Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-4. Je, yatupasa kumwamini Yesu?

Ndiyo, yatupasa kwa sababu ni Bwana wetu, aliye pekee wa haki, na kwa sababu ni mapenzi yake “kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Hakuna Mwokozi mwingine Yesu ndiye Mwokozi wetu wa pekee. Tutaweza kukombolewa na kuzaliwa upya pale tu tutakapo mwamini yeye. Kwa kuwa na imani kwake na ndipo tutaweza kwenda mbinguni na kupata uzima wa milele.