Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[14-2] Watakatifu Wafanye Nini Mara Mpinga Kristo Atakapoonekana? (Ufunuo 14:1-20)

(Ufunuo 14:1-20)
 
Ili kumshinda Mpinga Kristo mara atakapoonekana muda si mrefu toka sasa, basi imewapaswa watakatifu kujiandaa kuuawana kuifia-dini kwa imani yao katika Bwana. Ili kuweza kufanya hivyo, ni lazima wafahamu vizuri kuhusu mipango miovu ambayo Mpinga Kristo ataileta hapa duniani. Ni baada ya kuifahami mipango hiyo ndipo watakatifu watakapoweza kusimama kinyume naye na kumshinda kwa imani. Shetani atajaribu kuziangamiza imani za Wakristo kwa kuwafanya watu waipokee alama ya jina lake au namba yake. 
Sababu inayomfanya ajaribu kuiharibu imani ya Wakristo ni kwamba anasimama kinyume na Mungu na kwa hiyo analenga kuishusha imani ya wenye haki, na lengo lake kuu ni kuwazuia watu wasiweze kupokea ondoleo la dhambi zao kwa kupitia injili ya maji na Roho. Mpinga Kristo atawageuza watu na kuwafanya watumishi wake na kuwafanya wasimame kinyume na Mungu. Hivyo, Mpinga Kristo na watumishi wake watakaokuwa wamebaki katika ulimwengu huu watapokea adhabu kubwa na mapigo. 
Wenye haki ni lazima waishi maisha yao ya kiimani hali wakiwa na uelewa sahihi wa mapigo ya mabakuli saba ambayo Mungu atayamimina kwa maadui zake. Kama vile Mungu anavyosema katika Kumbukumbu la Torati 32:35, “Kisasi ni changu mimi, na kulipa,” Mungu atalipa kisasi kwa ajili ya vifo vya watoto wake. Kwa hiyo, ni lazima tuilinde imani yetu na kisha kuishi maisha ya ushindi, badala ya kuzidiwa na hasira na kisha kufanya matendo ya hasira. Watakatifu ni lazima wapambane dhidi ya Mpinga Kristo hali wakiuamini ukweli kwamba Mungu atawaangamiza wale wote watakaosalia katika dunia hii baada ya wao kuuawa na kuifia-dini. 
 

Neno la Kweli Ambalo Halipaswi Kamwe Kusahauliwa
 
Kile ambacho wale wote waliopokea ondoleo la dhambi wanapaswa kukikumbuka ni ukweli kwamba watakatifu wasio na dhambi ndio watakaofufuliwa na kunyakuliwa mara baada ya kuuawa na Mpinga Kristo na hivyo kuifia-dini. Siku ya kuonekana kwa Mpinga Kristo na mauaji ya watakatifu ya kuifia-dini vitakapowadia, basi tutapaswa kukumbuka wkamba ahadi zote za Mungu zitatimizwa. 
Kuanzia aya ya 14 na kuendelea, Neno la Mungu katika sura ya 14 linatufundisha kwamba ni hakika kuwa unyakuo utawajia watakatifu, na kwamba wakati wa kunyakuliwa utakuwa mara baada ya kuuawa na kuifia-dini. 
Tusisahau kwamba ufufuo na unyakuo wetu utakuja baada ya Shetani kuwafanya watu kuipokea alama yake. Ifahamike kwamba baraka ya ufufuo na kunyakuliwa inawangojea wenye haki ambao watauawa na kuifia-dini na Mpinga Kristo. Wenye haki watayapokea mauaji matakatifu ya kuifia-dini ili kuilinda imani yao, hii ni kwa sababu watakataa kuipokea alama ya Shetani. Hivyo wenye haki wafia-dini watapokea thawabu yao kulingana na kazi yao hapa duniani, kisha wataongezewa utukufu wa Mungu. 
Mara utakapowana watakatifu wenzako na watumishi wakiuawa na kuifia dini ili kuilinda imani yao usiomboleze na kukasirishwa. Badala yake, watakatifu wote wanapaswa kumshukuru Mungu na kumpatia utukufu kwa kuwaruhusu kuifia-fini ili kuilinda imani yao, maana mara baada ya kuifia-dini wafia-dini watafufuliwa katika miili mitakatifu na kisha kunyakuliwa na Bwana. 
 

Mapigo ya Mabakuli Saba Yaliyoandaliwa Kwa Ajili ya Wale Wanaosimama Kinyume na Mungu ni Yapi? 
 
Aya ya 19 inasema, “Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.” Wale ambao watakuwa wamesimama kinyume na upendo wa Mungu ni hakika kwamba wamepangiwa kupokea mapigo ya Mungu ya kutisha mara baada ya mauaji ya wafia-dini, hii ni kwa sababu walipokuwa hapa duniani, walikataa kuipokea injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana katika mioyo yao, na badala yake wakasimama kinyume na injili hii. Hawa ndio wale waliofanyika kuwa maadui wa Mungu kwa kutoamini katika wokovu wa Yesu Kristo, aliyekuja kwa damu na maji ili kuwaokoa toka katika dhambi. Ni lazima wapokee sio tu mapigo ya mabakuli saba yatakayomiminwa na Mungu, bali pia wanapaswa kupokea adhabu ya kutisha ya kuzimu milele. 
Haya ni mapigo saba ambayo Mungu atayaleta kwa wale ambao hawajanyakuliwa na Bwana. Baada ya mauaji ya watakatifu, Mungu, tena bila huruma atayashusha mapigo ya mabakuli saba ambayo atakuwa ameyaandaa kwa wale ambao, kwa kutoshiriki katika unyakuo, watakuwa wamebakia hapa duniani kama watumwa wa Shetani huku wakiendelea kuukufuru utukufu wa Mungu. 
Ni kwa nini Mungu atawafanya wenye haki kuuawa na kuifia-dini? Ni kwa sababu kama wenye haki wangelibakia katika dunia hii pamoja na wale ambao hawajazaliwa tena upya, Mungu angelishindwa kuyashusha mapigo yake ya mabakuli saba wakati utakapokuwa umewadia. Na kwa kuwa Mungu anawapenda wenye haki, anawaruhusu kuifia-dini ili kwamba kuungana naye katika utukufu wake. Hii ndio sababu Mungu atawafanya wenye haki kuifia-dini kabla ya kuyatelemsha mapigo ya mabakuli saba. Na baada ya kuwafufua na kuwanyakua wenye haki walioifia-dini, hapo ndipo Mungu atakapoyamimina mapigo haya duniani kwa uhuru. Mapigo haya ya mabakuli saba ni mapigo ya mwisho ambayo Mungu atayaleta kwa mwanadamu katika dunia hii. 
 

Ufalme wa Milenia na Mamlaka ya Watakatifu
 
Kipindi cha Ufalme wa Milenia kitaanza wakati Bwana, pamoja na watakatifu wake, watakaposhuka hapa duniani tena. Mathayo 5:5 inatueleza kwamba, “Heri wenye upole, maana watairithi nchi.” Wakati Bwana atakaporudi katika dunia hii pamoja na watakatifu, Neno la Zaburi 37:29, kwamba “wenye haki watairithi nchi,” litakuwa limetimizwa. 
Hivyo, wakati Bwana atakaposhuka hapa duniani pamoja na watakatifu wote, Bwana atawapatia mamlaka ya kuifanya dunia hii kuwa mali yao. Wakati huu, Bwana atawapatia mamlaka ya kutawala juu ya miji kumi, na wengine miji mitano zaidi. Bwana ataufanya ulimwengu huu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani yake kuwa vipya, kisha atawafanya watakatifu kutawala pamoja naye kwa miaka elfu moja na baadaye. 
Sasa, ni tumaini gani ambalo watakatifu wa kipindi hiki wanapaswa kuishi nalo? Wanapaswa kuishi hali wakitumainia siku ambayo Ufalme wa Kristo utakuwa umejengwa hapa duniani. Wakati Ufalme wa Bwana utakapokuja hapa duniani, amani, furaha, na baraka zinazotoka katika utawala wake zitakuwa juu ya dunia hii. Ukweli ni kwamba kuishi chini ya utawala wa Bwana, kutatufanya tusipungukiwe na kitu chochote, na hivyo tutaishi katika neema yake na ukamilifu. 
Wakati Ufalme wa Bwana utakapowadia katika dunia hii, matumaini yote na ndoto za wenye haki zitatimizwa. Baada ya kuishi katika dunia hii kwa miaka elfu moja, basi hapo ndipo wenye haki watakapoingia katika Ufalme wa Mbinguni wa milele, lakini wale waliosimama kinyume na Mungu watatupwa katika ziwa la moto la milele na kiberiti, watateseka milele na hawatapunzima mchana na usiku. 
Hivyo, wenye haki ni lazima waishi kwa matumaini, hali wakiisubiria siku ya Bwana. Wenye haki wote wanapaswa kukumbuka kwamba mauaji ya kuifia-dini, ufufuo, unyakuo, na uzima wa milele ni vyao. Naomba ulishike hili Neno la kweli na tumaini ulilolisikia kwa uthabiti wote. 
Wenye haki wataendelea kuishi hali wakiihubiri injili ya maji na Roho na kisha kuliweka tumaini lao katika Ufalme wa Mbinguni hadi siku ambayo Bwana atarejea. Wenye haki wana mamlaka ya kuishi milele katika Ufalme wa Mungu, na wana mamlaka ya kuihubiri injili ya maji na Roho katika dunia hii. 
 
 
Watakatifu Wanaoishi katika Kipindi Hiki Cha Giza Wanapaswa Kufanya Nini?
 
Ni dhahiri kwamba kipindi hiki ni kipindi cha giza, na ni kipindi ambacho inaendelea kuwa vigumu sana kuishi ndani yake. Hivyo, ni lazima tuihubiri injili ya maji na Roho kwa kwenye dhambi na kisha kuwalea. Wenye haki ni lazima waueneze upendo wa Mungu na ondoleo la dhambi zao linalopatikana kupitia injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu Kristo katika ulimwengu mzima. Hili ni jambo ambalo watakatifu wanapaswa kulifanya. 
Ikiwa watakatifu wataipoteza fursa hii, basi ni hakika kwamba fursa hii hawataipata tena. Kwa kuwa mwisho wa ulimwengu huu hauko mbali sana, basi tunapaswa kuihubiri injili ya maji na Roho zaidi, na kisha kuzilea nafsi zilizopotea kwa kuzipatia tumaini la Ufalme wa Mungu. Hili ni jambo jema ambalo wenye haki wanapaswa kulifanya. 
Katika ulimwengu huu wa sasa, kuna watu wengi ambao, pamoja na kuwa hawana Neno la injili ya maji na Roho, wanaendelea kudai kumwamini Yesu na kuishi maisha yao huku wakimtumikia Bwana. Lakini, wale wanaoishi maisha ya kidini pasipo ukweli halisi ni manabii wa uongo. Waongo hawa ni wadanganyifu ambao kazi yao ni kunyonya mali na vitu vya waamini kwa kutumia jina la Yesu. 
Hivyo, tunawaonea huruma wale wote wanaojaribu kuishi maisha yao ya kiimani huku wakidanganywa na hawa manabii wa uongo. Hali wakiishi pasipo kuwa na injili ya maji na Roho, na huku wakidai kumwamini Bwana, Wakristo hawa wa mazoea wanaendelea kubaki kuwa wenye dhambi na wanaendelea kuishi chini ya laana ya Torati ya Mungu. Wanaendelea kuishi katika dhambi wakati wote, hali wakiwa hawafahamu ukweli kwamba kama wangeliifahamu injli ya maji na Roho, basi dhambi zao zote zingelipotea na zingelifanywa kuwa nyeupe kama theluji, na kwa sababu hiyo wangelipewa Roho Mtakatifu kama karama. 
Lakini kinyume chake, watumishi wa Mungu wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanaendelea kuishi kwa amani. Watumishi wa Mungu na watu wake wanaifurahia injili ya maji na Roho. Wanashuhudia hivi: “Bwana Yesu amezifanya dhambi zote za ulimwengu kutoweka kwa kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake mara moja kwa ubatizo wake toka kwa Yohana, na kwa kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo Msalabani. Ninapouamini wokovu huu wa upatanisho, dhambi zangu zote ambazo zilikuwa zikinielemea zinatoweka. Sasa nimefanyika kuwa mwenye haki.” 
Watakatifu katika Kanisa la Mungu wanampatia Mungu utukufu kwa ushuhuda kama huo. Wale alio na imani hii wanaweza kuwa na tumaini Mbinguni. 
 

Ufufuo wa Kwanza ni Tukio Lililohifadhiwa Kwa Ajili ya Watakatifu
 
Hivi punde, Bwana atarejea hapa duniani. Muda mfupi tangu sasa, mtu mmoja ambaye atakuwa ni Mpinga Kristo ataonekana na kisha kuiweka chapa yake katika mikono ya kulia na katika vipaji vya nyuso vya watu wengi. Wakati huu utakapowadia, utapaswa kutambua kwamba ujio wa mara ya pili wa Bwana, pamoja na mauji ya wafia-dini, ufufuo, na unyakuo vitakuwa vimekaribia. Siku kama hiyo na saa kama hiyo itakapowadia, basi unapaswa kutambua kuwa itakuwa ni siku ya furaha kwa watakatifu, lakini kwa wenye dhambi ambao hawajazaliwa tena upya, itakuwa ni siku ya hukumu ya dhambi zao. 
Watakatifu wote watafufuliwa mara baada ya kuifia-dini, kisha watajiunga katika chakula cha harusi ya Mwana-kondoo pamoja na Bwana. Wakati wewe na mimi tutakapouawa na kuifia-dini wakati huo, muda si mrefu miili yetu itafufuliwa na kunyakuliwa. Haijalishi kitakachokuwa kimetokea kwa miili ya watakatifu waliotangulia kabla yetu—yaani hata kama miili yao imebadilika na kuwa vumbi au la, au hata kama miili yao haina umbo lolote, hakutakuwa na shida juu ya wao kufufuliwa. Wakati huu utakapowadia, watakatifu watafufuliwa sio katika miili dhaifu ya sasa, bali katika miili mikamilifu. Wenye haki watafufuliwa katika miili mitakatifu, na wataishi na Bwana milele. 
Hata wakati ambao nyakati ngumu zinatusubiri, yaani wakati ambapo Mpinga Kristo ataonekana na kututesa, basi sisi tunapaswa kuilinda imani yetu katika Yesu Kristo kwa kuamini katika Neno la Mungu ambalo tumelisikia hivi sasa. Pia tusisahau kwamba kwa kuwa wewe na mimi tumeamini katika injili ya maji na Roho, basi sisi sote tutashiriki katika mauaji ya kuifia-dini ya watakatifu, tutashiriki katika ufufuo na unyakuo. 
Sasa, hupaswi kuanguka na kuiacha imani yako katika ukweli huu, kisha unapaswa kuishi maisha ya kumpinga na kumshinda Mpinga Kristo. Kwa pamoja, yaani pamoja na wale waliookolewa kabla yetu kwa kuamini katika ukweli huu, tunapaswa kulishikilia Neno la Mungu, na kisha kumfuata Bwana kwa imani hadi siku hii itakapowadia. 
 

Hata Sasa, Kuna Waongo Wengi Wanaowadanganya Watu
 
Hata sasa, kuna idadi kubwa ya watu, ambao kama watumishi wa Shetani, wanafundisha imani ya uongo. Kimsingi, kuna waongo wengi sana ambao wanatetea na kuifundisha nadharia ya kunyakuliwa kabla ya mateso kwa waumini wao, hali wakijaribu kuwashawishi kwamba hawana jambo la kuhofia wala kufanya kuhusiana na Dhiki Kuu ya miaka saba. 
Kinyume chake, Biblia inaeleza wazi kwamba mauaji ya watakatifu ya kuifia-dini na kunyakuliwa vitatokea baada ya kupita miaka mitatu na nusu ya ile Dhiki. Hivyo, tusidanganywe na hao waongo. Badala yake hebu tufahamu na kuamini kwamba baada ya kipindi cha miaka mitatu na nusu kupita katika ile miaka saba ya Dhiki Kuu, basi sisi sote tutauawa na kuifia-dini, na muda mfupi baadaye tutafufuliwa na kunyakuliwa kwa pamoja. 
Hivyo, ni lazima mkae mbali na manabii wa uongo wanaofundisha kwamba hawatakuwa na cha kufanya kuhusiana na miaka saba ya Dhiki Kuu. Watakatifu wa kweli wanaamini kwamba mauaji yao ya kuifia-dini, ufufuo, na unyakuo, na karamu ya harusi ya Mwana-kondoo vyote vitatokea mara baada ya kupita ile miaka mitatu katika ile miaka ya Dhiki. 
 

Sasa, Sisi Sote Tuishi Vipi? 
 
Kwa sasa, unapaswa kutambua kwamba ikiwa mtu anamwamini Bwana kuwa ni Mwokozi wake—yaani Bwana aliyekuja katika ulimwengu huu, akazibeba dhambi za ulimwengu huu kwa ubatizo wake toka kwa Yohana, akaimwaga damu yake Msalabani, na akafufuka tena toka kwa wafu—basi Roho Mtakatifu atakuja katika moyo wa mwamini huyu kama karama yake. 
Unapswa kusikiliza kwa masiko yako na kisha kuamini kwa moyo wako kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kwa kupitia Kanisa la Mungu, na kisha udumu katika imani yako kwa Mungu. Watakatifu wote ni lazima waishi maisha yao yakiongozwa na Kanisa la Mungu. Hakuna mtu anayeweza kuihubiri, kuishika, au kuitumikia injili ya maji na Roho hali akiwa peke yake. Hii ndio maana Kanisa la Mungu n la muhimu sana hata kwa watakatifu ambao wamekwisha zaliwa tena upya. 
Hivyo, Mungu amelianzisha Kanisa Lake, na watumishi wake hapa duniani, na kwa kupitia hapo anawalisha wanakondoo wake. Kimsingi, kazi za Mungu zinakuwa ni za thamani sana na zenye umuhimu kadri nyakati za mwisho zinavyozidi kutukaribia, na kwa sababu hiyo, ninaomba na kuamini kwamba utaishi maisha ya uaminifu yaliyojazwa na Roho Mtakatifu. Kadri nyakati za mwisho zinavyozidi kukabiria, wenye haki ni lazima wafanye kazi kwa juhudi zaidi katika kuungana, kuomba, kutiana moyo, kuishikilia imani, na katika kusaidiana, na katika kuishi kwa ajili ya Bwana, hali wakiwa wameungana katika moyo mmoja na kwa nia moja. 
Mungu ameruhusu mauaji ya kufia-dini, ufufuo, unyakuo, na uzima wa milele kwa watakatifu. Hebu sisi sote tuishi maisha ambayo yanasimama kinyume na Mpinga Kristo, na kisha tusimame kwa uthabiti mbele za Mungu. Halleluya! 