Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-19. Kwa nini yatupasa kumwamini Yesu?

Yatupasa kumwamini Yesu:
① Kutimiza mapenzi ya Mungu.
② kuokolewa na dhambi zetu zote.
③kuingia ufalme wa Mbinguni ili tuishi milele na Bwana.
Sisi sote ni wenye dhambi ambao tutaangukia motoni pasipo imani katika Kristo, mwokozi wetu. Ni Yesu pekee ndiye mwokozi wetu ambaye ataweza kutuokoa toka motoni. Yatupasa kumwamini kwa kuwa ndiye pekee wa kweli.
• Ni wapi watu wenye kumwamini Yesu na kuokolewa mwishoni huenda? - Mbinguni -
• Ni wapi watu wasio mwamini Yesu wala kukombolewa mwishoni huenda?
- Motoni kwa dhambi zao zote; ziwa la moto liwakalo na kiberiti - (Ufunuo 21:8).
• Ni nani Kondoo wa Mungu? Wale wote wapokeao msamaha wa dhambi kwa kuamini ubatizo wa damu ya Yesu.
Na “Kondoo wale wasio wa zizi hili” (Yohana 10:16) ni wale mbuzi kwa sababu kuamini kwa ufinyu kwa kile wanachoelewa kwa kuchagua, kwa sababu bado ni wenye dhambi wakati wale wenye kuamini ubatizo na damu ya Yesu wameokolewa wote kwa wakati mmoja na kuwa kondoo wa Mungu.