Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-28. Hili ni jambo ambalo tayari nilikwisha amini na kufundishwa labda yawezekana unajaribu kulitilia mkazo mara kwa mara kwa kuwa ubatizo wa Yesu huwekwa kando mara nyingi katika mafundisho ya msingi. Nini zaidi kilicho cha tofauti kuhusiana na hii Injili ya maji na Roho?

“Kuokolewa” maana yake ni kupokea msamaha wa dhambi zetu zote. Na pia ni kuzaliwa upya. Wakati mwenye dhambi anapokuwa mtu mwenye haki kwa kuamini Injili ya uzima, tunasema “amezaliwa upya kwa maji na kwa Roho katika Wokovu wa Yesu.” Roho Mtakatifu huja juu ya wale waliokombolewa na kuzaliwa upya na kushuhudia ndani yao kuwa ni watoto wa Mungu. Hivyo kwa haya yote ni sawa; kupokea msamaha wa dhambi, kupokea Roho Mtakatifu, kukombolewa, kuzaliwa upya, kuwa watoto wa Mungu na kuwa watu wenye haki.
Yesu alisema “mimi ndimi njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa baba ila kupitia kwangu” (Yohana 14:6), hii ina maana Yesu ndiye pekee, mwana pekee wa Mungu kwa kupitia kwake tutaweza kuingia ufalme wa Mungu. Hivyo basi, yatupasa kuelewa jinsi ile Yesu alivyotakasa dhambi zetu zote na kutuhesabu kuwa watu wake, wenye haki ya kuingia ufalme wa Mbinguni.
Baadhi ya Wakristo bado hudhani kwamba kwa kuliitia jina la Yesu tu wataweza kuokolewa. Huamini katika Yesu bila hata ya kuifungua Biblia, bila hata ya kujua nini alichotufanyia ili kutuokoa sisi sote toka dhambini. Mungu ni Roho na Mtakatifu ambaye ndani yake habadiliki, lakini bado tunaendelea kuishi maisha ya dhambi mbele yake. Kuingia ufalme wa Mungu yawezekeana ikiwa tu kwa kupitia Yesu na tutaweza kumwamini yeye kwa imani katika “sheria ya Roho wa uzima” (Warumi 8:1-2).
Watu wengi hawajui hata kile Yesu alichofanya kwa wokovu wao, bali huamini kwa upofu juu yake katika njia panda husema “Bwana, Bwana!” Hudhani pia wameokoka lakini bado wanadhamira za dhambi mioyoni mwao. Ikiwa bado unadhambi au dhamira ya dhambi moyoni ingawa imani yako ipo kwa Yesu, sasa umeokolewa na kipi? Akija mtu na akakuuliza “kwa namna gani Yesu alizitakasa dhambi zako zote?” wengi hujibu kirahisi “Labda alizitakasa pale msalabani.” Ndipo kwa swali jingine “sasa je, bado unadhambi au dhamira ya dhambi moyoni mwako?” husema, “Bila shaka! Kwani ni nani asiye na dhambi duniani?”
Jina la Yesu maana yake “Mwokozi aokoaye watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21). Tunaamini katika Yesu ili tuokolewe kwa dhambi zetu.
Ingawa, ikiwa bado tunadhambi ndani ya mioyo yetu, huku tukimwamini bado sisi ni wenye dhambi tuliouzzwa katika nira ya dhambi na tutahukumiwa kwa hilo. Mtume Paulo alisema “Sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1). Hivi ndivyo baadhi ya watu ambao bado wanadhambi mioyoni mwao huku bado hawajawa na Kristo Yesu. Kwa nini bado wanabaki kuwa wenye dhambi wasio kombolewa na kupungukiwa wokovu ingawa bado humwamini Yesu? Hii ni kwa sababu wao huamini damu ya Yesu tu, bila ya kuweka dhambi zao juu yake kwa ubatizo. Hivyo bado watakuwa na dhamira za dhambi mioyoni mwao ingawa Yesu alikufa msalabani kwa dhambi zao. 
Upo umuhimu wa tofauti wa Wakristo wenye kuamini ubatizo wa Yesu na wale wasio amini, baadhi yao wana ukombozi na kuwa wenye haki kwa kuwa na imani katika ubatizo wa Yesu, hali wale wengine bado hubaki wenye dhambi Yesu alikuja kwa wenye hati tu, wale waliozaliwa upya kwa maji na kwa Roho.
Kwa haya Mtume Paulo alisema “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?” (Warumi 6:3) Watu wengi huamini kuwa Yesu alibeba dhambi zetu pale msalabani, lakini hatutoweza kukiri kwamba hatuna dhambi mioyoni mwetu ikiwa hatutoamini ubatizo wa Yesu. Ikiwa tutafanya hivyo tunatenda kosa la kumdanganya Mungu, ambalo huenda kinyume na dhamira zetu.
Hakika bado tunadhambi au dhamira ya dhambi mioyoni mwetu kwa kuwa hatujamtwika Yesu dhambi zetu ztoe kwa njia ya imani katika ubatizo wake. Wale wote basi ambao bado hawajaamini Injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba, wako hatarini kuangukia katika kaburi la wapendwa usawa wenye dhambi. Hivyo, haijalishi nini wanachofanya kwa usawa, kama vile kusali sana milimani au kusali kwa dhati kwa kuomba msamaha wakati wa mikutano ya sala, bado watajikuta wamebaki na dhambi mioyoni mwao.
Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana Bwana, atakaye ingia katika ufalme wa mbinguni bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi watamwambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo mtawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu!” (Mathayo 7:21-23)
Nani “ninyi mtendao maovu”? Ni wale ambao bado hawajapokea ukombozi wa kweli ndani ya mioyo yao kwa kuamini msalaba pekee. Hii ni imani ya kufikirika, siyo itokayo kwa Mungu. Tunavunja sheria ikiwa hatutoamini ukweli wa wokovu wa Yesu kupitia ubatizo na msalaba. Hatuwezi kamwe tukasema tunayo imani ya kweli kabla ya kuamini yote haya mawili ubatizo wa Yesu na msalaba.
Yesu alisema kwamba ikiwa watu watataka kuzaliwa upya ni rahisi ikiwa tu ni katika maji na Roho. Ikiwa pia kwa jinsi ile wangeweza kukombolewa toka mafuriko ya maji kama wangekuwa katika safina ya Nuhu ndivyo hivyo tutaweza kupokea ondoleo la dhambi zetu zote na kuishi maisha ya uaminifu ikiwa tu tutaamini Injili ya maji na Roho. Bila Injili ya maji na Roho hautoweza kupokea msamaha wa dhambi au kufanya mtoto wa Mungu.