Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 8-6] Wale Waurithio Ufalme wa Mungu (Warumi 8:16-27)

(Warumi 8:16-27)
“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu tukikutazamia kufanywa wana, yaani ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? Basi tukikitarajia kitu tusichokiona twakingojea kwa saburi. Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.”
 

Watu wote ambao wamesamehewa dhambi zao wanaamini katika injili ya maji na Roho na wana Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Katika 1 Yohana 5:10 Biblia inasema, “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake”. Yeye aliye na haki ya Mungu katika moyo wake anaye huyo Roho Mtakatifu ndani yake, na ni imani katika injili ya maji na Roho inayomfanya Roho Mtakatifu aweze kukaa milele katika moyo wa mtu. 
Tulifanyika watoto wa Mungu kwa dhambi zetu kusamehewa kwa kupitia imani yetu katika injili ya maji na Roho. Roho Mtakatifu amekaa katika mioyo yetu na amefanyika kuwa shahidi wetu hali akisema, “Ninyi ni watoto wa Mungu na watu wake.” Kwa wale wasio na Roho Mtakatifu katika mioyo yao, Sheria inawashuhudia ikisema, “Ninyi si watoto wa Mungu, bali ninyi ni wenye dhambi.”
Kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho, Roho Mtakatifu anawashuhudia, “Ninyi ni watoto wa Mungu. Ninyi ni watu wa Mungu msio na dhambi.” Mungu aliliweka jambo hilo wazi ili kwamba tuweze kutambua kuwa ili kufanyika watoto wa Mungu basi ni lazima tumaini katika injili ya maji na Roho. 
Unaweza kujiuliza, “sijisikii chochote, je, hiyo ina maanisha kuwa mimi si mtoto wa Mungu?” Baadhi ya watu bado ni wachanga sana katika imani zao na wanaweza wasitambue kuwa wana Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Lakini Roho Mtakatifu anatuthibitishia kuwa hata kama tuna nafsi zenye mashaka, Roho anatufurahisha kwa kusema, “Oyaa! Wewe ni mtoto wa Mungu! Kwa kuwa unaiamini basi wewe ni mtu wa Mungu.” Ikiwa tunaamini katika injili ya maji na Roho, basi hata pale tunapokuwa na mashaka tunabakia kuwa ni watoto wa Mungu. Roho Mtakatifu anashuhudia kuwa sisi tu watoto wa Mungu. Roho Mtakatifu si kitu kinachokaa katika mioyo yetu kwa kupitia fahamu zetu na hisia. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho hawana dhambi katika mioyo yao, na kwa kuwa hawana dhambi, basi Roho Mtakatifu anakaa ndani yao. Kwa hakika wao ni watoto wa Mungu. 
Roho Mtakatifu anatueleza sisi katika mioyo yetu kuwa, “Mnamwamini Yesu, Msalabala wake, na mmesamehewa; basi kwa hiyo hamna dhambi na ninyi ni watoto wa Mungu.”
Hata hivyo, ushahidi wake hauji katika sauti kama ile ya mwanadamu. Hivyo, usitarajie kusikia sauti ivumayo! Ikiwa unatamani kuisikia sauti basi Shetani anaweza kupenyeza sauti yake kama mwanadamu na kisha akajaribu kukujaribu. Shetani anafanya kazi kwa kupitia katika mawazo ya watu wakati Roho Mtakatifu anatenda kazi kwa mujibu wa Neno la Mungu. 
 

Wale Walio na Haki ya Mungu Ndio Watoto na Warithi wa Mungu
 
Hebu tusome aya ya 17 kwa pamoja. “Na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.”
Ikiwa sisi tu watoto wa Mungu, basi sisi pia ni warithi wa wake. Mrithi ni yule anayepokea kila kitu toka kwa wazazi wake. Kwa maneno mengine, tuna haki ya kushiriki katika kila kitu ambacho Mungu anacho. Kama ningeuliza, “Nani ni warithi wa Mungu Baba?” bila shaka tunaweza kujibu, “Warithi wa Mungu ni watu wanaoamini katika injili ya maji na Roho na waliosamehewa dhambi zao.” 
Watu walio na aina hii ya imani wamebarikiwa na wataurithi utukufu wa Mungu katika Ufalme wa Mungu pamoja na Kristo. Maandiko yanasema kuwa kwa kuwa sisi tu warithi pamoja na Kristo, basi ili tuweze kutukuzwa pamoja naye ni lazima na sisi tuteswe pamoja naye. Kuwa warithi pamoja na Kristo maana yake ni kuishi katika Ufalme wa Baba yetu milele. Ikiwa unaamini katika injili ya maji na Roho, basi wewe ni mrithi pamoja na Kristo. Sisi tu warithi kwa kuwa tutarithi kila kitu ambacho Baba yetu anacho. 
Kwa nyakati mbalimbali, ninauhisi Ufalme wa Mungu ukitukaribia. Kila kinatokea kwa wakati wake mzuri. Ahadi za Mungu katika Biblia zinatimizwa moja baada ya nyingine. Sasa kilichobakia ni kwa watu wa Israeli kutubu, kumkiri Yesu kuwa ni Mwokozi wao, na kisha kuokolewa toka katika dhambi zao na mambo mengine machache. Israeli inatakiwa kumpokea Yesu kuwa ni Mwokozi wao katika kipindi cha miaka Saba ya Mapigo. 
Kutambulika kwa Ufalme wa Mungu duniani na Mbinguni kunahusiana kwa karibu na toba ya Waisraeli. Ninaamini kuwa siku ya mwisho itakuja karibu. Ninaamini kuwa siku i karibu wakati wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho watakapoishi pamoja na Mungu milele. Ulimwengu mzima ulisubiri kuja kwa mwaka 2000 na ilidhaniwa kuwa huenda ikawa ndio siku ile ya mwisho, lakini mwaka 2000 umepita. Ile hofu kuhusiana na mwisho wa Milenia imeshapita na sasa tupo nusu ya mwaka 2002 na katika kipindi ambacho watu wengi walifikiri kuwa mabadiliko mengi duniani yangalitokea katika mwaka wa 2000. 
Hata hivyo, Ufalme wa Kristo ambao umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu sasa umekaribia na unaendelea kukaribia kwa kila mmoja wetu. Pia Roho Mtakatifu anatuongoza sisi ambao tulishasamehewa dhambi zetu kuhisi kule kukaribia kwa Ufalme wa Mungu. Sasa, kama hapo kabla, kila kitu kitatimizwa kama Mungu alivyosema. Hebu tuisubirie siku ile kwa imani. 
Hapo baadaye, Isareli itafanyika kuwa jiwe la kujikwaa na kizuizi kuhusiana na amani ya ulimwengu, na kwa sababu hii itajipatia uadui toka kwa mataifa mengi. Hivi ndivyo Biblia inavyotueleza—kuwa Israeli itakuwa adui wa wengi na baadhi ya Waisraeli watatambua ya kuwa kwa hakika Masihi ambaye wamekuwa wakimsubiri kwa miaka mingi alikuwa ni Yesu. Watasamehewa dhambi zao kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Kile ambacho Mungu amekipanga kinakaribia kutimizwa muda si mrefu. Hata hivyo, mambo haya yote yatatokea kwa wakati wake, hivyo hatupaswi kuyasubiria mambo hayo kutokea kwa tarehe maalum kama ambavyo baadhi ya waeskatolojia wanavyotabiri. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho watapata nafasi ya kuona unabii wa Mungu ukikamilika. Waamini wana tumaini ya kuwa Ufalme wa Mungu uliotabiriwa hapa duniani na Ufalme wa Mbinguni unakuja. Ninaamini kuwa siku hiyo inatukaribia. 
Wakati utafika hivi karibuni ambapo yale mambo ambayo Bwana ameyaahidi yatatokea kweli moja baada ya jingine. Nina ujasiri kuwa siku ile wakati Ufalme wa miaka Elfu Moja na Ufalme wa Mungu ulioahidiwa na Mungu vinatukaribia. Hali ukiwa umevuviwa na Roho Mtakatifu, Je, wewe pia unafikiria kama ninavyofikiri? Je, unaamini kuwa kila unabii wa Mungu utatimizwa kwa kupitia Roho Mtakatifu? Roho Mtakatifu anatusaidia kuziamini kiukweli ahadi za Mungu kwa mioyo yetu yote. 
Kwa kupitia Roho Mtakatifu tuna hakika katika mioyo yetu kuwa ahadi za Mungu kuhusiana na siku za mwisho zinakuja hivi karibuni. Tunaamini kwa kupitia Roho Mtakatifu kuwa kile kinachopita katika fikra zetu na matumaini yetu kitakuwa kweli pamoja na unabii wa Mungu. Na hii ndiyo imani ya kweli. 
Wewe na mimi ni warithi wa baraka za Mungu zilizoahidiwa; kwa hiyo tunapaswa kusubiria hali tukiwa ndani ya Roho Mtakatifu. Ufalme wa Mungu utakuja kwetu hivi karibuni. Waisraeli watafikia hatua ya kumwamini na kumpokea Yesu Kristo kuwa ni Masihi wao hivi karibuni. 
Watu wengi wanamsubiri Yesu Kristo hali wakisema, “Tafadhali na uje Bwana Yesu.” Paulo alisema kuwa kwa kuwa alikuwa ni mrithi wa Mungu, basi yale mateso ambayo aliyapitia hayakuweza kufananishwa na ule utukufu ambao alikuwa akiutarajia kuupokea. Hii ina maanisha kuwa ili kuupokea utukufu pamoja na Kristo basi inatuapasa kuteseka pamoja naye. Hii ni kwa sababu tunaamini na tunausubiria Ufalme wa Mungu ili uje. Ili kupokea utukufu pamoja na Kristo basi inatupasa kuteseka pamoja naye. 
Tumaini la Paulo lilikuwa ni kwa uumbaji wote wakiwemo wanyama na mimea, yaani kuwekwa huru toka katika kifo. Hii ndiyo sababu uumbaji wote unasubiria kwa hamu ujio wa watoto wa Mungu. Tumaini juu ya watoto wa Mungu ni kwamba siku ile itakuja ambapo viumbe vyote vitaweza kuishi milele. 
Kwa hiyo, ni lazima tutambue kuwa sisi waamini tumebarikiwa kwa maisha ya milele. Tunapaswa kuendelea kuisubiri siku hiyo tukiwa hai au hata kama Bwana atatufufua toka katika usingizi wa mauti ili kutuchukua pamoja naye. 
 

Je, Ule Utukufu wa Mungu Utakaofunuliwa Kwetu Ni Mkuu?
 
Utukufu ambao utafunuliwa mara kwa wenye haki ni utukufu wa milele—unaohusisha kuurithi Ufalme milele na kuishi milele katika utukufu wa Mungu. Hakutakuwa na kifo tena, hakuna huzuni, hakuna kulia. Katika Ufalme wa Mungu hakutakuwa na maumivu, na Ufalme huo hauhitaji jua wla mwezi kwa kuwa utukufu wa Mungu utaung’azia. Mwanakondoo atakuwa ndiye mwanga wake. Ni mahali ambapo ni Yesu tu pamoja na wale waliozaliwa tena upya, yaani waamini wasio na dhambi watakapokuwa, na patajazwa na utukufu wa Mungu. Ufalme utajazwa na miale ya dhahabu. Ule utukufu wa Ufalme wa Mungu ambapo tutaishi milele umejazwa na utukufu ambao hauwezi kuelezewa. Kwa kuwa utukufu huu tunaousubiria ni mkuu sana, basi Paulo anatueleza sisi kuwa mateso tunayoyapata kwa sasa hayana lolote ukilinganisha na ule utukufu ambao utafunuliwa kwetu. 
Wakati fulani tunaweza kuuona utukufu wa Mungu katika hali ya kiasili wakati tunapomtumikia Mungu katika ulimwengu huu. Tunapoyaangalia maua yenye rangi mbalimbali, nyasi ndefu, uoto wa asili unaonekana katika matawi ya majani yanayong’aa, hali ya hewa ya joto katika majira ya kuchipua, ubora wa misitu, upepo safi, nyota ambao zinang’aa kwa utukufu katika giza; basi tunapoyaangalia yale majira manne hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kufikiria jinsi Mbingu itakavyokuwa bora. Tunapoyaangalia maajabu haya yote ya uumbaji wa Mungu, basi tunatumaini kuwa Ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni. 
Wakati Ufalme wa Mungu utakapokuja, hakutakuwa na kifo tena na tutaishi kwa utukufu. Hakutakuwa na kitu kinachokosekana na kwa sababu hiyo tutaishi kwa furaha na mafanikio. Kule kufikiria tu kuwa nitaishi kwa utukufu mahali ambapo kila kitu ni kikamilifu na sahihi basi hali hiyo tu inaujaza moyo wangu kwa utukufu wa Mungu. Ule ukweli kuwa vitu hivyo vyote vitakuwa vyetu sisi waamini, kwa kweli ni kama ndogo, na inatufanya sisi kushukuru zaidi na zaidi kwamba tumezaliwa tena upya kwa faida. Ninamshukuru Bwana ambaye ameujaza moyo wangu kwa tumaini kamilifu. 
Sasa tunaweza kuwa na tumaini la Mbinguni katika fikra zetu, lakini tunafahamu kuwa hapo baadaye, ahadi zote za Mungu zitakuwa za kweli. Basi kwa jinsi hiyo, matumaini yetu yanakuwa mapana zaidi na ile hali ya kufikiria kukaribia kwa utukufu wa Mungu inakuwa na nguvu zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda. 
Hii ndiyo sababu waamini wanautarajia wakati ujao. Imani katika Mungu na tumaini kwa yajayo ni utukufu na ni imani ya wale ambao wataurithi Ufalme wa Mungu. Je, imani hii iliyotukuzwa ni baraka ambayo imetolewa kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho Tu? Kwa hakika jibu ni ndiyo! Ni muda tu ndio utakaopita kabla utukufu huu haujakabidhiwa kwa wenye haki, yaani kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho. Kwa wakati maalum, ahadi za Mungu kuhusiana na utukufu wake wote utafanyika na kuwa kweli kwetu sisi sote. Mambo haya yote yenye utukufu yatawatokea waamini. Utukufu ambao unatusubiri sisi ni wa kushangaza na mkuu na wenye uzuri sana. 
Wewe na mimi ambao tuna imani inayofanana katika injili ya maji na Roho ni watu ambao tutaingia katika Ufalme wa Mungu wa utukufu. Ulimwengu unaochanganya na wenye maovu unaweza kuifanya mioyo yetu kuwa myeusi katika baadhi ya nyakati, na tunaweza kukatishwa tamaa. Lakini wale ambao wamezaliwa tena upya wanaweza kuyashinda magumu haya kwa kuamini kuwa wamekwishafanyika kuwa warithi wa Mungu. Pamoja na kuwa kunaweza kuwa aina mbalimbali za shida katika mioyo ya waamini wasio na dhambi, ukweli ni kuwa waamini hao wanaweza kupata nguvu na kuendelea kuishi kwa kujikumbusha juu ya ahadi za Mungu. Ninashukuru kuwa Roho Mtakatifu anabakia katika mioyo yetu hali akitufariji, na anazishuhudia roho zetu kuwa sisi tu watoto wa Mungu. 
Wale ambao wamekombolewa hivi karibuni toka katika dhambi zao pia wanapaswa kuutazamia utukufu wa Mbinguni na kuishi katika tumaini. Sisi sote tulifanyika kuwa watu wa Mungu kwa usawa. Ikiwa umeishi maisha ya imani katika kanisa kwa muda mrefu basi unaweza kumwona Roho Mtakatifu ndani yako akifurahi kutokana na utajiri ulio katika urithi wako wenye utukufu. 
 

Hata Mioyo ya Wenye Haki Inaugua Katika Dunia Hii 
 
Hebu tusome aya ya 23 kwa pamoja. “Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.” Hebu tujiulize wenyewe, “Tunatumainia kitu gani katika maisha?” Sisi waamini tunaishi hali tukiutarajia ukombozi wa miili yetu. Tunaposema kuwa sisi tu watoto wa Mungu, ina maanisha kuwa ni roho zetu tu ndio watoto wa Mungu. Miili yetu bado haijaupokea utukufu, kwa hiyo waamini wote wanatarajia kuwa miili yao pia itabadilishwa. 
Wakati miili ya waamini ikapouvaa utukufu wa Mungu, basi wataweza kupita katikati ya moto bila kuungua na wataweza kupenya katika kizuizi chochote au ukuta. Miili yetu iliyobadilishwa itakuwa huru kutokana na ukomo wa muda na mahali. 
Lakini miili yetu bado haijabadilika, na kwa sababu hiyo sisi ambao tuna matunda ya kwanza ya Roho tunaugua ndani yetu. Hivyo, wenye haki ambao wamezaliwa tena upya kwa kuamini katika injili ya maji na Roho wanausubiria ukombozi wa mwili. 
Kuugua! Imeandikwa kuwa hata sisi ambao tunapokea matunda ya kwanza ya Roho tunaugua. Je, umewahi kusikia Roho Mtakatifu akiugua ndani yako? Ni lini alipougua? Roho Mtakatifu anaugua tunapojaribu kuyafukuzia matamanio ya mwili. 
Tunapouangalia ulimwengu na kuyapenda yale tunayoyaona, basi Roho Mtakatifu aliye ndani yetu anaugua. Miili yetu haijabadilika na kwa hiyo inafurahia inapojaribu kuyafuata mambo ya kidunia, lakini kwa kuwa nafsi zetu zimekwisha badilishwa, basi Roho Mtakatifu aliye ndani yetu anaugua. Hivyo ni lazima tuigeuze mioyo yetu inapojaribu kufuata starehe za dunia na kisha tupokee mwongozo wa Roho Mtakatifu. 
Roho Mtakatifu anaugua ndani yetu sisi ambao tu warithi wa Mungu, hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu. Tunapoishi katika ulimwengu huu tunaweza kuona jinsi ambavyo wakati wetu wa baadaye ulivyo gizani na jinsi miili yetu ilivyo na udhaifu; katika nyakati kama hizi tunapaswa kuzitazamia baraka za warithi wa Mungu kwa kuwa tunafahamu kuwa miili yetu pia itakombolewa kikamilifu. 
 

Kuishi Kwa Tumaini Lenye Utukufu
 
Hebu tusome aya za 24 na 25 kwa sauti moja. “Kwa maana tuliokolewa katia taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kuonekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? Bali tukikitarajia kitu tusichokona twakingojea kwa saburi.” 
“Je, tulipokea msamaha wa dhambi zetu zote katika tumaini la Ufalme wa Mungu?” Hebu tujiulize swali hili. Tulisema kuwa tulipokea msamaha wa dhambi zetu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Mungu anasema, “Bali tukikitarajia kitu tusichokona twakingojea kwa saburi.” 
Ili kwenda Mbinguni na kuwekwa huru toka katika dhambi zetu ni lazima tuokolewe kwa kuamini katika Neno la maji na Roho Mtakatifu. Baada ya kuwa tumeokolewa toka katika dhambi zetu zote, ikiwa tutaligeuza jicho letu na kuutazama ulimwengu halafu tukatarajia kile kinachoweza kuonekana, basi hii itamaanisha kuwa hatuufahamu utukufu wa Mungu na kwamba hatuusubiri utukufu huo. Ikiwa tunatarajia kile kinachoonekana basi kitu hicho hakiwezi kuwa tarajio. Ndio maana Paulo aliuliza, “Kwa nini mtu asubirie kile anachokiona?” Sisi ambao sasa tumefanyika kuwa wenye haki hatupaswi kutarajia yale au kile kilichopo hapa duniani, bali kwa mujibu wa ahadi zake, tunapaswa kuitarajia mbingu mpya na nchi mpya ambapo wenye haki wa Mungu wataishi. (2 Petro 3:13). 
Aina hii ya imani ndiyo ile ambayo wenye haki wanayoitarajia. Wenye haki wanaishi hali wakiitarajia nchi na Mbingu mpya. Kile tunachoweza kukiona kwa macho yetu ya kimwili si kitu ambacho ndicho tunachokitarajia. Hatuwezi kuona kwa macho yetu ya kibinadamu, kwa hiyo tunausubiria Ufalme wa Mungu wa utukufu ulioahidiwa na Mungu kwa macho yetu ya kiroho. Hii ndiyo sababu wale ambao ni wenye haki kwa kweli wanayaweka matarajio yao katika Ufalme wa Mbinguni. Na tarajio ni kuamini kuwa kile ambacho Mungu ametueleza kitatokea kwa kweli. 
Mungu alisema, “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo (1 Wakorintho 13:13). Tumepokea ondoleo la dhambi zetu kwa kupitia imani yetu na tumaini kwa Ufalme wa Mbinguni. Ufalme wa Mungu utakuja hapa duniani na utakuwepo Mbinguni, na tunatarajia kuwa tutaishi milele katika Ufalme wake. Hii ndiyo sababu tunaamini katika ahadi za Neno la Mungu na tunayavumilia mateso ya sasa. 
Hapa imeandikwa kuwa, “Bali tukikitarajia kitu tusichokiona twakingojea kwa saburi.” Kitu ambacho tunakitarajia kwa saburi si kitu ambacho tunaweza kukiona kwa macho yetu. Tunazisubiria ahadi za Mungu ambazo hatuwezi kuziona kimwili. Ahadi za Mungu zitatimia kwetu sisi waamini kwa sababu tuliambiwa kuwa utukufu wa Mungu utafunuliwa hivi karibuni nasi twaiamini ahadi hii ya Mungu. Kwa kuwa tunaamini kuwa Bwana wetu anakuja tena katika dunia hii, basi sisi tunaweza kuyavumilia mateso yetu makubwa. 
Bila shaka Ufalme wa Mungu utakuja hapa duniani. Ufalme wa Mungu utakuja wakati injili itakapokuwa imeenezwa katika mataifa yote. Wenye haki wanaisubiria siku hiyo kwa uvumilivu. Bwana wetu atakuja hali tukiwa bado tunasubiria. Huu ndio ukweli kwangu mimi na kwako wewe ambao tunaishi katika wakati huu. 
Kuna mtenda kazi mwenzetu wa kike kutoka Ukrania ambaye anatafsiri vitabu kwenda katika lugha ya Kiukrania. Hivi karibuni aliona majengo ya kituo cha biashara ulimwenguni yakianguka kutokana na mashambulio ya kigaidi na akasema kuwa alijisikia kuchanganywa na kupata hofu. Aliuliza ikiwa hali hii inatangaza “kipindi cha farasi wa kijivujivu” katika ufunuo na akauliza kama kuna kitabu chochote kuhusiana na sehemu hii ya Maandiko. 
Hatuwezi kusema kwa hakika kuwa tukio hili ni ufunguo au sehemu ya kipindi cha farasi wa kijivujivu, lakini pia hatuwezi kukana kuwa inaweza kuwa na uhusiano na kipindi hicho. Ikiwa mambo kama haya yanatokea mara nyingi, basi kutakuwa na vita, na mataifa yatapigana yenyewe kwa yenyewe. Wakati vita inapoamka ni wazi kuwa ulimwengu utapata shida kutokana na njaa na pengine kile kipindi cha “farasi wa kijivujivu” kinaweza kuwa cha kweli. 
Hivyo, wakati ninapoyaona matukio haya yanayoeleza juu kuja kwa maangamizo ya ulimwengu, basi hapo ndipo ninapoipa nia yangu nguvu ya kwamba tunapaswa kuieneza injili hadi mwisho wa dunia. Ni kweli kuwa tunapoteza matumaini kwa ulimwengu huu na kwamba mioyo yetu inaugua wakati majanga yanapotupiga. Hata hivyo, kadri tuishivyo, tunapaswa kuendelea kuusubiri Ufalme wa Mungu ambao hatuwezi kuuona kwa macho yetu ya kimwili bali kwa macho yetu ya kiroho. 
Kwa kuwa tunaamini katika injili ya maji na Roho, basi tunautarajia Ufalme wa Mbinguni na tunausubiria kwa saburi. Kwa kuwa tunaamini kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia, basi tunaweza kuyavumilia magumu yote. Hii inawezekana kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika mioyo yetu. 
Je, unaugua? Vumilia na uwe na subira. Si wewe peke yako unayeteseka bali sisi sote pia. Tunatumaini kuwa baada ya hali hii kupita mambo yote yatageuka kuwa mazuri. Je, hufahamu kuwa huwezi kuwa na tumaini kiroho ikiwa hupati magumu kimwili? Wakati mwili unapokuwa na raha sana, basi mara nyingi hatumtafuti Mungu na kuomba baraka zake. Na mara nyingi tunapokuwa na raha ndipo tunapoachana na Mungu. Sisi ambao tumezaliwa tena upya ni lazima tuwe na tumaini kwa utukufu unaokuja na kisha tuyavumilie magumu yaliyopo. 
Mungu alisema kuwa wale ambao watavumilia shida kwa saburi kwa ajili ya Bwana ndio waliobarikiwa. Siku ambayo Ufalme wa Mungu utakuja hapa duniani itafika nasi tutaingia katika Ufalme wake. Tunapaswa kuvumilia, kuwa na saburi, na kutokata tamaa wala kupoteza tumaini tunapoingojea siku hiyo. Haijalishi jinsi tunavyoweza kuwa na huzuni na kuwa na magumu kwa wakati huu wa sasa, bado tunapaswa kusubiri na kuvumilia hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja kama Mbingu na Nchi mpya. 
 

Roho Mtakatifu Anawasaidia Wale Walio na Haki ya Mungu
 
Hebu tusome aya ya 26. “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”
Je, Roho Mtakatifu anaomba kwa ajili yetu? Ndiyo anafanya hivyo! Roho Mtakatifu anafahamu madhaifu yetu na anatuombea.
Nilizungumzia kidogo kuhusu kuugua kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anaugua wakati tunapoelekea katika uelekeo ambao Mungu Baba yetu hapendi tuelekee huko. Wakati tunapoangalia mazingira ya kidunia halafu tukaugua pamoja nayo, tunapoelekea katika uelekeo ambao Mungu Baba yetu hapendi tuelekee huko, au wakati tunapoyadharau mapenzi ya Mungu na kuishi kinyume na mapenzi ya Mungu. 
Wakati Roho Mtakatifu anapofanya kazi ndani ya mwamini aliyezaliwa tena upya anaugua kwa namna isiyoweza kutamkwa hasa wakati ule tunapopoteza nguvu na kuwa wadhaifu katika mioyo yetu. Ni wakati huo ndipo Roho Mtakatifu anapotufanya sisi kuomba. Wakati fulani Roho Mtakatifu anafanya maombi kwa ajili yetu au anatuweka wazi kuwa tunahitaji kuomba. 
Roho Mtakatifu anaugua katika mioyo yetu na anatufanya sisi kuomba mbele za Baba yetu kwa mujibu wa mapenzi yake. “Bwana Mungu, umezitoweshea mbali dhambi zetu kwa kupitia ubatizo wako na damu yako Msalabani, na kwa kupitia haya tumefanyika kuwa watoto wako. Tunaamini kuwa kuja kwako mara ya pili hapa duniani kutakuja hivi karibuni. Tunaomba kwamba mapenzi yako yatendeke.” Basi huwa tunaomba kama hivi. 
Tunaomba kwa ajili ya imani ya kiroho. “Mungu, sisi ni maskini na wenye mapungufu mbele ya macho yako, hivyo tunaomba utupe imani inayohitajika ili mapenzi yako yaweze kutendeka.” Basi Mungu anatusaidia kwa sababu anaufahamu udhaifu wetu. Roho Mtakatifu hatuachi peke yetu bali anatufanya tuombe kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu na kisha anatuombea na sisi pia, hali akiimarisha mioyo yetu. 
Roho Mtakatifu anatufanya tuombe kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, na wakati tunapoomba msaada, Roho Mtakatifu anatufanya tuyaelewe mapenzi ya Mungu kwetu na anatupatia nguvu mpya. 
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”
Je, wakati mwingine unajihisi kuwa na mambo haya? Wakati ambao unafikiri na kutenda kinyume na jinsi Mungu anavyotutaka tutende, Je, unajihisi Roho Mtakatifu akikueleza kuwa kuna kitu ambacho hakijaenda sawa? Roho Mtakatifu anasema, “Hee, umekosea!” halafu mioyo yetu inaanza kuugua. Je, unafahamu kuwa huyu ni Roho Mtakatifu ndiye anayeugua? Pengine umewahi kupitia uzoefu kama huo, wakati roho ya mtu mwenye haki inapokuwa katika furaha ni kwa sababu Roho Mtakatifu anafurahi ndani yake. Basi ikiwa umewahi kupitia uzoefu huo wa furaha hapo juu basi utaona wazi wakati moyo wako unapougua basi ni Roho Mtakatifu ndiye anayeugua. 
Wakati tunapokuwa wadhaifu na kutenda kwa makosa, Roho Mtakatifu anafanya maombi ya kutuombea kwa ajili yetu, halafu Mungu Baba yetu anatupatia nguvu. Roho Mtakatifu ametufanya sisi kuomba kwa vitu vyote hali akitupatia sisi nguvu mpya ya kiroho. Hii ndio sababu wale walio na Roho Mtakatifu katika mioyo yao wana furaha sana. Roho Mtakatifu anatupatia nguvu kwa kupitia Neno la Mungu. Kwa maneno mengine, Roho Mtakatifu anafanya kazi pamoja na Neno lake ndani ya mioyo yetu ili kutupatia nguvu mpya ya kiroho. 
Roho Mtakatifu hapendi kuongea kwa kupitia mambo mengine. Anatupatia nguvu kwa kupitia Maandiko, Kanisa la Mungu, na kwa kupitia ushirika wetu na kaka na dada zetu. Hii ndio sababu kanisa la Mungu ni la muhimu sana, na hii ndiyo sababu kanisa lina jukumu muhimu sana la kufanya kuhusiana na kazi za Roho Mtakatifu. 
Katika kanisa kuna waamini, kuna ushirika au faragha yao, sifa, na ujumbe wa Neno. Roho Mtakatifu yupo na anafanya kazi kupitia wahubiri waliopo bila kujalisha kuwa ni akina nani ili kwamba waweze kuutoa ujumbe sahihi unaohitajika kwa wakati muafaka. Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani ya wote, yaani wale wanaotoa ujumbe na wale wanaoupokea ujumbe, hali akiziamsha akili zao na kuwapatia baraka wanazozihitaji. Roho Mtakatifu anatenda haya ndani ya Kanisa la Mungu mahali ambapo wenye haki wamekusanyika. Hii ndio sababu kanisa ni la muhimu sana kwa waamini. Wakati mwamini anapopitia katika wakati mgumu katika moyo wake halafu ikiwa mwamini huyo hawashirikishi wengine maumivu aliyonayo, basi watumishi wa Mungu wanaweza wakaielewa hali hiyo kwa kupitia Roho Mtakatifu. Ikiwa waamini wapo katika kusanyika la kanisa la Mungu, Roho Mtakatifu anaweza kuigusa na kuifariji mioyo yao. Roho Mtakatifu atawasaidia kuyashikilia Maandiko na kisha atawapatia nguvu ya kupona. 
Tunapoyaishi maisha yetu ya imani, basi sisi tunaamini katika injili ya maji na Roho, tunapokea msamaha wa dhambi zetu, tunafanyika watoto wa Mungu, na kama ushahidi, tunampokea Roho Mtakatifu kama karama. Kisha Mungu anatupatia kanisa lake. Baada ya kutupatia kanisa lake, Mungu anaongea kwa watumishi wake kwa kupitia kanisa na anawafanya watumishi wake kuhubiri kuuhubiri ujumbe wake. Mungu anayatibu majeraha yetu kwa Maandiko, anawapatia nguvu wale walio dhaifu, anawabariki wale ambao ni maskini wa roho, na anawapatia uwezo wa kuiendeleza kazi yake. Mungu anayatekeleza mapenzi yake kwa kupitia sisi. Kwa hiyo, waamini hawawezi kamwe kujitoa toka katika kanisa. 
Waamini hawawezi kujitoa toka katika mazungumzo na mahusiano na wenye haki wengine, pia hawawezi kujitoa toka katika kukua kwa kupitia Maandiko ya Mungu. Ukweli kamili unapatikana tu ndani ya kanisa la Mungu. Kwa hiyo, waamini wanahitaji kuungana kila mmoja katika kanisa. Imani pasipo umoja ni imani ya uongo. 
Je, unaamini kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika moyo wako? Kama inavyoelezwa katika Maandiko na kama kanisa linavyotueleza katika ujumbe wake, tunapoungana na kanisa la Mungu, Roho Mtakatifu atatusaidia na kutufunua macho yetu kuulewa ukweli hali akitupa baraka. Hivyo ungana na kanisa ukiwa na imani kama hiyo. Basi hapo Roho Mtakatifu atafurahi. 
Tumeendelea kuishi hadi saa hii kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Pia tutaishi kwa kuutegemea msaada wake hapo baadaye. Hii ndio sababu Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana kwetu ambao tumepokea msamaha wa dhambi zetu zote. Tunapaswa kufahamu na kuamini kuwa Roho Mtakatifu yupo na anaishi. Tunapaswa kufahamu kuwa tunatakiwa kuishi kwa Roho Mtakatifu na kupokea mwongozo wake katika mioyo yetu. Wale walio na Roho Mtakatifu katika mioyo yao wanayafuata mapenzi ya huyo Roho Mtakatifu. Ikiwa wewe ni mtu mwenye haki, basi Roho Mtakatifu anakaa ndani yako na kwa hiyo ni lazima ufuate sheria ya maisha kadri Roho Mtakatifu anavyokuongoza. 
Hebu tusome aya ya 27 kwa pamoja. “Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.” Mungu Baba yetu anaifahamu nia ya Roho anayekaa ndani yetu. Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu katika akili zetu; hivyo, Mungu Baba anafahamu kila kitu kilicho katika akili zetu. Kwa hiyo, “Yeye, Roho Mtakatifu hufanya maombi kwa ajili ya wakatifu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.” 
Hii inamaanisha kuwa Baba yetu anafahamu kile kilicho katika mawazo au akili za Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu anatuombea kwa mujibu wa mapenzi ya Baba. Hivyo waamini wanapata fursa ya kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Hii ndio sababu wale waliosamehewa dhambi zao wanaona faida ya maisha yao ya kiimani kwa kupitia Roho Mtakatifu. Akili za wenye haki zinaongozwa kwa uamsho wa Roho Mtakatifu. 
Matatizo yanatokea kanisani wakati wale wasio na Roho Mtakatifu katika mioyo yao wanapokuwepo ndani ya kanisa la Mungu. Wale wasioamini katika injili ya maji na Roho hawana Roho Mtakatifu ndani yao, na kwa sababu hiyo hawawezi kuwasiliana vizuri na waamini wa kweli walio na Roho Mtakatifu. Watu waasi wa Roho Mtakatifu wanaleta matatizo mengi katika kanisa. Wakati wale walio na Roho Mtakatifu wanapoyasikiliza mahubiri ya mtumishi wa Mungu aliyejazwa na Roho Mtakatifu, mioyo yao inakuwa na amani kwa sababu wanaelewa kile ambacho Mungu anataka kuwaeleza kwa kupitia mtumishi wake. 
Kwa hakika yeyote yule aliyesamehewa dhambi zake ana Roho Mtakatifu akaaye ndani yake. Sisi tuna Roho Mtakatifu ndani yetu na tunaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu na kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu. 
Roho Mtakatifu anatuongoza sisi kwa njia hizi zifuatazo: wakati mwingine kwa kupitia kanisa, wakati mwingine kwa kupitia faragha na ushirika wa waamini, na wakati mwingine kwa kupitia maneno ya Mungu. Roho Mtakatifu anatufanya sisi kuyatafuta mapenzi ya Mungu na anaturuhusu kuzifuata njia za haki za Mungu. Roho Mtakatifu anatupatia nguvu mpya ili kuishi upande wa Mungu hadi tutakapofikia katika Ufalme wake. 
Kwa hiyo, wewe na mimi ni lazima tutambue jinsi Roho Mtakatifu alivyo na umuhimu katika maisha yetu ya kiimani. Tunapoamini katika injili ya maji na Roho, tunapokea Roho Mtakatifu kama karama kama inavyoelezwa katika Maandiko, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38). 
Mungu alitupatia Roho Mtakatifu kama karama ili kwamba aweze kutuongoza sisi kuishi kwa mujibu wa mapenzi yake. Haya ni mapenzi ya Mungu Baba yetu. Mungu anatueleza kuwa ni lazima tuishi kwa kufuata mapenzi yake ili tuweze kuingia katika Ufalme wake. Tunapaswa kuwa na Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu, na ni wale tu wanaoamini katika injili ya maji na Roho ndio wanaompokea Roho Mtakatifu. Hivyo ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho ili tuweze kupokea Roho Mtakatifu kama karama na kisha kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu na hatimaye kuingia katika Ufalme wa Mungu. 
Hatupokei Roho Mtakatifu na ukombozi tofauti. Siku hizi watu wanafikiria kuwa baraka hizi mbili ni vitu viwili tofauti. Wanafikiria kuwa Roho Mtakatifu atawashukia ikiwa watakwenda kuomba kwa nguvu katika mapango ya milimani, hali wakiwa wanaomba katika lugha mpya. Wanafikiria kuwa Roho Mtakatifu atawashukia na kisha atawapatia ujumbe moja kwa moja na kuongea pamoja nao. Lakini mawazo kama haya si ya kweli. 
Roho Mtakatifu na Maandiko hayawezi kutenganishwa, na Roho Mtakatifu na mwamini hawawezi pia kutenganishwa. Hii ndio sababu mahusiano kati ya mwamini na Roho Mtakatifu, mwamini na kanisa, na mwamini na Mungu Utatu—Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu—yapo karibu sana. 
Sisi tunaoishi katika kipindi hiki cha mwisho tunaishi kwa kumfuata Roho Mtakatifu. Sisi tunaishi kwa mujibu wa mapenzi ya Baba kwa kupitia Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anayafahamu mapenzi yote ya Mungu. Baba yetu anafahamu kila kilicho katika akili na nia ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anayaongoza mawazo na akili zetu na anawasiliana na Mungu. Kwa njia hii, Roho Mtakatifu anaomba kulingana na mapenzi ya Mungu, na Baba yetu anayajibu majibu hayo kwa kutufanya sisi tuishi kulingana na mapenzi yake. 
Hii ndio sababu Paulo alizungumza katika Warumi sura ya 8 aya ya 16 hadi 27 kuhusiana na kazi za Roho Mtakatifu. 
Tunaweza kuusubiria Ufalme wa Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Tunaweza kuyavumilia magumu na mateso ya wakati huu na kisha kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Bwana hali tukiutarajia Ufalme wa Mungu kwa nguvu za Roho Mtakatifu anayekaa katika mioyo yetu. Tunaweza kuvumilia na kuwa na saburi kwa kupitia Roho Mtakatifu, na kuwa na uwezo wa kumtumikia Bwana wetu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Tumepewa mambo haya yote kwa kupitia Roho Mtakatifu. Ni lazima tutambue kuwa sisi ni watu ambao tunaenenda pamoja na Roho Mtakatifu, hali tukilisoma Neno la Mungu wakati wote, hali tukiiunganisha mioyo yetu na Neno, na huku tukilisikiliza na kulifuata hilo Neno. Ni lazima tuishi maisha yetu kwa kiasi kuwa Baba yetu na Roho Mtakatifu wafurahi ndani yetu, na kamwe tusiishi maisha ya kimwili ambayo yanaifurahisha miili yetu tu. Hivi ndivyo asemavyo Paulo katika kifungu hiki. 
Siku zote Mungu yupo pamoja nasi katika maisha yetu. Mungu anaitunza mioyo yetu na anataka kutusaidia. Bwana na aendelee kutubariki sisi. Wakati Bwana wetu atakapokuja tena kila kitu kitabadilishwa katika utukufu. Sisi ambao tuna haki ya Mungu tunaurithi Ufalme wa Mungu wote pamoja na utukufu. Yeyote anayetaka kuurithi ufalme wa Mungu ni lazima asikilize kwa makini na aamini katika injili ya maji na Roho. 
Halleluya! Ninaomba kuwa haki ya Mungu iwe pamoja nawe na ikubariki.