Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-5. Je, sisi Wakristo tutaweza kuwa wenye dhambi?

Hapana. Mtume Paulo anasema katika 1Timotheo 1:15 kwamba yeye alikuwa “wa kwanza wao” wenye dhambi akikumbuka nyakati zile kabla ya kukutana na Yesu. Katika jumuiya za Kikristo leo hii wapo wengi wanaodhani ni wenye dhambi hata baada ya kumwamini Yesu. Lakini hivyo sivyo.
Sisi sote ni wenye dhambi kabla ya kumwamini Yesu. Ingawa tunapomwamini Yesu tu, katika njia iliyo sahihi tokana na Neno lake, tunakuwa wenye haki mara moja Mtume Paulo anakumbuka nyakati zile kabla ya kumjua Yesu na kumkiri kwamba alikuwa Mkuu wa wenye dhambi wote.
Paulo aliyeitwa Sauli alikutana na Yesu akiwa njiani kuelekea Dameski na aligundua kwamba Yesu ndiye Mwokozi, hivyo aliamini na kumshukuru. Na kwa maisha yake yote alishuhudia kwamba haki ya Mungu, ubatizo wa Yesu uliweza kufuta dhambi zote za ulimwengu na ilimpasa afe ili kufuta dhambi zote za ulimwengu.
Kwa maneno mengine, alikuja kuwa mtumishi wa Mungu aliyehubiri Injili ya maji na Roho kwa jinsi hiyo, Wakristo wengi bado hudhani kwamba Mtume Paulo alikuwa mwenye dhambi hata baada ya kukuutana na Yesu. Wanaelewa visivyo juu ya maelezo yahusuyo Mkristo mwenye dhambi, ambaye hajazaliwa upya.
Ukweli ni huu, hakuwa tena mwenye dhambi baada ya kukutana na Yesu, bali alikuwa na uwezo wa kukutana naye popote atakapo. Alijitolea maisha yake yote kuhubiri Injili ya wokovu, ule ukombozi wa ubatizo na damu ya Yesu. Hata baada ya kufariki kwake, bado nyaraka zake zipo kwa ajili yetu kwenye Biblia, kushuhudia Injili ya maji na Roho ndiyo Injili iliyo ya kweli toka Kanisa la mwanzo. Hivyo kukiri kwake katika 1 Timotheo 1:15 kulikuwa ni marudio ya nyakati zake za nyuma na kumshukuru Bwana pia.
Je alikuwa mwenye dhambi tena baada ya kumwamini Yesu? Hapana. Alikuwa ni mwenye dhambi kabla ya kuzaliwa upya. Kwa nyakati ile alipomwamini Yesu kama Mwokozi wake, ndipo pia alipogundua kwamba dhambi za ulimwengu zilitwikwa kwa Yesu, kupitia ubatizo wake, na wakati huo kuamini upatanisho wa damu yake msalabani na akawa mwenye haki.
Sababu ya kujiita mkuu wa wenye dhambi, ilikuwa kwa sababu alikumbuka nyakati zile alizowatesa wafuasi wa Yesu na kumshukuru Mungu kwa kumuokoa, yeye aliye kosa tumaini.
Ni nani awezaye kumwita mwenye dhambi? Ni nani awezaye kumuita mtu fulani mwenye dhambi ikiwa atakwa mwenye haki kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu kuwa ndipo wokovu? Ni wale wasio elewa ukweli wa wokovu wa Yesu ndiyo wenye kuweza kufanya hivyo.
Mtume Paulo alikuja kuwa mwenye haki kwa kuamini wokovu kupitia Yesu na kuanzia muda huo, kama mtumishi wa Mungu, alihubiri Injili ya kuwa mwenye haki kwa kumwamini Yesu Kristo kwa kila mmoja Mwana wa Mungu kama Mwokozi. Tokea hapo, Mtume Paulo hakuwa mwenye dhambi tena bali mwenye haki Mtumishi wa Mungu, Mtumishi wa kweli aliyehubiri Injili kwa wenye dhambi ulimwenguni pote.
Je mwenyedhambi aweza kuhubiri kwa wenye dhambi? Haitofanikiwa. Ni vipi mwenye dhambi ataweza kumhubiria mwenye dhambi mwenzake kila ambacho yeye hana! Mtu asiye okoka ataweza vipi kuokoa wengine!
Ikiwa mtu amesukumwa ataweza vipi kumvuta mtu kwake asiye okoka, wote wataishia kuanguka. Mwenye dhambi ataweza vipi kuokoa wengine? Ataweza kwenda nao motoni. Mgonjwa ataweza vipi kumtunza mwenye ugonjwa mwingine? Anayedanganywa na Shetani ataweza vipi kuokoa wengine?
Mtume Paulo alikuwa ni mwenye dhambi, lakini akawa mwenye haki alipoamini ubatizo na damu ya Yesu na kuokolewa toka dhambini. Hivyo, aliweza kuwa mtumishi wa Mungu na kuhubiri Injili kwa wenye dhambi ulimwenguni. Aliokoa wenye dhambi wengi kwa haki ya Mungu yeye binafsi hakuwa tena mwenye dhambi tokea hapo.
Alizaliwa upya na kuishi si kwa haki ya sheria bali kwa haki ya Mungu. Akawa mtumishi wa Mungu na Mhubiri wa haki ya Mungu, na aliweza kuvua roho za wengi wasio idadi kwa Mungu. Hakuwa Mhubiri kwa msisimko wake au kwa haki ya sheria, bali kwa haki ya Mungu.
Je aliendelea kuwa mwenye dhambi hadi mwisho? Hapana. Alikuwa mwenye haki. Akiwa hivyo, alikuwa Mtume wa kweli kwa Mungu. Usimwite mwenye dhambi kwa sababu itakuwa ni kejeli kwa Mungu na pia dhahiri kutoelewa ukweli. Alikuwa mwenye haki. Tusimkejeli yeye wala Yesu kwa kufikiri namna hii.
Ikiwa tutaendelea kusema ni mwenye dhambi baada ya kukutana na Yesu ni sawa na kumwita Yesu ni mwongo. Yesu alimfanya kuwa mwenye haki, na ndiye aliyemfanya kuwa mtumishi wa haki yake.