Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-16. Upi ni mshahara wa dhambi?

Mshahara wa dhambi ni mauti. Haijalishi ni dhambi ipi au ya namna gani, kila dhambi itahukumiwa mbele ya Mungu, na hukumu ya kila dhambi ni kifo. Ili tuweze kupata upatanisho wa dhambi, watu wa Israeli iliwapasa kutoa kondoo asiye na doa mbele ya Mungu. Lakini aina hii ya sadaka haikuweza kwa namna Fulani kutakasa dhambi zote kwa wakati wote, “maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi” (Waebrania 10:4).
Kwa hiyo, Mungu alitayarisha sadaka ya Kondoo kukomboa watu toka dhambini. Kila mnyama wa sadaka alipaswa kuwekewa mikono kuweza kubeba dhambi zote na kufa badala yao.
Katika Agano Jipya, Yesu alichukua dhambi zote kwa kupitia ubatizo wake katika mto Yordani akiwa ni Mwanakondoo wa Mungu na kufa kwa ajili yetu. “Mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Mshahara wa dhambi ni mauti, lakini Yesu alionyesha upendo wake kwa kufa badala yetu na kutuletea zawadi ya uzima wa milele kwa sisi wale tulio wenye dhambi ulimwenguni.