Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-10. Sababu gani Yesu alijitoa sadaka katika msalaba?

Kujitoa kwa Yesu kama sadaka kwa ajili ya dhambi zetu kulifanyika kutokana na kujitoa kwake kupitia ubatizo wake. Alitupa mwili wake ili kulipia dhambi zetu zote ili tuweze kuachwa huru toka hukumu ya dhambi zetu zote.
Tunachopaswa kuelewa ni kwamba, Yesu alibatizwa katika mto Yordani ili kubeba dhambi zetu zote. Yatupasa kuamini kwamba Yesu alikufa msalabani kwa sababu hii.
Ikiwa Yesu asingebatizwa kabla ya kusulubiwa na ikiwa asinge kufa pale msalabani, dhambi zetu zingebaki pale pale. Hivyo, yatupasa kuamini yote haya mawili, ubatizo na damu ya Yesu. Kwa sababu Yesu ni mwana wa Mungu, Mwana kondoo wa sadaka, alitolewa sadaka ili kufuta dhambi zetu zote.
Yatupasa sisi sote kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwamba alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu, na alisulubiwa kwa dhambi hizo. Yesu alibatizwa na kusulubiwa ili wenye dhambi waweze kuokolewa na kuachwa huru toka katika adhabu ya dhambi – mauti.