Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-29. Na uhakika kwamba kuamini katika Yesu kumeniokoa. Nina amani na huhuda moyoni. Lakini bado sijaelewa juu ya ujumbe wako. Je yanipasa kuamini ubatizo wa Yesu pamoja na msalaba wake ili niokolewe?

Ikiwa huamini ubatizo wa Yesu, hii ni hakika kwamba bado una dhambi moyoni. Mtume Yohana alisema “Tukisema kwamba hatuna dhambi twajidanganya wenyewe wala kweli haimo mwetu” (1 Yohana 1:8) ukisema ya kwamba huna dhambi, ingawa ukweli ni kwamba unadhambi kwa sababu kuamini ubatizo wa Yesu ni tendo la kujidanganya katika dhamira yako na ni ushahidi tosha ya kwamba kweli haimo ndani yako. Ushuhuda wa wokovu huingia moyoni mwetu pale tunapopokea ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu kuwa kipawa kwa kuamini ubatizo wa Yesu na msalaba wake.
Mtume Paulo alisema “…Injili ya namna nyingine wala si nyingine…” (Wagalatia 1:6-7). Hakuna Injili nyingine zaidi ya Injili ya maji na Roho, ambayo Mitume walipokea toka kwa Yesu na kuhubiri kwa watu, ndiyo itakayo tuokoa na dhambi zetu zote. Ikiwa hatutoamini Injili ya maji na Roho ambayo mitume walihubiri, hakika bado dhambi imo kati yetu.
Ni kwa namna gani tunaweza kuwa na dhamira ya wokovu ikiwa bado tuna dhambi? Pale Wakristo, ambao hawajazaliwa upya wanapokuwa na tabia njema mbele ya Mungu wanakuwa na uhakika juu ya wokovu wao wakiwa na furaha na uhakika kwa jinsi hii wanakosa uhakika na wana woga wa mzigo wa dhambi ulio moyoni mwao pale inapojitokeza kwamba wametenda dhambi mbaya. Huu ni wokovu wa kwenda pasipo mwelekeo wa kutumainiwa ulio na msingi wa hisia na mawazo yetu ambamo Mungu hausiki. Watu wa aina hii wamo hatarini zaidi katika ule mpango wa kufanya sala za toba kila siku ili waweze kuwa watakatifu hatua kwa hatua na kuendelea na wokovu uyumbao.
Wale wote wenye kuamini wokovu usio wa kweli hufikiri kwamba wataendelea kuwa na wokovu ulio sahihi katika nyakati zijazo za maisha yao ikiwa wataweza kuendelea kuishi maisha matakatifu kwa kumuomba Mungu msamaha kila siku na kufuata sheria yake kwa matendo. Hati hivyo bado ni wenye dhambi ikiwa bado hawajamtwika Yesu dhambi zao kwa kupitia imani katika ubatizo wake.
Wokovu Mungu alioufanya ni wokovu ulio sahihi unatueleza juu ya Yesu kubeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wa Yohana kule Yordani na alifuta kabisa dhambi hizo msalabani.
Kwa haya yote Mtume Yohana alisema “Tukizi ungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” (1 Yohana 1:9). Ikiwa dhambi zetu zote hazijasamehewa kupitia Injili ya maji na Roho kwa kutoijua, yatupasa kukiri mbele ya Bwana kuwa ni wadhambi, ingawa tunamwamini Yesu na kujua kuwa ni wenye dhambi bado ambao mwisho wetu ni jehanamu kwa dhambi hizo. Huku ndiko kukiri kwa ukweli dhambi. Dhambi hazitoweza kutakaswa bila Injili ya maji na Roho, haijalishi udogo wa dhambi. Tunapokiri kwa namna hii basi, Injili ya maji na Roho hututakasa dhambi zetu mara moja na kutufanya wenye haki.
“Sasa ndio wakati uliokubalika” (2 Wakorintho 6:2). Kwa yeyote asikiaye na kuiamini Injili ya ubatizo wa Yesu na msalaba wake ataokolewa na dhambi zake zote, kuwa mwenye haki, na anayo imani madhubuti ya kuweza kuingia ufalme wa Mbinguni wakati Bwana atakapo rudi. Imani yeyote katika mafundisho, kanuni na thiologia zaidi ya Injili ya kweli, hakuna wokovu wa dhambi zetu ile ni mitego tu ambayo ibilisi ameiweka ndani ya mawazo ya wanadamu. Yatupasa kurudia Injili ya maji na Roho na kupokea wokovu wa kweli toka dhambi zilizomo mioyoni mwetu. Huku ndiko kumpenda Yesu na alichotufanyia.