Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-15. Je, ondoleo la dhambi limetolewa mara moja au hatua kwa hatua?

Limetolewa mara moja kwa sababu Yesu alibeba dhambi zetu mara moja na kwa wakati wote kwa kubatizwa mara moja na kupokea hukumu kwa wote mara moja. Amesema kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3:15 “kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”
Katika Yohana 1:29 Yohana Mbatizaji alisema “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” na katika Yohana 19:30 Yesu alisema “Imekwisha.”
Katika Waebrania 10:9-18 “Ndipo aliposema Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatiifu naye atashuhudia kwa maana baada ya kusema, hili ni agano mtakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo, Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”
Ubatizo na damu ya Yesu umefuta dhambi zote za ulimwengu mara moja.