Search

Mahubiri

Somo la 10: Ufunuo (Ufafanuzi juu ya Ufunuo)

[19-2] Ni Wenye Haki Tu Ndio Wanaoweza Kusubiria Kurudi Kwa Kristo Katika Tumaini (Ufunuo 19:1-21)

(Ufunuo 19:1-21)
 
Katika sura iliyopita, tuliona jinsi ambavyo Mungu atakavyoyaleta mapigo yake ya kutisha katika ulimwengu huu. Katika sura hii, sasa tunamwona Kristo na jeshi lake lenye utukufu likipigana na kulishinda jeshi la Mpinga Kristo, na kisha kumtupa Mnyama na watumishi wake katika ziwa la moto hali wakiwa hai, huku wakiua jeshi la Mpinga Kristo lililosalia kwa upanga wa Neno utokao katika kinywa cha Bwana, na hivyo kuhitimisha vita vyake dhidi ya shetani. 
Yaliyomo katika sura hii yanaweza kugawanywa katika mada kuu tatu: 1) watakatifu walionyakuwali wanamsifu Mungu kwa kuileta hukumu ya mapigo makuu katika ulimwengu huu; 2) kutangazwa kwa ujio wa karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo; na 3) kushuka kwa Bwana toka Mbinguni pamoja na jeshi la Yesu Kristo. 
Sisi sote ni lazima tutambue kwa hakika kwamba Mungu atatimiza kila kitu kama alivyosema kwetu kupitia Kitabu cha Ufunuo. 
 
 
Hukumu ya Mungu!
 
Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho na ambao wamefanyika kuwa watu wa Mungu kwa kupitia imani watakuwa wakimsifu Mungu kwa kuwaokoa toka katika dhambi zote za ulimwengu. Hebu tuangalie aya ya 3-5: “Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu!”
Waebrania 9:27 inatueleza kwamba, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.” Mwanadamu atahukumiwa mbele za Mungu mara moja, lakini maamuzi ya hukumu hii ni ya mwisho na wala hayatarudiwa. Kwa maneno mengine, Mungu ataitoa hukumu yake ya mwisho kwa kuwatupa wenye dhambi katika moto uwakao milele kwa kupitia hukumu yake hii ya mara moja kwa kila mtu. Hii ndio sababu Biblia inatueleza kwamba “moshi wake hupaa juu hata milele na milele.”
Baadhi ya watu wanaweza kufikiri na kusema, “Ukisha kufa, basi hapo ndio mwisho wa kila ktu.” Lakini haya ni mawazo binafsi ya mtu, na si mawazo ya Mungu. Kwa kuwa kila mtu ana mwili pamoja na nafsi, basi kila mtu anafahamu katika hali ya asili kwamba Mungu yupo, na kwamba muda si mrefu kila mtu atahukumiwa kwa dhambi zake mbele za Mungu, hii ni kwa watu wote bila kujalisha kwamba wanamwamini Mungu au la. 
Kwa kuwa kuna uwepo wa roho za watu, basi ndio maana wanafahamu kwamba, pamoja na kuwa Mungu haonekani kwa macho yao, ukweli ni kuwa Mungu yupo. Uwepo unaoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu hauwezi kudumu milele, na kwamba upo uwepo wa kweli na wa milele ambao hauonekani kwa macho yetu. Utajiri wa mali katika dunia hii ukiambatana na fikra juu ya fedha na utafutaji wa mali haviwezi kuwa ndio sababu ya mwanadamu kuwepo duniani; ukweli ni kwamba sababu ya msingi ya mwanadamu kuwepo hapa duniani ni kuingia katika uwepo wa milele wa baraka kwa kumfahamu Mungu, ambaye ni Muumbaji wa ulimwengu mzima, na kwa kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana. 
Sio kwamba tunapaswa kufahamu kile ambacho Mungu ametueleza, bali tunapaswa kuamini kile ambacho Mungu ametueleza. Hatupaswi kuishia kuzimu kwa kuamini kwa mujibu wa mawazo yetu binafsi tu. Kabla ya kukabiliana na mateso ya milele kwa ajili ya dhambi zetu, basi tunapaswa kusamehewa dhambi zetu zote na kupokea uzima wa milele kwa kuiamini injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu wakati tukiwa hapa duniani. 
Maisha hapa duniani ni mafupi sana kwa kila mtu. Ni kama vile jua linapochwea na kuwia kila siku, safari fupo ya maisha yetu inafikia ukomo kwa haraka, ikiwa haina matunda na isiyo na maana, kana kwamba tumekuwa tukikimbia kama nguchiro juu ya uwanda mfupi. Hata kama utaishi kwa miaka mia moja, bado huwezi kusema kwamba umeishi muda mrefu sana. 
Ikiwa utatoa shughuli mbalimbali zinazojitokeza katika maisha yako ya kila siku, kama vile muda unaoutumia ukiwa umelala, ukila, ukienda bafuni, na kufanya vitu vya kidunia visivyo sisimua, yaani katika muda wote wa maisha yako, basi utajikuta kwamba umebakiwa na muda mfupi sana. Unapoviona vitu ambavyo umewahi kuviona tangu ulipozaliwa, na unapokutana na watu ambao umewahi kukutana nao hapo zamani, na mara unapoziona nywele zako zikibadilika na kuwa na mvi, basi unajikuta ukikabiliana na mwisho wako. 
Sababu inayofanya maisha yetu sisi watakatifu kutokuwa na maana ni kwa sababu, baada ya kuzaliwa katika ulimwengu huu, tumekutana na Bwana ambaye amekuja kwetu kwa kupitia maji na Roho, na hivyo tukamwamini, na hivyo kupokea ondoleo la dhambi zetu zote. Kwa kweli sisi ni watu wenye baraka na wenye shukrani! Kama isingelikuwa ni Bwana aliyekuja kwetu kupitia maji na Roho, basi ni hakika kwamba tungelikuwa tumefungwa kuingia katika moto wa milele na kuteseka ndani yake. 
Ninapofikiria hili, kwa kweli naona bado linanitisha, na kwa sababu hiyo najikuta nikampatia Bwana shukrani zaidi na zaidi. Kwa kweli kuzimu, ambayo imetokea kwa sababu ya Shetani, ni mahali panapotisha sana na ambapo mateso yake ni makuu mnno kiasi kwamba mtu atatamani kufa, lakini kwa bahati mbaya hataweza kufa. Ni mahali ambapo moto na kibiriti vinawaka milele. 
Ili kuweza kuifahamu kiusahihi injili ya maji na Roho iliyotolewa na Yesu, na ili kuweza kupokea Roho Mtakatifu, basi inampasa mtu kukutana kwanza na watumishi wa Mungu ambao wameshakutana na injili hii ya maji na Roho na ambao wameshazaliwa tena upya. Yeyote anayetaka kulipata jibu la swali la kuzaliwa tena upya kwa maji na Roho na kupokea Roho Mtakatifu anaweza kupata majibu yake kwa kuamini katika injili ya maji na Roho na kisha kuishi kama Mkristo. 
Biblia inatueleza kwamba Roho wa Mungu anatolewa kama karama kwa wale wote wanapokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho (Matendo 2:38). Wale tu walio na Roho Mtakatifu katika mioyo yao kutokana na kusamehewa dhambi zao zote kwa kupitia imani yao katika injili ya maji na Roho wanaweza kueleweka kwamba wana imani sahihi katika Yesu, na hao walio na imani hii ndio wanaoweza kuingia katika Ufalme wa Mungu wa milele (Yohana 3:5). Kubarikiwa au kulaaniwa kwa mtu kunatokana na ukweli ikiwa mtu huyo amepokea ondoleo la dhambi ka kuamini katika injili ya maji na Roho au la. 
 

Wamevikwa Kitani Safi, Angavu na Inayong’aa 
 
Wale wanaofikiria kuhusu hatma yao ya baadaye na wanaotaka kutatua tatizo la ondoleo la dhambi zao hao ndio wenye hekima na waliobarikiwa. Pamoja na kuwa mtu anaweza kuwa ameishi maisha yenye mapungufu mengi, ikiwa mtu huyo ameamini katika injili ya maji na Roho na amepokea ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu katika moyo wake, basi mtu huyo atakuwa ndiye aliyeishi maisha yenye mafanikio. 
Ufunuo 19:4-5 says, “Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu!” 
Hapa, hii sentesi inayosema “mnaomcha Mungu” maana yake ni kulipokea Neno la Yesu Kristo katika moyo wa mtu na kisha kuishi kwa mujibu wa uongozi wa Mungu. Ni wale tu waliosamehewa dhambi zao ndio wanaoweza kuona na kumsifu Mungu katika Ufalme wa Mbinguni. Lakini wale ambao hawajapokea ondoleo la dhambi zao watateseka katika moto uwakao wa kuzimu na kisha kulaaniwa na Mungu. 
Hebu tuendelee na aya ya 6-9: “Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing`arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.”
Hapa vifungu hivi vinaeleza kwamba Mtume Yohana aliisikia sauti ya kusifu, sauti kama ya makutano ya watu wengi, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Sauti hii si nyingine bali ni sauti ya wale waliopokea ondoleo la dhambi wakiwa wamekusanyika pamoja wakimsifu Mungu. Huu wimbo wa kusifu ulioundwa kwanza kwa sifa za kumsifu Mungu kwa kuwaruhusu kuwa chini ya utawala wa Mungu Mwenyezi, na kisha kutawaliwa na Mungu, na kisha kuishi na Mungu katika utukufu. Mambo haya yote yamewafanya watakatifu kuwa na furaha kuu na kisha kumpatia Mungu utukufu mkuu. Na ndio maana hawawezi kufanya lolote zaidi ya kumsifu Mungu huku wakipiga kelele, “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake”
Pili, watakatifu wanaendelea na sifa zao: “kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing`arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.” Hii ina maanisha nini? Ina maanisha kwamba kama Mungu alivyowaahidi wanadamu, Yesu atarudi hapa duniani, atafunga ndoa na wale waliopokea Roho Mtakatifu kwa kumwamini Yeye na kwa kuzaliwa tena upya, na kisha kuishi pamoja nao milele. 
Ndoa ni muungano wa bwana harusi na bibi harusi. Kwa maneno mengine, wakati Yesu atakaporudi hapa duniani, atawapokea na kisha kuishi nao wale tu waliozaliwa tena upya kwa maji na Roho. Pia ina maanisha kwamba Yesu ataujenga Ufalme wake wa Milenia na Mbingu na Nchi Mpya ili aweze kuishi pamoja na watakatifu milele na milele. Utukufu wa bibi harusi kuishi pamoja na Bwana harusi ni mkuu mno kiasi kwamba hauwezi kuelezewa vizuri. Mioyo yetu inajawa na furaha kila tunapoufikiria utukufu huo. 
Wakati ulimwengu ambao Yesu atatawala utakapofika, mabibib harusi wake watakuwa na furaha sana ambayo haiwezi kuelezewa na maneno. Ni furaha kiasi gani watakuwa nayo wakati watakapokuwa wakitawaliwa na Mchungaji Mwema? Kwa kuwa Yesu Kristo ni Bibi harusi wa wema mkamilifu, basi hivyo ndivyo na utawala wake utakavyokuwa na wema na ukamilifu. Yesu atatawala katika Ufalme wa Mbinguni. 
 

Injili Ya Pekee Ambayo Itakustahilisha Kwenda Mbinguni 
 
Ili mtu aweze kupokea Roho Mtakatifu na kuingia Mbinguni, basi imempasa mtu huyo kuamini kikamilifu katika ubatizo wa Yesu na damu yake. Kwa kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani ili kuwaokoa wenye dhambi wote toka katika dhambi zao zote kwa kuzichukua dhambi hizo za mwanadamu katika mwili wake, basi ndio maana ilimpasa kubatizwa na Yohana. Hivyo, Yesu Mwenyewe alisulubiwa Msalabani kwa niaba yetu mara baada ya kuwa ameupokea ubatizo wake, alihukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu zote, akafufuka tena toka kwa wafu, na akafanyika Bwana wa wokovu wa milele kwa wale wote wanaoamini. 
Huyu Bwana atarudi hapa duniani, atawapokea watu wake ambao wamefanyika mabibi harusi wake kwa imani, kisha ataishi nao milele. Wale waliofanyika mabibi harusi wake sasa wataishi pamoja na Bwana katika nchi mpya yenye utukufu, kwa baraka yenye utukufu kwa mabibi harusi. Hivyo, watoto wa Mungu waliookolewa watampatia Yesu Kristo utukufu kwa kumsifu milele. Watu hawa ambao watatawaliwa na Mungu watashangilia katika furaha yao. Na kwa furaha hii, watampatia Bwana harusi utukufu wote. 
Wanadamu wote wamekuwa wakilisubiria tukio hili tangu wakati wa uumbaji. Tukio hili linatimizwa wakati Yesu atakaporudi, na kuwainua wale wote waliopokea Roho Mtakatifu, na kisha kuishi nao. Mungu amefanya ulimwengu mpya kwa ajili ya wanadamu na ulimwengu huu mpya unatungojea. Tunaishi kwa ajili ya hili, na tumezaliwa hapa ulimwenguni kwa ajili ya hili. 
Kama kifungu kikuu kinavyotueleza, “Na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing`arayo, safi,” Mungu amewavika wale wanaomwamini Yesu Kristo kwa kitani safi na ing’arayo. Kwa maneno mengine, wale wanaoliamini Neno hili wamepokea ondoleo la dhambi na mioyo yao imegeuka na kuwa myeupe kama theluji. 
Vivyo hivyo, mabibi harusi wa Yesu Krito wamekwishaandaliwa mapema kwa injili ya maji na Roho. Mtu anaweza kuzaliwa tena upya na kuwa bibi harusi wa Kristo kwa kuisikia na kuiamini injili ya maji na Roho wakati akiwa hapa duniani. Imani hii ndio inayoufanya uwe bibi harusi wa Kristo, na imani hii ndiyo inayokustahilisha kuingia Mbinguni. 
 

Wale Wanaosubiria Katika Tumaini
 
Kifungu kikuu kinatueleza kwamba, “Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!” Wale waliopokea ondoleo la dhambi zao wanapaswa kuishi kwa aina ipi ya imani? Mabibi harusi waliokutana na Bwana harusi Yesu na wanaoishi aktika utukufu wanapaswa kuishi maisha yao katika imani na tumaini, hali wakitazamia siku ya kuunganishwa na Bwana harusi. 
Kadri ulimwengu unavyozidi kuwa mweusi zaidi na zaidi, bado kuna tumaini kwa mabibi harusi waliookoka. Tumaini hili si jingine bali ni lile la kusubiria siku ambayo Yesu Kristo, baada ya kuwa ameiandaa Mbingu na Nchi Mpya kwa ajili ya mabibi harusi wake, atarudi ili kuja kuwachukua. Kisha, Bwana harusi atawafufua mabibi harusi wake wote, na kuwapatia uzima wa milele. Ulimwengu ambamo Bwana harusi na mabibi harusi wataishi milele ni mahali ambapo hapana maovu, hapana dhambi, na hawapungukiwi na chochote. Mabibi harusi wanaisubiria siku hii tu. Hii ndio sababu sisi sote tuliopokea ondoleo la dhambi tunaishi kwa imani na tumaini hilo. 
Kimsingi, mabibi harusi wanaoishi katika wakati wa sasa, wana mapungufu mengi katika mwili. Lakini kama 1 Wakorintho 13:13 inavyotueleza, “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo,” kwa kuwa Bwana harusi anawapenda mabibi harusi wake, basi atazisafisha dhambi zao zote kwa ubatizo wake na kisha kuwapokea na kuwakubali kama mabibi harusi wakamilifu. 
Ulimwengu huu unakimbilia kwenda katika hatma yake na hakuna tumaini lililosalia ndani yake. Lakini pamoja na kuwa kila kitu kinaelekea karibu na maangamizi, mabibi harusi wanapaswa kuishi maisha yao kwa tumaini lao maalumu. Wakati wa kutimizwa kwa tumaini hili sasa unatukaribia. Ulimwengu mzima sasa upo katika hatari ya kuanguka na kuvunjika kutokana na matetemeko. Siku imekaribia ambapo kila mtu katika ulimwengu huu atatoweka kama vile dinosauria wa nyakati za kale walivyotoweka. Ulimwengu huu utaanguka hivi punde. 
Hata hivyo, kila bibi harusi ana tumaini, kwa kuwa wakati utakapowadia, miili ya mabibi harusi itabadilishwa na kuwa katika miili mikamilifu, na wataishi pamoja na Bwana, ambaye amefanyika kuwa Bwana harusi milele na milele. Hivyo, mabibi harusi ni lazima waihubiri injili ya maji na Roho kwa uaminifu kwa watu wa ulimwengu wa wakati huu. 
 

Hebu Tuliamini Neno la Kweli la Mungu!
 
Katika Yohana 3:5 Yesu anaeleza kwamba, “Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Sasa, injili ya maji na Roho ni kitu gani? Kwanza kabisa, Biblia inatueleza kwamba “maji” maana yake ni ubatizo wa Yesu na mfano wa wokovu (1 Petro 3:21).
Wakati Yesu alipofikisha umri wa miaka 30, alikwenda kwa Yohana, aliyekuwa akiwabatiza watu wa Israeli katika Mto Yordani. Yesu anatueleza kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ni mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu wa mwisho wa Agano la Kale. Mara baada ya kukutana na Yohana, Yesu aliupokea ubatizo toka kwa Yohana, ubatizo ambao uliitimiza haki yote ya Mungu (Mathayo 3:15, 11:11-14). Hivyo, ubatizo ambao Yesu aliupokea ulikuwa ni sadaka ya milele ambao kwa huo dhambi zote za ulimwengu zilipitishwa kwenda kwa Kristo Mwenyewe. 
Kitendo cha Yesu kufanyika mwili kupitia Roho Mtakatifu, ubatizo wake, damu yake na kifo chake Malabani, na ufufuo wako na kupaa—haya yote ni matendo ya Roho Mtakatifu. Wakati mtu anapoamini kwamba Yesu alikuja hapa duniani, na kwa kupitia maji na Roho alizifanya dhambi zake zote kutoweka mara moja, basi mtu huyo anaweza kufanyika mwenye haki, aliye huru toka katika dhambi, na bibi harusi wa Kristo. Hiki si kitu au mambo yaliyokamilishwa kwa mawazo ya mwanadamu, bali ni mambo yanayotoka katika mawazo ya Mungu Mwenyewe. 
Ukweli ni kwamba maji, damu, na Roho Mtakatifu ni vitu muhimu sana kwa wokovu wa mwanadamu toka katika dhambi, na hakuna kimoja wapo kinachoweza kuondolewa. Katika hili Biblia inaeleza vizuri na kwa wazi katika 1 Yohana sura ya 5. Inatueleza kwamba vitu hivi vitatu yaani maji, damu, na Roho Mtakatifu vyote ni umoja, na kwamba wokovu wetu toka katika dhambi hauwezi kukamilishwa na kuthibitishwa ikiwa kimoja wapo kati ya hivyo vitatu kinakosekana. 
Tunapoufahamu na kuuamini ukweli huu, kwamba wokovu kamili ni kuamini katika hivi vitatu―maji, damu, na Roho Mtakatifu—basi hapo tunaweza kutambua na kuupokea upendo wa Yesu ambao umetuokoa, na kwa sababu hiyo mioyo yetu kwa hakika itakuwa haina dhambi kabisa. Katika Matendo 2:38 Biblia inatuahidi ikisema, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” 
Ni nini basi, je, hili Neno linatuwezesha kupokea Roho Mtakatifu? Hili si jingine bali ni Neno la Yesu la ubatizo (maji), na la kifo chake Msalabani (damu), na la yeye kuwa ni Mungu, ufufuo na kupaa (Roho Mtakatifu). Neno hili la wokovu lilikuwa limetabiriwa katika maandiko ya Musa na manabii wengine wa Agano la Kale, na lilitimizwa na kushuhudiwa katika injili zote nne za Agano Jipya. Pia “wokovu wa milele wa upatanisho umekamilishwa mara moja,” umeandikwa kwa kina katika Kitabu cha Waebrania, na habari hii inashuhudia tena na tena juu ya haki ya Mungu, ambayo tumeipokea kupitia imani yetu. 
Pamoja na kuwa kila mtu katika ulimwengu huu wenye dhambi anaishi maisha ya kimwili ambayo yana mapungufu sana mbele za Mungu, ukweli unabaki kwamba mtu huyo anapaswa kupokea ondoleo la dhambi linalotolewa na Mungu, na kisha kuishi hali akiliweka tumaini lake Mbinguni. Hii ni zawadi ambayo Mungu amewapatia wanadamu. Sisi sote tunapaswa kuipokea neema hii bure. Kuliamini Neno ya kwamba Bwana wetu atarudi, na kwamba ataujenga Ufalme wake mpya, na kwamba ataturuhusu kuishi ndani yake ni tumaini letu la kweli. Tunapaswa kuishi kwa tumaini hili, na hivi ndivyo ninavyoamini kwa nguvu zangu zote. 
Je, unafahamu dhambi imeenea kwa kiasi gani hapa ulimwenguni? Ukilinganisha na wakati wa gharika ya Nuhu, dhambi za kipindi hiki zimeenea zaidi kuliko wakati huo. Wakati wa Nuhu, Mungu, baada ya kuona kwamba mawazo ya mwanadamu yalikuwa ni maovu wakati wote, aliamua kuuangamiza ulimwengu wa kwanza kwa gharika, akamwambia Nuhu kuijenga safina, na akawaokoa wale walioingia katika safina hii kwa kuliamini Neno lake. 
Pamoja na kuwa Mungu alisema kwa hakika kwamba atauhukumu ulimwengu kwa maji, ni watu nane tu wa familia ya Nuhu ndio walioliamini Neno lake. Hivyo waliitengeneza safina kwa muda wa zaidi ya miaka mia moja, kisha wakaingia ili kuikwepa gharika. Baada ya kufanya hivyo, Mungu alianza kuileta hukumu yake kwa ulimwengu wa kwanza. Ghafla anga liligeuka na kuwa jeusi, kisha mvua yenye tufani ikaanza kunyesha. Pengine baada ya saa moja maji yalikuwa yameshafikia karibu ghorofa ya tatu. Hivyo mvua ikanyesha kwa siku 40, ikauzamisha ulimwengu wote chini ya maji. 
Kama ambavyo Nuhu na familia yake walivyoingia katika safina huku wakiamini kwamba ulimwengu mpya unakaribia kufunguliwa, wewe na mimi tunapaswa kuishi katika kipindi hiki kwa tumaini. Kama walivyoweza kuijenga safina kwa miaka mia moja kwa kuwa walimwamini Mungu, basi mimi ninaamini kwamba, sisi nasi, tunapaswa kuvumilia na kuihubiri injili. Mungu alimwambia Nuhu, “Ujifanyie safina (Mwanzo 6:14).” Neno hili linatueleza kwamba “ ili sisi tuweze kuilinda imani yetu,” basi tunapaswa kwanza kujitoa sisi wenyewe kwa Bwana na katika kuihubiri injili. 
Pamoja na kuwa waliozaliwa tena upya wana tumaini, hakuna tumaini kwa wale wasioamini katika injili hii. Kwa kweli kwa hawa wasioiamini injili hii wana mahangaiko matupu. Bila kujali kwamba watu wanaiamini injili ya maji na Roho au la, tunapswa kuendelea kuihubiri injili hii kwao kwa imani. Wakati uliopo ni wakati ambapo watu ni lazima waamini katika injili hii ya kweli mapema kadri iwezekanavyo. Wale wanaoamini katika injili hii tunayoihubiri watapata furaha, lakini wale wasioiamini injili hiyo watalaaniwa. Hawa wa mwisho—yaani, wale wasioamini katika injili—ni wajinga ambao watapokea hukumu ya Mungu ya milele na kisha kutupwa kuzimu. 
Usiliache tumaini lako. Ikiwa wenye haki watalipoteza tumaini lao, basi ni hakika kuwa kifo kitakuwa kikiwangojea. Ikiwa hatuna tumaini, basi ni wazi kuwa hatutakuwa na nia wala hamu, wala sababu yoyote ya kuishi. Hivyo, hebu tuishi tukiwa na tumaini. 
Katika wakati wa sasa, wale wanaomwamini Yesu na ambao wamezaliwa tena upya kwa kweli hao ndio wenye furaha. Kwa wanadamu, tumaini pekee lililobakia ni kupokea ondoleo la dhambi—yaani, hakuna tumaini jingine zaidi ya kupokea Roho Mtakatifu. Wakati watu wanaposamehewa dhambi zao zote, wanaweza kuwa na tumaini na kisha kuishi kwa furaha milele, lakini kama hawana tumaini, basi ni hakika kuwa maangamizi yanawangojea, hii ni kwa sababu watakuwa hawajapokea Roho Mtakatifu. 
Ninaishi katika ulimwengu huu nikiwa na tumaini kwa sababu nimepokea ondoleo la dhambi zangu zote. Ni matumaini yangu kwamba wewe nawe, utaishi maisha yako ukiwa na tumaini hili. Ninaomba ili kwamba usije ukajiungamanisha na mawazo ya ulimwengu huu, badala yake uishi maisha yako kama bibi harusi mwenye hekima, hali ukiwapenda ndugu zako wenye haki, hali ukiwasaidia kusimama imara katika Kristo, wala usiipoteze imani yako, uendelee kumngojea Bwana harusi, na hatimaye uweze kuonana naye atakapokuja kukuchukua. 
Ninamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuishi katika utukufu wake.