Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[7-2] Hebu Tuwe na Imani Inayopigana Vita (Ufunuo 7:1-17)

(Ufunuo 7:1-17)
 
Wakristo wa leo ni lazima waufahamu ukweli wa Biblia kiusahihi. Hasa, ni lazima tuwe na uelewa sahihi wa kunyakuliwa kwa watakatifu na kisha kuishi kwa imani kwa kupitia Neno la Ufunuo.
Kwanza kabisa, ni lazima tutambue kuwa kunyakuliwa kutatokea katikati ya kipindi cha Dhiki Kuu, yaani baada ya miaka mitatu na nusu kati ya ile miaka saba. Makanisa na watakatifu ni lazima wawe na imani inayoweza kupigana vita katika nyakati za mwisho, ili kuyatimiza mapenzi ya Mungu ya kumkomboa mwanadamu toka katika dhambi na kumpatia uzima wa milele kama alivyopanga katika Yesu Kristo.
Mungu aliruhusu shughuli au kazi za Mpinga Kristo ili kuyatimiza mapenzi yake. Kipindi ambacho Mpinga Kristo atainuka zaidi ni ile miaka mitatu na nusu ya kwanza kati ya ile miaka saba ya Dhiki Kuu. Mungu alimruhusu Mpinga Kristo kuufuatilia mwisho wake katika nyakati hizi. Kwa nini? Kwa sababu ili Mungu aweze kuyatimiza malengo aliyopanga kwa ajili yetu, basi ni lazima amfunge Shetani katika shimo lisilo na mwisho, na ili kufanya hivyo ni lazima Bwana arudi hapa duniani. Hii ndio sababu Mungu wetu alimruhusu Mpinga Kristo kuyafanya mambo yake kwa nguvu katika kipindi cha kwanza cha miaka mitatu na nusu kati ya ile miaka saba ya Dhiki Kuu.
Mungu alimpatia kila mtu Neno lake la ukombozi toka katika dhambi na uzima wa milele, na ili kulitimiza Neno hili, Mungu alipanga kuwepo kwa Dhiki Kuu. Katika kifungu kikuu cha maandiko katika sura hii, imeandikwa hivi, “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.” Pia Mungu amepanga kuwakomboa Waisraeli 144,000 toka katika maangamizi yao, kwa kuwa alimwahidia Ibrahimu kuwa atakuwa Mungu wake na Mungu wa uzao wake. Ili kuitimiza ahadi hii, Mungu ataitoa neema yake ya wokovu juu ya Israeli na atawakomboa watu 144,000 wa uzao wa Ibrahimu katika nyakati za mwisho.
Ili Mungu aweze kuwapatia watakatifu wake Ufalme wa Milenia na Mbingu na Nchi Mpya, basi kwa hakika Mungu ataruhusu Dhiki Kuu kuja duniani. Baada ya kuuruhusu wakati wa Mpinga Kristo katika kipindi cha Dhiki Kuu, Mungu atamkamata Shetani na kumfungia katika shimo lisilo na mwisho. Sababu inayomfanya Mungu kuruhusu uwepo wa Mpinga Kristo na Dhiki Kuu ni kwa ajili ya kuitimiza ahadi yake ya kuiokoa Israeli na kuwapatia neema yake ya uzima wa milele Wamataifa ambao watavikwa katika mavazi meupe kwa kupitia Dhiki Kuu.
Kwa hiyo, Dhiki Kuu na utawala wa Mpinga Kristo ni hatua ambazo tunapaswa kuzipitia. Ni lazima tutambue kuwa mambo haya yote ambayo Mungu ameyaruhusu ni sehemu ya mpango wake wa kutuokoa sisi sote na kutuvika katika neema yake ya uzima wa milele katika Ufalme wa Kristo. Hivyo, ni lazima tupambanue vizuri kuwa sasa tunaishi katika wakati upi na kisha tujiulize juu ya aina ya imani tunayopaswa kuwa nayo tunapoishi. Kwa ufupi, imani yetu ni lazima iwe wazi na ya uhakika.
Sisi tunaliamini Neno la Mungu. Pia tunaamini kuwa hili Neno litatimizwa, kimwili na kiroho. Wakati wa sasa tulio nao ni wakati ambao unaelekea katika nyakati za mwisho. Wakati Mpinga Kristo na wafuasi wake wengi watakapoinuka katika nyakati za mwisho, basi ni lazima tupambane dhidi yao ili kuilinda imani yetu hata ikiwa ni kwa gharama ya kuyatoa maisha yetu kwa kuifia-dini. Wakati wa jinsi hiyo unatukaribia kwa haraka sana. Ikiwa tunaliamini Neno, basi ni lazima tupambane dhidi ya Mpinga Kristo na wafuasi wake, na ambaye ni adui yetu mkubwa. Hii ndiyo imani inayopigana vita. 
Kupigana vita maana yake ni kupambana. Lakini ninaposema kupambana, simaanishi kuwa ni mapambano ya kimwili ya kupigana na kudundana. Bali, ni kuilinda imani pasipo kusalimu amri chini ya Mpinga Kristo, ambaye ni mtumishi wa Shetani atakayesimama dhidi ya injili ya wokovu ambayo Bwana ametupatia, na ambaye atawatesa waamini. Wale watakaouawa kwa kuifia-dini katika nyakati za mwisho ndio wale walio na ushuhuda wa Yesu na waliolitunza Neno la Mungu. Wanachoshuhudia ni juu ya Yesu aliyekuja kwa kupitia injili ya maji na Roho.
Kupigana vita ni kuilinda imani katika injili ya maji na Roho. Ili kuilinda imani hii, basi wale wote waliozaliwa tena upya kwa kuamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana ni lazima waungane na watakatifu wengine waliozaliwa tena upya katika makanisa ya Mungu ya waliozaliwa tena upya. Pia ni lazima tukubaliane kwa ujasiri kuingia vitani hali tukiwa na dhamiri imara ya kuieneza imani yetu kwa watu wengine na kisha kuziokoa roho zao. Kuwa tayari kwa ajili ya vita maana yake ni kuilinda imani yetu na pia kuziokoa roho nyingine; imani hii ya kanisa ndio barabara ielekeayo kwenye ushindi na inayompendeza Mungu. Watumishi wa Mungu na watakatifu wake ni lazima waishikilie na kuitunza imani hii inayoweza kupigana vita.
Je, wakati wa leo ambapo tunapaswa kuishi tukiwa na imani inayopigana vita ukoje? Ni wazi kuwa wakati uliopo unapitia katika mabadiliko mengi sana. “Nadharia” nyingi kuhusiana na kunyakuliwa na kuja kwa Kristo mara ya pili zimetokea na kutoweka, na kwa sababu hiyo imani za watu pia zimekuwa zikibadilika kulingana na nadharia hizo.
Kabla ya nadharia mpya ya kunyakuliwa haijatolewa katika miaka ya mwanzoni ya 1800, kila mtu alikuwa akiamini na kuhubiri juu ya fundisho la imani la kunyakuliwa baada ya dhiki, fundisho ambalo linadai kuwa Kristo atarudi baada ya watakatifu kupitia kipindi chote cha Dhiki Kuu, na kwamba kunyakuliwa na kufufuliwa kwao kutatokea wakati huo Kristo atakaporudi. Lakini nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki ambayo ilikuja kupata umaarufu katika miaka ya mwanzo ya 1800 iliweza kuipiku nadharia ya kunyakuliwa baada ya dhiki.
Nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki inadai kuwa waamini katika Yesu watapaishwa mbinguni kabla ile miaka saba ya Dhiki Kuu haijaanza. Ingawa mwanzoni nadharia hii ilikataliwa na watu wengi, kwa sasa karibu watu wengi sana wanaiamini nadharia hii ya kunyakuliwa kabla ya dhiki. Lakini nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki sio tu kwamba haipatani na Neno la Mungu, bali pia inalifanya Neno la Mungu na mpango wake kuonekana kuwa hauna maana. Hata hivyo, katika mawazo ya wale wasioifahamu Biblia, nadharia hii ya kunyakuliwa kabla ya dhiki imepandikizwa kwa nguvu sana ndani yao.
Mitume wa kale walizigawa nyakati za Mungu katika nyakati mbili. Nyakati hizi zilikuwa ni wakati wa kwanza wa wokovu kwa imani katika Yesu Kristo, na wakati wa pili ni wakati wa Dhiki Kuu utakaokuja baada ya wakati wa kwanza. Wanazuoni wa leo wanasema kuwa ingawa wanauelewa wakati wa kwanza wa wokovu kwa imani katika Yesu, ukweli ni kuwa wanashindwa kuuelewa wakati wa pili wa Dhiki Kuu, ambao ni wakati wa kurudi kwa Kristo na kunyakuliwa kwa watakatifu kwa kuwa ni wakati mgumu sana kuuelewa.
Wakristo wengi wanaoamini juu ya nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki kwa sababu ya kutozifahamu nyakazi hawawezi kukwepa kuwa na imani potofu. Hali wakijifanya kutabiri siku yao au tarehe yao binafsi ambapo Kristo atarudi, na huku wakiifanya imani yao kutuama kwa uvivu hali wakifikiri kuwa watanyakuliwa kabla ya Dhiki Kuu—basi ukweli ni kuwa hayo yote ni matokeo ya kuiamini nadharia hii potofu ya kunyakuliwa kabla ya dhiki. Kuna Wakristo wengi sana ambao wameangukia katika utepetevu wa kiroho huku wakifikiri kuwa, “Nani anajali ikiwa ulimwengu utakabiliana na magumu? Nitanyakuliwa kabla ya kuanza kwa Dhiki Kuu, na kwa sababu hiyo mambo yote yapo sawa.” Mkanganyiko huu wote umeletwa kutokana na kukosekana kwa uelewa sahihi wa kibiblia na ufahamu sahihi wa kunyakuliwa.
Scofield aliitetea nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki, na kwa sababu hiyo akili za wale wote walioiamini nadharia hii zimeishia katika uelekeo wa starehe hali wakifikiri hivi, “Tutanyakuliwa kabla ya Dhiki Kuu haijaja duniani, basi hebu sasa tuishi kwa starehe kadri tutakavyoweza.” Hivyo imani yao imekuwa ya uzembe na uvivu.
Lakini Biblia inasema nini kuhusu Dhiki Kuu na kunyakuliwa? Biblia inazungumzia juu ya kunyakuliwa katikati ya dhiki. Inaeleza kuwa Waisraeli na Wamataifa wanaoamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu watapata mateso toka kwa Mpinga Kristo katika ile miaka mitatu na nusu ya kwanza ya kipindi cha Dhiki Kuu ndani ya wakati wa farasi wa kijivujivu.
Biblia inatueleza kuwa baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza ya Dhiki Kuu, Mpinga Kristo atawaua watakatifu—yaani watakatifu watauawa kwa kuifia-dini. Pia Biblia inatueleza kuwa watakatifu wote, yaani wale wote waliouawa kwa kuifia-dini na wale ambao hawakuuawa watafufuliwa na miili yenye utukufu, na sambamba na ufufuo wao watanyakuliwa kwenda angani. Wakati watakatifu watakapokuwa wamenyakuliwa katikati ya Dhiki Kuu, basi ulimwengu utafikia mwisho wake kwa kumiminiwa mapigo ya mabakuli saba. Kisha Bwana atarudi duniani kumhukumu Shetani, Mpinga Kristo, pamoja na wafusi wake.
Ufunuo 13 inatueleza kuwa wale ambao majina yao hayajaandikwa katika Kitabu cha Uzima watasalimu amri mbele ya Mpinga Kristo na sanamu zake. Kwa maneno mengine, ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima ndio ambao hawatasalimu amri mbele ya Mpinga Kristo na wafuasi wake. Wale ambao majina yao hayajaandikwa katika Kitabu cha Uzima kwa kukataa kuamini katika injili ya maji na Roho katika mioyo yao wataishia kuabudu sanamu na kusalimu amri mbele ya Shetani.
Hii ndio sababu Biblia inatueleza kuwa watakatifu watabakia hapa duniani katika kipindi cha Dhiki Kuu, na kwamba baada ya kupita nusu ya kipindi cha Dhiki ndipo watakaponyakuliwa mawinguni. Wale watakaosalimu amri kwa Shetani na kuipokea alama ya yule Mpinga Kristo katika kipindi cha cha miaka saba ya Dhiki Kuu watatupwa katika ziwa la moto, lakini wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima na ambao hawakusalimu amri kwa sanamu watanyakuliwa katikati ya kipindi cha Dhiki Kuu.
Kunyakuliwa halisi kutatokea baada ya kupita nusu ya ile miaka saba ya Dhiki Kuu. Habari za kina za kibiblia kuhusu wakati wa kunyakuliwa zitazungumziwa katika toleo la pili la kitabu hiki linalofuata. Hata hivyo, kuna watu wengi ambao wanaliona tukio la kunyakuliwa kuwa liko karibu sana, wanaendelea kuzungumzia juu ya kunyakuliwa kabla ya dhiki, na baadhi yao wanaliona tukio hilo kuwa litatokea baadaye sana kiasi kuwa wanakazia juu ya kunyakuliwa baada ya dhiki. Wanazuoni wanazungumzia juu ya nadharia ya kunyakuliwa kabla ya dhiki ilhali wao wenyewe hawajashawishika na maelezo yake, wakati huo huo waumini wengi wanaendelea kuishikilia nadharia hii na kuiamini. Baadhi ya watu wanachangia vyote walivyo navyo katika makanisa yao, huku baadhi yao wakisubiri pasipo kutumia akili vizuri tarehe iliyotangazwa ya kurudi kwa Kristo.
Hapo zamani kidogo, waumini wa dhehebu moja waliitangaza tarehe na kisha kuamini kuwa Kristo atarudi katika tarehe hiyo waliyoichagua. Hivyo, wote walipanda mlima, wakaifunga miili yao pamoja kwa kamba, na wakasubiri kunyakuliwa kwao wakati wa usiku. Muda ulizidi kwenda na Yesu hakurudi pamoja na kuwa walingojea kwa shauku sana. Basi hatimaye walikata tamaa, wakajifungua kamba zao na kisha wakashuka toka mlimani wakiwa wamejaa aibu. Kwa bahati mbaya, aina hii ya kushindwa imekuwa ni ya kawaida katika ulimwengu wa Kikristo. Matukio kama hayo sio kwamba yamekuwepo hapa Korea tu, bali yanatokea katika sehemu nyingi ulimwenguni kama vile Ulaya, Marekani, Asia, na kwingineko.
Hivyo, tunachopaswa kukifahamu kwa usahihi ni kuwa Mungu atairuhusu Dhiki Kuu hata kwa watakatifu wake wa imani. Huu ni mpango wa Mungu. Sababu inayomfanya Mungu airuhusu Dhiki Kuu hata kwa watakatifu ni katika lengo la kuzitimiza ahadi zake—yaani kwa kupitia Dhiki, kumtupa Shetani pamoja katika moto wa milele, kuubadilisha ulimwengu huu kuwa katika ulimwengu mpya kwa kuuanzisha Ufalme wa Kristo kwa miaka elfu moja ambapo watakatifu watatawala pamoja na Kristo, na kuwapatia waamini wa Yesu Mbingu na Nchi Mpya. Haya ni mapenzi ya Mungu ambayo yameiruhusu Dhiki Kuu kutujia kwa malengo maalum.
Miaka saba ya Dhiki Kuu bado haijaanza. Ikiwa tunadhani kuwa majanga ya kiasili tuliyokutana nayo hadi sasa yanaweza kulinganishwa na moto unaowaka kiwandani ambao unaweza kuzimwa na wazima moto, ukweli ni kuwa majanga yanayousubiri ulimwengu katika kipindi cha Dhiki Kuu si ya kawaida, yakilinganishwa na moto ambao utateketeza theluthi ya misitu ya dunia.
Ili kuweza kutoyumbishwa na kuyavumilia majanga kama hayo na mapigo yatakayoupiga ulimwengu, basi watumishi na watakatifu wa Mungu ni lazima wawe na imani inayopigana vita. Kwa kuwa tutabakia hapa duniani hadi katikati ya kipindi cha Dhiki Kuu, basi ni lazima tuuishi wakati huo wa mwisho tukiwa na imani isiyoshindwa wala kusalimu amri kwa Mpinga Kristo na wafuasi wake. Ni lazima uihubiri injili ya maji na Roho katika ulimwengu mzima ili kuziokoa nafsi nyingi zaidi ikiwamo famili yako mwenyewe hali ukiwa na moyo wenye nia kama askari anayeingia vitani.
Ulimwengu hautaendelea kuwa na amani wakati wote kama hivi ulivyo. Lakini hata wakati mkanganyiko utakapokuwa ukiitawala dunia na magumu yatakapokuwa yakiyazunguka maisha yetu, basi itakuwa ni lazima tuishi kwa uaminifu hali tukiamini kuwa Mungu atatulinda hadi siku ya mwisho. Dini za ulimwengu na Shetani wanawadanganya watu kwa maneno mbalimbali ya kubembeleza, hali wakiziiba roho zao na hatimaye kuwatumbukiza kuzimu.
Hata sasa, kuna watu wengi sana na hasa katika madhehebu makubwa ambao wanaiamini nadharia ya Scofield ya kunyakuliwa kabla ya dhiki, jambo ambalo linawapeleka wengi katika imani potofu. Wale wanaoamini kuwa watanyakuliwa kabla ya Dhiki Kuu hawaoni umuhimu wa kuziandaa imani zao ili kuweza kuhimili misukosuko katika kipindi cha Dhiki Kuu. Wao wanafikiri kuwa kitu pekee wanachopaswa kukifanya ni kuwa waaminifu katika maisha yao ya sasa na kisha kunyakuliwa mawinguni wakati Bwana atakapowaita. Lakini kunyakuliwa kwa watakatifu kutatokea baada ya kuipita miaka mitatu na nusu ya Dhiki Kuu, na kwa sababu hiyo wanapaswa kuiandaa imani yao kwa ajili ya Dhiki inayokuja bila kujalisha kuwa Kristo atarudi lini. Ni lazima tuamini kuwa Mungu atawaokoa Waisraeli na Wamataifa wengi katika kipindi cha miaka saba ya Dhiki Kuu.
 Aya ya 14 inatueleza kuwas, “Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” Maelezo haya yana yanaelezea juu ya kuifia-dini. Kuifia-dini maana yake ni kufa kwa ajili ya kazi ya haki kwa mujibu wa imani ya mtu. Imani sahihi kabisa kwa watakatifu waliokombolewa toka katika dhambi ni kuamini katika injili na kuilinda imani hii kwamba Bwana amezifanya dhambi zetu zote kutoweka. Lakini siku zote Shetani anajaribu kuivunja vunja imani ya watakatifu. Hivyo ni lazima tutangaze vita ya kiroho na kupambana dhidi ya Shetani.
Ikiwa tutasalimu amri mbele ya Shetani katika vita hivi, basi ni hakika kuwa tutatupwa kuzimu pamoja na Ibilisi na watumishi wake, lakini ikiwa tutapambana na kuilinda imani yetu hata kama itatugharimu kifo, basi ni hakika kuwa tutauawa kwa kuifia-dini na hatimaye tutaingia katika Ufalme wa Mungu tukiwa na imani hii ya kuifia-dini. Kwa kuwa tunapambana katika vita hii ya kiroho ili kuilinda imani yetu, basi kifo chetu kitakuwa ni kifo cha haki na chenye utukufu.
Hivyo, ni lazima tuwe na imani inayopambana kwa ajili ya kazi za haki. Ni lazima tuamini kuwa tupo katika vita kwa ajili ya kuziokoa roho za wengine, na ni lazima tuilinde imani yetu hadi mwisho na kisha kushinda katika vita hii ili tuweze kuzipeleka roho hizo Mbinguni. Ni lazima tumshinde Shetani katika vita vyetu dhidi yake kwa upanga wa Neno la Mungu wetu hadi pale tutakapopokea taji ya ushindi.
Watu wanazaliwa mara moja na wanakufa mara moja. Haijalishi jinsi wataalamu wa sayansi ya madawa walivyopiga hatua, ukweli ni kuwa kila mtu hatimaye atakufa. Haijalishi kuwa watu wanakufa wakiwa na umri wa miaka 10 au 80, watu hao wote watakutana na hukumu ya dhambi toka kwa Mungu. Wale wanaokufa pasipo kuamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana watakutana na hukumu yao na wataadhibiwa na kutupwa katika moto wa milele. Ingawa dhambi zao zote zilikuwa zimeoshelewa mbali kwa maji na damu ya Yesu na kuwafanya kuwa weupe kama theluji, basi kwa sababu dhambi yao ya kutouamini ukweli huu haikusamehewa, watu hawa wasioamini watahukumiwa kwa dhambi zao zote ambao walizifanya mbele za Mungu na wanadamu walipokuwa wangali hapa duniani na watalipa gharama ya dhambi hizo.
Ili kukwepa kutupwa katika moto wa kuzimu mbele za Mungu, ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu inayotukomboa toka katika dhambi zetu zote. Injili ya maji na Roho inayozipatanisha dhambi zetu zote ni tofauti na injili inayoamini katika damu ya Msalaba tu. Nimekuwa nikiihubiri injili ya maji na Roho katika nyakati za kawaida na katika nyakati zisizo za kawaida. Ni kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndipo tunapoweza kumpokea Roho Mtakatifu na kisha baraka ya kufanyika kuwa watoto wa Mungu. Tunapomwamini Yesu, basi ni lazima tuachane na kutoziamini injili za uongo zinazoundwa na damu ya Yesu tu.
Agano la Kale linazungumzia juu ya injili ya kweli kwa kuwekewa mikono na katika birika la kunawia. Katika Agano la Jipya, Neno la Mungu linatueleza kuwa dhambi zetu zilipitishwa kwenda kwa Yesu mara moja na kwa wote kwa kupitia ubatizo wake ambao Kristo aliupokea. Birika la kunawia la Agano la Kale na ubatizo wa Agano Jipya vyote vinazungumzia imani moja katika injili ya maji na Roho ambayo imetuokoa toka katika dhambi zetu zote—kwa kupitia ubatizo wa Yesu ambao ulizikabidhisha dhambi zetu zote kwa Yesu, na kwa kifo chake Msalabani, na kwa ufufuo wake. Hakuna mtu anayeweza kuokolewa pasipo injili hii ya maji na Roho.
Ni lazima tuendelee kuishi kwa imani yetu katika injili ya maji na Roho hadi tutakapofikia katikati ya kipindi cha Dhiki Kuu. Ni lazima tuutambue wakati huu, na kisha tuishi hizi siku chache zilizobakia kama Mungu anavyotaka tuishi, hali tukiuhubiri Ufalme wa Mungu na kuwapelekea wote habari njema. Bwana alituambia kuwa watu wengi wataokolewa hata katika siku zile za mwisho.
Pamoja na kuwa hakuna maji, mimea michache inaweza kuishi jangwani, hii ni kwa sababu jangwani kuna mchanga na jua kali. Lakini hata katika jangwa kama hili ambalo limejawa na mchanga wa moto na mkavu, mvua ikinyesha kuna mimea ambayo inachipuka, inatoa maua, na kuzaa matunda kwa muda wa wiki moja tu. Kitu ambacho jangwa linakikosa ni maji; lakini pamoja na kuwa mbegu ambazo zipo chini ya mchanga haziwezi kuchipuka, ukweli unabakia kwamba mbegu hizo bado zipo hai na hazijafa na kwamba zinangojea mvua. Na wakati unyevunyevu unapozifikia hizi mbegu kavu, zinachipuka kwa haraka. Mbegu hizi zinachipuka kwa siku moja, siku ya pili zinakua, na siku ya tatu zinatoa maua na kuzaa mbegu. Na katika siku yake ya mwisho mimea hii inaangusha mbegu zake ardhini na kwa mara nyingine mbegu hizi ngumu zinajificha chini ya mchanga.
Kama ilivyo kwa mimea hii katika jangwa ambayo inaonekana kuwa ni vigumu kukua inavyoweza kuchipuka na kukua wakati maji yanapomiminwa, basi vivyo hivyo tunaamini kuwa katika nyakati za mwisho kutakuwa na nafsi katika ulimwengu ulio kama jangwa ambazo zitaweza kuchipuka, kutoa maua, na kisha kuzaa matunda ili mradi tu zikikutana na kiasi kidogo tu cha maji ya injili ya maji na Roho. Tunaamini kuwa wakati mapigo ya matarumbeta saba yatakapokuwa yamepigwa, wengi waliosikia juu ya Dhiki Kuu kwa kupitia Neno wataitambua injili iliyopandwa ndani yao, watailinda, na muda si mrefu imani ya kuifia-dini itakua.
Kwa hiyo, wakati wewe na mimi tutakapokuwa tumeuawa kwa ajili ya kuilinda imani yetu, basi kutakuwa na watu wengi wa imani ambao watainuka kama mimea ya jangwani ambayo inakua katika ardhi kavu ambao watajiunga katika kuifia-dini kwa kukataa kuipokea alama na kuabudu sanamu. Injili hii ya maji na Roho ambayo tunaihubiri sasa itawawezesha watu wengi kuzikuza imani zao kwa muda mfupi na kisha kupokea mauaji ya kuifia-dini, na kuwabadilisha na kuwa watumishi wa Mungu wanaoweza kupambana.
Tangu watoto hadi watu wazima, sisi sote ni askari katika jeshi la Bwana. Kama watu wa Kristo, ni lazima tuishi kwa imani sahihi hali tukiiandaa mioyo yetu wakati wote kwa ajili ya vita, tukijiweka imara kutodanganywa na uongo. Kwetu sisi ambao tutashinda vita, Mungu atatupatia taji ya ushindi. Hivyo, ni lazima tuyaishi maisha yetu hali tukizitumikia kazi za haki za Mungu hali tukiwa na imani inayopambana na Shetani, na uongo wake wote, na uovu wote wa hapa ulimwenguni.
 
 
Mungu Atatupatia Imani Yenye Ujasiri Katika Nyakati za Dhiki
 
Wakati wa farasi wa kijivujivu utakapowadia, Mungu atatupatia ishara yake. Aya ya 1 inasema, “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.” Upepo unaotajwa hapa unahusu upepo wa dhiki ambao Mungu atauleta. Ufunuo 7:1-8 inatueleza kuwa ili kuwaokoa watu wa Israeli, Mungu atawawekea muhuri na kwa sababu hiyo atauzuia upepo kwa muda mfupi. Lakini wakati utakapowadia—yaani wakati wa farasi mweusi, yaani wakati wa njaa kati ya zile nyakati saba za Mungu utakapopita—basi Mungu ataufungua wakati wa farasi wa kijivujivu. Hapo ndipo zile pepo nne za dunia zitakapoinuliwa na kuleta upepo wa dhiki ulimwenguni.
Mara utakapofikia wakati wa farasi wa kijivujivu, basi upepo wa kutisha wa dhiki utaanza kuvuma, na Waisraeli wengi watauawa, na Wamataifa wengi tukiwemo sisi tutauawa pia. Wakati wa farasi wa kijivujivu utakapowadia, basi hapo ndipo wakati wa dhiki utakapoanza.
Kwa kuwa sasa ni wakati wa farasi mweusi, basi upepo wa njaa unavuma ulimwenguni kote. Mara wakati huu utakapokwisha, wakati wa farasi wa kijijivu utaanza na kuuleta upepo wa dhiki. Upepo wa dhiki utaonyesha kuanza kwa kipindi kamili cha miaka saba ya Dhiki Kuu. Wakati Mungu atakapoileta Dhiki Kuu katika ulimwengu huu kwa mara ya kwanza tangu kuumbwa kwa ulimwnegu na historia ya mwanadamu—yaani wakati upepo wa dhiki utakapoanza kuvuma wa kipindi cha farasi wa kijivujivu—basi hapo ndipo kila kitu kitakapofikia mwisho na kufanywa upya.
Ni lazima tutambue kuwa mara wakati wa farasi wa kijivujivu utakapowadia, basi hapo ndipo wakati wa dhiki utakapoanza. Kadri watawala duniani wanavyozidi kuungana, basi baadhi ya wanasiasa watajinyakulia mamlaka kamili, na wale wote ambao hawayatii maagizo yao watatupwa katika dhiki na kifo. Watu wataona vigumu sana kuishi katika kipindi cha farasi wa kijivujivu kwa kuwa watakuwa wakikabiliana na magumu mengi sana kuanzia majanga ya kiasili yatakayokuwa yameletwa na mapigo ya matarumbeta saba, lakini pia hali ya kisiasa ya wakati huo itakuwa ni ya kutisha sana. Lakini hata katika hali kama hii, Mungu ataendelea kufanya kazi miongoni mwa watu huku akiwaongoza Wamataifa wengi katika wokovu wao.
Mara upepo wa dhiki utakapovuma katika wakati wa farasi wa kijivujivu, basi tumaini litaweza kupatikana mahali pamoja tu. Kama Neno linavyotueleza, kuwa “Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Tumaini hili pekee linapatikana katika Mungu Baba yetu na Yesu Kristo. Wakati upepo wa kutisha wa dhiki utakapokuwa umevumishwa, Mpinga Kristo atainuka hapa duniani, atawaunganisha si wanasiasa tu bali hata jamii za ulimwengu, yaani kuanzia uchumi, desturi, hadi dini. Dhiki maana yake ni kupitia katika mateso ya kutisha. Huu ndio upepo ambao utavumishwa. Na mambo haya yote yatatokea mara moja.
Upepo wa kuunganisha uchumi unaendelea kuvuma katika ulimwengu wa sasa. Kwa sasa kuna majadiliano mazito kuhusu biashara huru, kuhusu kuondoa ukuta wa ushuru wa forodha kati ya nchi wanachama katika jumuia fulani za kibiashara. Chini ya utawala wa kulinda mifumo ya biashara, ilikuwa vigumu sana kwa bidhaa toka katika nchi moja kwenda na kushindana kwa bei katika nchi nyingine kwa kuwa ushuru wa forodha uliokuwa ukitozwa ulizifanya bidhaa toka nchi nyingine kupanda bei sana hata kama bei ya bidhaa hiyo ilikuwa ndogo.
Lakini hizi kuta za ushuru wa forodha zinaanza kuanguka taratibu. Mfano mzuri unaweza kupatikana Ulaya ambako ushuru wa forodha umeondolewa. Kwa mfano, hakuna ushuru wa forodha tena kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (UU). Huu ni mwanzo wa muunganisho mkuu ambao utakuja baadaye ukiashiria kuinuka kwa umoja wa kisiasa na kitamaduni. Haya ni maendeleo ya kushangaza. Kwamba nchi inaweza kuuza bidhaa zake katika nchi nyingine pasipo ushuru wa forodha. Huu ni msingi wa mabadiliko unaoonyesha mageuzi ya mazingira ya kiuchumi duniani. Ikiwa Umoja wa Ulaya utafanikiwa kukamilisha muunganisho wao wa kiuchimu, basi ni dhahiri kuwa muunganisho wa uchumi wa kidunia utapata kasi zaidi.
Hivi karibuni, Korea, China, na Japani zilifikia makubaliano ya kukopeshana mikopo ya dharura kwa matukio ya baadaye ya kudorora kwa uchumi barani Asia, kama ule uliolikumba bara la Asia mwaka 1997. Katika mgogoro wa uchumi wa Asia wa mwaka 1997, msaada wa kifedha ulitolewa na Marekani. Lakini kwa makubaliano haya, hizi nchi tatu zimekubaliana kupeana msaada wa fedha ikiwa mojawapo ya nchi hizo itaingia katika mdodoro wa uchumi au mgogoro wowote wa kifedha. Hii ina maanisha kuwa ni kuundwa kwa ushirikiano wa kiuchumi. Kama nchi za Ulaya zilivyoweza kuondoa ushuru wa forodha na kuelekea katika kuunganisha nguvu za kiuchumi kwa ajili ya mafanikio ya kiuchumi ya nchi wanachama, basi vivyo hivyo hizi nchi tatu za Mashariki ya Mbali pia zimeamua kuweka rasilimali zao pamoja. Uunganishaji wa nchi binafsi kama huo na asasi zake za maendeleo hatimaye utasababisha muunganisho wa kisiasa.
Muungano wa kiuchumi kwa kuondoa ushuru wa forodha maana yake ni muunganisho usiopingwa wa nchi binafsi katika taifa lililo juu zaidi. Wakati majanga ya asili ya mapigo saba yatakapopiga na mahangaiko kuenea katika ulimwengu mzima, basi wawakilishi wa asasi na taasisi kama hizo za kimataifa wataungana ili kumtafuta kiongozi mkuu. Kwa maneno mengine, watajaribu kuleta nidhamu kwa ulimwengu utakaokuwa kwenye machafuko kwa kuufanya ulimwengu uwe kitu kimoja kisiasa kwa kumwinua kiongozi mwenye mamlaka kubwa na kamilifu.
Upepo wa dhiki utavuma katikati ya mchakato huu. Badala ya kuheshimu haki za watu binafsi, kutakuwa na kuzikanyaga haki za wachache kwa ajili ya walio wengi. Upepo huu utavuma wakati wa farasi wa kijivujivu utakapowadia. Msingi wa matukio kama hayo umewekwa katika wakati wa farasi mweusi, na matokeo yake halisi yatakuja kuonekana katika wakati wa farasi wa kijivujivu.
Wakati Korea ilipokumbwa na mgogoro wa fedha wa mwaka 1997 na kisha kuwekwa chini ya uangalizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Korea ilikumbwa na majanga makubwa sana ya kiuchumi. Bei za vitu zilipanda sana, watu walipoteza kazi zao kwa siku moja, na tabaka la watu wa kati lilisukumwa na kuondolewa mitaani. Majanga ya kiuchumi kama hayo yamekuwa ni mambo ya kawaida katika sehemu nyingi duniani kiasi kuwa haiwezi kupita siku usisikie juu ya mgogoro wa fedha katika nchi fulani. Huu ni upepo wa njaa. Tupo katika wakati huu wa njaa, yaani wakati ambapo maisha yako yanaonekana kuwa hayana maana unapokuwa hauna fedha. Hapo baadaye, upepo huu wa njaa utafuatiwa na mvumo wa upepo wa dhiki.
Mungu alizishikilia pepo za pembe nne za dunia kwa muda ili watu 144,000 wa Israeli waweze kutiwa mihuri. Baada ya kuwazuilia ili wasipate madhara, basi Mungu aliziachia zile pepo za dhiki. Wakati upepo huu wa dhiki utakapoondoka katika mikono ya malaika, basi upepo wa Dhiki Kuu utavuma. Upepo wa dhiki utauunganisha ulimwengu, na kwa kufuatia kuinuka kwa Mpinga Kristo, ulimwengu wote utakuwa chini ya mamlaka ya Shetani, na kisha utapitia katika kipindi cha miaka saba ya majanga ya kiasili toka katika mapigo ya yale matarumbeta saba. Mapigo haya ya matarumbeta saba yatafuatiwa na mapigo ya mabakuli saba.
Katika kipindi hiki cha utawala wa kikatili wa Mpinga Kristo na wakati ambapo uhuru wa imani utatoweka, basi njaa na vifo vya njaa vitakuwa vimefikia kiwango kibaya sana, kiasi kuwa watu wengi wataweza kuishi kwa kutegemea misaada ya chakula toka serikalini tu. Kila mtu hapa ulimwenguni atakabiliana na wakati huo. Neno la Ufunuo sura ya 7 linatupatia picha ya jumla ya mambo haya yatakayokuja hapo baadaye.
Je, ni kitu gani kingine kinachotungojea katika wakati huu? Wakati wa farasi wa kijivujivu utakuwa na idadi kubwa ya vifo vya wafia-dini vya Waisraeli na Wamataifa pia. Wakati Dhiki Kuu itakapowadia kutakuwa na tumaini moja tu litakalokuwa limesalia. Aya ya 10 inasema, “wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Kwa maneno mengine, wokovu wetu unapatikana katika Mungu wetu tu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo. Kama tunavyoweza kuona katika sura ya 4, ambayo inatueleza kuwa kiti cha enzi kiliandaliwa kwa ajili ya Yesu Kristo, na Yeye aketiye katika kile kiti cha enzi ni Yesu Kristo, akiwa si mnyonge bali kama Mwana wa Mungu, Mungu Mwenyezi na hakimu wa wote. Mungu Baba bado ameketi katika kiti chake cha enzi. Hivyo, tunapozungumzia juu ya Mungu Utatu, Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wote hao ni Mungu mmoja. Hivyo, wokovu wetu kamili upo kwa Mungu wetu na Mwana-Kondoo, ambaye ni Yesu Kristo.
Ni wapi tunapoweza kupata tumaini wakati Dhiki ya kutisha itakapokuja? Wakati Mpinga Kristo atakapoinuka katika kipindi cha Dhiki Kuu, basi Mpinga Kristo huyo ataitengeneza sanamu yake na atatishia kuwaua wote watakaokataa kuiabudu sanamu yake na wale watakaokuwa hawajaipokea alama ya jina lake katika mikono yao au katika vipaji vya nyuso zao (Ufunuo 13).
Kwa maana hali ya mazingira ya asili itakuwa imefikia hali mbaya sana, kwa kuwa moto na mvua ya mawe vitakuwa vikinyesha toka mbinguni, matetemeko yataipiga nchi, na mapigo mengine yatafuata. Hakuna mahali hapa duniani ambapo hapataguswa na mapigo. Katika mazingira haya mabaya, ambapo ardhi itakuwa imemeguka kutokana na matetemeko, ambapo jua, mwezi, na nyota zitakuwa zimepoteza nuru yake, na bahari na mito itakuwa imekufa kutokana na mapigo, hali ya kisiasa ya wakati huo itakuwa mbaya sana na ya aina yake. Mpinga Kristo atatawala kwa utawala wa kikatili kadri itakavyowezekana, maana atajichukulia mamlaka na atawaweka viongozi wengine wa ulimwengu chini ya mamlaka yake.
 

Kwa Nini Mpinga Kristo Anatokea? 
 
Kwa kuwa Shetani atazitoa nguvu zake kwa muda kwa Mpinga Kristo akijaribu kuyatimiza mapenzi yake ya mwisho—yaani kuitimiza hamu yake ya kuitwa Mungu na watu ili aweze kuinuliwa na kuwa juu ya Mungu wa kweli. Lakini, Shetani mwenyewe anafahamu kuwa nia yake hii haitaweza kutimizwa. Lakini kwa mara ya mwisho, Shetani atajaribu kutukuzwa kwa kupitia wanadamu huku akiwaua wale wote ambao hawatamtii. Hiyo ndiyo tabu ambayo itawakuta watakatifu wote. Wakati huu, watakatifu hawatakuwa na chaguo jingine zaidi ya kufa, kwa kuwa tumaini lao pekee litakuwa katika Mungu wa wokovu wetu, na katika Yesu Kristo Mungu wetu ambaye ametuokoa kwa kupitia injili ya maji na Roho. Tunaweza kumtegemea huyu Mungu tu, na ni kwa kumwamini yeye tu ndipo tunapoweza kukombolewa toka katika kifo katikati ya hayo mapigo makuu na dhiki.
Katika nyakati hizi za mwisho, tumaini letu pekee litakuwa kwa “Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Watakatifu watauawa na kuifia-dini kwa imani yao katika Mungu, na kwa kumwamini Mungu watakombolewa toka katika mapigo ya kutisha na kifo. Hivyo Ufunuo sura ya 7 inatupatia yale yote ambayo yatatokea katika kipindi cha miaka saba ya Dhiki Kuu.
Hebu tuendelee na matukio ambayo upepo wa dhiki utayaleta. Aya ya 9-10 zinatueleza, “Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Nilipoulizwa kuwa umati huu toka katika makabila yote na lugha za watu wakiwa wamevikwa mavazi meupe ni akina nani, mmoja wa wale wazee 24 alijibu, “Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.”
Hii inatueleza kuwa idadi kubwa ya watu wataokolewa katikati ya kipindi cha Dhiki Kuu, ambapo idadi kubwa ya watu wanaofia dini itakapoongezeka toka katika watu wa mataifa yote, na kabila na lugha mbalimbali. Kwa maneno mengine, kutakuwa na mafuriko ya wale wanaomwamini Mungu kuwa ni Mwokozi wao katika ile dhiki na mapigo yote ya wakati huo. Kwa ufupi, hii ina maanisha kuwa wokovu unapatikana katika Mungu Utatu tu.
Kwa kuwa Mungu ametupatia injili ya maji na Roho ambayo imetuokoa toka katika dhambi zetu, na kwa kuwa tunaamini katika injili hii, basi wakati Mpinga Kristo atakapotokea na kututaka tusalimu amri mbele yake kwa kumuita yeye kuwa ni Mungu, basi ni hakika kuwa hatutamtetemekea. Zaidi ya yote, hata kama baadhi yetu watasalimu amri mbele ya Mpinga Kristo, ukweli ni kuwa hali hiyo haitawasaidia kuishi, kwa kuwa itawapaswa kuyapitia mapigo yenye machafuko na jaribio la mwisho la kumwabudu Shetani. Kwa kweli hakuna kinachoweza kuwa salama katika wakati huu.
Hivyo hatuna chaguo jingine zaidi ya kumwamini Mungu aliyetuokoa. Tutaweza kukubaliana na kuuawa kwa kuifia-dini kwa kumwamini Mungu ambaye atatupatia Ufalme wake wa Milenia na Mbingu na Nchi Mpya, kwa maana atatufufua toka kwa wafu, atatunyakua, na kisha atatupatia utukufu wote wa Mbingu na Nchi Mpya. Hii ndio sababu kutakuwa na watu wengi sana ambao watavikwa katika mavazi meupe yaliyooshwa katika damu ya Mwana-Kondoo.
Kwa hakika kutakuwa na watu wengi ambao watauawa na kuifia-dini kwa sababu ya imani yao kwa Mungu. Watakatifu na wale wote ambao waliuawa na kuifia-dini katika wakati huo toka katika kila taifa watayatoa maisha yao kwa ajili ya imani yao katika Mungu. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho ambayo sasa tunaihubiri watapokea kuuawa na kuifia-dini kwa kumwamini Mungu kwamba atawakomboa toka katika hofu yote ya dhiki na mapigo ya wakati huo. Ni Mungu tu ndiye anayeweza kutukomboa toka katika mapigo haya ya kutisha.
Ninakueleza matukio yote muhimu ambayo yatatokea katika kipindi cha miaka saba ya Dhiki Kuu. Wakati upepo wa dhiki utakapovuma katika ulimwengu huu, kutakuwa hakuna tumaini litakalokuwa limebakia hapa duniani. Ulimwengu huu kama tunavyoufahamu hivi sasa hautakuwepo, kwa maana mbingu na nchi zitakunjwa kama vile ukurasa unavyokunjwa.
Kisha Mungu ataiumba nchi mpya, na atawafanya wafia-dini kutawala katika nchi hiyo mpya kwa miaka elfu moja, na baada ya Ufalme huu wa Milenia kuisha, Mungu atawapeleka katika Ufalme wa milele. Ni Mungu wetu tu ndiye aliyetukomboa toka katika dhambi zetu zote, na ambaye ndiye atakayetuokoa toka katika kifo na maangamizi ya Dhiki Kuu, na ambaye ndiye anayeweza kutupatia tumaini. Wakati wa kuifia-dini utakapowadia, wewe na mimi pamoja na watu wengine duniani kote waliosikia na kuamini katika injili watauawa kwa ujasiri na kuifia-dini kwa kumwamini Mungu ambaye ametuokoa toka katika dhambi zetu. Sisi tutapokea kifo chetu cha kuifia-dini hali tukiwa na imani yetu jasiri na katika tumaini. Yeye, atakayetukomboa toka katika mapigo ya kutisha na dhiki ni Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi.
Kwa hiyo, hatuwezi kuuawa na kuifia-dini pasipo kuamini kuwa Mungu aliyetuokoa toka katika dhambi pia ni Mungu ambaye atatukomboa toka katika mapigo haya ya kutisha. Wafia-dini wa wakati huu ni wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Lakini hakuna hata mmoja ambaye jina lake halijaandikwa katika Kitabu cha Uzima atakayeweza kuuawa na kuifia-dini.
Injili hii itahubiriwa katika ulimwengu wote, na kila mtu duniani ataisikia na kuifahamu. Injili ya maji na Roho inashuhudiwa ulimwenguni kote kwa sababu tunaieneza injili hii bila kukoma. Kuna nafsi nyingi katika ulimwengu huu ambazo wakati Dhiki Kuu itakapowadia watayaweka matumaini yao katika Mwana-Kondoo, watamwamini Mungu na kuwa tayari hata kuutoa uhai wao, na wataweza kukubaliana na kuifia-dini. Na injili ya maji na Roho inayowawezesha waamini kuandikwa majina yao katika Kitabu cha Uzima itaendelea kuhubiriwa.
Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho watauawa na kuifia-dini katika nyakati za mwisho. Ufunuo 13:8 inatueleza kuwa, “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.” Ni ukweli halisi kuwa mtu yeyote ambaye jina lake halijaandikwa katika Kitabu cha Uzima atasalimu amri kwa yule Mnyama.
Ni Yesu Kristo na Mungu Baba yake ndiye atakayeweza kutukomboa toka katika Dhiki Kuu ya siku za mwisho. Sasa Roho Mtakatifu anakaa katika mioyo yetu. Ninaamini kuwa tunaokolewa na Mungu, na hata kama tutauawa kwa ajili yake, ukweli ni kuwa Mungu atatufufua toka kwa wafu, atatunyakua mawinguni, na atavibadilisha vitu vyote duniani na kuvifanya upya, na ataturuhusu kuishi katika Ufalme wa Milenia.
Wakati huu wa farasi wa kijivujivu ukiongozana na upepo wa dhiki unatukaribia sana kwa haraka. Wakati wa farasi mweusi unapita kwa haraka sana. Mara wakati huu utakapoishia, basi wakati wa farasi wa kijivujivu utawadia. Tangu wakati huo, ulimwengu mzima utaingia katika kipindi cha miaka saba ya Dhiki Kuu. Kipindi hicho kitakuwepo si chini wala zaidi ya miaka hiyo, kipindi hiki cha Dhiki Kuu kitatimizwa, kwa maana ni mpango wa Mungu.
Hebu tudhanie kwa muda kidogo kuwa kipindi cha Dhiki Kuu kimeanza. Miti na nyasi katika ulimwengu mzima inaungua, anga linajazwa na moshi, jua limefichwa chini ya wingu kubwa la moshi na kuuacha ulimwengu katika giza hata nyakati za mchana, watu wanakufa kila mahali, na tunasikia hata sauti za watu ambao wanatufuatia. Ni nani ambaye tutamwamini? Je, utamwamini Mungu ambaye ametuokoa toka katika dhambi zetu zote, na aliyeahidi kutufanya sisi kuwa wafia-dini ambao hatutasalimu amri kwa Mpinga Kristo, na ambaye atarudi tena hapa duniani ili kutufufua na kutunyakua na kutupeleka katika Mbingu na Nchi Mpya, au hautamwamini Mungu? Kwa hakika tutamwamini Mungu! Mungu ndiye tumaini letu pekee! Kumsujudu Mpinga Kristo wala kuzitegemea nguvu zetu wenyewe hakuwezi kutukomboa; kujificha mapangoni wala kutorokea na kuishi angani hakutatukomboa pia, atakayetukomboa si mwingine bali ni Mungu tu!
Wakati vimwondo vitakapoipiga sayari hii, basi mabaki yote ya vimwondo hivyo yataangukia duniani, na kuiharibu sayari nzima. Kila kitu ambacho Mungu alikiumba kwanza kitaharibiwa. Hapo ndipo tumaini la kweli litachipuka katika mioyo yetu. Ni nani basi ambaye tunaweza kuliweka tumaini letu kwake? Ni Mungu tu ndiye tunayeweza kumtazama na kuhitaji msaada wake, kwa kweli hakuna mwingine zaidi ya Mungu ambaye ndiye aliyetuokoa!
Kwa kuwa tumeokolewa kwa kuamini katika Neno la injili ya maji na Roho, basi tunamshukuru na kumtukuza Mungu kwa ajili ya wokovu huu. Lakini wakati wa Dhiki Kuu utakapowadia, tutamshukuru na kumsifu Mungu kwa kila kitu tulichonacho kwa kutukomboa toka katika mapigo ya kutisha na kifo. Ni Mungu tu ndiye anayeweza kutukomboa toka katika mikono ya Mpinga Kristo. Hakuna mwingine yeyote zaidi ya Mungu. Kwa kuwa tunayaweka matumaini yetu na imani katika huyu Mungu, na kwa kuwa tunaamini kuwa Mungu atatufufua na kuturuhusu kuishi katika Ufalme wa Milenia katika Mbingu na Nchi Mpya katika furaha ya milele, basi ni hakika kuwa tutaweza kuhimili na kuishinda dhiki itakayokuja.
Wakati utawadia ambapo Mpinga Kristo atatuburuza na kutupeleka mbele ya sanamu yake akidai, “Sujudu mbele ya sanamu hii, na niite mimi kuwa ni Mungu. Yesu si Mungu. Mimi ni Mungu, na ni mimi ndiye ninayeweza kukuokoa.” Hivyo, wakati Mpinga Kristo atakapotudai kumwabudu yeye, ukweli ni kuwa hakuna hata mmoja kati ya sisi tuliozaliwa tena upya atakayekubali kuisujudia sanamu yake. Kwa nini? Kwa sababu akisha tulazimisha kuipokea chapa yake, Mpinga Kristo atatufanya sisi kuwa watumwa wake, na atatutumia sisi kuwaua watu wengine na baadaye atatuua na sisi pia.
Wakati unakuja ambapo huyu Mpinga Kristo atasimama na kujitangaza mwenyewe kuwa ni Mungu. Na kwa kweli si muda mrefu sana ambapo Mpinga Kristo huyo ataitengeneza sanamu yake na kisha kumtaka kila mtu ulimwenguni kumwita kuwa ni Mungu, na kisha kuunda kwaya za kumwimbia sifa. Ikiwa amani itakuwepo katika wakati huo na ikiwa mazingira ya asili yatabakia kuwa yenye afya na mazuri, basi mtu anaweza kufikiri kuwa ulimwengu mpya umefika. Lakini misitu itakapokuwa imeungua, jua litakapokuwa limetoweka na ulimwengu utakapokuwa gizani, na watu watakapokuwa wakipiga kelele huku wakifa, na wakati mitaa itakapokuwa imefurika maiti za watu zilizoungua, basi hakuna hata mmoja wetu atakayetii amri ya Mpinga Kristo ya kusujudu mbele ya sanamu yake na kumuita yeye kuwa ni Mungu wetu. Kila mwamini aliyezaliwa tena upya atafahamu kuwa huyo ndiye Mpinga Kristo aliyetabiriwa na Neno la Mungu.
Pia Roho Mtakatifu anatufundisha. Anatupatia mioyo ambayo haiwezi kusalimu amri. Anatupatia mioyo yenye ujasiri inayoweza kusema, “Ikiwa ni lazima niue, lakini ikiwa nitakufa, Bwana atanilipia kisasi na ni hakika kuwa atanifufua!” Tunaamini kuwa kama Bwana wetu alivyofufuka toka kwa wafu katika siku ya tatu, basi sisi nasi, tutafufuliwa na kuwa hai tena. Kisha Bwana atatunyakua pasipo shaka.
 

Wenye Haki Hawatasalimu Amri Kwa Mpinga Kristo
 
Wale waliolisikia Neno hili la ahadi, kwamba Mungu atauharibu ulimwengu wa kwanza na kisha kuujenga Ufalme wa Milenia ili kuwafanya wenye haki kuishi katika ufalme huo kwa miaka elfu moja, na ambao wamezaliwa tena upya kwa kuliamini Neno hilo hawatasalimu amri kwa Shetani; kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani ya mioyo yao, basi wataweza kufahamu kila kitu. Lakini wale wasio na Roho Mtakatifu watayatetea maisha yao na kusalimu amri kwa Shetani, huku wakiogopa kuwa maisha yao yanaweza kupotea ikiwa hawatafuata kile ambacho kitakuwa kikionekana kama ni nidhamu ya ulimwengu mpya. Hivyo, kila mtu atakapokuwa akikiogopa kifo na kuwa mtumwa kwa ajili ya kifo, basi wale waliozaliwa tena upya ndio wanaoweza kuwekwa huru toka katika hofu hii ya kifo na wataweza kukubaliana na kuifia-dini kwa ujasiri kama jua linalochomoza.
Waliozaliwa tena upya wanaweza kufanya hivyo kwa sababu wana tumaini kuwa watafufuliwa katika miili mipya. Hii ndio sababu wale wanaotawaliwa na Roho Mtakatifu sio kwamba hawatakuwa na hofu ya kifo, bali wataweza kusimama dhidi ya Mpinga Kristo na kumwangusha kwa maneno ya ujasiri yanayotoka katika Roho Mtakatifu. Kwa sasa wanaweza kuwa waoga, lakini wale ambao wametiwa muhuri na Roho Mtakatifu kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, na kwa kupitia Roho Mtakatifu wataongea maneno ambayo maadui zao hawataweza kuyajibu kabisa. Sisi tunaliamini hili Neno la Mungu.
Mpinga Kristo atachukia wakati watakatifu watakapomweleza, “Unadirikije kujiita Mungu! Ulifukuzwa kutoka mbinguni, na hivi punde utafukuzwa pia kutoka duniani! Siku zako zimehesabiwa!” Idadi kubwa ya watu toka katika mataifa yote watainuka na kusimama dhidi ya Mpinga Kristo. Kisha Mpinga Kristo atawaua wote. Wakati huo watakatifu hawatakuwa wanyonge tena hata pale watakapokuwa wakiuawa. Kama Neno la Mungu linavyotueleza kuwa “Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo,” sisi sote tutakufa katika tumaini na uhakika mkubwa wa imani yetu itakayokuwa ikitoka katika Roho Mtakatifu.
Kama Kitabu cha Matendo kinavyoshuhudia, wakati Stefano alipokuwa akipigwa mawe hadi kifo, alitazama mbinguni na akaona katika maono kiti cha enzi cha Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu akingojea kumpokea. Hata alipokuwa akifa, Stefano aliendelea kuwaombea msamaha wale wote waliokuwa wakimpiga mawe kama vile Yesu alivyowaombea msamaha wale watu waliokuwa wakimsulubisha.
Kama vile Stefano, watakatifu watakaouawa kwa kuifia-dini katika nyakati za mwisho, hali wakiwa wamejaa Roho Mtakatifu, hatawaogopa bali watakuwa wajasiri. Ingawa kwa sasa wanaweza kuonekana kuwa ni waoga na kwamba imani yao inaweza kuonekana kuwa ni dhaifu, ukweli ni kuwa wale wote wanaolisikia Neno hili sasa watakuwa na imani yenye ujasiri wakati huo utakapowadia.
Usiogope. Hakuna kitu cha kuogopa, kuanzia kuinuka kwa Mpinga Kristo hadi kuja kwa upepo wa dhiki, mambo hayo yote yatatokea kwa ridhaa ya Mungu na ndani ya mpango wake kama ilivyodhihirishwa katika Ufunuo sura ya 6.
Kuifia-dini hakuji kutokana na nguvu yetu binafsi ya kimwili. Kuifia-dini kunawezekana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu tu na imani yetu katika ukweli. Kwa maneno mengine, tunaweza kuuawa na kuifia-dini kwa kumwamini Mungu na katika Neno lake la ahadi, na katika ule ukweli kuwa Mungu mwenyezi ni Mungu wetu.
Sasa ni lazima utambue kuwa mauaji ya kuifia-dini ambayo Mungu ameyaruhusu katika ile miaka saba ndani ya mpango wake ni majaliwa ya Mungu. Tusilifikirie suala la kuifia-dini nje ya mpango wa Mungu, bali tunapaswa kuuamini mpango huo katika mioyo yetu kwa mujibu wa Mapenzi ya Mungu. Hebu tuliamini Neno la Mungu, kwamba wakati utakapowadia wa kuifia-dini Mungu atatupatia nguvu zaidi ya kuweza kukabiliana na hilo.
Katika kila ulimwengu kuna mtawala mkuu. Wale waliozaliwa tena upya wanatawaliwa na Mungu, wakati wale ambao hawajazaliwa tena upya wanatawaliwa na roho ya Shetani. Nyakati za mwisho zitakapowadia, basi wale waliozaliwa tena upya, hali wakiongozwa na Mungu, watazipokea nguvu za kuweza kuyavumilia majaribu yote na dhiki. Kwa upande mwingine, wale wanaoongozwa na Shetani watakuwa hawana la kuchagua zaidi ya kufuata mapenzi ya Shetani kwa lazima maana watakuwa chini ya utawala wa Shetani.
Lakini ni nani ambaye nguvu zake ni kubwa? Ikiwa tunabarikiwa au kulaaniwa mambo hayo yatategemea kuwa ni ni nani aliye na nguvu zaidi kati ya Mungu na Shetani. Anayeokolewa katika nyakati za mwisho inategemea kuwa anamwamini nani. Wale waliomwamini Mungu na Neno lake watalindwa, watabarikiwa, na kupewa uzima wa milele kwa nguvu yake kuu na mamlaka yake milele. Lakini wale walioyasikia maneno ya Shetani na wakasalimu amri mbele yake watatupwa kuzimu pamoja naye Shetani ambaye hawezi kuwakomboa toka kuzimu. Hii ndiyo sababu Mungu alilitoa Neno lake kwa kupitia Ufunuo sura ya 1-7.
Kuanzia sura ya 8 na kuendelea, kitabu cha Ufunuo kinaeleza kwa kina yale ambayo yatatokea katika wakati wa farasi wa kijivujivu. Kwanza kabisa, mapigo ya yale matarumbeta saba yataishukia dunia. Hebu tuliangalie pigo la kwanza linalopatikana katika aya ya 7: “Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.” Kwa pigo la tarumbeta la kwanza, mvua ya mawe ikiwa imechanganyikana na damu itanyesha juu ya nchi. Hii haitakuwa ni mara ya kwanza kwa moto kushuka duniani maana sayari ya dunia itakuwa imepigwa na vimwondo na nyota katika matukio kadha wa kadha.
Hadi wakati huu, hakuna kati ya mapigo hayo ya vimwondo ambayo yameshaleta uharibifu mkubwa katika ulimwengu mzima, lakini wakati wa farasi wa kijivujivu utakapowadia, basi upepo wa dhiki utavuma juu ya dunia. Wakati upepo huu utakapoinuka kama bomu la tornado na utakapoharibu mazingira ya kiasili, basi moto utainyeshea dunia hii na kuunguza theluthi ya miti na nyasi, na kila mtu atakimbilia katika kuuzima moto huo.
Neno la Mungu linatueleza kuwa baada ya misitu ya duniani kuunguzwa kwa pigo la kwanza, basi kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto utaangukia baharini—na hiyo inawezekana ikawa ni vipande vya nyota au vimwondo. Hali hii inaelezwa zaidi katika pigo la tatu: “Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji.” Kwa maneno mengine, kimwondo kitagongana na dunia. Kama ilivyo katika sinema inayoitwa Deep Impact, ambapo kimwondo kiliangukia baharini na kusababisha mawimbi makubwa sana, basi hilo pigo la tatu litaleta madhara yanayofanana na hayo ya kwenye sinema hiyo. Pigo hili linaweza lisiwe kama inavyoelezwa katika sinema hii, lakini kitendo cha nyota au kimwondo kupiga sehemu mbalimbali za dunia hii kitaleta madhara makubwa kwa sayari hii ya dunia. Mawimbi hayo makubwa yatawaua theluthi ya viumbe waliopo baharini na yataharibu theluthi ya meli.
Wakati upepo wa dhiki utakapoanza kuvuma, sisi sote tutambua ujio wa wakati wa farasi wa kijivujivu. Hapo baadaye, utakapoona habari ikielezwa katika luninga yako ikieleza kuwa moto unashuka toka angani na kwamba theluthi ya misitu ya dunia inateketea kwa moto, basi utapaswa kutambua kuwa yale ambayo yalipaswa kuja yameshawasili. Wakati serikali zitakapokuwa zikiwapanga watu wakubwa kwa wadogo ili kuuzima moto basi utapaswa kuwa na hakika kuwa mwanzo wa nyakati za mwisho umeshawadia.
Kwetu sisi tunaoamini katika injili ya maji na Roho, tumaini la wokovu ambalo litatukomboa toka katika mapigo haya ya kutisha linapatikana katika Mungu Mwenyezi tu. Wakati Mpinga Kristo atakapotuua, basi tutaifia-dini kwa kuwa hatuna nguvu za kidunia za kupambana naye, hata hivyo, tutaifia-dini katika furaha kuu. Mungu Mwenyezi atatufufua sisi ambao tutakubali kuifia-dini katikati ya Dhiki ya kutisha katika imani, na Bwana atafanyika kuwa Mchungaji wetu na atatuongoza kwenda katika mto wa maji ya uzima.
Baada ya kuujenga Ufalme wa Mungu, Mungu atatupeleka katika ufalme huo, yaani mahali ambapo hatutateseka kamwe kwa moto, wala kwa kiu, wala kwa madhara ya jua. Neno linatueleza kuwa Mungu ataishi pamoja nasi katika Ufalme huu, atatufariji, atayafuta machozi yetu, na ataturuhusu kuishi katika utukufu milele ili kwamba tusiteseke tena.
 

Simama Imara Katika Neno la Ahadi
 
Ninapodumu katika Biblia, basi moyo wangu unajazwa na Roho Mtakatifu katika tumaini, na ndipo ninapotambua kuwa ni Mungu pekee tu ndiye anayeweza kutukomboa toka katika mapigo haya ya kutisha. “Na uje Bwana Yesu!” ninamwamini Bwana wetu. Ninaamini kuwa Bwana atanikomboa toka katika Dhiki ya kutisha kama alivyonikomboa toka katika dhambi zangu zote. Ninaamini pia kuwa Bwana atawakomboa na watakatifu wenzangu pia. Hata kabla ya kuja kwa siku za mwisho, ninaamini kuwa wokovu wangu upo katika Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi cha Mwana-Kondoo, pia ninaamini kuwa wokovu wako pia unapatikana katika Mungu.
Hivi punde ulimwengu utajawa na mapigo na dhoruba za Dhiki Kuu. Lakini haijalishi jinsi ulimwengu huu unavyoweza kubadilika na kuwa mgumu, mimi ninaamini kuwa Mungu wetu atatukomboa toka katika dhiki na mapigo ya nyakati na mateso ya adui zetu, hii ni kwa sababu Mungu ametukomboa toka katika dhambi zetu zote na ametupatia haki ya kufanyika kuwa watoto wake.
Wale ambao hawajazaliwa tena upya wana matatizo makubwa kuliko sisi. Je, halitakuwa ni jambo la kusikitisha kutokuwa na Mungu ambaye wanaweza kuweka tumaini lao, wakati kila kitu kitakapokuwa kikiungua na machafuko kuenea? Baadhi ya watu hawataona shaka kushikilia dini zao, kwamba ni dini ya Budhaa au Uislamu, lakini wataona hakuna tumaini katika dini hizo. Kitakachokuwa kikiwangojea ni kuchanganyikiwa na huzuni. Kutakuwa na watu wengi sana ambao watakabiliana na mauti yao katika hali ya huzuni kiasi hicho. Sisi nasi, tutakabiliana na machafuko na magumu kama yatakayowapata watu hawa. Lakini mioyo yetu ni tofauti na mioyo yao. Sisi ambao tunaiandaa imani yetu sasa tupo tofauti na wengine, kwa kuwa Mungu ametufanya tusio na dhambi kwa kupitia injili ya maji na Roho.
Yohana 1:12 inatueleza kuwa, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” Kwa maneno mengine, Mungu ametuwekea muhuri wa haki kufanyika watoto wa Mungu, hali akitueleza, “Ninyi ni watoto wangu.” Mungu ametupatia hii haki kuu na yenye utukufu. Sisi ni watoto wa Mungu. Tunapoiamini injili ya maji na Roho, je kunakuwa na dhambi yoyote iliyosalia ndani ya mioyo yetu? Kwa kweli hapana! Je, sisi hatujafanyika kuwa watoto wa Mungu? Kwa kweli tumefanyika! Ikiwa watoto wa Mungu wanapungukiwa ufahamu wa Neno la Mungu na wana mapungufu mengi, je, hii ina maanisha kuwa Mungu hatawalinda kama Baba yao? Kwa kweli sio hivyo! Kama wazazi wanavyohitaji kuwa makini katika kuwaangalia watoto wao ambao hawana ufahamu, basi Mungu anatoa nguvu zaidi na ulinzi zaidi kwetu sisi ambao ni wadhaifu.
Wakati machafuko yatakapoenea kwa sababu ya ujio wa Mpinga Kristo, Mungu atawafanya watoto wake kuwa imara kwa kupitia Roho Mtakatifu, na atawapatia imani, tumaini, na ujasiri. Kwa kuwa Mungu atatupatia ujasiri, basi ni hakika kuwa hatutakuwa na woga. Hatutakuwa na kitu cha kuogopa zaidi ya hofu yenyewe kuinuka ndani ya mioyo yetu. Watu wanaweza kuogopa na kuyakwepa yale yanayotendeka karibu yao, lakini hofu katika mioyo yao haiwezi kuondolewa hata kama watapelekwa mahali gani. Hata kama watajificha vyumbani, au katika ngome, au katika nyumba za kujikingia mabomu, ukweli ni kuwa hawawezi kuikimbia hofu iliyo ndani ya mioyo yao.
Kwa upande mwingine, mioyo ya watakatifu haina uoga bali ina ujasiri na kwa sababu hiyo inaweza kukabiliana na kuifia-dini kwa ujasiri hali ikijisemea, “Kile kilichokuwa kinangojewa sasa kimewadia. Sasa ni wakati wa kurudi kwa Bwana! Muda si mrefu Bwana atatuchukua!” Hapa ndipo kunyakuliwa kutakapotokea—si katika siku ya kawaida kama ya leo, bali ni wakati ambapo theluthi ya ulimwengu itakapokuwa ikiteketea kwa moto. Lakini kabla Dhiki haijawa mbaya zaidi, Mungu atawanyakua watakatifu kwenda mawinguni.
Je, unaamini sasa kuwa Mungu amezipanga nyakati saba kwa ajili yako? Ufunuo sura ya 6 inatueleza kuwa Mungu amezipanga nyakati hizo. Kama Mungu alivyopanga, basi Mungu atahakikisha kuwa kila kitu kina washuhudia watakatifu kama ilivyoandikwa. Kwa hiyo, wale waliopatanishwa dhambi zao wamebarikiwa sana, lakini wale waliosita na ambao hawakuamini katika injili wana bahati mbaya ya kuishia kuzimu. Mungu anatueleza kuwa mapigo ya kutisha yatakuja hapo baadaye, na wakati mapigo haya yatakapokuwa yamepita, basi wale waliozaliwa upya watatupwa katika ziwa la moto. Hii ndiyo sababu Mungu ametupatia ulimwengu wenye amani kwa sasa, na hii ndio sababu Mungu ametukabidhi injili yake katika wakati wa amani kama huu.
Takribani miaka 2000 iliyopita Mungu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu. Aliupokea ubatizo kwa ajili yetu ili kuzichukua dhambi zetu zote na kisha akafa Msalabani ili kutukomboa toka katika dhambi zote za ulimwengu. Mungu alituokoa sisi kama Mwokozi wetu. Mungu ametupatia baraka yake ambayo imeturuhusu kuokolewa kwa kumwamini Mungu na wokovu wake. Hii ni neema ya Mungu. Hii ni injili ambayo imetukomboa toka katika dhambi zetu zote na hukumu ya Mungu kwa kumtuma Mwana wake pekee, kwa kuzipitisha dhambi zetu kwenda kwake, na kwa kumhukumu Mwanawe pekee kwa niaba yetu. Kwa kuamini katika ukweli huu sasa, basi tunavikwa katika neema ya Mungu na tunapokea uzima wa milele toka kwake. Kwa kuwa tunaamini katika ukweli huu, basi sisi tumefanyika kuwa watoto wa Mungu, na kwa kuwa tumefanyika kuwa watoto wa Mungu, basi Mungu atatuita na kutulinda wakati Dhiki ya wakati wa mwisho itakapokuwa katika hatua zake za mwisho.
Katika wakati huu, watoto wa Mungu na watoto wa Shetani watatofautishwa kwa wazi. Tofauti zao zitaonekana wazi. Jambo hili litajadiliwa kwa kina hapo baadaye. Unachopaswa kukikumbuka sasa ni kuwa wakati Dhiki Kuu itakapotujia na kuuawa kwa kuifia-dini, basi tutafufuliwa na kunyakuliwa kwenda mbele za Mungu. Haijalishi kiwa mtu anaamini katika ukweli huo au la; jambo hili litatokea kwa kuwa Mungu amesema kuwa ataziinua pepo na hivyo kuyafanya mambo haya yote kupita.
Aya ya 1 inatueleza kuwa, “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.” Mungu anazishikilia pepo hizi ili kwamba zisiweze kuvuma sasa. Kwa lugha nyingine, hii ina maanisha kuwa wakati Mungu atakaporuhusu, basi hizi pepo zitavuma toka katika pembe nne za dunia. Wakati pepo hizi zitakaporuhusiwa na Mungu, basi malaika wa Mungu wataziachia zile pepo na kuanzisha wakati wa farasi wa kijivujivu. Hivyo wakati upepo wa Dhiki Kuu utakapoanza kuvuma hali ukileta majanga ya kiasili na vita kila sehemu ulimwenguni, basi kila mtu atakuwa katikati ya matatizo hayo. Lakini hadi sasa, bado Mungu amezishikilia hizo pepo kwa nguvu.
Nchi nyingi duniani zinawekeza fedha nyingi katika uzalishaji wa silaha. Unaweza kuwadia wakati ambapo mataifa yenye nguvu yatatumia asilimia 30 ya pato lao la kitaifa lijulikanalo kama GNP kwa masuala ya kijeshi. Hata sasa, rasilimali nyingi zinapelekwa katika matumizi ya kijeshi kwa lengo la kukuza kiwango kikubwa cha silaha, yaani silaha za maangamizi. Kila inapotokea kuwa uchumi umeboresheka, basi mabaki ya fedha hupelekwa katika kupanua shughuli za kijeshi.
Kwa mfano, kwa sasa Marekani inajaribu kusukuma wazo la kuanzisha mpango wa kujihami uliopewa jina la “Mpango wa Vita vya Nyota.” Wakati mpango huu utakapokuwa umeshaendelezwa kikamilifu, vita haitapiganwa tu hapa duniani bali itaweza kupiganwa hata katika anga za mbali wakati ambapo satalaiti zenye silaha zitaweza kupiga mabomu ya masafa marefu kwenda ardhini. Vita ya angani kwa wakati huo itakuwa na maana nyingine kabisa. Kwa hiyo swali la msingi ni hili kuwa ni nani atakayekuwa wa kwanza kutengeneza silaha zaidi za hewani na kisha kutawala anga za mbali kwa matumizi ya kijeshi.
Tunapoyaangalia maendeleo kama hayo, tunaweza kuona kuwa wakati Mungu atakaporuhusu, na wakati mapigo ya kutisha yatakaposhuka duniani, basi yule mtawala aliyetabiriwa mwenye nguvu kamili atainuka.
Hata hivyo, haya mambo yote yatatokea wakati Mungu atakapoyaruhusu. Haijalishi jinsi ulimwengu utakavyogeuka na kuwa mgumu, tunaamini kuwa Mungu atakuwa Mchungaji wetu, atatuongoza kwenda katika kijito cha maji ya uzima, na atayafuta machozi yetu yote. Hii ndiyo sababu waliookolewa wamebarikiwa sana.
Unapomwamini Yesu, huwezi kumwamini Yesu kwa namna yoyote ile unayojisikia. Imani ya kweli ni imani ya wale wanaoamini katika Neno la Mungu.
Ufunuo 7:14 inatueleza kuwa, “Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” Kule kusema, “wameyaosha mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo,” maana yake ni kwamba waliuawa na kuifia-dini kwa sababu ya imani yao katika Bwana. Unapaswa kuwa makini katika kuifafanua aya hii; aya hii haimaanishi kuwa tunaokolewa kwa kuamini katika damu ya Msalaba tu.
Bali, unachopaswa kukitambua ni kuwa wale ambao mioyo yao haikaliwi na Roho Mtakatifu si watoto wa Mungu, na kwamba wale wasio amini katika injili ya maji na Roho ndio wale wasioiamini injili kabisa. Ni wale tu wanaoamini katika injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kukubaliana na kuifia-dini, kuishinda Dhiki, na kwa sababu hiyo kumpatia Bwana utukufu.
Kwa kuwa tunamwamini Mungu, basi wakati wa shida kuu na mateso hatutaipoteza imani yetu wala hatutasalimu amri kwa Shetani, bali tutapokea kuuawa kwetu kwa kuifia-dini kwa nguvu tutakayoipokea toka kwa Mungu. Kisha tutafufuliwa na Bwana na kulindwa na Yeye. Mwana-Kondoo atafanyika kuwa Mchungaji wetu na atayafuta machozi katika macho yetu, na hatutapata njaa tena, wala hatutaona kiu, wala joto halitatudhuru, wala kuteseka kwa kitu chochote kile. Kwa nini? Kwa sababu Mungu atayaondoa mateso milele, kwa kuwa tutakuwa tumeshapitia kipindi cha Dhiki Kuu. Hivi ndivyo ulimwengu wa Mungu wa kushangaza unaoitwa Mbinguni utakavyokuwa. Kwa kuwa ni mahali pa kushangaza na pazuri sana, watu wanapaita mahali hapo Paradiso au Mbinguni kama kitovu cha mema yote.
Paradiso ni mahali penye furaha isiyo na mwisho. Katika Ubudha, paradiso ni mahali palipohifadhiwa kwa wale tu waliofanyika kuwa miungu, yaani Budha. Lakini ni kweli kuwa kuna mtu anayeweza kugeuka na kuwa Budha, yaani mtu anayeweza kugeuka na kuwa mungu? Kwa kweli hapana! Siddhartha alipokuwa amelala kitandani karibu ya kufa alisema, “Fanyika kuwa mungu; ni kwa kufanyika mungu ndipo unapoweza kuyakwepa mateso na mahangaiko ya ulimwengu.” Lakini ni vigumu kwa mtu yeyote kuikwepa dhambi na kuvikwepa vitisho vyake vya mauti kwa nguvu zake binafsi. Yeye mwenyewe Siddhartha alishindwa kuikwepa dhambi na vitisho vyake, na hivyo ndivyo kila mtu asivyoweza kukwepa. Kama Neno linavyotueleza, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Wokovu wetu unatolewa na Mungu mwenyewe tu, ambaye ni Yesu Kristo aliyeuumba ulimwengu wote na aliyetuumba sisi. Ukweli huu, kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi ambaye atatukomboa toka katika mapigo ya kutisha, ndio ukweli ambao Mungu anatufundisha kwa kupitia Roho Mtakatifu.
Mbinguni ni mahali pazuri zaidi. Je, unapenda kuishi milele kwa furaha katika heshima na utukufu? Je, unapenda kutambuliwa kama mtu wa thamani na kuishi katika furaha ya milele? Je, unapenda kuishi katika ukamilifu na katika baraka ya kutokupungukiwa na kitu? Basi mahali ambapo Mungu atatuita ili tukaishi ni mahali kama hapo. Yaani ni Mbinguni. Hiyo Mbingu haina upungufu wa kitu chochote kile. Hutaugua kamwe tena, wala joto halitakudhuru, na wala hutamwaga machozi tena.
Wakati Yesu aliposulubiwa, alimwambia yule mwizi aliyesulubiwa pamoja naye, “leo hii utakuwa pamoja nami peponi [Paradiso].” Kiuandishi, “Paradiso” maana yake ni bustani ya furaha. Ni mahali ambapo mtu anaweza kuzifurahia furaha zote. Yale yanayotufanya tuwe na furaha na kuufurahia ulimwengu huu yanatoka katika sehemu hii ya Paradiso mahali ambapo Mungu atatuita ili tukaishi. Hebu amini, ili uweze kuifanya Paradiso, Mbingu, ambao ni Ufalme wa Mungu kuwa mali yako. Ufalme wa Mungu ni mkamilifu na mwema, kwa maana hakuna uchafu wa falme za kidunia unaoweza kupatikana katika Ufalme wa Mungu.
Kwa kuwa Mungu ni mwenyezi, basi ni hakika kuwa atatupatia Ufalme wake. Kwa kuwa Bwana wetu ni Mungu Mwenyezi, basi atawakomboa watu wake na kuwafanya wasimwage machozi tena, wala wasiteseka kwa kitu chochote kile. Mungu atatuongoza kwenda katika chemchimi za maji ya uzima, na furaha ya milele. Ninaamini kuwa mambo haya yote yanawezekana kwa kuwa nguvu za Mungu ni kuu.
Ikiwa Mungu aliyetuokoa sisi angelikuwa hana nguvu, basi sisi nasi tungelikuwa hatuna nguvu. Lakini Mungu aliyetukomboa ana nguvu kamilifu. Ametufanya sisi kuwa tusio na dhambi kwa nguvu zake kamili, na ndio sababu tunaitwa watakatifu wake.
Haijalishi aina ya maisha tuliyonayo hapa duniani. Kwa kuwa sisi ni watoto wa Mungu na tuna nguvu za Mfalme wa wafalme, basi hata kama maisha yetu ni mabaya kuliko ya wale ambao hawajazaliwa tena upya, basi kipindi cha farasi wa kijivujiuvu kitakapowadia na wakati Bwana atakaporudi, ni hakika kuwa Bwana atatuita mawinguni na kutufanya tuishi katika Paradiso yake. Hatatupungukiwa chochote na tutatawala kwa mamlaka kamili na ambapo hata malaika watakuwa ni watumishi wetu. Watakatifu wataishi milele katika utukufu wote.
Watakatifu hawatakufa tena milele. Hivi ndivyo dini zote zinavyoota—yaani kuishi milele, kutawala, na kuingia Mbinguni. Baraka hii si kwa ajili yangu tu bali Mungu ameitoa sawa sawa na kwako wewe pia.
Wakati muda utakapowadia, ninaamini kuwa Mungu atauinua upepo wa dhiki, na wakati upepo huu wa dhiki utakapovuma, basi Mungu atatutia nguvu ili kusimama kinyume na Ibilisi, na hatimaye kutuchukua pamoja naye. Pia ninaamini kuwa Mungu ataturuhusu kuishi milele kwa furaha.
Je, Mungu hakutuahidia haya mambo yote? Kwa kweli ametuahidia! Mungu alitueleza kuwa, “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali, Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.” (Yohana 14:1-3). Hivi ndivyo Bwana wetu alivyotuahidi. Neno lote la Mungu katika Ufunuo sura ya 20-22 ni Neno la ahadi kwetu.
Halleluya! Ninamtolea Mungu shukrani.