Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[2-3] Barua Kwa Kanisa la Smirna (Ufunuo 2:8-11)

(Ufunuo 2:8-11)
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahaudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. ”
 

Mafafanuzi 
 
Aya ya 8: “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.”
Kanisa la Smirna lilianzishwa wakati Paulo alipokuwa akihudumu katika Kanisa la Efeso. Kwa mujibu wa kifungu hicho hapo juu, waumini wa kanisa hili walikuwa ni maskini na ambao walitukanwa na kudhihakiwa na Wayahudi kwa sababu ya imani yao. Uthibitisho wa jinsi kanisa hili lilivyoteswa na Wayahudi unaweza kuonekana kwa kupitia kuuawa kwa Polikap ambaye aliuawa kwa kuifia-dini akiwa ndiye askofu wa kanisa hilo katika kipindi cha Mababa wa Kanisa. Watakatifu wa Kanisa la Mwanzo walipata mateso mengi toka kwa waamini wa Kiyahudi ambao walimkataa Kristo kuwa ni Masihi wao. 
Kanisa la Smirna lilianzishwa na Mtume Paulo. Kwa kule kusema “yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai,.” Yohana ana maanisha kuwa ni Bwana aliyeuumba ulimwengu. Bwana wetu, aliyezaliwa na Bikira Mariam, alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana na alihukumiwa kwa ajili ya dhambi hizi kwa kuimwaga damu yake Msalabani. Kisha siku ya tatu akafufuka toka kwa wafu na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yesu anazungumza na malaika wa kanisa la Mungu si tu kama Mwokozi bali kama Mungu Mwenyezi.
 
Aya ya 9: “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahaudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.”
Bwana aliyatambua magumu yote na mateso ambayo Kanisa la Smirna lilikutana nayo. Pamoja na kuwa lilikuwa ni kanisa maskini kwa maana ya mali au vitu, ukweli ni kuwa kanisa hili lilikuwa ni tajiri sana kiroho. Katika mji wa Smirna walikuwepo Wayahudi wengi wakiishi ambao Mungu anawataja kama “hao wasemao ya kuwa ni Wayahaudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.” Hawa Wayahudi walijitoa wao wenyewe kama zana za Shetani ili kuyatimiza malengo ya Shetani na kwa sababu hiyo waligeuka na kuwa ni kikwazo katika kuihubiri injili ya maji na Roho, huku wakilitesa kanisa la Mungu. Wayahudi hao waliamini kuwa wao walikuwa ni Wayahudi wa kiorthodoksi, na kwamba wao peke yao ndio walikuwa wana wa Ibrahimu. Lakini ukweli ni kuwa walishindwa kuifuata imani ya Ibrahimu na mbaya zaidi waliishia katika kumkataa Mungu halisi wa baba zao. Hali likiwa limeteswa kwa nguvu sana na Wayahudi, Kanisa la Smirna likajikuta likiwa maskini, lakini pamoja na hayo kanisa hilo lilikuwa ni kanisa ambalo lilikuwa na utajiri wa kiroho. 
 
Aya ya 10: “Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Mungu aliliambia Kanisa la Smirna kutoogopa “Usiogope mambo yatakayokupata” Pia aliliambia kanisa hilo kuwa “Uwe mwaminifu hata kufa,” na akaahidi kuwa atalipatia kanisa hilo “taji ya uzima.” Bwana alitambua kabla kuwa Shetani atawatisha baadhi ya watakatifu wa Kanisa la Smirna na kujaribu kuivunja imani yao. Hii ndiyo sababu Mungu aliahidi kuwa ikiwa watakuwa waaminifu kwake hadi kifo, basi atawapatia taji ya uzima. 
Kile ambacho Bwana anatueleza kwa kupitia kifungu hiki ni kuwa watumishi wa Mungu na watakatifu wake wanaoishi katika nyakati za mwisho na wao pia watateswa na Shetani na wafuasi wake. Lakini pamoja na mateso hayo tutakuwa na nguvu ya kuendelea kuwa waaminifu kwa Mungu hadi kifo, kwa kuwa nguvu hiyo inakuja kwetu kwa wingi toka katika imani yetu katika injili ya maji na Roho na tumaini letu kwa Mbingu Mpya na Nchi Mpya ambavyo Mungu ametuahidia.
 
Aya ya 11: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pi
Waamini wa nyakati za mwisho watahusika katika vita dhidi ya Mpinga Kristo na wale wanaosimama kinyume na Mungu. Mungu anatueleza kuwa wale walio na tumaini kwa injili ya kweli na Mbingu watashinda kwa imani yao. Mungu amemwezesha kila mwamini kuwashinda adui zake kwa kutupatia Neno lake la kweli na imani. Swali pekee linalobakia ni kuwa ikiwa tutakuwa upande wa Mungu na watumishi wake au la.
Warumi 8:18 inatueleza kuwa “nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.” Mateso tutakayoyapata toka kwa Mpinga Kristo na wafuasi wake yatadumu kwa muda mfupi, pengine hata kwa siku 10. Ukimtumainia Mungu unaweza kukivumilia kipindi hiki kifupi cha mateso, unaweza kumshinda Mpinga Kristo, na kisha ukamtukuza Mungu na kupokea Ufalme wake wa Milele kama thawabu yako. Mungu amewapatia watakatifu nguvu ya kushinda vita dhidi ya Mpinga Kristo.
Hebu tumshinde Mpinga Kristo kwa imani yetu katika injili ya maji na Roho, na hebu sisi sote tukutane tena katika Ufalme wa Milenia na katika Mbingu na Nchi Mpya na kisha kuishi kwa pamoja milele. Kifo cha kwanza kinachozungumzwa hapa ni kifo cha kimwili ilhali kifo cha pili ni kifo cha kiroho kikiandamana na adhabu ya milele huko kuzimu. Kwa watakatifu kuna kuuawa kwa kuifia-dini, kuna kifo chao cha kimwili, lakini hakuna kifo cha kiroho.
Ninamshukuru Mungu kwa kutupatia sisi waamini katika nyakati hizi za mwisho heshima na utukufu wa kuifia-dini kama alivyowapatia wafia-dini wa Kanisa la Mwanzo.