Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-9. Ni ipi Injili ya kweli?

Injili ya kweli ni ile pekee yenye kutuwezesha kuwa huru kwa dhambi zetu kikamilifuu, mara moja na kwa wakati wote pale tunapoiamini Nguvu ya Injili ya Mungu ni ile iendeleayo daima bila kupungua.
Injili ya Mungu ni ile “Yesu Kristo alilipa deni la wadaiwa (wenye dhambi) wasio weza bila shaka kulilipia wenyewe.” Sababu ya kuita ni Injili ya “nguvu iendeleayo” ni pale inapotupasa kufa kwa dhambi na kwenda motoni kwa hukumu mwana wa Mungu akaja kuwa sadaka ya kujitoa kwa ajili yetu ili kufuta dhambi zetu zote.
Alikuja hapa ulimwenguni na kubeba dhambi zote kwa ubatizo wake katika mto Yordani na kututakasa daima.
Amelipia mshahara wa dhambi kwa kuchukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake Yordani na kwa kufa msalabani Kalvari. Yesu alizifuta dhambi zote za ulimwengu kwa mithili ya nguvu kwa ubatizo na damu yake. Hii ndiyo habari njema (Injili) ya kweli.
Injili ya kweli ni ile Yesu kuja ulimwenguni na kwa ubatizo wake na damu yake msalabani umetuokoa sisi sote wenye kuiamini.
Kama iandikwavyo katika 1 Yohana 5:6 “Huyu ndiye aliye kuja katika maji na katika damu – Yesu Kristo si kwa maji tu, bali katika maji na katika damu.”