Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-17] Sadaka ya Ondoleo la Dhambi Inayotolewa Katika Kiti cha Rehema (Kutoka 25:10-22)

Sadaka ya Ondoleo la Dhambi Inayotolewa Katika Kiti cha Rehema
(Kutoka 25:10-22)
“Nao na wafanye sanduku la mti wa mshita; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili. Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu. Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa. Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa. Nawe fanya kiti cha rehema cha dhahabu safi; urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.”
 


Kiti cha Rehema

Kiti cha RehemaDhiraa ni urefu unaoanzia katika ncha ya kidole cha mkononi hadi kwenye kiwiko. Katika Biblia, dhiraa inakadiriwa kuwa na kipimo cha sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Urefu wa kiti cha rehema ulikuwa ni dhiraa mbili na nusu, na kwa hiyo kipimo hicho kinapo badilishwa katika vipimo vya kisasa, urefu huu unakuwa sawa na sentimita 113 (futi 3.7). Na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja na nusu ambao ni sawa na takribani sentimita 67.5 (futi 2.2). Vipimo hivi vinatupatia sisi ule ufahamu wa kawaida juu ya kipimo cha kiti cha rehema. 
Sanduku la Ushuhuda kwanza liliundwa kwa mbao za mshita na kisha lilifunikwa kwa dhahabu ndani na nje. Lakini kiti cha rehema, ambacho kiliwekwa juu ya sanduku la Ushuhuda kilitengenezwa chote kwa dhahabu safi. Katika miisho yake makerubi wawili waliwekwa hali wakiwa wameyakunjua mabawa yao kwa kwenda juu huku wakiufunika mfuniko wa juu wa sanduku—hii ni kusema kuwa, kiti cha rehema—na makerubi walielekezeana nyuso kukielekea kiti cha rehema. Kiti cha rehema ni mahali ambapo Mungu anaitoa neema yake kwa wale wanaomwendea yeye kwa imani.
Bangili nne za dhahabu ziliwekwa katika kila kona ya lile Sanduku. Bangili mbili za shaba ziliwekwa kila upande, na kisha miti iliwekwa kwa kupitia katika bangili hizo ili kwamba hilo Sanduku liweze kubebeka. Miti hii ilitengenezwa kwa mbao za mshita na kisha ilifunikwa kwa dhahabu. Kwa kuweka miti katika bangili hizi mbili kwa upande mmoja na kisha kuweka mhimili mwingine katika bangili mbili za upande mwingine, Mungu alihakikisha kuwa watu wawili walitosha kabisa kulibeba sanduku na kulichukua. Kisha Bwana wetu akasema, “Nitakutana nanyi katika kiti hiki cha rehema.” 
Mungu aliwafanya waisraeli kulibeba Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema kwa kuweka miti kupitia katika Sanduku. Hii inamaanisha kuwa Mungu anatuhitaji sisi kuieneza injili ulimwenguni kote. Hii ni sawa na ilivyokuwa katika madhabahu ya uvumba—ambapo, bangili ziliwekwa pia katika pande zake zote mbili, miti iliwekwa kupitia katika bangili hizo, na hivyo watu wawili walitayarishwa kuibeba madhabahu hii. Hii pia inamaanisha kuwa ni lazima tuombe msaada wa Mungu kila tunapopata magumu, na kwamba ni lazima pia tuombe kwa ajili ya kuieneza injili ulimwenguni mwote mahali popote tutakapokwenda.
Ndani ya Sanduku la Ushuhuda, kulikuwa na vitu vitatu vilivyowekwa: kulikuwa na bilauri ya dhahabu iliyokuwa imejaa mana, kulikuwa na fimbo ya Haruni ambayo ilichipuka, na kulikuwa na mbao nne za mawe ya Agano. Je, vitu hivyo vina maanisha nini? Kwanza, bilauri ya dhahabu ilikuwa inamaanisha kuwa Yesu Kristo anatoa maisha mapya kwa waamini. Wakati fulani Yesu alisema, “Mimi ndimi chakula cha uzima; Yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe” (Yohana 6:35). 
Fimbo ya Haruni iliyochipuka inatueleza sisi kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa ufufuo na kwamba anatupatia sisi uzima wa milele. Mbao za mawe za Agano zinatueleza sisi kuwa hatuwezi kabisa kukwepa hukumu mbele za Sheria. Hata hivyo, rehema za Mungu ni kuu sana kiasi kuwa inazifunika adhabu zote za dhambi zetu ambazo Sheria imetuhukumu katika hizo. Kiti cha rehema kilitosha kabisa kuwa mfuniko wa Sanduku la Ushuhuda ili kwamba ile laana ya Sheria isiweze kutoka kabisa. Mungu amekikamilisha kiti cha rehema kwa sadaka kamilifu ya Mwana wake Yesu. Kila mwamini katika injli ya maji na Roho basi anaweza kuja kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema ambacho ni kiti cha rehema.
 

Damu ya Thamani Ambayo Ilinyunyuziwa katika Kiti cha Rehema!
 
Kwanza ni lazima tutafute juu ya fumbo lililofichwa katika kiti cha rehema. Mara moja kwa mwaka, Kuhani Mkuu aliichukua damu ya sadaka ya kuteketezwa na kisha aliingia katika Patakatifu pa Patakatifu. Kisha aliinyunyuzia damu hii ya sadaka ya kuteketezwa juu ya kiti cha rehema mara saba kamili. Mungu alisema kuwa atakutana na waisraeli katika kiti hiki cha rehema. Mungu anakutana na yeyote mwenye imani sawa na ile ya Kuhani Mkuu, ambayo ni imani katika ondoleo la dhambi iliyofunuliwa katika utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. 
Damu ya sadaka iliyonyunyiziwa juu ya kiti cha rehema inaonyesha hukumu ya Mungu juu ya dhambi na rehema yake kwa wanadamu. Katika ile Siku ya Upatanisho, yaani siku ile ya kumi ya mwezi wa saba, Haruni Kuhani Mkuu aliilaza mikono yake juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka ya kuteketezwa ili kuzipitisha dhambi zote za mwaka mzima za watu wa Israeli juu ya mnyama huyo. Kisha alimchinja huyo mnyama na akaikinga damu yake, kisha aliichukua dhamu hii ndani ya lile pazia na akainyunyuzia juu ya kiti cha rehema (Mambo ya Walawi 16:11-16). 
Kwa kupitia ile damu ambayo ilinyunyiziwa, Mungu alikutana na waisraeli na akawapa baraka ya ondoleo la dhambi. Ilikuwa ni neema ya Mungu juu ya waisraeli kwamba Mungu alikuwa ameanzisha utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Kwa kule kuweka mikono juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na damu yake, Mungu alikuwa amezitoweshea mbali dhambi zao na kuwapatia rehema yake, ambayo ni ondoleo la dhambi zako kwa neema. 
Je, tunawezaje basi kuipokea neema hii? Je, ni kwa Neno gani ambalo kwa hilo Mungu amezitoweshea mbali dhambi zetu zote mara moja na kwa ajili ya wote? Mungu ametuwezesha sisi kutambua kwamba ni lazima tuwe na imani inayofahamu na kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa kwetu ili kwamba tuweze kupokea ile karama ambayo Mungu ametupatia. Mungu alifanya iwezekane kwa haki yake kutimizwa katika vigezo hivi viwili; kule kuwekea mikono juu ya kichwa cha mwanasadaka na damu yake. Sadaka hii ya Agano la Kale haielezei kitu kingine zaidi ya ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea na damu ambayo aliimwaga Msalabani. 
Yesu Kristo Mwana wa Mungu alibatizwa na Yohana kwa ajili ya dhambi zetu ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, akafanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa juu ya Msalaba ili kulipa mshahara wa dhambi, alikufa kwa ajili yetu, kisha akafufuka tena toka kwa wafu ili kutufanya sisi kuwa hai. Ubatizo ambao Yesu Kristo aliupokea na damu yake aliyoimwaga Msalabani zilipangwa kutupatia ondoleo la dhambi, na ni neema ya baraka za kweli zinazowawezesha wote walio na imani kama hiyo kuonana na Mungu. Ukweli huu ni kivuli cha injili ya maji na Roho. Injili ya maji na Roho ni ukweli ambao umeanzisha msingi wa imani ya kweli unaowawezesha wenye dhambi kupokea ondoleo la dhambi toka kwa Mungu. Yesu Kristso alifanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alifanyika kuwa ni daraja la ukweli unaoturuhusu sisi kumwendea Mungu Baba Mtakatifu. 
Tena, tunaweza kupata uthibitisho wa kuhitimisha kwa ukweli huu katika rangi za nyuzi nne zilizotumika katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania: nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa maneno mengine, nyuzi nne za mlango wa Hema Takatifu la Kukutania zinatupatia sisi uthibitisho wa injili ya kweli. 
Uthibitisho wa kwanza ni fumbo la nyuzi za bluu lililodhihirishwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. Fumbo hili linahusu kuwa Yesu Kristo alibatizwa na Yohana, ambalo linamaanisha kuwa Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake. Kwa maneno mengine, Yesu alizipokea dhambi zetu ambazo zilikabidhiwa kwake na Yohana. Na ndio maana Yesu alimsihi Yohana ili ambatize kwa kusema “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” (Mathayo 3:15).
Uthibitisho wa pili ni nyuzi za zambarau zilizodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Rangi ya “Zambarau” ni rangi ya mfalme. Yesu Kristo ni Mfalme wa wafalme aliyekuja hapa duniani kama Mwokozi wa wanadamu ili kuwakomboa toka katika dhambi. Yesu aliuacha utukufu wa Mbinguni na akaja hapa duniani ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu. Yesu Kristo ni Mungu mwenyewe katika uwepo wake, lakini ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote, Yesu alikuja hapa duniani, na akabatizwa na kusulubiwa kwa unyenyekevu kwa mapenzi ya Baba. Kwa maneno mengine, ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote, Mungu aliacha kiti cha enzi cha utukufu wa Mbinguni na akazaliwa katika mwili wa Bikira Mariam hapa duniani ili kuwaokoa wenye dhambi. Kwa hiyo ni lazima tuamini kwamba Mungu mwenyewe alipaswa kuzaliwa katika mwili wa bikira, kubatizwa, kuimwaga damu yake, yote hayo ni kwa mujibu wa ahadi ambayo Mungu aliitoa kwa Nabii Isaya zaidi ya miaka 700 iliyopita. 
Uthibitisho wa tatu ni nyuzi nyekundu. Nyuzi hizi zinaonyesha juu ya damu ya Yesu. Ukweli huu unadhihirisha kwamba Yesu aliukamilisha utume wa wokovu wa Mungu kwa kuimwaga damu yake Msalabani. Damu ya Yesu iliyomwagika Msalabani ilikuwa ni adhabu iliyokuwa imehifadhiwa kwa ajili ya watu waliokuwa waovu kuliko wote. Kwa kupitia adhabu ya dhambi ambayo Yesu aliibeba kwa kupitia ubatizo wake, dhambi zote za mwanadamu zilihukumiwa. Yesu alibeba adhabu ya dhambi zote za ulimwengu kwa kusulubiwa na kuimwaga damu yake na kwa hiyo ametuokoa sisi toka katika dhambi. Kwa kuzipokea dhambi zetu toka kwa Yohana kwa kupitia ubatizo wake na kwa kumtii Baba hadi kifo, Mungu amewaokoa wenye dhambi wote toka katika maovu yao. 
Je, unatambua kuwa Yesu aliimaliza adhabu yote ya dhambi na kwamba amewafanya waamini kuwa wana wa Mungu kwa yeye, pasipo hatia, kubeba adhabu yetu kwa kuadhibiwa na kusulubiwa? Mungu alifanya mambo haya yote ili kwamba tuweze kuamini katika ukweli huu na kisha kupokea uzima wa milele. Kule kusema kuwa Yesu alibatizwa na kisha akahukumiwa juu ya Msalaba kunamaanisha kuwa Yesu ametuokoa sisi toka katika dhambi. Na hii ndio maana Yesu alilia kwa sauti katika pumzi yake ya mwisho akisema, “Imekwisha!” (Yohana 19:30) Yesu alitangaza kwa furaha kuu kuwa ameukamilisha wokovu wetu toka katika dhambi kutokana na mapenzi ya Mungu Baba. 
Mwisho, kitani safi ya kusokotwa inaonyesha kuwa Yesu ni Mungu wa Neno. Yesu anayafunua mapenzi ya Mungu kwa kupitia Neno lake lililoelezwa kwa kina na lenye haki. Katika maeneo yote ya Agano la Kale, Mungu alisema mapema kuwa atakuja hapa duniani na kuwaokoa wanadamu wote kwa ubatizo wake na kusulubiwa. Kisha Mungu alizitimiza ahadi zake zote vizuri katika Agano Jipya. Hii ndio sababu Biblia inasema, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yohana 1:1, 14).
Ukweli huu umetuwezesha sisi kuoshwa dhambi zetu zote na kuwa nyeupe kama theluji. Ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu yake aliyoimwaga si kitu kingine bali ndio kule kuwekewa mikono na upatanisho wa hukumu wa utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa. Yesu aliimwaga damu yake Msalabani kwa sababu alikuwa amebeba dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake. Kwa kuwa Yesu alibatizwa ili kuzibeba dhambi zetu kwa niaba yetu, na kisha akaenda Msalabani na kuimwaga damu yake juu ya dhambi hizo, basi ukweli huu ndio ambao umefanyika kuwa upatanisho ambao umezioshelea mbali dhambi zetu. 
Ubatizo ambao Bwana wetu aliupokea alipokuja hapa duniani kama mwanadamu na damu yake ambayo aliimwaga Msalabani ni ukweli ambao umedhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Yesu alizaliwa hapa duniani miaka 2,000 iliyopita, alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, akafa Msalabani, akafufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu, alibeba ushuhuda kwa siku 40 zilizofuatia, na kisha akapaa kuumeni katika kiti cha enzi cha Mungu—huu ni ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Mungu anatuambia sisi kuamini katika ukweli huu, kwamba Yesu ametuokoa sisi toka katika dhambi zote kwa kuzitoweshea mbali dhambi zetu. 
Tunapouamini ukweli huu, Mungu anatueleza sisi kuwa, “Sasa, mmefanyika kuwa watoto wangu. Ninyi si wenye dhambi. Ninyi ni watu wangu na si wenye dhambi tena. Nimewaokoa toka katika dhambi zetu zote, adhabu, na laana. Nimewakomboa kwa upendo usio na masharti. Kwa sababu mnapendwa sana na Mimi, nimewaokoa ninyi pasipo masharti yoyote. Kwa sababu ninawapenda ninyi, nimewaokoa ninyi kwa uwezo wangu mwenyewe. Si tu kwamba nimewapenda ninyi, bali pia nimeonyesha upendo wangu kwa vitendo kwa njia hii. Tazameni damu ya kusulubiwa kwangu. Huu ni uthibitisho wa upendo wangu kwenu. Nimewaonyesheni uthibitisho huu.”
Wakati tulipokuja kwa Bwana kama masikini wa roho, Mungu alituonyesha kuwa ametuokoa sisi kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Bwana alikuja hapa duniani, alibatizwa, alidharauriwa na kuadhibiwa hadi kifo juu ya Msalaba, alifufuka tena toka kwa wafu, na kisha alipaa Mbinguni. Mungu anakutana na yeyote anayeamini katika upendo wake wa wokovu. 
Mungu anatoa neema ya wokovu juu ya wale wanaoamini. Wokovu wa Mungu umevigeuza viumbe vya kawaida kuwa wana wa Mungu mwenyewe. Mungu anasema kwetu kuwa, “Ninyi ni watoto wangu. Ninyi ni wana na mabinti zangu. Ninyi si wana wa Shetani tena, bali ni wana wangu. Ninyi si viumbe tena, bali ni watu wangu mwenyewe. Nimezipatanisha dhambi zenu zote kwa kupitia Mwana wangu Yesu. Sasa nimewafanya ninyi kuwa watu wangu, nanyi mmefanyika kuwa watu wangu kwa imani.” Mungu hajawaokoa wenye dhambi tu, bali pia amewapatia neema ya kuwafanya wao kuwa watoto wake mwenyewe. 
Mungu aliuita mfuniko wa Sanduku la Ushuhuda katika Hema Takatifu la Kukutania kuwa ni kiti cha rehema. Makerubi wawili waliwekwa wakikiangalia kwa chini kile kiti cha rehema. Kwa nini Mungu alisema kuwa atakutana na watu wa Israeli juu ya kiti cha rehema? Sababu ya hili ni kwa sababu Mungu aliziondosha dhambi za watu wa Israeli kwa kuipokea damu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa ambapo kwa hiyo dhambi zao zote zilikuwa zimepitishwa kwa kuwekewa mikono. 
Kwa maneno mengine, Mungu alisema hivyo kwa sababu alitaka kuwapatia watu wa Israeli ondoleo la dhambi kama karama kwa kuwafanya wazipitishe dhambi zao katika mnyama wao wa sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yao juu ya kichwa cha yule mwanasadaka, na kwa kumfanya mwanasadaka huyu kulipa mshahara wa dhambi hizi kwa niaba yao, haya yote yalifanyika ili kuzitoweshea mbali dhambi na uovu wa watu wake. Kwa kuwa Mungu hakuweza kukutana na wenye dhambi pasipo sadaka ya upatanisho, basi ni kwa kupitia sadaka hii ya kuteketezwa ndipo Mungu alizitoweshea mbali dhambi zao na akakutana nao. 
Kila mtu anazaliwa katika ulimwengu huu hali akiwa na dhambi kwa kuwa ni uzao wa Adamu. Kwa hiyo kila mmoja ana dhambi, na hakuna anayeweza kukutana na Mungu pasipo sadaka ya kuteketezwa. Hii ndio sababu Mungu alisema kuwa ataipokea sadaka ya kuteketezwa ambayo ilizipatanisha dhambi za waisraeli na hivyo Mungu akakutana nao juu ya kiti cha rehema. 
Mungu aliwafanya watu wa Israeli kuitenga siku ya kumi ya mwezi wa saba kuwa ni Siku ya Upatanisho. Mungu alimfanya Kuhani Mkuu kuzipitisha dhambi za mwaka mzima juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuitoa damu hii ya mwanasadaka kwa Mungu. Siku ile ile, dhambi zote za watu wa Israeli ziliondolewa kwa mwaka mzima, na hii ilikuwa kwa sababu katika siku hii, Kuhani Mkuu alitoa sadaka ya dhambi kwa niaba yao. 
 


Utaratibu wa Sadaka ya Kuteketezwa wa Agano la Kale kwa Ajili ya Ukombozi wa Wenye Dhambi Toka Katika Maovu Yao

 
Kama ambavyo Mambo ya Walawi 1:4 inavyosema, “Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake,” dhambi zote za mwenye dhambi zilipitishwa katika mbuzi wa kisingizio kwa kuiweka mikono juu ya kichwa cha mwanasadaka huyu. Mungu anapokea kwa raha aina ya sadaka inayotolewa kwa imani inayoamini kwa kweli katika Neno lake. Hii ilikuwa ni hatua muhimu na ya kwanza katika utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ambao Mungu aliuanzisha kwa watu wa waisraeli. 
Kisha mtu alimchinja koo lake na kuikinga damu na kisha aliwapatia damu hii makuhani. Kisha makuhani waliiweka damu hii katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, kisha wakaiweka nyama yake katika madhabahu na wakaichoma, na kwa jinsi hiyo walimtoa mwanasadaka huyo kwa Mungu kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za mwenye dhambi. Hii ilikuwa ni sheria ya wokovu ambayo Mungu aliipanga ili kuweza kuziondoa dhambi za kila mwenye dhambi. 
Hata hivyo, katika ile Siku ya Upatanisho, siku ya kumi ya mwezi wa saba, Mungu aliwaruhusu watu wake kutoa sadaka ambayo itaziondosha dhambi zao za mwaka mzima. Katika siku ile, Kuhani Mkuu, ambaye ni mwakilishi wa waisraeli wote, alipaswa kuandaa mbuzi wawili. “Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura nyingine kwa ajili ya azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya BWANA, na kumtoa awe sadaka ya dhambi” (Mambo ya Walawi 16:8-9). Haruni alipaswa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa kwanza ili kwamba dhambi za mwaka mzima za waisraeli ziweze kuhamia kwa mwanasadaka huyu. Kisha aliikinga damu yake kwa kumchinja, akaenda katika Patakatifu pa Patakatifu, na kisha aliinyunyuzia ile damu mara saba kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande ule wa mashariki, na pia alinyunyizia hiyo damu mbele ya kiti hicho mara saba. Kwa kuipokea damu hii ya sadaka ya kuteketezwa, Mungu alizioshelea mbali dhambi zao zote na akawathibitisha kuwa watu wake wenyewe. 
Baada ya hili, Kuhani Mkuu alitoka nje ya Hema Takatifu la Kukutania, kisha akamtoa yule mbuzi mwingine mbele ya watu wa Israeli. Ili kuzipitisha kabisa dhambi za watu wake, ilimpasa Kuhani Mkuu kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka wa kuteketezwa. Kisha alikiri, “Ninazipitisha dhambi zote ambazo watu wangu wamezifanya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita juu ya mwanasadaka huyu.” Baada ya jambo hili, Kuhani Mkuu alimpeleka yule mwanasadaka jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 
Mbuzi huyu alipaswa kupelekwa mbali katika nyika za kavu ili aweze kufa (Mambo ya Walawi 16:20-22). Hii inatujulisha kuwa dhambi za watu wa Israeli ziliondolewa zote mara moja na kwa ajili ya wote kwa ile sadaka ya dhambi ambayo ilitolewa katika Siku ya Upatanisho. 
Mbuzi hawa wa kisingizio walionyesha kivuli cha Yesu. Sadaka hii ya dhambi inaudhihirisha ukweli wa wokovu ambao Yesu Kristo ameukamilisha kwa kubatizwa na Yohana na kwa kusulubiwa ili kuzitoweshea mbali dhambi za kila mtu ulimwenguni. Mungu aliahidi kukutana na watu wa Israeli juu ya kiti cha rehema pale walipotoa sadaka ya kisheria kwa kupitia Kuhani Mkuu. Watu wa Israeli walimchukulia Kuhani Mkuu na kiti cha rehema kuwa ni vitu vya thamani, kwa kuwa alikuwa ni Kuhani Mkuu ambaye ndiye aliyeitoa sadaka ya dhambi kila mwaka kwa niaba yao, na kwamba ni pale katika kiti cha rehema ambapo maovu yao yalisamehewa. 
Vivyo hivyo, Yesu alitupatanisha sisi na Mungu, baada ya kuitoa sadaka moja ya mwili wake kwa ajili ya dhambi zetu milele kwa kupitia ubatizo na damu yake iliyomwagika. Hii ndio sababu hatuwezi kutoa shukrani za kutosha kwa Bwana Yesu, na hii pia ndio sababu inayotufanya sisi tuamini katika ubatizo wake pamoja na kusulubiwa kwake. 
 

Kiti cha Rehema Kilizifunika Mbao Mbili za Mawe za Amri Kumi Ambazo Ziliwekwa Ndani ya Sanduku la Ushuhuda.
 
Katika Mlima Sinai, Mungu alimwamuru Musa kuziweka zile mbao mbili zilizokuwa zimeandikwa zile Amri Kumi ndani ya Sanduku la Ushuhuda na kisha kulifunika Sanduku hilo kwa kiti cha rehema. Mungu alifanya hivyo kwa sababu alipenda kulitoa pendo lake la rehema kwa watu wa Israeli, kwa kuwa walishindwa kuifuata Sheria. Kwa meneno mengine, ni kwa sababu Mungu hakuweza kujishughulisha na watu wa Israeli ambao walikuwa wakitenda dhambi kila siku hali wakiwa na Sheria yake ya haki ambayo ilitangaza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Hili pia lililenga katika kuwapatia ondoleo la dhambi watu wa Israeli. 
Kwa maneno mengine, watu wa Israeli walikuwa na mapungufu mbele za Mungu ya kuitunza na kuifuata Sheria kwa matendo yao. Kwa hiyo Mungu aliwapatia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa pamoja na Sheria. Hii ilikuwa ni kuwafanya waweze kusafishwa dhambi zao kwa kupitia sadaka ya kuteketezwa. Hii inatuonyesha kuwa ili kuzitoweshea mbali dhambi za watu wa Israeli, Mungu aliwataka kuzipitisha dhambi zao katika sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kumchinja kwa niaba yao. Mungu alitoa sheria ya upendo wake wa wokovu sambamba na sheria ya hasira yake ya haki kwa watu wa Israeli. Kwa hiyo, sisi pia tunahitaji kuamini katika sehemu mbili za ukweli wa wokovu wa Mungu; ubatizo ambao Masihi aliupokea toka kwa Yohana na damu ambayo Yesu aliimwaga Msalabani. 
Mnyama wa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi katika Agano la Kale ulikuwa ni mwili wa Masihi katika Agano Jipya. Sadaka ya kuteketezwa ambayo sisi tulipewa katika Maandiko ulikuwa ni upendo wa Mungu wa rehema ambao unazitoweshea mbali dhambi zetu zote. Sasa, kama mwanzo, ili tuweze kuondolewa dhambi zetu, kwa hakika tunahitaji sadaka ya kuteketezwa ya upatanisho. Tangu zamani, ili kuwepo na kule kuziondolea mbali dhambi za wanadamu ni lazima kuwepo na haki ya Mungu na upendo wake wa rehema. 
Kwa sababu haki ya Mungu ni lazima ituhukumu ikiwa tuna dhambi, basi tulipaswa kuzioshelea mbali dhambi zetu kwa kuzipitisha dhambi hizo katika sadaka ya dhambi. Kama ambavyo msemo mmoja hapa Korea unavyosema, “Ichukie dhambi, lakini usiwachukie wenye dhambi,” Mungu alizichukia dhambi zetu lakini hakuzichukia nafsi zetu. Kwa kuwa ili Mungu aweze kuzitoweshea mbali dhambi za nafsi zetu, tulipaswa kuiweka mikono yetu juu ya sadaka ya kuteketezwa, kuikinga damu yake na kisha kumpatia Mungu. Kule kusema kuwa Mungu amezipatanisha dhambi za watu wa Israeli katika Agano la Kale kunamaanisha kuwa Mungu alizipokea sadaka zao za kuteketezwa na hivyo aliziondoa dhambi zao. 
Mtengenezaji wa Sheria kwa watu wa Israeli alikuwa ni Mungu mwenyewe. Yehova, ambaye alijifunua yeye mwenyewe mbele za watu wa Israeli, ndiye ambaye anaishi kwa uwezo wake mwenyewe. Kama ambavyo tunamtambua Mungu kuwa ndiye msajiri wa Sheria, ni lazima tutambue kuwa yeye ni Mungu wetu sote na kisha tuupokee utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ambao aliupanga ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu. Kwa kupitia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa ambao Mungu aliuanzisha, tunaweza kutambua jinsi ambavyo Mungu alitupenda na jinsi ambavyo Mungu ametukomboa kwa haki toka katika dhambi zetu. Na kwa kupitia Sheria ya Mungu, sisi pia tunaweza kutambua jinsi ambavyo hatuwezi kuzifuata amri zake. Kwa misingi yetu binafsi, sisi tulikuwa wenye kuabudu miungu mbele za Mungu, hali tukifanya kila aina ya uovu na makosa. Kwa hiyo, hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kukubali kuwa tulifungwa kuzimu kwa ajili ya dhambi zetu wakati wote. Hii ndiyo sababu Mungu mwenyewe alikuja kwetu kama Mwokozi wetu. 
Yesu Kristo aliutoa mwili wake kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu milele. Yesu alijitoa yeye mwenyewe katika njia ambayo ni sawa kabisa na ile iliyotumika katika sadaka ya dhambi katika Agano la Kale, hasa ule utaratibu unaoonyeshwa katika Siku ya Upatanisho: kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mwanasadaka na kuimwaga damu. Mbao mbili za mawe katika Sanduku la Ushuhuda na kiti cha rehema vilikuwa ni vitu muhimu sana kwa watu wa Israeli ili waweze kupokea ondoleo la dhambi, kwa kuwa Mungu aliwawezesha wale walioamini katika Sheria ya haki ya Mungu na ahadi zake za maisha kupokea maisha mapya. Siku hizi, Sheria ambayo inaonyesha haki ya Mungu na Neno la kweli ambalo linaleta wokovu wa milele toka katika dhambi haliwawezeshi watu wa Israeli tu bali pia na sisi sote ili tuweze kuonana na Mungu na kupokea uzima wa milele. 
Wewe na mimi ambao tunaishi katika nyakati hizi ni lazima tufahamu na kuamini kuwa Mungu wetu ni nani, na kwamba anatuambia nini, na kwa kupitia kitu gani ametufanya sisi kupokea ondoleo la dhambi zetu. Kwa kupitia ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizodhihirishwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania katika Agano la Kale, Mungu amekuita wewe na mimi, ametupokea sisi, na ametupatia imani inayoamini katika hili. 
 


Nyuzi za Bluu Zinamaanisha Hasahasa Ubatizo Ambao Yesu Aliupokea

 
Hebu tugeukie Mathayo 3:13-17: “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, ‘Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’” 
Kwa kupitia sadaka zilizotolewa chini ya utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa katika Agano la Kale, kwa kweli Mungu Baba alionyesha kuwa atazipitisha dhambi zote za ulimwengu kwa Mwana wake pekee Yesu Kristo. Kwa kweli Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kuitimiza haki yote ya Mungu. Kwa kuwa dhambi za ulimwengu zilipitishwa kwa hakika kwa Yesu pale alipobatizwa na Yohana, basi wale wote wanaoamini hivi wataondolewa dhambi zao zote katika mioyo yao. 
Ubatizo huu ambao Yesu aliupokea kwa kweli una maana nyingine tofauti toka katika ubatizo wa maji ambao watu wanaupokea kama taratibu ya kiimani ili watu waweze kuwa Wakristo. Kwa maneno mengine, ubatizo wa maji ambao watu wa siku hizi wanaupokea kwa kweli ni ishara ya nje ya kuongokea dini ya Kikristo. Yesu alibatizwa katika Mto Yordani ili kuzichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa kuwekewa mikono na Yohana Mbatizaji, ambaye ni mwakilishi wa wanadamu. Ubatizo ambao Yesu aliupokea ulikuwa ni ubatizo ambao ulitimiza ahadi ya Mungu ya wokovu wa milele, ahadi ya ondoleo la dhambi ambayo Mungu aliianzisha kwa kupitia utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi. Upendo wa Mungu kwa wanadamu na ondoleo kamilifu la dhambi linatokana na ukweli kuwa Yesu alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa yeye mwenyewe na kwa kuimwaga damu yake Msalabani hadi kifo ili kulipa mshahara wa dhambi hizi. 
Mungu Baba alimfanya Mwanae kubatizwa na Yohana ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zote za ulimwengu. “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” (Mathayo 3:15). Neno “Kwa kuwa” lina maanisha kuwa Yesu atazichukua katika mwili wake dhambi zote za wanadamu katika ulimwengu kwa kubatizwa. Kwa sababu Yohana alimbatiza Yesu Kristo, basi dhambi zetu zote zilipitishwa kwenda kwa Yesu. Kwa kuwa Yesu Kristo alikuwa amezichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake basi ndio maana aliimwaga damu yake na kufa kwa niaba yetu. Ubatizo ambao Yesu aliupokea ni upendo wa Mungu wa sadaka ya kuteketezwa na ondoleo la dhambi. Baada ya kuwa Yesu amezipokea dhambi zetu zote zilizokuwa zimepitishwa kwake, alizama katika maji. Kule kuzama katika maji kunamaanisha juu ya kifo chake. Na kule kutoka nje ya maji kunashuhudia juu ya kufufuka kwake mapema kabla ya ufufuo huo. 
 


Yesu ni Muumbaji na Mwokozi Wetu

 
Ni kweli kuwa Yesu Kristo aliyekuja kwetu ni Mungu mwenyewe aliyeuumba ulimwengu wote na vitu vyote vilivyomo ndani yake. Mwanzo 1:1 inasema, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi,” na Mwanzo 1:3 inasema, “Mungu akasema, ‘Iwe nuru’; ikawa nuru.” Yohana 1:3 pia inasema, “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.” Kwa kweli Yesu Kristo aliuumba ulimwengu wote akiwa na Baba na Roho Mtakatifu. 
Wafilipi 2:5-8 inasema, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.” Yesu ni Muumbaji halisi aliyeuumba ulimwengu huu na kutuumba sisi wanadamu. Ili kutuokoa sisi toka katika dhambi, Huyu Bwana mwenyewe alikuja kwetu kama mwanadamu, akazichukua dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana, akamwaga damu yake kwa sababu ya ubatizo huu, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu zote. 
Kwa kweli Masihi aliwafanya waisraeli kuifanya milango yote ya Hema Takatifu la Kukutania kwa kuifuma kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kule kuona kuwa Mungu aliwafanya waisraeli kutumia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kwa ajili ya milango ya Hema Takatifu la Kukutania kunadhihirisha ile nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote toka katika dhambi zao: kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo ambao Yesu ataupokea toka kwa Yohana na kisha kulipa mshahara wa dhambi hizo kwa damu yake Msalabani. 
Katika Agano la Kale, wenye dhambi walizileta sadaka zao za kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania na kisha walizipitisha dhambi zao juu ya sadaka hizo kwa kuiweka mikono yao juu ya vichwa vya wanasadaka hao mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Kisha mhusika aliikinga damu baada ya kuwa amemchinja mwanasadaka huyo na kisha aliipeleka damu hii kwa makuhani. Kisha makuhani waliitoa sadaka hii kwa Mungu kwa kuiweka damu juu ya zile pembe nne za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kisha kuimwaga damu iliyokuwa imesalia katika ardhi. 
Katika Siku ya Upatanisho, wakati Kuhani Mkuu alipoichukua damu ya mwanasadaka wa kuteketezwa ambaye alikuwa ameweka mikono yake juu yake na kisha kuingia nayo katika Patakatifu pa Patakatifu na kuinyunyizia ile damu katika kiti cha rehema, basi Mungu aliipokea damu hii ya mwanasadaka wa kuteketezwa kuwa ni hukumu ya haki juu ya watu wake. Kwa nini mnyama wa sadaka ya kuteketezwa alipaswa kuuawa? Ni kwa sababu mnyama huyo alikuwa amezichukua dhambi zote za waisraeli kwa kule kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu katika kichwa chake. Kwa maneno mengine, damu yake ilikuwa ni matokeo ya huku kuwekewa mikono. Kwa hiyo, Mungu aliipokea damu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha alinusa harufu nzuri ya kule kuchomwa kwa yule mwanasadaka juu ya madhabahu na kwa hiyo aliziondoa dhambi zote za watu wa Israeli. 
Katika kipindi cha Agano Jipya, Yesu alikuja kufanya kitu kama hikihiki. Ili kuzichukua dhambi zetu na kubeba adhabu ya dhambi hizi, ilimpasa Bwana wetu kuja hapa duniani kwa kupitia mwili wa Bikira Mariam, na akaukamilisha wokovu kwa kubatizwa na Yohana na kuimwaga damu yake Msalabani. Kwa kweli nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni injili inayodhihirisha ukweli kuwa Yesu, ambaye ni Mungu mwenyewe, alibatizwa na kisha kusulubiwa. 
Yesu ameketi katika mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu kwa sababu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake na kusulubiwa, kumwaga damu yake, kufa, na kisha kufufuka baada ya siku tatu, na hivyo amefanyika kuwa Mwokozi kwetu sisi tunaoamini. Yesu Kristo amewawezesha wale ambao wanamwamini yeye kuwa ni Mwokozi kumwita Mungu Abba, yaani Baba kwa kuondolewa dhambi zao zote mara moja na kwa ajili ya wote mbele ya Mungu Baba. Haya ni mafumbo ya ukweli uliofichika katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Kwa kupitia ubatizo na damu ya Msalaba, Masihi alitimiza kusafishwa kwa dhambi zetu na akabeba adhabu ya dhambi zetu badala yetu. Sasa, Yesu amefanyika kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Kwa hiyo, ni lazima tuamini kuwa mlango wa Hema Takatifu la Kukutania katika Agano la Kale uliundwa kwa kuzifuma nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na pia ni lazima tuamini kuwa katika Agano Jipya, Masihi Mwokozi wetu alikuja hapa duniani, akazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake, kisha akabeba adhabu ya dhambi hizo zote pale Msalabani—Kwa hiyo ni lazima tupokee ondoleo la dhambi zetu zote. 
 

Sisi Kama Wakristo, Tunalizingatia Kiasi Gani Neno Lake?
 
Kutoka 25:22 inasema, “Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya Sanduku la Ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.” Basi wewe upo karibu kiasi gani na injili ya maji na Roho, injili ya upatanisho? Ni wapi ambapo Mungu alisema atazungumza na wale ambao mnamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi? Katika Kutoka 25:22, Mungu alisema kuwa atakupatia amri zake zote toka juu ya mfuniko wa Sanduku la Ushuhuda. Mungu alisema kwa watu wa Israeli katika Agano la Kale kuwa atazungumza nao kuhusu kila kitu toka katika kiti cha rehema. 
Unapaswa kutambua kuwa hii ni ahadi ya Mungu kwamba atayaongoza maisha yenu baada ya kuwapatia ondoleo la dhambi kwa kupitia sadaka ya kuteketezwa ya kisheria na kuwafanya ninyi kuwa watu wake. Mungu anatueleza sisi kuwa haijalishi ni kwa kiasi gani wale wanaoamini katika Ukristo wakijaribu kuongozwa na Bwana, ikiwa unamwamini Yesu wakati bado huufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho, basi Mungu hawezi kukuongoza wewe. Kwa hiyo, ikiwa kweli unapenda kuongozwa na Bwana, basi ni lazima kwanza uufahamu na kuupokea ukweli wa ondoleo la dhambi ambao umeziondolea mbali dhambi zako zote mara moja na kisha endelea kusubiri mwongozo wa Mungu. 
Kuna kitu kimoja ambacho ninapenda kukueleza, na kitu hicho ni hiki, ikiwa unapenda kuwa mtoto wa Mungu, na ikiwa unapenda kuwa sehemu ya Kanisa lake, basi ni lazima kwanza uondolewe dhambi zako kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, ambalo ni fumbo la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Ni baada ya kufanya hivi tu ndipo unapoweza kupokea maagizo na amri za Bwana zikiongelewa kwako toka juu ya Sanduku la Ushuhuda. 
Ni lazima tukumbuke na kuamini kwamba kwa hakika Bwana ameyaamuru na kuyaongoza maisha yetu pale tunapokuwa na imani katika injili ya maji na Roho ambayo imetuwezesha sisi kupokea ondoleo la dhambi. Je, unapokea sasa amri na maagizo ya Bwana yanayoletwa kwako toka katika kiti cha rehema? Au unamfuata Bwana hali ukizitegemea hisia zako mwenyewe? 
Hisia zako na mihemko yako binafsi haiwezi kuijenga imani yako, bali mambo hayo yatakuongoza kwenda katika shida. Ikiwa unatafuta kufuata amri za Mungu zikizungumzwa kwako toka juu ya Sanduku la Ushuhuda, basi ni lazima utambue na kuamini kwamba nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizozungumziwa katika Hema Takatifu la Kukutania ni ondoleo la dhambi ambalo Mungu ametupatia. 
Halleluya! Ninamshukuru Mungu kwa ubatizo wa Bwana, damu ya Msalaba, na nguvu zake na upendo ambavyo vimetuokoa sisi toka katika dhambi zote za ulimwengu.