Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-27. Ni maandiko yapi huthibitisha kwamba “Mitume waliwekea mkazo mkubwa wa ubatizo wa Yesu?”

Kati ya yote, yatupasa kung’amua maana ya ubatizo wetu toka ule ubatizo wa Yesu. Hatutoweza kuzaliwa upya kwa kupokea ubatizo wa maji tu. Tutaweza kuzaliwa upya pale tu tutakapo mwamini Yesu Kristo. Ibada kama ubatizo au tohara ni vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa wa kuwepo katika wokovu wa Mungu. Biblia haijaelezea ubatizo wa washirika kama jambo la lazima kwa wokovu. Bali inawekea mkazo juu ya ubatizo wa Yesu alioupokea toka Yordani na Yohana Mbatizaji.
Kwa kweli, sehemu nyingi katika Biblia huunga mkono kwamba ubatizo wa Yesu ni kitu cha lazima na muhimu kwa wokovu wetu. Kwanza ya yote, ubatizo wa Yesu umetamkwa kama utangulizi kwa tendo lake la haki kwa kila Injili zote nne. Kwa mfano, Injili ya Marko huanza na Injili juu ya Yesu Kristo, mwanzo toka ubatizo wa Yesu, na Yohana na aliandika Injili katika mfumo wa tarehe, kwa kutumia maneno kama “siku ya pili yake” (1:29) “na siku ya tatu” (2:1) akianzia siku ile Yesu alipobatizwa.
Yohana Mbatizaji alitamka Neno la Mungu katika siku ile Yesu alipobatizwa, kwa kusema, “Tazama! Huyu ndiye mwana kondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29) ujumbe huu maana yake ni kwamba dhambi zetu zote ulimwenguni zilibebeshwa kwake Yesu pale Yohana Mbatizaji kumbatiza. Na ndipo, alikufa msalabani kwa upatanisho wa dhambi zetu kwa kusema “Imekwisha” (Yohana 19:30) na kufufuka tena toka kifoni siku ya tatu.
Mtume Paulo alisema “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko” (1 Wakorintho 15:3) maandiko hapa humaanisha katika Agano la Kale. Ni kwa namna gani mwenye dhambi ataweza kutoka sadaka ili aweze kusamehewa katika Agano la Kale? Ilimpasa kuweka mikono juu ya kichwa cha sadaka ya mnyama wa kuchinjwa kabla. Ikiwa ataondoa mpangilio wa “kuwekea mikono” juu ya kichwa cha sadaka ya mnyama hangeweza kupata msamaha kwa kutoa sadaka iliyo kinyume cha sheria.
Mtume Paulo alisema “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:3). Hivyo, ni kwa vipi itawezekana kubatizwa katika Yesu? Kubatizwa katika Kristo Yesu ni kuuamini ubatizo wake Yordani, na si ubatizo wetu. Tunapo amini ukweli wa Yohana Mbatizaji kumtwika Yesu dhambi zetu kwa kumwekea mikono juu ya kichwa chake, ndipo tutaweza kubatiza naye.
“Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27) wale wote waliomtwika Yesu dhambi zao kupitia ubatizo wa Yohana kwa imani wamekuwa watoto wa Mungu wasio na dhambi tena!
“Katika yeye mmetahiriwa kwa tohana isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo” (Wakolosai 2:11). Njia ya kukombolewa toka dhambini kwa kuvua mwili wa dhambi ni kutahiriwa kiroho bila ya kutumia mikono (Warumi 2:29 inasema “na tohara ni ya moyo, katika roho”) maana yake, kuamini ubatizo wa Yesu ulio ondoa dhambi za moyoni, Paulo alisema.
“Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo” (1 Petro 3:21). Ubatizo ni mfano tu uletao wokovu kwetu. Kama tulivyokwisha jua, watu walipotoka nyakati zile za Nuhu kwa kutoamini maji na hivyo ndivyo ilivyo hata leo, wapo ambao bado hawatii na watapotea ingawa wanaweza kuwa wanamwamini Yesu, kwa sababu hajauamini ubatizo wa Yesu ambao ni maji.
Mtume Yohana aliweka bayana kila kitu juu ya Injili hii katika waraka wake wa kwanza kwa kuandika “Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo si katika maji tu, bali katika maji na katika damu” (1 Yohana 5:6). Yesu alikuja katika yote mawili kwa ubatizo wa msalaba kutuokoa sisi sote kwa dhambi zetu zote Yohana pia alisema kwa maana wako watatu washuhudiao “mbinguni, Baba na Neno na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja” (1 Yohana 5:8). Hii inatueleza kwamba ubatizo wa Yesu, msalaba na Roho vyote kwa pamoja vimeunda wokovu mmoja ulio sahihi.
Yesu alimwambia Nikodemasi “Amin, amin na kwambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Tunazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho Imani katika ubatizo wa maji na msalaba wa Kristo ndicho unachohitaji ili ukombolewe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Na hii ndiyo maana Biblia inasema “kuzaliwa upya.”
Kwa hayo, Mtume Petro alisema “tubuni na kila mmoja abatizwe katika jina la Yesu Kristo ili mpate kusamehewa dhambi na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38). Ili tuweze kupokea msamaha wa dhambi zetu, zote na kipawa cha Roho Mtakatifu, yakupasa uwe na imani isiyo badilika juu ya ubatizo wa Yesu kwa moyo wako wote. Nini tena tunachoweza kusema? Usikane ukweli ambao ujumbe mwingi huunga mkono ubatizo wa Yesu kuwa ni jambo lisiloweka kando tendo la haki yake kwa wokovu wetu. Ukristo unalazimika sasa kuirudia Injili ya maji na Roho.
“Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na Imani kwa Mungu na wa mafundisho ya mabatizo na kuwekea mikono na kufufuliwa wafu na hukumu ya milele” (Waebrania 6:1-2). Hapa tunaweza kupata chanzo cha kuweza kutafuta juu ya Injili halisi ya Kanisa la Kale. Walifundisha juu ya kanuni za ubatizo, kuwekea mikono, ufufuko wa wafu na hukumu ya milele kwa wale waliokuwa wapya katika Ukristo. Yatupasa sisi sote tuamini kwa moyo wetu kwamba Yesu Kristo alibeba dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake na kufa msalabani ili kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo kulingana na sheria ya haki ya Mungu.