Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 8-3] Mkristo ni Nani? (Warumi 8:9-11)

(Warumi 8:9-11)
“Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.”
 

Ikiwa mtu ni Mkristo wa kweli au la mtu huyo anatofautishwa kwa kigezo ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yake au la. Inawezakanaje kwa mtu kuwa Mkristo ikiwa mtu huyo hana Roho Mtakatifu katika moyo wake? Paulo anatueleza sisi kuwa hata kama tunamwamini Yesu hilo sio suala muhimu sana bali ikiwa tunamwamini Yesu hali tukiwa tumeigundua haki ya Mungu au la. Imani ya kweli inayohitajika kwa watakatifu ni ile imani ambayo iko tayari kupokea na kufanywa makao ya Roho Mtakatifu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndio unaoweza kukutambulisha ikiwa wewe ni Mkristo au la. 
Kwa hiyo, Paulo alisema, “Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” Paulo alisema “awaye yote”. Haijalishi ikiwa mtu ni mtumishi, mwinjilisti, au mwanauamsho. Ikiwa mtu hana Roho Mtakatifu ndani ya moyo wake, basi mtu huyo si wake. Ni lazima ukumbuke kuwa ikiwa huamini katika haki ya Mungu ambayo inakuongoza ili uweze kumpokea Roho Mtakatifu, basi wewe ni mwenye dhambi ambaye umepangiwa kwenda kuzimu. Hivyo sisi sote tunapaswa kuizingatia injili ya maji na Roho ambayo ina haki ya Mungu. 
Ikiwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu hii ina maanisha kuwa sisi tunakuwa wafu kwa dhambi kwa kupitia imani yetu katika ubatizo wa Kristo. Lakini roho zetu zinafanywa kuwa hai kwa sababu ya haki mpya tunayoipata. Zaidi ya yote, katika siku ile ambayo Bwana wetu atarudi tena, basi miili yetu ya uharibifu itapokea pia. Hii ndiyo sababu tunapaswa kumfikiria yule ambaye ametupatia Roho Mtakatifu. 
Ikiwa hauna imani inayoamini katika haki ya Mungu basi wewe si wa Kristo. Kwa upande mwingine, ikiwa una imani hii katika haki ya Mungu basi Roho wa Mungu anakaa ndani yako. Pasipokuwa na imani hii, Roho Mtakatifu hawezi kukuongoza. Kwa hiyo, ikiwa hauna Neno la ukombozi ambalo lina haki ya Mungu basi wewe si wa Kristo hata kama utaendelea kuikiri na kuikariri Imani ya Mitume katika kila ibada ya Jumapili. Ikiwa wewe si wa Kristo roho yako italaaniwa na itakuongoza katika uharibifu na maangamizi ya milele hata kama utajitahidi kufanya mema kiasi gani.