Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-6. Je sala ya toba itaweza kutakasa dhambi zetu?

Hakika Sala ya toba haitoweza kamwe kutakasa dhambi zetu kwa sababu ukombozi hauwezi kuja kwa kupitia matendo yetu. Bali, ili tuweze kuwa wenye haki kamili na kwa wakati wote tukiwa tumeoshwa dhambi zetu zote, yatupasa kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu, na kuamini kuwa Yesu ni Mungu. Ukombozi kamili hupatikana kwa wale tu wenye kuamini kuwa Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kutoa damu yake msalabani kutupa uhai mpya.
Sasa basi, je tutaweza kutakasa dhambi zetu za kila siku kwa kufanya sala za toba kila mara? Hapana. Dhambi zote tuzitendazo maishani mwetu kila siku zilikwisha takaswa takribani miaka 2000 iliyopita pale Yesu alipozibeba kwa ubatizo wake. Hakika tumepata utakaso wa kudumu kwa dhambi zetu zote kwa ule ubatizo wa Yesu na kutoka kwa damu yake pale msalabani. Amekuwa mwanakondoo wa sadaka kwa ajili yetu wenye kumwamini, kusafishwa dhambi zetu zote, na kulipia yote kwa ubatizo na kwa damu yake msalabani.
Hata zile dhambi tuzitendazo baada ya kumwamini Yesu zilikwisha safishwa kwa imani katika kijito kimiminikacho cha wokovu wa ubatizo, ukombozi wa kweli; Yesu tayari alikwisha kuwa Mwokozi na kubeba dhambi zetu zote tutakazo tenda hadi pale mwisho wa kifo chetu. Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa “hivi ndivyo” (Mathayo 3:15) impasavyo kuitimiza haki yote kwa kubeba dhambi zetu zote. Mwana wa Mungu alichukua hukumu ya dhambi zetu kwa kubatizwa.
Ubatizo wa Yesu una maana ya “kutakaswa” kwa sababu dhambi zetu zote alibeba yeye pale alipobatizwa, na hakika tukasafishwa kabisa na kutuacha huru toka dhambi zote.
Ubatizo pia una maana “kuzamishwa, kuzikwa.” Ikiwa dhambi zetu zote alibeba Yesu ilimbidi afe kwa niaba yetu sisi wenye dhambi hizo. Wale wote wenye kuamini kwamba dhambi zote alibeba Yesu kwa kupitia ubatizo hakika hawatakuwa na dhambi tena!
Imani ya kweli ni kuamini kwa moyo wote kwamba dhambi zetu zote, hata zile tutakazo tenda mbeleni maishani, zilikwisha bebwa na Yesu miaka 2000 iliyopita, alipo pata ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji na “hivi ndivyo” kutimiza haki yote ya Mungu.
Ikiwa hajasafisha dhambi zetu bado katika muda wote uliopita kwa ubatizo wake, basi pasingekuwepo na njia kwetu kuweza kutakaswa dhambi zetu. Kumbuka kwamba Yesu alitakasa dhambi zetu zote miaka mingi iliyopita.
Imani ya kweli na wokovu wa kiroho katika nyakati hizi maana yake ni kuleta mbele za Yesu dhambi zetu ili tuwe na uhakika kwamba zimekwisha takaswa kabisa kwa kusema “Yesu ulikwisha takasa dhambi hizi zote pia je, hivi ndivyo?” Ina maana pia kumwamini yeye na kumshukuru. Na ndiyo maana alikuja ulimwenguni, alibatizwa, akafa msalabani na alifufuliwa baada ya siku 3; kwa hayo yote yeye ni Mwokozi wetu.
Heri wale waliotakaswa dhambi zao kwa kuamini ubatizo wa Yesu uliosafisha dhambi zetu zote. Huu ni ukweli wa kutakaswa dhambi zetu za kila siku. Imani ya kweli ni kumwamini Yesu, aliyebeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake.