Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-8. Je kwa kutubu dhambi kutafanya dhambi hizo kufutika?

Hapana. Dhambi haziwezi kufutika kwa toba, bali kwa imani katika Injili ya maji na Roho. Dhambi zetu zaweza kufutika ikiwa tu tutaamini ubatizo na damu ya Yesu, ambayo imetutakasa sisi sote kwa dhambi zote. Hii ni Injili ya wokovu wa roho utokao kwa Yesu aliye takasa dhambi zetu zote kwa ubatizo katika mto Yordani.
Kutubu dhambi ni njia pekee ya kuonyesha kwamba mtu Fulani bado ana fuata sheria ya Mungu, lakini ukombozi umetolewa kwetu wale wenye kuamini ubatizo na msalaba wa Yesu.
Maji ya ubatizo na damu ya Kristo ndiyo kweli ya mbinguni ambayo ndiyo iokoayo watu wote na dhambi, na wokovu wetu hautegemei jinsi tufanyavyo toba, bali katika kumwamini Yesu kwamba alikwisha beba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Kusulubiwa kwa Yesu ilikuwa ni adhabu kwa zile dhambi zote alizo beba kwetu sisi wenye dhambi.
Hivyo, ukweli wa wokovu wetu upo katika ubatizo katika mto Yordan na damu ya msalabani sababu ya kutakaswa kwetu na dhambi zetu zote ni kwa kuwa tunamwamini Yesu yeye aliye takasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu yake.
Wale wote wenye kuhubiri kwamba, tutaweza kukombolewa kwa toba ya dhambi wanadharau ukweli wa wokovu wa Mungu.
Hivyo yatupasa kuamini ubatizo na damu ya Yesu, wokovu wa Mungu. Usithubutu kusema tena kwamba dhambi zote za wanadamu zitaweza kusamehewa kwa kutubu mbele ya Mungu kila mara.
Ujue ya kwamba dhambi zetu zitatuweka motoni lakini tukimwamini Yesu ubatizo na damu yake ambao ndio ukombozi na njia ya haki mbele ya Mungu, na ndipo dhambi zetu zote kwa mara moja kwa kuamini maneno ya kweli, maji na damu ya Yesu (1 Yohana 5:4-8).
Dhambi haziwezi kufutwa kila tunapotubu. Ikiwa utaendelea kusisitiza kutegemea toba utaishia motoni! Hebu na tuamini Injili ya kweli ili dhambi zetu mioyoni mwetu ziweze kutakaswa. Amini kwa moyo wako wote, na si kwa akili zako tu na uwe huru kwa dhambi hizo daima.