Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-14. Sadaka ipi ilikuwa ni ya upatanisho wa milele?

Ilikuwa ni upatanisho wa dhambi za ulimwengu ni wa mara moja kwa kumwamini Yesu. Kwa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na Bwana aishiye milele, ataweza kubeba dhambi zote za ulimwengu milele. Ni kwa vipi alibeba dhambi zetu milele?
Ni kwa namna hii:
① kwa kuzaliwa katika mwili wa kibinadamu.
② kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji – Yordani.
③ kwa kusulubiwa msalabani kubeba hukumu yote kwa niaba yetu.
Mwana wa Mungu alikuja ulimwenguni katika mwili wa mwanadamu na kubatizwa ili kubeba dhambi zote za dunia kupitia Yohana Mbatizaji. Na pia alitoa damu yake msalabani kuokoa wanadamu kwa dhambi zao milele (Walawi 16:6-22, Mathayo 3:13-17, Yohana 1:29, Waebrania 9:12, 10:1-18).