Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-11. Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu ni nani hasa?

Mungu aliwapa Waisraeli sheria kupitia Musa na pia mpango wa kutoa sadaka ili waweze kupatanishwa kwa dhambi na uovu watakao utenda mbele yake. Alimchagua Haruni, kaka yake Musa, kuwa Kuhani Mkuu na akamwamuru kutoa sadaka ya upatanisho katika siku ya kumi ya mwezi wa saba, siku ya upatanisho, ili dhambi zote za mwaka za Israeli ziweze kusafishwa (Walawi 16).
Mungu alitaja namna moja ya sadaka katika siku ya upatanisho iwe tu ikitolewa na Haruni na Makuhani warithi kati ya uzao wake. Mungu alifungua njia kwa Israeli kupatanishwa kwa dhambi zao zote kupitia kuwekea mikono ya Haruni juu ya sadaka ya mnyama wa Kafara. Hii ni sheria ya upatanisho iliyowekwa na kuanzishwa na Mungu kwa ajili yao.
Kwa kivuli hiki, amefanya ieleweke wazi kwamba Yesu alikuwa mwokozi wa wanadamu. Katika nyakati za Agano Jipya. Mungu alimtuma Yohana Mbatizaji, mrithi wa Haruni (1 Nyakati 24:10, Luka 1:5) na Kuhani Mkuu wa Mwisho wa Agano la Kale (Mathayo 11:11-13). Yohana Mbatizaji mtume aliyeletwa na Mungu, mwakilishi na Kuhani Mkuu wa wanadamu, alimbatiza Yesu ili kumtwika dhambi zote za wanadamu juu yake, Mwana wa Mungu aliyekuja kwa ajili ya wenye dhambi.
Watu wote wamebarikiwa hakika kuweza kutwika dhambi zao kwa Yesu kupitia Yohana Mbatizaji. Nafasi ya Yohana ilikuwa ni Kuhani Mkuu aliyewakilisha wanadamu na ni Mtumishi wa Mungu aliyemtwika dhambi zote Yesu.
Yohana Mbatizaji alikuwa mwakilishi na Kuhani Mkuu wa wanadamu aliyetumwa na Mungu, na ni mjumbe aliyetumwa miezi 6 kabla ya Yesu. Kwa upande mwingine, Yesu alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi zote za ulimwengu hali Yohana Mbatizaji alikuwa Kuhani Mkuu wa mwisho aliyemtwika Yesu dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo. Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtumishi wa Mungu.