13-17 na nikachunguza kifungu hicho tena, “‘Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.... Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini... ‘Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’” Kisha mashaka yangu yote yakayeyuka. “Ili kuitimiza haki yote,” ilimlazimu kuupokea ubatizo wake. Kwa kweli Yesu aliitimiza hii kazi ya haki ya kuwaokoa watu kwa kupitia ubatizo wake.
Ubatizo ni sawa na lile tendo la kuwekea mikono katika Agano la Kale, pale mikono ilipowekwa juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka kwa mujibu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa wa Hema Takatifu la Kukutania. Kitendo cha wenye dhambi kuleta sadaka ya kuteketezwa mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketeza, kitendo cha wenye dhambi kuiweka mikono yao juu ya wanyama wa kuteketezwa na kisha kuzitubu dhambi zao na kuzipelekwa kwa wanyama wao wa kuteketezwa; kitendo cha Kuhani Mkuu kuzikiri dhambi zote za watu wa Israeli na kuzipeleka kwenye sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya waisraeli na wao wenyewe; na kitendo cha Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika kipindi cha Agano Jipya—mambo haya yote yanawiana na kufanana. Mwishowe nilitambua kuwa Yesu aliupokea ubatizo wake (kuwekewa mikono) ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake na kuzifanya dhambi za kila mtu kutoweshwa.
Hivyo niliyaangalia maandiko matakatifu ya asili. Niliangalia jinsi maneno, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote,” yalivyoandikiwa katika Kiyunani “Ἄφες ἄρτι, οὕτως γὰρ πρέπον ἐστὶν ἡμῖν πληρῶσαι πᾶσαν δικαιοσύνην.” Katika maneno haya, “kwa kuwa” na “haki” yanalingana na kuwiana na “hoo’-tos gar (οὕτως γὰρ)” na “dikaiosune (δικαιοσύνην)” kwa Kiyunani. Hilo neno la kwanza linamaanisha “kwa njia hii,” “kwa uhakika,” “kwa njia hii tu,” “inayofaa zaidi,” au “kwa mtindo huu.” Na neno la mwisho linamaanisha, “haki, kuhesabiwa haki au usawa wa kukubalika na Mungu.”
Habari hii inatueleza kuwa Yesu aliwaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao. Inatueleza kuwa Yesu aliitimza haki ya Mungu kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake. Kwa maneno mengine, inamaanisha kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Hivyo mashaka yetu yote yalisuluhishwa, kwa kuwa sasa tunatambua sababu iliyotufanya tuhangaike na kuchanganyikiwa. Ni kwa sababu Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kwamba akaenda na kufa Msalabani kama hukumu ya dhambi hizi. Huu ulikuwa ni ukweli uliopatikana katika injili ya maji na Roho.
Kwa maneno mengine, sisi, tuliozaliwa upya tulikuja kutambua kuwa ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana ulikuwa ni kitu muhimu sana kwa wokovu wetu, na kwamba alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa ubatizo wake. Wewe pia unapaswa kuutambua ukweli huu katika injili ya maji na Roho. Ni hapo utakapoutambua ukweli huu ndipo nafsi yako itaangaziwa.
Kwa kweli, hatuwezi kuifahamu siku ambayo Yesu aliupokea ubatizo toka kwa Yohana. Hatuwezi kamwe kusahau siku ambayo tulitambua kuwa dhambi zetu zote zilipelekwa kwa Yesu. Tumeyaona mabadiliko ambayo yalitokea katika mioyo yetu kwa kuutambua ukweli huu. Mabadiliko hayo yalienea katika mioyo yetu kama vile mawimbi yanavyotawanyika ziwani. Hali ikipenya gizani, mwanga mng’avu ulituingia sisi na ukaturuhusu kuufahamu ukweli wa wokovu.
 


Ubatizo Ambao Yesu Aliupokea Ulizipitisha Dhambi za Ulimwengu Kwa Yesu

 
Baada ya kusoma Mathayo 3:13-17, sikuweza kusema neno lolote kwa muda mrefu. Pamoja na kuwa nilikuwa ni mwenye dhambi, Yesu aliupokea ubatizo wake, na akasema, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” Kwa hiyo, sababu iliyomfanya Yesu akaimwaga damu yake Msalabani (nyuzi nyekundu) ilikuwa ni ubatizo wa Yesu (nyuzi za bluu). Huyu Yesu alikuwa ni Mungu mwenyewe (nyuzi za zambarau). Na kwa Neno la Agano Jipya na Agano la Kale (kitani safi ya kusokotwa), ametufundisha sisi ukweli halisi wa wokovu. Kwa maneno mengine, Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake.
“Je, bado tuna dhambi au hapana? Wakati Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji, dhambi za kila mtu zilipelekwa kwa Yesu. Je, dhambi zetu pia zilipelekwa kwa Yesu? Je, dhambi za ulimwengu zilipelekwa kwa Yesu kwa wakati ule? Je, dhambi ambazo tulikuwa nazo tayari wakati bado tumo katika matumbo ya mama zetu ni dhambi za ulimwengu au hapana? Je, vipi kuhusu dhambi ambazo tulizifanya wakati tulipokuwa na umri wa mwaka mmoja? Je, hizi si dhambi za ulimwengu? Vipi kuhusu dhambi ambazo tumezifanya katika utoto wetu? Je, hizo si sehemu ya dhambi za ulimwengu?”
Ni lazima tujiulize sisi wenyewe maswali haya ili kuhakikisha kuwa tupo katika njia na mwelekeo sahihi. Kama hivi, imani ni kuhakikisha kuwa tunasimama katika msingi imara kwa Neno la Mungu. Dhambi ambazo tulizitenda utotoni kwa hakika ni dhambi za ulimwengu, kama zilivyo dhambi ambazo tulizitenda tulipokuwa vijana ambazo nazo ni dhambi za ulimwengu. Dhambi zote tunazozifanya katika muda wetu wa kuishi zote ni dhambi za ulimwengu. Dhambi hizo zote za ulimwengu zilikwishapelekwa kwa Yesu. Hakuzikupelekwa? Kwa kweli zilipelekwa! Imeandikwa kuwa Bwana wetu alizichukua sio dhambi zetu tu, bali dhambi za kila mwanadamu. Hivyo tulitambua, “Kwa kweli dhambi zetu zote zilipelekwa kwa Yesu. Je, bado tuna dhambi tena? Hapana, hatuna dhambi tena zilizobakia ndani yetu!”
Ni kwa sababu Yesu alibatizwa na Yohana ndio maana Yohana Mbatizaji anashuhudia, “Tazama! Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi za ulimwengu!” (Yohana 1:29) Yesu alizichukua dhambi zote za kila mtu aliyewahi kuishi na atakayeishi, tangu mwanzo wa mwanadamu hadi mwisho. Dhambi zote ambazo mtu aliwahi kuzifanya katika maisha yake yote, na dhambi za kila mtoto wa kila mtu, zote zilichukuliwa zote na Yesu. Haijalishi ni kwa muda gani ulimwengu huu utaishi, kwamba ni miaka maelfu kwa maelfu au hata mabilioni ya miaka, Bwana wetu alizichukua katika mwili wake dhambi za watu wote wa ulimwengu huu kwa ubatizo wake, akazibeba dhambi hizi katika mabega yake kuelekea Msalaba, alisulubiwa, na hivyo akaipokea hukumu yote ya dhambi kwa ajili yetu—hivi ndivyo tulivyoitambua na kuifahamu habari ya wokovu.
Kwa hiyo, kwetu sisi tuliozaliwa upya, kwa kweli tulitambua kuwa Yesu alifufuka tena toka kwa wafu na akafanyika kuwa Mwokozi wetu, na tuliamini hivyo, na kwa jinsi hiyo maswali yetu yote yalijibiwa.
Ni kwa ubatizo kwamba Yesu alizipokea dhambi na kuimwaga damu yake Msalabani Bwana wetu alizishughulikia dhambi zetu zote. Hii ndio sababu Biblia inazungumzia juu ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, na ndio maana Biblia inatueleza katika 1 Yohana 5:4-6 kwamba Yesu alikuja kwetu si kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Hivyo tulikuja kutambua, “Kwa hiyo ndio maana Biblia inatueleza sisi kwamba Mwokozi wetu Yesu aliitimiza haki yote ya Mungu kwa kuupokea ubatizo wake. Huu ni ukweli! Hata hivyo, viongozi wa Kikristo hawakutufundisha ukweli huu kwa kuwa wote walikuwa hawaufahamu!”
Sisi tulifanyika tusio na dhambi wakati ule ukweli wa Mungu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ulipotueleza kuwa hatuna dhambi. Hakuna hata mmoja anayeweza kuthibitisha wokovu wa nafsi nyingine. Haisaidii kupata maneno mazuri toka kwa watu wengine. Je, jinsi ambavyo watu watazungumzia habari zetu—kwamba sisi ni Wakristo wazuri sana, au hata wakitupanga katika daraja la Wakristo wa kundi A+—je inaweza kuupa nguvu wokovu wetu toka katika dhambi? Tunafanyika tusio na dhambi si kwa sababu watu wanatuthibitisha, bali ni pale Neno la Mungu linapotueleza kuwa Kristo alizifanya dhambi zetu zote kutoweshwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa.
Neno la Mungu linatueleza kwamba Yesu hakuzifanya dhambi zangu kutoweka tu, bali pia hata dhambi zako. Linatueleza kuwa kwa sababu Yesu Kristo Masihi amezifanya dhambi zote za watu wote kutoweshwa, sisi sote tunaweza kupokea ondoleo la dhambi ikiwa tu tutamwamini. Hivi ndivyo tunavyoweza kuingia katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, kwa kulipokea ondoleo la dhambi kwa kupitia maji na Roho.
 


Je, Imani Sahihi ni Ipi?

 
Lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa. Kila mmoja ni lazima awe na imani hii sahihi inayoamini kwamba Bwana wetu alikuja hapa duniani na kwa hiyo akatuokoa toka katika dhambi zetu zote. Tunapoamini kwamba Bwana alizaliwa katika ulimwengu huu katika mwili wa mwanadamu, na kwamba alibatizwa na Yohana, akafa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo akafanyika Mwokozi, ndipo sisi sote tunapoweza kufanyika wana wa Mungu. Ingawa matendo yetu yanapungukiwa, na ingawa mwili wetu hauna thamani, kwa kuamini katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa katika mioyo yetu, tumefanyika tusio na dhambi. Kwa hiyo, ili kuwa wenye haki inawezekana kwa kupitia imani tu. Kwa kuuamini wokovu uliodhihirishwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, sisi sote tumefunikwa na haki ya Mungu. Kwa kifupi, kwa kuiamini injili ya maji na Roho, sisi tumefanyika wana wa Mungu.
Baadhi yenu bado mnaweza msielewe kikamilifu. Ikiwa ndivyo, unachotakiwa kufanya ni kuendelea kukisoma kitabu hiki au kuhudhuria Kanisa la Mungu. Hadi sasa tumejadili mambo ya jumla ya Hema Takatifu la Kukutania, lakini utakapoanza kusoma mafafanuzi ya kina, ninyi nyote mnaweza kuufikia ufahamu mkamilifu wa Hema Takatifu la Kukutania. Ni kitu rahisi kiasi kuwa hata mtoto mdogo anaweza kufahamu.
Ikiwa watu wataiweka imani yao katika ufahamu wa ovyo wa Yesu, hawataweza kuokolewa kamwe toka katika dhambi zao bila kujali kuwa ni kwa muda gani wamekuwa wakimwamini Yesu hata kama ni maelfu au makumi elfu ya miaka. Bado watatendelea kuwa na dhambi kila siku. Hivyo watendaelea kulia kila siku, kwa sababu hawawezi kuikwepa laana ya dhambi zao. Mambo yatakapoanza kuwaendea vizuri, watafikiria kuwa Mungu anawasaidia. Lakini mambo yatakapoenda vibaya hata kama ni kidogo watashangaa, “Je, ni kwa sababu sikutoa zaka? Au ni kwa sababu sikwenda kanisani Jumapili iliyopita? Nimetenda dhambi na nimeshindwa kumtumikia Mungu kikamilifu, na ninafikiri kuwa ananiadhibu kwa makosa hayo.” Kwa njia hii, wanaishia kufa hali wakiwa wamefungiwa katika Sheria, kwa kuwa maandiko yanatueleza kuwa “sheria inaleteleza hasira” (Warumi 4:15).
Ili kwa hakika kuwa na imani ambayo ni kamilifu, ni lazima tuzifahamu kiusahihi na kuziamini huduma nne za Yesu Kristo ambaye alikuja kwetu kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni lazima tuutambue ukweli uliotolewa na Yesu Kristo. Ni pale tu tutakapokuwa na ufahamu mzuri wa ukweli huu wenye sehemu nne na tukauamini, ndipo tunapoweza kuwa na imani ambayo ni kamilifu mbele za Mungu, na kwa kweli tutafanyika watoto wake wakamilifu. Kwa sababu tumefanyika tusio na dhambi kwa kuziamini huduma hizi nne za Yesu, kwa hakika sisi ni wenye haki tusio na dhambi, hata pasipo jitihada zetu za kujitoa toka katika kongwa la dhambi. Hata pasipo kutumia nguvu yetu ya hiari, sisi ni watu wa imani tusio na dhambi. Hata pasipo matendo yetu mazuri, sisi ni wana wakamilifu wa Mungu ambao dhambi zao zote zilioshwa na kuwa nyeupe kama theluji.
Kama vile mtoto anavyocheza na kupumzika kwa amani chini ya macho ya ulinzi ya wazazi, basi kuuamini ukweli huu, basi kwa hakika sisi tuna amani na raha katika mioyo yetu mbele ya macho ya rehema ya Mungu Baba. Ijapokuwa matendo yako yanaweza kuwa hayastahili, unachotakiwa kufanya ni kuziamini kazi za Bwana, kwa kuwa kadri usivyostahili ndivyo utakavyouona zaidi upendo wa Bwana wetu.
Je, unahangaika kwa kupiga makelele ili kupokea ondoleo la dhambi zako, je, bado huna imani ambayo inaamini katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa? Sasa, wale wanaoufahamu ukweli huu hawahitaji kuhangaika kwa kupiga makelele ili kupokea ondoleo la dhambi, lakini amini kimya kimya. Wale waliofanyika wana wa Mungu kwa imani ni wale wanaomfahamu na kumwamini Yesu Kristo katika kweli, ambaye alikuja kwetu kwa kupitia maji, na damu, na Roho. Wanamtumikia Mungu si kwa matendo ya juu juu, bali wanampenda na kumtumikia kwa imani yao kwanza. Kwa sababu tunaamini, Mungu anatupatia hadhira yake na anatembea pamoja nasi. Kwa sababu tunamwamini yeye, anatusaidia. Na kwa sababu tunamwamini Yesu ambaye ametuokoa kwa ubatizo na damu ambamo tunaiweka imani yetu, basi tumefanyika watumishi wa Mungu ambao tunaitumia kazi yake ya haki.
Sasa ni lazima sisi sote tuutambue ukweli kwamba Mungu alilifanya lango la wokovu wetu katika ua wa nje wa Hema Takatifu la Kukutania, akalifuma kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, ili kutupatia wokovu wenye uhakika wa ondoleo la dhambi. Maandiko yanatueleza kuwa Yesu alikuja kwetu kwa kupitia maji, na damu, na Roho, na kwamba ametuokoa toka katika dhambi zetu kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ya lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania katika Agano la Kale. Bwana wetu amefanyika kuwa lango la wokovu wetu toka katika dhambi. Ni lazima tuamini na kuamini tena katika kazi hizi nne za Masihi ambaye kwa hakika ametuokomboa toka katika dhambi zetu zote.
 

Ubatizo Ambao Yesu Aliupokea Toka Kwa Yohana Ni Kiini Halisi cha Nyuzi za Bluu Zilizodhihirishwa Katika Lango la Ua wa Hema Takatifu la Kukutania
ubatizo wa Yesu
Hebu tuangalie tena Mathayo 3:13-17: “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’” Katika kipindi hiki wakati Yesu alipobatizwa, ilikuwa ni miaka 30 tangu alipozaliwa na bikira Maria. Neno “Kisha” linaonyesha kipindi ambacho Yohana Mbatizaji na Yesu walikuwa wamefikisha miaka 30.
Yohana Mbatizaji alizaliwa miezi sita kabla ya Yesu, alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu wa dunia hii ambaye alikuwa akiwapatia wanadamu ubatizo wa toba (Mathayo 3:11, 11:11). Wakati Yesu alipofikisha miaka 30, alikuja kwa huyu Yohana aliyekuwa akiwabatiza watu katika Mto Yordani, ili abatizwe. Lakini Yohana Mbatizaji alijaribu kumzuia akisema, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” Yesu akajibu akamwambia, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Yohana akamruhusu, na Yesu akabatizwa na Yohana. Maandiko pia yananukuu kwamba baada ya Yesu kubatizwa, mbingu zilimfunukia, na sauti ikatoka mbinguni ikisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”
Katika Mathayo 3:15, Yesu anatueleza sababu kuwa ni kwa nini alibatizwa na Yohana. Ukweli huu unahusishwa na nyuzi za bluu za ua wa Hema Takatifu la Kukutania: “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Dhumuni la ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana ilikuwa ni kuyasamehe makosa ya wenye dhambi kwa kupitia kazi zake zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu za Hema Takatifu la Kukutania—“kwa kuwa [ilikuwa] itupasavyo [wao] kuitimiza haki yote.”
Kwamba Yesu Kristo atazichukua dhambi za kila mtu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji huo ulikuwa ni upendo wa haki wa Mungu na utimilifu wa kazi yake ya wokovu kwa wenye dhambi wote. Kama Yohana 3:16 inavyosema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.” Yesu alibatizwa ili kutuokoa toka katika dhambi za ulimwengu, ili kwamba tusiadhibiwe kwa sababu ya dhambi zetu. Hii ndio sababu Yesu aliichukua haki yote ya Mungu na dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, kwa kuwa ndivyo ilivyowapasa kuitimiza haki yote.
Je, “haki ya Mungu ni nini?” kifungu hicho hapo juu kinatueleza kwamba sababu iliyomfanya Yesu akabatizwa na Yohana Mbatizaji ilikuwa ni kuitimiza haki yote ya Baba.
Hapa tunahitaji kuchunguza vizuri juu ya haki ya Mungu kuwa ni nini. “Haki yote” inaeleza ukweli kuwa kwa kubatizwa na Yohana, Yesu Kristo alizichukua dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake. Kwa ubatizo wake alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake mara moja. Kwa kuwa dhumuni la kuzaliwa kwake lilikuwa ni kuzitowesha dhambi zote za ulimwengu mara moja, hivyo basi ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana kwa kweli ulikuwa ni haki. Kuitimiza haki yote ya Mungu maana yake ni kuzitimiza kazi za haki zinazozifanya dhambi zote za ulimwengu kutoweshwa—yaani kuutimiza wokovu.
Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni njia ya muhimu sana ambayo kwa hiyo Mungu atatukomboa toka katika dhambi zetu. Mungu alipanga katika Agano la Kale kuwa ili kuzitowesha dhambi zetu, atamwinua Yohana Mbatizaji kama mwakilishi wa wanadamu, na atamfanya Yohana ambatize Mwanae Yesu Kristo, na hivyo atazipitisha dhambi zetu zote katika mwana wake. Hakuna kazi nyingine ya rehema za Mungu zaidi ya hii. Kwa sababu Mungu alitupenda sana, Mungu alimfanya Yesu abatizwe na Yohana ili kutugeuza sisi kuwa wana wake mwenyewe na kuikamilisha kazi ya haki ya kuzitowesha dhambi zetu. Hii ndio sababu iliyomfanya Mungu kunena maneno mara baada ya Yesu kubatiwa na kutoka majini, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye” Kwa maneno mengine, Mungu Baba, alisema, “kwa ubatizo wake, Mwanangu amezichukua dhambi zenu zote katika mwili wake.”
Kwa maneno mengine, Yesu Kristo, alikuja hapa duniani na kwa njia hii ya kubatizwa na Yohana, alizibeba dhambi zetu zote mara moja katika njia inayofaa, na hivyo akafanyika sadaka ya kuteketezwa ili kuzifanya dhambi zetu kutoweshwa.
Ni kwa sababu Mwana wa Mungu alibatizwa kwa ajili yetu, na kwa sababu alizipokea dhambi zetu zote katika mwili wake, na kwamba akazibeba dhambi hizi kuelekea Msalaba, alisulubiwa na akaimwaga damu yake ya thamani, na hivyo akafanyika Mwokozi wetu sote. Kwa maneno mengine, Yesu ametuokoa sisi tunaoamini kwa kubatizwa kwa ajili ya dhambi zetu, akijitoa sadaka kwa damu yake Msalabani, na kwa kufufuka tena toka kwa wafu. Na baada ya kufufuka toka kwa wafu na kuzikamilisha kazi zake za wokovu, sasa ameketi katika mkono wa kuume wa kiti cha enzi za Mungu, na muda wake utakapowadia, kwa hakika atakuja. Ukweli huu ni injili ya maji na Roho na ambayo ni kiini cha wokovu.
Katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania Kitabu cha Kutoka 27:16 kinaandika kuwa, “Na kwa lile lango la ua kutakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa na nguo ya rangi ya bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa, kazi ya mshona taraza.” Hivyo lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Hii inatueleza ukweli kuwa tunaingia mbinguni kwa kuiamini zawadi ya wokovu.
Nyuzi za bluu zilizofumwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha ukweli kuwa dhambi zetu zote zilipelekwa kwa Yesu alipokuja hapa duniani na kubatizwa.
Nyuzi za Zambarau zinatueleza sisi kuwa Yesu Kristo, ambaye alibatizwa kwa ajili ya dhambi zetu, kimsingi, alikuwa ni Muumbaji mwenyewe aliyeuumba ulimwengu wote na kila kilichomo ndani yake, Yesu ni Bwana wangu na wako. Zambarau ni rangi ya wafalme (Yohana 19:2-3), na kwa hiyo inatueleza kuwa Yesu Kristo ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa wote. Neno “Kristo” linamaanisha “Mpakwa mafuta,” na ni wafalme, makuhani, na manabii tu ndio walioweza kupakwa mafuta. Kwa hiyo, ingawa Yesu Kristo alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, utambulisho wake wa kweli ulikuwa ni Mfalme wa wafalme. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa ni Bwana na Muumbaji aliyeumba ulimwengu mzima. Yesu alikuwa ni Mungu Mwenyezi na Mwana pekee wa Mungu Baba. 
Nyuzi nyekundu katika lango la Hema Takatifu la Kukutania kunamaanisha sadaka ambayo Mfalme wa wafalme aliitoa baada ya kuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu na kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake, alisulubiwa na akamwaga damu yake Msalabani. Yesu Kristo alilipa mshahara wa dhambi zetu kwa niaba yetu, kwa kubatizwa, kwa kuimwaga damu yake ya thamani, na hivyo akajitoa sadaka kwa niaba yetu. Nyuzi nyekundu zinadhihirisha sadaka ya damu ya Yesu Kristo.
Mwisho, Kitani safi ya kusokotwa inamaanisha Neno la Mungu la kutatanisha la Agano la Kale na Agano Jipya. Biblia inatueleza sisi kuhusu wokovu wetu kwa kupitia Neno la Agano la Kale na Agano Jipya. Toka katika Agano la Kale, Mungu aliahidi kuwa atakuja kwetu kama Mwokozi wa wenye dhambi, na katika Agano Jipya, kama alivyoahidi, Yesu Kristo, ambaye ni Mungu mwenyewe, alikuja hapa duniani, akabatizwa, na akamwaga damu yake Msalabani—akajitoa mkamilifu kuwa sadaka ya dhambi zetu.
Kwa kutumia nyuzi za bluu, Mungu alilidhihirisha Neno kwamba Yesu Kristo alikuja hapa duniani ili kutuokoa toka katika dhambi zetu na akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake; na kwa nyuzi za zambarau, alidhihirisha kuwa huyu aliyebatizwa alikuwa ni Mungu mwenyewe. Na kwa nyuzi nyekundu, Mungu alidhihirisha kuwa ametuokoa mimi na wewe toka katika dhambi zetu kwa kuja hapa duniani kama Mwokozi wetu, kwa kubatizwa, kwa kuzibeba dhambi za ulimwengu Msalabani, na kwa kuimwaga damu yake ya thamani.
Kwa upande mwingine, kwamba wokovu huu umekuja kwa Neno la Mungu lililoahidiwa toka katika Agano la Kale kulidhihirishwa na kitani safi ya kusokotwa. Hii ndiyo sababu lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Tunapoliangalia lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, lango hili linadhihirisha na linatuonyesha sisi kwa wazi jinsi ambavyo Mungu ametuokoa toka katika dhambi zetu na kutufanya sisi kuwa watu wake; kwa hiyo, ni lazima sisi sote tuamini katika maana ya kiroho ya nyuzi nne zilizotumika katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
Tukizungumzia juu ya rangi la lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, Biblia kwanza inataja nyuzi za bluu. Mara nyingi tunafikiri katika mfuatano wa zambarau, bluu, na nyekundu, lakini Biblia inaziorodhesha nyuzi hizi katika mfuatano wa bluu, zambarau, na nyekundu. Hii inatuonyesha umuhimu wa nyuzi za bluu. Wakati Yesu Kristo alipokuja hapa duniani kama Mwokozi wetu, kama asingalibatizwa na Yohana, tusingeweza kusafishwa dhambi zetu. Hii ndiyo sababu, ili kutuokoa toka katika dhambi za ulimwengu, Yesu alibatizwa na Yohana na akasulubiwa, alifanya yote kwa unyenyekevu kwa mapenzi ya Baba.
Yesu ni Bwana wa ulimwengu aliyeviumba vitu vyote, na ni Mungu wetu. Yeye ni Mungu mwenyewe ambaye ametuumba sisi ili tuzaliwe katika dunia hii, ambaye ametupatia maisha mapya, na ambaye anatawala maisha yetu. Ili Yesu aweze kutuokoa dhambi zetu, ilimbidi kubatizwa na mwakilishi wa wanadamu wote na hivyo akazichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. Kwa maneno mengine, ni kwa kubatizwa na Yohana ndio maana Yesu Kristo amefanyika Mwokozi wetu wa kweli.
Yesu alikuja hapa duniani ili atuokoe dhambi zetu, na alibatizwa ili kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. Ikiwa kama ubatizo wake usingekuwa wa kwanza, Kristo asingeweza kusulubiwa. Hii ndiyo sababu lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania linatuonyesha sisi kwa wazi jinsi ambavyo Yesu Kristo ametuokoa toka katika dahmbi zetu—ambayo ni njia sahihi ya wokovu wake.
Rangi za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatueleza sisi kuwa Yesu Kristo atakuja hapa duniani, atazichukua dhambi zote za wanadamu katika mwili wake kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, na atasulubiwa—kwa meneno mengine, atazishughulikia dhambi zetu yeye mwenyewe. Wakati Yesu alipobatizwa, mlango wa mbinguni ulifunguka, na Mungu Baba akasema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Yesu Kristo ni Masihi wetu na Mwokozi, lakini pia ni Mwana wa Mungu, Mungu mwenyewe muumbaji aliyeuumba ulimwengu wote kwa Neno lake. Kwa kuwa ni Mungu Mtakatifu, Yesu aliweza kuzibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa ili aweze kufanyika Mwokozi wetu wa kweli.
Yesu Kristo ambaye aliuumba ulimwengu wote na ambaye anautawala ametuonyesha sisi wokovu wa wazi toka katika dhambi zetu. Ni kwa sababu ili kuzitowesha dhambi zetu Yesu Kristo alikuja hapa duniani, alizichukua dhambi hizo katika mwili wake kwa ubatizo wake na akafa Msalabani ili kwamba mimi na wewe tuweze kuokolewa. Yesu Kristo ni muumbaji anayetawala maisha yetu na kifo, aliyeuumba ulimwengu mzima, na aliyewaleta baba zetu na wanadamu wote katika dunia hii. Ndiye kiini halisi cha nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Mungu mwenyewe alikuja hapa duniani kama sadaka ya kuteketezwa kwa wenye dhambi. Yesu aliyetuokoa alikuwa pamoja na Mungu mwenyezi, na mwenye rehema. Ni kwa sababu Yesu Kristo alizichukua dhambi zote katika mwili wake kwa ubatizo wake ndio maana aliitimiza haki yote ya Mungu, na hii ndio sababu alizichukua dhambi za ulimwengu katika Msalaba, alisulubiwa na kuimwaga damu yake ya thamani. Kama ilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, Yesu Kristo alifanyika sadaka yetu ya kuteketezwa ili kuzitowesha dhambi zetu zote. 
Hii ndio sababu lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, lango la Mahali Patakatifu, lango la Patakatifu pa Patakatifu, na mapaa yote ya Nyumba ya Mungu yote yalifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa sababu Yesu Kristo alibatizwa kwa ajili yako ili kwamba wewe na mimi tusafishwe dhambi zetu zote kwa kuuamini ubatizo wake. Yesu alibatizwa ili kuitimiza haki yake, na haki hii ilitimizwa kwa kuzibeba dhambi za watu wote katika mwili wake kwa kupitia ubatizo. Kwa hiyo, kitu cha lazima tunachotakiwa kukifanya ni kutambua kuwa dhambi zetu zilipelekwa pia kwa Yesu kwa wakati huo na tuamini hivyo.
Hata hivyo, kuna Wakristo wengi ambao wanamwamini Yesu juu juu na kizembe. Ni wagumu na wakaidi mno kuziacha imani zao za kidini na za kihalifu, hali zikimpa Mungu changamoto tangu awali. Ni lazima tumwamini yeye kwa mujibu wa njia ya wokovu ambayo ametupatia. Yesu alisema, “Mimi ni njia, na kweli, na uzima” (Yohana 14:6). Yesu anatueleza sisi kuwa, “Mimi ni njia. Mimi ni njia inayokuongoza kwenda mbinguni. Mimi ni Mchungaji, njia na kweli. Kwa hakika mimi ni uzima unaokuokoa wewe.” Kwa kutuokoa toka katika dhambi zetu, Yesu Kristo amefanyika Bwana wa maisha mapya kwetu.
 

Tunapomwamini Yesu Tunawezaje Kumfahamu na Kumwamini Yeye?
 
Tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuamini kiusahihi kuwa Yesu alikuja hapa duniani na ametuokoa. Neno “imani” linajumuisha maana kama “kutegemea,” “kushikilia,” na “kukabidhisha.” Watu wazima mara nyingi wanawategemea watoto wao mara wanapokuwa wazee sana, kwa kuwa wanaona ni vigumu sana kuishi peke yao. Vivyo hivyo, sababu inayotufanya tuishi kwa kujikabidhisha sisi wenyewe kwa Mungu ni kwa sababu hatuwezi kuzifanya dhambi zetu kutoweshwa kwa juhudi zetu wenyewe. Hata kama sisi wenyewe tunajitahidi kutotenda dhambi, tunajikuta tukiishia kuishi maisha yetu hali tukiwa tunatenda dhambi. Tunamwamini Mungu na kuyaweka matumaini yetu katika Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu kwa kuamini yale ambayo ameyafanya kwa ajili yetu kwa sababu hatuwezi kujikomboa sisi wenyewe toka katika dhambi zetu.
Hii ndiyo sababu tunapomwamini Yesu na kuutafuta wokovu wetu, ni lazima kwanza tufahamu kuwa ni aina ipi ya imani ambayo ni sahihi. Zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, Yesu alikuja hapa duniani kutuokoa wewe na mimi—na kila mwanadamu wa ulimwengu huu—toka katika dhambi zetu. Alipofikisha miaka 30, alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kwa hiyo akazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake. Ni lazima sisi sote tuuamini ukweli huu. Ni lazima tuamini kwamba Yesu alizipokea si tu dhambi zako na zangu bali dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake, kila dhambi iliyopita, iliyopo, na hata ijayo, zote zilikwisha chukuliwa na Yesu Kristo.
Hata hivyo, watu wengi bado wanaudharau ukweli huu kuwa sio tu dhambi zote za ulimwengu bali pia dhambi zao zilipelekwa kwa Yesu wakati alipobatizwa, na watu hao bado wanaendelea kuamini katika damu ya Msalaba tu. Ndio maana hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kutambua kuwa imani ipi ni sahihi pamoja na kuwa wote wanaona wazi kuwa malango yote ya Hema Takatifu la Kukutania yalifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Wakati Yesu Kristo alipokuja hapa duniani ili kutuokoa, hakutuokoa katika mtindo wa juu juu. Ni kwa sababu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake na akabeba adhabu ya dhambi zetu kwa kusulubiwa kwake ndio maana mimi na wewe tumeokolewa kikamilifu. Hivi ndivyo Yesu Kristo alivyowaokoa wanadamu wote. Hii ndio sababu Bwana wetu alisema, “Wala yeyote ajaye kwangu sintamtupa nje kamwe” (Yohana 6:37).
Tunaposema kuwa tunamwamini Yesu, hatuziamini tabia zake tu, wala hatuziamini nguvu zake tu. Bali, tunaokolewa kwa kuamini kuwa Kristo, pamoja na kuwa yeye ni Mungu kweli, alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zako na zangu katika mwili wake kwa ubatizo wake, na akateketezwa Msalabani kwa ajili yetu. Tunapouangalia wokovu uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania, inakuwa dhahiri na wazi kwetu hasa juu ya imani sahihi ambayo tunatakiwa kuwa nayo pale tunapokiri kumwamini Yesu.
Siku hizi, kuna watu wengi ambao wanaamini katika damu ya Msalaba tu, wanaimba hali wakighadhibisha, “♫Je, unaweza kuwa huru toka katika mzigo wa dhambi? ♪Kuna nguvu katika damu, nguvu katika damu♫,” na wanapiga kelele kiupofu, kwa nia zao wenyewe, “Bwana! Ninaamini!” Kwa watu wa jinsi hiyo, haijalishi wanamwamini Yesu kwa nguvu kiasi gani, hawawezi kuwekwa huru kamwe toka katika dhambi zao kwa kuiamini damu ya Msalaba tu.
Kwa sababu hatuwezi kuwekwa huru kamwe toka katika dhambi zetu katika kipindi chote cha maisha yetu, kwa hakika tunahitaji Mwokozi, na Mwokozi huyu si mwingine bali ni Yesu Kristo. Yesu Kristo aliyekuja kutukomboa wewe na mimi ni Mwokozi, Mfalme wa wafalme, Muumbaji aliyeuumba ulimwengu mzima na vyote vilivyomo ndani yake, na ni Bwana wa maisha yetu. Alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake, na akazisafisha dhambi zetu kwa kufa Msalabani. Kwa maneno mengine, tumeokolewa kwa kumwamini Yesu Kristo, aliyebeba adhabu zote za dhambi zetu kwa ubatizo wake na Msalaba kama Mwokozi wetu. Hivi ndivyo ambavyo lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania linavyotueleza na kutuonyesha kwa wazi.
 

Watu Wanaomwamini Yesu Kidini Tu
 
Katika zama hizi, watu wanadai kuwa wanaweza kuokolewa kwa kuiamini damu ya Msalaba tu. Kufanya madai matupu ya jinsi hiyo si kitu zaidi ya kuifunua imani yao ya kidini. Watu hawa wanasema, “Nilipotoa maombi yangu ya toba kwa Mungu, Roho Mtakatifu alizungumza nami katika moyo wangu, ‘Mwanangu, nimekusamehe dhambi zako.’ Kwa kweli nilishukuru sana nilipoisikia sauti yake!” Wanatoa madai hayo wakisema kuwa imani ya jinsi hiyo ndio ushuhuda wao wa imani.
Lakini wokovu wetu hauji kwa mawazo yetu ya kihisia. Bali, tunaokolewa kwa vipimo vyote vya utu wetu: ufahamu, hisia, na utashi wa dhamira. Kwa maneno mengine, ni lazima tuokolewe kwanza kwa kufahamu jinsi ambavyo Mungu Mwokozi wetu alivyotuokoa, na kisha tuamini hivyo. Lakini vipi kuhusu dini? Ni vitu gani? Dini si kitu kingine bali ni taasisi zilizoundwa na watu kutokana na mawazo na fikra zao.
Zamani, katika familia yangu, mama yangu alikuwa ni mpishi mkuu hotelini. Nilizoea kuwa msaidizi wake, nikimfuata katika jiko lote hali nikimuuliza msaada aliokuwa akiuhitaji—kama vile Yakobo katika Biblia. Wakati mama yangu alipokuwa amebanwa na shughuli nyingi jikoni akiandaa chakula, mimi pia nilikuwa na shughuli nyingi nikiandaa meza ya chakula. Mimi na mama yangu tulikuwa tukifanya muungano mzuri sana. Tulipoamka asubuhi tulikoka moto, tuliandaa meza, na baada ya chakula, tulisafisha sakafu ya jikoni kwa ufagio. Kazi zote za kuchosha za asubuhi zilimalizika kwa ufagio huu.
Hili halikuwa tukio la pekee katika zama hizo huko Korea. Lakini kitu cha kufurahisha zaidi ni kwamba ufagio huu ambao ulitumika katika kusafishia sakafu ya jiko mara nyingine uligeuzwa kuwa ni mungu ambaye anaweza kutupatia kila kitu tunachokiomba. Kwa maneno mengine, kulikuwa na watu walikuwa wakitoa sala zao kwa mifagio hii iliyochakaa. Upuuzi wa jinsi hii ulikuwa ni wa mara kwa mara katika maisha yetu; na sio hilo tu, kila ilipotokea kukawa na bahati mbaya katika familia au majirani, tulizoea kumuita mganga wa kienyeji ili kuja kufanya uganga. Kwa sababu katika zama hizo watu walikuwa wameshikilia imani ya miungu wengi na waliamini kuwa miungu wapo kila mahali, na si kwa ufagio tu uliotumika katika kusafishia sakafu ya jiko ambao uligeuzwa kuwa mungu, bali hata mabamba ya wazee wao wa zamani ambamo majina ya mababu zao yaliandikwa, pia mwamba mkubwa mlimani, au kitu chochote ambacho kilionekana mbele yao kuwa kinaweza kugeuzwa kuwa mungu.
Baada ya muda kupita, siku hizi watu wameendelea kutoka taratibu katika aina hii ya ujinga, lakini kwa wakati huo lilikuwa ni jambo lililotokea mara kwa mara kiasi kwamba kitu chochote kiliweza kugeuzwa kuwa mungu. Kwa hiyo, miongoni mwa biashara zilizokuwa zimechangamka katika zama hizo ni pamoja na biashara ya kufanya uchawi na uganga. Ninakumbuka nilikuwa nikiwaona waganga na wachawi wakinena maneno yasiyoeleweka wakati walipokuwa wakifanya uganga na uchawi wao. Nilizoea kuigiza namna ya kuimba maneno ya kunuizia ya wachawi na waganga nikisema, “Abrakadabra Abrakadabra, mwanga na ujitokeze, mwanga na ujitokeze, kila kitu ni changu pale mwanga utakapotoka. Belo la maboga lilivunjwa kwa sababu ya ukosefu wa kujitoa. Abrakadabra Abrakadabra.” Kwa kweli sikuwa nafahamu kuwa maneno haya yalikuwa na maana gani.
Wakati uganga na uchawi wa jinsi hiyo ulipofanywa katika moja ya nyumba za majirani, kila mtu kijijini alikusanyika ili kujionea. Mkazo wa matukio kama hayo ulikuja pale ambapo malipo yalijazwa katika kichwa cha nguruwe aliyekufa, na aliyekuwa akitabasamu bila ishara. Kiasi cha malipo kilichojazwa kilitumika katika kutathmini manuizio ya mganga na uwezo wake. Uganga na uchawi wa jinsi hii uliendelea usiku mzima hadi pale mwanga utakapojitokeza.
Miongoni mwa mahusiano mengi ya zamani, kulikuwa na mtu mmoja aliyedai kuwa na zimwi bikira. Alizoea kudai kuwa aliweza kuyaondoa mapepo yaliyo mengi ati kwa sababu alikuwa na zimwi hili bikira—iliaminika kuwa mazimwi bikira yalikuwa na nguvu zaidi kuliko aina nyingine za mapepo na mazimwi. Alisema kuwa ikiwa atakutana na pepo mwenye nguvu zaidi, yeye mwenyewe atanyongwa badala ya kuliondoa pepo hili, lakini hakuwahi kusema kuwa anaweza kuyaondoa mapepo yote. Na mtu huyu si mwingine bali ni mchawi.
Mtu huyu aliutumia muda wake katika hali ya kawaida kama mtu mwingine yeyote. Lakini ilipotokea mtu akamwomba kupunga mapepo, alibadili mavazi yake na kuvaa mavazi rasmi ya kichawi na akafanya onyesho lake la kushangaza. Ni kwa sababu mioyo ya watu imegubikwa na mawazo hayo ya kishirikina kiasi kuwa wanazifuata dini hizi za kipuuzi ambazo hazijishughulishi kwa lolote na Neno la Mungu na zinazoishia kuamini vitu vya kipuuzi na vya aibu.
Kwa meneno mengine, watu wamejifanyizia dini zao wenyewe. Kama ilivyo kwa hadithi hiyo hapo juu, wamejitengenezea miungu yao wenyewe. Kwa sababu watu wana aina hii ya tabia, hata wanapokuwa Wakristo, wanapoelezwa kuwa Yesu alisulubiwa kwa ajili yao, basi wanaweza kuzidiwa na hisia zao juu ya jambo hili na mwisho wanaishia kumwamini Yesu kwa upofu. Na wanapoambiwa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na Muumbaji aliyeumba ulimwengu mzima, wanafurahi sana, na kwa mara nyingine wanaamini pasipo utaratibu maalum. Pia wanapenda kusikia, “Mimi ni njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba bali kwa njia ya Mimi,” kisha wanaamini tena pasipo utaratibu na ufahamu mzuri. Kwa kuwa Neno la Mungu halina makosa, basi pale wanapolisikia Neno zuri kwa mara ya kwanza, wanachoweza kusema ni kuwa wanampenda Yesu.
Lakini Yesu atakuja kuwahukumu watu hawa ambao mioyo yao inabakia kuwa ni yenye dhambi ingawa wanaikiri imani yao katika Yesu. Pia atakuja kuwachukua wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho. Watu wengi ambao hawaufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho na wanaomwamini Yesu kwa kuyategemea mawazo yao binafsi ndipo hatimaye watatambua, kuwa kwa miaka 10 tangu walipoanza maisha yao ya kidini bado wamebaki kuwa ni wenye dhambi ambao hawawezi kuishi kwa kuifuata Sheria ya Mungu.
Mimi pia nilizoea kumwamini Yesu kijuu juu. Nilizoea kuimba sifa wakati wote, kwa ufupi nilifurahi sana kukutana na Kristo. Lakini baada ya kumfahamu Yesu, nilikuja kuitambua Sheria, na baada ya kuitambua Sheria, ndipo nilipozitambua dhambi zengu. Baada ya kuzitambua dhambi zangu, ndipo nilipotambua kuwa kutakuwa na hukumu ya milele ya dhambi, na kama matokeo ya kutambua hivyo nilianza kuteseka kwa sababu ya dhambi.
Ili kutatua mateso haya ya dhambi, basi nilitoa maombi yangu ya kweli ya toba. Hata hivyo, imani ya jinsi hiyo ilikuwa ni kama imani ya kishirikina ambayo kwa hiyo watu waliomba ili waweze kubarikiwa kwa kila kitu. Kwa sababu moyo wangu ulisumbuliwa sana baada ya kuifahamu Sheria iliyoandikwa katika Neno la Mungu na baada ya kuzitambua dhambi zangu, nilifikiria kuwa ni lazima nitoe sala zangu za toba, na kwa kweli sala hizo za toba ziliniletea kwa sehemu mapumziko ya kihisia. Lakini dhambi ilibakia katika dhamiri yangu, na nikatambua kuwa nafsi yangu ilikuwa bado katika utumwa wa dhambi, kwa hiyo nikaendelea kuteseka.
Kwa njia hii, si kwa sababu nilikuwa nimefungwa na dhambi zangu ndipo nikaja kumwamini na kumpenda Yesu, bali kwa sababu nilikuwa nimemwamini Yesu ndipo nikaja kuzitambua dhambi zangu, na ilikuwa ni pale nilipozitambua dhambi zangu ndipo mateso yakanijia. “Pengine nimemwamini Yesu mapema mno,” nilifikiria, na niliishia kujuta kuwa nimemfahamu na kumwamini Yesu mapema mno katika ujana wangu. Hata hivyo, sikuweza kujizuia kumwamini Yesu. Hivyo, ili kujiondoa toka katika kongwa hili la utumwa wa dhambi, nilizitoa sala zangu za toba, lakini, kimsingi sala hizi zilinisaidia kidogo sana katika kutatua tatizo hili. 
Watu wa kawaida hawazifahamu dhambi ambazo wamezitenda hata pale wanapozitenda, lakini wanapoanza kwenda Kanisani ndipo wanapoisikia Sheria na ndipo wanapoanza kuzitambua dhambi zao, na hivyo wanajikuta wamefungwa katika dhambi zao. Ndipo wanapojaribu kulitatua tatizo la dhambi zao kwa kutoa maombi yenye hisia ya toba, lakini kadri muda unavyozidi kwenda, ndivyo wanavyozidi kutambua jinsi walivyofungwa katika dhambi zao na kwamba ni lazima wasamehewe dhambi zao.
Haijalishi jinsi ambavyo wanatoa maombi yao ya toba, kadri wanavyozidi kuomba, ndivyo wanavyozidi kuzitambua dhambi zao, ndivyo zinavyozidi kufunuliwa vizuri zikiwakumbusha zaidi juu ya wakati wao uliopo. Inapofikia mahali kama hapa maisha ya kidini ya watu wa jinsi hiyo yanageuka kuwa yenye maumivu na wanaendelea kuteseka. Wanajikuta wakishangaa, “Nilijisikia vizuri sana nilipoamini mara ya kwanza, lakini kwa nini ninajisikia vibaya zaidi sasa kuliko miaka 5, 10 iliyopita? Kwa nini ninasumbuliwa zaidi?” Wanatambua kuwa hata msimamo wao wa wokovu, ambao ulikuwa imara sana walipoamini kwa mara ya kwanza kuwa haupo tena. Hali wakifikiri kuwa wamekuwa ni wenye dhambi baada ya kumwamini Yesu, wanaamua kutumia aina zote za mafundisho katika imani zao na mwishowe wanaishia kuwa ni watu wa dini.
Ni kwa sababu watu hawa hawaufahamu ukweli kuwa Yesu amewaokoa toka katika dhambi zao kwa nyuzi zake za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ndio maana wanajikuta wakiishia kuwa ni wana dini. Ingawa wanakiri kumwamini Yesu, lakini bado wanasumbuliwa, kwa sababu mioyo yao haina amani. Watu wa jinsi hiyo hawawezi hata kukimbilia kubadili miungu mingine, kwa kuwa hata kama wakijaribu, ukweli unabaki kuwa wanafahamu tayari kuwa kukiamini kitu chochote zaidi ya Mungu ni kutenda dhambi ya kuabudu sanamu. Kwa sababu wanafahamu kwa wazi kuwa Yesu ndiye Mwana wa Mungu, na kwa kwamba yeye mwenyewe ni Mungu, na kwamba yeye ni Mwokozi wao, kwa hiyo hawawezi kuabudu miungu tofauti. Na kwa sababu hawaufahamu ukweli, wanaendelea kuishi katika mateso hali wakisumbuliwa na dhambi zao mara kwa mara.
Hii ndiyo sababu kwamba ni lazima wamfahamu na kumwamini Yesu Kristo kwamba alikuja kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Pia Wakristo hawa wanaoishia kuwa ni wana dini wanafahamu kuwa Yesu ni Mfalme, na kwamba aliimwaga damu yake Msalabani, na kwamba Neno la Biblia ni Neno la Mungu.
Hata hivyo, wasichokifahamu ni kuwa Yesu hakuzichukua dhambi zao tu bali dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake, na ujinga huu wa kutokufahamu ndio sababu inayowafanya waishi kama wenye dhambi hata pale wanapoikiri imani yao, na hii ndio sababu wataishia kwenda katika sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya wenye dhambi. Kwa sababu Wakristo wana dini wa jinsi hiyo hawafahamu jinsi ambavyo Yesu alizishughulikia dhambi zao, wanaamini katika hisia zao binafsi kila wanaposimama. Kama matokeo ya imani yao, ukweli halisi hauendani na kile wanachokiamini, kama vile kipofu anapojaribu kumchora tembo kwa kujaribu kuvigusa viungo vyake. Ndio maana hawatambui kabisa makosa katika imani yao, na ndio maana wanaishia katika machafuko tena.
 

Nini Kitatutokea Ikiwa Hatuamini Katika Ukweli wa Nyuzi za Bluu?
 
Nini kitatutokea ikiwa tungemwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wetu hali tukiwa tumeziacha nyuzi za bluu nje ya lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania? Wakati Mungu alipoamuru kulijenga lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kufuma nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, je Mungu angesema nini ikiwa Musa angewaeleza waisraeli kulitengeneza lango kwa nyuzi za zambarau, nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, halafu waisraeli wakalikamilisha lango kwa namna hii? Je, Mungu angelikubali hilo lango kuwa ni lango la Hema lake Takatifu la Kukutania? Kwa hakika, asingelikubali hilo lango. Kwa sababu Mungu aliwaambia waisraeli kulijenga lango la Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi za rangi nne tofauti, ikiwa lingejengwa tofauti, lisingeweza kamwe kuitwa lango la Hema Takatifu la Kukutania. Hakuna hata uzi mmoja kati ya hizo nyuzi nne unaoweza kuachwa.
Lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania lilitakiwa kufumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa sababu Yesu, ambaye ni Mungu mwenyewe, alikuja hapa duniani kama Mwokozi wetu katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, akafa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo amezisafisha dhambi zetu zote zikawa nyeupe kama theluji, ni kwa kuamini katika huyu Yesu Kristo sisi tumekombolewa toka katika dhambi zetu. Rangi za lango la Hema Takatifu la Kukutania zinatueleza sisi jinsi tunavyopaswa kumwamini Yesu ili tuweze kuokolewa toka katika dhambi zetu. Wale wanaouamini ukweli uliodhihirika katika lango la Hema Takatifu la Kukutania wote wameokolewa toka katika dhambi zao. Wote wamepokea ondoleo la dhambi zao, zimekuwa nyeupe kama theluji. Yesu Kristo ameziosha dhambi zako na zangu, ametugeuza tumekuwa weupe kama theluji. Yesu Kristo amefanyika Mwokozi halisi wa kwako na wa kwangu.
Huu ndio ukweli halisi uliodhihirishwa katika lango la Hema Takatifu la Kukutania. Hata hivyo kuna watu wengi siku hizi ambao hawaiamini maana ya nyuzi za bluu, hata pale wanapokiri kuamini maana ya nyuzi za zambarau na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Ili kufanya utatifi wa mwanzo wa kitabu hiki, kwanza nilienda katika duka la vitabu vya Kikristo. Nikavikuta vitabu kadhaa kuhusu Hema Takatifu la Kukutania vilivyoandikwa na baadhi ya viongozi mashuhuri wa Kikristo. Hata hivyo, baadhi ya vitabu hivyo havikuzungumzia kabisa lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, wakati vitabu vingine vilitoa maelezo yasiyothibitishwa kama ifuatavyo: “Je, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa za ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatueleza nini? Bluu ni rangi ya anga, na kwa hiyo inatueleza kuwa Yesu ni Mungu. Rangi nyekundu inamaanisha damu ya thamani ya Yesu aliyoimwaga Msalabani alipokuja hapa duniani. Rangi ya zambarau inatueleza kuwa Yesu ni Mfalme.”
Aina hii ya ufafanuzi ni njia iliyo nje ya alama. Kwamba Yesu ni Mungu inaelezwa katika nyuzi za zambarau. Wakati Mungu amekwisha tuambia kupitia nyuzi za zambarau kwamba Yesu ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabawana, kwa nini arudie jambo hili kwa nyuzi za bluu tena? Ni kwa sababu hawa watu hawafahamu fumbo la nyuzi za bluu ambalo wameshindwa kulifafanua vizuri.
Kwa sababu wanaifahamu damu ya Msalaba tu, basi wanaweka msisitizo mkubwa katika nyuzi nyekundu tu. Tunapoiona michoro yao ya lango la Hema Takatifu la Kukutania, tunaona kuwa imetawaliwa na rangi nyekundu na nyeupe. Wakati rangi nne za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni lazima zionekane vizuri katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, michoro yao inaonyesha rangi nyekundu na nyeupe tu, pamoja na kiasi cha rangi ya zambarau, lakini hawaweki rangi ya bluu kabisa.
Kuna watu wengi sana katika ulimwengu huu ambao wanazungumza juu ya imani hiyo potofu pasipo kuutambua ukweli wa nyuzi za bluu. Kuna watu wengi sana katika nyakati za sasa ambao wanadai kuwa wanaweza kuokolewa kwa kuiamini kipekee damu ya Yesu Msalabani, hata pale ambapo hawatambui kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake mara moja na kwa wote ili kubeba hukumu yetu ya adhabu. Mioyo ya watu ya jinsi hiyo inabakia kuwa ni yenye dhambi. Watu wa jinsi hiyo wanabaki kusumbuliwa kwa kuwa hawawezi kuwekwa huru toka katika dhambi zao, wanabaki wakisumbuliwa hivyo leo, kesho, na baadaye. Kwa hiyo baadhi ya watu wanakiri kuwa, “Mimi ni mwenye dhambi mbele za Mungu mpaka nitakapokufa.” Lakini, hii ni imani sahihi, kwamba watabakia kuwa wenye dhambi hadi kifo chao hata pale wanapomwamini Yesu?
Baada ya kumwamini Yesu, je, ni lini hasa tunapofanyika wenye haki? Je, mbingu si mahali palipohifadhiwa kwa ajili ya watu wasio na dhambi kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu? Kwa hakika, mbinguni ni mahali pa wenye haki, na wala si mahali pa wenye dhambi. Ni wenye haki tu ambao wameokolewa kikamilifu toka katika dhambi zao ndio wanaoweza kuingia mbinguni.
Wale ambao wanajitangaza wenyewe kuwa ni wenye dhambi hadi kifo hata pale wanapomwamini Yesu kwa kweli hawana uhakika wa wokovu wao; haijalishi ni mara ngapi wamekuwa wakiikiri imani yao katika Yesu, kwa kuwa hawazifahamu nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Hata pale wanapomwamini Yesu na kumwomba, bado hawana uhakika kuwa maombi yao yatajibiwa. Ingawa wanamwamini Yesu, hawasaidiwi na wala hawapendwi na Yesu. Wanaweza kuhisi kuwa wanapendwa pale wanapoonyesha kujitoa kwao, lakini wanapoacha kufanya tendo hilo la kujitoa, wanajihisi kana kwamba wameachwa na Mungu, kana kwamba wanachukiwa na Mungu. Wanafikiri kuwa Mungu anawapenda na anawabariki pale tu wanapotoa sadaka zao na kujitoa kwake, na kwamba hawapendi kabisa pale wanaposhindwa kumtolea sadaka zao. Wanapokutana na nyakati ngumu, wanafikiri kuwa Mungu anawachukia, wanashindwa kufahamu kuwa ni kwa nini wanapaswa kuzipitia nyakati ngumu kama hizo, na mwishowe wanaishia kumlaumu Mungu kutokana na matatizo yao na wanaacha kabisa kumwamini.
Mwishoni, uaminifu kati ya watu wa jinsi hiyo na Mungu unavunjika. Kwa sababu imani yao ni matokeo ya mawazo na hisia zao binafsi, ni imani isiyo na msingi maalum, ya hatari, na potofu. Tunapomwendea Mungu, ni lazima tuweke mbali misukumo na hisia zetu. Tunapomwendea Mungu, ni lazima tumwendee na imani yetu ambayo inaamini katika ukweli kuwa Yesu Kristo ametuokoa sisi ambao tulifungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu kwa ubatizo wake na damu yake. Mbele ya Neno la Mungu na Neno la Sheria, mbele ya injili ya maji na Roho, na kwa dhamiri zetu pia, ni lazima tutambue kuwa sisi ni wale ambao tulipaswa kufungwa kuzimu pasipo kasoro yoyote. Ni pale tu tunapotambua, tunapojifunza, tunapoamini, na kuamini jinsi tulivyo wenye dhambi na jinsi ambavyo Mungu ametuokoa toka katika dhambi zetu ndipo tunapoweza kutambua kuwa Yesu Kristo amekwishafanyika Mwokozi wetu wa kweli.
 

Ni Kwa Imani ya Kweli Tu Ndipo Tunapoweza Kupokea Zawadi ya Wokovu
 
Kwa hiyo, wewe na mimi ni lazima tutambue kwamba tunaokolewa toka katika dhambi zetu kwa kuamini katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na si kufanya matendo mema kwa kujitegemea sisi wenyewe. Na ni lazima tufahamu na kuamini kuwa ili kutuokoa toka katika dhambi zetu, Yesu Kristo alikuja kwetu kwa wazi katika ukweli huu wa pembe nne. Aliahidi katika Agano la Kale kuwa atakuja kama Masihi, na kama alivyoahidi, kwa kweli alikuja hapa duniani, na kwa ubatizo wake, alizichukua dhambi zetu na dhambi za wanadamu wote katika mwili wake mara moja na kwa wote. Kisha akazibeba dhambi hizi za ulimwengu Msalabani, akasulubiwa, akamwaga damu yake ya thamani, na akafa baada ya kutamka, “Imekwisha!” (Yohana 19:30) Baada ya kufufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu, alishuhudia kwa siku 40 zaidi na kisha akapaa mbinguni katika mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu huku akiahidi kurudi. Ni lazima tuyaamini mambo haya.
“Nimekuokoa kikamilifu kwa huduma zangu za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Na nitakuja tena kuwachukua wale wanaouamini ukweli huu wa wokovu. Pia nitawapatia haki ya kufanyika wana wa Mungu. Kwa wale wanaouamini ukweli huu katika mioyo yao, nitazisafisha dhambi zao na kuzifanya kuwa nyeupe kama theluji, nitawapatia Roho Mtakatifu, na nitawafanya kuwa wana wangu.” Hivi ndivyo ambavyo Bwana wetu ametuambia.
Ni lazima tuliamini Neno hili. Bwana wetu amekwisha zitimiza ahadi hizi, na kwa hakika anafanya kazi katika maisha ya wale wanaoamini hivyo katika dunia hii. Anawalinda wale wanaouamini ukweli huu na anawashuhudia. Hivi ndivyo tulivyookolewa kupitia kazi za Bwana wetu za ubatizo na damu, kuishi kwa neema, ulinzi na upendo wa Mungu, na kuishi maisha ya wenye haki. Ni kwa sababu ametuokoa ndio maana tumekombolewa toka katika dhambi zetu kwa kuamini.
Wakati kitabu hiki kinachohusu Hema Takatifu la Kukutania kinapotafsiriwa katika lugha zote za ulimwenguni, ninaamini kuwa watu wa ulimwengu mzima wataokolewa toka katika dhambi zao kwa kupitia imani yao katika ukweli huu. Wale wanaodai kuwa ondoleo la dhambi linakuja kwa damu ya Yesu tu hawataweza kamwe kuendelea kutoa madai kama hayo, badala yake watakuja kutambua jinsi ambavyo madai yao yalikuwa ni ya uongo. Hawataweza kamwe kuendelea kushikilia kitu ambacho si cha kweli na kudai kuwa huu ndio wokovu. Hawataweza kusema kwamba wanaokolewa kwa kuiamini damu ya Yesu tu.
Katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania inapatikana injili ya maji na Roho, Neno la wazi la wokovu la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa sababu hili ni Neno la Mungu lililoahidiwa na kutabiriwa toka katika Agano la Kale, na kwa sababu Mungu ameitunza ahadi hii katika Agano Jipya kwa kuutimiza wokovu toka katika dhambi zote kwa ubatizo wake na kwa kusulubiwa kwake, ikiwa tutaiamini zawadi hii ya wokovu katika furaha na shukrani, basi sisi sote tunaweza kupokea ondoleo la dhambi la milele.
Hili ni Neno ambalo ni rahisi na sahihi, lakini pia ni ukweli ambao hauwezi kufahamika kwa ufahamu wote wa ulimwengu mzima, ikiwa hauna imani halisi katika Neno lake. Ndio maana ni lazima tuliamini Neno lake kama lilivyo. Kwa sababu ni ukweli wenye thamani ambao hatuwezi kubaki wajinga pasipo kuufahamu, wewe na mimi ni lazima tuiamini kwa hakika injili ya maji na Roho. Kwa kutufundisha ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania kwa uhuru na kwa urahisi, Mungu ameturuhusu kuipata zawadi hii ya thamani ya wokovu kwa imani yetu.
Wewe na mimi ambao tunauamini ukweli huu, sisi sote tunamtolea Mungu shukrani zetu kwa upendo wake wa kweli. Lakini kuna watu wengi ambao bado hawaufahamu ukweli halisi wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na wanawafundisha na kuwaongoza watu katika njia zao za upotofu. Tunataka kuueneza ukweli huu kwa watu hao pia. Kwa wale ambao mioyo yao inateswa kwa sababu ya ujinga wa kutokuufahamu ukweli, basi tunawahubiria injili hii ya kweli ya maji na Roho tukitaka wawekwe huru toka katika dhambi zao na kisha waingie katika mlango wa wokovu. Tunapouhubiri ukweli wa Hema Takatifu la Kukutania, wale wanaouamini wataokolewa, lakini wale wasiouamini wataadhibiwa kwa dhambi zao. Ikiwa tumeamua kumwamini Yesu, ni lazima tumwamini hali tukiufahamu ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Hakuna anayeufahamu ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu tangu mwanzo. Mungu ametueleza kuwa, “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Kweli ni nini? Kweli ni injili (Waefeso 1:13), ambayo ni injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kuzifahamu kikamilifu na kuziamini nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ndiyo imani sahihi katika ukweli.
Kwa nini Mungu anasema na hiyo kweli itawaweka huru? Je, mmeokolewa vipi toka katika dhambi zenu? Kwa kuziamini nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, je, si kwamba mmeokolewa toka katika dhambi zenu zote, lakini mioyo yenu pia si makazi ya Roho? Toka katika mioyo yenu na dhamiri zenu, je dhambi zenu zimetoweshwa kikamilifu? Je, unaamini kweli na unaweza kukiri toka katika kina cha moyo wako kwamba Mungu ni Baba yako? Kwa sababu Mungu anawatambua wale wasio na dhambi kuwa ni wana wake, anazikubali imani za wale wanaofahamu na kuamini katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizofumwa katika lango ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Wenye dhambi si wana wa Mungu; wale waliozaliwa upya wanaoamini katika injili ya maji na Roho ambayo ni injili pekee ambayo Mungu ametupatia, hao ndio wana wa Mungu Baba.
Ingawa tunakutana na magumu mengi na mateso mengi tunapoishi katika ulimwengu huu, kwa sababu Mungu anaishi pamoja nasi, kwa kweli tuna furaha. Ingawa tuna mapungufu, tunaishi maisha yetu yaliyobarikiwa hali tukiamini katika haki ya Mungu na huku tukiuhubiri ulimwengu mzima injili ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, injili ambayo inatupatia sisi haki ya Mungu.
Ninamshukuru Mungu sana kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Mara ya kwanza nilipomwamini Yesu, bila kujali jinsi ambavyo nilimwamini kwa nguvu, bado nilibakia ni mwenye dhambi, na nilisumbuliwa sana kwa ajili ya hili. Haijalishi jinsi ambavyo nilikiri kumwamini Yesu kwa uaminifu, bado dhambi iliendelea kuwapo katika dhamiri yangu. Mtu anaweza kufahamu ikiwa yeye ni mwenye dhambi au la mbele za Mungu kwa kuiangalia dhamiri yake mwenyewe. Kwa maneno mengine, wale ambao bado wana dhambi ambazo zimeandikwa katika dhamiri zao ni wale ambao hawajapokea ondoleo la dhambi zao. Ikiwa dhamiri zao zina dhambi hata kama ni ile ndogo, basi huu ni ushuhuda kuwa watu hawa hawajapokea ondoleo la dhambi.
Hata hivyo, wakati nilipokuwa siufahamu ukweli ambao utatatua shida ya dhambi zangu zote, hata zile dhambi ndogo kuliko zote, na wakati ambapo maswali ya aina nyingi yalipojitokeza katika moyo wangu, Mungu alikutana nami kupitia Neno lake la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Neno hili lilipatikana katika injili ya Mathayo ambayo tuliisoma hapo kwanza. Nilipokuwa nikisoma Mathayo 3:13-17, nilikutana na kifungu kinachosema, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” (Mathayo 3:15). Ndipo nilipotambua na kuamini kwamba wakati Yesu alipobatizwa na kupanda toka katika maji, Mungu aliishuhudia haki yake, na haki yote ilitimizwa pale dhambi zote zilipotoweshwa kupitia ubatizo wa Yesu.
Wakati Yesu Kristo alipobatizwa na Yohana, dhambi zangu zote zilipelekwa kwake, na alizishughulikia dhambi zote mara moja pale Msalabani. Ndipo kwa wakati huo nilipotambua na kuamini juu ya sababu zilizomfanya Yesu kubatizwa, matatizo yote na maswali kuhusu dhambi zangu yalijibiwa, dhambi zangu zote zilikatwa mara moja toka kwangu. Nilishukuru sana kwa ukweli huu wa ondoleo la dhambi, kutokana na ukweli kuwa nilipokea ondoleo la dhambi kwa kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, ambayo ni Neno la kweli la Mungu.
Bwana alikuja kwangu kupitia Neno lake lililoandikwa, na nilipokea ondoleo la dhambi zangu kwa kupitia Neno hili la maji na Roho, na kuliamini katika moyo wangu. Tangu wakati huo, kwa kupitia Neno la Agano la Kale na Agano Jipya, nimekuwa nikiishuhudia injili ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kwa watu wengi, na hata sasa, ninaendelea kuueneza ukweli huu na fumbo hili la wokovu. Injili ya kweli si kitu ambacho kimetengenezwa kwa mawazo, mafundisho, au uzoefu wa kihisia wa wanadamu.
Bwana wetu alizitowesha dhambi zetu zote kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, kila mtu katika ulimwengu mzima atakuja kuufahamu vizuri ukweli wa wokovu na kutambua kuwa ukweli huu si mwingine bali ni injili ya maji na Roho. Huu pia ni ukweli ambao unahitajika kabisa katika nyakati za mwisho. Watu wengi wasiohesabika watakuja kuuamini ukweli huu.
Kipindi cha sasa ni kipindi ambacho haki ya watu inavunjika vipande vipande na maovu yao yanazidi kuongezeka sana. Wakati mazingira yanayowazunguka yanapofifia, watu wanaumwaga uovu wote ambao kimsingi ulikuwa umefungwa ndani yao. Lakini pamoja na hili, Bwana wetu ametuokoa wewe na mimi toka katika dhambi zetu kwa kupitia injili ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Baraka hii ya gharama inapaswa kushukuriwa sana. Ninamshukuru Bwana wetu kwa wokovu huu wa wazi, kwa kuwa nimejawa na furaha.
Ulimwengu wa sasa unaelekea katika zama za mwisho zilizotabiriwa na Mungu, na kwa sasa umekwisha ingia katika zama hizo. Katika nyakati kama hizi, wakati kunapokuwa na watu wachache zaidi wanaomtumikia Mungu kwa moyo, na wakati ambapo hata imani ya waamini inadhoofishwa, ikiwa utajaribu kujitoa mwenyewe kwa kitu kingine zaidi ya ukweli wa injili ya maji na Roho, kwa hakika utaishia kuwa na majeraha katika moyo wako. Unapomwamini Mungu, ikiwa hauiamini injili ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, kwa hakika utakatishwa tamaa, kwa kuwa hutapata kitu chochote cha maana katika moyo wako na wala haitazalisha matunda yanayoonekana.
Kwa sababu ukweli wa injili ya rangi nne ya Hema Takatifu la Kukutania—yaani ya nyuzi za rangi ya bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa—ndio ukweli wa wazi, na ni injili pekee ambayo ni nzuri kwa ulimwengu huu wa giza. Kwamba tunaishi maisha yetu hali tukiwa tumepokea ondoleo la dhambi zetu kwa kuufahamu na kuuamini ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania hiyo ni baraka kubwa, na zawadi yenye thamani, na furaha kuu kwetu.
Kwa sababu wale wanaoufahamu na kuuamini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa iliyodhihirishwa katika lango la Hema Takatifu la Kukutania wanautumikia ukweli na si uongo, na kwa kweli furaha kuu inapatikana katika mioyo yao daima.
Je, wewe pia unaufahamu na kuuamini ukweli huu uliofunuliwa katila lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania? Ni lazima uufahamu, na ni lazima uuamini.