Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-12] Kisitiri na Nguzo za Mahali Patakatifu (Kutoka 26:31-37)

Kisitiri na Nguzo za Mahali Patakatifu
(Kutoka 26:31-37)
“Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguzo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana. Nawe utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini. Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza. Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu; nawe utasubu vitako vya shaba vitano wa ajili yake.”
 


Mahali Patakatifu

Mahali Patakatifu
Nitapenda kutafakari juu ya maana ya kiroho iliyomo katika nguzo za Mahali Patakatifu na rangi za kile kisitiri chake. Hema Takatifu ambalo tunalizama hapa lilikuwa na vipimo vya mita 13.5 (futi 45) kwa urefu na mita 4.5 (futi 15) kwa upana, na lilikuwa limegawanywa katika vyumba viwili vilivyoitwa Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Ndani ya Mahali Patakatifu kulikuwa na kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba, na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kulikuwa na Sanduku la Ushuhuda na kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku lile. 
Likiwa na Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu, Hema Takatifu la Kukutania lilizungukwa katika pande zote na mbao za mti wa mshita zilizokuwa na kipimo cha sentimita 70 (futi 2.3) kwa upana na mita 4.5 (futi 15) kwa urefu. Na katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa na nguzo tano za mti wa mshita zilizokuwa zimefunikwa dhahabu. Mlango wenyewe, ambao kwa huo mtu aliutumia ili kuingia katika Hema Takatifu la Kukutania toka katika ua wa nje ulikuwa umetengenezwa kwa kisitiri kilichokuwa kimefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa.
Katika ule ua wa nje wa Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa na nguzo sitini zikiwa zimesimamishwa, kila nguzo ilikuwa na kipimo cha mita 2.25 (futi 7.5) kwa kimo. Lango la ua ambalo lilikuwa upande wa mashariki pia lilikuwa limefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na ni kwa kupitia katika lango hili ndipo mtu angaliweza kuingia katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Katika ua huu wa Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na birika la kunawia. 
Baada ya kupitia maeneo haya mawili mtu aliweza kuufikia mlango wa Hema Takatifu la Kukutania uliokuwa na kipimo cha mita 4.5 (futi 15) kwa kimo. Mlango huu wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na nguzo tano, ambapo vitako vyake vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Kama ilivyo kwa lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania, mlango wa Hema Takatifu la Kukutania pia uliundwa kwa kisitiri kilichokuwa kimefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa na kisha kikatungikwa katika kulabu zilizokuwa zimewekwa juu ya zile nguzo tano. Kisitiri hiki ndicho kilichogawanyisha kati ya ndani na nje ya Hema Takatifu la Kukutania. 
 

Tunachotakiwa Kukiangalia Kwanza Ni Nguzo za Mlango wa Hema Takatifu la Kukutania
 
Nguzo tano za Mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zilikuwa na kipimo cha mita 4.5 (futi 15) kwa kimo. Katika nguzo hizi kulikuwa na kisitiri kilichokuwa kimefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Kwanza kabisa, hebu tuangalie katika ukweli kuwa nguzo tano za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zilikuwa na urefu wa mita 4.5 (futi 15) kwa kimo. Je, ukweli huu unamaanisha nini? Unamaanisha kuwa Mungu mwenyewe alilipa gharama kubwa ya sadaka ya kuteketezwa ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu na kisha kutufanya sisi kuwa wana wake. Kwa kuwa kimsingi mimi na wewe tu viumbe wadhaifu na wenye mapungufu, tunaishi katika ulimwengu hali tukitenda maovu mengi sana. Kwa kuwa mimi ni wewe ni wenye dhambi wabaya kabisa ambao hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi kila dakika katika ulimwengu huu, basi sisi tuna maovu mengi na mawaa. Nguzo hizi za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha sisi kuwa ili kutukomboa sisi toka katika mawaa kama hayo na katika dhambi za ulimwengu, Mungu alimtoa Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili kuwa mshahara wa dhambi zetu, na kwa hakika Yesu ametukomboa sisi toka katika dhambi za ulimwengu.
Kwa maneno mengine, Yesu Kristo aliutoa mwili wake kama sadaka ya kuteketezwa mbele za Mungu na akalipa mshahara wote wa dhambi za ulimwengu kwa ajili ya mawaa yetu na dhambi tulizozifanya hapa ulimwenguni, na kwa hiyo akawa ametuokoa. Ikiwa mtu alitenda dhambi, na akawa amefanya dhambi pasipo kutambua kuhusiana na vitu vitakatifu vya Bwana, basi mtu huyo ilimpasa kuleta mwanakondoo dume kama sadaka ya dhambi, na pia alipaswa kuongeza moja ya tano na kisha kuwapatia makuhani (Mambo ya Walawi 5:15-16). Hii inamaanisha kuwa Yesu Kristo alijitoa yeye mwenyewe ili kutuokoa wewe na mimi toka katika dhambi zetu na kwa hiyo amelipa mshahara wote wa dhambi zetu na zaidi. Bwana wetu alikuja hapa duniani ili kuzitoweshea dhambi zetu na kisha alijitoa yeye mwenyewe kama sadaka yetu ya dhambi kwa ajili ya hizi dhambi zetu. 
Sadaka za Biblia, kama vile sadaka za kuteketezwa, sadaka za dhambi, na sadaka za amani zilitolewa ili kwamba watu ambao walitenda dhambi waweze kuzitowesha dhambi zao kwa kuiweka mikono yao juu ya vichwa vya wanasadaka wao wa kuteketezwa na hivyo kuzipitisha dhambi zao zote juu ya wanasadaka hao. Katika sadaka hizo, sadaka za hatia zilikuwa ni zile ambazo sadaka ya kuteketezwa ilitolewa ili kuyatoweshea mbali makosa ya mtu. Sadaka ya hatia ilitolewa wakati mtu alipokuwa amemjeruhi mtu mwingine kwa uzembe ili kumlipa aliyejeruhiwa na kisha kuurudisha uhusiano. Pia sadaka ya hatia ilihusisha kuongeza asilimia 20 kama fidia kwa fidia ya jumla ikiwemo adhabu na fidia. Hili lilikuwa ni hitaji la msingi katika sadaka ya hatia. Ilikuwa ni sadaka ambayo ilitolewa kwa madhumuni maalum ya kuyapatanisha mawaa ya mtu fulani alipokuwa amemdhuru mtu mwingine (Mambo ya Walawi 5:14-6:7).
Je, wewe na mimi tupo mbali toka katika dhambi? Je, hatuishi maisha yetu yote hali tukiwa tunatenda dhambi? Sisi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kufanya hivyo, kwa kuwa mimi na wewe tu wazawa wa Adamu. Sisi wenyewe tunafahamu jinsi ambavyo tuna mapungufu mengi, na jinsi ambavyo tunayaishi maisha yetu hali tukitenda dhambi nyingi. Ni maovu mangapi ambayo tumefanyiana dhidi ya sisi wenyewe na dhidi ya Mungu? Ni kwa sababu sisi ni wazito na wenye mapungufu kuweza kuyatambua maovu haya kuwa ni dhambi basi ndio maana mara nyingi tunayasahau maovu hayo kadri tunavyoishi katika maisha yetu. Lakini mimi na wewe hatuwezi kukwepa bali tutatambua kuwa tumefanya makosa na hatia nyingi mbele za Mungu dhidi ya majirani zetu na dhidi ya Mungu, na kwamba tutajiona kuwa sisi ni wenye dhambi tu mbele za Mungu. 
Ili kuwakomboa wenye dhambi kama hao toka katika dhambi zao, Mungu alitaka kumtuma Yesu Kristo ili awe sadaka yao ya hatia. Kwa kule kumpata Yesu Kristo kuzibeba adhabu za dhambi zetu kwa kupitia gharama ya kusulubiwa kwake, Mungu ametupatia sisi karama ya wokovu. Wakati Mungu Baba amemtuma Mwana wake hapa duniani na akamfanya abatizwe na kusulubiwa, yote hii ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote na kutufanya sisi kuwa watu wake mwenyewe, tunawezaje basi kujilinganisha sisi wenyewe na thamani ya sadaka yake? Ili kutuokoa sisi wenye dhambi toka katika dhambi zetu zote, Bwana wetu alisulubiwa ili kulipa mshahara wote wa dhambi, na kwa hiyo ametuokoa sisi toka katika dhambi za ulimwengu. Jambo hili linaweza kuwa kitu gani kingine zaidi ya neema ya Mungu ya kushangaza? Upendo wake ni mkubwa, wa kina, na mpana kiasi gani? Ule ukweli kuwa nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zilikuwa na kimo cha mita 4.5 (futi 15) kunatueleza sisi juu ya upendo wa Mungu kwetu ambao tumepewa kwa kupitia Yesu Kristo. 
Ili kutuokoa viumbe tusiofaa kama sisi toka katika adhabu ya dhambi, Bwana wetu ametuokoa sisi kwa kupitia sadaka yake—ninamshukuru sana Bwana kwa ukweli huu. Wakati tulipokuwa hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kufungwa kuzimu kwa ajili ya adhabu ya dhambi zetu, na wakati Bwana alipoutoa mwili wake mwenyewe kwa ajili yetu ili kutuokoa toka katika dhambi zetu hizi, inawezekanaje basi tusimshukuru Mungu? Tunampa Mungu shukrani! Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake wa thamani kwa kubatizwa na Yohana, akalipa mshahara wa dhambi zetu kwa damu yake Msalabani, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu na adhabu ya dhambi. Kwa hiyo tunaweza kumshukuru yeye tu kwa imani yetu katika injili hii. Hii ndio maana halisi ya wokovu unaopatikana katika nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. 
Kila nguzo katika zile nguzo tano za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania ilikuwa na kimo cha mita 4.5. Namba “5” katika Biblia ina maanisha ni “neema ya Mungu”. Kwa hiyo, kule kusema kuwa kulikuwa na nguzo tano kuna maanisha juu ya karama ya wokovu ambayo Mungu ametupatia. Kwa kutupenda na kutufunika katika upendo wake wa wokovu, Mungu ametufanya sisi tusikose kitu chochote kile ili kufanyika watu wake mwenyewe. Katika Biblia, dhahabu inamaanisha ni juu ya imani inayoamini katika Mungu ambaye ametuokoa sisi kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa maneno mengine, Biblia inazungumza juu ya “imani” inayoamini kikamilifu katika ukweli kwamba Mungu mwenyewe alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa, akafa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo ametufanya sisi kuwa wenye haki wakamilifu. Hii ndio sababu nguzo za Mahali Patakatifu zilifunikwa zote kwa dhahabu. 
Kule kusema kuwa vitako vya nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania viliundwa kwa shaba kunadhihirisha kuwa Bwana, baada ya kuhukumiwa kwa haki, ametuokoa sisi ambao tusingeweza kukwepa zaidi ya kufungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu kwa kupitia ubatizo wake na damu ya Msalaba. Kwa kuwa tulikuwa tumejawa na mawaa mengi, sisi tulikuwa ni viumbe tusiofaa ambao tusingeweza kukwepa kifo, lakini ili kutufanya sisi kuwa watu wake mwenyewe, basi Mungu mkamilifu na wa kweli alijisulubisha yeye mwenyewe, yeye ambaye anafaa zaidi kuliko sisi, na kwa hiyo ametufanya sisi kuwa watoto wa Mungu Baba. Hii ndio maana dhahabu inamaanisha ni imani inayoamini katika ukweli huu. Hivi ndivyo inavyotupasa kuzifahamu rangi za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania, na pia ni lazima tutafakari juu ya rangi hizo na kisha tuziamini katika vina vya mioyo yetu.
 

Vitako vya Shaba vya Nguzo za Hema Takatifu la Kukutania
 
Katika Hema Takatifu la Kukutania, ni vitako vya nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania ndivyo vilivyokuwa vimeundwa kwa shaba. Hii inamaanisha kuwa katika dunia hii mimi na wewe tumetenda dhambi nyingi dhidi yetu wenyewe na dhidi ya Mungu, na kwamba kwa hiyo tusingeweza kukwepa zaidi ya kuhukumiwa kwa dhambi hizi. Ukweli uliofichika katika vitasa hivi vya shaba unatufanya sisi tufikirie juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kitu cha kwanza ambacho wenye dhambi walikutana nacho wakati walipokuwa wakiingia katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kupitia lango lake ilikuwa ni madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambapo sadaka ya kuteketezwa ilitolewa. 
Neno “madhabahu” hapa lina maanisha ni “kupaa.” Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa inazungumzia juu ya ukweli kuwa Yesu Kristo alibatizwa na kisha kusulubiwa Msalabani kwa haki kwa niaba yetu sisi wenye dhambi wote. Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa palikuwa ni mahali ambapo zile sadaka zilizokuwa zimezipokea dhambi kwa kuwekewa mikono ziliuawa kama adhabu ya dhambi hizi. Makuhani waliweka damu ya wanasadaka hawa wa kuteketezwa katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na kisha waliimwaga damu iliyosalia katika ardhi chini ya madhabahu hiyo, na kisha waliichoma miili ya wanasadaka hao katika hiyo madhabahu kwa moto. Palikuwa ni mahali pa kifo ambapo sadaka zilizopokea dhambi katika miili yao ziliuawa. 
Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa iliwekwa kati ya lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania na Hema Takatifu la Kukutania lenyewe. Kwa hiyo, yeyote aliyetaka kuingia katika Hema Takatifu la Kukutania ilimpasa kwanza kupita katika madhabahu hii ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo, pasipo kupitia katika madhabahu hii ya sadaka ya kuteketezwa, hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuweza kuingia katika Hema Takatifu la Kukutania. Ni kweli kuwa madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ni kivuli cha ubatizo wa Yesu Kristo na Msalaba. Na ubatizo wa Bwana wetu na Msalaba ndivyo vinavyoondoa maovu ya wenye dhambi wote wanaokuja mbele za Mungu. 
Kwa hiyo, pasipo kuzileta dhambi zao kwanza na kisha kusimama katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na pasipo kukumbuka kuwa sadaka ya kuteketezwa imewaokoa toka katika dhambi zao kwa kuzichukua dhambi kwa kuwekwa mikono na kisha kuimwaga damu yake katika mahali hapa, basi hakuna mwenye dhambi yoyote anayeweza kamwe kwenda mbele za Mungu. Imani hii ni njia ya kwenda mbele za Mungu, na kwa wakati huo huo ni imani inayotuongoza sisi kwenda katika baraka za ondoleo la dhambi zetu na kubeba adhabu ya dhambi zetu (yaani kuifia dhambi). 
Wakati watu wa Israeli walipoleta sadaka ili kuziondoa dhambi zao, kwanza walizipitisha dhambi zao kwa mwanasadaka kwa kumuwekea mikono yao juu ya kichwa chake, walimchinja na kisha wakaikinga damu yake ya kusulubiwa, na kisha waliiweka damu hii katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kisha wakaimwaga damu yote iliyosalia katika ardhi chini ya ile madhabahu. Ile ardhi chini ya ile madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ni dunia. Dunia hapa ina maanisha ni mioyo ya wanadamu. Kwa hiyo, inatueleza sisi kuwa wenye dhambi wanapokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika mioyo yao kuwa sadaka ya kuteketezwa imezipokea dhambi zao na kuwa imekufa kwa niaba yao kwa mujibu wa sheria ya wokovu. Pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa zinatueleza sisi juu ya dhambi ambazo zimeandikwa katika Kitabu cha Hukumu kiroho. 
Wenye dhambi wa kipindi cha Agano la Kale waliweza kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kuamini katika ukweli kuwa wameiweka mikono yao juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa na kwa hiyo wamezipitisha dhambi zao juu yake, na kwamba mwanasadaka huyu ameimwaga damu yake na kisha kutolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kama kusingekuwa na kule kuwekewa mikono na kifo na kule kuichoma sadaka ya kuteketezwa, tendo ambalo liliwawezesha wenye dhambi kuzipatanisha dhambi zao, basi njia ya wao kwenda mbele za Mungu ingekuwa imefungwa kabisa, na wasingeweza kabisa kwenda mbele za Mungu mtakatifu. Kwa kifupi, hakukuwa na ukweli mwingine zaidi ya utaratibu huu wa sadaka ya kuteketezwa ambao uliwawezesha wao kwenda mbele za Mungu. 
Vivyo hivyo, pasipo imani yetu katika ubatizo wa Yesu Kristo, kifo chake, na sadaka yake ya upatanisho, basi hakuna njia nyingine kwa sisi kupokea ondoleo la dhambi zetu na kisha kwenda mbele za Mungu. Haijalishi jinsi ambavyo watu wa Israeli wangalileta wanakondoo wazuri, safi, wakamilifu na wasio na mawaa kwa makuhani, lakini ikiwa mikono yao ingekuwa haijawekwa juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kama mwanasadaka huyo angekuwa hajazipokea dhambi zao, na kama mwanasadaka huyo asingeliimwaga damu yake na kufa, basi sadaka hii isingekuwa na matokeo yoyote. 
Inapofikia katika suala la imani yetu, ikiwa hatuamini kuwa ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea toka kwa Yohana na damu yake ya thamani aliyoimwaga Msalabani vimetuondolea dhambi zetu zote, basi hatuwezi kusema kuwa tumepokea ondoleo la dhambi kamilifu. Ubatizo ambao Yesu aliupokea na kifo chake Msalabani vinasimama kwa kazi kati ya wenye dhambi na Mungu Baba, na kwa hiyo vimefanyika kuwa ni vitu vya kiupatanisho vinavyowaokoa wenye dhambi toka katika maovu yao yote. 
Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ni muundo ambao unajumuisha mpango wa wokovu ambao Mungu mwenyezi huko Mbinguni alikuwa ameuandaa na kuutimiza katika Yesu Kristo. Musa alilijenga Hema Takatifu la Kukutania kwa mujibu wa mbinu ya wokovu na mfano ambao Mungu alikuwa ameuonyesha kwake katika Mlima Sinai. Tunapoangalia katika Biblia, tunaweza kuona kuwa maelekezo haya yalitolewa kwa kurudiwa rudiwa. Kama ambavyo Kutoka 25:40 inavyoeleza, “Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, ulioonyeshwa mlimani.”
Watu waliweza kutengeneza msalaba na kumsulubisha Yesu Kristo juu yake, lakini zaidi ya hapa, hawakuweza na wasingeweza kufanya kitu kingine chochote. Waliweza kumfunga mikono na kumburuza hadi Kalvari. Walimsulubisha hali wakiwa hawajui kile ambacho walikuwa wakikifanya mbele za Mungu. Wenye dhambi waliweza kufanya haya mambo yote kwa sababu mambo haya yalipaswa kutimizwa kwa mujibu wa mipangilio ambayo Mungu alikuwa amekwisha ipanga. Hata hivyo, ni Yesu Kristo ambaye ndiye amewaokoa wenye dhambi wote kwa kupitia ubatizo wake na damu ya Msalaba mara moja na kwa wote kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji na hivyo kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, na kisha kuzioshelea mbali mara moja na kuimwaga damu yake Msalabani. 
Kwa hiyo, kabla ya kifo cha Bwana Yesu Kristo Msalabani, ubatizo ambao alikuwa ameupokea toka kwa Yohana ulikuwa ni tendo muhimu sana linalohitajika kwa wokovu wetu. Kule kuzibeba dhambi na adhabu ya dhambi kuliazimiwa na Mungu hata kabla ya uumbaji. Katika Yohana 3, Yesu alimwambia Nikodemu kuwa hii ni injili ya maji na Roho. Kwa hiyo, ubatizo wa Yesu na Msalaba ni majaliwa ya Mungu yaliyokuwa yamepangwa na kuazimiwa kabla ya kuja kwa Yesu Kristo. 
Yesu mwenyewe alisema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Na katika ubatizo wa Yesu, Petro pia alisema, “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi...” (1 Petro 3:21). Pia imeandikwa katika kitabu cha Matendo, “Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua” (Matendo 2:23).
Ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu ya Msalaba zote zilitimizwa kwa dhumuni na mpango wa Mungu mwenyezi. Kwa hiyo, kwa kuwa hakuna anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu pasipo kuupokea ukweli huu katika moyo wake na kuamini katika ukweli huu, basi ni lazima tutambue kwamba anatutaka sisi tuwe na imani, na ni lazima tuwe na imani hiyo. Pasipo imani inayoamini katika injili ya maji na Roho, hakuna hata mmoja anayeweza kuokolewa. Kama Yesu asingelijitolea kubatizwa na Yohana, kujitoa mwenyewe katika mikono ya wenye dhambi, na kuimwaga damu yake Msalabani, basi wenye dhambi wasingeliweza kumsulubisha. Yesu hakuburuzwa kwenda Kalvari kwa bahati mbaya na kwa maamuzi ya watu wengine, bali ilikuwa ni kwa ridhaa yake mwenyewe ndio maana alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, kuimwaga damu yake Msalabani, na kwa hiyo amewaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao. 
Isaya 53:7 inasema, “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.” Kwa hiyo, ubatizo wa Bwana Yesu Kristo na kifo chake Msalabani vilikuwa ni kwa mujibu wa mapenzi yake mwenyewe, na kwa kupitia vitu hivyo amewaokoa wote wanaoamini katika ubatizo wake na damu ya Msalaba toka katika dhambi zao zote. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaandika hivi kuhusu kazi hizi za Bwana, “Lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake” (Waebrania 9:26).
Katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo inatuonyesha sisi juu ya kivuli cha ubatizo wa Kristo na kifo chake juu ya Msalaba, basi tunaweza kwa hakika kushuhudia karama ya kiroho ya wokovu ya Mbinguni. Kifo cha sadaka ya kuteketezwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kinamaanisha juu ya ubatizo na kifo cha Yesu ambacho kilihitajika kwa ajili ya dhambi za kila mmoja. Katika Agano la Kale, wenye dhambi walipatanishwa makosa yao kwa kupitia sadaka yao ya kuteketezwa ambayo ilizichukua dhambi zao katika mwili wake kwa kuwekewa mikono na kisha kufa kwa niaba yao. Kwa namna iyo hiyo, katika Agano la Kale, kabla Mwana wa Mungu hajauawa katika mikono ya wakatili pale Kalvari, kwanza alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, na ni kwa sababu ya ubatizo huu ndio maana Yesu alisulubiwa, akaimwaga damu yake na kufa. 
Kwa hiyo, Mungu alipanga ana akampangia Yesu kuwekewa mikono na kusulubiwa hadi kifo, yote haya ili kuleta amani kati ya wauaji hawa waliomuua Mwana wake na Mungu mwenyewe. Mungu aliipanga sheria ya wokovu ikijumuisha kuwekewa mikono na kifo, na kwa mujibu wa sheria hii, aliruhusu watu wa Israeli kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kutoa sadaka za kuteketezwa. 
Kwa maneno mengine, Mungu mwenyewe alifanyika sadaka ya amani kikamilifu ili kuwaokoa wenye dhambi. Hivi ndivyo Wokovu huu wa Mungu ulivyo na haki na busara kiasi hiki! Hekima yake na kweli ni vitu vya kushangaza sana, vitu ambavyo ni vigumu hata kufikirika kwetu. Ni nani anayeweza kudiriki kuwazia juu ya majaliwa ya wokovu unaoundwa kutokana na kuwekewa mikono na kuimwaga damu kuliko dhihirishwa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa? Kama vile Paulo, tunachoweza kukifanya ni kushangaa, “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!” (Warumi 11:33) Injili ya maji na Roho ndiyo injili pekee ya haki ambayo kwa hiyo Mungu amewaokoa wenye dhambi kikamilifu. 
 

Pembe za Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa
 
Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa
Pembe za shaba zilikuwa zimewekwa katika kona nne za madhabahu ya kuteketezwa iliyokuwemo katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Katika Biblia, pembe zinaonyesha juu ya hukumu ya dhambi (Yeremia 17:1: Ufunuo 20:11-15). Hii inatuonyesha sisi kuwa injili ya Msalaba inajengwa katika ubatizo wa Yesu ambao aliupokea. Ndio maana Mtume Paulo alisema, “Kwa maana siionei haya injili kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Warumi 1:16). Pia, katika 1 Wakorintho 1:18, imeandikwa, “Kwa sababu neno la msalabala kwa wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.”
Zile pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa zinatangaza wazi kuwa hukumu ya Mungu ya haki na wokovu vimekamilishwa kikamilifu kwa kupitia ubatizo wake, kifo Msalabani, na ufufuko wake. 
 

Miti Miwili Iliyowekwa Katika Pete za Madhahabu ya Sadaka ya Kuteketezwa
 
Vyombo vyote vya Hema Takatifu la Kukutania lililokuwa limejengwa jangwani vilikuwa vinahamishika. Hii ilikuwa ni njia endelevu ikihusianishwa na desturi ya kimaisha ya wafugaji wahamaji wa Israeli. Waliendelea kuzunguka jangwani na nyikani hadi walipofikia kuweka makazi ya kudumu katika nchi ya Kanaani. Kwa kuwa maisha yao ya kuhiji yaliendela wakati walipokuwa wakipita katika jangwa, Mungu aliwafanya kuiandaa miti miwili ili kuipachika katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ili kwamba makuhani wao waweze kuichukua madhabahu hiyo wakati watu wa Israeli walipokuwa wameamriwa na Mungu kusonga mbele. 
Kama Kutoka 27:6-7 inavyosema, “Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba. Na hiyo miti itatiwa katika pete, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua.” Kwa kuwa miti miwili iliwekwa kwa kupitia pete za shaba za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa katika pande zake mbili, basi Walawi waliweza kuibeba katika mabega yao na kuisafirisha wakati watu wa Israeli walipokuwa wakihama. Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa inadhihirisha juu ya ubatizo wa Kristo na Msalaba. Kwa hiyo, kama ambavyo Walawi walivyoibeba ile madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ile miti miwili katika jangwa, basi injili ya ubatizo wake na Msalaba pia inatolewa katika jangwa zima la ulimwengu huu na watumishi wake. 
Jambo jingine ambalo ni lazima tulichunguze kabla ya kuendelea ni ule ukweli kuwa kulikuwa na miti miwili ambayo iliwawezesha waisraeli kuihamisha madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Vivyo hivyo, injili ya maji na Roho pia imeundwa katika sehemu mbili. Moja ni ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana, na nyingine adhabu ambayo Bwana Yesu Kristo aliibeba pale Msalabani. Vitu hivi viwili vinapounganishwa, basi wokovu wa ondoleo la dhambi unakamilika. Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ilikuwa na miti miwili. Ukisema kwa lugha nyingine ni kuwa madhabahu hiyo ilikuwa na vishikio. Mti mmoja haukuweza kutosha kwa sababu kwa kutumia mti mmoja ingekuwa vigumu kuibeba ile madhabahu kwani ingeyumba wakati wa kutembea.
Vivyo hivyo, injili ya maji na Roho pia ina sehemu mbili. Sehemu hizi ni ubatizo wa Yesu Kristo alioupokea toka kwa Yohana na damu yake aliyoimwaga Msalabani. Kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani ni vitu vinavyohusiana na kuheshimiana pamoja ili kuutengeneza ukweli wa haki. Ubatizo na damu ya Yesu vimelitimiza ondoleo la dhambi la wenye dhambi kwa haki. Ikiwa moja kati ya haya mawili litadharaulika (ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani), basi itakuwa ni sawa na kulidharau jambo jingine lililosalia. Hakuwezi kuwa na wokovu pasipo ubatizo wa Kristo na damu yake aliyoimwaga. 
Kwa kweli ufufuo wake pia ni wa muhimu sana. Pasipo ufufuo wa Kristo, kifo chake kingekuwa ni utupu na kisicho na matokeo yoyote yale. Ikiwa tungeamini katika Kristo aliyekufa, basi asingeliweza kumwokoa yeyote ikiwemo hata yeye mwenyewe. Lakini Kristo ambaye alibatizwa, akamwaga damu hadi kifo pale Msalabani, na akakishinda kifo kwa kufufuka ili kuishi tena amefanyika kuwa Mwokozi wa kweli kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho na kisha kwenda mbele za Mungu. Pia Yesu amefanyika kuwa Bwana wa milele wa wokovu na mlinzi.
Kueneza kifo cha Kristo peke yake pasipo ufufuo wake ni kujichanganya tu. Na pasipo ufufuo wa Kristo, basi Msalaba wake ungekuwa ni alama ya kushindwa kwa Mungu. Pia kushindwa huko kungemgeuza Yesu kuwa ni mtuhumiwa asiye na maana. Si hilo tu, bali hali hiyo ingemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kitu ambacho kingesababisha Neno la Biblia kudhihakiwa. Kristo alibatizwa na Yohana, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wa kweli kwa wale wanaomwamini. 
Injili inayouacha ubatizo wa Yesu toka katika injili nzima, ambayo ndiyo injili ambayo watu Wakristo wengi wa siku hizi wanaifuata, inamsaliti Mungu, inawadanganya watu na inaziongoza nafsi kwenda kuzimu. Na kwa kweli kuamini katika injili ya jinsi hiyo ni sawa na kulikataa Neno la Mungu la uzima wa milele. Manabii wa uongo ambao wanafundisha juu ya Msalaba wa Kristo peke yake wanaubadilisha Ukristo kuwa kama moja ya dini za ulimwengu huu. Hii ndiyo sababu kuwa ile injili ambayo wapo radhi kuifuata inatofautiana sana na injili ya kweli ya maji na Roho. 
Ukristo ni dini pekee inayoamini katika Mungu na Kristo aliye hai. Hata hivyo, hata kama Ukristo unawezekana kuonekana kuwa upo juu ya dini nyingine zote za ulimwengu na ikajitangazia kuwa ndio ukweli halisi, kama itaendelea kujitangaza katika imani yake ya Mungu mmoja na kisha kuachilia mbali injili ya maji na Roho, basi itakuwa si imani ya upendo na kweli bali itabakia kuwa ni dini ya upotofu.
 

Mahali pa Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa
 
Hapa hebu tuangalie mahali ambapo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa iliwekwa katika ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Katika vifaa vyote vya Hema Takatifu la Kukutania, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ndiyo kubwa kuliko. Pia kilikuwa ni kifaa cha kwanza katika vifaa vya Hema Takatifu la Kukutania ambacho makuhani walikutana nacho wakati walipoingia kwa kufuata ule mfuatano unapoingia katika Mahali Patakatifu kwa ajili ya kuabudu. Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ni mahali pa kuanzia kiimani katika Mungu, na inahitaji watu kufuata kanuni yake ili waweze kumkaribia. Kwa meneno mengine, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa inadhihirisha ukweli kwamba watu ni lazima walitatue tatizo la dhambi zao zote kwa kufanyika waamini kuliko kuwa wasioamini, kwa kuwa kutokuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana na Msalaba hakuwezi kumruhusu mtu kwenda mbele ya Mungu aliye hai. 
Sisi tumeokolewa toka katika dhambi kwa kuamini katika ubatizo na kifo cha Mwana wa Mungu, na hatujaokolewa kwa kutokuamini. Sisi tumeokolewa toka katika dhambi zetu na tumepokea maisha mapya kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Mwana wa Mungu iliyomwagika. Kwa kuwa injili hii ya maji na Roho ni ya muhimu sana, na ya msingi, na iliyo kamilifu sana, basi ni lazima tuendelee kuitafakari kwa kuirudiarudia katika mioyo yetu. Ni lazima tuitambue injili hii na kisha kuiamini. Ni lazima tuamini katika mioyo yetu kuwa sisi sote tulikuwa tumefungwa kuzimu, na pia ni lazima tuamini, pamoja na imani hii, kuwa Bwana alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kubatizwa na kubeba adhabu ya dhambi zetu kwa kuimwaga damu yake Msalabani. 
Pamoja na madhabahu hii ya sadaka ya kuteketezwa, kule kusema kuwa vitako vya nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania viliundwa kwa shaba kunatueleza sisi kuwa ni lazima tukiri ukweli kuwa sisi sote tunastahili kutupwa kuzimu kwa sababu ya mawaa tuliyonayo. Na kwa mujibu wa hukumu ya Mungu, ambayo inatangaza kuwa “mshahara wa dhambi ni mauti,” ni wazi kuwa sisi sote tumefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu. 
Lakini ili kutuokoa sisi viumbe wadhaifu namna hiyo ambao kwa kweli ni lazima twende kuzimu toka katika dhambi zetu zote na hukumu ya dhambi, Bwana wetu alifanyika mwili na akaja hapa duniani, akazichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa, akazibeba dhambi za ulimwengu hadi Msalabani, alihukumiwa na kuimwaga damu yake, na kwa hiyo ametuokoa wewe na mimi kikamilifu toka katika dhambi zetu na adhabu ya dhambi. Ni wale tu wanaoamini katika ukweli huu ndio wanaoweza kuungana na Kanisa la Mungu na kufanyika watu wake. Kisitiri na nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania vinatuonyesha sisi kuwa ni wale walio na imani hii tu ndio wanaoweza kufanyika watu wa Mungu na kisha kuingia katika Ufalme wake. 
 


Ni Lazima Tuamini katika Ukweli Uliodhihirishwa katika Rangi Nne za Kisitiri cha Mlango wa Hema Takatifu la Kukutania

Ni Lazima Tuamini katika Ukweli Uliodhihirishwa katika Rangi Nne za Kisitiri cha Mlango wa Hema Takatifu la Kukutania
Je, unaamini kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa kuja hapa duniani kwa kupitia huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa? Nyuzi za zambarau zinaonyesha kuwa Yesu ni Mungu mwenyewe; nyuzi za bluu zinaonyesha kuwa Yesu alifanyika mwanadamu na akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa hapa duniani; na nyuzi nyekundu zinamaanisha kuwa Yesu Kristo ambaye alikuwa amezipokea dhambi zetu zote, aliutoa mwili wake wa thamani kwa kusulubiwa. Ni muhimu sana kwetu kuamini kuwa Yesu aliyebatizwa na aliyesulubiwa alifufuka tena toka kwa wafu na kwa hiyo ametuokoa wewe na mimi kikamilifu. 
Ni wale tu wanaoamini katika ukweli huu ndio wanaoweza kufanyika kuwa wafanyakazi wa Kanisa la Mungu. Nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zina maanisha kuwa ni wafanyakazi. Zinatuonyesha sisi kuwa wale wanaoamini kwa namna hii ni watu wa Mungu, na kwamba ni watu wa jinsi hiyo tu ndio wanaoweza kutumiwa na Mungu kama wafanyakazi wake na nguzo. 
Nyuzi za kitani safi ya kusokotwa zinatueleza sisi kuwa wale waliofanyika watu wa Mungu, yaani wenye haki, ndio wale ambao hawana dhambi kabisa katika mioyo yao. Wenye haki ni wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi zao kwa kuamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Bwana wetu alikuja hapa duniani na amewaokoa wenye dhambi wote kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana na damu ya Msalaba. Kwa kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa kuyatoa maisha yake ya thamani, basi sisi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumwamini yeye aliyekuja kwa maji na damu (1 Yohana 5:6). 
Nyuzi za zambarau zinazungumzia kuwa Yesu ni Mfalme wa wafalme. Kwa meneno mengine, ni lazima tuamini kuwa Bwana ametuokoa sisi ambao ni wa chini na tuliojawa na mawaa kwa kuyatoa maisha yake ya thamani, na kwamba kwa jinsi hiyo ametufanya sisi kuwa watu wa Mungu. Sasa, ikiwa tutauamini ukweli huu katika mioyo yetu, basi kwa imani yetu katika wokovu mkamilifu, sisi sote tunaweza kufanyika wenye haki wasio na dhambi. Ni lazima tumshukuru Mungu kwa kutupatia sisi karama hii ya imani ili kwamba tuwe na imani kama hiyo. 
Kwa kweli, kule kufikia hatua ya kuuamini ukweli huu ni kitu ambacho twaweza kukiita kuwa ni karama toka kwa Mungu. Wokovu wetu toka katika dhambi pia ni karama toka kwa Mungu. Je, Mungu hajatukomboa sisi toka katika dhambi zetu kwa kutupatia maisha yake ya thamani ambayo yana heshima kuliko sisi? Kwa kuwa Yesu alibatizwa, akafa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo ametupatia karama ya wokovu, basi wale wote wanaoamini katika injili hii wanaweza kupokea karama ya wokovu na kufanyika watu wa Mungu mwenyewe. Inapofikia katika wokovu, kwa hakika hakuna jambo au kazi yetu binafsi. Sisi hatuna kitu cha zaidi cha kukifanya bali kuamini katika Yesu Kristo aliyekuja kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Wokovu huu ni karama ya Mungu kwetu. 
Imani katika Yesu inaanza kwa kufikiria kwanza ikiwa ni ni “kweli au sikweli kuwa tumefungwa kuzimu.” Kwa nini? Kwa sababu tunapotambua kwanza na kukiri ile hali yetu ya dhambi, basi hatuwezi kukwepa zaidi ya kuamini katika ukweli kuwa Yesu alifanyika kuwa sadaka yetu ya hatia kwa ajili ya dhambi zetu. Kule kusema kuwa tunaweza kuokolewa wakati tukiendelea kutenda dhambi kumewezekana kwa karama ya wokovu iliyotolewa na Bwana ambaye alijitoa mwenyewe kusulubiwa kwa ajili yetu. Je, sisi tumeokolewa kwa kumwamini Bwana? Je, tumefanyika kuwa wana wa Mungu kwa imani? Je, ni kweli kuwa tuna imani ya jinsi hiyo? Je, tunaweza kukiri kuwa wokovu wetu ni karama ya Mungu na sio matendo yetu? Je, tunakiri kweli kuwa tulikuwa tumefungwa kuzimu kabla ya kuamini katika karama ya wokovu iliyotolewa na Mungu? Ni lazima tuyachunguze mambo haya mara moja zaidi. 
 


Hema Takatifu la Kukutania Ni Taswira ya Wazi na Ya Kina ya Yesu

 
Ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania kunaifunga midomo ya manabii wa uongo. Tunapolifungua Neno la Hema Takatifu la Kukutania na kisha kulizungumzia mbele yao, basi ule uongo wao wote unafunuliwa. 
Nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zilifunikwa zote kwa dhahabu. Hii inaonyesha kuwa hakuna mahali katika Hema Takatifu la Kukutania panapoweza kuwa na alama za kibinadamu. Kila kitu ndani ya Hema Takatifu la Kukutania kilifunikwa kwa dhahabu. Nguzo za mlango wake zilifunikwa kwa dhahabu, pia na vifuniko juu ya nguzo pia vilifunikwa kwa dhahabu. Hata hivyo, vitasa vya nguzo viliundwa kwa shaba. Hii inatueleza kuwa, kwa sababu ya dhambi zetu na mawaa, basi wewe na mimi tulifungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi hizi. Je, hii si kweli? Je, si ndivyo hali ilivyo? Je, unaamini kuwa ulifungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zako alizokuwa ukizifanya kila siku? Kule kusema kuwa ulifungwa kuzimu kwa ajili ya dhambi zako hiyo ni hukumu ya haki ya Mungu iliyotoelwa na Mungu. Je, unaikubali kweli hukumu hii? Ni lazima uikubali! Hili si suala la ufahamu tu, bali ni lazima uukubali ukweli huu kwa kuuamini. 
Biblia inasema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10). Tunapotambua katika mioyo yetu kwamba tulifungwa kuzimu, na tunapoamini katika ukweli kwamba Bwana ametuokoa sisi kwa kutupatia karama ya wokovu iliyotimizwa katika kazi zake zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi sisi sote tunaweza kuingia na kuishi Mahali Patakatifu. Sisi tunaamini kuwa Bwana alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa, na kwamba akaimwaga damu yake na kufa Msalabani, na kwamba kwa kufanya hivyo amezioshelea mbali dhambi zetu zote na toka katika adhabu yetu ya dhambi. Bwana ametufanya sisi kuwa wenye haki kwa kutuokoa kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Ni lazima tuuamini ukweli huu katika kina cha mioyo yetu. Ni wale tu wanaoamini katika ukweli huu katika kina cha mioyo yao ndio wanaoweza kufanyika watu wa Mungu na wafanyakazi wake. Kuupokea ukweli huu kama ni moja ya mawazo yaliyotolewa na wanadamu hiyo si imani ya kweli. “Aah, kwa hiyo Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na maana hii. Nimesikia mara nyingi kuhusu nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu katika kanisa langu, kwa hiyo maana yake inaweza kutafsiriwa kama vile!” Hata kama uliamini katika ukweli kwa mawazo yako tu hadi sasa, sasa ni wakati ambapo unaweza kwa ukweli kabisa kuamini katika injili ya maji na Roho katika moyo wako. 
Vitako vya nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania viliundwa kwa shaba. Lakini vitako vya shaba vilitumika kwa ajili ya zile nguzo tano tu za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania; nguzo za pazia la Patakatifu pa Patakatifu hazikuwa na vitako vya shaba bali vilikuwa na vitako vya fedha. Katika Biblia, fedha inamaanisha kuwa ni karama na neema ya Mungu, ilhali dhahabu inasimama badala ya imani ya kweli inayoamini katika kina cha moyo. Kwa upande mwingine, shaba inasimama badala ya hukumu ya dhambi. Je, sisi hatukufungwa ili kuhukumiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zetu? Kila mmoja wenu alipaswa kuhukumiwa kwa sababu ya dhambi zake mbele za Mungu na mbele za watu. Je, hivi si ndivyo ilivyo? Sisemi kuwa ninyi nyote mlikuwa kama hivi. Bali, ninakiri mbele za Mungu kuwa mimi mwenyewe nilikuwa kama hivyo. Kwa maneno mengine, ninalizungumzia jambo hili sio kwenu tu bali hata na mimi mwenyewe. Mimi binafsi, ninatambua kikamilifu mbele za Mungu kuwa nilikuwa nimefungwa kuzimu ili kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi zangu na kwa mujibu wa Sheria yake. Ninalikiri jambo hili vizuri. 
Bwana alikuja hapa duniani kwa ajili ya kiumbe kama mimi. Bwana alikuja katika mwili wa mwanadamu, akazichukua dhambi zangu zote katika mwili wake kwa kubatizwa, alibeba adhabu ya dhambi zangu kwa kufa Msalabani, na amefanyika kuwa Mwokozi wangu mkamilifu kwa kufufuka tena toka kwa wafu. Hivi ndivyo ninavyoamini. Na nilipoamini hivyo, wokovu wangu ambao Mungu alikuwa ameupanga hata kabla ya uumbaji basi wokovu huo ulitimizwa wote. Wokovu huo ulitimizwa wakati nilipoamini katika ukweli huu katika kina cha moyo wangu.
Mioyo yenu pia ipo kama hivi. Kwa kuamini katika ukweli huu, wokovu wenu ambao Mungu alikuwa ameupanga katika Yesu Kristo hata kabla ya misingi ya ulimwengu huu, utatimizwa katika mioyo yenu. Mpango wa Mungu ili kuwafanya ninyi kuwa watu wake unatimizwa wakati mnapoamini katika mpango huu katika vina vya mioyo yenu. Ni kwa kuamini katika mioyo yenu ndipo wokovu wa kweli unapokuja katika vina vya mioyo yenu. Wokovu haufikiwi kwa mawazo ya mwili. Wokovu hauji kwa fundisho lolote la kitheolojia. Bali unakuja kwa imani katika ukweli.
 


Wokovu Huu Ulikuwa Umepangwa Katika Yesu Kristo Hata Kabla ya Uumbaji

 
Wokovu ni karama ambayo imetolewa kwetu katika Yesu Kristo kwa kupitia ubatizo wake na damu ya Msalaba. Wokovu huu ulitimizwa hapa duniani takribani miaka 2,000 iliyopita. Na hakuna anayetengwa katika karama hii ya wokovu kwa sababu Yesu ameutimiza mpango wa Mungu wa wokovu ili kuzitoweshea mbali dhambi za kila mtu. Kwa hiyo, wale walioamini katika wokovu huu katika vina vya mioyo yao basi wamefanyika wote kuwa wana wa Mungu. Dhambi zao zote zimetoweshewa mbali na kufanywa kuwa nyeupe kama theluji, na wote wamepokea ondoleo la dhambi zao bure. 
Lakini bado kuna watu wengi katika ulimwengu huu ambao hawajapokea ondoleo la dhambi. Watu hawa ni akina nani? Ni wale wasioamini katika ukweli hata pale wanapoufahamu. Wale ambao hawajakiri katika vina vya mioyo yao kwamba wamefungwa kuzimu, na wale ambao hawajaitambua injili ya maji, na damu na Roho—basi watu wa jinsi hiyo hawana lolote la kufanya kuhusiana na Bwana. 
Wokovu wa Mungu unatolewa kwa wale tu kwa wale wanaoifahamu asili yao ya dhambi na kutambua ya kuwa wamefungwa ili kuhukumiwa na kutupwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zao. Ni wapi basi ambapo palikuwa na nguzo tano za mlango wa kisitiri wa Hema Takatifu la Kukutania ambao ulikuwa umefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilipokuwa zimesimamishwa? Zilikuwa zimesimamishwa katika vitako vya shaba. Wewe na mimi tulikuwa tumefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu. Ni mpaka pale tunapoukubali ukweli huu ndipo wokovu wetu unapoweza kuinuliwa na kutambuliwa. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,” Bwana wetu alikuja hapa duniani kwa ajili yangu na yako, alibatizwa na Yohana Mbatizaji, akaimwaga damu yake Msalabani na akasulubiwa, na kwa hiyo ametupatia wokovu toka katika dhambi zetu. 
Kwa hiyo, wewe na mimi ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho katika vina vya mioyo yetu. Mioyo yetu ni lazima itambue walau mara mora kuwa, “Kwa kweli nimefungwa kwenda kuzimu, lakini Bwana ameniokoa mimi kwa kupitia maji na Roho.” Ni lazima pia tuamini katika mioyo yetu kuwa sisi tumeokolewa. Kama Warumi 10:10 inavyosema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” 
Ni lazima tuamini kwa kweli katika wokovu wetu katika vina vya mioyo yetu na kisha tukiri kwa vinywa vyetu: “Bwana ameniokoa mimi kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Nilipaswa kutupwa kuzimu na kuhukumiwa, lakini Bwana amezioshelea mbali dhambi zangu kwa niaba yangu, amezichukua dhambi zangu katika mwili wake, amebeba adhabu yangu badala yangu, na kwa hiyo ameniokoa mimi kikamilifu. Bwana amenifanya mimi kuwa mwana wa Mungu kikamilifu.” Kwa njia hii ni lazima tuamini katika mioyo yetu na kisha kukiri kwa vinywa vyetu. Je, unaamini? 
Je, kwa namna yoyote ile bado huuamini ule ukweli kuwa ulifungwa kuzimu hata wakati unapoamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na hata pale unapoamini kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa njia hii? Biblia inasema, “Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Imani ya kweli ni kuamini kuwa pamoja na kuwa wote wamefanya dhambi na kwamba watapaswa kwenda kuzimu, Bwana alikuja hapa duniani, alibatizwa, alikufa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametufanya sisi kuwa wenye haki kikamilifu. 
Wokovu huu ni wa kushangaza kiasi gani? Je, si kitu cha ajabu? Hema Takatifu la Kukutania halikufanywa kwa namna yoyote ile bali lilitengenezwa kwa mujibu wa Neno la Mungu lililoelezewa kwa kina. Kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania, Mungu alitueleza sisi mapema kabla na kwa kina kuwa atatuokoa kwa kuyatoa maisha yake ya thamani. Anatueleza sisi kuwa kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania ndio maana Yesu ametupatia wokovu wa thamani kwa kubatizwa na kufa Msalabani, na tunachotakiwa kukifanya hapa ni kuamini katika ukweli huu katika vina vya mioyo yetu. Ni nani anayeweza kuutoa wokovu kwa ajili yako? Unaweza kuokolewa kwa kuamini katika Yesu Kristo aliyekuja katika mwili wa mwanadamu kama wewe mwenyewe. 
Ikiwa mtu amezichukua dhambi zako na alihukumiwa kwa haki kwa niaba yako, basi bila shaka utakuwa na sababu nyingi za kumshukuru, lakini Bwana Yesu ambaye ana thamani na tajiri zaidi mara milioni kuliko sisi aliutoa mwili wake wa thamani kuwa sadaka kwa ajili yetu—hili ni jambo la kushukuru kiasi gani? Ule ukweli kuwa Bwana ametupatia karama ya thamani ya wokovu kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni wa thamani kiasi gani? Je, inawezakanaje basi tukashindwa kuuamini ukweli huu katika mioyo yetu? 
Hii ndiyo sababu wale wote wanaokiri ile hali yao ya dhambi ni lazima waamini katika ukweli huu. Wale ambao wanastahili kuamini katika ukweli huu ni wale wanaokiri kuwa hawawezi kukwepa zaidi ya kutupwa kuzimu. Ni wale tu wanaojitambua kuwa ni wenye dhambi, na kwamba wamefungwa kuzimu ndio wanaostahili kuamini katika wokovu wa Mungu wa thamani pamoja na kuupokea wokovu huo kwa imani. Na wale wanouamini ukweli katika mioyo yao wanaweza kufanyika wafanyakazi ya Kanisa la Mungu. 
Sisi ni viumbe wadhaifu ambao hatuna kitu cha kujivunia, hata pale tunapojilinganisha sisi wenyewe na wale ambao wamekuwa mashuhuri katika ulimwengu pamoja na uwezo wao wote wenye mipaka. Hali inapokuwa hivi, tunawezaje basi kujivuna sisi wenyewe mbele ya Mungu mtakatifu, mkamilifu, na mwenye nguvu zote? Kitu ambacho tunaweza kukifanya mbele yake ni kukubali tu kuwa Bwana ametuokoa sisi hata pale tulipokuwa hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kufa kwa sababu ya makosa yetu. 
Biblia inatuambia sisi kuwa, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23). Kwa kweli, tulipaswa kulipa mshahara wa kifo kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini kwa sababu Bwana wetu ametuokoa sisi ambao tulikuwa tumefungwa kuzimu, basi sasa tunaweza kuingia mbinguni kwa imani hii. Ikiwa tutaiacha imani yetu, basi sisi sote tumefungwa kuzimu mara mia. Je hivi si ndivyo ilivyo? Kwa kweli ndivyo ilivyo. Sisi sote tunastahili kutupwa kuzimu. 
Lakini kwa sababu Bwana mtukuka kwa upendo wa kina alikuja hapa duniani, alibatizwa, na akaimwaga damu yake na kisha akahukumiwa Msalabani, sasa tumekiepuka kituo chetu hakika cha kuzimu. Kwa sababu Bwana ameyatoa maisha yake yenye thamani kwa ajili yetu, basi sisi tumepokea ondoleo la dhambi. Hali inapokuwa hivi, tunawezaje basi kutoamini kuwa Bwana ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu mara moja na kwa ajili ya wote, na kwamba ametupatia sisi karama ya wokovu? Tunawezaje kukataa kufanyika wenye haki? Unawezaje kutoamini katika hili? Kama ambavyo nguzo katika mlango wa kisitiri wa Hema Takatifu la Kukutani zilivyofunikwa kwa dhahabu, basi vivyo hivi sisi nasi tunapaswa kuifunika mioyo yetu kwa imani. Ni lazima tujifunike sisi kikamilifu katika imani. Ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho katika vina vya mioyo yetu. Pasipo kuamini katika injili hii ya kweli katika vina vya mioyo yetu, basi hatuwezi kwenda mbele za Mungu. 
Ni kwa imani tunaweza kuwa wenye dhambi tuliofungwa kwenda kuzimu. Ni kwa imani pia tunaweza kufanyika wenye haki mbele za Mungu. Kwa maneno mengine, ni kwa imani ndipo wenye dhambi wanaweza kupokea ondoleo la dhambi zao—kwa kuamini kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa kupitia maji na damu. Hivi ndivyo Neno la Bwana wetu lisemavyo, “na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27), lilivyotimizwa. 
Wakati tulipozaliwa hapa ulimwenguni mara moja, tulikuwa tayari tunapaswa kuhukumiwa kwa dhambi zetu. Hata hivyo, Mungu ametupatia karama ya wokovu kwa kupitia Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho katika vina vya mioyo yetu, basi tumewezeshwa kufanyika wana wa Mungu. Mungu amewapatia upendo wake usio na masharti kwa wale wanaoamini. Lakini Mungu atawahukumu na kuwaadhibu wale wasioamini katika injili hii kwa ajili ya dhambi zao na kutokuamini (Yohana 3:16-18).
 

Ni Lazima Tuamini katika Kweli Hizi Mbili za Wokovu
 
Sisi tulikuwa ni wenye dhambi ambao tulifungwa ili kuhukumiwa na kisha kuuawa kwa ajili ya dhambi zetu, lakini kwa kuamini katika wokovu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambao Mungu alikuwa ameupanga na akatupatia, sisi tumepokea ondoleo la dhambi zetu. Kwa kweli ni lazima tukiri kwa Mungu, “Kwa kweli nimefungwa kuzimu,” na pia ni lazima tukiri, “Lakini ninaamini kuwa Bwana ameniokoa kwa kupitia maji na damu.” Ni lazima tuamini katika injili ya maji, damu na Roho; ambayo ni ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa kuamini katika ukweli huu katika vina vya mioyo yetu ndio maana tumeokolewa. Ni kwa kuamini katika injili ndio maana tumeokolewa. 
Sisi tumeokolewa kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Watu wanaweza kufanyika watu wa Mungu mwenyewe wakati wanapoamini kuwa Bwana amewaokoa wanadamu wote ambao walikuwa wamefungwa kuzimu kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Je, unaamini? Imani katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ndiyo imani ya kweli. 
Hii ndiyo maana ya kiroho iliyodhihirishwa katika mlango wa kisitiri wa Hema Takatifu la Kukutania. Je, unaamini? Wakati watu wanafikia kuuamini ukweli katika mioyo yao, basi wanaweza kuongea kwa usahihi juu ya imani ya kweli. Imani ya kweli si kule kuukiri ukweli kwa midomo tu ilhali mtu haamini katika moyo, bali ni kukiri kwa kinywa na kisha kuuamini ukweli huo katika kina cha moyo. Ninyi nyote ni lazima muamini katika wokovu wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambavyo vimekuokoa wewe milele. 
Hatuwezi kumshukuru Mungu vya kutosha hata kama tutamtumika kwa nguvu kiasi gani. Tunawezaje basi kuusahau wokovu wetu? Tunawezaje kusahau kuwa Bwana ametuokoa wewe na mimi, ambao tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kufungwa kuzimu toka katika dhambi zetu zote? Tunawezaje kuisahau injili ya maji na Roho wakati mawaa yetu yanafunuliwa kila siku? Tunawezaje kuidharau injili hii wakati hakuna njia nyingine ya sisi kuokolewa kwayo zaidi ya injili hii? Tunashukuru sana. Tunafurahia wakati wote. Hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumsifu Mungu. 
Wale ambao hawaufahamu ukweli huu wanasema kuwa Mungu aliwafanya wanadamu kama midori tu na anafurahia anapowaona. Hali wakisimama kinyume na Mungu wanasema, “Ni lazima Mungu anachoshwa. Alituumba sisi kama midori yake ili aweze kucheza pamoja nasi. Anafahamu kuwa tutatenda dhambi, na pia anatuangalia tu tunapotenda dhambi, na sasa Mungu anasema kuwa amewaokoa wenye dhambi. Je, si kwamba Mungu ametufanyia mchezo wa mdori? Mungu ametuumba na kisha anatuchezea kadri anavyotaka. Je, Mungu hakutufanya sisi kuwa midori yake?” Watu wengi wasiohesabika wanafikiria kama hivi. Wanambebea Mungu malalamiko dhidi ya Mungu hali wakisema ikiwa anawapenda kweli wanadamu, basi angaliwaumba kuwa viumbe vikamilifu badala ya kuwaumba kama wenye dhambi wenye mapungufu. Kuna watu wengi ambao wanabakia hawaufahamu moyo wa Mungu na kwa hiyo wanaendelea kumnyooshea kidole cha shutuma. 
 

Sisi Sote Ni Viumbe Tulioumbwa na Mungu
 
Kama mimea na wanyama, wanadamu pia ni viumbe ambao wameumbwa na Mungu. Lakini Mungu hakutuumba sisi wanadamu kama mimea na wanyama. Hata kabla ya kutuumba, Mungu alikwisha amua kutufanya sisi kuwa watu wake mwenyewe katika Yesu Kristo Mwanae na kisha kuturuhusu kujiunga katika utukufu wake, Mungu alituumba sisi kwa dhumuni hili. Dhumuni la uumbaji kwa wanadamu lilikuwa tofauti na lile la viumbe wengine. Je, ni kwa dhumuni gani ambalo kwa hilo Mungu alituumba sisi? Ni ili wanadamu hao waweze kuishi milele katika Ufalme wake katika utukufu wote, tofauti na mimea na wanyama ambavyo vyenyewe vimeumbwa ili tu kwamba viutukuze utukufu wa Mungu. Dhumuni la uumbaji wa Mungu kwa mwanadamu lilikuwa ni kuwawezesha kuzifahamu nafsi zao za dhambi, kumtambua na kumwamini Mwokozi ambaye amewaokoa kama Bwana wa uumbaji, na hivyo kufanyika wakamilifu na baadaye kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Mungu hakutufanya sisi kuwa kama maroboti au midori, lakini alituumba sisi ili tuweze kufanyika watoto wake kwa kumtambua Muumbaji, kumwamini Mwokozi, na kuzaliwa tena upya kwa kupitia injili ya maji na Roho. Kwa hiyo, kufuatia dhumuni hili la uumbaji wetu, sisi tutapokea na kuufurahia utukufu. Ingawa katika dunia hii tunajitoa wenyewe ili kuzitumikia nafsi zingine kwa injili, basi sisi nasi tutatumikiwa katika Ufalme wa Mungu. Unafikiri dhumuni la msingi la Mungu kwa mwanadamu lilikuwa ni nini? Ilikuwa ni kuwawezesha wanadamu kuufurahia utukufu wa Mungu milele. Dhumuni la Mungu katika kumuumba mwanadamu ilikuwa ni kuwafanya watu kuwa watu wake mwenyewe na kisha kuwaruhusu kushiriki katika ukuu na utukufu wake. 
Kwa nini tulizaliwa? Dhumuni la maisha ni nini? Je, sisi tulitoka wapi, na tunakwenda wapi? Maswali ya kifalsafa kama hayo bado hayajajibiwa, na kwa hiyo watu bado wapo kwenye huzuni wakijaribu kutatua tatizo hili. Hali wakiwa hawafahamu hali yao ya baadaye, baadhi ya watu wanabadilika na kuwa wabashiri na wachawi. Yote haya ni matokea ya kushindwa kwa mwanadamu kumtambua Mungu halisi aliyetuumba sisi na kuamini katika wokovu ambao Mungu amewapatia. 
Hata hivyo, ili kutufanya sisi kuwa watoto wake mwenyewe, Mungu alitufanya sisi kuwa tofauti kabisa na viumbe vingine vyote. Na ametuokoa sisi kwa kupitia maji na Roho, hali akiwa ameupanga wokovu wetu hata kabla ya uumbaji kwa kutumia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa kweli Mungu amelitimiza dhumuni lake kwetu kwa kutuokoa sisi kwa sheria ya wokovu iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Kwa hiyo, sasa ni lazima tutambue na kuamini katika dhumuni hili la Mungu la kutupatia uzima wa milele katika Yesu Kristo. Ikiwa hatulitambui dhumuni hili, basi fumbo la maisha litabakia bila kutatuliwa daima. Kwa nini tulizaliwa katika ulimwengu huu? Kwa nini ni lazima tuishi? Kwa nini ni lazima tule? Kwa nini ni lazima tuishi maisha yetu kwa kitambo tu? Tunaweza kutatua tatizo la maisha na kifo, maisha ya kuzeeka na kuugua? Kwa nini ni lazima twende kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu? Kwa nini maisha yana huzuni? Kwa nini maisha yana maumivu sana? Maswali hayo yote yanaweza kupata majibu yake toka kwa Mungu kwa kupitia injili ya maji na Roho ambayo imetuokoa sisi katika Yesu Kristo.
Mungu alituruhusu kuzaliwa hapa duniani na ametufanya sisi kuutarajia Ufalme wa Mbinguni katikati ya kuchoka na maisha magumu ili kwamba aweze kukuokoa wewe na mimi ambao tulikuwa tumefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu ili kwamba tuweze kupokea uzima wa milele. Tunapoamini katika injili ya maji na Roho, basi fumbo la maisha linakuwa limetatuliwa lote.
 

Mungu Alikuwa na Mpango Mkuu Kwa Ajili Yako na Mimi
 
Kama Mungu alivyopanga, alimtuma Mwana wake Yesu Kristo kuja hapa duniani, akazipitisha dhambi zetu zote katika mwili wake wa thamani kwa kumfanya abatizwe, alihukumiwa hadi kifo kwa ajili yetu na hiyo ametuokoa sisi ambao tulikuwa tunakabiliana na uharibifu wa milele toka katika dhambi zetu zote, adhabu na laana. Sasa ni lazima tuamini katika ukweli huu, na ni lazima tutoe shukrani zetu kwa Mungu kwa kutuondoa toka katika majaliwa ambayo tusingeweza kukwepa ya uharibifu kwenda katika Ufalme wa Mwana wa Mungu na kisha kuufurahia uzima wa milele. Kwa maneno mengine, ukweli wa wokovu toka kwa Mungu ni injili ya maji na Roho ambayo imedhihirishwa katika kisitiri kilichofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa na kisha kutungikwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania.
Vitako vya shaba vya nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania vinatuonyesha sisi kimsingi juu ya nafsi zetu zenye dhambi, na kisha kutuwezesha sisi kuamini katika injili ya maji na damu ya Yesu. Nguzo za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania na kisitiri kilichokuwa kimefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa vinadhihirisha juu ya rehema za Mungu ambazo zimetuokoa sisi ambao tulikuwa tumefungwa kuzimu na kutoka katika adhabu yetu ya dhambi kwa kupitia sadaka yenye thamani ya Yesu Kristo. Kwa hiyo kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, mimi nimeokolewa toka katika dhambi zangu zote. Je, wewe pia unaamini hivyo?
Je, unaamini katika ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania? Wewe na mimi tuna bahati. Kwa kweli ni baraka kuu sana, kwa kuwa hata kama kuna watu wengi ambao wanaelekea kuzimu, sisi tumeupata ukweli na sasa tunaishi ndani ya Yesu Kristo. Kwa kweli tulikuwa hatufai na tusio na maana katika ulimwengu huu, kwa kuwa tulikuwa tumezaliwa ndani ya ulimwengu huu hatukuweza kukwepa bali tulitenda dhambi na hivyo tukafungwa kuzimu ili tukaishi huko. Lakini hata hivyo, Bwana wetu alikuja hapa duniani, alibatizwa, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi toka katika dhambi zetu milele. Tunaweza kushangazwa kutokana na ukweli kuwa hatuna jambo lolote la kufanya kuhusiana na kuzimu lakini zaidi ya yote tumefanyika wenye thamani ambao tunaweza kuzifanya kazi zake za haki. 
Wale wanaoweza kuingia katika Mahali Patakatifu ni wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi zao mara moja kwa wote. Bwana wetu hakuzitoweshea tu dhambi zetu zilizopita, lakini kwa kubatizwa, alizichukua dhambi zote za muda wetu wa kuishi katika mwili wake, na kwa kufa kwake Msalabani amezitoweshea mbali dhambi zetu zote milele. Kwa hiyo, wale wanaoamini katika wokovu uliotimizwa wote mara moja, ndio hao walio na imani ya makuhani, na ni watu kama hao ndio wanaoweza kuingia Mahali Patakatifu.
Tukiongea kwa mkazo, kwa mujibu wa utaratibu wa Hema Takatifu la Kukutania, makuhani wa kawaida hawakuruhusiwa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu, bali Kuhani Mkuu ndiye aliyeruhusiwa. Na Kuhani Mkuu wa milele si mwingine bali ni Yesu Kristo. Ni wale tu wanaoamini kwamba Yesu Kristo ametuokoa sisi ndio wanaoweza kuingia katika Nyumba ya Mungu, hata katika Patakatifu pa Patakatifu wakiwa pamoja na Yesu Kristo.
“Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake; na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi” (Waebrania 10:18-22). Wale wanaojitambua wenyewe kuwa ni waovu na kwamba wamepangiwa kuzimu na wanapokea ondoleo la dhambi zao kwa kusafishwa kwa maji safi (Ubatizo wa Yesu) na damu ya Yesu wanaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu na kukaa naye milele.
Sisi hatujasafishwa kwa sababu tumezitubia dhambi zetu kila siku, bali ni kwa sababu Bwana alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi zetu za ulimwengu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kubatizwa, alisulubiwa Msalabani na ndio maana amezitoweshea mbali dhambi zetu zote. “Kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Yesu alibatizwa na akazichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake mara moja na kwa wote, alizibeba dhambi za ulimwengu hadi Msalabani na akafa juu yake, na akafufuka tena toka kwa wafu na kwa hiyo ametuokoa sisi milele mara moja. Ni wale tu wanaoamini katika ukweli huu katika vina vya mioyo yao ndio wanaoweza kuingia Mahali Patakatifu. Tunapokea ondoleo la dhambi mara moja kwa wote kwa kuamini kwamba Bwana wetu ametuokoa sisi sote mara moja, na kwamba alizishughulikia dhambi zote katika siku zote za maisha yetu za ulimwengu mzima.
Je, unaamini kuwa Bwana alizichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wote kwa kubatizwa? Na je unaamini kuwa Yesu alizibeba dhambi za ulimwengu, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi mkamilifu mara moja? Katika miaka yake 33 ya maisha, Bwana wetu amezitoweshea mbali dhambi zote za ulimwengu milele. Amezifanya dhambi hizo kutoweka bila ya kuacha hata doa moja. Mimi ninaamini hivi katika kina cha moyo wangu. Ninaamini kuwa wakati alipobatizwa, alizichukua dhambi za ulimwengu mara moja na kwa wote katika mwili wake, na ndio maana alibeba adhabu ya dhambi zangu zote mara moja kwa kuimwaga damu yake Msalabani, na kwamba amefanyika kuwa Mwokozi wangu mkamilifu kwa kufufuka toka kwa wafu na kuishi tena mara moja na kwa wote. Ni kwa imani hii ndio maana nimeokolewa toka katika dhambi zangu zote. 
Kwa kuamini katika imani hii, sisi sote tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni, na wakati tunapoishi hapa duniani ni lazima tuitafakari imani hii kila siku. Kwa nini? Kwa sababu Bwana alizichukulia mbali hata dhambi ambazo bado hatujazifanya. Lakini kila wakati tunapofanya dhambi ni lazima tukiri. Na ni lazima tuamini katika vina vya mioyo yetu kwamba Bwana alizichukua katika mwili wake hata hizo dhambi kwa ubatizo wake. Ni lazima tutambue kuwa Bwana alishughulikia dhambi za ulimwengu kwa kuamini tena. Kwa nini? Kwa sababu ikiwa hatutafakari katika injili ya maji na Roho mara kwa mara, mioyo yetu inaweza kuchafuliwa. Kwa kuwa Bwana alizichukulia mbali hata zile dhambi ambazo bado hatujazitenda, basi kila inapotokea kuwa udhaifu wetu unafunuliwa, basi ni lazima tumshukuru Mungu kwa imani yetu katika huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Ni lazima sisi tuamini kuwa Bwana alikuja hapa duniani na akazichukua dhambi zetu katika mwili wake mara moja na kwa wote. Dhambi zetu zilipitishwa kwa Yesu Kristo mara moja na kwa wote kwa kuwa alizipokea dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake. Kwa kuwa Yesu Kristo ametupatia wokovu wa milele kwa kubatizwa na kufa Msalabani, basi ni lazima tuamini katika ukweli huu kikamilifu na kwa ujasiri. Bwana wetu Yesu alisema kuwa tunaweza kuutwaa Ufalme wa Mungu kwa imani yetu imara katika ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana. Yesu alisema, “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka” (Mathayo 11:12). Ni kwa imani hii ndipo tunapoweza kuondolewa dhambi zetu zote za mawaa ya miili yetu, mawazo, fikra, na mwili. Kwa kuamini kuwa Bwana wetu alizichukua dhambi hizi zote katika mwili wake kwa ubatizo wake na kwamba alibeba adhabu zote za dhambi, basi ni lazima tuokolewe toka katika dhambi zetu zote na tuweze kuutwaa Ufalme wa Mungu. 
Haijalishi jinsi ambavyo mnaweza kuwa na mapungufu, ikiwa mna imani hii, basi ninyi ni watu wa imani. Japokuwa mna mapungufu, Bwana amewaokoa ninyi kikamilifu na kwa hiyo ni lazima muamini katika ukweli huu. Kwa kuwa Bwana wetu anaishi milele basi hata wokovu wetu ni mkamilifu milele. Tunachotakiwa kukifanya ni kuamini tu katika wokovu wetu ambao Yesu Kristo ametupatia. Hiyo ni sahihi! Sisi tumeokolewa kwa kumwamini yeye katika mioyo yetu. 
Kwa kuwa Bwana ni Mwokozi wetu mkamilifu, yeye amelitatulia mbali tatizo la dhambi zetu. Je, unaamini kuwa Bwana wetu alibatizwa, akamwaga damu yake Msalabani, akafa mara moja, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwamba ametupatia wokovu wa milele? Wokovu huu wa kushangaza kiasi gani? Ingawa tuna mapungufu mengi katika matendo yetu, bado tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kuamini katika ukweli huu. Ni kwa imani ndio tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu na kuufurahia utukufu wote na ukuu wa Mungu. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanastahili kufurahia furaha hizo za mbinguni. Lakini pasipo imani hii hakuna hata mmoja anayeweza kutia mguu wake katika Ufalme wa Mungu. 
Ukweli ambao umetuokoa sisi kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ulikuwa umepangwa na Mungu katika Yesu Kristo hata kabla ya uumbaji. Kwa kuwa Mungu alidhamiria kutuokoa, alikuja hapa duniani, alibatizwa na kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake mara moja na kwa wote, akazibeba dhambi za ulimwengu hadi Msalabani na akahukumiwa mara moja, akafa mara moja, akafufuka toka kwa wafu mara moja, na kwa hiyo ametupatia wokovu wa milele. Huu ni wokovu wetu ulioundwa kwa huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na ni lazima tuamini katika wokovu huu. Ni mpaka hatua hiyo ndipo tunapofanyika watu wa Mungu tuliokamilishwa kwa imani. Ni hapo tu ndipo tunapofanyika wafanyakazi wa Mungu kwa imani. Sisi tutaingia katika Ufalme wa Mungu mkamilifu na kuishi milele. 
Mungu mkamilifu ametuokoa sisi kikamilifu, lakini bado tuna mapungufu kila siku, kwa kuwa miili yetu ina mapungufu. Lakini inakuwaje hivyo? Wakati Bwana alipobatizwa kikamilifu mwili mzima, je ni kweli kuwa alizichukua dhambi zetu au la? Kwa kweli alizichukua! Kwa sababu Bwana wetu alizichukulia mbali dhambi zetu kwa ubatizo wake, basi tunatambua kuwa kwa hakika dhambi zetu zote zilipitishwa katika mwili wake kwa ubatizo. Je, unatambua kuwa dhambi zako zilipitishwa kweli kwa Yesu? Kwa kufanya hivyo, Yesu alizibeba dhambi zetu na dhambi za ulimwengu hadi Msalabani, alisulubiwa, na kwa hiyo aliutimiza kikamilifu mpango wa Mungu wa wokovu. Ingawa tuna mapungufu, tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kuamini. Kwa kuamini katika nini? Tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kuamini katika huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Baada ya kupokea ondoleo la dhambi, basi ni wale wenye mapungufu ndio wenye imani safi na wanafanya vizuri katika Kanisa. Kanisa la Mungu si mahali ambapo wenye nguvu wanatawala, bali ni mahali ambapo wenye mapungufu wanatawala kwa imani. Kwa nini? Kwa sababu katika Kanisa la Mungu tunaweza kumfuata Bwana kwa imani tu pale tunapotambua kuwa sisi tuna mapungufu. Kanisa ni mahali pa kutunzana na kuponyana majeraha. Kwa kuwa Mbinguni ni mahali ambapo mtoto anyonyae anaweza “kuweka mkono wake katika tundu la nyoka” (Isaya 11:8) na hatang’atwa, basi paradiso ya hapa duniani si nyingine zaidi ya Kanisa la Mungu. Hili ni fumbo la kushangaza la Kanisa la Mungu. 
Ni kwa imani ndipo tunapoweza kuingia katika Ufalme wa Mungu. Ni kwa nguvu za wenye imani ndio wanaoweza kuutwaa Ufalme wa Mbinguni. Unaamini juu ya ukweli huu katika moyo wako? Mimi, pia, ninaamini, na ndio sababu ninatoa shukrani zangu kwa Mungu. 
Na ni kwa sababu ninamshukuru Mungu ndio maana ninaitumikia injili hii. Ninaishi kwa ajili ya ukweli huu na ninaitumikia injili kwa kuwa kuna watu wengi ambao bado hawaufahamu ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Lakini hivi sasa, ukiachilia mbali swali la kusema kuwa kama kuna wengine wanaoitumikia injili hii au la, kinachohitajika kwako ni kuamini kwanza ukweli huu ndani yako. 
Ninaamini na ninaomba kuwa ninyi nyote mtaamini katika ukweli kuwa Yesu amewaokoa ninyi toka katika dhambi zenu mara moja na kwa wote, na hivyo kuokolewa toka katika dhambi zenu zote.