Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-13] Wale Wanaoweza Kupaingia Patakatifu pa Patakatifu (Kutoka 26:31-33)

Wale Wanaoweza Kupaingia Patakatifu pa Patakatifu
(Kutoka 26:31-33)
“Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo ya kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya mahali patakatifu na patakatifu pa patakatifu.”
 


Vifaa vya Hema Takatifu la Kukutania

 
Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni jengo dogo lililokunjwa na lililokuwa limefunikwa na aina nne za mapaa. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa limeundwa kutokana na vifaa mbalimbali—kwa mfano, kuta zake ziliundwa kwa mbao 48 za mti wa mshita. Kimo cha kila ubao kilikuwa ni mita 4.5 (dhiraa 10: futi 15), na upana ulikuwa sentimita 67.5 (dhiraa 1.5: futi 2.2). Mbao zote zilifunukwa kwa dhahabu. 
Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania yaliundwa kwa vifaa vifuatavyo: paa la kwanza liliundwa kwa mapazia yaliyofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu na kitani safi ya kusokotwa; paa la pili liliundwa kwa singa za mbuzi; paa la tatu liliundwa kwa ngozi za kondoo waume iliyotiwa nakshi ya rangi nyekundu, na paa la nne liliundwa kwa ngozi za pomboo.
Kama tulivyokwisha chunguza, milango yote ya Hema Takatifu la Kukutania ilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Rangi za nyuzi nne zilizotumika kwa ajili ya mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu zinadhihirisha kazi za Yesu Kristo ambazo zimewaokoa watu toka katika dhambi. Kwa kuwa rangi hizi nne ni mwanga wa ukweli unaodhihirisha kuwa Yesu Kristo atatupatia sisi karama ya ondoleo la dhambi, basi ni vitu ambavyo waamini wanavishukuru sana.
 

Vifaa vya Milango ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu
Vifaa vya Milango ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa PatakatifuVifaa vya milango ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu vilikuwa ni vitambaa vilivyofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Milango ya Hema Takatifu la Kukutania iliundwa kwa vitambaa hivi. Mtu aliweza kuuelekea mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu baada ya kuwa amepitia mlango wa Hema Takatifu la Kukutania uliokuwa ukielekeza kwenda katika Mahali Patakatifu. Mlango wa Patakatifu pa Patakatifu unatuonyesha sisi kuwa Bwana ameziondoa dhambi zetu kwa huduma zake nne zinazodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Nyuzi za rangi ya bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu ni kivuli kinachofunua kuwa Masihi atakuja hapa duniani, atabatizwa, atamwaga damu yake, na hivyo atazikamilisha kazi za wokovu. Miongoni mwa kazi hizi, nyuzi za bluu ni kivuli kinachodhihirisha ubatizo ambao Yesu ataupokea, na nyuzi nyekundu ni kivuli cha sadaka ya kuteketezwa ambayo Yesu ataitoa (mwili wake) kwa ajili ya dhambi za ulimwengu ambazo alizichukua katika mwili wake. Ili kuzioshelea mbali dhambi zetu, Bwana wetu alibatizwa na kubeba adhabu ya dhambi. Hivi ndivyo mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu unavyomaanisha. 
 

Sadaka ya Hema Takatifu la Kukutania
 
Hema Takatifu la Kukutania lilijengwa katika mchanga uliosawazishwa, yaani ardhi. Hapa udongo una maanisha ni mioyo ya watu. Kule kusema kuwa sakafu ya Hema Takatifu la Kukutania ilijengwa kwa mchanga na udongo kunatueleza sisi kwamba Yesu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu ili kuzitoweshea mbali dhambi za mioyo yetu. Kwa sababu aliyapitia madhaifu yote ya mwanadamu, aliziosha dhambi zao zote kwa ubatizo alioupokea na kwa damu ya thamani aliyoimwaga pale Msalabani. Bwana wetu alikuja hapa duniani kuuangaza mwanga wa ukweli kwa ulimwengu huu na kutatua tatizo la msingi la mwanadamu la dhambi. Yesu ni Mungu wa uumbaji aliyeuumba ulimwengu mzima na vitu vyote vilivyomo ndani yake, na yeye ni mwanga wa wokovu aliyekuja hapa duniani kuwakomboa wanadamu toka katika laana na dhambi zao zote. 
 
 
Nguzo za Patakatifu pa Patakatifu
 
Nguzo za Patakatifu pa Patakatifu ziliundwa kwa nguzo nne za mti wa mshita. Katika Biblia, namba 4 ina maanisha ni mateso. Nguzo za Patakatifu pa Patakatifu zinatuonyesha sisi kuwa watu hawawezi kuokolewa hadi pale watakapoamini katika mwanga unaong’aa wa wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa maneno mengine, nguzo hizi zinadhihirisha kuwa tunaweza kuugundua mwanga unaong’aa wa wokovu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho iliyotimizwa na Mungu mwenyewe kwa kupitia mateso yake. 
Yeyote anayependa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu na kusimama mbele za uwepo wa Mungu ni lazima aamini katika injili inayong’aa ya maji na Roho, injili ya wokovu ambayo Mungu ameiandaa. Lakini wale wanaomjia Mungu pasipo kuamini katika injili iliyowekwa na Mungu watakabiliana na hasira kali ya Mungu. Wale wanaosimama mbele za Mungu ni lazima wawe na imani inayoamini katika ukweli unaong’aa uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa kupitia mwanga wa ukweli unaong’aa, sisi sote ni lazima tupaingie Patakatifu pa Patakatifu mahali ambapo Mungu anakaa. 
Injili ya ondoleo la dhambi iliyofunuliwa katika Agano la Kale ni ukweli wa wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Injili ya kweli ya ondoleo la dhambi iliyofunuliwa katika Agano Jipya ilitimizwa kwa kupitia ubatizo ambao Yesu aliupokea, kwa kupitia damu ya Msalaba, na ufufuo wa Yesu. Tunaweza kupaingia Patakatifu pa Patakatifu tunapokuwa na imani inayoaamini katika injili hii takatifu sana. 
 
 

Ni Lazima Tuamini Katika Wokovu Wetu Uliodhihirishwa Katika Nyuzi za Bluu, Zambarau, na Nyekundu

 
Waebrania 11:6 inasema, “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.” Mungu ataishi milele. Na ili kutupatia uzima wa milele, Mungu ametubariki kupokea ondoleo la dhambi kwa imani katika Yesu Kristo aliyekuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alibatizwa na kusulubiwa, alikufa, kisha akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu. Bwana ametuvika utakatifu mkamilifu kwa kuzioshelea mbali dhambi zetu zote za nafsi za kale kwa kupitia hukumu takatifu kwa ajili ya dhambi zetu, na kwa kuzipatia nafsi zetu imani inayoamini katika injili ya maji na Roho. 
Kwa kutuvika sisi katika maisha mapya, Bwana wetu ametuwezesha kwenda mbele za Mungu na kumwomba yeye. Zaidi ya yote, pia ametupatia neema ya kuwa tayari kusimama mbele za uwepo wa Mungu na kumwita yeye Baba yetu. Vitu hivyo vyote ni karama za Mungu ambazo zimekuja kutokana na wokovu ambao Mungu ametupatia. Mungu ametufanya sisi kuwa na imani inayotuwezesha kuokolewa na kusimama mbele za Mungu kwa kutuletea wokovu huu kupitia ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Ikiwa mimi na wewe tungekufa kesho, je, tunajiamini vya kutosha kuwa tutaenda Mbinguni? Hebu tufikirie kidogo kuhusu siku zetu za baadaye. Wakati watu wanapokufa, wote wanasimama mbele ya kiti ya cha hukumu cha Mungu. Hii inamaanisha kwamba ni lazima tutatue tatizo la dhambi zote tulizozifanya hapa duniani—je, tunawezaje basi kulitatua jambo hili? Ikiwa tunamwamini Yesu kwa upofu kuwa ni Mwokozi wetu, je, hii haimaanishi kuwa tunakuwa tukiiamini dini tu? 
Kulikuwa na wakati katika maisha yangu nilipokuwa sifahamu chochote kuhusu injili ya maji na Roho na nilijaribu kutatua tatizo la dhambi zangu kwa kuamini kwa upofu katika damu ya Msalaba tu. Kwa wakati huo, nilikuwa nimeamini kwa nguvu kabisa kwamba Yesu alisulubiwa na kufa kwa ajili ya watu kama mimi, na kwamba aliyatatulia mbali matatizo yote ya dhambi. Lakini kwa imani hii, sikuweza kutatua tatizo la dhambi za kila siku nilizokuwa nikizifanya. Ukiachana na hali hiyo, ni mpaka pale nilipoamini katika wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ndipo roho yangu ilipozaliwa upya kikamilifu. 
Je, dhambi zetu zote zilitoweshwa pale tulipomwamini Yesu kwa upofu kuwa ni Mwokozi? Imani inayotuwezesha kwenda mbele za Mungu mtakatifu haipatikani kwa kumwamini Mungu kiupofu, bali inapatikana kwa kuufahamu na kuuamini ukweli. Haijalishi ni kwa nguvu kiasi gani tunaweza kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wetu, ikiwa hatuifahamu injili ya kweli ambayo imewaokoa wenye dhambi kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi ni kweli kuwa hatuwezi kuonana na Mungu mtakatifu. Ni pale tu tunapokuwa na imani inayoamini katika injili ya maji na Roho ndipo tunapoweza kuonana na Mungu mtakatifu. Je, ni vifaa gani vya imani vinavyouwakilisha ukweli unaotuwezesha sisi kusimama mbele za Mungu kama tuliookolewa? Je, ni injili ipi inayotuwezesha sisi kuwa na imani kama hiyo? Injili hii ni injili inayong’ara ya maji na Roho. 
Bwana wetu alikuja hapa duniani, alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, alisulubiwa, akamwaga damu yake, akafufuka toka kwa wafu siku ya tatu, na kwa hiyo aliutimiza wokovu wake mkamilifu kwetu sisi tunaoamini. Ikiwa nafsi zetu zinatamani kusafishwa toka katika dhambi, basi ni pale tu tunapouamini ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana (Mathayo 3:15) na damu ya Msalaba (Yohana 19:30) ndipo tunapoweza kuingia katika himaya angavu ya ukweli. Hatuwezi kuwa na mioyo ambayo ni myeupe kama theluji hadi pale tutakapomwamini Yesu Kristo ambaye amekuja kutokana na injili inayong’aa ya maji na Roho kuwa ni Mwokozi wetu.
Wakati mwingine tunapoyaangalia madhaifu ya miili yetu tunajikuta tukiomboleza kwa ajili ya miili hiyo. Lakini hata hivyo, kwa sababu ya injili ya maji na Roho, bado tunakuja kutoa shukrani zetu kwa Mungu, kwa kuwa Bwana amezitoweshea mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu yake. Wewe na mimi tusingeweza kufanyika watakatifu kwa namna yoyote ile, lakini kwa kuamini katika injili ya maji na Roho tumefanyika kuwa watakatifu. Bwana wetu ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi. Kwa kuamini katika injili ya nyuzi za bluu na nyekundu, tunaweza kugundua mwanga angavu wa ukweli uliotuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote. Bwana ametufanya sisi kuwa watakatifu kwa kupitia injili ya maji na Roho.
Katika Mathayo 19:24, Bwana wetu alisema, “Ni rahisi ngamia kupenya tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” Wale ambao ni matajiri katika roho hawawezi kuokolewa, kwa kuwa hawaamini kuwa wanaweza kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Ni wale tu ambao ni maskini wa roho, wale wanaotamani kuingia Mbinguni, wanaoomba msaada wa Mungu, wanaoweka mbali haki yao binafsi na badala yake wanaamini katika haki ya Mungu kwa asilimia 100 ndio wanaoweza kupokea uzima wa milele kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Injili ya maji na Roho imeangaza mwanga angavu wa wokovu ili kwamba tuweze kuonana na Mungu mtakatifu. Kwa kuzitegemea nguvu zetu wenyewe hatuwezi kamwe kufanyika watakatifu, lakini pale tunapoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana, basi kwa hakika ndipo tunapoweza kufanyika watakatifu na kuingia katika himaya angavu ya ukweli. 
 

Ni Lazima Tuachane na Imani ya Kidini na Imani ya Kimafundisho
 
Katika Yohana 3:3, Yesu mwenyewe alisema, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Katika hili, Nikodemo akauliza tena, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” (Yohana 3:4). 
Kwa wale ambao hawajazaliwa upya, kuzaliwa tena upya kwa imani inaonekana ni kitu kisichowezekana. Kwa nyakati fulani hata wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno yake na waliyatilia mashaka. Kwa hiyo, wakati mmoja Bwana aliwaambia wanafunzi wake, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana” (Mathayo 19:26). Kwa kweli, ni vigumu kwa wanadamu kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa imani yao ya kidini, lakini inawezekana kwao kuuingia Ufalme wa Mungu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Pamoja na kuwa hatuwezi kuwa watakatifu kwa kuzitegemea nguvu zetu, wale wanaoamini kuwa Bwana alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake, akasulubiwa, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwamba amewaangazia mwanga unaong’aa wa wokovu ambao umezitoweshea mbali milele dhambi zetu zote—basi Mungu amewawezesha kuingia katika Ufalme wake. 
Ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika kama vifaa katika Hema Takatifu la Kukutania kwa hakika vinahusiana sana na injili ya maji na Roho ambayo Yesu aliitimiza katika Agano Jipya. Kwa maneno mengine, injili ya maji na Roho ni sawa na ule ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni kivuli cha wokovu wake mkamilifu, na injili ya maji na Roho ni kitu halisi cha kivuli hiki. 
Kwa hiyo tunaweza kuugundua ukweli unaong’aa wa wokovu kwa kupitia injili ya maji na Roho na kisha kupumzika ndani yake. Kuna amani katika injili ya maji na Roho inayong’aa, kama vile mtoto aliyeachishwa ziwa anavyocheza, akapumzika, na kisha kulala kwa amani katika mikono ya mama. Ni kwa kuugundua mwanga mkuu mtakatifu katika injili ndipo tumeweza kuonana na Mungu mtakatifu. Ni kwa kuamini katika injili inayong’aa ndipo tunapoweza kuupata wokovu ambao Mungu ametupatia. Ni wale tu wanaoamini katika wokovu huu uliotolewa na Mungu ndio wanaoweza kupokea pumziko la milele. 
Kwa ufupi, kuamini katika injili takatifu zaidi ya maji na Roho ni imani pekee inayotuwezesha sisi kupaingia Patakatifu pa Patakatifu. Imani inayoamini katika injili hii inayong’aa ya maji na Roho inatuwezesha sisi kulipokea ondoleo la dhambi na kulifanya kuwa letu. Bwana wetu alikuja hapa duniani pamoja na ukweli wa injili ambao umezitoweshea mbali dhambi zetu mara moja na kwa ajili ya wote kwa kupitia ubatizo wake na Msalaba. Mungu ametimiza ahadi aliyoifanya kwetu kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni wale tu wanamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao na wanaoiamini injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kupokea uzima milele na kuingia Mbinguni. 
Ikiwa injili hii ya kweli ya maji na Roho ingekuwa imehubiriwa tangu miaka 30 iliyopita, basi kwa hakika ingekuwa imeenea ulimwenguni kote. Lakini ni mpango wa Mungu kwamba injili hii ienezwe katika nyakati za mwisho. Bwana wetu alisema katika Ufunuo kwamba watu wengi wasiohesabika wataokolewa toka katika dhambi zao katika nyakati za mwisho. Pia alisema kuwa kutakuwa na wafia dini au wafia imani wengi sana, na kwamba katika kipindi cha mateso watu wengi wataionyesha imani yao kwa kumwamini Bwana na kisha kupokea vifo vyao kutokana na dini au imani. Kwa meneno mengine, Bwana wetu, amelenga katika kipindi cha mwisho kuwa ni kipindi cha kuvuna nafsi nyingi. Mpango wa Mungu ni kwa wale tu wanaoamini kwa kweli katika injili hii ya kweli ili kupokea karama ya wokovu toka katika dhambi zote. 
Ni kwa sababu umekuwa na bahati ya kutosha kuweza kuisikia injili hii ya maji na Roho katika nyakati hizi kiasi kwamba umeweza kuokolewa toka katika dhambi zako zote. Kwa kweli ninamshukuru Mungu sana kwa kutupatia injili hii ya maji na Roho. Ni nini kingetokea kwetu sote ikiwa tusingeisikia injili hii ya maji na Roho? Lakini ni ukweli kuwa hata sasa si kila mtu anaipokea na kuikubali injili ya maji na Roho. Ukweli huu si kitu ambacho kinaweza kuingia kirahisi katika moyo wa kila mtu. 
Kwa kweli, tunaona kuwa ingawa kuna Wakristo wengi ulimwenguni mwote, wengi wao ni ama hawafahamu wala hawaamini katika injili ya maji na Roho. Je, inawezekanaje basi kwa watu hawa ambao hawaitambui injili ya kweli kukombolewa toka katika dhambi? Hii ndio maana Mungu ameturuhusu sisi kuieneza injili ya kweli kwa kupitia maandiko ya Kikristo. 
Kuna watu wengi ulimwenguni mwote ambao wanashuhudia kuwa wamekuja kutambua maana ya injili ya maji na Roho baaada ya kusoma maandiko ya injili ambayo tumekuwa tukiyasambaza. Kabla ya kuifahamu injili hii wao walikuwa wakifahamu kuhusu damu ya Msalaba tu, lakini sasa wanamshukuru Bwana kwa kuweza kuufikia uelewa mzuri wa injili ya maji na Roho na kisha kuuamini ukweli huo. Pia kuna wengi wanaoshuhudia kwamba hawakuufahamu umuhimu mkubwa uliokuwa umejificha katika ukweli kuwa Yesu alibatizwa na Yohana. Kwa sasa wanaiamini injili hii na wanashindwa wamshukuru Mungu kwa kiasi gani. 
Tunaweza kuona kwamba kama vile ilivyo kwa injili ya maji na Roho, lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania pia liliundwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Rangi hizi nne ni sawa na injili ya maji na Roho. Na kwa namna ile ile, injili inayong’aa ya maji na Roho pia inadhihirishwa katika kisitiri cha mlango wa Mahali Patakatifu na katika mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu. Zaidi ya yote, paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania pia lilifumwa kwa rangi hizo nne; bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ukweli huu unamaanisha juu ya ubatizo na damu ya Yesu. Hii ndiyo sababu Yesu alijitangaza yeye mwenyewe kuwa yeye ni njia ya kwenda katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa kuja hapa duniani na kwa kuwaokoa wenye dhambi kwa ukweli wa injili ya maji na Roho, Yesu amewafanya wale wanaoamini kuwa wasio na dhambi.
Njia ya kuelekea katika Ufalme wa Mbinguni inapatikana katika imani inayoamini juu ya ubatizo na damu ya Yesu. Kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, Yesu ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi. Je, unafikiria ni wapi unapoweza kuupata ukweli huu? Ikiwa unaamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake ya Msalaba, basi wewe utaokoka toka katika dhambi zote na kisha kupokea uzima wa milele mara moja na kwa ajili ya wote. 
Je, kuna tofauti gani basi kati ya imani inayoamini katika Yesu Kristo kwa kiwango fulani na imani inayoamini kikamilifu katika injili ya maji na Roho? Kwa sababu ni kwa injili ya maji na Roho ambayo kwa hiyo Bwana amewaokoa wenye dhambi toka katika makosa yao, basi kuamini katika injili hii ni kumwamini Bwana kiusahihi. Kwa sababu Bwana amewaokoa wenye dhambi kwa ubatizo wake na damu yake ya Msalaba, kumwamini huyu Bwana kuwa ni Mwokozi ni sawa na kuokolewa toka katika dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ambayo aliitimiliza. Kuliamini jina lake kwa sehemu tu hakumaanishi kuwa dhambi zetu zitaondolewa na kisha sisi kuingia Mbinguni. 
Bali, ni kwa kuamini kikamilifu kwamba Yesu Kristo alibatizwa na Yohana kwa ajili yetu, akaimwaga damu yake Msalabani, akabeba adhabu ya dhambi zote, na kisha akafufuka toka kwa wafu ili kwamba tuweze kupokea ondoleo letu la dhambi na kufanyika watu wa Mungu mwenyewe. Mungu anawaruhusu wale tu ambao wana imani inayoamini katika injili takatifu sana ya maji na Roho kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Lakini wale ambao hawaamini katika injili ya maji na Roho hawawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu, kwa kuwa hawajazaliwa tena upya. 
Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania, tumeweza kuipokea imani takatifu sana hali tukiwa tunaishi hapa duniani. Pamoja na kuwa matendo yetu yana mapungufu, tunapokuwa na imani ya jinsi hiyo ni nani basi anayeweza kusema kuwa hatujafanywa kuwa wenye haki? Tunapokuwa tumefanyika watakatifu kwa kuiamini injili ya maji na Roho, inawezakenaje basi tukawa bado tuna dhambi? Baadhi ya watu wanashangaa jinsi tunavyoweza kusema kuwa hatuna dhambi wakati bado tupo katika mwili unaoendelea kutenda dhambi. 
Lakini haya ni mawazo yao binafsi kuhusiana na mwili. Wale wanaofahamu na kuamini katika injili ya maji na Roho wanakubali kuwa wanadamu wana miili yenye mapungufu na kwa hiyo hawawezi kujisaidia lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi hadi watakapokufa. Hata hivyo, pia wanaamini kuwa dhambi zao zote zimeondolewa milele zikiwemo dhambi ambazo watazitenda hapo baadaye, kwa kupitia wokovu mkamilifu wa ubatizo wa Yesu na Msalaba wake. 
Ule ukweli kwamba wewe na mimi tunaweza kushirikishana Neno la imani ya kiroho na kuwa na ile imani takatifu sana tunapoishi hapa duniani ni kwa sababu ya ukweli kuwa Bwana ametupatia wokovu wetu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa sababu Bwana ametupatia imani inayotuwezesha sisi kuamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho kama karama yake kwetu. Kwa imani yetu katika Bwana, tunaweza kuwa na ushirikiano miongoni mwetu na kisha kuyaishi maisha yetu wakati tukiendelea kumtumikia Bwana na kupendana sisi kwa sisi—hapa ndipo furaha yetu ya kweli inapokaa. 
Hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumshukuru Mungu kwa injili yake. Ni jambo la kufurahisha kiasi gani kwamba nimefikia hatua ya kuifahamu injili ya maji na Roho na kisha kuiamini! Nilipokuwa sina punje ya ufahamu juu ya ubatizo wa Yesu kwa kupitia Neno la kweli, Mungu ameupatia moyo wangu imani ambayo inaamini katika injili hii ya maji na Roho. Sisi sote tumepokea baraka za Mbinguni kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. 
 

Kwa Sababu ya Injili ya Kweli katika Moyo Wangu, Ninaihubiri Injili kwa Shukrani
 
Hali tukiisoma Biblia, swali linaanza kujitokeza katika mawazo yangu: kwa nini Yesu alibatizwa? Kwa sababu swali hili liliendelea kujitokeza, niliwaza kutafuta jibu lake kwa kupitia Biblia, lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kunifundisha mimi juu ya swali hilo. Na hii ndiyo sababu nilianza kuvutiwa sana katika mada hii hadi pale nilipoweza kuifahamu injili ya maji na Roho. 
Mara nyingi ninasoma kifungu cha maandiko toka Mathayo 3:13-17, hasa pale ambapo Yesu alimwambia Yohana kabla ya kubatizwa, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote,” lakini sikuweza kuifahamu maana yake. Kwa hiyo mara nyingi niliwauliza wengine kuhusu sababu ni kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani, lakini kamwe sikuweza kusikia jibu kamili la kuridhisha. Hata hivyo, Mungu aliniwezesha mimi kutambua dhumuni la ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana. Haya yalikuwa ni mapinduzi ya kiroho kwangu mimi, kana kwamba ni kipofu aliyepata kuona tena. Kwa hiyo, ilikuwa ni baada ya kuipata maana ya Mathayo 3:13-17 ndipo nilipokuja kuutambua ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambazo zimeniokoa mimi toka katika dhambi zangu. 
Kabla ya kuupata ukweli, nilikuwa nikiamini katika damu tu ya Msalaba kama wokovu wangu lakini ukweli ulikuwa ni kwamba bado nilikuwa na dhambi na kwa hiyo nilikuwa ni mtenda dhambi. Kwa wakati huo, niliamini kuwa dhambi zangu za asili zinaweza kuondolewa tu kwa damu ya Yesu, lakini dhambi zangu halisi bado zilibakia katika moyo wangu. Nilikuwa sijaifahamu imani inayomfanya mtu kuwa mkamilifu asiye na dhambi—yaani, nilikuwa sielewi chochote kuhusu ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana. Hata hivyo, Mungu aliuangazia moyo wangu kwa mwanga unaong’aa wa ondoleo la dhambi kama vile mwanga unavyowashwa katika chumba chenye giza. “Aah, ubatizo ambao Yesu aliupokea toka kwa Yohana unahusianishwa kwa karibu na kile kitendo cha kuwekea mikono juu ya sadaka ya kuteketezwa katika Agano la Kale! Kwa hiyo hivi ndivyo injili ya maji na Roho ilivyo!” 
Lakini nini kilifuata? Hali nikiwa nimeshangazwa na ule ugunduzi wangu, shida kubwa ilianza kujitokeza katika moyo wangu baada ya kuutambua ukweli huu: ikiwa hakuna injili nyingine zaidi ya injili hii ya maji na Roho ambayo ndiyo injili ya kweli, je, nini kitatokea kwa ulimwengu huu? Nilifikiria kuwa imani ya waevanjelikali ilikuwa sahihi kwa mujibu wa Biblia. Lakini sasa, nimefikia hatua ya kutambua kuwa injili zote zaidi ya injili ya maji na Roho ni injili zisizo za kweli zinazotoka kwa Shetani. 
Kwa hiyo, kitu ambacho nimekifanya tangu wakati huo ni kuamini na kuhubiri kuwa hakuna injili nyingine ya kweli zaidi ya injili ya maji na Roho. Baadhi ya watu wamenishutumu mimi kwa ajili ya injili hii. Mungu amenionyesha mimi pia juu ya mtu mwenye mapungufu mengi, ukweli wa wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na pia ameniwezesha kuamini na kuhubiri kwamba ukweli huu ndiyo injili halisi. Kuna injili nyingi zinazofanana katika ulimwengu huu, lakini kuna injili moja tu ya kweli. Hii ndiyo sababu nimeamua kuieneza injili ya maji na Roho ulimwenguni mwote. 
Ninapofikiria jinsi ambavyo nilifikia kuanza kuuhubiri ukweli wa ondoleo la dhambi, na jinsi nilivyofikia hatua ya kuufahamu na kisha kuamini na kisha kuihubiri injili ambayo ni takatifu sana ya maji na Roho, ndipo ninatambua jinsi ambavyo Mungu amenibariki sana. Kitu ambacho nilikifanya ilikuwa ni kuamini kwamba Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana na kwa kuimwaga damu yake Msalabani, na kwamba dhambi zangu zote zimetoweka! Injili ya maji na Roho ni ukweli halisi na ninamshukuru Bwana kwa kunipatia injili hii. Mimi ni mtu ambaye kwa kweli nimebarikiwa sana na Mungu. Ninyi nyote mnaoamini katika injili ya maji na Roho pia ni watu mliobarikiwa na Mungu. 
Ninaamini kuwa mambo haya yote ni baraka ambazo Mungu ameziweka juu yangu. Kama Mtume Paulo alivyokiri, “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure,” (1 Wakorintho 15:10) Siwezi kufanya lolote zaidi ya kuisifu neema yake iliyo juu yangu. Hebu niseme wazi, kama isingekuwa ni ndani ya Kanisa la Mungu, ungepata wapi kuisikia injili ya kweli iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu? Kila mtu anayesikia na kuamini katika Neno la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa moyo wake utasafishwa. Je, wale ambao hawaiamini injili ya maji na Roho wanafikiria chochote kuhusu injili hii? Kwao, ukweli wa maji na Roho ni kitu kinachochosha tu. 
Je, unayo imani inayoamini katika nyuzi za bluu na nyekundu za pazia la mlango wa Patakatifu pa Patakatifu? Unapolisikia Neno hili usifikiri kuwa tayari unalifahamu, bali jichunguze wewe mwenyewe kuona ikiwa ukweli huu unapatikana katika moyo wako. Kwa maneno mengine, ni lazima uwe miongoni mwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho kwa mujibu wa Neno la Maandiko Matakatifu. Itakuwa ni bahati na baraka ikiwa utakuja katika Kanisa la Mungu, ukalisikia Neno la Mungu, kisha ukawa na nafasi ya kuingia Mbinguni. 
Lakini ikiwa hivi sivyo, ikiwa hauwezi kuifahamu injili ya maji na Roho, na hauwezi kuwa na imani ya kweli, na ikiwa hauwezi kuingia katika Ufalme wa Mbinguni, ati kwa sababu tu unasikiliza hadithi za kila siku zilizoundwa na wanadamu, je, ni faida gani ambayo utaipata kutokana na hilo? Ikiwa injili unayoiamini ni tofauti na injili ya maji na Roho, basi inawezekanaje nafsi yako kuwa na maana yoyote mbele za Mungu? Neno la Mungu na imani yako ni lazima viwe sawasawa kama ambavyo imani ya Mtume Paulo na imani yetu vilivyo sawa. Injili ya maji na Roho ambayo Petro aliiamini pia ni sawa na injili ambayo sisi tunaiamini (1 Petro 3:21).
Ninamshukuru sana Mungu kwa kuturuhusu sisi kuamini katika injili ya kweli ya maji na Roho katika nyakati hizi za mwisho. Na unapoushikilia ukweli wa injili ya maji na Roho katika vitabu vyetu na kisha ukawashirikisha na wengine, wao pia, watafikia hatua ya kupokea ondoleo la dhambi na kisha wakamshukuru Mungu katika furaha yao. Ni lazima tutambue kwamba miundo yote na vyombo vya Hema Takatifu la Kukutania vinatoa taswira ya wazi na ya kina ya Bwana wa wokovu ambaye amezitoweshea mbali dhambi zetu zote, na ni lazima tumshukuru Mungu kwa ukweli huu. 
Tunabarikiwa sana kuokolewa na kuingia Mbinguni pale tunapouamini ukweli uliofunuliwa katika pazia la mlango wa Patakatifu pa Patakatifu. Zaidi ya yote, Mungu ametuwezesha sisi kuueneza ukweli wa ondoleo la dhambi uliofanywa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa kwa ulimwengu mzima. Mungu ametukabidhi sisi kazi hii. Toka katika maeneo maalum ya kimajukumu, sisi tu waaminifu kwa kazi zote ambazo kila mmoja wetu amepewa kuzifanya, na Mungu anatubariki sisi kwa ajili ya uaminifu huu. 
Ninatoa shukrani zangu kwa Mungu. Ninamtukuza Mungu kwa imani yangu hali nikiamini kuwa injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika ua wa lango la Hema Takatifu la Kukutania ni sawa na rangi nne zilizofunuliwa katika mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu. Sasa, ni matumaini yangu kuwa ninyi nyote mtakuwa ni watu waliookolewa toka katika dhambi zote kwa imani, ambao mnaweza kupangia Patakatifu pa Patakatifu mahali ambapo Mungu anaishi milele. Je, imani yako inasimama imara katika ukweli huu pia?