Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-15] Vitako Viwili vya Fedha na Ndimi Mbili kwa Kila Ubao wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-37)

Vitako Viwili vya Fedha na Ndimi Mbili kwa Kila Ubao wa Hema Takatifu la Kukutania
( Kutoka 26:15-37 )
“Nawe fanya hizo mbao za maskani za mti wa mshita, zenye kusimama. Kila ubao utakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu. Kila ubao utakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganywa huu na huu; ndiyvyo utakavyozifanya mbao zote za maskani. Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini. Nawe ufanye vitako arobaini vya fedha chini ya zile mbao ishirini, vitako viwili chini ya ubao mmoja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya ubao mwingine kupokea zile ndimi zake mbili; na upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini; na vitako vyake vya fedha arobaini; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao mwingine. Kisha ufanye mbao sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi. Tena ufanye mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma. Upande wa chini zitakuwa ni mbili mbili; vivyo zitaungwa pamoja mbao pacha hata ncha ya juu katika pete ya kwanza; zote mbili ndiyo zitakavyokuwa; zitakuwa kwa ajili ya hizo pembe mbili. Mbao zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha, vitako kumi na sita; vitako viwili chini ya ubao mmoja na vitako viwili chini ya ubao wa pili. Nawe fanya mataruma ya mti wa mshita; mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajii ya mbao za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi. Na hilo taruma la katikati, lililo katikati ya zile mbao litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu. Na hizo mbao utazifunika dhahabu, na pete zake za kutilia yale mataruma utazifanya za dhahabu; na hayo mataruma utayafunika dhahabu. Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake ulioonyeshwa mlimani. Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi za bluu, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri yenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana. Nawe utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini. Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya bluu, na rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza. Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu, kulabu zake zitakuwa za dhahabu; nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.”
 
 
Mbao
Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa mbao 48; kulikuwa na mbao 20 kwa kila upande wa kusini na kaskazini, mbao sita ziliwekwa upande wa magharibi, na mbao mbili ziliwekwa katika kona mbili za nyuma. Kila ubao ulikuwa na kipimo cha mita 4.5 (futi 15) kwa urefu na takribani sentimita 67.5 (futi 2.2) kwa upana. Ili kila ubao uweze kusimama vizuri ukiwa umenyooka kulikuwa na vitako viwili vya fedha na ndimi mbili ambavyo vilifungamana pamoja vizuri. Hii inatuonyesha tena kuwa wokovu wa Mungu unapatikana kwa neema yake tu kwa imani katika Kristo.
 


Wokovu kwa Neema kwa Kupitia Imani katika Kristo

 
Wakristo wengi wanafahamu na hata wamekariri kifungu mashuhuri cha Waefeso 2:8-9, “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” Lakini kwa bahati mbaya, wengi hawafamu jinsi ambavyo neema yake ilivyo na aina ipi ya imani ambayo wanapaswa kuwa nayo ili waweze kuokolewa. Hata hivyo, fumbo la vitako viwili vya fedha na ndimi mbili ambazo zilifungamana vizuri linatuonyesha sisi juu ya fumbo la wokovu wa Mungu. 
Ili tuweze kuutambua ukweli wa “ndimi mbili na vitako viwili vya fedha” vilivyokuwa vimewekwa chini ya mbao, tunahitaji kwanza kuufahamu ukweli wa msingi wa injili. Milango yote ya Hema Takatifu la Kukutania ilifumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Rangi hizi nne zinatuonyesha sisi kuwa ili tuweze kuokolewa toka katika dhambi zetu na uharibifu, basi ubatizo na damu ya Yesu ni vya muhimu sana. Na zinatuwezesha kuamini katika ukweli wa wokovu wa Yesu pasipo kuwa na mashaka yoyote. Ni lazima tuwe na ufahamu mzuri wa ukweli ambao umetuokoa uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa na kisha tuuamini ukweli huu. 
Yesu alisema, “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Kwa hiyo, sisi sote ni lazima tupokee ondoleo la dhambi kamilifu kwa kuufahamu ukweli wa kiroho ambao umefichwa katika rangi nne zilizodhihirishwa katika mlango wa kisitiri wa Hema Takatifu la Kukutania na pazia la Patakatifu pa Patakatifu. Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ni vifaa vya mlango vya Hema Takatifu la Kukutania. 
Kwa maneno mengine, Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme wetu sisi tunayeamini, sisi ambao Yesu ametuokoa mara moja toka katika dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana na kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake mweneywe mara moja na kwa wote, na kwa kuzichukua dhambi za ulimwengu na kuimwaga damu yake Msalabani. Kule kusema kuwa Yesu Kristo, ambaye ni Mfalme, aliweza kutuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu ni kwa sababu alibatizwa na kusulubiwa. Kwa hiyo, nyuzi za bluu na nyekundu zinatueleza sisi kuhusu ukweli halisi ambao hauwezi kuachwa ili sisi tuweze kuokolewa toka katika dhambi. Ili kuzichukua dhambi zetu, Yesu alibatizwa na Yohana, na kwa kuzibeba dhambi za ulimwengu na kuimwaga damu yake Msalabani, Yesu ametuokoa sisi mara moja na kwa wote toka katika dhambi zetu, kwa hiyo amezikamilisha kazi zake za wokovu.
Hapa ni lazima tuamini kuwa dondoo nne za nyuzi za bluu (ubatizo wa Yesu), nyuzi nyekundu (damu yake aliyoimwaga), nyuzi za zambarau (Yesu ni Mfalme wetu), na kitani safi ya kusokotwa (Yesu ni Mungu wa Neno, na ametufanya sisi kuwa wenye haki) vyote ni vifaa vilivyotumika kwa ajili ya wokovu wetu. Ni lazima tutambue kuwa ikiwa tutajaribu kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuuamini kitu kimoja tu kati ya hivi, basi wokovu wa namna hiyo hauwezi kuwa mkamilifu. Kwa nini? Kwa sababu chini ya kila ubao wa Hema Takatifu la Kukutania, kulikuwa na ndimi mbili zilizochomoza ili ziweze kuunganishwa katika vile vitako vya fedha ili kuushikilia ubao. 
Katika Biblia fedha inamaanisha neema ya Mungu, ambayo ni karama ya Mungu. Katika Warumi 5:1-2 imeandikwa hivi, “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.” Wokovu wetu unaweza kupatikana kwetu wakati imani yetu inapokubaliana na neema ya Mungu kiusahihi. Kama ambavyo kulikuwa na ndimi mbili chini ya kila ubao wa Hema Takatifu la Kukutania, na ndimi hizi ziliunganishwa na vitako vya fedha ili kuushikilia ubao, Mungu anatueleza sisi kuwa wokovu unakamilika pale tunapooamini vivyo hivyo katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. 
Sisi sote tulipaswa kuamini katika ufahamu na vitu halisi kuwa ilikuwaje basi kila ubao ukawa na ndimi mbili zilizoinuka. 
Vitako hivi viwili na ndimi mbili za ubao ni vivuli vya injili ya maji na Roho, kwamba katika kipindi cha Agano Jipya Yesu Kristo atakuja, atabatizwa na Yohana Mbatizaji, atasulubiwa, na atamwaga damu yake na kufa Msalabani, na kwa hiyo atautimiza wokovu kikamilifu. 
Kwa maneno mengine, neema ya ondoleo la dhambi inatolewa katika mioyo ya wale ambao wanaamini kwa kweli katika wokovu wao wa haki ambao Yesu ameutimiza kwa kubatizwa na Yohana na kuimwaga damu yake Msalabani ili kuzitoweshea mbali dhambi zao. Kwa hiyo, ili sisi tuweze kuokolewa toka katika dhambi zetu, tunahitaji kuwa na imani inayoamini katika kazi hizi mbili za Yesu. Kusema kweli, kila kitu cha Hema Takatifu la Kukutania kinatoa taswira ya wazi na ya kina ya Yesu ambaye ametuokoa sisi toka katika dhambi. Si kweli kuwa Bwana aliwaambia waisraeli kutumia ndimi mbili na vitako viwili vya fedha katika kila ubao wa Hema Takatifu la Kukutania pasipo sababu yoyote. 
Sisi tumeokolewa na kukombolewa toka katika dhambi zetu zote na adhabu yote ya dhambi kikamilifu kwa kupitia kazi za ubatizo na kuimwaga damu ambazo Mungu ametupatia. Kwa maneno mengine, ni kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndio maana tunapokea haki ya kufanyika watoto wa Mungu. Imani yetu ambayo ni kama dhahabu safi imejengwa kwa kuipokea karama hii ya Mungu.
 

Je, Bado Unajifahamu Kuwa Wewe ni Nani Hata Pale Unapomwamini Yesu?
 
Je, unajifikiria wewe mwenyewe kuwa ni mwema? Je, kwa namna yoyote ile na ama kwa muundo wowote ule unadhania kuwa wewe mwenyewe unayo tabia ya haki ambayo haiwezi kuvumilia lolote lisilo la haki kabisa? Je, unafikiria kuwa angalau kwa sehemu wewe una haki mbele za Mungu ati kwa kuwa unazifuata sheria za Mungu katika moyo wako kila siku na kwamba unazitii na kuzitenda katika maisha yako? Kwa kweli yote ambayo tunayafanya ni kule kujifanya kuwa sisi ni wenye haki hali tukifanya uzinifu na umalaya kisirisiri. 
Siku hizi, kuna vituo vingi vya Televisheni (luninga) ambavyo huonyeshwa kutoka katika masafa mbalimbali au katika satalaiti. Hali vikifanya kazi kwa masaa 24 kwa siku vituo hivi vina programu zao ambazo huwekwa kwa mfuatano. Miongoni mwa vituo hivi, vituo ambavyo ni vya kibiashara zaidi na vyenye mafanikio ni vile vituo vya watu wazima. Kuna vituo vingi vya jinsi hiyo vinavyoitwa vituo vya watu wazima ambapo kuna picha nyingi za ngono zinaweza kutazamwa kwa kuangalia katika vituo hivi. Je, ni vipi kuhusu tovuti za ngono? Bila hata ya kuhitaji kusema, hivi sasa kuna barua pepe nyingi ambazo ni mbovu na zinabeba ujumbe wa ngono kwenda kwa watu katika ulimwengu mzima. Kila mmoja anajionea mwenyewe uovu uliomo katika tovuti hizi, lakini tunapofikiria juu ya kanuni ya “mtawanyo wa bidhaa na mahitaji,” basi tunaweza kusema kuwa vituo hivi vinapata mafanikio sana kwa sababu watu wengi wanafurahia tovuti hizi katika wakati wao wa siri. 
Uzoefu huu unatuonyesha kuwa sisi wanadamu kimsingi tuna mapungufu na madhaifu. Biblia inataja juu ya mioyo ya wanadamu yenye dhambi hali ikitaja mambo kama uasherati, uzinifu, na uchafu. Mungu alisema kuwa vitu hivi vinatoka katika mioyo ya watu na vinawachafua na kwamba wana dhambi kwa sababu hiyo. Je, sisi sote hatujajawa na dhambi? Mungu alisema tena kwa kurudiarudia kuwa kitu kilichotujaa sisi ni dhambi. 
Lakini, je, tunalikubali kweli jambo hili? Je, jambo hili likoje? Je, tunaweza kukwepa toka katika hali ya dhambi ambayo imetujaa sisi kwa kuyafumba macho yetu na kuyafunika masikio yetu? Sisi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda aina mbalimbali za dhambi kwa mawazo na fikra zetu. Hata kama tukizielezea nafsi zetu kuwa tunapaswa kuondoka toka katika dhambi za jinsi hiyo, na hata kama tukijitahidi kiasi gani kufanya hivyo, basi juhudi hizo zote zitaishia katika utupu. Kwa kweli, miili yetu ipo hivyo kiasi kuwa hatuwezi kamwe kufanyika watakatifu wakamilifu ambao hatufanyi dhambi yoyote, bali ukweli ni kuwa tuna ushirika na dhambi na hatutamani kukaa mbali nayo. Miili na roho za wanadamu mara nyingi inapelekwa mbali toka katika vitu ambavyo ni vitakatifu, na ukweli ni kuwa si kuwa mioyo hii inapenda kuwa karibu na dhambi bali inapenda hata kuzifanya dhambi kubwa zaidi. 
Huko Mashariki, watu wengi wanajifunza mafundisho ya Konfusio tangu wanapozaliwa, na kwa hiyo wanajitahidi sana kuyaweka mafundisho haya katika vitendo. Kwa upande mwingine, huko Magharibi, Ukatoliki na makanisa ya Kikristo ya kihalali yametawala maisha yao ya kidini, na watu wengi wa Magharibi wamejaribu sana kuifuata Sheria ya Mungu hali wakidhani kuwa wataendelea kuwa watakatifu zaidi na zaidi kadri wanavyoifuata sheria na kujitahidi kuitenda. Lakini bila kujalisha misingi yao ya kidini ilivyo, wanapokuwa wamejiweka mbele za Mungu na wanapokuwa wamejifunua katika nafsi zao za kweli, basi wote hao ni kama lundo la dhambi na mbegu za watenda maovu. 
Wanadamu si wenye haki, wamejawa na mawaa, na ni lundo la dhambi lililofanywa kwa mavumbi na uchafu. Hata wale watu ambao wanaonekana kuwa ni wema ambao matendo yao mema yanatendwa kinyume na utambuzi bali toka katika mioyo yao yenye ukweli, na ambao wanachukia kupokea sifa zozote kutokana na matendo yao mema, nao pia hawawezi kukwepa ule ukweli kuwa uwepo wao kimsingi ukitazamwa mbele za Mungu, basi nao pia wataonekana kuwa ni lundo la dhambi na mbegu za watenda maovu. Kwa kuwa kuitetea haki ya mwanadamu ni uovu mkuu mbele za Mungu, basi watu hawawezi kukwepa toka katika adhabu ya dhambi hadi pale watakapoitambua adhabu yao na kuipokea injili ya maji na Roho ambayo ni upendo wa Mungu. Mbele za Mungu, juhudi za mwanadamu haziwezi kutafsiriwa kuwa ni uzuri wowote hata ule uzuri mdogo kama punje ya vumbi, na kwa kweli mapenzi ya mwanadamu ni uchafu tu mbele za Mungu. 
Katika Biblia, wanadamu wamekuwa wakitazamwa kuwa ni kama mti. Gogo la mti wa mshita lenyewe haliwezi kuinuliwa kuwa kama nguzo katika lango la kuingilia katika Hekalu la Mungu hadi pale Mungu alifunike kwanza kwa dhahabu. Na pasipo neema ya wokovu inayotolewa na Mungu, watu si kitu zaidi ya kuwa ni mavumbi ambayo hayawezi kufanya lolote zaidi ya kuikabili hukumu ya moto. 
Hata hivyo, Mungu aliziondolea mbali dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi kwa kumfanya Yesu Kristo Masihi kupokea ubatizo na kufa hadi kifo hata pale ambapo tulibakia kuwa ni wenye dhambi. Wokovu wa jinsi hiyo ulitabiriwa kwa kina na Mfalme Daudi takribani miaka elfu kadhaa iliyopita kabla Masihi hajaja: “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi, Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi” (Zaburi 103:12-14).
Kabla hatujaifahamu haki ya Mungu, haki ya mwanadamu ilikuwa ndio kipimo chetu cha maisha. Mimi pia nilikuwa kama hivyo hasa wakati ule nilipokuwa siifahamu karama ya Mungu ya wokovu na wakati sina imani katika Neno lake. Kwa kweli, mimi sikuwa na haki yangu binafsi, lakini bado nilijifikiria mwenyewe kuwa ni mwema. Kwa hiyo tangu utoto wangu kulikuwa na nyakati nyingi ambapo sikuweza kuvumilia utovu wa haki na hivyo nikajikuta nikipigana na watu ambao sio wa rika yangu. Kauli mbiu yangu ilikuwa ni “Ishi maisha ya yaki”. Vivyo hivyo, kwa kuwa nilikuwa nimeshindwa kujiona mimi mwenyewe mbele za Mungu, basi nilijazwa na haki yangu binafsi. Kwa hiyo nilijidhania kuwa mimi ni bora kuliko wengine na nilijitahidi sana kuishi kwa haki. 
Lakini kiumbe kama mimi sikuwa lolote zaidi ya lundo la dhambi mbele ya haki ya Mungu. Sikuwa mtu ambaye niliweza kuifuata hata moja ya zile Amri Kumi au zile sheria 613 ambazo Mungu aliamuru zifuatwe. Ule ukweli wenyewe kuwa nilikuwa na nia ya kuzifuata basi tendo hili lenyewe lilikuwa ni kinyume na haki kwani nia hiyo ilikuwa inaliasi Neno la Mungu ambalo linasema wazi kuwa mimi sina chochote ninachoweza kukifanya zaidi ya kuendelea kutenda dhambi, na kwa jinsi hiyo nilikuwa ninasimama kinyume na Mungu. Haki zote za mwanadamu ni utovu wa haki mbele za Mungu. 
Kizazi hiki, ambacho kimempoteza Mungu na Sheria yake katika mafuriko ya uchafu na rushwa, pia kimepoteza ile fahamu ya dhamiri ya dhambi. Hata hivyo, tunapaswa kutambua kuwa sisi wanadamu hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi kila siku na kwa hiyo tumepangiwa kwenda kuzimu pasipo ila yoyote. 
 

Sisi Tulikuwa Wasio na Haki na Tulijawa na Dhambi, Lakini Bwana Ametufanya Sisi Kuwa Watu Wake Mwenyewe Kwa Kutuokoa Toka Katika Dhambi Zetu kwa Injili ya Maji na Roho.
 
Sisi sote tulikuwa ni wale tusio na haki, lakini kwa kupitia karama ya wokovu, Bwana ametuokoa viumbe wa jinsi hiyo kama sisi toka katika dhambi zetu zote. Kila ubao wa Mahali Patakatifu ulikuwa na vipimo vya mita 4.5 (futi 15) kwa urefu na sentimita 67.5 (futi 2.2) kwa upana, paliundwa kwa mbao za mshita ambazo zilifunikwa kwa dhahabu na kisha zikainuliwa kuwa kuta za Mahali Patakatifu. Chini ya kila ubao, kulikuwa na vitako viwili vya fedha ili kuushikilia ubao. Vitako vya fedha vinadhihirisha kuwa Mungu amekuokoa wewe na mimi kikamilifu kwa uwezo wake mweyewe. 
Ule ukweli kuwa Mungu ametuokoa sisi toka katika dhambi ni ule upendo wake, na katika upendo huo Yesu Kristo alikuja hapa duniani na akabatizwa ili kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake, alibeba adhabu ya dhambi kwa kufa Msalabani, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi za ulimwengu na adhabu yote ya dhambi. Sisi tumezaliwa tena upya kwa kuamini katika karama ya wokovu ambayo Mungu ametupatia. Karama ya wokovu ambayo Bwana ametupatia ni kitu kisichoharibika kama dhahabu na kwa hiyo ni kitu kisichobadilika milele. 
Wokovu ambao Mungu ametupatia unatokana na ubatizo na damu ya Yesu, na kwa kweli wokovu huo umezitoweshea mbali dhambi zetu zote kikamilifu. Ni kwa sababu Bwana ametuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote ndio maana wewe na mimi tunaweza kukombolewa kikamilifu toka katika dhambi zote tunazozifanya kwa mawazo, kwa fikra zetu, na kwa matendo yetu halisi. Kwa kuamini katika karama ya wokovu ambayo Mungu ametupatia katika mioyo yetu, sisi tumefanyika kuwa watakatifu wake wenye thamani. Kwa kupitia vile vitako viwili ambavyo viliushikilia kila ubao wa Hema Takatifu la Kukutania, Mungu anatueleza sisi juu ya wokovu wa maji na Roho. Mungu anatueleza sisi kuwa tumefanyika kuwa watoto wake kwa asilimia 100 kutokana na neema yake na karama yake. 
Ikiwa tutaindoa imani ya ubatizo na damu ya Yesu toka ndani yetu, basi kutakuwa hakuna kitu kilichobakia ndani yetu. Sisi tulikuwa ni viumbe ambao tulifungwa ili tuhukumiwe kwa ajili ya dhambi. Sisi tulikuwa ni viumbe tunaoharibika ambao tulipangiwa kutetemeka mbele ya kifo chenye uhakika kwa mujibu wa sheria ya Mungu ambayo ilitangaza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, ambao tulipaswa kuendelea kuomboleza kwa sababu ya hukumu ya haki ya moto ambayo ilikuwa ikitusubiri. Hii ndio sababu kuwa sisi si kitu ikiwa tutaiacha imani yetu katika injili ya maji na Roho. 
Hali tukiishi katika kipindi ambacho kimejawa na dhambi, basi tusisahau kamwe kuwa majaliwa yetu yalikuwa ni yale ya kusubiri hukumu ya moto. Sisi tulikuwa ni viumbe dhaifu kiasi hicho. Hata hivyo, neema ya Mungu imewekwa juu yetu kikamilifu kwa sababu Mungu ametupatia wokovu wa maji na Roho. Masihi alikuja hapa duniani, alibatizwa na Yohana, akaimwaga damu yake na kufa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu zote na kutoka katika kule kutokuwa na haki na adhabu yetu yote. Kwa kuamini katika injili hii sahihi ya maji na damu, basi sisi sasa tumeokolewa toka katika dhambi zetu zote, na kwa hiyo tunaweza kumshukuru Mungu kwa imani yetu tu. 
Pamoja na kuwa tuna mapungufu katika mwili, wafanyakazi wetu, wahudumu, na mimi tunaihubiri injili hii ya maji na Roho katika ulimwengu wote. Pamoja na kuwa kipindi hiki kimegubikwa sana na rushwa, lakini kwa sababu tunaamini katika injili ya maji na Roho, basi tumeweza kumtumikia Bwana kwa usafi hali tukiwa safi toka katika uovu wowote. Kule kufikia kuwa na ufahamu huu katika mawazo yetu hakutokani na nguvu zetu wenyewe bali ni kwa sababu Bwana ametupatia utakatifu kwa kutufunika katika neema yake ya wokovu. 
Sisi tumefunikwa katika nguvu ya wokovu huu kwa sababu Bwana ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi na adhabu, na ni kwa sababu ya jambo hili basi ndio maana tumeweza kumtumikia Bwana kwa usafi. Kwa kuwa Bwana ametuokoa sisi toka katika dhambi zote kwa maji na Roho, basi ninaamini kuwa tunaweza kumtumikia yeye bila kujalisha madhaifu yetu, mapungufu, tukiwa hatujafungwa tena katika dhambi na adhabu ya dhambi. 
 

Kwamba Niko Hivi Jinsi Nilivyo Kwa Kweli Ni Kwa Neema ya Mungu
 
Kwa kweli kama isingekuwa ni kwa neema hii ya Bwana, basi mambo haya yote yangelikuwa ni vigumu kuyafanya. Kwa kweli kama isingekuwa neema ya Mungu, basi isingewezekana kabisa kuineneza injili ya maji na Roho katika ulimwengu wote na kuitumikia kwa usafi. Mungu ametupatia neema ya wokovu kwa asilimia 100 ili kwamba mimi na wewe tuweze kuishi maisha yetu hali tukiilinda na kuitumikia injili. 
Sisi tumefanyika kuwa nguzo za Hekalu la Mungu (Ufunuo 3:12) na watu wa Ufalme wa Mungu kwa imani. Kwa kuwa Mungu ametupatia imani kama dhahabu, basi sasa tunaishi katika Nyumba ya Mungu. Katika nyakati hizi ambapo ulimwengu umefurikwa na dhambi, katika kipindi ambacho watu walio wengi wanamsahau au kumdhihaki Mungu, sisi tumeoshwa kwa maji safi na tumefanyika kuwa safi, na tumewezeshwa kuyanywa maji safi na kumtumikia Bwana kwa usafi—sina maneno ya kutosha kuelezea jinsi ambavyo ninamshukuru Mungu kwa baraka hii. 
Kwa kweli hivi ndivyo imani yetu ilivyo. Je, tungewezaje sisi kufanyika wenye haki? Tumewezaje basi sisi wenyewe kujiita ni wenye haki wakati hakuna wema ndani yetu. Je, inawezekanaje basi sisi viumbe wenye dhambi kiasi hicho kama vile wewe na mimi kuwa tusio na dhambi? Je, ungeweza kufanyika usiye na dhambi na kuwa mwenye haki kutokana na haki ya mwili wako? Mawazo ya mwili, jitihada zako mwenyewe, na matendo yako mwenyewe—je, kuna lolote katika haya linaweza kukufanya wewe kuwa usiye na dhambi au kuwa mwenye haki? Je, usingeliweza kufanyika mwenye haki kwa imani katika injili ya maji na Roho? Je, ungeliweza kufanyika mwenye haki kwa imani yako katika wokovu wa Mungu uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa? Je, ungeweza kufanyika mwenye haki pasipo kuamini katika wokovu kwa kupitia injili ya maji na Roho iliyotimizwa na Masihi na kufunuliwa katika Neno la Mungu? Usingeweza kufanyika hivyo! Hatuwezi kufanyika wenye haki ikiwa tutaamini katika nyuzi za rangi nyekundu tu. 
Kwa kuwa Yesu Kristo, Mwokozi wetu na Masihi alibeba dhambi zote za ulimwengu, zikiwemo dhambi zote katika kipindi chote cha maisha yetu kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu kwa niaba yetu, basi sisi tumefanyika kuwa ni wenye haki kwa imani. Kama ambavyo sadaka ya kuteketezwa ya Agano la Kale ilivyozibeba dhambi wakati wenye dhambi au Kuhani Mkuu walipoiweka mikono yao juu ya kichwa cha mwanasadaka, basi katika kipindi cha Agano Jipya, Yesu alizipokea dhambi zote za ulimwengu ambazo zilipitishwa kwake kwa kubatizwa na Yohana. Kwa kweli Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake (Mathayo 3:15) na alishuhudiwa na Yohana kuwa “Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). 
Baada ya kuupokea ubatizo wake, Yesu aliishi miaka mitatu inayofuata ya maisha yake kwa ajili ya wokovu wetu, hali akizimaliza dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi kwa kuelekea Msalabani na kisha kuutoa mwili wake kwa Mungu kama mwanakondoo anyamazae mbele yao wamkatao manyoya, na kwa hiyo ametupatia sisi maisha mapya. 
Kwa kuwa Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana ndio maana aliweza kujitoa yeye mwenyewe kimya kimya na akapigiliwa misumari katika mikono yake na miguu pale aliposulubiwa na askari wa kirumi. Hali akiwa ameangikwa Msalabani, Yesu aliimwaga damu yote iliyokuwamo katika mwili wake. Na aliweka kipindi cha mwisho kwa wokovu wetu pale aliposema, “Imekwisha” (Yohana 19:30). 
Baada ya kufa, Yesu alifufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu, akapaa kwenda katika Ufalme wa Mungu, na amefanyika kuwa Mwokozi wetu kwa kutupatia uzima wa milele. Kwa kuzibeba dhambi za ulimwengu kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, na kwa Msalaba, ufufuo, na kupaa, Yesu amefanyika kuwa Mwokozi wetu mkamilifu. Kwa hiyo, Biblia inatangaza, “Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:18).
 


Imani Katika Damu ya Msalaba na Fundisho la Utakaso Unaoongezeka Havijakuokoa Kamwe Kikamilifu Toka Katika Dhambi Zako

 
Wakristo ni lazima watambue kuwa hawawezi kuokolewa kikamilifu toka katika dhambi zao kwa kuamini katika damu ya Yesu tu pale Msalabani. Kwa kuwa watu wanatenda dhambi kila siku kwa macho yao na matendo, basi hawawezi kuzitoweshea mbali dhambi zao kwa kuamini tu katika damu ya Msalaba peke yake. Moja kati ya uovu unaopotosha unaofanywa katika maisha ya watu siku hizi ni uovu wa ngono. Kama desturi ya uwazi na uchafu, ngono inaupotosha ulimwengu, dhambi hii imo ndani ya miili yetu. Biblia inaamuru kutotenda uzinifu, lakini ukweli wa siku hizi ni kuwa kutokana na mazingira yanayowazunguka watu, watu wengi wanaishia kuitenda dhambi hii hata pale ambapo hawapendi kufanya hivyo. 
Mungu anasema kuwa mtu yeyote anayemwangalia mwanamke kwa tamaa amekwisha kuzini naye katika moyo wake (Mathayo 5:28), na kwa kweli yale ambayo macho yetu yanaona kila siku ni uchafu mtupu. Kwa hiyo wanatenda dhambi chafu kama hizo kila dakika na kila sekunde. Hali inapokuwa hivi, wanawezaje basi kutakaswa kwa kutoa sala zao za toba na kisha kuingia katika Ufalme wa Mungu? Wanaweza kufanyika wenye haki? Je, mioyo yao ilifanyika kuwa yenye haki walipojiwekea nidhamu kwa kipindi kirefu na kisha kutakaswa kwa kiwango fulani walipokuwa wazee? Je, tabia yao ilifanyika kuwa ya unyenyekevu? Je, walikuwa wavumilivu zaidi? Kwa kweli sivyo! Kinachotokea ni kitu tofauti na hali ilivyo. 
Miongoni mwa mafundisho mengine ya Kikristo ni pamoja na “fundisho la utakaso unaoongezeka.” Fundisho hili linashikilia kuwa wakati Wakristo wanapoamini katika kifo cha Yesu Msalabani kwa muda mrefu, wanapotoa maombi ya toba kila siku, na wanapomtumikia Mungu kila siku, basi hatimaye watafanyika kuwa watakatifu na wenye tabia nzuri. Fundisho hili linadai kuwa kadri muda unavyozidi kwenda tangu tulipoanza kuamini katika Yesu, basi ndivyo tunavyozidi kufanyika wale wasio na dhambi na ambao matendo yao ni mema, na kwamba hadi kifo kitakapotukaribia, basi tutakuwa tumekwishatakaswa kikamilifu na hivyo kuwa tusio na dhambi kabisa. 
Pia fundisho hili linatufundisha kuwa kwa kuwa tutakuwa tumetoa sala zetu za toba wakati wote, basi tutakuwa tumeoshwa dhambi zetu kila siku, kama ambavyo nguo zetu zinavyooshwa, na kwa hiyo tutakapokufa baadaye tutaenda kwa Mungu kama watu ambao tumefanyika kuwa ni wenye haki wakamilifu. Kuna watu wengi wanaoamini hivi. Lakini hizi ni hisia za kinafiki ambazo zimeundwa na mawazo ya mwanadamu. 
Warumi 5:19 inasema, “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.” Kifungu hiki kinatueleza kuwa sisi sote tumefanywa tusio na dhambi kwa utii wa mtu mmoja. Kitu ambacho mimi na wewe hatukuweza kukifanya, Yesu Kristo alikiweza wakati alipokuja hapa duniani. Hali akifahamu kuwa wewe na mimi hatuwezi kujiweka huru toka katika dhambi, Yesu aliziondoa dhambi zetu kwa niaba yetu, kitu ambacho mimi na wewe tusingeweza kukifanya. Yesu amekuokoa wewe na mimi na ametusafisha toka katika dhambi zetu zote mara moja na kwa wote kwa kuja kwake hapa duniani, kwa kupokea ubatizo, kwa kusulubiwa, na kwa kufufuka tena toka kwa wafu. 
Yesu aliweza kuutoa wokovu kwa watu wake kwa kuwapatia ondoleo la dhambi zao kwa sababu alikubali kuyatii mapenzi ya Mungu. Hali akiyatii mapenzi ya Mungu kama Masihi, basi Yesu Kristo ametupatia neema ya wokovu kwa kupitia ubatizo wake, Msalaba, na wokovu. Hivyo, kwa kutupatia karama ya wokovu, Yesu ametimiza ondoleo la dhambi kikamilifu. Na sasa, kwa imani, tumefunikwa katika neema ya wokovu kwa kuwa Bwana ameutimiza wokovu wetu toka katika dhambi ambao usingeweza kupatikana kwa juhudi zetu wenyewe. 
Hata hivyo, Wakristo wengi hawaamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea, na badala yake wanaamini tu katika damu ambayo aliimwaga Msalabani na wanajaribu kutakaswa kwa kutegemea matendo yao binafsi. Kwa meneno mengine, hata pale ambapo Yesu alizichukua dhambi zote za mwanadamu wakati alipobatizwa na Yohana, bado kuna watu ambao hawaamini katika ukweli huu. Sura ya 3 ya Mathayo inatueleza sisi kuwa kitu cha kwanza ambacho Yesu alikifanya katika huduma yake ya wazi ilikuwa ni kuupokea ubatizo toka kwa Yohana. Huu ni ukweli ambao umethibitishwa na waandishi wa injili zote nne. 
Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji, ambaye ni mwakilishi wa wanadamu na mkuu kuliko wote waliozaliwa na wanawake, lakini kuna watu wengi sana ambao wanaudharu ukweli huu na hawauamini. Watu wa jinsi hiyo wanamwamini Yesu pasipo kuuamini ubatizo wake, na wanapendelea kuitukuza damu ya thamani ya Msalaba peke yake ambayo Yesu aliimwaga. Hali wakiwa wanatiwa uchungu na kifo cha Yesu Msalabani, wanainuka katika hisia zao na kufanya aina zote za mbwembwe katika kusifu kwao hali wakipaza sauti, “♫Kuna damu ya ajabu katika damu. ♪Kuna nguvu, nguvu ya kutenda miujiza katika damu ya thamani ya Mwanakondoo!♫” Kwa maneno mengine, wanajaribu kumwendea Mungu hali wakiwa wamejazwa na hisia zao binafsi, mihemko na nguvu. Lakini ni lazima utambue kuwa kadri wanavyozidi kufanya hivyo ndivyo wanavyozidi kuwa wanafiki hali wakijifanya kuwa ni watakatifu lakini kusema kweli hali wakizidi kuziruka dhambi katika mioyo yao kwa siri. 
 
 

Tunawezaje Kumwamini Yesu Kuwa Ni Mwokozi Wetu Pasipo Hata Kuifahamu Injili ya Maji na Roho?

 
Tunapowasikia watu wakizungumza juu ya Hema Takatifu la Kukutania, tunatambua kuwa hawafahamu kabisa kuhusu jambo wanalolizungumzia. Inapofikia suala la kuamini katika Hema Takatifu la Kukutania, tunawezaje kuamini katika jambo lolote ambao tunadhani kuwa ni sawa? Kwa kuwa wokovu toka katika dhambi ambao Mungu ameutimiza ni mpana, basi Mungu ametuwezesha sisi kutambua jinsi ambavyo wokovu huu ni mpana na jinsi ambavyo umetimizwa. 
Kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania, Mungu ametufanya sisi kutambua kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa nyuzi za bluu na zambarau, na kwa maji na damu. Tunakuja kutambua kuwa ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu, Bwana alikuja “si kwa maji tu, bali kwa maji na damu” (1 Yohana 5:6). Maji, damu, na Roho ambavyo tunaviamini ni kitu kimoja. Mungu ametuokoa sisi kwa kuja kwake Yesu kama mwanadamu, na kubatizwa na Yohana Mbatizaji, kufa, na kufufuka tena toka kwa wafu. Kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania, tumeweza kugundua na kuamini katika taswira hii ya wazi na ya kina ya wokovu. Kwa kusoma habari kuhusu ndimi mbili na vitako viwili vya fedha vya kila ubao, tumekuja kutambua mbinu ambayo kwa hiyo Yesu ametuokoa toka katika dhambi zetu. Na kwa hiyo tumeupata ukweli kuwa ni lazima kwa hakika tuamini katika huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Hakuna mahali pengine mbali na Biblia ambapo wokovu huu unaweza kuipata asili yake. Tunahitaji karama ya wokovu ambavyo inatokana na vitu hivi viwili vya ubatizo na Msalaba. Wale wanaoamini katika ukweli huu wanaweza kufanyika wale ambao wamezaliwa na Mungu. Mungu ameutimiza wokovu wetu kikamilifu kwa kutukomboa sisi toka katika dhambi kwa maji na Roho. 
Kwa maneno mengine, ndimi mbili zilitengenezwa chini ya kila ubao na ziliunganishwa katika vitako viwili vya fedha. Ukweli huu ni wa msingi sana na wa muhimu sana kwetu na kwa ajili ya ondoleo letu la dhambi. Jambo la muhimu sana, ni lazima tuamini katika wokovu wetu ambao Mungu ameutimiza kwa ajili yetu, kwa kuwa kama hatuamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, hatuwezi kuokolewa kamwe. 
Kama ambavyo kila ubao wa Hema Takatifu ulihitaji vitako viwili vya fedha ili uweze kusimama wima, basi inapofikia katika suala la kuamini katika Yesu Kristo, kweli mbili za neema yake ni za muhimu sana. Kweli hizo ni zipi? Kweli hizo ni kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa, na kwamba alibeba adhabu yote ya dhambi zetu na laana kwa kuzibeba dhambi hizo hadi Msalabani na kisha kusulubiwa. Yeyote ambaye amefanywa kuwa mwenye haki anaweza kufanywa hivyo pale anapoamini kikamilifu katika neema hizi mbili za wokovu mkamilifu. Imani yetu katika ubatizo wa Yesu na damu ya Msalaba, ambayo ni misingi miwili ya karama yake ya wokovu, inatufanya sisi kusimama imara katika Nyumba ya Mungu. Kama ambavyo ndimi mbili zilivyowekwa pamoja katika vitako viwili vya fedha, basi kila ubao uliweza kusimama wima. 
Vivyo hivyo, ni kwa imani yetu sahihi inayoamini katika misingi hii miwili ya wokovu wake ndio maana tumefanywa kuwa watu wake wa kweli tusio na mawaa. Kwa kuamini katika injili ya maji na damu iliyotolewa na Yesu, tunapokea imani kama dhahabu ambayo haibadiliki milele. Kwa kuamini katika injili hii ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, sisi tunafanyika watakatifu ambao tumepokea wokovu wa ondoleo la dhambi kamilifu. 
 

Theolojia Hadi Sasa na Kipindi cha Injili ya Maji na Roho
 
Ukikitoa kipindi cha Kanisa la Mwanzo, tangu tamko la Milan katika mwaka 313 B.K., Ukristo, ukiwemo Ukristo wa siku hizi umekuwa ukiieneza injili ya msalaba ambayo inauachilia mbali ubatizo wa Yesu. Tangu katika kipindi cha Kanisa la Mwanzo hadi mwaka 313 B.K., ambapo Ukristo ulihalalishwa kuwa ni dini mpya ya Kirumi, Ukristo ulikuwa ukihubiri injili ya maji na Roho, lakini baadaye kidogo Kanisa Katoliki la Rumi lilikuja kutawala wimbi la kidini. Kisha tangu mwanzoni mwa karne ya 14, kulianza kujitokeza desturi ambayo iliweka mambo yote katika mawazo ya mwanadamu na kusisitiza urudishwaji wa ubinadamu, desturi hii ilianza kwanza kuonekana katika miji mashuhuri ya kaskazini mwa Italia. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mabadiliko na mageuzi mapya. 
Hadi mwishoni mwa karne ya 16, mkondo wa desturi hii uliokuwa umeanzia huko Italia ulianza kuenea katika ulimwengu wote wa magharibi, na wanazuoni ambao walikuwa wamesomea juu ya ubinadamu, yaani falsafa iliyoundwa na mwanadamu walianza kusomea theolojia. Hali wakiitafsri Biblia kwa vichwa vyao wenyewe walianza kujenga mafundisho kadhaa ya Kikristo. Lakini kwa sababu walikuwa hawaufahamu ukweli basi walishindwa kuifahamu Biblia kiusahihi na kikamilifu. Kwa hiyo yale ambayo hawakuweza kuyafahamu kwa ufahamu wao, basi waliweza kushinda hali hiyo kwa kutumia ufahamu na mawazo yao ya kidunia, na kwa njia hiyo walizalisha mafundisho ya Kikristo ya aina yao. 
Kama matokeo, lundo la mafundisho ya Kikristo na theolojia ziliinuka katika historia ya Ukristo: Ulutheri, Ukalvin, Uarminian, Theolojia Mpya, Uhafidhina, Umantiki, Theolojia Makini, Theolojia ya Kimafumbo, Theolojia ya Ukombozi, Theolojia ya Kike, Theolojia Nyeusi, na hata Theolojia ya Upagani, n.k. 
Historia ya Ukristo inaweza kuonekana kuwa ni ndefu sana, lakini kusema kweli si ndefu kiasi hicho. Kwa miaka 300 tangu kipindi cha Kanisa la Mwanzo, watu waliweza kujifunza kuhusu Biblia, lakini hapa palifuatiwa na kipindi cha kati, ambacho ni kipindi cha giza kwa Ukristo. Katika kipindi hiki, walei hawakuruhusiwa kusoma Biblia maana kufanya hivyo kulikuwa ni kosa linalostahili adhabu hadi kifo kwa kukatwa kichwa. Ni mpaka ilipofikia katika miaka ya 1700 wakati upepo wa theolojia ulipoanza kuvuma, na ndipo Ukristo ukaonekana kama unachanua katika miaka ya 1800 na 1900 baada ya theolojia za wakati huo kukua na kuwa na nguvu, lakini sasa watu wengi wameanguka katika mafundisho ya kimafumbo hali wakimwamini Mungu kwa kutegemea katika uzoefu wao binafsi. Lakini pamoja na tofauti za kitheolojia, matawi yote ya Ukristo yametawaliwa na imani moja kimsingi, ambayo ni kuamini katika damu ya Yesu tu. 
Lakini je, huu ni ukweli? Unapoamini kwa namna hii, je, dhambi zako zinatoweka kweli? Unafanya dhambi kila siku. Unafanya dhambi kila siku kwa moyo wako, mawazo, matendo, na mapungufu. Unaweza basi kuondolewa dhambi zako kwa kuamini katika damu ya Yesu tu ambayo aliimwaga Msalabani? Kule kusema kuwa Yesu alizibeba dhambi zetu kwa kubatizwa na kufa Msalabani huo ni ukweli wa kibiblia. Hata hivyo kuna watu wengi sana ambao wanasema kuwa dhambi zao zimeondolewa kwa kuamini katika damu ya Yesu tu pale Msalabani na kwa kutoa sala zao za toba kila siku. Na bado kuna watu wengi sana wanaodai kuwa dhambi zao zimeondolewa kwa kuamini katika damu ya Msalaba tu na kutoa sala zao za toba kila siku. Je, dhambi za dhamiri zako zilisafishiliwa mbali kwa kutoa sala za toba za jinsi hiyo? Hii haiwezekani. 
Ikiwa ninyi ni Wakristo, basi ni lazima mfahamu na kuamini katika wokovu wa ukweli huu kwamba Yesu alikuja hapa duniani na akazichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana. Pamoja na haya, je, bado unaudharau ukweli huu, kiasi kuwa hutaki hata kuufahamu na kisha kuuamini? Ikiwa ndivyo, basi ufahamu kuwa unafanya dhambi ya kumdhihaki Yesu, dhambi ya kulishusha na kulidharau jina lake, na kwa jinsi hiyo huwezi kusema kuwa unaamini kweli katika Yesu kuwa ni Mwokozi wako. Kwa kuuacha ubatizo wa Yesu toka katika wokovu huu uliotimizwa na Yesu Kristo na kwa kumuamini Yesu kwa namna yoyote unayoipenda, basi kwa kweli huwezi kuvikwa katika neema ya wokovu. 
Hata hivyo Wakristo wengi bado hawaamini katika ukweli huu kama ulivyo, kwamba Yesu amezitoweshea mbali dhambi zetu zote, lakini badala yake wanafuata mawazo yao binafsi na wanaamini katika ukweli ambao umepindishwa na wanaoutaka kuuamini. Siku hizi, mioyo yao imefanywa kuwa migumu zaidi na zaidi kutokana na mafundisho haya ya kimaani yenye makosa, hali wakiamini kuwa dhambi zao zinaweza kutoweshwa kwa kuamini katika damu ya Msalabani peke yake. 
Lakini jibu la wokovu lilipangwa na Mungu ni kama lifuatalo: tunaweza kupokea ondoleo la dhambi la kudumu kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu, kifo chake Msalabani, na ufufuko wake. Lakini bado kumeinuka namba isiyohesabika ya watu ambao wanamwamini Yesu hali wakioundoa ubatizo wake toka katika ukweli huu wa wokovu, hali wakiielewa vibaya na kuiamini vibaya kanuni ifuatayo kuwa ni sheria isiyoweza kubadilika na kukosea: “Yesu (Msalaba na ufufuo wake) + sala za toba + matendo mema = wokovu unaopatikana kwa kupitia utakaso unaoongezeka.” Wale wanaoamini katika njia hii wanasema hivyo kwa midomo yao tu kwamba wamepokea ondoleo la dhambi. Hata hivyo, ukweli ni kuwa mioyo yao kwa kweli imejawa na mlundikano wa dhambi ambazo bado hazijatatuliwa.
Je, bado una dhambi katika moyo wako? Ikiwa una dhambi katika moyo wako hata pale unapomwamini Yesu, basi kwa hakika kuna tatizo kubwa katika imani yako. Hii ni kwa sababu unamwamini Yesu kama suala la kidini tu na ndio maana dhamiri yako si safi na una dhambi. Hata hivyo, ule ukweli kuwa unaweza kutambua kuwa bado una dhambi ambazo zimo katika moyo wako basi ni jambo la bahati. Kwa nini? Kwa sababu wale ambao wanatambua kwa kweli kuwa wana dhambi basi watatambua kuwa hawawezi kufanya lolote zaidi ya kufungwa kwenda kuzimu kwa ajili ya dhambi hizo, na watakapotambua hivyo basi hatimaye watakuwa maskini wa roho na kwa hiyo wataweza kulisikia Neno la kweli la wokovu. 
Ikiwa unapenda kupokea ondoleo la dhambi toka kwa Mungu, basi ni lazima moyo wako ujiandae. Wale ambao mioyo yao ipo tayari mbele za Mungu wanakiri kuwa, “Mungu, ninataka kupokea ondoleo la dhambi. Nimemwamini Yesu kwa muda mrefu, lakini bado nina dhambi. Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, siwezi kufanya lolote zaidi ya kutupwa kuzimu.” Vivyo hivyo, wanajitambua wenyewe kuwa ni wenye dhambi wakamilifu mbele za Mungu. Wale wanaolitambua Neno la Mungu, ndio wale wanaoamini kuwa Neno la Mungu limetimizwa kikamilifu pale linapozungumza nao. 
Mungu anakutana na nafsi hizo pasipo ila yoyote. Watu wa jinsi hiyo wanalisikia Neno lake, wanaliona Neno kwa macho yao wenyewe na wanalithibitisha, na kutokana na kufanya hivyo ndipo wanapokuja kutambua, “Aah, nilikuwa nikiamini kimakosa. Na kuna idadi kubwa isiyohesabika ya watu ambao wanaamini kimakosa hadi sasa.” Na kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, bila kujalisha ambavyo wengine wanaweza kusema, basi hatimaye wanapokea ondoleo la dhambi. 
 


Wale Ambao Wameokolewa Toka Katika Dhambi Zao Zote Ni Lazima Wailinde Imani Yao Kwa Kuamini Katika Injili ya Maji na Roho

 
Hata hivyo, ulimwengu huu umejazwa na mafundisho mengi maovu ambayo yanaweza kupotosha na kuchafua hata mioyo ya waliozaliwa tena upya. Bwana Yesu alituonya sisi, “Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode” (Marko 8:15). Lakini hatuwezi hata kuhesabu juu ya idadi ya mafundisho hayo yenye chachu, ambayo yanaichafua mioyo ya watu kwa kule kusikia mara moja. Ni lazima tutambue jinsi ambavyo ulimwengu huu unayumba katika tabia mbovu ya ngono. 
Sisi ambao tunaamini ni lazima tufahamu kwa hakika kuwa tunaishi katika kipindi gani ili tuweze kuilinda imani yetu. Hata pale tunapokuwa tukiishi katika ulimwengu huu wenye dhambi, ndani ya mioyo yetu kuna ule ukweli usiotuama kuwa Bwana ametukomboa toka katika dhambi. Neno la Ushuhuda ambalo linabeba ushuhuda kwa wokovu wetu usiobadilika ni injili ya maji na Roho. Ni lazima tuwe na imani katika ukweli huu ambao hautikiswi na au kuburuzwa na ulimwengu. 
Kila kitu toka katika ulimwegu huu si kweli. Mungu alitueleza sisi kuwa wenye haki wataushinda ulimwengu. Ni kwa imani katika injili ya kweli isiyobadilika ndipo wenye haki wanapomshinda Ibilisi na kisha kuushinda ulimwengu. Ingawa tuna mapungufu, miili yetu bado ipo katika Nyumba ya Mungu na inasimama imara katika injili ya wokovu kwa imani. Sisi tunasimama imara katika injili ya maji na damu ambayo kwa hiyo Bwana ametuokoa sisi. 
Kwa sababu ya hili, tunamshukuru sana Mungu. Haijalishi jinsi ambavyo dhambi ipo katika ulimwengu huu, angalau sisi wenye haki tuna dhamiri zisizo na mawaa na imani inayong’aa kama dhahabu katika mioyo yetu. Sisi wenye haki tutaishi sote maisha ambayo yanaushinda ulimwengu kwa imani. Sisi sote tutaendelea kuisifu imani hii hadi siku ile Bwana atakaporudi na hata pale tutakapokuwa katika Ufalme wake. Tutamsifu milele Bwana ambaye ametuokoa sisi na tutamsifu Mungu ambaye ametupatia sisi imani hii. 
Kwa kuwa imani hii ambayo tunayo mbele za Mungu imesimikwa katika mwamba, basi imani hii haiyumbishwi kwa namna yoyote ile. Kwa hiyo, bila kujalisha kinachotutokea tunapoishi hapa duniani hadi siku ile tutakaposimama mbele za Mungu, sisi tutandelea kuitetea imani yetu. Hata kama kila kitu katika ulimwengu huu kimeharibiwa, hata kama ulimwengu huu unaelea katika dhambi, na hata kama ulimwengu huu utakuwa mbaya kuliko sodoma na Goroma za zamani, bado sisi hatutaufuata ulimwengu huu, bali tutaendelea kumwamini Mungu kwa uaminifu, tutaitafuta haki yake, na tutaendelea kuzifanya kazi ambazo zinaeneza neema hizi mbili (ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani) za wokovu, ambazo ni neema za kweli za Mungu. 
 
 
Wale Wanaojifanya Kuamini katika Injili ya Kweli
 
Baadhi ya watu, hata pale ambapo hawaamini katika injili ya maji na Roho, bado wanajifanya kuwa wanauamini ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Lakini tunaweza kuona kuwa watu wa jinsi hiyo wana dhambi katika mioyo yao kwa kutokuamini katika injili ya maji na Roho kwa uaminifu. Ni kama wale waliopoteza kichwa cha shoka cha chuma klichokuwa kimeazimwa toka kwa jirani halafu kikatumbukia katika maji (2 Wafalme 6:5). 
Kwa namna iyo hiyo, inawezakana kabisa, hasa pale mahitaji yanapoongezeka kwa baadhi ya watu kuitumia injili ya maji na Roho kwa muda mfupi. Lakini pasipo kuamini kuwa injili hii ya maji na Roho ni ukweli, basi wanashindwa kuongea wakiwa na imani ya kweli wanapohubiri au wanapokuwa na faragha. Na wale wasio na imani mara nyingi wanaishia kuyakana maisha yao ya imani wakiwa katikati. Lakini ukweli wa injili ya maji na Roho haubadiliki, na kwa sababu hii wanapaswa kuamini katika injili hii ya Maji na Roho. 
Lakini nikinukuu Waebrania 7:12, ambayo inasema, “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike,” baadhi ya watu wanadai, “Sheria pia imebadilika. Kwa hiyo wokovu ambao Yesu ameutimiza hakuutimiza kwa namna ile ile kama katika Agano la Kale. Yesu Kristo alikuja na ametuokoa sisi kwa kufa tu Msalabani, mbinu ambayo imebadilishwa.” Baadhi yao wanadai, “Inaonyesha kuwa ni wakati Yesu alipokufa Msalabani ndipo ambapo Mungu alizipitisha dhambi zetu kwa Mwanae.” 
Lakini madai ya jinsi hiyo ni uongo na hayana msingi wowote. Tunaweza kuyakanusha madai yao kwa kusema, “Je, hii ina maanisha kuwa Mungu alimsulubisha Yesu ambaye hakuwa na dhambi na akazipitisha dhambi za ulimwengu juu yake wakati akisulubishwa?” Tunapoamini katika Neno la Mungu, ni lazima tuliamini kama lilivyo, na wala tusikazie katika mawazo yetu binafsi. Hata kama ikitokea tukawa na hoja zetu binafsi, ikiwa Biblia inatuambia kuwa hoja hizo ni dhambi, basi tunapaswa kuivunja hiyo haki yetu wenyewe na kisha kuamini katika Neno la Mungu. 
Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo tunavyozidi kushukuru na kuona thamani ya ukweli kuwa Bwana ametuokoa sisi kwa kupitia injili ya maji na Roho. Wakati tulipoamini kwa mujibu wa mawazo yetu binafsi, kulikuwa na nyakati wakati maisha yetu ya kiimani yalikuwa hatarini na ilikuwa karibu kabisa tuanguke kabisa toka Kanisani. Lakini kama ambavyo zile ndimi mbili zilivyoushikilia kila ubao wa Hema Takatifu la Kukutania kwa kuwekwa katika vitako viwili vya fedha, imani yetu katika ukweli wa Yesu, kuwa alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na kwa kuimwaga damu yake inatushikilia sisi kikamilifu. Kwa kubatizwa na Yohana na kuibeba adhabu yetu, kwa kusulubiwa na kuimwaga damu yake, Bwana wetu ametuokoa sisi toka katika dhambi zote. Kwa hiyo, imani yetu haiwezi kuyumba milele. 
Mithali 25:4 inasema, “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji.” Kama ambavyo kifungu hiki kinaonyesha, hata pale uovu na vitu vingi vibaya vinapojitokeza katika mawazo yetu ya mwili, kwa ubatizo wake na damu, Yesu ametusafisha sisi kutokana na vitu hivyo viovu, ambavyo vinatokana na dhambi za mwanadamu, na ametufanya sisi kuwa wafanyakazi wa haki ya Mungu. Bwana ametusafisha sisi toka katika dhambi za ulimwengu. Yesu ametusafisha na kutuokoa sisi toka katika dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana na kwa hiyo kuzipokea dhambi zetu zote mara mora na kwa wote, na kwa kusulubiwa na kuimwaga damu yake na hivyo kuibeba adhabu yote ya dhambi zetu. 
Kwa hiyo, wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho wamehakikishiwa juu ya wokovu wao wa kudumu. Matendo yetu yanaweza kuwa mabaya kwa baadhi ya nyakati, lakini injili ya maji na Roho inaishikilia imani yetu kwa nguvu kama ambavyo vile vitako vya fedha vilivyokuwa vimeushikilia kila ubao kwa kuzikamata ndimi zake mbili. 
 

Neema ya Wokovu ya Kudumu Inayotushikilia Sisi
 
Sasa hebu tugeuzie mawazo yetu katika yale mataruma yaliyokuwa yameshikilia mbao za Hema Takatifu la Kukutania pamoja. Kutoka 26:26-27 inasema, “Nawe fanya mataruma ya mti wa mshita; mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi.” Umbo la jumla la Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni mstatiri. Nguzo ziliwekwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania na kwa ajili ya pazia la Patakatifu pa Patakatifu, na vyote vilivyosalia vilifanywa kwa mbao. Mbao hizi zilishikiliwa pamoja kwa mataruma matano. 
Ili kuyashikilia mataruma haya, pete tano za dhahabu ziliwekwa katika kila ubao na katika mataruma yenyewe, mataruma haya yalitengenezwa kwa mti wa mshita kisha yakafunikwa dhahabu. Mataruma matano yaliwekwa katika mbao katika pande zote tatu za Hema Takatifu la Kukutania, kaskazini, kusini, na magharibi. Kwa kuwa mbao hizi zilishikiliwa na mataruma haya kwa kupitia katika pete za dhahabu, basi zilibaki zikiwa zimeshikamana vizuri. Kwa hiyo hali zikiwa zinashikiliwa kwa chini na vitako vya fedha, na kuungamanishwa pamoja katika pande zake kwa mataruma matano, basi zile mbao zilisimama imara na bila kuyumbayumba. 
Kadri zile mbao 48 zilivyokuwa zimezungukwa kwa mataruma matano na kisha kusaidiana zenywe kwa zenyewe, basi watu wa Mungu pia wanaungamanishwa na Mungu kwa injili ya maji na Roho. Kanisa la Mungu ni mahali ambapo wale waliopokea karama ya wokovu ya maji na Roho wanakutana pamoja na kuishi maisha yao ya imani. Yesu alimwambia Petro kuwa atalijenga Kanisa lake katika mwamba (Mathayo 16:18-19). Kwa hiyo, mahali ambapo Ufalme wa Mungu unaundwa kwa makusanyiko ya wale waliopokea ondoleo la dhambi basi hapo ni Kanisa la Mungu. Mungu anatueleza sisi kuwa ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi za ulimwengu kwa kazi za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Kutoka 26:28 inasema, “Na hilo taruma la katikati, lililo katikati ya zile mbao litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu.” Taluma hili la katikati liliundwa refu la kutosha ili kuweza kuziunganisha mbao zote za upande mmoja mara moja. Je, nini basi maana ya taruma hili lililopita katikati ya mbao toka mwisho huu hata mwisho huu? Ina maanisha kuwa wenye haki wataungana na wenzao, na kwamba imani yao itashirikiana na imani ya wenye haki wengine. Kwa maneno mengine, kwa kuamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana, basi wanaweza kushirikiana na wenzao katika imani. Wenye haki watakutana macho kwa macho na kwa imani yao. Hii ndio sababu tunapokutana na watakatifu wenzetu wahudumu na kuwa na faragha pamoja nao, basi kwa hakika tunaweza kuuhisi ushirika huu katika mioyo yetu. 
 

“Imani Moja, Ubatizo Mmoja, na Mungu Mmoja”
 
Hebu tugeukie Wefeso 4:3-7: “Na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili moja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana Mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.” Mtume Paulo alituambia sisi kuwa tujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Ubatizo wa Yesu na Msalaba—wakati tunapopokea karama ya wokovu iliyotengenezwa kwa mambo haya mawili basi ndipo amani inapokuja katika mioyo yetu. Wakati tunapopokea ondoleo la dhambi katika mioyo yetu, basi tunafanyika kuwa familia moja katika Kristo. Kwa kifupi tunafanyika kuwa mwili mmoja. 
“Bwana Mmoja.” Yesu Kristo aambaye ametuokoa sisi ni mmoja. “Imani moja.” Je, unaamini nini? Unaamini katika wokovu wa maji na damu ya Yesu na Roho vilivyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. “Ubatizo mmoja.” Mtume Paulo alisisitiza tena juu ya ubatizo wa Yesu kwa mara nyingine. Hapa hakuzungumzia juu ya Msalaba, bali alikazia juu ya ubatizo wa Yesu ambao uliwasafisha waamini wote pasipo masharti yoyote. Kwa sisi kuamini katika ubatizo wa Yesu ni kubatiwa katika Kristo na hivyo kumvaa Kristo (Wagalatia 3:27). “Mungu mmoja.” Mungu ni mmoja. Huyu Mungu ametuokoa sisi kwa kumtuma Mwanae pekee. 
Mambo haya yote yanazungumzia juu ya imani moja katika maji, damu na Roho (1 Yohana 5:8). Ni mpaka pale tunapokuwa na imani katika injili ya maji na Roho ndipo mioyo yetu inapoweza kushirikiana na mioyo ya wengine. Wale waliopokea ondoleo la dhambi wanaweza kukutana na kila mmoja wao macho kwa macho. Kunaweza kuwa na nyakati chache ambapo wanaweza kushindwa kuelewana kabisa. Lakini kama ambavyo taruma la katikati lililopitishwa katikati ya mbao toka mwisho huu hadi mwisho huu, basi ikiwa kweli wamepokea ondoleo la dhambi katikati ya mioyo yao basi wanaweza kushirikiana wao kwa wao. “Huyu ndugu pia ameokolewa toka katika dhambi, lakini mwili wake ni mdhaifu sana na kuna mabaki mengi ya uovu katika moyo wake. Kama mtu mwingine yeyote, yeye pia ni kama mbegu ya mtenda maovu, lakini hata hivyo Bwana ameziondolea mbali dhambi zake kwa injili ya maji na Roho.” Vivyo hivyo, watafikia hatua ya kuelewana wao kwa wao na hivyo kumtukuza Mungu. 
Haijalishi jinsi ambavyo watu wanaweza kuwa na mapungufu, lakini ikiwa wamepokea ondoleo la dhambi na kuendelea kukaa Kanisani, basi sura zao zitaangaza, mawazo yao yataangaza, fikra zao zitaangaza, mioyo yao itaangaza pia, na wataweza kushirikiana na wenzao. Wenye haki wanaweza kuonana wao kwa wao kwa macho. Je, nini kinachofanya hili liwezekane? Ni imani inayofanya hili liwezekane. Wanaweza kutazamana macho ana kwa ana si kwa sababu ya jambo jingine lolote bali ni kwa sababu ya imani. Je, ni nini basi kinachoweza kuelezea kule kushindwa kwetu kushirikiana na wengine? Mioyo yetu haiwezi kushirikiana na wale wasio ndani ya Kristo kwa sababu hawaamini katika mioyo yao juu ya ukweli katika injili ya maji na Roho. Wale wasioamini katika injili hii ya maji na Roho hawawezi kushirikiana nasi kabisa. 
Kaka zangu na dada zangu, Je, Kanisa la Mungu ni kitu gani? Ni kusanyika la wale ambao wametakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa kuwa watakatifu (1 Wakorintho 1:2). Ni kusanyiko la waamini wale wanaoamini katika ukweli kuwa Yesu Kristo amezioshelea mbali dhambi zao kwa kubatizwa, na kwamba amewaokoa wao kwa kuzibeba dhambi hizi na kubeba adhabu ya dhambi hizi Msalabani, na kwamba alifufuka tena toka kwa wafu na kwamba amefanyika kuwa Mwokozi wao. Kanisa la Mungu si kitu kingine zaidi ya kusanyiko la wale waliofanyika kuwa wamoja kwa kuamini katka injili ya maji na Roho. 
Ni kwa sababu imani hii imo katika mioyo yote, yaani moyo wangu na mioyo yenu ndio maana tunaweza kuangaliana macho tunapokuwa katika Kanisa lake Mungu. Kama ambavyo Mungu haangalii utu wetu wa nje bali katika kina cha moyo pale anapotuangalia, vivyo hivyo sisi pia tuliopokea ondoleo la dhambi hatuangalii pia utu wa nje, bali tunakuwa na ushirikiano kwa kuangalia katika kina cha imani ya kila mtu. “Je, mtu huyu anaamini kweli katika ukweli katika moyo wake?”—hivi ndivyo tunavyoangalia. Haijalishi jinsi ambavyo mtu anaweza kuwa na tofauti katika mwonekano wake, hii haijalishi kabisa ili mradi huyu mtu anaamini katika “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; Mungu mmoja na Baba wa wote.” 
Kwa sababu tunaamini, sisi tumefanyika kuwa ni nguzo na mbao za Hema Takatifu la Kukutania, na kwa sababu tunaamini, sisi tumefanyika kuwa familia ya Mungu. Je, unaamini katika injili ya maji na Roho? Ni kwa sababu tunaamini kuwa tunaueneza mwanga wa wokovu katika ulimwengu mzima, kama dhahabu safi (imani) inavyong’aa katika Nyumba ya Mungu. Tunaweza kuishirikisha mioyo yetu na wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi hivi karibuni, kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika mioyo yao pia. Ikiwa tumepokea ondoleo la dhambi, basi tunaweza kushirikiana na kila mmoja wetu, lakini kama hatujapokea ondoleo la dhambi basi hatuwezi kushirikiana na wengine. Wenye dhambi wanaowatenga watu kwa kuangalia utu wao wa nje wanafanyiana tofauti kwa kutegemea mambo hayo ya nje kama mwonekano, utajiri, au umashuhuri, lakini sisi wenye haki hatufanyi mambo haya katika mioyo yetu. Hakuna ubaguzi kwa wenye haki. 
Wakati watu wanapopokea ondoleo la dhambi kwanza, mara nyingi huwa nawauliza, “Je, umepokea kweli ondoleo la dhambi? Je, bado una dhambi, au je, dhambi zako zote zimetoweshwa? Kwa kweli, ni lazima uwe na maswali mengi kuhusu Biblia, je si ndivyo? Waulize katika wakati ambapo unaendelea kuishi katika maisha yako ya imani. Pia mapungufu yako yatafunuliwa na pengine utafanya makosa kadhaa katika safari ya kimaisha. Lakini viongozi na wale ambao walikutangulia katika Kanisa watakusaidia, na kila kitu kitageuka kuwa chema.” 
Kaka zangu na dada zangu, sisi wenye haki tunalihitaji Kanisa. Hema Takatifu la Kukutania linamaanisha pia kuwa ni Kanisa la Mungu. Wale wasioamini katika maji na damu hawawezi kuja katika Kanisa la Mungu na kukaa humo. Wale wasioamini katika injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu hawawezi kuja na kukaa katika Kanisa lake. Ni wale tu wanaoamini katika ukweli ndio wanaoweza kukaa katika Kanisa, na kufanyika watu wa Mungu na watenda kazi wake, na kisha wakauona utukufu wa Mungu pia. Watu hawawezi kufanyika watoto wa Mungu kwa damu tu au kwa sifa fulani toka katika miili yao. Haijalishi jinsi ambavyo baadhi ya wachungaji wanaweza kuwa na mamlaka, lakini kama hawaamini katika injili ya maji na Roho basi hao si wana wa Mungu.
 
 

Yesu Aliyekuja Kwa Maji na Damu Ametuokoa Sisi Kikamilifu

 
Kile ambacho Bwana alikitenda alipokuja hapa duniani kinaweza kujumuishwa kwa kuzaliwa kwake, ubatizo, kuimwaga damu, na ufufuo. Vyote hivyi ni huduma zake za ondoleo la dhambi. Yesu ameutimiza utume wake kwa huduma zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania zilikuwa ni kwa ajili ya wokovu wetu toka katika dhambi. Wokovu wa Mungu ni mpana kiasi kuwa hatupaswi kumwamini yeye katika njia zetu. Tunapaswa kuuamini wokovu wake kama ulivyo. 
Imani yetu ni lazima iendane vizuri na zile kweli mbili za wokovu wake: Ubatizo wake na damu yake Msalabani. Hii ndiyo sababu ndimi mbili ziliunganishwa kwa usahihi katika mashimo ya vitako vya fedha. Hatuwezi kuuchukulia ukweli ambao Yesu ametupatia kama moja ya elimu za ulimwengu huu na kisha kuziamini kwa jinsi hiyo tu. Wewe na mimi ndio ambao tumeokolewa toka katika dhambi mbele za Mungu kwa kuamini katika kazi za Yesu za wokovu zilizodhihirishwa katika vitako viwili vya fedha. 
Hema Takatifu la Kukutania linatueleza sisi juu ya mbinu ya wokovu ya Yesu ya kina, na wokovu huu kwa kweli umetimizwa kwetu tayari. Amini katika karama mbili za wokovu ambazo Mungu amekupatia. Dhahabu iliyotumika katika Hema Takatifu la Kukutania inamaanisha imani. Ikiwa unaamini katika ukweli kama ulivyo, basi wokovu na utukufu wa Bwana utakuwa wa kwako, lakini hauwezi kuwa wako ikiwa hautaamini katika wokovu huo. Je, unapenda kuishi ndani ya Hema Takatifu la Kukutania kwa imani, hali ukiwa umefunikwa kwa utukufu wa Mungu na kulindwa naye, au unapenda kulaaniwa milele kwa kutoendelea kuamini? Ikiwa unaamini katika damu ya Msalaba tu, basi huwezi kuokolewa. Ni lazima uamini kuwa damu ya Msalaba na ubatizo ni kitu kimoja. Karama ya Mungu inaundwa na vitu hivi viwili. 
Roho wa Mungu anakaa katika mioyo yetu pale tunapoamini katika vitu hivi viwili (ubatizo wa Yesu na damu iliyomwagika). Roho Mtakatifu hakai kamwe katika mioyo ya wale ambao hawaamini vitu hivyo viwili. Ikiwa unaikiri imani yako kwa midomo yako tu lakini hauamini katika moyo wako, na kama ufahamu wako ni kama zoezi la kiakili tu, basi kwa hakika huwezi kuokolewa kamwe. Ili uweze kuokolewa, ni lazima kwanza uchore mstari wa wazi wa mpaka ukiweka bayana mpaka wa wokovu wako: “Hadi sasa, nilikuwa sijaokoka. Wokovu ambao nilikuwa nikiuamini haukuwa halisi. Lakini kwa kuamini katika Yesu ambaye alikuja kwa maji na na kwa damu, sasa nimeokolewa.” Watu wanaweza kufanyika wenye haki pale wanapokuwa kwanza ni wenye dhambi walau mara moja. Ni lazima wakiri kuwa kama watu ambao hawajaokoka, wamefungwa ili kuhukumiwa kwa sababu ya dhambi zao, na kisha watu hawa watafanyika wakamilifu waliookolewa kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. 
Kwa kupitia nyuzi za bluu na nyekundu, yaani ubatizo na damu ya Yesu, basi ni lazima sisi tuupokee wokovu wetu mkamilifu. Bwana ametupatia sisi karama ya wokovu mkamilifu kwa ubatizo wake na damu yake. Ili kutuzuia sisi kuamini kutokana na mawazo yetu binafsi, Bwana aliufunua wokovu huu kwa kina kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania. Kwa sababu wokovu huu ni wa thamani sana na mkamilifu, basi inampasa kila mtu kuuamini. Usiamini katika kitu kimoja tu cha wokovu wa Yesu ambacho ni damu ya Msalaba tu, bali uamini katika ubatizo na katika damu ya Msalaba kwa pamoja mara moja! Ikiwa kuna mtu yeyote miongoni mwetu ambaye hajaokolewa bado, basi ni matumaini yangu kuwa mtu huyo ataokolewa kwa kuamini hata sasa katika ukweli huu. 
Je, kuna mtu yeyote kama huyu miongoni mwetu? Kwa kweli inawezekana akawepo. Lakini matumaini yangu ni kuwa uwezekano huu usiweze kutambuliwa miongoni mwetu. Bila kujalisha kinachoweza kutoka, mimi siwezi kuwa miongoni mwa wasiookolewa. Sisi ni wale ambao tumeokolewa kikamilifu kwa kuamini katika vitu hivi viwili (bluu na nyekundu)—ambavyo ni ubatizo na damu ya Yesu. Ninamshukuru Mungu kwa karama hizi mbili za wokovu ambazo kwa hizo Bwana ameniokoa mimi. Kwa sababu Mungu ameutimiza wokovu wangu kikamilifu, basi mimi nimewekwa huru toka katika laana na hukumu pia. 
Kwa kweli, wokovu wetu ambao umekuja kwa kupitia nyuzi za bluu na nyekundu ni wa thamani sana kuliko maneno yote. Kumbuka na uamini kuwa wokovu wako unafanywa kuwa mkamilifu si kwa damu ya Msalaba tu, na wala si kwa ubatizo wa Yesu tu, bali kwa ubatizo na damu ya Msalaba, na ni kwa kuamini katika vitu hivi viwili ndipo unapoweza kufanyika mwana wa Mungu. Sisi tumepokea uzima wa milele kwa kuamini katika Neno la injili ya maji na Roho, fumbo lililofichika katika ndimi mbili na katika vitako viwili vya fedha vya mbao za Hema Takatifu la Kukutania. 
Ninatoa shukrani zangu nyingi sana kwako Bwana ambaye umetuokoa sisi toka katika dhambi za ulimwengu. Halleluya!