Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-17. Kwa nini Yesu ilimpasa afe msalabani?

Kifo cha Yesu ilikuw ni malipo ya dhambi zote za ulimwengu alizobeba kwa kupitia ubatizo wake. Wanadamu walikuwa na adhabu ya kifo cha motoni kwa dhambi zao, lakini kwa kuwa Yesu alitupenda alikubali ubatizo, ambao ulimbebesha dhambi zote juu yake na kufa msalabani ili kutuokoa.
Alijitoa mhanga ili kutuokoa toka dhambini na laana ile ya jehanamu. Kifo chake kilikuwa ni malipo ya dhambi za wanadamu. Alibatizwa ili azichukue dhambi zote za dunia na kujitoa ahukumiwe msalabani ili kutuokoa toka dhambini, hukumuni na kwenye laana. 
Kifo cha Yesu ni kwa ajili ya dhambi za ulimwengu alizobeba pale Yordani ili aweze kupokea hukumu ya dhambi za wanadamu. Alikufa msalabani na kufufuka ili kutuwezesha kuishi tena kama wenye haki.