Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 10-1] Utangulizi Kwa Sura ya 10

Je, kuna watu ambao wanaifuata haki yao wenyewe huku wakiwa wanaiamini injili ya maji na Roho? Maandiko yanasema kuwa watu wa jinsi hiyo wasioiamini haki ya Mungu na badala yake wanaifuata haki yao wenyewe wanasimama kinyume na Mungu. Watu hawa watafanya nini? 
Je, Mungu alipanga kuwapatia wanadamu wote wokovu wake, ambayo ni haki ya Mungu na kumtuma Yesu Kristo kwa kupitia Waisraeli? Kwa kweli Mungu alifanya hivyo! Kwa mapenzi mema Yesu alitaka kumwokoa kila mwenye dhambi toka katika dhambi zake ndio maana alikuja hapa duniani, alisulubiwa Msalabani, na akafufuka toka kwa wafu. Kwa maneno mengine, alikuja kuwaokoa wote wanaomwamini Yeye. 
Mungu Baba alimtuma Yesu Kristo kwa Waisraeli ili kuwaokoa toka katika dhambi zao, lakini Waisraeli hawakumpokea Yesu ambaye ni haki ya Mungu. Badala yake waligubikwa na kuifuata haki yao wenyewe. Hata sasa bado hawajaweza kumpokea Yesu kuwa ni Masihi wa watu wao na Mwokozi wa nafsi zao. 
Paulo alisema kuwa kuna wale ambao wanatumwa na Mungu na kwamba kwa kupitia hao injili nzuri inaweza kusikika. Injili iliyotumwa toka kwa watumishi wa Mungu waliokuwa wametumwa na Mungu ni injili ambayo ina haki ya Mungu. Hupaswi kuikosa nafasi hii. Kwa kuisikia na kuiamini injili ya maji na Roho ambayo inahubiriwa na watumishi wa Mungu ambao wana haki ya Mungu, ndipo unapoweza kuamini kuwa Mungu amekupatia ondoleo la dhambi zako zote na kukupatia haki yake. 
Injili ya maji na Roho ni habari njema kuliko zote ulimwenguni. Hii habari njema ambayo ni nzuri kuliko zote ndiyo iliyowaokoa wenye dhambi toka katika dhambi zao. Habari hii njema inazijaza kwa upya nafsi za watu kwa kuwa injili ya maji na Roho ni chakula cha kweli kwa nafsi. 
Katika injili nzuri ya ukombozi iliyotolewa na Mungu kuna nguvu ya kusamehe dhambi za kila mtu. Injili ya maji na Roho ina nguvu ya baraka ya kutupatia amani katika akili zetu kwa ondoleo la dhambi zetu. 
Hali wakiwa wemejikita katika sheria ya Mungu, Waisraeli walikuwa wametingwa hali wakiendelea kuifauta haki yao binafsi. Kwa sababu walifikiria kuwa haki yao binafsi ilikuwa ikiendana na vizuri na kule kuitii sheria, na kwa sababu hiyo hawakumpokea Yesu kuwa Mwokozi wao. Walikuwa makini katika kuyafuta matendo ya sheria na kwa sababu hiyo hawakuweza hata kuivumilia haki ya Mungu. Walishindwa kumpokea Bwana kuwa ni Mwokozi wao hadi sasa huku wakiendelea kuifuata haki ya wenyewe. 
Je, Maandiko yanatueleza kuwa Waisraeli waligeuka na kuwa kinyume na haki ya Mungu ili kuziimarisha haki zao wenyewe? Hali akizungumzia Waisraeli ambao walikuwa wametekwa na sheria, Paulo aliikemea imani yao kwa kusema, “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki” (Warumi 10:4). 
Imani ya kisheria inayoifuata haki ya mtu binafsi si imani sahihi mbele za Mungu. Wakati Waisraeli wakiwa wametingwa na kuzifuata sheria za Agano la Kale, walishindwa kutambua kuwa Yesu, ambaye alifanyika kuwa haki ya Mungu alikuwa ni Mwokozi wao na badala yake wakageuka na kuwa kinyume naye. Katika tamaa yao ya kujivunia kuwa wao walikuwa ni watu walioteuliwa na ambao walipewa Neno la Mungu ili walifuate, basi Waisraeli walijikuta wakiishia kuwa ni taifa ambalo lilisimama kinyume na haki ya Mungu. 
 

Je, Umeshikilia Kule Kuiimarisha Haki Yako Mwenyewe? 
 
Tatizo la wivu wa Waisraeli kwa sheria ulitokana na ukweli kuwa nia yao ilikuwa ni kuiimarisha haki yao binafsi. Kwa sababu ya haki yao binafsi, haki ya Mungu iliyoanzishwa na Bwana wetu ilidharauliwa kabisa. 
Matokeo ya imani ya kisheria ya Waisraeli iliishia katika kuwafanya wao kuwa kinyume na haki ya Mungu; na kwa hiyo bado hawajayatambua madhara makubwa yanayotokana na matokeo haya. Je, walipata faida gani kwa kuendelea kuyashikilia matendo ya sheria? Hamu yao ya kulifuata Neno la Mungu iliishia kuwa kama kizuizi kilichowazuia kuifahamu na kuiamini haki ya Mungu. Kwa mara nyingine tena, ni lazima tutambue kuwa “hamu” ya wale wasio na ufahamu sahihi wa sheria itawaongoza wao kugeuka na hatimaye kuwa kinyume na haki ya Mungu. 
Maandiko yanatueleza wazi kuwa Yesu amefanyika kuwa mwisho wa sheria kwa kila mwenye haki anayeamini. Bwana wetu aliitimiza haki ya Mungu kwa kuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake na damu yake aliyoimwaga Msalabani ili kuziosha dhambi za Wayahudi na Wamataifa. Kwa hiyo, injili ya maji na Roho iliyo na haki ya Mungu na si sheria, imefanywa kuwa kama Oasisi katika jangwa kwa ajili ya wenye dhambi. Injili ya maji na Roho ndiyo iliyozitoweshea mbali dhambi zetu na kutupatia kibali ya kweli. Je, ni wapi tena ambapo wenye dhambi wangeliweza kupata kibali cha kweli katika mioyo yao zaidi ya injili ya maji na Roho? 
Katika kitabu cha Warumi, Paulo anatueleza kuwa kuiimarisha haki ya mtu binafsi pasipo kuamini katika haki ya Mungu ni dhambi ya kifo. Ni aina ipi ya injili ambayo ingelikuwa ni injili nzuri kwetu sisi wamataifa? Ni injili ambayo imetueleza kuwa Bwana wetu Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake. 
Injili hii ni injili iliyoandikwa katika Mathayo 3:13-17, ambayo inamshuhudia Yesu akizichukua dhambi za ulimwengu: “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Hivi ndivyo Yesu alivyozichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake toka kwa Yohana. 
Paulo aliwakemea watu wa kisheria ambao walikuwa hawaiamini haki ya Mungu kwa kuwauliza, “Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani ni kumleta Kristo chini).” Kwa lugha nyingine, swali hili linauliza hivi, “Ni nani anayeweza kuokolewa kwa kuifuata sheria tu?” Dhumuni la swali la Paulo ilikuwa ni kuipigia mstari hoja kuwa kuifuata sheria hakutaweza kuleta wokovu toka katika dhambi. Kwa maneno mengine, Paulo anatueleza kuwa hakuna tunachoweza kukifanya ili kujiondoa sisi wenyewe toka katika dhambi. 
Mara nyingi Paulo alizungumzia juu ya haki ya Mungu katika nyaraka zake. Jibu la Paulo kuhusiana na imani ya kweli linapatikana katika Warumi 10:10 ambapo anasema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Injili iliyohubiriwa na Paulo ilikuwa ni injili inayotueleza kuwa tunaipokea haki ya Mungu kwa kuuamini ubatizo wa Bwana wetu na damu yake Msalabani ambayo kwa hiyo haki ya Mungu imefunuliwa. Ni lazima tuamini kuwa Bwana alitupatia injili ya maji na Roho na kwamba aliwaruhusu wale wote wanaoamini katika injili hii kuwa amani ya akili. 
 

Imani ya Kweli Huja Kwa Kulisikia Neno la Mungu 
 
Je, Paulo anatueleza nini kuhusu imani ya kweli? Warumi 10:17 inasema, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Kwa maneno mengine, imani ya kweli inakuja tunapoisikia injili ambayo watumishi wa Mungu wanaihubiri. 
Uhakika wetu wa imani ya kweli unakuka kwa kulisikia Neno la Mungu, na kwa hiyo ili kuwa watu wa imani ya kweli, ni lazima tulisikie na kuliamini Neno lake. Tunaweza kuwa na imani ya kweli na inayokua kwa kulisikia Neno la Mungu tu. Hii ndiyo sababu Mungu ametutumia watumishi wake ambao wanaihubiri haki yake. 
Tunapoamini katika injili ya maji na Roho waliyopewa wanadamu na Mungu, basi tunaweza kupokea ondoleo la dhambi na kisha tukapumzika katika mioyo yetu. Ukombozi toka katika dhambi unawezakana kwa kuamini katika haki ya Mungu tu ambamo twaweza kupata amani katika akili zetu. 
Je, hatujaambiwa kuwa haki ya Bwana wetu itayafuta machozi yetu na kutukomboa toka katika maumivu yetu yote? Kwa kweli tumeambiwa hivyo. Maumivu yetu yote yanaweza kuchukuliwa mbali kwa kuamini katika haki ya injili ya maji na Roho iliyotolewa na Mungu. Injili ya maji na Roho ndiyo habari njema zaidi katika ulimwengu huu na ndio utimilifu wa haki ya Mungu. 
Mungu alimtuma Bwana wetu aliyeitimiza haki yake kwa Waisraeli, lakini kwa sababu ya kuifuata haki yao binafsi walikataa kumgeukia Bwana. Sasa, Mungu alifanya nini? Ili kuwafanya Waisraeli kuwa na wivu, Mungu aliitoa injili hiyo kwa Wamataifa ili waamini. Kwa hiyo Mungu aliwaruhusu kwa kuwapa nafasi Wamataifa kuamini katika injili ya maji na Roho? Ndivyo ilivyo, Mungu aliwapatia Wamataifa nafasi ya kuamini katika injili ya maji na Roho hata pale ambapo hawakumtafuta, hawakumwita, na hata pale ambapo waliabudu mbali kabisa na Wasraeli. 
Hii ndiyo sababu Wamataifa waliweza kufanyika watoto wa Mungu kwa kuamini katika habari nzuri za utimilifu wa haki ya Mungu. Hii ndiyo sababu maandiko yanatueleza kuwa haki ya Mungu iliheshimiwa na kutukuzwa nje ya Israeli. 
Ni watu wangapi ambao wanamshukuru Bwana kwa kutupatia sisi sote injili ya majina Roho ambayo imeitimiza haki ya Mungu? Bwana wetu amezichukulia mbali dhambi zote za ulimwengu kwa injili nzuri ya maji na Roho. Lakini bado kuna Wakristo wengi ambao hawauamini ukweli huu. Je, kwa hiyo tuna haki yoyote ndani yetu ambayo tunaweza kuiweka mbele za Mungu? Hapana, hatuna! Kama ni hivyo, kwa nini hatuamini? Ni kwa sababu hatuifahamu ile injili ambayo imbayo imeitimiza haki ya Mungu jinsi ilivyo? Lakini kuifahamu injili hii ni rahisi! 
Sisi pia ni aina ya watu ambao tungeliifuata haki yetu wenyewe kama Waisraeli walivyofanya, lakini Mungu alituokoa toka katika dhambi zetu zote kwa kutupatia injili nzuri ya maji na Roho. Tunamshukuru Bwana kwa kutupatia injili ya maji na Roho, ambayo ni utimilifu wa haki ya Mungu ili tuweze kuiamini. 
 

Usiseme, Ni Nani Atakayepanda Kwenda Mbinguni?” 
 
Aya ya 6 inasema, Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, “Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani ni kumleta Kristo chini).” Ukombozi wetu na kuitumikia injili ya kweli kunawezekana kwa imani yetu katika injili ya maji na Roho na si kwa matendo. Kama isingekuwa ni kwa imani yetu katika ukweli ulioitimiza haki ya Mungu, basi sisi tungelikuwa si chochote zaidi ya kuwa wenye dhambi kama wale watu wa kisheria ambao wanaifuata haki yao wenyewe. 
Kama ambavyo wokovu wetu ulivyokuja kwa kuamini katika haki ya Mungu, basi tunaweza kuishi kwa ajili ya Bwana wetu kwa kuwa na imani katika haki hii. Ile nguvu ya kuendelea katika maisha yetu inatokana na imani yetu katika haki ya Mungu kwa kuwa ufahamu wetu katika haki hii unaamshwa na imani yetu katika injili ya maji na Roho. 
Kwa wale ambao wanaotaka kukombolewa, je, kuna ukweli wowote zaidi ya imani katika haki ya Mungu? Kwa kweli hakuna ukweli wowote. Umaana wa Ukristo umejengwa katika imani, na kwa hiyo hakuna kutia chumvi kuwa haki ya Mungu inahusu imani nzima ya Ukristo. Wale ambao wamehesabiwa haki wanaweza kuishi na kuihubiri injili kwa imani yao katika haki hii ya Mungu. Je, wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanakutana na matatizo pia? Ndio wanakutana nayo pia. Lakini waamini hao wanaweza kuyashinda matatizo yote kwa imani katika haki ya Mungu kwa kuwa kadri wanavyoamini Mungu basi Mungu anaweza kuyashughulikia matatizo yao. Imani ya jinsi hiyo inatoka katika imani inayoiamini haki ya Mungu. 
Je, ni vipi kuhusu imani nyingine ambazo haziihusishi haki ya Mungu? Je, imani hizo zote ni imani potofu ambazo zimejengwa katika msingi wa matendo ya mwanadamu? Kwa kweli zote ni potofu. Imani za wale wanaoamini katika Yesu pasipo kuamini katika haki ya Mungu si imani za kweli. 
Je, mimi na wewe tunaweza kukombolewa toka katika dhambi zetu pasipo kuamini katika haki ya Mungu? Je, tunaweza kuishi kwa imani yetu katika Mungu pasipokuwa na imani katika haki yake? Haiwezekani. Nguvu ya wenye haki ya kumtumikia Bwana inakuja kutokana na nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo imetolewa kwao kama karama kwa imani yao katika haki ya Mungu. Je, unaweza kuishi katika ulimwengu huu kwa nguvu zako binafsi au kwa mali zako za hapa duniani? Je, unaweza kweli kupata amani ya akili kwa mambo haya? 
Tunaweza kuitumikia injili katika amani kwa kuamini katika haki ya Mungu. Wale wanaoitumikia injili ya maji na Roho wana imani, ujasiri, nguvu, na amani. Wenye haki ambao hawaitumikii injili ya maji na Roho, ambayo ni utimilifu wa haki ya Mungu, hawana amani wala ujasiri. Je, akili za mwenye haki zinahitaji amani? Ni kweli zinahitaji. Akili zao zinahitaji amani si tu kwa ajili ya kuieneza injili ya maji na Roho bali pia ni kwa ajili ya kuyaishi maisha yao kwa ukamilifu. 
Je, akili zako zina amani? Ikiwa ungelikuwa unaishi kwa ajili yako mwenyewe, basi kungekuwa hakuna sababu ya wewe kuwa na amani katika akili zako ili uweze kukua. Kwa nini uhitaji amani zaidi wakati unahitaji kuyatimiza mahitaji ya mwili ili uishi katika mwili? Lakini ikiwa utamtumikia Mungu, basi amani katika akili zako inahitaji kukua. Ili uweze kuitumikia injili ya maji na Roho ambayo imeitimiza haki ya Mungu basi imani yako na akili zako ni lazima zikue. 
Wale wanaoamini katika injili ya haki ya Mungu wanawajibika kuieneza amani yao katika ulimwengu mzima. Kwa kuwa hili si jambo la mtu binafsi, bali ni hitaji la kuieneza amani ya akili iliyotolewa na Yesu Kristo kwa kila mtu, hivyo tunahitaji kuihubiri injili ya haki ya Mungu katika ulimwengu mzima. Amani ya Mungu bado inahitajika kwa wengine na kwetu sisi. Tunahitaji maombi zaidi toka kwa Mungu ili tuweze kuieneza amani hii kwa wengine. Tunapokuwa tukiishi kwa kuieneza haki ya Mungu, basi amani ya akili zetu itakua na kisha tutaliona lengo letu la thamani katika maisha yetu. 
Ikiwa unataka kujifunza juu ya amani ya kweli inayotolewa na Mungu, basi unahitaji kuifahamu na kuiamini injili ambayo imeitimiza haki ya Mungu. Unahitaji wewe mwenyewe kupata uzoefu wa amani ya akili ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili yako. 
Kwa kweli umemtumikia Mungu vizuri hata sasa, lakini bado unatakiwa kuendelea kumtumikia yeye vizuri hadi utakapoitwa kwenda katika uwepo wake ili kwamba wengine waweze kuishiriki ile amani yako. Unapoifikia amani kwa imani yako katika haki ya Mungu, basi wale waamini ambao wanazifuata nyayo zako kuelekea katika ukombozi wanaweza pia kuishi kwa amani na watu wengine. 
Wale walio wachanga katika imani yao ni wanafunzi katika mzingo wa imani, na uwezo wao wa kufahamu una mipaka. Lakini tunapoishi kwa imani, basi wale walio nyuma yetu wanaweza kufikia hatua ya kufahamu jinsi waliokombolewa wanavyoishi maisha yao kwa amani kwa kuzifuata nyayo zetu za imani ingawa inaweza kuchukua muda kidogo. 
Je, unaona vigumu kuwafundisha wale wanaoufuata uongozi wako jinsi ya kuishi kwa imani? Maisha hayo ya kufundisha hayawezi kufikiwa kwa usiku mmoja. Unaweza hata kuchukua muda mrefu kabla hujaweza kuwaongoza kwenda katika aina ya imani inayohitajika ili kuishi maisha ya amani. Lakini kwa wakati, wale waliokombolewa kwa kuamini katika haki ya Mungu hatimaye watajifunza kuishi kwa amani kama watu wa imani. Waamini wanaomtumikia Mungu wanaweza kuipata amani ya akili zao toka kwa Mungu kwa kujifunza kwa wale waliowatangulia. 
Wewe na mimi ni lazima tuishi kwa imani katika haki ya Mungu. Wenye haki ni lazima waishi kwa imani katika Neno. Maisha yetu yote yaliyopo na ya baadaye ni lazima yaongozwe na imani. Maandiko yanatuuliza, “Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14) Kwa kuwa tunaamini katika haki ya Mungu, basi ni lazima tuihubiri injili kwa ulimwengu. Tunaweza kupambana na changamoto zote tunazokutana nazo tunapoieneza injili kwa imani. 
Maisha ya wenye haki yasiyoishi kwa kufuata imani ni ya wale waliopoteza amani ya akili. Kuamini katika haki ya Mungu kunawaruhusu watu kuipata amani ya akili zao. Tunapoamini katika Neno la Mungu na haki yake kwa mambo yote basi tutapewa ile amani yetu. 
Ni lazima usimame imara katika amani yako na imani kwa kuamini katika haki ya Mungu. Pia ni lazima umsifu Mungu, kwa kuwa Bwana amekuruhusu kuishi kwa ukombozi wa haki yake na amani. Basi uyaishi maisha yako kwa kuihubiri injili kwa imani katika Mungu ambaye kwa huyo umepokea amani yako. 
Je, tumeweza kujifunza toka katika kitabu cha Warumi jinsi haki ya Mungu ilivyo kamilifu? Warumi inaelezea kwa kina jinsi hii haki ya Mungu ilivyo. Haki ya Mungu ambayo tunaizungumzia si haki iliyoundwa na mwanadamu bali ni ile ya Mungu mwenyewe. 
Haki ya Mungu ni kamilifu na ya kutosha kabisa kutuokoa sote toka katika dhambi zetu. Yesu alizishughulikia dhambi zote kikamilifu kwa kuzichukua dhambi zote za ulimweng kwa kupitia ubatizo wake. Kule kusema kuwa tunaweza kumwamini Yesu Kristo ni kutokana na ukweli kuwa haki ya Mungu ni sahihi na kamilifu. Kwa kuwa haki ya Mungu imetuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu zote, basi ni muhimu sana kwetu kuiamini injili ambayo imeitimiza haki ya Mungu. 
Tunaweza kuishi maisha yetu kwa shukrani na kumsifu Mungu hali tukiiamini haki ya Mungu. Watu wanaweza kuishi katika utakatifu wa Mungu kwa kuamini katika haki yake. Mawazo yetu yanasafishwa kwa kuamini katika haki hii na kwa sababu hiyo tunaweza kumsifu Mungu na kuendelea kuyaishi maisha yetu kwa utukufu wake. 
Kama haki ya Mungu isingelikuwa ni sahihi basi tusingeliweza kukombolewa toka katika dhambi zetu zote. Ingawa dhambi yetu ya asili inaweza kuwa imesamehewa kwa kumwamini Yesu, basi kila dhambi ambayo tungeitenda hapo baadaye kila siku ingelituhitaji kufanya maombi ya toba kila siku. 
Baada ya kuwa tumekombolewa kwa kuamini katika haki ya Mungu iliyofunuliwa katika injili ya maji na Roho, basi tuliweza kutambua kuwa haki hii ya Mungu ni kamilifu. Hii ndiyo sababu ilinibidi kuwa mtu wa shukrani kutokana na ukweli kuwa haki ya Mungu inaweza kuaminika na ni kamilifu hadi milele. Kwa kuwa haki ya Mungu imetukomoboa toka katika dhambi zote ambazo tungeliweza kuzifanya katika kipindi cha maisha yetu, basi tunaweza kuokolewa toka katika dhambi kwa kuiamini haki ya Mungu. 
Wale wasioilinganisha haki ya Mungu na uovu wetu wa kibinadamu hawawezi kuiamini haki ya Mungu kwa sababu hawafahamu jinsi haki hiyo ilivyo kuu. Hata mtu yule ambaye ni mkamilifu sana bado hawezi kulinganishwa na haki ya Mungu, na hii ndio sababu tunaiamini haki ya Mungu na kwa sababu hiyo tunaishi na kukaa katika utakatifu wa Mungu. Kwa maneno mengine, tunafanyika wale ambao tunamtukuza Mungu kwa kuamini na kukaa katika haki yake. 
Tunahitaji kuwa na ufahamu sahihi wa haki ya Mungu katika mioyo yetu, ni lazima tutambue kuwa haki ya Mungu imetokana na dhambi zetu. Je, tunatenda dhambi nyingi katika kipindi cha maisha yetu? Inawezekaneje basi kwa Mungu kulifanya tendo la haki ambalo limetukomboa toka katika dhambi kama hizo zisizohesabika? Mungu aliitimiza haki hiyo kwa kuja hapa duniani katika mfano wa mwili wetu, akazichukua dhambi zote kwa kubatizwa na Yohana, akafa Msalabani, na akafufuka toka kwa wafu hali akiitimiza haki yote ya Mungu. 
Kila mtu awe mtoto au mzee, awe tajiri au maskini, awe na nguvu au dhaifu anatenda dhambi. Ni nani basi aliyetuokoa toka katika dhambi hizo zote za ulimwengu? Ni Yesu Kristo ambaye kwa kuitimiza haki ya Mungu alitukomboa toka katika dhambi zetu zote. Haki ya Mungu ni kule kusema kuwa Mungu alimtuma Yesu ili kuzichukua dhambi zetu zote katika mwili wake na kisha kuziondolea mbali kikamilifu. 
Hakuna kitu kingine zaidi ya hiki kinachoweza kuitwa kuwa ni haki ya Mungu ambayo imetuokoa toka katika dhambi zetu zote. Haki ya Mungu imetukomboa toka katika dhambi zote za ulimwengu mara moja. Je, haki yake si sahihi na kamilifu? Hii haki ya Mungu ndiyo tunayoiita kuwa ni upendo wa Mungu ambao Mungu ametupatia na ambao utadumu milele. 
Kama Yohana Mbatizaji alivyotangaza wakati alipomwona Yesu siku moja baada ya kumbatiza, “Tazama! Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29) Kama Yesu alivyomwambia Yohana baada ya kukataa kumbatiza, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” (Mathayo 3:15). Je, vifungu hivi vina maanisha nini? Vina maanisha wazi kuwa ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani ndio haki yenyewe ya Mungu. Haki ya Mungu haituachi wakati tunapokuwa na udhaifu na kupungukiwa na utukufu wake. 
Tunaweza kumsifu Mungu na kumtukuza yeye kwa ajili ya upendo wake huu mwingi ambao umetuokoa na kuturuhusu kukaa katika haki yake. Wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanafikia hatua ya kuishi katika haki ya Mungu maisha yao yote yaliyosalia. Ni vizuri sana kwetu kumwamini Mungu kuliko kuwaamini wanadamu au ulimwengu. Maisha mazuri ni yale ambayo yanaihubiri injili hii ya ukombozi kamili toka katika dhambi. Hii ndiyo sababu tunapaswa kufahamu na kuiamini kikamilifu haki ya Mungu. 
Wale waliolipokea ondoleo la dhambi wanaweza kushuhudia hivi, “Yesu amezichukulia mbali dhambi zangu zote kwa ubatizo wake toka kwa Yohana! Na kwamba alihukumiwa kwa niaba yangu kwa ajili ya dhambi zote za ulimwengu!” Tunapoiamini haki ya Mungu, basi tunaweza kumshukuru Mungu kwa baraka hizo. 
Unapojikwaa kwa sababu ya udhaifu wako, kisha ukaanguka katika dhambi kwa sababu ya mwili, au wakati unapokatishwa tamaa na kudharirishwa kwa sababu ya dhambi zako, basi itazame haki ya Mungu ambayo imekufanya wewe kuwa mkamilifu. Je, haki ya Mungu si imetufanya na sisi kuwa wenye haki? Je, si kweli kuwa Yesu amezichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake? Je, ukombozi wa Yesu si umetuokoa toka katika dhambi zote zikiwemo zile dhambi ambazo tutazifanya baadaye? 
Ni pale tu tunapoamini kuwa Yesu Kristo ametuokoa kikamilifu basi hapo tunakuwa tukiiamini haki ya Mungu. Ni mpaka pale tunapoiamini haki ya Mungu ndipo tunapoweza kuhesabiwa haki. Wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanaweza kufanyika vyombo vya haki yake. Usahihi wa haki ya Mungu ni mkamilifu. Wale wanaoifuata haki ya binafsi hali wakiwa hawaifahamu haki ya Mungu ni wajinga tu wanaokaa katika uharibifu wao na kulaaniwa na Mungu. 
 

Zingatia Usemi wa Paulo, “Wanajuhudi Kwa Mungu Kwa Ajili ya Mungu Lakini Si Katika Maarifa”
 
Tunaweza kuishi maisha ya imani, tukakombolewa, na kufanyika watu wa Mungu ikiwa hatuifahamu haki yake? Wale wanaoifuata sheria ni lazima watambue kuwa dhambi zao zitawaongoza kwenda katika uharibifu na hivyo wanapaswa kushukuru kuwa haki ya Mungu imewaokoa kikamilifu. Kule kusema kuwa Yesu amefanyika kuwa Mwokozi wetu na kwamba tunamwamini yeye, na kwamba tunamtukuza yeye ni kwa sababu tunaifahamu na kuiamini haki ya Mungu. Ni kwa kuamini katika haki ya Mungu tu ndipo tunapoweza kufanyika watoto wa Mungu wasio na dhambi na kupokea uzima wa milele. Wale wanaokiri kuwa wanamwamini Yesu na kwamba wanaishi maisha ya uaminifu lakini hawaifahamu haki ya Mungu basi inawapasa watambue wazi kuwa watalaaniwa. 
Paulo alitoa ushahidi wake katika Warumi kuwa Waisraeli, hali wakiwa hawaifahamu haki ya Mungu, walizingatia kuiimarisha haki yao binafsi, na kwa kufanya hivyo waliidharau haki ya Mungu. Wao pia inawapasa kuamini katika haki ya Mungu. 
Ni lazima tuamini kuwa Mungu ametukomboa toka katika dhambi za ulimwengu. Dhambi zetu zote zimejumlishwa katika dhambi hizi za ulimwengu. Dhambi zote zimetoweka kwa utimilifu wa haki ya Mungu. Je, unauamini ukweli huu? 
 

“Kwa Maana Kristo ni Mwisho wa Sheria Kwa Kila Aaminiye” 
 
Haki ya Mungu ni mwisho wa sheria. Hii ni kwa sababu Yesu Kristo aliyajibu mahitaji yote ya sheria kwa kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake na kusulubiwa kwake. 
Kwa hakika matokeo ya dhambi ni mauti, lakini imeandikwa kuwa haki ya Mungu ni mwisho wa sheria. Kwa nini? Hii ni kwa sababu Mungu Baba ametuokoa sisi kikamilifu kwa kumtuma Mwanawe pekee kuja hapa duniani ili kubatizwa na kuzichukua dhambi zote za mwanadamu katika mwili wake, kufa Msalabani, na kufufuka toka kwa wafu. 
Kuiamini haki ya Mungu kwa moyo wako wote na kuifuata haki ya sheria ni vitu viwili tofauti kabisa. Je, ulipokea ondoleo la dhambi zako kwa matendo yako? Je, ulipokea wokovu kwa matendo yako mema? Dini zote katika ulimwengu huu zinafundisha kuwa njia ya kushughulikia dhambi zako ni kwa kufanya matendo mema. Kwa mfano, uelewa wa Wabudha juu ya dhambi unafundisha kuwa unaweza kuzikomboa dhambi zako za maisha yako yaliyopita kwa kutenda matendo mema katika wakati uliopo. Je, inaleta maana kwako? 
Mtu anazaliwa mara moja na kufa mara moja na baada ya hapo hukumu itafuata. Kwa kuwa kila mtu anazaliwa katika ulimwengu huu mara moja tu na baada ya hapo anarudi kwa Mungu, basi hakuna mtu anayeweza kurudi tena duniani katika mzunguko mwingine wa maisha. Hii ndio sababu ni lazima watu wakombolewe kwa kuamini katika haki ya Mungu wakiwa hapa duniani. Mafundisho ya kibudha ya karma hayana maana yoyote. 
Kuamini kuwa tumekombolewa toka katika dhambi zetu ni kuamini katika haki ya Mungu. Kuamini katika haki ya Mungu ni kuiamini haki ya Mungu tu na wala si katika matendo yetu. Sasa imani yako katika haki ya Mungu inasema nini? Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Warumi, haki hiyo ya Mungu inasema hivi, “Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni?” Hii ni kwa sababu haki ya Mungu inapatikana kwa kuamini katika moyo wa mtu na si kwa namna ya nguvu za kimwili. 
Tunafanyika watoto wa Mungu na watu wasio na dhambi ambao wanaupokea uzima wa milele kwa kuamini katika haki ya Mungu. Kwa sababu hatuwezi kuzitatua dhambi zetu sisi wenyewe hata kama tukijitahidi kutenda mema kiasi gani, juhudi zetu zinaishia kuwa ni dhambi zaidi mbele za Mungu. Hii ndiyo sababu inatupasa kuziachilia mbali imani za jinsi hiyo na kisha tuamini katika haki ya Mungu na kuifuatia haki yake pekee. Baadhi ya watu wanauliza, “je, hatuwezi kuokolewa kwa kumwamini tu Yesu hata kama hatuifahamu yaki ya Mungu? Je, haijaandikwa kuwa yeyote aliitiaye jina la Bwana ataokoka?” Lakini wokovu hauji kwa kuliitia tu jina la Yesu bali kwa kufahamu na kwa kuamini kikamilifu juu ya haki ya Mungu. 
 

Yeyote Anayeiamini Haki ya Mungu Hana Aibu 
 
Aya ya 11 inasema, “Kila amwaminiye hatatahayarika.” Nini maana ya kifungu hiki? Kila amwaminiye hatatahayarika kwa sababu anaiamini haki ya Mungu. “Kila amwaminiye” maana yake ni mwamini katika haki ya Mungu. 
Vipi kuhusu kifungu hiki, “Yeyote aliitiaye jina la BWANA ataokolewa?” (Warumi 10:13) Kifungu hiki kina maanisha kuwa wale wanaofahamu na kuamini katikainjili ya maji na Roho wanaweza kumwita Yesu kwa kuwa wanamwamini yeye kuwa ni Mungu Mwokozi. Kama tulivyoupokea wokovu wetu kwa kupitia haki ya Mungu, basi tunaamini kuwa ukombozi wetu unapatikana kwa kuamini katika ukweli huu. 
Kwa maneno mengine, pasipo kuwa na imani hii, hata kama tunaliitia jina la Yesu mara nyingi hatutaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu. Kwa kuwa Maandiko kwa ujumla yanazungumzia juu ya haki ya Mungu katika Yesu, hivyo kuliitia jina la Bwana tu hakuwezi kutupatia ukombozi wetu. 
Tangu mwanzo Biblia inatueleza sisi kuhusu haki ya Mungu. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Mwanzo, Mungu aliuweka mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya katika Bustani ya Edeni, na akamwambia Adamu na Hawa kuwa wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Alichokuwa akikitaka ni Mungu ni ile imani yao katika Neno la Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu aliwaambia wale matunda ya mti wa uzima ili waweze kupata uzima wa milele. 
Neno la Mungu linasema, “Mwenye haki wangu ataishi kwa imani.” Sisi pia tunaishi kwa imani katika haki ya Mungu katika maisha yetu yote—tangu tulipoanza kumwamini yeye ili kuokolewa, hadi tulilipokea wokovu wetu, na hatimaye hadi tutakapoufikia Ufalme wa Mungu. 
Wakristo wengi katika ulimwengu huu wanasema kuwa wokovu toka katika dhambi unatolewa kwa kumwamini Yesu, lakini ukweli ni kuwa wengi kati ya Wakristo hao hawajakombolewa toka katika dhambi zao kwa kuwa hawaifahamu haki ya Mungu. Nini kitatokea ikiwa watu wanamwamini Yesu pasipo kuifahamu haki ya Mungu? Watu wa jinsi hiyo wanaweza kuonyesha dalili za nje kuwa wao ni waamini waliojitoa kwa kupitia ibada na maombi yao. Lakini kwa kuwa hawaifahamu haki ya Mungu watabakia kuwa kama watendaji wa kidini na wenye dhambi ambao hawajakombolewa. 
Watu wengi katika jamii ya Kikristo na miongoni mwa Waisraeli hawaifahamu haki ya Mungu na kwa sababu hiyo hawaitii haki yake. Wale wanaomwamini Yesu lakini hawaiamini haki ya Mungu basi ni vema watambue kuwa wanaikanyaga hii haki ya Mungu. Waamini katika Yesu hawawezi kuipokea haki ya Mungu kwa kutegemea matendo mema, kwa kutoa sadaka kubwa, au kwa matendo mengine hali wakiwa hawaifahamu haki ya Mungu. 
Wale wanaoiamini haki ya Mungu wanaiamini haki hiyo bila kujalisha mazingira waliyomo, na kwa sababu hiyo wanaishi maisha ya shukrani na kuusifu utukufu wa Mungu. Kwetu sisi tunaoiamini haki ya Mungu, kadri mapungufu yetu yanavyojifunua ndiyo haki ya Mungu inavyozidi kutung’aria katika nafsi zetu. Ninakuombea ili wewe nawe uwe na uamsho kama huo. 
Tunaweza kuipokea haki ya Mungu ati kwa sababu tuna kiasi fulani cha haki katika miili yetu? Kwa kweli hapana! Hakuna kitu ambacho ni cha haki ndani yetu kuliko ile haki ya Mungu. Kwa kuwa Bwana ametuokoa kikamilifu toka katika dhambi zetu kwa haki yake, basi sisi tunaamini na kuisifu haki hii. Haki ya Mungu imetuokoa kikamilifu toka katika dhambi zetu. 
Unapokutana na kona zenye giza katika maisha yako usingukie katika imani inayojengeka katika matendo, bali wakati wote uamini katika haki ya Mungu bila kujalisha mazingira yatakayokuwepo. Haki ya Mungu ni kamilifu hadi milele. Kila mtu katika ulimwengu huu ni lazima aifahamu haki ya Mungu, ni lazima waiamini haki hii kwa kuitii injili ya maji na Roho. Kwa kuwa watu wengi wanaodai kuwa wanamwamini Yesu bado wanaishi kwa kuifuata haki ya sheria, basi watu hao ni lazima wahakikishe kuwa wanaifahamu haki ya Mungu. 
Paulo anahitimisha kwa kusema kuwa injili ya Mungu inaitimiza haki yake. Pasipokuwa na ufahamu katika injili ya kweli ya Mungu, hakuna anayeweza kuielezea vizuri hii haki ya Mungu. Watu wa jinsi hii wakiulizwa kuielezea haki ya Mungu wanaweza kusema hivi, “Yesu ni Mwokozi wangu aliyekufa Msalabani, alifufuka toka kwa wafu, na kwa sababu hiyo ameniokoa toka katika dhambi zangu.” Lakini pia wataongezea kuwa wanapaswa kutoa maombi ya toba kila siku wanapotenda dhambi, na kwamba ili kuwa wakamilifu wanapaswa wazidi kutakaswa taratibu. 
Ili uweze kuifahamu haki ya Mungu basi wewe mwenyewe unapaswa kwanza kuifahamu. Ikiwa unajifahamu wewe mwenyewe na haki ya Mungu, basi hutakuwa na chaguo zaidi ya kuiamini haki ya Mungu, kwa sababu utaitambua na kuifahamu haki ya Mungu jinsi ilivyo kuu hasa pale unapojilinganisha na wewe mwenyewe. Lakini kama hauifahamu haki ya Mungu, basi utajikita katika kuifuatia haki yako binafsi. Wale ambao wanaishikilia haki yao binafsi hawaitii haki ya Mungu kwa kuwa wanapenda kuifuatilia haki yao binafsi. 
Tunapaswa kuifahamu haki ya Mungu kabla hatujaiamini na kutoa shukrani kwa ajili ya hiyo. Kwa kuifahamu haki ya Mungu tunaweza kuamini kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake na kwa kufa Msalabani. Ikiwa tunaweza kuhesabiwa haki kwa matendo yetu mema, basi hatuuhitaji wokovu kwa haki ya Mungu. Lakini tunapotambua kuwa haiwezekani kuupata wokovu kwa matendo mema, basi tunaweza kuishukuru haki ya Mungu zaidi kwa kuwa Mungu ametuokoa sisi ambao tusingeliweza kuisha vema kwa kutegemea matendo mema. 
Je, akili na matendo yako yote ni mema? Kwa kweli hapana. Hii ni kwa sababu tuna mapungufu mengi ndio maana Mungu ametuokoa kikamilifu kwa haki yake. Kwa kuwa kuiamini haki ya Mungu kumetuokoa, basi tunatamani kuihubiri haki yake kwa wale wote wasioifahamu katika ulimwengu huu. 
Yule asiyejifahamu yeye mwenyewe huyaona makosa ya wengine na kuwazungumzia vibaya. Lakini kama mtu huyo ni mwamini katika haki ya Mungu, basi mtu huyo anapaswa kuitangaza kwa majivuno haki hii na hapaswi kujivunia haki yake mwenyewe. Lakini wale wasioiamini haki ya Mungu wanafanya dhambi ya kuikashifu haki ya Mungu. Mungu atawahukumu kwa dhambi zao. 
Mungu alimtuma Mwanawe kuja hapa duniani na amekupatia wewe haki yake. Kadri tunavyoisogelea siku ya mwisho, hatupaswi kubishana kuwa ni haki ipi ya sheria ambayo ni bora au mbaya. Wale wanaoamini katika haki ya Mungu hawapaswi kuiangalia miili yao tu bali wanapaswa kuwa watu wa shukrani kwa Mungu kwa kuamini katika haki yake. 
Hebu na tumshukuru Mungu wetu ambaye ametuokoa kikamilifu kwa haki yake. Kwa kuwa haki ya Mungu imezisamehe dhambi zako zako, basi usiwe kama wale wanaosimama kinyume na Mungu kwa kuifuata haki yao binafsi.