Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 8-8] Roho Mtakatifu Anayewasaidia Wenye Haki (Warumi 8:26-28)

(Warumi 8:26-28)
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.” 
 

Roho Mtakatifu yumo katika mioyo ya wale wanaoamini katika haki ya Mungu. Roho Mtakatifu anawafanya wao kuomba na anawasaidia kufanya hivyo. Pia Roho Mtakatifu huugua kwa kufanya maombi kwa niaba yao kusikoweza kutamkwa. Hii ina maanisha kuwa Roho Mtakatifu anawasaidia kuomba kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo sababu wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanaitwa wana wa Mungu. Bwana anawaahidia wao kuwa atakuwa pamoja nao wakati wote hadi mwisho wa dahari. 
Roho Mtakatifu yumo ndani ya wenye haki hali akifanya maombi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Je, unafikiri kuwa unawezaje kumpokea Roho Mtakatifu? Ni kwa kuomba? Je, unafikiri kuwa unaweza kumpokea Roho Mtakatifu hali ukiwa na dhambi zako zote? Roho Mtakatifu anafanya kazi na anakaa katika mioyo ya wale wanaoamini katika haki ya Mungu tu. 
Wakristo wanaopenda kuomba kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu wanapokea msaada toka kwa Roho Mtakatifu. Wanajifunza na kufahamu kile wanachopaswa kukiombea. Ikiwa umepokea Roho Mtakatifu kwa kuamini katika haki ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atafanya maombi kwa ajili yako na kisha ataiongoza njia yako. 
 

Mambo Yote Yanafanya Kazi Pamoja Kwa Ajili ya Mema 
 
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.” (Warumi 8:28).
Mungu yupo katika upande wa waamini hali akifanya mambo yote kufanya kazi pamoja kwa ajili ya mema kwa wale wanaompenda Mungu. Mungu anawapenda waamini waliozaliwa upya tena. Wakati mwingine Mungu anaweza kuwatumia adui zetu kwa ajili ya faida yetu binafsi lakini mwishoni anawaadhibu adui hao kwa dhambi zao. Hivyo kila aliye adui yetu atakuja kupotelea katika adhabu ya milele kwa kuwa kila kitu ambacho Mungu anakiruhusu ni kwa ajili ya mema kwa waamini.