Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-14] Pazia Ambalo Lilipasuliwa (Mathayo 27:50-53)

Pazia Ambalo Lilipasuliwa
(Mathayo 27:50-53)
“Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatatemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.”
 

Patakatifu pa Patakatifu palikuwa ni mahali ambapo Mungu aliishi. Na ni Kuhani Mkuu tu ndiye aliyeruhusiwa kuingia hapo mara moja kwa mwaka, katika ile Siku ya Upatanisho hali akiwa amebeba damu ya mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi la waisraeli. Kuhani Mkuu alifanya hivyo kwa sababu Patakatifu pa Patakatifu katika Hema Takatifu la Kukutania palikuwa ni mahali patakatifu sana ambao hakuweza kuingia mpaka awe na damu ya mwanasadaka, ambaye kwa huyo mikono iliwekwa juu ya kichwa chake ili kuyatoweshea mbali maovu ya wenye dhambi. Kwa msemo tofauti, hata Kuhani Mkuu hakuweza kuikwepa adhabu ya Mungu hadi baada ya kuwa amepokea ondoleo la dhambi zake kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kabla ya kuingia katika uwepo wa Mungu. 
Je, ni lini pazia la Hekalu lilipasuka? Lilipasuka wakati Yesu alipoimwaga damu yake na kufa Msalabani. Kwa nini ilimpasa Yesu kuimwaga damu yake Msalabani na kisha kufa? Kwa sababu Yesu Mwana wa Mungu kwa kuja kwake hapa duniani katika mwili wa mwanadamu alikuwa ameyachukua katika mwili wake maovu yote ya wenye dhambi kwa kubatizwa na Yohana katika Mto Yordani. Kwa sababu Yesu alikuwa amezichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake, basi Yesu aliweza kuzimaliza adhabu zote za dhambi ikiwa tu angeliimwaga damu yake na kisha kufa Msalabani. Hii ndio sababu lile pazia lililokuwa likitenganisha kati ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu lilipasuliwa toka juu hadi chini. Hii inamaanisha kuwa ule ukuta wa dhambi ambao ulimtenganisha Mungu na mwanadamu ulikuwa umeanguka chini mara moja na daima. 
Kwa maneno mengine, kwa kupitia ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani, Yesu amezifanya dhambi zote kutoweka. Kwa ubatizo na damu ya Yesu Kristo, Mungu Baba amezitoweshea mbali dhambi zetu zote mara moja na kwa wote na ameufungua mlango wa Mbinguni, ili kwamba mtu yeyote aweza kuingia Mbinguni kwa kuamini katika ubatizo huu na damu ya Yesu iliyomwagika. 
Wakati Yesu alipokuwa Msalabani, giza lilipafunika pale alipokuwepo kwa masaa matatu. Baada ya kuwa amezibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani, Yesu alisulubiwa na karibu na kifo chake alilia, “Eloi, Eloi, lama sabaktani?”, maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46). Kisha akasema neno lake la mwisho, “Imekwisha!”, kisha akafa. Na baada ya siku tatu akafufuka tena toka kwa wafu, akabeba ushuhuda kwa siku 40, na kisha akapaa Mbinguni mbele ya macho ya wanafunzi wake na wafuasi wake wengi.
 

Je, Ni Kweli Kuwa Baba Alikuwa Amemwacha Yesu?
 
Maumivu ambayo Yesu aliyapata yalikuwa ni makubwa sana kiasi kuwa alifikiri kuwa Baba yake amemwacha. Mateso ya adhabu ya dhambi yalikuwa ni makubwa sana kiasi hicho. Kwa sababu Yesu alikuwa amezichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, Yesu alikuwa ameachwa kwa muda na Baba pale alipokuwa ameibeba adhabu ya dhambi Msalabani. Mungu Baba alipaswa kumuadhibu mtu yeyote ambaye alikuwa na dhambi, na kwa sababu dhambi zote za ulimwengu zilikuwa zimepitishwa kwa Yesu, basi Yesu alipaswa kuraruliwa na kisha kuimwaga damu yake Msalabani kama adhabu ya dhambi hizi. 
Kwa sababu Yesu ambaye ni Mungu mwenyewe katika uwepo wake alikuwa amezichukua dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa, basi dhambi za ulimwengu zilikuwa zimehamishiwa katika mwili wake mtakatifu. Kwa hiyo, baada ya kuwa Yesu amezichukua dhambi za ulimwengu, basi alipaswa kuachwa na Mungu Baba kwa kitambo tu, kuteseka hadi kifo Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zetu zote na hivyo kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi zote. Hii ndiyo sababu Yesu alipaswa kunyenyekezwa hadi katika mateso ya adhabu ya dhambi na hii ndiyo sababu iliyomfanya Mungu kumgeuzia mwanae uso wake kidogo. 
Lakini hii haimaanishi kuwa Yesu alikuwa ameachwa na Baba daima. Bali ina maanisha kuwa alipaswa kubeba adhabu ya haki ya dhambi zetu, na kwa hiyo ilimpasa kuachwa na Baba kwa kitambo tu. Wakati Yesu alipopaza sauti akiwa katika maumivu, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” ni kwa sababu Yesu alikuwa ameteseka sana kutokana na dhambi kiasi kuwa ndio maana sisi tumeokolewa toka katika adhabu ya dhambi. Sisi tulikuwa ni watu ambao tulikuwa tumeachwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, akapata mateso ya adhabu ya dhambi Msalabani, na zaidi ya yote, aliachwa hata na Baba kwa kitambo kwa ajili yetu. 
Kama ambavyo unafahamu, baada ya kujengwa kwa Hekalu katika utawala wa Mfalme Sulemani, basi nafasi ya Hema Takatifu la Kukutania ilichukuliwa na Hekalu. Lakini msingi ya utaratibu wa Hema Takatifu la Kukutania iliendelea kutumika katika Hekalu kama ambavyo ilikuwa ikitumika katika Hema Takatifu la Kukutania kabla Hekalu halijajengwa. Kwa hiyo, kulikuwa na pazia ambalo lilitenganisha kati ya Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu katika Hekalu. Na wakati ule ule wakati Bwana wetu alipopiga kelele Msalabani, “Eloi, Eloi, Eloi, lama sabaktani?” pazia hili la Hekalu lilipasuka toka juu hadi chini. Ukweli unaozungumziwa na tukio hili ni kuwa kwa sababu Bwana amezioshelea mbali dhambi zetu kwa ubatizo ambao aliupokea na kwa damu ya thamani ambayo aliimwaga Msalabani, basi sasa lango la Mbinguni sasa limefunguliwa ili kwamba wote wanaoamini waweze kuingia. Sasa, kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, sisi sote tunaweza kuingia Mbinguni kwa imani. 
Kwa kupitia ufunuo wa utaratibu wa Hema Takatifu la Kukutania, watu wa Agano la Kale pia walimwamini Yesu atakayekuja kuwa ni Masihi, na kwa hiyo nao pia waliondolewa dhambi zao zote na kufanyika watoto wa Mungu. Katika Agano Jipya, ile haki yote ya Mungu ya ondoleo la dhambi ilitimizwa mara moja na kwa wote wakati Bwana wetu alipobatizwa katika Mto Yordani na kisha kufa Msalabani. Sababu inayotufanya sisi kuwa na mioyo yenye shukrani baada ya kuwa tumesikia na kuamini katika injili ya ondoleo la dhambi ambayo Bwana wetu ametupatia, ni kwa sababu tunayo injili ya maji na Roho. 
Sisi wenyewe tusingeweza kuwekwa huru toka katika dhambi, lakini kwa sababu ya ukweli wa wokovu ambao Mungu ametupatia sisi kwa kupitia maji na Roho, basi tumeweza kuondolewa dhambi zetu kwa kuamini katika ukweli huu. Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ambayo Yesu ametupatia, dhambi zetu zimetoweshwa na sasa tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa imani. Tukiwa tumepewa hili, tunawezaje basi kutomshukuru Mungu? Tunaweza kumshukuru sana, kwa sababu tunafahamu sasa kuwa lango la Mbinguni lilivunjwa toka juu hadi chini wakati ule Bwana wetu alipokufa. Hizi ni habari za kufurahisha zinazotuambia sisi kuwa Bwana wetu alizichukua dhambi zote za wanadamu kwa kupitia ubatizo alioupokea katika Mto Yordani, alibeba adhabu ya dhambi kwa damu yake Msalabani, na kwa hiyo amewakomboa wote wanaoamini toka katika dhambi. 
Ule ukweli kuwa pazia la Hekalu lilipasuka toka juu hadi chini wakati Yesu alipokufa Msalabani unatufundisha sisi ukweli kwamba katika kipindi hiki, wale wote ambao wamesafishwa toka katika dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na damu wanaweza kuingia Mbinguni. Huu ni ushahidi wa ukweli wa wokovu ambao Bwana wetu ameuruhusu kwetu. Kwa sababu tulikuwa ni wenye dhambi, kulikuwa na ukuta wa dhambi ambao ulikuwa umetutenganisha uliokuwa ukituzuia sisi kuja mbele za Mungu, lakini kwa ubatizo na damu yake, Yesu ameufanya huu ukuta wa dhambi kupotea mara moja na kwa wote. Kule kusema kuwa Mungu alilipasua pazia la hekalu toka juu hadi chini kunamaanisha kuwa yeyote anayeamini katika ubatizo ambao kwa huo mwana wa Mungu aliyachukua katika mwili wake maovu yote ya wenye dhambi na katika damu ya Msalaba anaweza kusafishwa dhambi zake kikamilifu na kisha kuingia Mbinguni. Mungu ametuokoa sisi toka katika dhambi kwa namna hii. 
Yesu alilipasua pazia la Hekalu toka juu hadi chini kuwa ushuhuda wa kazi hizi za wokovu ambazo alizitimiza. Kwa hiyo Waebrania 10:19-22 inasema, “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake; na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.” 
Wakati Yesu alipokufa Msalabani, mlango wa kuingilia Patakatifu pa Patakatifu ulifunguliwa kwa kuwa pazia lake lilipasuliwa, na huu mlango uliofunguliwa wa Patakatifu pa Patakatifu ni Neno la Mungu la injili ambalo limefungua njia mpya na iliyo hai ya kwenda Mbinguni. Hapa, Biblia inatueleza sisi kuwa dhambi zote za mioyo yetu na miili yetu zilitoweshewa mbali kwa kupitia ubatizo wake (maji safi) na damu yake, na kwa hiyo tunaweza kusafishwa kwa uhakika wa imani katika wokovu wake mkamilifu. 
Katika jambo hili, ninampatia Mungu shukrani zangu zote. Kwa kweli tusingeweza kuingia Mbinguni hata kama tungejaribu kiasi gani, lakini kwa watu kama sisi, Yesu ametuokoa toka katika dhambi zetu zote kwa matendo yake ya haki ya ubatizo na kuimwaga damu yake Msalabani, na pia amelipasua lango la Mbinguni na kuliacha wazi ili kwamba wote wanaoamini katika injili ya maji na Roho waweze kuingia Mbinguni. Sasa imewezekana kwetu sisi kusafishwa toka katika dhambi zetu na kuingia Mbinguni kwa imani inayoamini katika injili ya maji na Roho. 
Kwa sababu Mungu alimefungua lango la Mbinguni kwa ajili yetu kwa kubatizwa na kusulubiwa, sasa tunaweza kuzioshelea mbali dhambi zetu na kuingia Mbinguni kwa kuamini katika ukweli huu. Tunaweza basi kutomshukuru Mungu? Kwa kweli hatuwezi kumshukuru vya kutosha kwa upendo wake wa kusulubiwa. Mlango wa pazia wa Patakatifu pa Patakatifu ulipasuliwa katikati na ubatizo ambao Yesu aliupokea ili kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake na sadaka ya kuteketezwa ya mwili wa Yesu ambayo aliitoa ili ihukumiwe kwa haki kwa ajili ya dhambi zetu hizi.
 


Kuna Njia Moja Tu ya Kuingia Mbinguni

 
Kwa sababu tunaamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani, basi sisi tutaingia Mbinguni. Hakuna njia nyingine ya kuingia Mbinguni bali kwa kuamini katika injili ya ukweli. Ni kwa kuamini tu katika yale ambayo Yesu amefanya kwa ajili yetu ndipo tunapoweza kuingia Mbinguni, kwa kuwa Mungu amefanya kazi hizo kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na damu ya Yesu. 
Hii ndio sababu Wakristo hawawezi kuingia Mbinguni kwa kupitia jitihada zao wenyewe, kujitoa, au majaribio mengine ya kinafiki. Mungu amedhamiria kuwa ni wale tu ambao wamesafishwa dhambi zao kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu alioupokea na katika damu yake aliyoimwaga ndio wanaoweza kuingia Mbinguni. Wale wanaoamini katika ukweli huu ndio wale wanaoamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu mwenyewe, na Mwokozi wa milele ambaye amewaokoa toka katika dhambi kwa kupitia ubatizo wake na damu yake aliyoimwaga. Mungu ameruhusu kusafishwa dhambi kwa watu kama hao. Ni kwa kupitia ubatizo tu ambao Yesu aliupokea na mateso ambayo aliyavumilia pale Msalabani, Mungu Baba amewawezesha wale wanaoamini katika haya kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa imani. 
Je, tunahitaji fedha ili kuingia Mbinguni? Ikiwa ingekuwa hivyo, basi tungekuwa tunaupata wokovu wetu kwa kuulipia na hivyo huu ungekuwa si wokovu ambao unatolewa bure na Bwana. Ili tuweze kuingia Mbinguni, hatuhitaji kingine chochote mbali na imani ambayo inaamini katika injili ya maji na Roho. Kwa maneno mengine, ili kuingia Mbinguni, hakuna malipo, matendo, au jitihada zetu zinazohitajika. Hakuna kitu ambacho kina asili ya mwanadamu kitabia ambacho ni cha muhimu ili kuingia Mbinguni. Ili sisi tuweze kustahilishwa kuingia Mbinguni, Mungu hahitaji jitihada yoyote, tendo, nia, fidia, au wema toka kwetu. 
Kuna kitu kimoja tu ambacho ni muhimu sana kwetu ili tuweze kuingia Mbinguni, na hii ni imani inayoamini katika ubatizo wa kuoshelea dhambi ambao Yesu aliupokea katika Mto Yordani na sadaka ambayo aliitoa kwa kuimwaga damu yake Msalabani kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu. Hakuna njia nyingine. Kitu pekee tunachokihitaji ni imani inayoamini katika injili ya ubatizo na damu ya Yesu. Hii ndio sababu ili sisi tuweze kupokea ondoleo la dhambi na kuingia Mbinguni, ni lazima basi tuamini katika injili ya maji na Roho ambayo Yesu ameitimiza. 
Yesu, Bwana wa upendo, ametimiliza wokovu wetu mkamilifu kwa kupitia injili ya maji na Roho. Kwa sababu Yesu amekwisha utimiza wokovu wa ondoleo la dhambi, basi ikiwa wenye dhambi wataiamini injili hii ya kweli kwa mioyo yao yote, basi wanaweza kuokolewa toka katika dhambi zao zote. Bwana ameziondolea mbali dhambi zetu zote bila kujalisha ikiwa tuna dhambi nyingi au chache, na amemuwezesha kila mtu kuingia Mbinguni kwa imani tu. 
Kule kusema kuwa Yesu amelifungua lango la Mbinguni ili kwamba wenye dhambi waweze kuingia kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ni neema ya wokovu ambayo ni maalum. “Bwana alibatizwa ili kuzibeba dhambi zangu zote na akafa Msalabani kwa niaba yangu! Amezioshelea mbali dhambi zangu na amefungua mlango wa Mbinguni kwa ajili yangu! Bwana alinipenda sana kiasi kuwa alibatizwa, akaimwaga damu yake, na amelitimiza ondoleo langu la dhambi kwa jinsi hii!” Kwa njia hii, unapoamini katika ukweli wa wokovu utaingia Mbinguni kwa imani hii. 
Kwa watu kuamini katika Yesu kuwa ni Mwokozi wao si kitu kigumu, bali kwa hakika ni kitu rahisi, kwa kuwa kile wanachotakiwa kukifanya ni kupokea katika mioyo yao ule ukweli ambao umekwisha kamilishwa ambao Yesu aliufikia wakati alipokuja hapa duniani na kisha waamini katika ukweli huo. Kwa sababu Yesu amezitoweshea mbali dhambi zote na ametukomboa toka katika dhambi hizo kwa kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani ambao aliupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, na kwa kupitia damu ambayo aliimwaga Msalabani na kwa kupitia Roho, basi tukimwamini huyu Yesu katika mioyo yetu tutaokolewa. 
“Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Kwamba dhambi zetu ni kubwa au ni chache, kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake, Yesu amezifanya dhambi hizo zote kutoweka. Ni kwa kuamini katika injili hii ya maji na Roho, ambao ni ukweli unaotuweka sisi huru toka katika dhambi, ndipo tunapoweza kupokea wokovu wetu wa milele na kukutana na uhuru wa wokovu huu wa kweli.
Kwa kuitimiza injili ya maji na Roho, Bwana wetu amelifungua lango la Mbinguni na kuliacha wazi. Bwana wetu alikuja hapa duniani, alibatizwa, alikufa Msalabani, na kisha akafufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu, ukweli huu ambao ni injili ya maji na Roho umetupeleka sisi kuwa karibu na Mungu, na umetufanya sisi kuifanya Mbingu kuwa ni makao yetu ya hapo baadaye. Sasa, ikiwa unapenda kuingia Mbinguni na kuwekwa huru toka katika dhambi na kufanyika mwana wa Mungu, basi ni lazima upokee ondoleo la dhambi zako kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Ni imani hii ambayo itakuwezesha wewe kupokea ondoleo la dhambi na kisha kukuongoza katika lango la Mbinguni. 
Bwana wetu anafahamu kila kitu kuhusu sisi. Anafahamu siku tuliyozaliwa, na anafahamu kuhusu dhambi zetu zote ambazo tumezifanya na ambazo tutakuja kuzifanya. Na pia anafahamu vizuri kuwa hata kama tukijitahidi kiasi gani hatuwezi kuzifanya dhambi zetu kutoweka kwa jitihada zetu wenyewe. Kwa sababu Bwana anatufahamu sisi vizuri, yeye mwenyewe amezitoweshea mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani. 
 


Kwa Nini Yesu Alikuja Hapa Duniani?

 
Jina Yesu linamaanisha kuwa ni Mwokozi. Yesu alizaliwa hapa duniani kwa sababu wokovu wetu toka katika dhambi hauwezi kukamilika kutokana na mwanadamu yeyote bali unaweza kukamilishwa na nguvu za Mungu. Hivyo, kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa na dhumuni halisi na la wazi. Hii ndio sababu ili kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi, Yesu alizaliwa hapa duniani kwa kupitia mwili wa bikira. Kwa maneno mengine, Yesu alizaliwa kwa kupitia mwili wa mwanamke kwa ajili ya wenye dhambi ambao waliirithi dhambi kwa sababu ya makosa ya Adamu na Hawa. Bwana alikuja hapa duniani, akafanyika mwili katika mwili wa bikira kwa nguvu za Mungu ili aweza kufanyika Mwokozi ambaye anawaokoa wenye dhambi wote wa ulimwengu huu toka katika maovu yao yote. 
Bwana wetu alizaliwa katika dunia hii kwa kupitia mwili wa uumbaji wake mwenyewe ili kwamba yeye mwenyewe aweze kufanyika sadaka isiyo na mawaa. Na wakati ulipowadia, hatua kwa hatua, aliendelea na mpango wake ili kutuletea wokovu. Wakati Bwana wetu alipofikisha umri wa miaka 30, alibatizwa katika Mto Yordani. Ili kulifikia dhumuni la kuzaliwa kwake hapa duniani, Yesu alipaswa kuzipokea dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa, na hivyo ili kulikamilisha jukumu hili Yesu alibatizwa na Yohana (Mathayo 3:13-17). 
Baada ya miaka mitatu kupita tangu Yesu alipokuwa amezipokea dhambi za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake, Yesu alisulubiwa. Ni kwa sababu Bwana wetu alibatizwa na kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake ndio maana alihukumiwa adhabu kwa haki kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa kupitia ubatizo ambao ulitolewa na Yohana Mbatizaji na damu yake Msalabani, Bwana amezifanya dhambi zote kutoweka, na kwa hiyo amewawezesha wale wanaoamini kuokolewa toka katika dhambi zao. 
Haijalishi kuwa watu wapo katika ujinga kiasi gani, au wapo katika udhaifu ambao umewakamata, au ni wenye dhambi wa aina gani, Mungu ametuwezesha sisi waamini katika injili ya maji na roho kuingia Mbinguni, ambao ni Ufalme wa Bwana. Yesu alibatizwa katika Mto Yordani na kisha kuimwaga damu yake Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi. Kwa sababu ya wokovu ambao Yesu ameukamilisha kwa kulipa mshahara wa dhambi zetu na kujitoa mwenyewe kusulubiwa, basi sisi ambao tunaamini tunaweza kuoshelewa mbali dhambi zetu kwa imani yetu tu katika injili ya maji na Roho. Huu ni ukweli wa msingi wa Ukristo na kiini cha ondoleo la dhambi. 
Bwana alikuja hapa ulimwenguni ili kufanyika Mwokozi wa wenye dhambi zote katika ulimwengu huu. Na kwa kweli Bwana ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu. Bwana wetu amewawezesha wenye dhambi wote, bila kujalisha ni akina nani, kuingia Mbinguni kwa kuamini katika kazi zake. 
Huu ni upendo wa Bwana. Ni kwa sababu Bwana wetu alitupenda sana ndio maana alibatizwa na kisha kuimwaga damu yake ili kutuokoa. Ili kutukomboa sisi toka katika dhambi, watu ambao alitupenda sana kama mwili wake mwenyewe, Bwana wetu aliutimiza wokovu kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake. Sisi tulikuwa ni wenye dhambi ambao tungeendelea kutenda dhambi hadi tutakapokufa. Hali tukiwa tunasumbuliwa kwa dhambi zetu, tuliendelea kutengana na Mungu zaidi na zaidi. Ili kutuokoa watu kama sisi, Bwana alipaswa kuzitimiza kazi za wokovu ambazo zinatuwezesha sisi kuunganishwa na yeye. 
Bwana wetu ametuokoa sisi ambao tulikuwa ni wenye dhambi kwa upendo wa Mungu. Ili kutuokoa sisi wenye dhambi toka katika maovu yetu, Yesu ameitimiza haki na upendo wa Mungu kwa kuupokea ubatizo wake na kuimwaga damu yake. Sisi ambao tunaamini katika injili hii tunamshukuru sana Bwana kwa kile ambacho amekifanya kwa ajili yetu kiasi kuwa hatuna maneno yanayotosha kuelezea shukrani zetu hizo za kiimani pale tunaposujudu mbele zake. Ukweli wa ondoleo la dhambi ambao Bwana wetu ametupatia ni upendo mkuu na mkamilifu sana ambao hakuna maneno ya hoja au maneno matamu yanayoweza kuuelezea. 
Kwa miaka 2,000 iliyopita, hakuna hata mmoja wetu aliyekuwa amezaliwa kwa wakati huo. Ilikuwa ni takribani miaka 2,000 iliyopita wakati pazia la Hekalu la hapa duniani na Hekalu la mbinguni la Ufalme wa Mungu yalifunguliwa. Hatukuwemo hata katika matumbo ya mama zetu kwa wakati huo, lakini Bwana wetu alikwisha kufahamu kuhusu haya yote kuhusu sisi. Alifahamu kuwa mtazaliwa, na kwamba ninyi nyote mtaishi maisha yenu kila mtu kwa namna yake ya pekee. Na Bwana amenipenda mimi—sio mimi tu, bali amekupenda wewe na kila mtu sawasawa. Bwana ametupenda sana kiasi kuwa amewawezesha wenye dhambi wote kuingia Mbinguni kwa kuamini katika injili ya maji, damu, na Roho ambayo Yesu ameitimiza kwa ajili yetu. Kwa kupitia maji na Roho (ubatizo na damu yake ya Msalaba), Yesu ameukamilisha wokovu wetu toka katika dhambi. 
Kule kusema kuwa pazia la Hekalu lilipasuka toka juu hadi chini kwa kweli ni tukio la kweli linaloshangaza sana. Inawezekanaje hili pazia la Patakatifu pa Patakatifu likapasuliwa ati kwa sababu tu Yesu amekufa Msalabani? Pazia hili lilikuwa ni sawa na mazulia ya siku hizi. Lilifumwa na kuwa zito na lenye nguvu. Huko Palestina, hata sasa unaweza kukutana na mapazia mazito kiasi hicho ambayo yamefumwa kama mazulia. Mazulia hayo yanafumwa kwa nguvu sana kiasi kuwa inasemekana kuwa inachukua farasi wanne kulivuta zulia moja katika uelekeo tofauti ili kuweza kulichana. Farasi ana nguvu kiasi gani? Lakini bado lilikuwa ni pazia ambalo linahitaji farasi wanne ili kuweza kulichana vipande ambalo lilipasuka katikati toka juu hadi chini wakati Yesu alipokufa Msalabani. 
Kwa nini pazia lilipasuliwa? Lilipasuliwa kwa sababu Yesu alikuwa ameziosha dhambi zote ambazo zilikuwemo katika mioyo ya wanadamu. Lilipasuliwa kwa sababu Yesu alikuwa amezitimiza kazi zake zote za haki kwa kubatizwa na kusulubiwa hadi kifo. Kwa kuzipokea dhambi za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake na kisha kuadhibiwa Msalabani, Yesu aliifungua njia kwa wale wanaoamini ili kuingia Mbinguni. Unachotakiwa kukifanya sasa ni kuamini tu. Bwana amelifungua lango la Mbinguni ili kwamba ninyi nyote muweze kuingia kwa kuamini. 
 


Je, Damu ya Yesu na Ubatizo Vyote ni Muhimu kwa Wokovu Wetu?

 
Ni kwa mujibu wa mbinu ya wokovu iliyokuwa imepangwa hata kabla ya wakati wa Agano la Kale kwamba mikono iliwekwa juu ya kichwa cha Yesu, yaani sadaka ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa tu. Kwa kuwa ni sheria ya Mungu ambayo iliwekwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kuzipokea dhambi zote kwa kuwekewa mikono na kisha kuuawa, Yesu, akiwa amekuja kama sadaka yetu ya kuteketezwa ili kutuokoa milele angeliweza kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote kwa kuupokea ubatizo wake, ambao ni mfano wa kule kuwekewa mikono. Hii ndiyo sababu ili kupaingia Patakatifu pa Patakatifu, hata Kuhani Mkuu alipaswa kuhakikisha kuwa anaibeba damu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja naye, sadaka ambayo ilikuwa imezichukua dhambi kwa kule kuwekewa mikono. 
Kwa nini basi ilimpasa Kuhani Mkuu kupaingia mahali hapa patakatifu akiwa na damu? Kwa kuwa maisha ya mwili yapo katika damu, Mungu alikuwa amempatia Kuhani Mkuu kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake kabla ya kuja mbele ya uwepo wake (Mambo ya Walawi 17:11). Watu wote walipaswa kufa kwa sababu ya dhambi zao, lakini kwa sababu Yesu alizibeba dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa katika Mto Yordani (dhambi zote zilipitishwa kwa Yesu kwa ubatizo wake) na akazibeba zote, basi Yesu alisulubiwa na kwa hiyo amewaokoa wote kwa uhai wake mwenyewe. Hii inatueleza sisi kuwa wakati wenye dhambi wanakuja mbele za Mungu basi ni lazima kwa hakika waje na imani inayoamini katika maji na damu. Ni pale tu tutakapoamini kwa mioyo yetu yote katika maji ya ubatizo wa Yesu na damu aliyoimwaga basi ndipo tunapoweza kukwepa kuhukumiwa kwa dhambi zetu. 
Sasa, Yesu amezioshelea mbali dhambi zote ili kwamba asiwepo mtu anayepaswa kutoa maombi ya toba au kufunga, au au kutoa matoleo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake. Hatupaswi kutoa maombi ya toba wala kuadhibiwa kwa sababu ya dhambi zetu kwa kuwa Yesu alikwishaitoa sadaka ya ondoleo la dhambi na adhabu yake. Tunachopaswa kukifanya ni kuamini kwa mioyo yetu yote katika wokovu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Kitu ambacho kila mtu anapaswa kukifanya ni kuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea kuwa ni nyuzi za bluu ambazo zilitumika katika Hema Takatifu la Kukutani la Agano la Kale, na kisha kuamini katika damu ambayo Yesu aliimwaga Msalabani sawasawa na nyuzi nyekundu. Na ukweli kuwa Yesu ni Mfalme katika uwepo wake wa msingi unadhihirishwa katika nyuzi za zambarau zilizotumika katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. Kwa hiyo, ikiwa tumeoshwa dhambi zetu kwa kuamini katika ondoleo la dhambi lililodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kisha kuamini kuwa adhabu yetu yote imekwisha isha, basi kila mmoja wetu anaweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Injili hii ndiyo injili halisi ya maji na Roho. 
 


Kwa Nini Pazia la Hekalu Lilipasuka Wakati Yesu Alipokufa Msalabani? Hebu Tutafakari Juu ya Hili Mara Moja Zaidi

MsalabaNyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizodhihirishwa katika Agano la Kale ni injili ambayo inaleta baraka za kupokea ondoleo la dhambi na kisha kuingia Uzima wa Mbinguni kwa wale wanaoamini. Hii ndio sababu pazia lilipasuliwa baada ya kuwa Yesu amebatizwa na kufa Msalabani. Kwa wale wanaomwamini Yesu, huu ni ukweli wa injili ya maji na Roho uliotolewa na Mungu mwenyewe. “Aah, ni kwa sababu Yesu alibatizwa na Yohana kwa niaba yangu ndio maana aliimwaga damu yake na kufa Msalabani, na hivyo akawa amelipa malipo ya kifo ambao ni mshahara wa dhambi.” Alipokuwa akifa Msalabani Yesu alisema, “Imekwisha,” na ilikuwa ni kwa wakati huu ndipo alipoifungua njia ya sisi kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. 
Yesu alikuja hapa duniani ili kuwaokoa wale ambao walikuwa wametenganishwa na Mungu kutokana na ukuta wa dhambi ambao wasingeweza kuukwepa zaidi ya kuendelea kuujenga. Haya yalikuwa ni mapenzi ya Yesu mwenyewe, lakini kwa wakati huo huo ilikuwa pia ni amri ya Mungu Baba na upendo wake kwetu. Hali akitii mapenzi ya Baba, Yesu aliupokea ubatizo ambao ulizipitisha kwake dhambi za ulimwengu katika mwili wake mwenyewe. Ni kwa sababu Yesu alikuwa amezibeba dhambi za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake, ndio maana basi alikwenda Msalabani, akasulubiwa, akamwaga damu yake na kufa, akafufuka toka kwa wafu baada ya siku tatu, na kwa hiyo akazitimiza kazi zake za wokovu. Hizi ni huduma ambazo zinadhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, ambazo ni ondoleo la dhambi ambalo linawakomboa wenye dhambi toka katika maovu yao na ukamilifu wa sadaka ya kuteketezwa. 
Kwa kuwa Yesu ameutimiza wokovu kwa huduma zake, basi lile lango la Mbinguni, ambalo hakuna mwanadamu ambaye angeliweza kuingia, limefunguliwa na kuachwa wazi. Hii inaonyesha kuwa mlango wa wokovu haufunguliwi tena kwa kuwekea mikono na damu ya mnyama iliyotumika katika utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa katika Agano la Kale, bali sasa unafunguliwa kwa imani inayoamini katika ubatizo wa Yesu alioupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani. Kule kusema kuwa pazia lilipasuliwa kunadhihirisha utimilifu wa wokovu, kwamba Mungu amemuwezesha mtu yeyote anayeamini na kufahamu katika injili ya maji na Roho ambayo imetimizwa kwa Bwana kuingia Mbinguni. Hii ndio sababu pazia la Hekalu lilipasuliwa. 
Ni lazima uuingie Ufalme wa Mbinguni kwa imani inayoamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Yesu ambaye hana dhambi kabisa alikuja hapa duniani akafanyika mwili na alibatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi zetu zote (Mathayo 3:15). Zaidi ya yote, Bwana wetu aliyatoa maisha ya mwili wake kuwa ni mshahara wa dhambi zetu na amefanyika kuwa ni sadaka ya upatanisho ya milele ambayo tunapaswa kuichukua tunapokwenda mbele za Mungu. Kwa hiyo, sisi sote ni lazima tuamini katika damu ambayo Yesu aliimwaga baada ya kubatizwa kuwa ni wokovu wetu. Ili kuwakomboa wanadamu toka katika dhambi na kuwafanya kuwa watu wa Mungu, Yesu alilifungua lango la Mbinguni kwa kuuchana mwili wake mwenyewe. 
Inapofikia kwa Yesu kutuokoa sisi ni lazima tufahamu kuwa hakuimwaga tu damu yake Msalabani. Miaka mitatu kabla ya kufa Msalabani, Yesu alikuwa amekwisha kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa katika Mto Yordani. Kwa hiyo Yesu alibatizwa na Yohana kwa ajili ya wanadamu wote na kisha alisubuliwa na askari wa kirumi. Hata kabla wewe na mimi hatujazaliwa hapa ulimwenguni, Yesu alikwisha kuzisafishilia mbali dhambi zetu zote kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake. 
Kule kusema kuwa Yesu alibatizwa na Yohana ilikuwa ni mbinu ya wokovu ambayo alipaswa kuitimiza kwa uhakika ili kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake mara moja na kwa wote. Na damu ambayo aliimwaga ilikuwa ni malipo ya mshahara wa dhambi hizi zote. Kwa sababu Yesu ni Mungu mwenyewe, ubatizo ambao aliupokea na damu ambayo aliimwaga Msalabani basi kwa hakika vinaweza kuunda wokovu wetu toka katika dhambi. Hii ilikuwa ni sadaka kamilifu ya Bwana wetu aliyoifanya kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote. Je, unaamini kuwa Neno la injili ya maji na Roho limekusafisha dhambi zako na limetukomboa toka katika dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi?
 


Kwa Kupitia Ubatizo wa Yesu na Damu ya Msalaba, Dhambi Zote za Mwanadamu Sasa Zimeoshelewa Mbali

 
Yesu alibatizwa na Yohana ili kuziosha dhambi za mwanadamu. Ikiwa tunaziangalia huduma za Yesu za wokovu kwa kuuacha ubatizo huu wa Yesu katika maisha yake hapa duniani, basi wokovu wa mwanadamu uliokuwa umepangwa katika Yesu Kristo kabla ya misingi ya ulimwengu utageuka na kuwa uongo. Hata kabla ya misingi ya ulimwengu, Yesu alikuwa tayari akijiandaa kubatizwa ili kuzichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake na kisha kuimwaga damu yake. 
Hii ndiyo sababu Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni mwakilishi wa wanadamu, na kwa hiyo akawa amezipokea dhambi zote (Mathayo 11:11-12; Mathayo 3:15). Mbinu ya wokovu ambayo Yesu aliitumia ilikuwa ni kuyaoshelea mbali maovu ya wenye dhambi kwa kubatizwa. Yesu aliyapokea maovu ya wenye dhambi na kuyasafishilia mbali, na badala ya sisi kufa kwa sababu ya dhambi zetu, Yesu alikufa kwa haki kwa niaba yetu, na kwa kufanya hivyo amewaokoa wale wanaoamini katika hili toka katika dhambi zao zote na adhabu ya dhambi. Kwa kupitia mbinu hii (mbinu ya kubatizwa), Yesu aliweza kuzipokea dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake na akabeba adhabu yote ya dhambi kwa kuimwaga damu yake Msalabani. “Kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Kule kusema kuwa Yesu alibatizwa katika Mto Yordani kulimaanisha kuwa Yesu alizipokea dhambi zote za sisi wenye dhambi. 
Kaka zangu na dada zangu, je, huwezi kuamini kuwa Yesu alikuja hapa duniani zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, na kwamba alibatizwa alipokuwa na miaka 30, na kwamba aliimwaga damu yake kwa ajili yako, ati kwa sababu tu hukuyaona haya kwa macho yako mwenyewe? Lakini hali akiyajua mapungufu yetu yote, Mungu alikwishaupanga wokovu wetu kwa maji na damu hata kabla ya misingi ya ulimwengu, na kwa kumtuma Yesu Kristo na Yohana Mbatizaji katika dunia hii kwa mujibu wa mpango wake, Mungu ameutimiza wokovu wetu sote. Ili kutuwezesha sisi kuutambua na kuufahamu ukweli huu wote, Mungu aliwafanya watumishi wake kuliandika Neno lake. Kwa kupitia Neno lake lililoandikwa, Mungu amefunua kila kitu kuhusu mpango wa wokovu na utimilifu wake kwa wanadamu wote. Mungu amemuwezesha kila mtu kutambua kwa kupitia Neno la Mungu lililoandikwa kwamba Yesu alibatizwa na Yohana katika Mto Yordani ili kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake. 
Sisi sote ni lazima tuamini katika ubatizo wa Yesu alioupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani kuwa ni wokovu wetu. Pamoja na kuwa hatujayaona hayo kwa macho yetu ya kimwili, ni lazima tuamini hivyo katika mioyo yetu. Imani ya kweli inakuja kwetu wakati imani yetu inapokuwa imejengwa katika Neno lake. Bwana alimwambia Tomaso, “Wa heri wale wasioona wakasadiki” (Yohana 20:29). Yesu amekuokoa wewe na mimi kwa ubatizo wake ambao aliupokea na damu yake ambayo aliimwaga. Mungu amemwezesha mtu yeyote anayeamini katika ukweli huu kuingia Mbinguni. 
Hii ndiyo sababu Mungu alilipasua pazia la Hekalu wakati Yesu alipokufa Msalabani. Yesu aliuangusha ukuta wa dhambi ambao ulikuwa umemtenganisha mwanadamu na Mungu. Kitu ambacho Yesu amekifanya kilitosha kabisa kuuvunjilia mbali ukuta wote wa dhambi. Yesu amefanya iwezekane kwa kila mtu kuingia Mbinguni kikamilifu pasipo kikwazo kwa kuamini katika injili ya maji na Roho katika moyo. Ninamshukuru sana Bwana wetu kwa kutupatia ukweli huu ili kwamba sisi sote tuweze kuingia Mbinguni ikiwa tu tutaamini katika mioyo yetu. 
Tendo hili ni kubwa kiasi gani, kwamba Yesu alizaliwa hapa duniani katika mwili wa kiumbe wa kawaida ili kuwaokoa wenye dhambi? Kwa kweli ni tukio la kweli na la kukumbukwa hata pale linapolinganishwa na uumbaji wa ulimwengu. Kwa kweli ni jambo la kawaida Bwana, ambaye ni Muumbaji aliyeumba vitu vyote, anaweza kuviumba viumbe vyake, lakini kusema kuwa Muumbaji alifanyika kuwa kama kiumbe, akazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, na akasulubiwa, basi tendo hili haliwezi kuwa kitu kingine chochote zaidi ya tukio kuu la wokovu. 
Inawezekanaje basi kwa muumbaji mwenyewe kufanyika kama moja ya viumbe wake? Lakini Yesu, Mungu mwenyewe, alijishusha mwenyewe hata akabatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu katika Mto Yordani. Hili ni tendo la kushangaza sana. Lakini huu sio mwisho wake, kwa kuwa Yesu alijishusha chini sana hata akawa mtii hata mauti, akavumilia mateso ya ukatili juu ya Msalaba, akamwaga damu yake na kufa. Mambo haya yote hayawezi kuwa kitu kingine chochote zaidi ya upendo wa Mungu, rehema zake na neema yake. 
Dhambi zote za mwanadamu zilisafishwa kikamilifu mara moja na kwa ajili ya wote kwa ubatizo wa Bwana na damu yake Msalabani. Na baada ya kuwa amelipasua pazia la Hekalu, Yesu alifufuka toka kwa wafu baada ya siku tatu, na sasa anataka kukutana katika kweli na wale wote ambao wanaamini katika ukweli huu. Vivyo hivyo, kazi za Bwana ambazo zimewaokoa wenye dhambi ni matendo ambayo ni makuu kuliko hata kazi za uumbaji ambazo ziliuumba ulimwengu wote na vitu vyote vilivyomo ndani yake. Kuzaliwa kwa Yesu, ubatizo wake, kifo chake Msalabani, ufufuko wake, kupaa kwake na kurudi, na kwamba ametufanya sisi kuwa wana wake mwenyewe, hizo zote ni kazi za upendo wa Mungu. 
Bwana wetu alituokoa wewe na mimi toka katika dhambi zetu. Bwana wetu ametukomboa wewe na mimi mara moja na kwa wote toka katika dhambi za ulimwengu kwa kupitia injili ya maji na Roho. Kwa hiyo tunaweza kufanyika wenye haki kwa imani na kumshukuru Mungu. Mungu ametupatia sisi baraka zake za wokovu katika ukamilifu wake. Je, unaamini? 
Kaka na dada zangu, wewe na mimi tulikuwa ni watu ambao tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kutupwa kuzimu. Tulikuwa ni watu ambao tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kuangamizwa kutokana na dhambi zetu na kuishi maisha yetu katika huzuni, lakini Bwana ametuokoa sisi toka katika dhambi kwa wokovu ambao aliupanga hata kabla ya misingi ya ulimwengu. Hatukuwa na chaguo lolote zaidi ya kuishi maisha yetu tukiwa tumekaa katikati ya dhambi zetu, tukilia, na kujuta, na kuilaani hatima yetu, lakini ili kutuwezesha watu kama sisi kuingia katika Ufalme wa Mbinguni, Bwana ametukomboa sisi toka katika dhambi zetu zote. Kwa hiyo Bwana wetu amefanyika kuwa ni Bwana wa wokovu wetu. 
Yesu ametupatia sisi injili ya maji na Roho, na pia ametuhakikishia ondoleo la dhambi zetu. Yesu mwenyewe amefanyika kuwa ni Bwana wa wokovu. Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi za ulimwengu kwa niaba yetu, alikufa kwa ajili yetu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu mkamilifu. 
 

Je, Unaamini Katika Ubatizo Ambao Yesu Aliupokea na Damu Aliyoimwaga?
 
Ukombozi wetu toka katika dhambi unakamilika kwa kuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea na katika damu ya Msalaba. Ili wenye dhambi waweze kuokolewa kwa kuamini katika Yesu, basi ni lazima wahakikishe kuwa wanautafakari ubatizo wake na Msalabala kwa mfuatano, na ni lazima waamini kuwa ni kwa muungano wa mambo haya mawili ndipo wokovu mkamilifu unapotimizwa. 
Kwa namna yoyote, je, hauamini kuwa Yesu alibatizwa na kufa Msalabani? Je, huudharau ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana na kukataa kuuamini? Haki ya Mungu ilitimizwa kwa sababu ubatizo ambao Yesu aliupokea ulikuwa ni mchakato ambao kwa huo Yesu aliyachukua maovu yote ya wenye dhambi katika mwili wake, na kifo ambacho alikipata kwa kuimwaga damu yake ya thamani ili kuwa ni adhabu ya dhambi zetu. Kwa hiyo, wakati wewe na mimi tunapokiri kuwa tunaamini katika Yesu, basi ni lazima tuuamini ubatizo wake na damu yake Msalabani kuwa ni wokovu mmoja. 
Mungu aliandika juu ya umuhimu wa ubatizo na damu ya Yesu iliyomwagika katika Neno lake, lakini pamoja na hayo bado kuna watu wengi ambao wanasisitiza kuwa wanahitaji kuamini katika damu ya Msalaba tu ili kuweza kuokolewa. Ikiwa wewe ni miongoni mwa hao, naomba ugeuke, na uamini katika mambo haya yote mawili. Ikiwa hautafanya hivyo na ukaendelea kuamini katika damu ya Msalaba tu, basi utaishia kuzifanya huduma takatifu za Bwana katika maisha yako na kisha kuishia katika utupu. Ikiwa utatokea kuipata imani ya jinsi hiyo, basi inakupasa kugeuka toka katika imani hii potofu na kisha uwe na imani sahihi ambayo imezungumzwa katika Biblia nzima. Pasipo ubatizo wa Yesu, je, kifo chake Msalabani kitakuwa na umuhimu gani kwetu sisi? Ikiwa Yesu angelikuwa hakubatizwa na Yohana Mbatizaji, basi kifo chake kingekuwa hakina lolote la kufanya kuhusiana na dhambi zetu. 
Kaka zangu na dada zangu, ikiwa ungelipaswa kulifuta jina lako toka katika orodha ya deni, je, usingepaswa kuleta fedha na kumlipa mdai? Wadeni ni lazima walipe fedha kulingana na kiwango wanachodaiwa, na hapo ndipo wanapoweza kuyafuta majina yao toka katika orodha. Vivyo hivyo, ili kulipa mshahara wa dhambi zetu, Yesu alizipokea dhambi hizo na maovu yetu kwa kupitia ubatizo wake na akazitoweshea mbali kwa kuimwaga damu yake. 
Kwa kupitia ubatizo ambao Yesu aliupokea, kwa kweli Bwana alizichukulia mbali dhambi zetu zote, na hii ndiyo sababu aliweza kuadhibiwa kwa sababu ya dhambi zetu zote kwa kuimwaga damu yake. Ili kulilipa deni, uelewa wa kawaida unasema kuwa mtu anatakiwa kuleta thamani inayolingana na deni hili. Ikiwa wadeni hawaleti fedha lakini wanadai kuwa wameshalipa deni lao na wanadai majina yao kufutwa toka katika bili, je, ni kweli kuwa majina yao yatafutwa? Haijalishi kuwa wanaamini kiasi gani kuwa majina yao yamefutwa, ukweli wa mambo utabaki kuwa majina yao bado yameandikwa katika orodha ya wadeni.
Kama ambavyo wadeni wanaweza kuwekwa huru toka katika madeni yao pale madeni yao yanapokuwa yamelipwa yote, basi ili sisi wenye dhambi tuweze kupokea ondoleo la dhambi, basi ni lazima tuwe na imani katika mioyo yetu inayoamini kuwa dhambi zetu zilipitishwa kwa Yesu kwa kupitia ubatizo alioupokea. Sisi wenyewe hatukuutoa ubatizo huu ambao ulizipitisha dhambi zetu katika kichwa cha Yesu. 
Lakini kwa kupitia mwakilishi aliyeitwa Yohana Mbatizaji, tuliweza kuzipitisha dhambi zetu kwa Yesu. Yesu ambaye alibatizwa na Yohana Mbatizaji alizibeba dhambi za ulimwengu, akauendea Msalaba, akaimwaga damu yake na kufa. Kwa kuamini katika ubatizo wake, mfano unaotupatia wokovu, ambao kwa huo Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake na akatuokoa, basi ndipo tunapoweza kupokea uthibitisho wa wokovu wetu. Kwa kuamini katika kile ambacho Bwana wetu amekifanya katika mioyo yetu, sasa tunaweza kupokea ondoleo la dhambi. Kwa nini? Kwa sababu kwa kupitia ubatizo wake na damu, Bwana wetu ametupatia sisi maisha mapya. 
Wakati Yesu alipokufa Msalabani, pazia la Patakatifu pa Patakatifu lilipasuliwa katika vipande viwili, ardhi ilitikisika, miamba ilivingirika, makaburi yalifunguka, na miili mingi ya watakatifu ambao walikuwa wamelala ilifufuliwa. Kwa kupitia matukio haya, Mungu alionyesha kuwa atawawafua wale wanaoamini katika Neno lake, kwamba Yesu Kristo atakuja na kuzitoweshea mbali dhambi zote za mwanadamu. Mungu alionyesha kuwa kwa hakika Yesu alifufuka toka kwa wafu, na kwamba wale wanaoamini katika Yesu pia wataletwa katika uzima. Yesu hajatuokoa sisi toka katika dhambi tu, bali ametupatia pia maisha mapya kwetu sisi ambao tulikuwa tumekufa kiroho. Yesu alibatizwa, akafa Msalabani, na akafufuka tena ili kutupatia sisi maisha mapya. Mungu ametuwezesha sisi kuuingia mji mtakatifu na kuishi ndani yake milele. Ninatoa shukrani zangu nyingi kwa Mungu kwa imani yangu. 
Mahali ambapo wale waliopokea ondoleo la dhambi wataishi ni Mbinguni. Kwa hiyo amini kuwa wale wote waliopokea ondoleo la dhambi katika dunia hii wataingia Mbinguni na kuishi humo. Mbingu ni ya wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi. Kuamini katika injili ya maji na Roho na kuzaliwa tena upya si vitu viwili tofauti, bali vyote ni vimoja. 
Ikiwa mtu yeyote anaamini katika Neno la injili ya maji na Roho, basi mtu huyu amezaliwa tena upya wakati ule ule anapoamini hivyo. Wakati wenye dhambi wanapokea ondoleo la dhambi, wanafanyika kuwa watoto wa Mungu mwenyewe, na Mungu anatoa karama ya Mbingu kwa watoto wake. Ingawa katika mwili wetu hatuna kazi ambayo ni yetu binafsi, bali tukikiangali kitu kimoja, ambacho ni imani yetu inayoamini katika Mwokozi, basi Bwana wetu ametupatia sisi ondoleo la dhambi na Mbingu kama zawadi yake kwetu sisi. 
Ule ukweli kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani, alibatizwa, na ameimwaga damu yake, mambo hayo yote ni ya kweli. Wakati Yesu alipokufa Msalabani, alikuwa amekwisha kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake. Kabla ya Yesu kusulubiwa, baada ya kuwa amebatizwa na Yohana, Yesu alikuwa anazibeba dhambi za ulimwengu. Kwa hiyo kwa kuwa Yesu alikuwa amezibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa ndio maana alibeba adhabu ya sheria iliyotangaza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Ili Yesu aweze kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi, Yesu alipaswa kufa Msalabani hali akiwa amezibeba dhambi za ulimwengu ambazo alikuwa amezichukua kwa kupitia ubatizo wake. 
Wakati Yesu aliposulubiwa, watu waliompigilia misumari hawakuwa Wayahudi, bali walikuwa ni askari wa kirumi. Yesu alisulubiwa na askari wa mataifa. Hali akiimwaga damu yake yote kwa ajili ya dhambi zetu, Yesu alipiga kelele akisema, “Imekwisha!” kisha akakata roho. Wakati ule ule Yesu alipokuwa anakufa, pazia la Hekalu lililpasuka katika vipande viwili toka juu hadi chini. Zaidi ya yote, Biblia inatueleza sisi kuwa nchi ilitetemeka, miamba ikapasuka, na makaburi yakafunguka; na kwamba miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala ilifufuliwa pia (Mathayo 27:51-52). Wakati yule akida na askari wa kirumi walipoona yaliyotokea wakati Yesu alipokufa Msalabani, walishuhudia wakisema, “Hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu!” (Mathayo 27:54). Mungu aliifanya midomo ya hawa askari wa mataifa kushuhudia, “Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu aliye hai.”
Sasa, wale ambao ni lazima washuhudie injili ya kweli katika ulimwengu mzima si wengine bali ni sisi, ambao ni waamini wa injili ya maji na Roho. Ni kwa kupitia injili ya maji na Roho ndipo kila mtu anapobadilishwa. Wakati watu wanapokea ondoleo la dhambi toka kwa Yesu, wanabadilishwa kiroho bila hata ya wao kujaribu, kwa kuwa Roho Mtakatifu anakuja kukaa katika mioyo yao. Mioyo ya wenye haki waliozaliwa tena upya wanafanywa upya kila siku, kwa kuwa katika Kanisa la Mungu wanaweza kulisikia Neno la Injili ya maji na Roho. Hawa waliozaliwa upya wanakuja kulisikia Neno, kumsifu Yesu, na kadri wanavyosifu, ndipo wanapopata uzoefu wa sifa hizo katika mioyo yao, na kwa hiyo wanaitia nguvu mioyo yao kila siku. Wenye haki wanaifanya mioyo yao iendelee kubadilishwa kila siku, na wanaweza kuyaona mabadiliko hayo wao wenyewe. 
Hali wakiona mabadiliko ya nafsi zetu, sisi ambao tumefanyika kuwa wenye haki, basi wasioamini ndipo wanakuja kushuhudia, “Kweli wameokolewa. Wao ni Wakristo wa kweli, watu wa Mungu.” Vivyo hivyo, ondoleo letu la dhambi si aina ya wokovu ambayo inaweza kuthibitishwa na sisi wenyewe tu. Yule akida mrumi na askari waliushuhudia ukweli huu, kuwa Yesu kama Mwana wa Mungu amewaokoa wenye dhambi toka katika dhambi za ulimwengu pale aliposulubiwa. Vivyo hivyo, Mungu mwenyewe anashuhudia kwa wale wanaoamini katika ukweli kuwa Yesu ametuokoa sisi toka katika dhambi zote kwa maji na damu. 
 


Injili ya Maji na Roho Iliyomfanya Hata Ibilisi Kusalimu Amri

 
Injili ya maji na Roho ni wokovu ambao hata Ibilisi amesalimu amri. Wakati Yesu aliposema, “Imekwisha” wakati wa kifo chake, pengine Ibilisi alisema, “Ahaa! Hii ni aibu, lakini hakuna ninachoweza kufanya kuhusu hili! Yesu yupo sahihi. Hakuna dhambi katika ulimwengu huu tena. Kila mmoja sasa amefanywa kuwa hana dhambi kabisa pasipo ila yoyote! Jambo hili linautafuna moyo wangu, lakini siwezi kufanya lolote kuhusu hili!” 
Kwa maneno mengine, Ibilisi mwenyewe hakuweza kufanya lolote zaidi yeye pia kuukiri huu wokovu ambao Yesu ameutimiza. Lakini bado anajaribu kuwazuia waliopokea ondoleo la dhambi ili wasiishi maisha yao ya imani. Kwa kuwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotimizwa na Yesu ni watoto wa Mungu, wanajaribu kuishi kwa ajili yake. Lakini kwa upande wa Ibilisi, na hii inamaanisha kuwa kuna baadhi ya wafuasi wake wachache ambao wamefanywa kuwa watumwa wa dhambi, anajaribu kuwazuia watumishi wa Mungu ili wasiueneza ukweli huu ulimwenguni kote. 
Ikiwa wale waliopokea ondoleo la dhambi wanaendelea kueneza injili ya maji na Roho, basi kutakuwa na watu wengi zaidi ambao wameondolewa dhambi zao. Hii ndiyo sababu Shetani anazamisha meno yake katika udhaifu wa watu ili kuwafanya wasiweze kusonga mbele, hali akiwazuia ili walau kuwepo na mtu hata mmoja ambaye atapotoshwa na kurudishwa nyuma katika kumfuata Yesu. 
Anaidanganya mioyo ya watu kwa kusema, “Muue Yesu!”, Ibilisi aliwafanya wao ili wamsulubishe Yesu hadi mauti. Lakini wakati Ibilisi alipofikiri kuwa kila kitu kimekwisha kwa tukio hili, basi Yesu hali akiwa amesulubiwa na alipokuwa akifa alipaza sauti yake na kusema, “Imekwisha!” Shetani alishtushwa na jambo hili. Mbali na kukatishwa tamaa, kwa kuzichukua dhambi zote katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani na kwa kufa Msalabani, Yesu kwa haki ameutimiza wokovu unaomkomboa mwanadamu toka katika dhambi na adhabu ya dhambi. Ibilisi alikuwa haitambui hekima hii ya Mungu. Yeye alidhani kuwa kila kitu kitakwisha baada ya kumuua Yesu Msalabani, lakini hali haikuwa hivyo. Baada ya kuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake, Yesu alilitimiza ondoleo la dhambi la wenye dhambi kwa kuutoa mwili wake Msalabani na kufa. 
Kwa kifo cha mwili wake, Yesu amekwishalipa mshahara wote wa dhambi. Kwa hiyo, dhambi haiwezi kupatikana tena kwa watu. Kwa nini? Kwa sababu kwa mujibu wa sheria iliyosema kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, Yesu amekwisha kufa badala ya wenye dhambi. Ni lazima tuamini kuwa kwa sababu Yesu aliuchukua uovu wa wenye dhambi wote katika mwili wake katika Mto Yordani, basi ndio maana aliweza kufa kwa haki badala ya wenye dhambi. 
“Imekwisha!” Hivi ndivyo Yesu alivyopaza sauti Msalabani katika pumzi yake ya mwisho. Kwa sababu Yesu alikufa, basi Ibilisi hawezi kamwe kutuambia sisi kuwa, “Una dhambi, si ndivyo?” Kwa sababu ya kuzaliwa kwa Yesu, ubatizo wake, kifo chake Msalabani, na damu na ufufuo wake, Ibilisi alishindwa kwa kishindo mbele za Yesu. Pamoja na kuwa Ibilisi alikuwa ameutenganisha uhusiano wetu na Mungu kwa kutufanya sisi kutenda dhambi kila wakati, mwishoni, kwa sababu ya hekima ya Yesu Mwana wa Mungu, yaani kule kuziosha dhambi na adhabu ya dhambi, Ibilisi hakuweza kukwepa zaidi ya kushindwa kabisa. 
Unapoamini katika ubatizo wa Yesu na damu ya Msalaba, je bado unakuwa na dhambi? Kwa kweli sio! Kusema kwamba hatuna dhambi si kitu kinachoweza kutamkwa tu kwa dhamiri ya mwili. Lakini kwa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu, basi tunaweza sasa kutangaza kwa ujasiri kuwa hatuna dhambi. Je, unauamini ukweli kuwa alizichukua dhambi zako katika mwili wake kwa kubatizwa katika Mto Yordani, kufa Msalabani kwa niaba yetu, na kwamba ametuokoa? Basi kwa imani yetu katika ukweli huu, tunaweza sasa kusema kuwa hatuna dahmbi. Na kwa kweli, hakuwezi kuwa na dhambi kabisa katika mioyo yetu, hata ile dhambi ndogo kama senti. Hii ndio sababu mioyo yenye shukrani inaruka ndani yetu mbele za Mungu, hali tukitoa shukrani zetu kwa imani. 
“Mungu, imani yangu inaweza isiwe kubwa, lakini hata kwa imani ambayo ni ndogo kama punje ya haradali, bado ninakupa shukrani zangu. Nilikuwa ni mtu ambaye sikuweza kuubeba upendo wako mkuu, lakini bado ulikuja ndani ya moyo wangu, na kwa hiyo kwa imani yangu inayoaamini katika injili ya maji na Roho, sasa ninaushikilia upendo wako katika moyo wangu. Moyo wangu unakushukuru wewe kila siku, kwa kuwa wewe ni Bwana unayekaa katika moyo wangu na upo pamoja nami. Ninakushukuru sana wewe kwa kunipatia mimi moyo huu.” Vivyo hivyo, Bwana wetu ametupatia sisi mioyo yenye shukrani. Na Bwana wetu anatubariki sisi kila siku. 
Kwa hiyo sio mimi tu, bali pia kila mtu anayesikia na kuamini katika ukweli wa wokovu wake mkamilifu, sisi kwa hakika hatuna dhambi kabisa katika mioyo yetu. Kwa sababu tunaamini katika ukweli wa maji na Roho, sisi tumepokea baraka ya wokovu, ya kufanyika wana wa Mungu mwenyewe. Na Mungu, kwa moyo wote, anawataka wote kutambua kuwa hakuna njia nyingine ya wao kuokolewa toka katika dhambi zao zote pasipo kuamini katika kuzaliwa kwa Yesu na ubatizo wake na damu yake, na kisha kumrudia yeye na kuamini katika ukweli huu.
Matendo 4:12 inasema, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Tunamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi. Kwa wale wanaoamini katika ukweli huu, mioyo yenye shukrani inaruka. Kwa hiyo sisi tuna mioyo ambayo ina shukrani kwa Mungu. Bwana wetu ametupatia wokovu, na pia ametupatia mioyo yenye shukrani. Bwana ametupatia sisi uzima wa milele. Hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumtukuza Bwana kwa shukrani zetu kwa kutupatia maisha haya yenye baraka nyingi. 
Hata kama imani yetu ni ndogo kama punje ya haradari, ikiwa tutaendelea kuamini katika kile ambacho Yesu amekifanya kwa ajili yetu katika mioyo yetu, sisi sote tunaweza kuokolewa. Ninawasihi ninyi nyote kutambua kuwa hakuna mahali pengine popote tunapoweza kuupata wokovu wetu zaidi ya kuamini, kuufahamu wokovu huu ambao Mungu ametupatia bure, na kisha kuamini katika wokovu huo. Kwa sababu ondoleo la dhambi haliwezi kupatikana kwa jitihada zetu wenyewe ndio maana Mungu bila masharti alizitoweshea mbali dhambi zetu zote na ametoa wokovu wake kwetu sisi tunaoamini. Sasa, kilichobakia kwetu sisi kukifanya ni kuamini ondoleo hili la dhambi kwa imani. 
Kuna msemo hapa Korea unaosema, “Ikiwa unapendelea vitafunwa vya bure, utapata upara.” Katika msemo wa kiingereza, ni sawa na kusema kuwa, “Hakuna kitu kama chakula cha bure.” Na hiyo ni kweli; hakuna kitu katika maisha kinachotujia bure. Na ni lazima tuwashangae wale wanaotaka kupokea zawadi pasipo kuwa na kitu cha kurudisha au kulipa. Hata hivyo, kuokolewa na kwenda Mbinguni kunapatikana kwa kuamini katika injili ya maji na Roho bure. Upara kwa sababu ya kupokea vitafunwa vya bure kunaweza kusionekane katika mwili, lakini upara wa kiroho kwa sababu ya kupokea karama za Mungu ni baraka mbele za Mungu. Ninaomba sana ili ninyi nyote muweze kutambua kuwa Mungu anafurahishwa kuiona mioyo yetu isiyo na dhambi, na kwamba anapoona hivi anatukumbatia sisi katika mikono yake. 
Tunaitamani neema ya Mungu ya bure. Na hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumshukuru Bwana: Bwana wetu alikuja hapa duniani, aliupokea ubatizo wake kwa maji, aliimwaga damu yake Msalabani, na kwa hiyo amelifungua lango la Mbinguni. Kwa kulipasua pazia la Patakatifu pa Patakatifu toka juu hadi chini, Yesu amemwezesha mtu yeyote anayezaliwa tena upya kwa kuamini katika injili ya maji na Roho kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Wewe pia, ni lazima uingie Mbinguni kwa kuamini katika injili hii ya maji na Roho katika moyo wako. 
Ninamshukuru Bwana wetu kubatizwa, kwa kuimwaga damu yake, kwa kufufuka toka kwa wafu, na kwa neema ambayo imeufungua mlango wa ondoleo la dhambi kwa ajili yetu.