Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[2-2] Imani Inayoweza Kukubaliana na Kuifia-Dini (Ufunuo 2:1-7)

(Ufunuo 2:1-7)
 
Wengi wetu neno kuifia-dini ni neno geni na ambalo hatujalizoea, lakini wale ambao wamezaliwa na kukulia katika tamaduni ambayo si ya Kikristo, basi neno hilo linakuwa ndio geni zaidi. Kusema kweli neno “kuifia-dini” si neno ambalo tunakutana nalo mara kwa mara katika maisha yetu ya kila siku; tunajiona kuwa mbali na neno hilo kwa sababu katika hali halisi ni vigumu kufikiria juu ya kuifia-dini. Hata hivyo, sura ya 2 na ya 3 ya Kitabu cha Ufunuo inazungumzia juu ya huku kuifia-dini, na toka katika Neno linalopatikana katika sura hizi ni lazima tuianzishe imani ya kuifia-dini katika mioyo yetu—yaani imani ambayo kwa hiyo tunaweza kuuawa na kuifia-dini.
Watawala wa Kirumi walikuwa ni watawala wakuu wa watu wao. Walitumia mamlaka yao kamili dhidi ya maeneo yao ya utawala, waliweza kufanya lolote ambalo mioyo yao ilitamani kulifanya. Baada ya kupigana vita na kushinda vita nyingi, Utawala wa Rumi uliyaweka mataifa mengi chini ya utawala wake, hali ukijitajirisha kwa kodi iliyolipwa na mataifa yaliyoshindwa vitani. Baada ya kutoshindwa vita hata moja, hili taifa dogo lilikua na kuwa dola kubwa zaidi ulimwenguni. Ni mbingu tu ndiyo iliyokuwa imewawekea ukomo wa mamlaka yao. Hivyo, mamlaka yao ilikuwa kubwa sana kiasi kuwa viongozi wa dola hiyo walianza kuabudiwa na watu wao kama miungu.
Kwa mfano kitendo cha kutengeneza sanamu ya sura zao na kuiweka ili watu waiabudu hakikuwa kitendo cha kawaida. Kwa hawa wakuu wa dola waliokuwa wamejitangazia wenyewe kuwa ni miungu, waliona kuenea kwa waamini katika Yesu kuwa ni tishio kwa mamlaka yao. Hali wakizuia kisheria mikusanyiko ya Wakristo, pia waliamua kupitisha sera za kiuonevu ili kuwatesa waamini, kuwafunga, na kuwaweka jela, na hatimaye hata kuwaua kwa sababu ya imani yao. Hii ndio sababu kuwa Wakristo wa Mwanzo walienda katika maeneo kama vile ya Katakombi ili kuyakwepa mateso, na ni mateso haya ndiyo yaliyowafanya waweze kukubaliana na kuifia-dini na kuilinda imani yao ya haki.
Hivi ndivyo wafia-dini walivyoinuka katika kipindi cha Kanisa la Mwanzo. Kwa kweli watakatifu wa wakati huo hawakuuawa kwa sababu ya kutoyatambua mamlaka ya watawala wa dola ya kirumi. Wao waliyatambua mamlaka ya kidunia, bali hawakukubaliana na mamlaka hizo wakati zilipowalazimisha kumwabudu mwanadamu kama mungu na kumkataa Yesu katika mioyo yao, katika hali kama hiyo walikuwa tayari hata kuyatoa maisha yao. Watawala wa Kirumi waliwaamuru Wakristo kumkana Yesu na kuwaabudu wao si tu kama watawala bali kama miungu. Hivyo, hali wakiwa hawawezi kukubaliana na amri kama hiyo, Wakristo wa Kwanza waliendelea kukabiliana na mateso na hatimaye kuuawa na kuifia-dini kwa sababu ya kuilinda imani yao hadi Mkataba wa kisheria wa Milani ulipopitishwa mwaka 313 B.K ambao uliwaletea uhuru wa kidini. Hivyo, kama ilivyo kwa hawa watangulizi wetu wa kiimani, sisi nasi itakuwa heri kama tutakufa kuliko kuikana imani yetu.
Kifungu kinachozungumzia juu ya makanisa saba ya Asia Ndogo sio tu kwamba ni maelezo ya kina kuhusu hali ya wakati ule, bali pia ni ufunuo wa ulimwengu utakaokuja baadaye. Katika maneno hayo kunapatikana ufunuo kuwa watumishi wa Mungu na watakatifu wa Mungu watauawa na kuifia-dini ili kuilinda imani yao. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha utawala wa Dola ya Rumi, utakuja wakati ambapo mtawala mkuu atainuka akiwa kama toleo la kisasa la Mfalme wa Rumi na ambaye atamweka kila mtu chini ya utawala wake wa kikatili, atatengeneza sanamu ya sura yake, na atawataka watu wote kuinama na kuiabudu sanamu yake, na atadai aabudiwe kama mungu. Kwa kweli matukio kama hayo hayapo mbali sana tangu sasa, na wakati nyakati hizi zitakapowadia, basi watakatifu wengi watazifuata nyayo za waamini wa Kanisa la Mwanzo za kuifia-dini.
Hivyo ni lazima tuliweke Neno la kutia moyo ambalo Bwana wetu aliyapatia makanisa saba ya Asia katika mioyo yetu. Katika kuyasalimia, kuyatia moyo, na kuyajenga makanisa saba ya Asia, Mungu aliwaahidi kuwa “yeye ashindaye” atakula “matunda ya mti wa uzima, ulio katika Paradiso ya Mungu,” na kisha atapokea “taji ya uzima,” “mana iliyofichwa,” “nyota ya asubuhi,” na zaidi! Hii ni ahadi ya Mungu yenye uaminifu kuwa wale watakaoshinda kwa kupitia kuifia-dini, Mungu atawapatia baraka za Mbinguni milele.
Je, iliwezekanaje basi kwa watakatifu wa Kanisa la Mwanzo kukabiliana na kuifia-dini? Kitu cha kwanza ambacho ni lazima tukikumbuke ni kuwa wale ambao waliweza kuuawa na kuifia-dini walikuwa ni watumishi wa Mungu na watakatifu wake. Si kila mtu anaweza kuuawa na kuifia-dini. Ni wale tu wanaomwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao, wasioweza kusalimu amri chini ya mateso, na wanaoweza kuishikilia imani yao na kumtumaini Bwana, basi hao ndio wanaoweza kukabiliana na mauaji ya kuifia-dini.
Mtume Yohana, ambaye tunamwona hapa akilikemea Kanisa la Efeso hali akiwa uhamishoni katika Kisiwa cha Patmo, yeye ndiye aliyekuwa wa mwisho akiwa hai kati ya wale Mitume kumi na mbili wa Yesu. Mitume wengine wote walikuwa wameshauawa na kuifia-dini pamoja na watakatifu wengine. Tukizungumza kwa mujibu wa historia, watakatifu wa yale makanisa saba ya Asia walikuwa ni wachache miongoni mwa Wakristo wengi wasio na idadi ambao waliuawa hadi kufikia mwaka 313 B.K. Hali wakiyakimbia mateso ya mamlaka ya Rumi, walikimbilia mabondeni na kuchimba mapango na makaburi ya chini kwa chini yanayojulikama kama Katakombi ili waweze kuabudu—pamoja na kuyapitia haya yote na zaidi, Wakristo hao wa mwanzo hawakuikana imani yao na walikubaliana kwa hiyari kuifia-dini.
Watumishi na watakatifu wa makanisa saba ya Asia, likiwemo Kanisa la Efeso, pamoja na kuwa walikemewa na Mungu, ukweli ni kuwa hata wao waliuawa na kuifia-dini. Kilichowawezesha kuuawa na kuifia-dini ilikuwa ni imani yao katika Bwana. Wao waliamini kuwa Bwana alikuwa ni Mungu, na kwamba alizichukua dhambi zao zote, na kwamba alikuwa ni Mchungaji ambaye atawaongoza wote kwenda katika Ufalme wa Milenia na katika Mbingu na Nchi Mpya. Imani na tumaini hili ndivyo vilivyowawezesha kuishinda hofu yao na maumivu ya kifo yaliyokuwa yameandamana na kuuawa kwao kwa ajili ya kuifia-dini.
Kwa sasa tunaishi katika nyakati za mwisho. Si muda mrefu ambapo ulimwengu utaunganishwa chini ya mamlaka moja na ambapo kiongozi mwenye mamlaka kubwa atainuka. Kama inavyoelezwa kwatika Ufunuo sura ya 13, mtawala huyu mwenye mamlaka atatishia maisha ya watakatifu na atawataka waikane imani yao. Lakini sisi wenye haki wa nyakati za mwisho, tutaweza kuvishinda vitisho vyake na amri yake ya kutulazimisha na kisha tutailianda imani yetu kwa kupitia kuuawa kwetu na kuifia-dini, hii ni kwa sababu tuna imani moja kama waliyokuwa nayo watakatifu wa Kanisa la Mwanzo.
Katika aya ya 4-5, Mungu alilikemea Kanisa la Efeso kwa kusema, “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.” Je, hii ina maanisha nini? Ina maanisha kuwa Kanisa la Efeso lilikuwa limeiacha injili ya maji na Roho. Watakatifu wote wa Kanisa la Mwanzo, wakiwemo wale wa Kanisa la Waefeso walikuwa wameamini katika injili ya maji na Roho. Hii ni kwa sababu wanafunzi wa Yesu walikuwa wameenea na kuihubiri injili ya maji na Roho. Hivyo injili ambayo watakatifu wa wakati ule waliipokea toka kwa Mitume ilikuwa ni injili ya maji na Roho, na wala si injili ya uongo, yaani injili iliyoundwa na mwanadamu inayoamini katika damu ya Msalaba tu.
Lakini hapa inaelezwa kuwa mtumishi wa Kanisa la Efeso alikuwa ameuacha upendo wake wa kwanza. Hii ina maanisha kuwa mtumishi wa Kanisa la Efeso alikuwa ameiacha injili ya maji na Roho katika huduma yake kwa kanisa. Hii ndio sababu Bwana alisema kuwa atakiondoa kinara chake toka mahali pake ikiwa hatatubu. Kukiondoa kinara toka mahali pake maana yake ni kuliondoa kanisa, ambapo Roho Mtakatifu asingeliweza kufanya kazi tena katika Kanisa la Efeso.
Kwa mtumishi wa Kanisa la Efeso, kitendo cha kurudi katika injili ya maji na Roho hakikuwa ni kitu kigumu sana kukifanya. Lakini hili lilikuwa ni tatizo dogo sana kwake. Lakini kitu kilichomfanya kuishia katika shida ni kwa sababu pamoja na kuwa alikuwa akiamini katika injili ya maji na Roho katika moyo wake, ukweli ni kuwa alishindwa kukihubiri kile ambacho alikuwa akikiamini. Aliwapokea katika kanisa lake wale wote waliokuwa wakimkiri Yesu kuwa ni Mwokozi wao pamoja na kuwa walikuwa hawajaiamini injili ya maji na Roho, ukweli ni kuwa kuikiri imani yao katika injili ya maji na Roho kuliwamaanishia waumini kujiandaa kwa ajili ya kuifia-dini.
Kwa maneneo mengine, aliwakaribisha wengine kuingia katika kanisa lake pasipo kujali ikiwa walikuwa na imani moja katika Mungu na katika injili yake ya maji na Roho. Kwa kuwa kuingia katika kanisa la Mungu kulihitaji kujitoa sadaka, na kwa kuwa mtumishi wa Kanisa la Efeso alikuwa akiogopa kuwa kujitoa sadaka huko kungeliweza kuwazuia wengine wengi kujiunga na kanisa, basi alishindwa kuuhuburi ukweli kamili katika usahihi wake.
Lakini kwa kuwa Roho Mtakatifu hawezi kukaa mahali pasipo na kweli, Mungu alisema kuwa atakiondoa kinara. Mungu alisema kuwa ataliondoa kanisa si kwa sababu ya upungufu wa matendo ya mtumishi na watakatifu wa Efeso, bali alimaanisha kuwa Mungu hataweza kukaa katika kanisa kwa sababu ukweli usingeliweza kupatikana ndani yake.
Kwa kweli matakwa ya Mungu ni kwamba kanisa la Mungu liweze kuifuata injili ya maji na Roho. Watumishi na watakatifu wa Mungu hawapaswi tu kuiamini injili bali wanapaswa pia kuihubiri na kuifundisha kwa usahihi, kwa kuwa ni katika injili hii tu ndipo tunapoweza kuupata upendo wa Mungu, neema yake, na baraka yake yote kwa ajili yetu.
Badala ya kuihubiri injili hii, mtumishi wa Kanisa la Efeso aliwapokea katika kusanyiko lake wale waliokuwa wakiamini katika damu ya Msalaba tu. Lakini hata mtumishi au mtakatifu aliyezaliwa tena upya, kitendo cha kuamini pasipo kuihubiri injili ya maji na Roho ambayo imezichukulia mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani basi kitaifanya kazi na matendo yetu yote kuwa yasiyo na maana mbele za Bwana. 
Pamoja na kuwa tunaweza kuwa na mapungufu mbele za macho ya Bwana, ikiwa tutaiamini injili na kuihubiri, basi ukweli ni kuwa Bwana anaweza kukaa na kufanya kazi ndani yetu kama Roho Mtakatifu. Hata kama watumishi wa Mungu au watakatifu wana mapungufu mengi, Bwana anaweza kuwafundisha na kuwaongoza kwa kupitia Neno lake. Katika kanisa la injili ya maji na Roho kunapatikana Roho Mtakatifu, na ule uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa hilo kuna maanisha kuwa kanisa hilo ni takatifu.
Kunaweza kusiwe na utakatifu kwa watumishi wa Mungu au watakatifu ikiwa hawaihubiri injili ya maji na Roho. Wanaweza wakasema kuwa hawana dhambi tena, lakini utakatifu hauwezi kupatikana mahali ambapo injili ya maji na Roho haijahubiriwa. 
Injili hii ya maji na Roho ni injili ambayo watakatifu wa Kanisa la Mwanzo waliiamini, injili ambayo inatangaza kuwa Bwana alikuja hapa duniani kuwaokoa wanadamu kwa kuzichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake na kwa kuzisafishilia mbali dhambi hizo kwa kifo chake Msalabani. Bwana aliuchukulia mbali udhaifu wetu wote na mapungufu yetu kwa ubatizo wake. Mungu alizichukulia mbali dhambi zetu zote toka katika udhaifu wetu na mapungufu yetu, na amefanyika kuwa Mchungaji wetu wa milele.
Baada ya kuwa tumebarikiwa kiasi hicho, inawezekanaje basi mtu akakubali kumbadilisha Yesu na mtawala wa Kirumi na kisha kumwabudu mwanadamu kama mungu wake? Kwa kuwa neema ya Mungu ilikuwa kubwa sana na ya kutosha, basi hakuna kinachoweza kuwafanya watakatifu kuukana upendo wa Bwana hata kama itakuwa ni mateso au vitisho, na kwa sababu hiyo watakatifu hao wapo tayari kukubaliana na kuuawa kwao kwa kuifia-dini ili kuilinda imani yao. Waliviasi vitisho vyote ambavyo vililenga katika kuwalazimisha ili waikane imani yao na kujaribu kuwahonga vyeo ili wawe wakuu katika jamii na hatimaye waweze kuachana na imani yao kwa faida ya vitu. Hakuna ambacho kingeliweza kuwafanya waikane imani yao na kumwacha Mungu wao, uaminifu huu usiokufa ndio ulioweza kuwafanya waifie-dini.
Mioyo ya wafia-dini ilijazwa na shukrani kwa neema na upendo wa Mungu ambao umewakomboa toka katika dhambi zao kwa kupitia injili ya maji na Roho. Wale ambao imani yao haikuweza kuukana upendo wa Mungu ambao umewakomboa milele toka katika dhambi zao walikubaliana na kuifia-dini kuliko kuikana imani. Wakati utawadia ambapo kama watawala wa Rumi walivyowataka watakatifu wa Kanisa la Mwanzo kuwatambua wao kuwa ni miungu na kuwaabudu, basi sisi nasi tutalazimishwa kuikana imani yetu. Wakati jambo hili litakapotokea, basi ni lazima tuzifuate nyayo za watangulizi wetu wa imani na kisha tuilinde imani yetu kwa kukubali kuifia-dini.
Pamoja na kuwa tuna mapungufu mengi, Mungu ametupenda sana kiasi kuwa ameyachukua mapungufu yetu mengi na dhambi zetu katika mwili wake. Haijalishi jinsi tunavyoweza kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Mungu ametupokea katika mikono yake. Sio tu kwamba ametukubali, bali ameyatatua matatizo yote ya dhambi na maangamizi na ametufanya sisi kuwa watoto wake na mabibi harusi wake milele. Hii ndio sababu hatuwezi kuikana imani yetu katika Yesu na ndio sababu tupo radhi kukubaliana na kuifia-dini kwa ajili ya jina lake. Kuifia-dini kunalenga katika kuulinda upendo wa kwanza ambao Mungu alitupatia. Kuifia-dini hakutokani na na hisia zetu za kibinadamu, bali kunatokana na imani yetu katika ukweli kuwa pamoja na mapungufu yetu na udhaifu, Mungu ametupatia baraka zake zote. Hatuifii-dini kwa sababu ya nguvu zetu binafsi na nia zetu bali tunaifia-dini kwa sababu ya imani yetu juu ya ukuu wa Mungu.
Ni kweli kuwa kuna watu wanaokufa kama wafia-dini lakini kwa sababu ya nchi yao au kwa sababu ya itikadi fulani. Watu hawa wanauhakika usioyumbishwa juu ya kile wanachokiamini kuwa ni sahihi na wapo tayari hata kuyatoa maisha yao kwa ajili ya jambo wanaloliamini. Lakini ni vipi kuhusu sisi? Inawezekanaje kwa watoto wa Mungu waliozaliwa tena upya kwa maji na Roho kwa imani yao katika Yesu Kristo kuuawa na kuifia-dini? Tunaweza kuifia-dini kwa sababu tunashukrani nyingi sana kwa ajili ya injili ambayo kwa hiyo Bwana wetu ametupenda na kutuokoa. Kwa kuwa Mungu ametukubali pamoja na mapungufu yetu mengi yasiyo na idadi, na kwa kuwa ametupatia Roho Mtakatifu, na kwa kuwa ametufanya sisi kuwa watu wake na ametubariki kuishi milele katika uwepo wake, basi ni hakika kuwa hatuwezi kumkana wala kumwacha.
Pia Mungu ametuahidi Mbingu na Nchi Mpya, na kwa tumaini hili pekee hatuwezi kuikana imani yetu. Haijalishi kinachoweza kutoka—hata kama Mpinga Kristo atatutishia na kututesa hadi kifo katika nyakati za mwisho—hatuwezi kamwe kumkana Bwana wetu na injili yake ya maji na Roho. Hata kama tutaburuzwa na kupelekwa chini ya miguu ya Mpinga Kristo na kisha kuuawa, hatuwezi kamwe kuikana neema na upendo wa Mungu ambavyo vimetuokoa. Kama msemo huu unavyosema, “hata kama ni kwa miili yetu kufa” hatutamkana Bwana. Tunaweza kulazimishwa kufanya mambo mengine, lakini kuna kitu kimoja ambacho hatutaweza kukubaliana nacho: hatutaweza kuiacha wala kuukana upendo wa Kristo ambao umetuokoa.
Je, unafikiri kuwa Mpinga Kristo atatuonea huruma ati kwa sababu tuna mapungufu? Kwa kweli hapana! Mpinga Kristo hatajali! Lakini Bwana wetu, bila kujalisha jinsi tulivyo wadhaifu na wenye mapungufu, ametufanya sisi kuwa wakamilifu kwa kuyachukua matatizo yetu yote katika mwili wake na kuhukumiwa kwa niaba yetu. Hii ndiyo sababu hatuwezi kuuacha upendo wa Bwana wa wokovu ambao umetukomboa kwa kupitia injili ya maji na Roho, na hii ndiyo sababu kuwa ni kwa nini hatuwezi kuikana imani yetu katika upendo wa kwanza. Hakuna kinachoweza kukanwa labda tukikane katika mioyo yetu kwanza.
Vivyo hivyo, ikiwa tutaiweka imani yetu katika vina vya mioyo yetu, basi tunaweza kuilinda imani yetu hadi mwisho hata kama kutakuwa na vitisho na kulazimishwa kwa hali ya juu. Ikiwa tutaufahamu upendo wa thamani wa Mungu kwetu katika mioyo yetu, na ikiwa tutaushikilia upendo huu hadi mwisho, basi ni hakika kuwa tunaweza kuilinda injili katika siku za mwisho. Kwa wale wanaotembea katika imani, kwa kweli si vigumu kukubaliana na kuifia-dini.
Sisi sote ni lazima tufikirie kwa kina juu ya mauaji ya kuifia-dini yanayotungojea. Kuifia-dini si kitendo cha kuvumilia maumivu na mateso. Miili yetu imeumbwa katika hali ambayo hata kipande kidogo sana cha mwiba kinaweza kuleta maumivu makubwa sana. Kuifia-dini hakumaanishi ni kuyavumilia maumivu kama hayo. Bali kuifia-dini ni suala la kuyatoa maisha yako, yaani kufa. Hivyo, kuifia-dini si suala la kuteseka kimwili kwa maumivu, bali ni suala la kupoteza uhai wa mtu. Wakati Mpinga Kristo atakapotutaka tumwabudu na kumwita yeye kuwa ni mungu, basi ni hakika kuwa tutampinga hadi tutakapokufa. Kwa kuwa ni Bwana tu ndiye aliye Mungu wetu, na kwamba ni yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa, basi ni vema na inatupasa kuuawa na kuifia-dini ili kulilinda jina lake. Hatuwezi kuibadilisha imani hii kwa jambo lolote.
Je, Mpinga Kristo anayemkana Mungu na anayetaka aabudiwe kama mungu anastahili kuabudiwa hivyo? Kwa kweli hapana! Ni Mungu tu ndiye aliye na uwezo wa kuumba ulimwengu. Ni yeye tu aliye na mamlaka juu ya uhai na kifo, ni Yeye tu ndiye asiye na mawaa wala dhambi na aliye mwenye haki mkamilifu mbele ya viumbe vyote, na ni yeye tu ndiye aliye na nguvu ya kuweza kuzichukulia mbali dhambi za ulimwengu. Sasa ni vipi kuhusu Mpinga Kristo? Kitu pekee ambacho Mpinga Kristo anacho ni mamlaka ya kidunia. Hii ndio sababu hatuwezi kumbadilisha Bwana wetu kwa ajili yake, na hii ndio sababu hatuwezi kuikana imani yetu katika Mungu Mwenyezi.
Kwa hakika ni Mungu ndiye atakayetufanya kuwa na furaha milele. Atawafufua wale waliofanywa kuwa hawana dhambi kwa kumwamini Yesu Kristo katika miili yenye utukufu na atawafungulia malango ya Ufalme wa Milenia na Mbingu na Nchi Mpya. Lakini wale wanaopiga magoti mbele ya Mpinga Kristo watakabiliana na hukumu ya milele na watatupwa kuzimu pamoja na Shetani. Litakuwa ni jambo la kijinga sana ikiwa tutaitupilia mbali furaha yetu ya milele kwa kusimama pamoja na Mpinga Kristo kwa kuogopa maumivu na mateso ya mpito. Hali wakiiufahamu ukweli huu, wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho katika mioyo yao watasimama kwa ujasiri kinyume na Mpinga Kristo, watauawa kwa kuifia-dini, na kisha watapokea furaha ya milele kama thawabu ya kujitoa kwao.
Wewe na mimi, sote tutauawa na kuifia-dini. Usifanye makosa: wakati wa farasi mweusi utakapoisha, basi wakati wa farasi wa kijivujivu utawadia, na hapo ndipo Mpinga Kristo atakapoinuka na ndipo mapigo ya yale matarumbeta saba yataanza. Ni hakika kuwa Mpinga Kristo atainuka, na ni hakika zaidi kuwa sisi watakatifu tutauawa na kuifia-dini, na ni hakika kuwa baada ya ufufuo wetu tutanyakuliwa. Na ni hakika kuwa tutaingia katika Ufalme wa Miaka Elfu Moja. Hii ndio sababu kuwa sisi sote tutauawa na kuifia-dini kwa hiari wakati Mpinga Kristo atakapotutesa na kutaka kutuua.
Sinema inayoitwa Quo Vadis, ambayo ni moja ya sinema za zamani inaelezea juu ya Wakristo wengi ambao waliyatoa maisha yao katika kuilinda imani yao na waliimba nyimbo za sifa hata wakati walipokuwa wakipelekwa kwenda kuuawa. Sinema yenyewe ni ya kubuniwa, lakini habari inayoieleza kihistoria ni habari ya kweli—kwamba Wakristo wengi waliyatoa maisha yao ili kuilinda imani yao. Kwa nini walifanya hivyo? Kwa sababu kile ambacho watawala wa Kirumi walikitaka toka kwao—yaani kumkana Mungu, kuabudu miungu mingine, na kuachana na imani hakikuwa ni kitu ambacho wangaliweza kukikubali.
Ikiwa wangelikubaliwa kumbadilisha Mungu wao kama watawala wa Rumi walivyotaka, basi ni hakika kuwa wangelikuwa wamebadilisha kila kitu. Kwa maana hiyo mtawala wa Rumi angelikuwa ndiye mungu wao, angeliwaweka chini ya utawala wake wa kikatili, na wangelikufa vitani kama vibaraka wake. Wasingeliweza kukombolewa toka katika dhambi wala kuweza kuingia katika Mbingu na Nchi Mpya. Hii ndio sababu hawakuweza kuikana imani yao na badala yake waliamua kukabiliana na kifo kwa furaha na kusifu. Waliweza kumwimbia Bwana nyimbo za sifa hata pale walipokuwa wakifa kwa sababu tumaini lao lilikuwa ni kubwa zaidi kuliko maumivu ya kifo.
Ni muhimu sana kwetu kuilinda injili ya maji na Roho. Pia ni muhimu sana kwetu kuishi kwa tumaini, hali tukiamini kuwa baada ya kifo chetu tunangojewa na uzima wa milele katika ulimwengu mpya uliojawa na furaha na utukufu.
Je, umeshawahi kuteseka kwa ajili ya Bwana? Ukiachana na mapungu yako na makosa binafsi, Je, umewahi kuteseka kweli kwa ajili ya Bwana? Ikiwa mateso yetu ni kwa ajili ya Bwana, basi maumivu yetu yote yatageuka na kuwa katika furaha kuu. Kama Mtume Paulo alivyoielezea furaha hii, “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu” (Warumi 8:18). Kwa kuwa furaha ya utukufu utakaofunuliwa kwetu ni kubwa sana kuliko maumivu ya mateso kwa ajili ya Bwana, basi mateso yetu ya sasa yatazikwa chini ya furaha kuu ya imani yetu.
Kwa maneno mengine, watakatifu na wafia-dini wa Kanisa la Mwanzo waliweza kuyashinda maumivu yao na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Bwana kwa sababu walifahamu kuwa furaha iliyokuwa ikiwangojea ilikuwa ni kubwa sana kuliko mateso yao ya muda mfupi. Mauaji yao ya kuifia-dini hayakuwa matokeo ya uwezo wao wa kuvumilia na kuyabeba maumivu, bali yalikuwa ni matokeo ya tumaini lao juu ya utukufu ambao unawangojea.
Kwa jumla, watu wanayavumilia mateso yao kwa kufikiri kuwa wanapaswa kukubalina nayo. Kwa kweli hii ni vita ngumu na ya kuchosha. Wakati kuvumilia kwao kunapoleta matokeo ya kukatisha tamaa, basi hapo ndipo kuchanganyikiwa kunapokuwa kukubwa zaidi huku wakiwaza kuwa wameteseka bure! Lakini kwetu sisi Wakristo, jambo ambalo ni kubwa ni ile furaha ya uvumilivu wetu, kwa maana tupo salama kwa tumaini la uhakika na thawabu tutakayopewa. Ikiwa tutayaweka mawazo yetu katika kumtumikia Bwana kwa mioyo yetu yote kama watumishi wake waaminifu, basi ni hakika kuwa tunafahamu kwamba furaha inayotungojea ni kubwa sana kuliko maumivu ya kujitoa kwetu sasa. Kwa kuwa magumu yote yamefunikwa katika furaha hii, basi sisi sote tunaweza kuishi maisha yetu kwa ajili ya Bwana na hata kukubaliana na kuuawa na kuifia-dini kwa ajili yake.
Watu wana nafsi, hisia, mawazo, na imani. Lakini kwa kuwa Roho wa Bwana anakaa katika nafsi za waliozaliwa tena upya, basi kule kuteswa kwa ajili ya haki yao kunaweza kuwaletea furaha isiyoelezeka kwa ajili ya utukufu unaowangojea. Lakini kama watauacha upendo wa kwanza, basi ni hakika kuwa Bwana hatasita kukiondoa kinara.
Ikiwa wale ambao wamekuwa wakiitumikia kwa furaha injili ya maji na Roho kwa mioyo yao yote wataacha kufanya hivyo, basi hiyo itamaanisha kuwa wameiacha furaha ya kuitumikia injili, ambao ni upendo wao wa kwanza hata kama watakuwa hawajaitupilia mbali injili hii. Wanaweza kuendelea kuishikilia imani yao binafsi, lakini ikiwa hawajivunii katika kuihubiri injili na ikiwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuokolewa—yaani kufahamu kuwa damu ya Msalaba pekee haitoshi kwa ajili ya wokovu—basi ni dhahiri kuwa imani yao itapunguzwa nguvu na kwa sababu hiyo kuuawa na kuifia-dini kitakuwa ni kitu ambacho hakiwezekani kwao. Na hapo ndipo Mungu atakapokiondoa kinara chao.
Wale wanaoitumikia injili kwa furaha na katika uvumilivu wataweza kukubaliana na mauaji ya kuifia-dini kwa hiari yao kwa sababu watakuwa hawajauacha upendo wao wa kwanza. Kwa kuwa watu hawa walibarikiwa na Mungu kwa kuamini na kuuhubiri upendo wa Kristo, basi ni hakika kuwa watu hawa wanaweza kuuawa na kuifia-dini. Haijalishi jinsi ulivyo na uwezo au jinsi ulivyo na karama; ikiwa hauienezi injili ya maji na Roho, basi ni hakika kuwa kanisa litaondolewa toka mahali pake. Huu ni ujumbe muhimu sana ambao Mungu anataka tuufahamu. Ikiwa tutautambua na kuuamini ukweli huu, basi ni hakika kuwa tunaweza kuifanya mioyo yetu kuwa mipya katika nyakati za mwisho na tutaweza kuifia-dini kwa ajili ya jina la Bwana.
Je, msingi wa asili unaoiwezesha imani yetu ni nini? Ni injili ya maji na Roho. Kama isingelikuwa injili ya maji na Roho, basi matendo yetu ya imani yangelikuwa na faida gani? Sababu inayotufanya tuweze kuitunza imani yetu ni kwamba Mungu ametupenda na ametukubali na kutukumbatia katika mikono yake kwa injili yake ya maji na Roho. Kwa kuwa upendo huu ni upendo usiobadilika unaotutukuza, basi ndio sababu tunaweza kuitunza imani yetu na kuendelea kuieneza.
Pamoja na madhaifu yetu, tunaweza kumkimbilia Mungu hadi mwisho, hii ni kwa sababu injili ya maji na Roho imetuokoa, na kwamba katika injili hii kunapatikana upendo wa Kristo. Tuna mapungufu mengi sana, lakini kwa kuwa tumefunikwa katika injili ya maji na Roho ambayo imejawa na upendo wa Bwana wetu, basi sisi nasi tunaweza kuwapenda kaka na dada zetu, tunaweza kuwapenda watumishi wa Mungu, na tunaweza kuzipenda nafsi nyingine zote za hapa ulimwenguni. Kimsingi, upendo mkamilifu upo nje ya uwezo wa mwanadamu. Hii ni kwa sababu hakuna upendo kati yetu, yaani hatuwezi kupendana wala kuwapenda wengine zaidi ya kujipenda wenyewe katika ubinafsi. Watu wengi wanadanganywa na kile kinachoonekana hadharani, wanaangalia uso wenye tabasamu ambapo tabasamu hilo lipo kwenye ngozi ya uso tu. Wanawafikiria watu kutokana na mali au mwonekano wa nje walionao. Lakini upendo wa Mungu upo miongoni mwa waamini wa kweli. Hiki ndicho kinachotuwezesha kuieneza injili, ambayo ni upendo mkamilifu wa Bwana wetu.
Bwana wetu alikuja hapa duniani, alibatizwa ili kuyapokea mapungufu yetu yote, na alitusafisha toka katika dhambi zetu zote ili aweze kutuokoa. Inawezekanaje basi kwa sisi kuuacha upendo wake wa kwanza ambao umetufanya sisi kuwa watoto wa Mungu? Tunaweza kupungukiwa na mambo mengi, lakini hatupaswi kupungukiwa imani katika ukweli huu. Ni lazima tuihubiri injili hii hali tukiwa na imani kamilifu. Kinachohitajika sana katika zile nyakati za dhiki ni imani kamilifu katika injili hii ya maji na Roho. Tunapokutana na majaribu na dhiki, basi ile nguvu ya kuilinda imani yetu na kuyashinda magumu itatoka ndani ya imani inayoamini katika injili ya maji na Roho. Ni kwa nguvu ya injili hii ndipo sura zetu zinapoweza kung’aa kwa furaha hata pale tunapochoka kutokana na mahangaiko mengi tunayokutana nayo katika maisha yetu ya kila siku. Huu ndio upendo wa Bwana wetu.
Wakati mwingine watu wanaangukia katika mtego wa maisha ya kisheria. Wanafikiri kuwa Mungu amewabariki kwa sababu ya yale waliyoyafanya. Kwa kweli siwezi kusema kuwa kufikiri hivyo ni mbaya kabisa, lakini Bwana amesema kuwa atawapenda wale wampendao. Lakini Mungu ametupenda na kutufanya tusio na dhambi si kwa sababu ya yale tuliyoyafanya. Kwa kuwa Mungu anazifahamu ahadi zote alizotuahidia, na kwa sababu anazifahamu dhambi zetu zote, basi Mungu ametukubali katika mapenzi na upendo wake mkamilifu na ametufanya sisi kuwa wakamilifu. Ni kwa sababu ya baraka zake ndipo tunapoweza kuishi kwa furaha. Ni kwa sababu Mungu ametufanya sisi kuwa watu wake na watumishi wake ndio maana tunaweza kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tunaweza kuvishwa utukufu wake, tunaweza kuihubiri injili kwa wengine, na wakati utakapowadia, tutauawa na kuifia-dini kwa ajili ya jina lake. Mungu ndiye anayetuwezesha sisi kuyafanya haya mambo yote.
Katika filamu ya Quo Vadis, je wale wanawake walipata wapi nguvu ya kuimba nyimbo za sifa kwa Bwana hata pale walipokuwa wakiuawa? Walipata nguvu katika upendo wa Bwana. Kwa kuwa upendo wa Kristo ulikuwa mkubwa sana, basi ndio maana waliweza kukubaliana na kuifia-dini hali wakiimba nyimbo za sifa.
Kanuni hiyo hiyo inatumika pia katika maisha yetu. Tunayaishi maisha yetu kwa sababu Bwana ametuwezesha kufanya hivyo; sisi hatuishi kama watoto na watumishi wa Mungu kwa sababu ya matendo yetu binafsi. Hatujafanya lolote lile linalotustahilisha kuwa watoto na watumishi wa Mungu. Sisi tunaweza kumfuata Bwana hadi mwisho hata pale tunapojikwaa katika nyakati mbalimbali kwa sababu ya upendo mkamilifu wa Mungu usiobadilika. Nguvu hizo tunazozipata si nguvu zetu binafsi bali ni nguvu za Mungu. Kuifia-dini kunawezekana kwa kupitia upendo wa Mungu tu ambao umetufanya sisi kuwa wakamilifu—ni kwa neema ya Mungu tu ndipo tunapoweza kukubalina na kuifia-dini. Kumbuka ukweli huu kwamba ni Mungu ndiye anayekuwezesha wewe kuifia-dini, na kwa sababu hiyo usipoteza muda wako kwa kujaribu kujiandaa kuifia-dini kana kwamba kuna kitu unachoweza kufanya kuhusiana na hilo. Ni imani yetu katika injili ya maji na Roho ndiyo itakayotuwezesha kumsifu Bwana hadi pumzi yetu ya mwisho.
Bwana aliyaambia makanisa saba ya Asia kuwa: “Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.” Mti wa uzima unapatikana katika Mbingu na Nchi Mpya. Huko kuna kiti cha enzi cha Mungu, nyumba zilizojengwa kwa mawe yenye thamani, na maji ya uzima yanatiririka. Mungu amewaadia paradisho yake wale wote watakaoshinda ambako wataishi milele pamoja naye katika ukamilifu.
Wale watakaoshinda wanafanya hivyo kwa imani yao katika injili ya maji na Roho. Kitu kingine chochote hakiwezi kumfanya mtu ashinde bali ni hii injili ambayo inaweza kupatikana kwa nguvu za Mungu tu na wala si kwa nguvu za mwanadamu. Nguvu inayotuwezesha kushinda inatoka kwa Mungu tu. Ni lazima tutambue na kukubali jinsi injili ya maji na roho ilivyo kubwa na jinsi wokovu wa Mungu na upendo wake ulivyo mkuu; hii ni kwa sababu ni injili hii ndiyo inayoweza kutupatia imani inayoweza kukubaliana na kuifia-dini. Sisi sote tunaweza kuwa wadhaifu, tusio na vipawa, tusio na karama, tusioweza, wajinga na wasiofahamu kitu, lakini ukweli ni kuwa bado tuna ile nguvu, kwa maana tuna ile injili ya maji na Roho katika mioyo yetu.
Majina ya wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho yameandikwa katika Kitabu cha Uzima. Kwa upande mwingine, mtu yeyote ambaye jina lake halijaandikwa katika Kitabu cha Uzima ataanguka na kusalimu amri mbele ya Shetani. Ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndio ambao hawatamsujudia Ibilisi. Ni lazima uhakikishe kuwa jina lako limeandikwa katika Kitabu cha Uzima.
Tutakapouawa na kuifia-dini, itakuwa hivyo kwa sababu ya imani yetu ambayo ni upendo wa kwanza wa Kristo ambao Bwana wetu ametupatia. Tunaweza kusubiria kifo chetu cha kuifia-dini pasipo hofu wala woga kwa sababu tunaamini kwamba Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu atatupatia nguvu ya kukabiliana na mauaji ya kuifia-dini. Kwa kuwa mateso ya kuifia-dini hayawezi kulinganishwa ule utukufu wa mbinguni ambao unatungojea, basi hatuwezi kuogopa mbele ya kifo na badala yake tutakubaliana na kuifia-dini kwa ujasiri ili kuilinda injili ya thamani. Sasa ni lazima tuachane na kuwaza jinsi tutakavyoweza kuuawa na kuifia-dini, maana sisi hatutaweza kuifia-dini kwa sababu ya jitihada zetu bali ni kwa sababu ya nguvu za Mungu.
Ninaamini kuwa siku moja tangazo lifuatalo litakuja kutolewa katika vipaza sauti: “Wapendwa wananchi, leo ni siku ya mwisho kuipokea alama. Ni wananchi wachache tu ndio wanaopaswa kuipokea alama hiyo leo hii. Kwa kweli tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu hadi sasa. Kwa kweli kuipokea alama ni jambo jema kwako kwa sababu litasaidia katika kuleta nidhamu katika nchi yetu. Kwa hiyo, tafadhali njooni katika ukumbi wa jiji ili mweze kuipokea alama haraka kadri inavyowezekana. Ninawakumbusha tena kuwa leo hii ni siku ya mwisho ya kuipokea alama. Wale ambao watakuwa hawajaipokea alama hadi muda utakapokwisha wataadhibiwa vikali. Hivyo, ili kuweka mambo wazi, nitaita majina ya wale ambao bado hawajaipokea alama.” Kwa kweli haya ni mawazo yangu ya kufikirika, lakini ni hakika kuwa mambo ya jinsi hiyo yatakuja kutokea hapo baadaye.
Waamini wa Kanisa la Mwanzo walitambuana wao kwa wao kwa kutumia alama ya samaki. Alama hii ya samaki ilikuwa ni namba ya siri miongoni mwao. Sisi nasi tutapenda kuwa na alama ambayo itatusaidia katika kuwatambua kaka zetu na dada zetu ili kwamba tuweze kutiana moyo katika kukubaliana na kuifia-dini
Kwa kuwa kuifia-dini si kitu ambacho tunaweza kukifikia kwa jitihada zetu wenyewe, basi tunaweza kuachana na hofu zetu na kisha kukabiliana na kuifia-dini kwa ujasiri. Hakuna cha kuogopwa mbele ya kifo chetu cha haki. Kitu pekee tunachopaswa kukifanya ni kuishi kwa ajili ya Bwana tunapokuwa hapa duniani. Tunaweza kujitoa kwa Bwana kwa sababu tunafahamu kuwa tumepangiwa kuifia-dini kwa ajili ya jina la Mungu wetu. Ni lazima utambue kuwa ikiwa utajaribu kukwepa kuifia-dini kwa hofu ya kuogopa kupoteza mali zako, basi ni wazi kuwa utakabiliana na mateso makuu na mahangaiko. Ni lazima mfanyike kuwa watu wa imani ambao hali wakifahamu kuwa watauawa na kuifia-dini kwa ajili ya Kristo, wanaishi maisha yao kwa ajili ya Bwana hadi mwisho.
Tunapotambua kuwa tutauawa na kuifia-dini, basi ni hakika kuwa tutakuwa na busara zaidi katika imani yetu, katika akili, na katika maisha yetu halisi. Ufahamu huu ni tiba ya ujinga wetu inayoturuhusu kuishi katika mambo yote yanayousubiri ulimwengu. Hii haimaanishi kuwa tutapaswa kuikana imani yetu, bali ina maanisha kuwa tunapaswa kuishi kwa ajili ya Bwana. Sisi tutaendelea kuishi kwa ajili ya Bwana ambaye ametuokoa, tutapambana na kumshinda Shetani na Mpinga Kristo, na tutampatia Mungu utukufu wote wa ushindi hadi nguvu za Mungu zitakapomtupa Shetani katika shimo lisilo na mwisho. Mungu anatutaka sisi ili tumtukuze. Ninamshukuru Bwana kwa kuturuhusu kumpatia Mungu utukufu kwa imani yetu.
Tunaamini kuwa hivi punde Bwana atarudi ili kutuchukua. Wakati roho nyingi zitakamporudia Mungu katika nyakati za mwisho, Mungu atazipokea roho hizo zote katika mikono yake na kuzichua kwenda mbinguni. Kama Mungu alivyosema kwa Kanisa la Filadelfia katika Ufunuo 3:10, “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.” Ni hakika kuwa Mungu atalitimiza Neno lake la ahadi.
Kule kusema, “umelishika neno la subira yangu,” Mungu anazungumzia juu ya maisha ya uaminifu ya watakatifu. Ina maanisha kuwa waliishikilia kwa subira imani yao bila kujalisha kile ambacho wengine walikuwa wanasema au kuwatendea. Mungu anaposema kuwa “nitakulinda utoke katika saa ya kuharibiwa,” ana maanisha kuwa wale waliolishika neno la subira yake wataepushwa toka katika majaribu ya kiimani.
Kwa maneno mengine, wakati muda wa dhiki na mauaji ya kuifia-dini utakapowadia, Mungu atatulinda na kutusafisha wakati tutakapokuwa tukiendelea katika maisha yetu ya kila siku ya huduma na maombi. Tunapojipanga katika akili zetu kuwa tutapaswa kuuawa na kuifia-dini, basi mioyo yetu itasafishwa toka katika uchafu wote na kwa matokeo hayo imani yetu itakuwa na nguvu zaidi. Ni lazima tuishi maisha yetu ya sasa ya imani mbele za Mungu hali tukikumbuka ahadi ya Mungu kuwa, kwa kuifia-dini, sisi sote tutaepushwa tusiingie katika saa ya kuharibiwa. Kwa kifupi, ni lazima tuishi kwa imani.
Wakati wa sasa ni wakati wa Ufunuo. Kuna Wakristo wengi wajinga ambao hali wakilidharau Neno la Mungu, wanaendelea kuishikilia kwa nguvu imani yao potofu juu ya fundisho la kunyakuliwa kabla ya dhiki. Wakati siku ya mwisho itakapowadia, hapo ndipo watakapotambua jinsi walivyokuwa na makosa. Siku zao za ushawishi na mamlaka zimeshakaribia kwisha; kitu pekee tunachopaswa kukifanya ni kuishi katika uhakika wa tumaini letu kwamba Mungu atalitimiza Neno lake la ahadi.
Tutakapofikia nusu au katikati ya Dhiki Kuu, sisi sote tutauawa na kuifia-dini ili kuilinda imani yetu, na kabla mapigo ya mabakuli sana hayajaanza, Mungu atatunyakua sote mawinguni na kisha tutaingia katika Ufalme wa Milenia. Wakati tumaini letu ya kutawala pamoja na Kristo litakapokuwa limeonekana, basi mateso yetu hapa duniani yatakuwa ni kama yamefidiwa na thawabu ambazo zinatungojea, na hatimaye kule kuingia katika Mbingu na Nchi Mpya kutatufanya tuwe na furaha kubwa isiyoelezeka. Leo hii tunaishi kwa imani, tunaishi kwa ajili ya Bwana hali tukiwa na tumaini la kutimizwa kwa ahadi hii ya Mungu. Hali tukimtumainia Bwana kuzitimiza ahadi zake, basi tunaendelea kuishi kwa matarajio yenye shauku ya kuiona siku ambayo tutaweza kuishi pamoja na Mungu milele katika miili yenye utukufu. 
Ninamshukuru Bwana kwa kutupatia injili ya ondoleo kamilifu la dhambi, kwa kutuwezesha kukubaliana na mauaji ya kuifia-dini ili kuilinda imani yetu kwake, na kwa kutufanya kusimama miongoni mwa waliobarikiwa.
 

Usuli wa Kanisa la Efeso
 
Efeso ulikuwa ni mji wenye bandari kubwa katika eneo la Asia Ndogo ambalo lilikuwa ni sehemu ya Dola ya Rumi, ulikuwa ni kituo mashuhuri cha biashara na shughuli za kidini. Katika wakati wa Kanisa la Mwanzo, ulikuwa ni mji wa kimataifa uliokuwa ukikua sana; upande wa kaskazini wa Efeso kulikuwa na mji wa Smirna na upande wake wa kusini kulikuwa na mji wa Mileto. Kwa mujibu wa maelezo ya kisasili, yaani maelezo yanayoambatana na miujiza, Amazoni, aliyekuwa mungu mke mashuhuri wa vita aliujenga mji huu katika karne ya 12 K.K kisha akampatia mji huo Androklusi aliyekuwa mwana wa mfalme wa Athene.
Kwa upande wa mali, Efeso ulikuwa ni mji wenye mafanikio sana kitu ambacho kina maanisha kuwa ulikuwa ni mji wa kidunia sana. Hii ndio sababu Mungu aliliambia Kanisa la Efeso kupambana hadi mwisho na kumshinda Shetani ili kwamba lisiweze kuipoteza injili yake ya maji na Roho. Ni lazima tutambue jinsi Neno la Mungu la kweli lilivyo la muhimu na ni lazima tuilinde imani yetu kwa nguvu zote.
Mungu aliliandikia Kanisa la Efeso kwa kupitia Mtume Yohana kuwa: “Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.” Kanisa la Efeso lilisifiwa na Mungu kwa ajili ya matendo yake, uvumilivu, kwa kutoyavumilia maovu, na kwa kuwajaribu na kuwagundua mitume wa uongo, kwa kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya jina la Mungu kwa subira na uvumilivu.
Lakini Kanisa la Efeso pia lilikemewa kwa matendo yake mabaya. Kama kifungu hiki kinavyoendelea kusema: “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu..”
Katika kifungu hicho hapo juu, Mungu anasema kuwa anawachukia Wanikolai. Wanikolai wanaotajwa hapa ni kundi fulani la waamini ambao walikuwa wamesimama kinyume na Mungu, kinyume na Kanisa lake, na kinyume na ukweli wa Mungu. Yale ambayo Wanikolai waliyafanya yameelezwa kwa kina katika kifungu cha maandiko kilichokuwa kimeelekezwa kwa Kanisa la Pergamo. 
 

Makosa ya Wanikolai 
 
Ufunuo 2:14 inasema, “Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.” Rejea ya Biblia ya kifungu hiki inaweza kupatikana katika Kitabu cha Hesabu sura ya 22 ambapo habari kuhusu Balaki, aliyekuwa mfalme wa Wamoabu imeandikwa.
Wakati Waisraeli walipokuwa wameufikia uwanda wa Moabu huko Kanaani baada ya kutoka Misri, walikuwa wamesha yashinda makabila saba ya nchi ile “kama fahari anavyopura majani ya kondeni.” Akiwa ameusikia ushindi huo, Balaki alimwogopa sana Mungu wa Israeli, kwa kuwa aliogopa kuwa hatma ya Wamoabu itakuwa kama ya yale makabila yaliyokwisha shindwa ya Kanaani. Ili kujaribu kuwapotosha Waisraeli na kisha kuwazuia wasiwashinde, Balaki alimwita Balaamu, aliyekuwa nabii wa uongo ili kwamba aweze kuwalaani Waisraeli kwa niaba yake.
Balaamu alikuwa ni nabii wa uongo, lakini watu Wamataifa walidhani kuwa alikuwa ni mtumishi wa Mungu. Yeye hakuwa mzao wa Kuhani Mkuu Haruni wala hakuwa Mlawi. Lakini Balaki mfalme wa Wamoabu, aliamini kuwa wale ambao Balaamu aliwabariki watabarikiwa na wale ambao atawalaani watalaaniwa. Kwa wakati huo, Balaamu alijulikana katika nchi nzima kuwa ni mchawi mashuhuri sana
Lakini Balaamu hakukubaliana na yale ambayo Mfalme Balaki alikuwa amemwomba ayafanye. Hii ni kwa sababu Waisraeli walikuwa ni watu wa Mungu, na kwamba Mungu asingelimruhusu Balaam kuwalaani Waisraeli na pia kujaribu kufanya hivyo kungeliifanya ile laana kumwishia yeye mwenyewe. Hali akiwa ameshangazwa na nguvu za Mungu, Balaamu hakuweza kufanya lolote zaidi ya kuwabariki Waisraeli. Hali akiwa amechukizwa na jambo hili, Balaki alimwomba Balaamu kuwalaani Waisraeli toka mahali ambapo hakuweza kuwaona. 
Balaamu alipokea kiasi kikubwa cha hazina toka kwa Balaki na kisha akamfundisha Balaki namna ya kuweza kuwalaani Waisraeli. Mpango wenyewe ulikuwa ni wa kuwafanya Waisraeli kufanya uzinzi kwa kuwaalika katika sherehe za Wamoabu na kisha kuwapatia wake zao, ili kwamba Waisraeli waweze kuadhibiwa na Mungu kwa dhambi zao. Hivi ndivyo nabii wa uongo Balaamu alivyomfundisha Balaki kuleta maangamizi kwa Waisraeli. 
Mungu alisema kuwa anamchukia Balaamu kwa sababu Balamu alikuwa ni mtu aliyependa fedha. Kuna watu wengi katika jumuia za Kikristo ambao wapo kama Balaamu. Kwa kweli wao ni manabii wa uongo, lakini wengi wao wanaheshimika sana. Lakini kile ambacho Balaamu alikitafuta ni kuwa na mali. Wakati alipojazwa fedha, alibariki na wakati aliponyimwa fedha alilaani. Ni jambo la aibu na kusikitisha kuona kuwa katika jamii ya Kikristo siku hizi kuna watu wengi sana ambao walipaswa kuwa watumishi wa Mungu wapo kama Balaamu. Inapotokea kuwa waamini wanaomwamini Mungu wanaishia kutafuta kupata vitu au mali, basi watajikuta wakiishia kuwa kama manabii wa uongo. Hii ndio sababu Mungu aliwachukia Wanikolai.
Je, unafahamu kinacholeta maangamizi katika kanisa la Mungu na watumishi wake? Ni tamaa ya fedha. Wale wanaotafuta kupata mali watakabiliana na maangamizi yao mbele za Mungu.
 

Makanisa Yanayomfuata Balaamu
 
Siku hizi, kama ilivyokuwa katika nyakati za Mitume, kuna makanisa mengi ya kidunia na watumishi wa uongo wanaoifuata njia ya Balaamu. Wanatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa wanavuna fedha toka kwa wafuasi wao. Kwa mfano, kuna huu msukumo wa kuwafanya waumini kushindana wao kwa wao ili kuithibitisha imani yao si kwa mtazamo wa kiroho bali kwa utoaji wa mali na sadaka, kana kwamba utoaji wa sadaka ndio kipimo cha imani. Lengo pekee la kuukazania mtazamo huu ni kwa lengo la kulitajirisha kanisa huku wakimaanisha kuwa imani ya wale waliotoa zaidi ni kubwa kuliko ya wale waliotoa kidogo jambo ambalo si kweli.
Kwa kweli ni jambo zuri sana ikiwa waamini wanaamua kumtumikia Mungu na injili yake kwa mioyo yao yote. Lakini manabii wa uongo kama Balaamu wanafanya mchezo wa mawindo kwa waamini ili kuyajaza matumbo yao binafsi. Wanawahamasisha wafuasi wao ili waweze kushindana katika utoaji wa vitu na katika kushuhudia juu ya utoaji kama vile, “Nilitoa zaka zangu kwa uaminifu, na kwa sababu hiyo Mungu amenibariki mara kumi katika biashara yangu.” Hali wakiwa wamedanganywa na Balaamu, waamini hao hufikiri kuwa hii ndiyo njia sahihi ya kwenda katika imani ya kweli wakati njia hiyo ni kuelekea katika umaskini wao wa kiroho na wa kimwili, katika majivuno binafsi, na hatimaye katika maangamizi yao.
“Matendo ya Wanikolai” si mengine zaidi ya matendo ya Balaamu. Kama vile Balaamu, katika tamaa yake alivyomfundisha Balaki ili kuweka ukwazo mbele ya Waisraeli, basi wengi wanaodai kuwa ni watumishi wa Mungu katika jamii ya Wakristo wanavutiwa zaidi na mifuko ya fedha ya waumini wao. Wale wanaopotoshwa na hawa manabii wa uongo wanaishia wakiwa hawana kitu baada ya kuwa wamevitoa vitu vyao vyote kwa wachungaji hawa wa uongo, lakini jambo baya zaidi ni kuwa muda si mrefu wataweza kufahamu na kutambua kuwa kile walichokuwa wakikiamini ulikuwa ni uongo kabisa. Hatimaye, watalilaumu kanisa la uongo na kuishia kuikana imani yao. Kwa bahati mbaya, ukweli wa kuhuzunisha ni kuwa hali hii ya kusikitisha inapatikana pia katika makanisa yanayojiita kuwa ni ya kiinjili. Hali wakidanganywa na Balaamu, waamini wengi wamepotoshwa na utapeli huu na mwishowe huishia wakiliacha kanisa. 
Maandiko yanatueleza kuwa Mungu anayachukia matendo ya Wanikolai. Ikiwa tutawafuata Wanikolai, basi ni hakika kuwa tutaipoteza imani yetu katika Mungu. Tuna shuhuda nyingi ambazo Mungu ametupatia, na shuhuda hizo ni hazina zinazotujenga kiroho. Lakini suala la kufuata mapato ya mali kwa kutumia shuhuda hizo ni jambo ambalo tunapaswa kuachana nalo kabisa, kwa kuwa hayo ni matendo ya Wanikolai ambayo yanachukiwa na Mungu mwenyewe.
 

Imani na Matendo 
 
Mungu alionya dhidi ya matendo ya Wanikolai kwa makanisa yote saba ya Asia. Kwa nyongeza, Mungu aliwaahidi kuwa wale watakaoshinda watakula matunda ya mti wa uzima. Tunapomtumikia Bwana, basi tunafanya hivyo kwa imani kwa sababu ya shukrani zetu kwake kwa ukombozi aliotupatia na kwa ufahamu unaotuwezesha kuieneza injili ya maji na Roho. Hatumtumikii Mungu ili kujionyesha kwa wengine, au kutufanya sisi tuonekane kuwa ni wema kwa namna yoyote ile. Kufanya hivyo si huduma ya kweli na wala si imani ya kweli. Katika kanisa la Mungu ni lazima tuwe waangalifu sana kuhusu matendo haya ya Wanikolai. Hii ndio sababu Bwana aliyaonya makanisa yote saba ya Asia kuhusu Wanikolai.
Je, unafahamu ni kwa nini makanisa mengi ambayo si makanisa ya waliozaliwa upya yameweza kukua kwa haraka sana? Makanisa haya yamekua haraka kwa sababu ya imani na shuhuda za uongo. Watumishi wa Mungu hawapaswi kujinufaisha toka kwa waumini wao kwa nia ya kuyajaza matumbo yao.
Imani ya kweli ni kuamini katika wokovu ambao Mungu ametupatia kwa ubatizo wa Yesu, kwa damu yake Msalabani, na kifo chake kwa niaba yetu. Lakini makanisa mengi yakiwemo ya waliozaliwa tena upya na yale ya wale ambao hawajazaliwa tena upya yanatumia shuhuda ili kuiteka mifuko ya waumini wao. Ni lazima uwe mwangalifu na mwenye hekima kutambua kuwa shuhuda za kweli zinaijenga imani yako na zinamtukuza Mungu wakati zile shuhuda za uongo zitakuwa ni mtego kwako.
Makanisa yote ambayo ni matajiri sana katika ulimwengu wa sasa yanaongozwa na watumishi walio kama Balaamu. Viongozi wa kanisa wanaoifuata njia ya Balaamu wanayatumia makanisa yao kuwanyonya wafuasi wao ili kuongeza mapato yao. Viongozi wa Kikristo kama Balaamu wananyakua fedha toka kwa waumini wao kwa kuwahamasisha katika mashindano ya ushuhuda wa utoaji mali. Kwa kweli ninayapinga matendo yao kwa nguvu zote.
Maisha ya kweli ya imani hayaanzi na kitu kingine zaidi ya imani. Ni lazima tuwe na hekima ya kutosha ili kuweza kuikwepa mitego ya Wanikolai ambayo Shetani ameitega. Kila mtu ni lazima afahamu jinsi matendo ya Wanikolai yalivyo, na asidanganywe kamwe na watumishi wa Shetani ambao tamaa yao haina hata mpaka. Watumishi wa Mungu wanapaswa kuwa waangalifu sana kuhusiana na jambo hili. Umakini huu unawahusisha pia watumishi wa kanisa. Inapotokea kuwa watumishi wa Kanisa wameelemewa sana na upatikanaji wa mali—yaani kuhusu magari wanayoendesha, jinsi nyumba zao zilivyo kubwa, jinsi wanavyomiliki mashamba, jinsi akaunti zao benki zilivyojaa fedha—basi ni hakika kuwa watumishi hao watafanya makanisa yao kuanguka na kuwapeleka katika njia ya Wanikolai.
Mungu aliyaambia makanisa saba ya Asia kuwa makini sana kuhusiana na jambo hili. Mtu anayeifuata imani ya Balaamu analenga katika kupata mali, utukufu binafsi, na hatimaye anaazimia kuwa mwanzilishi wa kikundi au dhehebu la dini. Kanisa la Mungu halipaswi kuangalia mapato ya mali. Kama Mungu alivyotuahidi kuwa atawabariki wale wanaoifuata injili ya maji na Roho, basi tunapaswa kutumia mali zetu katika kuieneza injili na wala si kuzihifadhi katika dunia hii
 

Wakatae Wachungaji wa Uongo
 
Hata waamini waliozaliwa tena upya watakuwa wameangamia ikiwa watakamatwa katika mitego ya Wanikolai. Mwanzoni wanaweza kufikiri kuwa imani ya viongozi hao ni kubwa sana na yenye nguvu, lakini hatimaye uongo wa wachungaji hao wa uongo utawapeleka katika maangamizi yao.
Mungu alimwambia malaika wa Kanisa la Efeso kuwa aliyachukia matendo ya Wanikolai. Ni hakika kuwa yeyote aliyetegwa na kunaswa na Wanikolai atakabiliana na taabu. Mtu yeyote yule bila kujalisha kuwa ni mwamini aliyezaliwa tena upya, mtumishi wa Mungu, au mtu yeyote yule, ikiwa atakuwa amekamatwa katika mtego wa Wanikalai basi ni vema atambue kwa hakika kuwa ataangamia. Kama mchungaji mbaya anavyoliongoza kundi kwenda katika mauti, basi vivyo hivyo, manabii wa uongo wanaleta laana. 
Hii ndio sababu Mungu aliwaambia watumishi wake “lisha kondoo zangu.” Watumishi wa Mungu ni lazima wawachunge waamini kama vile wachungaji wanavyowachunga kondoo, huku wakiwalinda katika hatari na kuwahudumia mahitaji yao. Kama wachungaji, ni lazima wahakikishe kuwa mifugo yao haiendi ovyoovyo, ni lazima watafakari hatari ambazo zinaweza kuwapata, na kisha kuwazuia ili wasiweze kuzikaribia hatari hizo
Nilisikia toka kwa watu wanaofuga kondoo kwamba ni miongoni mwa wanyama wagumu sana. Je, sisi si kama kondoo hawa wakaidi mbele za Mungu? Mungu alikuwa na sababu nzuri alipoutumia mfano wa kondoo katika kutuelezea, kwa kuwa kimsingi anatufahamu jinsi tulivyo wagumu.
Kwa nini Mungu anayazungumzia matendo ya Wanikolai, Yezebeli na Balaamu kwa kuyarudia rudia kwa makanisa saba ya Asia? Kwa nini anaahidi kuwa kwa wale watakaoshinda atawapatia matunda ya mti wa uzima? Mungu alifanya hivyo ili kutufundisha kuwa makini na kujilinda dhidi ya upotoshaji wa manabii wa uongo. Ni lazima tulitafakari Neno la Mungu na kisha tujiulize, “Je, injili ya kweli ya maji na Roho ni kitu gani?” Injili si kulichanganya Neno la Mungu na baadhi ya ufahamu wa wanadamu na kisha kulirasimisha. Kuna mahubiri mengi ambayo ni mazuri sana katika Ukristo wa leo ambayo hayaelezi chochote kuhusu injili ya maji na Roho. Wahubiri wengi mashuhuri wana waandishi wao maalum wa mahubiri ambao huandika mahubiri kwa niaba yao, na kwa sababu hiyo wao wanachokifanya ni kusoma yaliyoandaliwa na mtu fulani.
Hatupaswi kamwe kutegwa na kukamatwa na Wanikolai. Kanisa la walizoaliwa tena upya ni lazima liwe na uangalifu sana ili kutofuata mapato ya mali; watumishi wa kanisa ni lazima wawe makini katika hilo, na pia kila mtu katika kusanyiko la waamini anapaswa kuwa makini. Kujaribu kuvuna fedha toka kwa waumini wa kanisa, kulifanya kanisa kuwaza juu ya mali, na kujenga majengo ya kanisa ambayo yanaonekana kama ikulu kuliko kuonekana kama mahali pa kuabudia—hali wakihubiri kuwa kuja kwa Bwana kunakaribia!—basi ukweli ni kuwa matendo hayo yote ni matendo ya imani ya uongo na kwa hakika ni matendo ya Wanikolai. 
Ni lazima tuwe makini na wachungaji wa uongo, na ni lazima tuhakikishe kuwa hatudanganywi na kisha kuifuata imani yao. Kwa kweli watakatifu wanapaswa kuepuka tamaa ya kupenda fedha. Bali tunachopaswa kukipenda na kukitunza ni injili ya maji na damu, ambao ni upendo wa kwanza wa Mungu. Ni lazima tuishi maisha yetu ya uaminifu hali tukiushikilia ukweli kuwa Mungu ametuokoa kwa maji na damu ya Kristo hadi siku ile tutakapokutana naye. Ni lazima tuliamini Neno la Mungu kuwa Yesu amezichukulia mbali dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kifo chake Msalabani.
Wale wanaowafuata Wanikolai hawaihubiri kamwe injili ya maji na Roho. Wao hawapendi kujihusisha na kazi za injili ya maji na Roho, bali wanapenda kuingiza fedha tu. Hawa ndio akina Balaamu wa leo, wanaoweka ukwazo mbele ya Waisraeli na kisha kuwapotosha na kuwapeleka katika maangamizi yao. Unapaswa kulikumbuka jambo hili.
Hatimaye Balaamu aliuawa na Yoshua. Kama Kitabu cha Yoshua kinavyoeleza, huyu nabii wa uongo aliuawa na upanga wa Yoshua wakati Waisraeli walipoishinda Kanaani. Balaamu aliuawa kwa sababu hakuwa mtumishi wa kweli wa Mungu. Wale wote wanaolitumia jina la Kristo kuwanyonya wakristo waaminifu na kisha kuyalisha matumbo yao binafsi, basi hao ndio akina Balaamu wa leo. Ni lazima tukumbuke kuwa Balaamu alitumia kila mbinu ili kuiridhisha tamaa yake.
Mungu aliwaambia watumishi wa Kanisa la Efeso kuwa, “Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.” Kwa lugha nyingine, kifungu hiki kinaamanisha pia kuwa wale wanaosita na kushindwa watakufa. Kitendo cha kuifuata njia ya Balaamu ni kushindwa, na ni njia ya kuelekea katika mauti. Mungu alitupa Neno lake la tahadhari ili kwamba tusiangukie katika mtego wa Wanikolai, na kwa kweli ninamshukuru Mungu kwa hilo. Nina tumaini na ninaomba ili kwamba usisalimu amri kwa majaribu ya mali na hatimaye kuishia kukataliwa na Mungu kwa sababu tu ya tamaa zako.