Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[13-2] Kuonekana Kwa Mpinga Kristo (Ufunuo 13:1-18)

(Ufunuo 13:1-18)
Kwa kuzingatia kifungu kikuu hapo juu, sasa nitajadili juu ya kuonekana kwa Mpinga Kristo na mauaji ya wafia-dini. Kuanzia sura ya 13 tunamwona Mnyama akitoka katika bahari. Huyu Mnyama, ambaye ana pembe kumi na vichwa 7 si mwingine bali ni Mpinga Kristo. Kifungu hiki kinatueleza kwamba juu ya pembe za yule Mnyama kulikuwa na vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake kulikuwa na majina ya makufuru. Pia tunaelezwa kwamba huyu Mnyama alikuwa ni kama chui, na miguu yake ikiwa kama miguu ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama mdomo wa simba. Kwa nyongeza, yule Joka akampatia nguvu zake, kiti chake cha enzi, na mamlaka makuu. Moja ya kichwa chake kilikuwa na jeraha la mauti, lakini hili jeraha la mauti lilipona kwa miujiza. 
Ulimwengu wote ulianza kumfuata yule Mnyama kwa sababu ya maajabu hayo, na kwa kuwa alikuwa amepewa mamlaka makuu na yule Joka, basi wanadamu wakamwabudu Joka na yule Mnyama, huku wakisema, “Ni nani aliye kama Mnyama huyu? Ni nani anayeweza kufanya vita dhidi yake?” Hiki kifungu kinatueleza kwamba Mnyama alipewa kichwa cha kuongea maneno makuu na makufuru, na mamlaka ya kuendeleza kazi zake kwa miezi 42.
 
 
Mnyama Akitoka Baharini
 
Alichokiona Mtume Yohana ilikuwa ni kuonekana kwa Mpinga Kristo kati ya watawala wa ulimwengu huu katika nyakati za mwisho. Huyu Mpinga Kristo alikuwa ni Mnyama aliyekuwa akitoka baharini, mnyama mwenye pembe kumi na vichwa saba. 
Kwanza ni lazima tufahamu ikiwa Mnyama huyu ndiye yule Mnyama halisi ambaye ataonekana hapa ulimwengu. Kuna mambo mawili kuhusu Mnyama ambayo ni ya msingi: kwanza, ikiwa ni kweli au si kweli kwamba huyu Mnyama ataonekana hapa ulimwenguni na kisha kuwaua watu wengi; na pili ni ikiwa Mnyama huyu anamaanisha ni Mpinga Kristo katili ambaye atatokea kati ya watawala wa ulimwengu. Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanawavuta watu wengi sana. Wale wanaoyafahamu mambo haya wanaweza kusema kwamba mambo haya ni rahisi kuyaelewa, lakini kwa wale wasioyafahamu, ni kitu cha kawaida kwao kujiuliza juu ya ikiwa Mnyama huyo ataonekana kiuhalisia katika nyakati za mwisho na kisha kuwatawala watu au la. 
Kile ambacho Mungu anatueleza katika sura ya 13 ni kuhusu kuonekana kwa mfalme katika ulimwengu huu ambaye atatawalia na Shetani. Hii sentensi inayosema, “mnyama akitoka baharini,” maana yake ni kwamba mfalme kati ya wafalme saba wa ulimwenguni atakuwa ni Mpinga Kristo. Pia kifungu hiki kinatueleza kwamba mataifa kumi yataungana pamoja na Mpinga Kristo na kisha kutawala juu ya ulimwengu utakaokuwa umeharibiwa. 
Kwa upande mwingine, jeraha la mauti katika moja ya vichwa vya yule Mnyama na kisha kupona kwake, kunatueleza kwamba mmoja kati ya wale wafalme saba atajeruhiwa kwa jeraha la mauti, lakini pia jeraha lake hili la mauti litaponywa. Kwa misingi ya tiba za kawaida, huyu mfalme atatangazwa kuwa amekufa, lakini fahamu zake zitarudishwa kwa njia ya muujiza, kisha atatenda kama Joka. Huyu Joka anasimama kumwakilisha Shetani. Kama vile Joka, Mnyama atakuwa na mamlaka yote kuwadhuru na kuwaangamiza watu. Nyakati za mwisho zitakapowadia, mtu aliye kama mnyama ataoonekana hapa ulimwenguni na kisha kuwaua watu mauaji ya halaiki, atakuwa kama vile mnyama kama anavyoonekana Godzila katika sinema. 
Kwa kuonekana kwa huyo mtumishi wa Shetani, basi ulimwengu utakuwa umeanza kukimbilia kwenda katika maangamizi yake. Njia ambayo Shetani ameamua kuitumia katika nyakati za mwisho ni kuyafikisha mateso yake kwa wanadamu kwa kupitia watumishi wake. Hii ni kanuni kama ile ya Mungu kuwaokoa wanadamu toka katika dhambi zao kwa kupitia watakatifu wake. 
Tunapawa kufahamu kwa hakika kwamba kifungu hiki kinatueleza nini kwetu. Kwa kuwa kimoja kati ya vichwa vya yule Mnyama kilijeruhiwa, basi mtawala wa ulimwengu huu, huku akiwa amepata fahamu toka katika jeraha lake la mauti, atapokea mamlaka toka kwa Joka na kisha ataheshimiwa na wanadamu kana kwamba yeye ni Mungu. Hii ndio sababu tunapaswa kukumbuka jinsi watu walivyokuwa wakimnenea huyo Mnyama, “Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?”
Huyu Mpinga Kristo anayeonekana katika kifungu hiki ataheshimiwa na watu wote chini ya utawala wa Shetani na kisha kusimama kinyume na Mungu. Hii ina maanisha kwamba kiongozi mwenye nguvu atatokea katika ulimwengu wa mwisho na kisha kuutawala ulimwengu huo. Kiongozi huyu atakuwa ni mmoja wa viongozi wa mataifa ya ulimwenguni. Baada ya kuwa amepokea roho ya Mpinga Kristo toka kwa Shetani, basi yeye atatokea kama kiongozi mwenye nguvu sana. Kisha ulimwengu utakuja kuwa chini ya utawala wa kiongozi huu na kutawaliwa naye. Hapo baadaye ulimwengu utakuja kuungana na kuwa taifa moja. Mataifa ya sasa yaliyoendelea yatashirikiana na kupanua utawala wao kwa ulimwengu mzima kwa kumtanguliza kiongozi mwenye nguvu. 
Hivi sasa kule Ulaya, tunao Umoja wa Ulaya, pia umoja wa jinsi hiyo upo pia Marekani na pia kule Asia pia, na kuna baadhi ya asasi zinazotaka kuwe na muungano wa mataifa huru ili kuwa katika taifa moja. Wakati asasi kama hizo zitakapoendelea zaidi, basi muungano wa mataifa makuu utatokea, na kiongozi mwenye nguvu atatokea toka katika mataifa yale yaliyoungana. Huyu kiongozi atatenda kama Mpinga Kristo anayesimama kinyume na Mungu. Atakuwa ni kiongozi mwenye kipaji kikubwa na mwenye mamlaka ya kuutawala ulimwengu mzima kama atakavyo. 
Kwa nini? Ni kwa sababu kwa kupokea uwezo mkuu na mamlaka toka kwa Joka, Shetani, basi hekima na ufahamu wake vitakuwa tofauti na ule wa wanadamu wa kawaida, na pia fikra zake zitakuwa ni tofauti na zile za wanadamu wa kawaida. Hekima yake na mamlaka vitafika angani. Kile anachokisema kitatekelezwa pasipo shida yoyote, na hakuna hata mmoja atakayediriki kuitamani nafasi yake. Kipindi hiki cha utawala wa huyu Mpinga Kristo ni kipindi cha farasi wa kijivujivu kilichoandikwa katika Ufunuo sura ya 6.
Ni hakika kwamba kipindi cha farasi wa kijivujjivu kitaujia ulimwengu hivi karibuni, kisha ulimwengu utakuwa ni mali ya Mpinga Kristo kwa muda. Lakini wale wasioufahamu ukweli huu wanataka kumwona kiongozi mwenye nguvu kama vile Mpinga Kristo akitokea. Hata hivyo, watakatifu wanaufahamu ukweli huu na hivyo katika kipindi hiki watakuwa makini, na hivyo wakati huu utakapowadia, wataweza kupambana na Mpinga Kristo, na kisha kuuawa kama wafia-dini ili kuilinda imani yao. 
Siku hizi ni watu wachache sana wanaowaheshimu viongozi wa nchi zao. Bila kujalisha kuwa unaishi katika nchi gani, ukweli ni kuwa kwa ujumla watu wana ile hali ya kutoridhishwa na viongozi wao wa kisiasa. Hivi sasa katika sehemu mbalimbali duniani watu wanamngojea kiongozi mwenye nguvu na mwenye uwezo. Kwa nini? Kwa sababu wanataka kiongozi ambaye atayatatua matatizo yote ambaye yameuelemea ulimwengu huu, kuanzia upungufu wa chakula hadi kwenye uharibifu wa mazingira, matatizo ya kidini, mdodoro wa uchumi, machafuko ya kikabila, na kadhalika. Wakati kiongozi wa ulimwengu, hali akiwa na hekima kubwa na mamlaka, atakapokuwa na uwezo wa kuyatatua matatizo yote, basi kila mtu hapa ulimwengu atamheshimu kama vile ni Mungu na atafurahi kutawaliwa na kiongozi huyo. Kiongozi huyu, Mpinga Kristo ambaye ana ulimwengu mzima mkononi mwake, atayashughulikia matatizo hayo yote. 
Sisi sote tunataka kiongozi wa kisiasa ambaye tunaweza kumheshimu katika mambo yote, lakini matamanio ya jinsi hiyo ni makubwa sana kuweza kufikiwa, kwa kuwa ni vigumu kwa kiongozi kama huyo kupatikana katika hali ya kawaida. Lakini kwa kuwa Mpinga Kristo atakayekuja atayatatua matatizo mengi ya ulimwengu huu ya kiuchumi na ya kisiasa, basi atakuwa ni aina ya kiongozi ambaye kila mtu anamtaka, yaani yeye anayeweza kuleta utengamano wa kisiasa na kiuchumi duniani. 
Wakati kipindi cha farasi mweusi kitakapopita na kitakapokuwa kikianza kipindi cha farasi wa kijivujivu, na kwa sababu ya mapigo ya matarumbeta saba, basi ulimwengu ulio magofu utatafuta kiongozi mwenye nguvu na mwenye uwezo. Viongozi wasio na nguvu wa nchi ndogo hawawezi kutatua matatizo ya ulimwengu. Kwa hiyo, watu watamtafuta kiongozi sahihi na makini. Mpinga Kristo atatokea wakati huu, hali akizungumza na kutenda kama vile Mungu. Kwa kuwa atakuwa ameponywa toka katika jeraha lake la mauti, watu watamshangaa sana. Na kwa kuwa atatenda kama kiongozi mwenye mamlaka makuu, ujasiri, dhamira na ufahamu, basi watu wote ulimwenguni watamfikiria kuwa yeye ni Mungu. 
Kwa hiyo, hata watu wa Israeli watamwamini kuwa ndiye Masihi waliyemngojea kwa muda mrefu. Lakini hatimaye Waisraeli watatambua kuwa yeye ni mwongo na kwamba Yesu Kristo ndiye Masihi wao wa kweli, na hivyo wengi wao wataokolewa. Mpinga Kristo atawasikia watu wakisema hivi, “Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” Basi wale wote wasiomtii watauawa bila shaka. 
Kipindi cha farasi wa kijivujivu kitakapokuja, ulimwengu mzima sio kwamba utateseka tu kutokana mapigo ya kiasili, yaani ukiwa umeharibiwa na moto uliounguza theluthi ya misitu yote na kuvukizwa kwa moshi mkubwa, bali watu wa ulimwenguni wataungana chini ya kiongozi mmoja ili kumtumikia kama mfalme wao. Yeye atakayeyatua matatizo haya yote atainuliwa na wanadamu hao kuwa kama Mungu. 
Mambo haya yote ni miongoni mwa yale ambayo Mungu ameyapanga. Kwa kuwa ili mambo haya yote yaweza kutokea ulimwenguni, basi nilazima kuwe na mabadiliko makubwa ya kimazingira duniani, na kuwe na makubaliano miongoni mwa viongozi wakuu wa kila taifa juu ya hitaji la kuwa na serikali moja inayotawala. Hivi sasa, makubaliano ya kuwa na aina hii ya kiongozi yanazungumzwa na kupangwa sana katika kipindi hiki cha farasi mweusi. Hivi sasa ulimwengu unamuhitaji kiongozi imara. Kwa kuwa viongozi wa kila taifa wanashindwa kuiondoa hali ya kutoridhika ya watu wao, basi wanadamu hivi sasa wanamtafuta kiongozi mwenye nguvu anayeweza kuyatatua matatizo yote wanayokabiliana nayo. 
Ikiwa utaangalia kwa karibu juu ya kile kinachotokea hapa ulimwenguni, basi utatambua kwamba mambo haya yote yapo karibu sana kukamilika. Kiongozi aliyetabiriwa atakuwa ni mkatili sana, mtu mwenye nguvu kamili na uwezo mkuu, kama anavyoonekana kutokana na maelezo kwamba miguu yake ilikuwa ni kama ile ya dubu, na kinywa kama cha simba, na mwenye sura kama ya chui. 
Huyu mtu, hali akipokea mamlaka toka kwa Joka, atamkufuru Mungu, na malaika wake Mbinguni, na watakatifu wake. Naye atapigana na watakatifu na kisha kuwashinda. Mpinga Kristo atawaua watakatifu katika mapambano yake dhidi yao, huku akiwataka kuikana imani yao. Kwa kuwa watakatifu hawataikana imani yao wakati huu, basi watakatifu hao wote watauawa kama wafia-dini. Na kwa kuwa Mpinga Kristo atakuwa na mamlaka juu ya ulimwengu wote, basi atawaua kwa uhuru wale wote wasiozitii amri zake. 
Aya ya 8 inatueleza kwamba, “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.” Kwa kuwa Mpinga Kristo atatawala kama kiongozi mkuu wa wakati huo, basi yeyote asiyemtii yeye atauawa kwa amri yake. Hata hivyo, wakati huo utakuwa ni wakati wa kufia-dini kwa watakatifu wote. 
Katika aya ya 8 hapo juu, kuna neno “kusujudu” na maana yakeni kumheshimu na kumtumikia yeye aliye mkamilifu. Katika nyakati za mwisho, Mpinga Kristo ataabudiwa na watu hapa duniani kama vile ni Mungu, atapokea heshima kubwa sana ambayo hakuna mfalme yeyote aliyepita hapa duniani aliyewahi kuzipata. Hata hivyo kundi fulani la watu halitamsujudia kiongozi huyu. Na kundi hilo si jingine bali ni “Wakristo waliozaliwa tena upya.” Wao hawatamtambua Mpinga Kristo kuwa ni Mungu, na kwa hiyo, hawatamsujudia na kwa sababu hiyo watauawa ili kuilinda imani yao. 
 

Mnyama Mwingine Akitoka Katika Nchi
 
Mpinga Kristo pia anaye nabii wake wa uongo. Huyu nabii wa uongo ndiye atakayemwinua Mpinga Kristo, pia atawatisha na kuwaua wale wote wasiomtii Mnyama. Ufunuo 13:11 inasema, “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.” Mnyama wa pili anayeonekana hapa ni mtumishi wa Mnyama wa kwanza—yaani Mpinga Kristo. Kama Mpinga Kristo, yeye naye atasimama kinyume na Mungu na kuwaua watu wa ulimwengu na wenye haki. 
Hali akiwa amepokea mamlaka toka kwa Joka, atawalazimisha watu kumsujudia Mpinga Kristo aliyekuja kabla yake kama Mungu. Na kwa kuwa yeye naye atakuwa amepokea mamlaka toka kwa Joka, basi atatenda yale ambayo Joka anataka ayatende. Sio tu kwamba atawafanya watu wamwabudu Mpinga Kristo aliyekuja kabla yake na kuwaua wale wote wasiomtii, bali pia atatenda miujiza, kama vile kuleta moto toka angani, na pia atatenda kama Mpinga Kristo. Atamfanya Mnyama kuwa ni Mungu na atatengeneza sanamu za Mnyama, yaani yule aliyekuwa amepata jeraha la mauti lakini akapona toka katika jeraha lake. 
Ni nani basi ambaye atatenda mambo haya yote? Huyo ni nabii wa Mpinga Kristo. Kazi yake ni kutengeneza sanamu ya Mpinga Kristo aliyekuja kabla yake na kisha kuwafanya watu wamwinue huyu Mpinga Kristo kama vile Mungu. Ili kufanya hivyo, ataipulizia hiyo sanamu ya Mpinga Kristo pumzi ya uhai ili iweze kuongea, na kisha kuwaua wale wote ambao hawaisujudii sanamu hii ya Mnyama pasipo kujali idadi yao. Kwa kuwa watakatifu watauawa ili kuifia-dini kwa kukataa kuisujudia sanamu, basi idadi kubwa ya wafia-dini watauawa wakati huo. 
Kwa upande mwingine, kila mtu ulimwenguni ambaye hajazaliwa tena upya atatetemeka mbele ya kifo chake na kuishia kuwa mtumwa wa kifo chake. Kwa hiyo, watu wengi wataishia kumsujudia Mpinga Kristo kama vile ni Mungu. Wale walio na akili zenye ufahamu mzuri wanaweza kuinuka na kuleta upinzani dhidi ya huyo dikteta, lakini watauawa kwa haraka sana, watauawa kwa moto unaotoka katika kinywa cha yule nabii wa uongo na Mpinga Kristo. 
Huyu nabii wa uongo, baada ya kuwa ametengeneza sanamu ya Mpinga Kristo, atasema hivi, “Kila mtu ni lazima apokee alama ya jina lake au namba yake!” kisha atatengeneza sera yake kwamba yeyote asiyekuwa na alama ya huyu Mnyama kutofanya aina yoyote ile ya biashara, ili kwamba kila mtu aweze kupokea alama hii ya jina la Mnyama. Aya ya 18 inasema, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” 
Maelezo haya yapo wazi kabisa. Ingawa tunaweza kufikiri kwamba namba 666 kuwa ni kitu kilichojichanganya, kwa kweli namba hii ina maanisha ni jina la Mpinga Kristo au namba yake. Kupokea alama au chapa ya Mnyama maana yake ni kupokea alama ya jina lake katika kipaji cha uso au katika mkono wa kuume. Kitendo hicho kinalenga kuliandika jina la mtu katika mwili wa mtu, yaani likiwa limeandikwa katika namba au kuwekwa katika mfumo wa digitali wa baa-kodi. 
Alama hii itahitajika kila mahali wakati mtu akijaribu kununua kitu chochote. Hata ukipanda basi, utahitajika kuonyesha hii namba ya digitali ikiwa imeandikwa katika mwili wako, na pasipo kuwa na namba hiyo basi hutaruhusiwa kufanya safari yoyote. Kipindi cha leo ndio kipindi halisi cha digitali. Ni kipindi cha namba. Kwa kuwa kila kitu kimetafsiriwa katika namba, basi kile ambacho zamani kilikuwa kimefanywa kuwa kigumu hivi sasa kimerahisishwa. Ni katika kipindi hicho ndipo alama ya Mnyama itakapoonekana. 
Mpinga Kristo atatengeneza sanamu yake na kuwataka watu waiabudu kama vile ni Mungu. Ni hakika kwamba utafika wakati ambapo watu watatakiwa kumwita Mpinga Kristo kuwa ni “Mungu” wao, watamsifu na kisha kuliitia jina lake kwa heshima, kisha watalipokea jina lake katika mikono yao ya kuume au katika vipaji vya nyuso zao. Wakati mambo kama hayo yatakapotoka, basi watakatifu wote watauawa kama wafia-dini. Mpinga Kristo atawataka watakatifu kuipokea alama yake na kisha kumsujudia yeye, huku akisema, “Kwa hiyo mnamwamini Yesu? Mnamwamini kuwa ni Mungu wenu? Achaneni naye! Hebu muisujudie hii sanamu na badala yake mniite mimi kuwa ni Mungu! Niaminini mimi kwamba ndiye niliye mkamilifu! Ikiwa hamtafanya hivyo basi ni hakika kwamba mtakufa!” 
Mpinga Kristo atataka kuwe na imani moja ulimwenguni kote. Na atamtaka kila mtu kumwabudu yeye kama Mungu. Wale wasiokiri wakati huo kuwa yeye ni Mungu watauawa wote. Mpinga Kristo atawaua watakatifu wanaosimama kinyume naye hadharani. 
Wale wote ambao majina yao hayajaandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-kondoo wataipokea alama ya Mnyama na kumwabudu. Tunapopokea ondoleo la dhambi katika mioyo yetu, Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu, na majina yetu yanaandikwa katika Kitabu cha Uzima katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa kuwa majina yetu yameandikwa katika Kitabu cha Uzima na kwa kuwa Roho Mtakatifu ameitia mihuri mioyo yetu, basi sisi sote tutainuliwa kama watoto wa Mungu wakati atakapotuita. 
Je, tunaweza kweli kumkana Yesu Kristo ambaye ametuokoa, na kisha kuitangaza sanamu ya Mnyama kuwa sasa ndio Mungu wetu na Mwokozi? Kwa kweli haiwezekani! Haijalishi hata kama tuna mapungufu kiasi gani mbele ya Mungu, ukweli ni kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, akazisafisha dhambi zetu zote kwa kuzichukua dhambi hizo katika mwili wake kwa ubatizo wake, kisha akatuokoa kwa kuhukumiwa kwa niaba yetu Msalabani. 
Pia, kwa kuwa Bwana wetu amekwisha tuambia kuhusu mambo haya yote yatakayokuja mapema, basi sisi wenye haki hatuwezi kuikana kamwe imani yetu wakati huo wa Mpinga Kristo. Ingawa wakati wa dhiki utatujia na kisha kufuatia na vifo vyetu, bado tunaamini kwamba Bwana wetu atatufanya kuishi katika Ufalme wake wa Mbinguni na kutufufua na kutunyakua mara baada ya kuuawa kwetu na kuifia-dini. 
Kwa kuwa tunaamini kwamba baada ya kunyakuliwa kwetu Mungu atauangamiza ulimwengu huu kwa kuyamimina mapigo yake ya mabakuli saba, na kwamba baada ya mapigo haya tutashuka hapa duniani na kisha kutawala kwa miaka elfu moja, hatuwezi kamwe kupiga magoti mbele ya sanamu. Hii ndio sababu watumishi na watakatifu wa Mungu watayatoa kwa hiyari maisha yao. 
Nabii wa uongo atajaribu kutushawishi kinyume chake. Atajaribu kutununua huku akisema, “Tazama, kwa sasa machafuno ni mengi sana katika ulimwengu huu. Wakati kila mtu wakiwemo wataalamu na wanazuoni wanamwamini na kumfuata huyu kiongozi mkuu kama Mungu, inawezekanaje basi kwa ninyi kumkataa huyu mfalme wetu mkamilifu?” Lakini kama tutalifahamu na kuliamini Neno la Mungu wakati wote, basi hapo mwishoni tutashinda kwa kuyakubali na kuyapokea mauaji yetu ya kuifia-dini. 
Katika Ufunuo 14 kunaonekana watakatifu 144,000 wakimsifu Mungu Mbinguni. Hii inatueleza juu ya ufufuo wa watakatifu na unyakuo wao mara baada ya kuuawa kama wafia-dini. Tunaweza pia kuona juu ya unyakuo katika sehemu mbalimbali katika Biblia, kama alivyotueleza Paulo juu ya ujio wa Kristo mara ya pili, au yale ambayo watumishi wengine wa Mungu walioyatabiri katika Agano la Kale, yaani kwamba watakatifu watainuliwa angani na kujiunga katika karamu ya harusi ya Mwana-kondoo pamoja na Bwana. Watakatifu wataingia katika karamu hii ya harusi. 
Wakati watakatifu watakapokuwa wameingia karamu ya harusi ya Mwana-kondoo huko Mbinguni, basi mapigo ya mabakuli saba yatamiminwa hapa duniani, nayo yataufanya ulimwengu huu kuwa magofu. Baada ya hili, dunia itafanywa kuwa mpya, kisha watakatifu watashuka pamoja na bwana na kisha kutawala katika Ufalme wa Kristo kwa miaka elfu moja itakayofuata. Tunapoufahamu ukweli huu wote, je, tunaweza kweli kumwita Mpinga Kristo kuwa ni Mungu? hata kama atatutupa katika kila aina ya majaribu na vishawishi ili kutufanya tuisujudie sanamu yake, yaani tumsujudie kama ni Mungu, anaweza kweli kutufanya tuikane imani yetu katika Mungu wa kweli? Kwa kweli hapana!
Kama ilivyoandikwa katika Biblia, “imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Waebrania 11:1),” manabii wanaamini katika yale ambayo Mungu amewaeleza mapema kuhusu mambo yatakayojiri. Watumishi na watu wote wa Mungu wanaoliamini Neno ni makuhani na manabii. Mungu anaziongoza nafsi nyingi kupokea ondoleo lao la dhambi kwa kutufanya sisi kuihubiri injili ya ondoleo la dhambi kwa kila mtu ulimwenguni. Kwa kuwa Bwana wetu ametuokoa bila kujalisha mapungufu tuliyo nayo mbele yake, basi Mungu ametufanya sisi kuwa watu wake, na hadi wakati huu, Mungu ametupenda, ametuongoza, na kutubariki pasipo kubadilika. 
Si tu kwamba Bwana ametupatia amani ya moyo, bali ametufanya sisi kuyaweka matumaini yetu katika Ufalme wa Mbinguni kwa kutupatia Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, tunapomsikia Mpinga Kristo akitueleza kumsujudia yeye kama Mungu, basi ukweli ni kuwa hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kumpinga kwa kina toka katika mioyo yetu. 
Mara ya kwanza tunaweza kutatizwa na mfuatano wa matukio hadi tutakapotambua kwamba wakati ambao Mungu aliuongelea umewadia, lakini sisi watakatifu tutapata ufahamu wetu haraka na kuanza kumpinga Mpinga Kristo. “Kwa hiyo unadhani wewe ni Mungu halisi? Je, uliuumba ulimwengu? Je, ulimuumba mwanadamu? Je, wewe ndiwe Bwana kweli wa roho za watu?” Haya ndiyo maneno ambayo tutayatumia kumpinga Mpinga Kristo. 
Wakati Mpinga Kristo atakapowaua watakatifu na watumishi wa Mungu wakatio huo, basi ni hakika kwamba sisi nasi tutakufa. Kwetu sisi hakuwezi kuwa na mabadiliko ya Mungu. Imani haiwezi kuja kwa kulazimishwa. Wala imani haiwezi kuonekana au kutoweka kwa misingi ya kutumia nguvu. Ukweli ni kuwa imani ya kweli ina nguvu sana ya kuweza kushinda shuruti. Hivyo, watakatifu watauawa kama wafia-dini, na Mpinga Kristo ataishia kuwakosa watakatifu. 
Wakati Mpinga Kristo atakapotengeneza sanamu ya sura yake na kuwataka watakatifu kuisujudia kama Mungu, watakatifu na watumishi wa Mungu watampigia kelele wakisema, “Wewe ni mtumishi wa Mungu au mtumishi wa Shetani? Je, unaifahamu injili ya maji na Roho? Je, unafahamu na kuamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu? Yesu Kristo atakaporudi hapa duniani atawatupa watu kama wewe katika shimo la kuzimu! Umesikia wewe mwana wa Shetani?” Kisha Mpinga Kristo na nabii wake watawaua watakatifu, na watakatifu watavipokea kwa furaha vifo vyao ya kuifia-dini kwa ajili ya Mungu. 
Aya ya 10 inatueleza kwamba “mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga.” Hii ina maanisha kwamba ikiwa Mpinga Kristo atawaua watakatifu, basi Mungu atamtupa na yeye na wafuasi wake katika shimo la kuzimu lisilo na mwisho, pia atawaua hapa duniani. Wakati wale wanaosimama kinyume na Mungu watakapowatesa watakatifu, basi ni hakika kwamba hata wao watakabiliana na mateso makubwa zaidi toka kwa Mungu. 
Kwa hiyo, ni lazima tusimame dhidi ya Mpinga Kristo kwa kuishikilia imani yetu. Kipindi cha mateso ya watakatifu wakati huo kitadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu tu. Lakini Mungu anaweza kuyapunguza mateso ya watakatifu na dhiki yao, kwa kupunguza kipindi hicho kuwa miezi michache au wiki kadhaa. Ingawa watakatifu watauawa, ukweli ni kuwa wataishi tena. Watafufuliwa na kunyakuliwa, kisha watabarikiwa kutawala pamoja na Yesu Kristo katika Ufalme wa Milenia. 
Wakati Ufalme wa Mileni utakapokuja, uzuri wa hali ya mazingira utafikia kiwango chake cha juu, na watakatifu watatawala pamoja na Bwana wakiwa katika miili mitakatifu iliyobadilishwa toka katika miili yao ya kimwili ya kale. Kisha wataishi kwa furaha pamoja na Bwana katika Mbingu na Nchi Mpya. Inawezekanaje basi, sisi tunaofahamu na kuamini katika mambo haya yote kushindwa kuvumilia mateso ya muda mfupi yatakayotujia kwa ajili ya imani yetu katika Yesu? 
Haijalishi jinsi dhiki ya wakati huo itakavyokuwa kali, ukweli ni kuwa watakatifu wengi watauawa kama wafia-dini, na kwa sababu hiyo hakuna msingi wowote wa sisi kutovikubali na kuvipokea vifo vyetu kama wafia-dini. Kwa kuwa mambo haya yote ni ya kweli, basi ni hakika kwamba hatutasalimu amri kwa Dhiki ambayo itatudumu kwa muda mfupi tu hapa ulimwenguni. Kwa mfano wa mbali, hata kama ulimwengu utageuka na kuwa kama paradiso kwa miaka mia au kwa maelfu ya miaka, sisi hatutaweza kusalimu amri kwa Mpinga Kristo. Mambo haya yote hayapo mbali nasi, bali yatatimia kwetu sisi hivi karibuni. 
Hivyo, ni lazima tuihubiri injili ya maji na Roho hivi sasa, yaani wakati ambapo ulimwengu una amani. Kwa sasa tunaieneza injili ya maji na Roho kwa juhudi ili kujiandaa kwa ajili ya nyakati za Dhiki Kuu. Kwa muda wa mwaka mmoja, injili hii tunayoihubiri itazitenda kazi zenye maajabu sana. Kitaifa na kimataifa kazi njema kabisa za injili zitajitokeza. Kwa mara ya kwanza, watu wanaweza kuichukulia injili ya maji na Roho kwa wepesi, lakini watu wengi wasiolifahamu Neno la Ufunuo watalitafuta na kulisikia na kisha kuirudia injili ya maji na Roho, hii ni kwa sababu watavutiwa sana na Neno la Ufunuo na kwa sababu hiyo watalichukua Neno hilo kwa uzito. 
Ufunuo 13 ni sura ya mauaji ya kufia-dini ya watakatifu. Wakati mauaji ya kufia-dini yatakapowadia, watakatifu watauawa kwa panga au kupigwa risasi hadi kifo. Hivyo watakatifu wengi watauawa kwa mkono wa Mpinga Kristo. Lakini tutaweza kukabiliana na vifo vyetu pasipo hofu, kwa kuwa vitakuwa ni vifo vyetu vya miili tu, na wala havitakuwa vifo vya imani yetu. Hali tukiwa tumejazwa na Roho Mtakatifu, tutatoa maneno yasiyoweza kuelezewa ya kijasiri. 
Hakuna kitu unachopaswa kukihofia, hata kama utakuwa huwezi kuongea vizuri au hata kama una kigugumizi. Hebu fikiria juu ya watakatifu wa zamani katika kipindi cha Kanisa la Mwanzo. Watakatifu wa wakati huo hawakusalimu amri kwa nguvu za Shetani kwa sababu hawakuuawa kila mtu peke yake bali waliuawa kwa pamoja, pia ni kwa sababu walikuwa wamejazwa na Roho Mtakatifu. Pia kumbuka kwamba Yesu alikwisha kutueleza kwamba, “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.” (Mathayo 10:19-20). Tukiwa kama watu wa Mungu, hatuwezi kujitolea kufa ili kuupokea Ufalme wa Mungu? Kwa kweli tunaweza kujitolea. 
Ulimwengu huu utaharibiwa kikamilifu kwa mapigo ya Mungu ya matarumbeta saba, wakati ambapo mtawala katili aitwaye Mpinga Kristo atakapotawala kwa muda. Tunawezaje basi kubadilisha Mbingu ya milele kwa kitu chochote hapa ulimwenguni, hata kama kitu hiyo ni kizuri sana? Wakati ulimwengu utakapokuwa umebadilika na kuwa mahali pasipofaa kuishi, yaani ambapo mito itakuwa imegeuka na kuwa pakanga, bahari imegeuka na kuwa damu, huku hali ya mazingira ikiwa imeharibiwa na kuwa kama takataka, basi ni hakika kwamba hatutaweza kamwe kusalimu amri kwa mwanadamu aliye kama mnyama ambaye atataka tuikane imani yetu. 
Kuanzia siku ile tutakapouawa na kuwa wafia-dini, basi ulimwengu utakaowangojea wale wanaobakia hapa duniani utakuwa ni ule uliogubikwa na mapigo yasiyoelezeka huku mimea ikiacha kutoa mazao, kwa kuwa yatakuwa yamepigwa kwa mvua ya mawe. Ukweli ni kuwa hata ukiachilia mbali suala la kiimani, hakuna hata mtu mmoja atakayetamani kuishi katika ulimwengu huu tena. 
Kitabu cha Ufunuo kinatuonyesha juu ya mambo yatakayokuja baadaye. Wakati kipindi hiki cha farasi mweusi kitakaposogea mbele kidogo, basi kipindi cha farasi wa kijivujivu kitawadia. Kwa maneno mengine, Bwana wetu atakuja mapema. Ninachokisema hapa ni kwamba hupaswi kuacha mali zako zote ati kwa sababu ujio wa Bwana upo karibu. Bali ninachokisema hapa ni kwamba tunapaswa kuendelea kumtumikia Bwana wetu hadi siku Mpinga Kristo atakapoonekana, hali tukiwa waaminifu na tusiobadilika kama hivi sasa. 
Ikiwa, kwa namna yoyote ile unasumbuliwa au una mashaka hivi sasa, basi usihofie tena. Wakati wewe na mimi tunatambua kwamba tutakuwa wafia-dini, basi ni hakika kwamba mioyo yetu itakuwa na amani na utulivu. Kwa maneno mengine, kuwa tutakuwa wafia-dini, basi ni choyo au tamaa ipi itakayokuwa imebakia ndani yetu? Ikiwa kuna tamanio lolote lililobakia ndani yetu, basi tamanio hilo litakuwa ni kuihubiri injili kwa kila mtu katika ulimwengu mzima, ili kwamba watakatifu wengi waweze kuinuka katika nyakati za mwisho, ili waweze kuokolewa na kuifia-dini kwa kuamini katika injili hii, na hatimaye waweze kuipokea Mbingu na Nchi Mpya. Pia ninatumaini kwamba watakatifu wote wataufanya Ufalme wa Kristo kuwa mali yao kwa imani yao, watafanya hivyo baada ya kuwa wamejengwa kwa ukweli huu, na hatimaye kuwa tayari kuyapitia mambo haya yote yanayowangojea katika wakati wa Mpinga Kristo. 
Mungu ametupatia baraka yake ya kuwa wafia-dini. Si kila mtu anaweza kuwa mfia-dini, na wala si kila mtu anaweza kuishi kwa ajili ya Bwana. Ninamshukuru sana Mungu kwa kutupatia baraka kama hiyo, nina furaha sana kutokana na ukweli kwamba nitakufa kwa ajili ya imani. Kwa kuwa hatuna tumaini lolote kwa ulimwengu huu, basi kitendo cha kuyapokea mauaji yetu na kuwa wafia-dini litakuwa ni jambo la furaha sana kwetu. 
Tunachopaswa kukifanya ni kuwa na tumaini katika Ufalme wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni ambao Mungu ameuandaa kwa ajili yetu, kisha tuishi maisha yetu kwa kuziunganisha juhudi zetu katika kuihubiri injili ulimwenguni kote hadi siku ile Bwana atakaporudi, na kisha tukampokea Bwana kwa furaha wakati atakaporudi, na kisha kufurahia mahali ambapo tuliweka tumaini letu. Uliamini Neno hili kwa kuwa haya ni mambo ambayo kwa hakika yatatokea. 
Hatuwezi kupokea alama ya Mpinga Kristo, kwa kuwa sisi ni watu wa Ufalme wa Mbinguni. Kwa kuwa suala la kuipokea alama litakuwa ni juu ya hiari ya mtu binafsi, basi jambo hili halitafanywa kwa nguvu za kulazimisha, bali kwa hiari ya moyo. 
Hata kwa watoto wetu, ikiwa injili hii inapatikana katika mioyo yao, basi wao nao watayapokea mauaji ya kuwa wafia-dini tena kwa ujasiri mkubwa kuliko hata watu wazima, hii ni kwa sababu hata hao watoto watakuwa na Roho Mtakatifu akikaa ndani yake. Kama watu wazima wanavyozidi kukiri kwamba Yesu ni Mwokozi wao, basi ikiwa Roho Mtakatifu anapatikana katika mioyo ya watoto, basi na wao pia, watakiri kwamba Yesu ni Mwokozi na Mungu. Biblia inatueleza kutofikiria kile ambacho tutakisema pale tutakapoburutwa na kupelekwa mbele ya Mpinga Kristo, kwa kuwa Roho Mtakatifu ataijaza mioyo yetu kwa maneno ambayo tutayaongea. 
Watoto wa Mungu pia wanaweza kuogopa kwa kuwa bado ni wachanga kiroho na wadhaifu, lakini Roho Mtakatifu aliye ndani yao haogopi. Watauawa kama wafia-dini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayekaa ndani yao. Kwa kuwa na wao pia ni mali ya Mungu, Mungu atazipokea roho zao, ataruhusu miili yao kuuawa, kisha atawapa thawabu ya kutawala katika ulimwengu bora zaidi. 
Mungu atakuwa ameishaijaza mioyo ya wale waliozaliwa tena upya kwa maji na Roho kwa Maneno yake ili wayaongee. Kwa kuwa ni roho zilizochaguliwa na kupokelewa na Mungu ndizo zinazoweza kuuawa kama wafia-dini, basi Mungu ataiandaa imani yao kwa ajili ya jina lake. Kutokana na ukweli kwamba Roho Mtakatifu anakaa katika mioyo yetu kwa sababu tumeamini katika injili ya maji na Roho, basi sisi sote tutapokea thawabu ya Ufalme wa Milenia na utukufu wa Mbingu na Nchi Mpya. 
Katika nyakati za mwisho, sisi sote tutapitia uzoefu wa ujazo wa Roho Mtakatifu katika mioyo yetu. Kwa kuwa tumejaliwa kuwa wafia-dini, basi wakati tutakapouawa na kuwa wafia-dii kwa mujibu wa mpango wa Mungu, ni hakika kwamba sisi sote tutayapitia mauaji ya kuwa wafia-dini hali tukisifu, tukimwabudu, na kumtukuza Yeye katika uwepo wake. Kwa kuwa tunamwamini Mungu, basi tunamfuata Yeye kwa imani yetu tu ambayo inasema “Amen!” Kwa kuwa tunafahamu kwamba tutauawa na kuwa wafia-dini, basi matamanio yetu ya mwili yatatowekea mbali, na hivyo kuzifanya roho zetu kuwa safi sana. 
Kuuawa na kuwa wafia-dini, ambayo ni mapenzi ya Mungu kwetu sisi, ni kupokea baraka kubwa na kisha kutukuzwa zaidi. Kwa kuwa watakatifu wana tumaini la kuishi milele katika Mbingu na Nchi Mpya, basi watapambana dhidi ya Mpinga Kristo na kisha kuilinda injili ya maji na Roho katika mioyo yao hadi mwisho. Wakati wa Dhiki Kuu, watakatifu wote, hali wakimtambua Yesu Kristo kuwa ni Mungu wao na huku wakiamini katika wokovu mkamilifu ambao amewapatia, basi watayapokea mauaji ya kuwa wafia-dini mbele za Mungu. 
Ninamshukuru Bwana ambaye ametupatia baraka hii ya kuwa wafia-dini.